Dunia ya Soka ilipotekwa na Sir Alex

Dunia ya Soka ilipotekwa na Sir Alex

barcelona-fc-bayern-muenchen-manchester-united-12-vlnr-mehmet-scholl-picture-id52927157
Miaka ya nyuma palikuwa na vidonge tiba ya maralia ulikuwa ukivimeza baadhi ya watu walikuwa wakiwashwa miili yao sasa nimemuona kuffor hapo nimekumbuka mbali ilikuwa unajikuna mpaka akili zinakuruka.
 
Mzee mwenzangu wakumbuka bibi zetu ukiwaliza "mwanao wa ķwanza ulimzaa mwaka gani? walikuwa hawapepesi macho wala kuangalia tarehe wenyewe walimaliza hivi "yule baba yenu mkubwa wakati wa nzige au ndui au vita sasa weye msomi ni jukumu lako kuingia penye makabrasha ujue nzige walitawala kipindi gani. Lakini ni ngumu miaka ijayo kumwambia mjukuu wako kuwa baba yake ulimpata waqt giggs aliposepa na kijiji chaarsenal au hii ya msimu ulopita ya hazard sababu kwa nini teknolojia imekuwa.
hakika mkuu!
 
Ni miaka 18 sasa, tangu Man Utd alipofanya maajabu katika fainali ya UCL ya mwaka 1999 kwa kutoka nyuma na kubeba ubingwa. Man Utd akatawala soka la Ulaya na Dunia nzima chini ya Sir Alex. Tuambie unapoona kikosi hiki unakumbuka wapi? Mchezaji gani ulimkubali katika kikosi hiki? Karibu utiririke...
26th-may-1999-uefa-champions-league-final-barcelona-spain-manchester-picture-id79054293
Malizia jina zima basi mkuu Sir Alex Ferguson
 
duuh sisi wakina mess na ronaldo tulikosa uhondo
 
Swadakta imeweka rekodi sawa palichimbika pale nou camp jasho na damu kimuhemuhe ila ilikuwa dhulmu ya hali ya juu SAF na wanae walipeleka ujerumani na kwa mashabiki wote ambao walikuwa wakiichukia united. Vikombe vya maana vitatu kwa msimu mmoja tena kwa style ya aina yake siku chache nyuma giggs alifungasha wakazi wa kijiji kile kina keown Lee dixon winterburn na mwenyekiti tonny adams hakika ulikuwa mwaka wa kukumbukwa.
baada ya iyo game ya kukusanya kijiji ndipo bifu la united na aseno lilipozidi kupamba moto mpaka leo
 
Nakumbuka wakati Man Utd wanashambulia hadi wakapata Kona iliyozaa goli la kwanza, commentator alisema hizi ni United dakika za United kufunga n they always score mara pap la kwanza mara la pili. Nakumbuka nilikuwa form 1 usiku naangalia game peke yangu ndani wengine wamelala. Nilipiga kelele hadi nyumba nzima wakaamka.
Siwezi kusahau hii siku
 
Nakumbuka wakati Man Utd wanashambulia hadi wakapata Kona iliyozaa goli la kwanza, commentator alisema hizi ni United dakika za United kufunga n they always score mara pap la kwanza mara la pili. Nakumbuka nilikuwa form 1 usiku naangalia game peke yangu ndani wengine wamelala. Nilipiga kelele hadi nyumba nzima wakaamka.
Siwezi kusahau hii siku
Wakati Man utd walipopata kona ya kwanza iliyoenda kuzaa goli, Commentator alisikika akisema?

" Can Manchester United score? They always score "

Kona ikapigwa goli likaingia.
 
Back
Top Bottom