Bado natafuta
Senior Member
- Oct 3, 2021
- 126
- 138
Habari wanajamvi, niruhusu niingie moja kwa moja kwenye mada husika. Hata hivyo, nataka kuwashukuru wale wote wanaochangia katika kuleta mawazo ya maendeleo, hata kama wewe ni mfanyabiashara mdogo, lakini ukileta wazo la kujenga, kuna watu wanafaidika zaidi kuliko wewe.
Napenda uzi usiwe mrefu sana. Siku moja katika wiki nilikuwa napita katika maeneo fulani. Nikamsikia mtu akiongea kwa simu kuhusu kuingia kwenye klabu na akasema, "Klabu ile ina burudani sana, nimeipenda sana hahaha. Na hiyo pombe ya thamani ya 600,000 ina ladha ya kipekee sana."
Maneno hayo niliyoyanasa akilini yalinifanya niwaze jinsi ya kupata mtaji. Neno lililonivutia sana ni "pombe ile ya 600,000" ni kweli kabisa.
Hili lilinifanya niulize maswali mengi kuhusu matumizi ya fedha. Kama kuna mtu anayetaka kujua jinsi ya kupata mtaji wa milioni moja, kuna mwingine anayetumia fedha hizo kwa muda mfupi, si kwa uzalishaji bali kwa anasa.
Kuna mwingine anayetamani laki moja kujaribu biashara fulani, mwingine anapoteza hiyo laki kwa masaa machache tu.
Hili jambo limechochea fikra zangu na kunipa motisha ya kutafuta kwa bidii zaidi.
Nilipokuwa nikiendelea na safari yangu kuelekea kwenye maeneo ya mageto, nilibadilisha mwelekeo na kwenda kuchunguza jambo ambalo ningelishughulikia siku iliyofuata.
Dunia ina mambo mengi ya kufikiria.