Dunia ya Soka impe Luka Modric heshima yake

Dunia ya Soka impe Luka Modric heshima yake

Mkuu...ningependa nikuweke sawa apo unaposema kroos ni kiungo Wa kawaida kumlinganisha eti na pogba na fabregas unakosea...sasa Huyo jamaa ndo kabisa huwa uwepo wake kwenye match ni kama vile hayupo ila akitolewaga tu utagundua dimba pale kati limepwaya...hii ilijidhihirisha baada ya kroos kutolewa na sub katika 2nd-leg ya atletico kwenye ligi ambapo game iliisha 1-1,so far pale kati dimbani Madrid kuna viungo Wa maana si mchezo...tukianza na Kroos ni Master pass na penetration kuntu(HUYU NI MZURI ZAIDI TIMU IKIWA INASHAMBULIA),MODRIC ni mmiliki mzuri wa mpira na hutuliza pressure ya mpira pale dimbani(HUYU NI MZURI ZAIDI TIMU INAPO POSSESS MPIRA)...Pia kuna CASEMIRO huyu ni mkabaji makini(HUYU NI MUHIMU SANA TIMU IKIWA INASHAMBULIWA)...Na kila mmoja ana umuhimu wake kwa mfano Casemiro akitokaga na timu ikiwa inashambuliwa lazima Ramos adungwe RED...tafsiri yake mabeki wameelemewa na pale kati kumekuwa uchochoro,Modric asipokuwepo utaona kabisa midfilders za timu pinzani wanamiliki Mpira kuliko madrid na mipira mingi huwa inapotea sana pale kati(hapa naona Isco sherehe hii ya kumiliki Mpira pale kati anaweza ifanya vyema sikuizi isipokuwa tatizo lake huwa anapoza sana mipira anayopewa na wenzie maana hadi afanye udambwi wake ule ndo atoe Pasi...muda mwengine hii hukata morale ya timu) na Kroos asipokuwepo utagundua utoaji wa pasi za mwisho na penetration ni ovyo ila Kroos huwa sio mzuri pale Ramos anapopataga RED ambapo Casemiro inamlazimu arudi pale nyuma kumsaidia varane/nacho na hivyo inawalazimu Kroos na modric kubaki pale kati...apa mzigo huwa unamwelemea sana modric kwa kuwa Kroos si mkabaji kivile bora modric na kwa kuwa timu haipandi kama awali Kroos anashindwa kufanya kazi yake anayoifanyaga ya kutoa pasi za mwisho(katika situation kama hii kroos anakuwaga mzigo na huchoka vibaya kwa kuwa dimba huchafukwa na wao pale kati wapo Wawili tu yeye na luka...ukizingatia kukaba sana sio haiba yake...na apa mara nyingi sub inayoingia badala yake utaona ni Kovacic ana afadhali kwenye kukaba kuliko Kroos).

Aiseeee!!! mkuu inabidi umrithi Mourinho pale OT......maana sio kwa mitactics iyo!!
 
Aiseeee!!! mkuu inabidi umrithi Mourinho pale OT......maana sio kwa mitactics iyo!!

Hahaha!...kawaida hayo,ukiwa na nia utayafahamu tu...utayajua kama ukiangalia mechi nyingi za mipira kwenye ligi kubwa na ukijua mifumo ya timu wanayotumia na pia ukifahamu aina ya uchezaji wa wachezaji husika na namba wanazoweza kuzicheza wanapokuwa uwanjani pamoja na maelewano ya mchezaji na wenzake(yani ile combo ya kuelewana baina ya mabeki au midfilders au forwards) pindi wanapokuwa mchezoni.
 
Wewe Ni Tahira zaidi ambapo nia yako ni kuwaponda tu mashabiki wa Madrid lakini umesahau hata Messi alikuwa anakusanya Tuzo alizostahili Iniesta..
weee ndo ambao unawaambia watoto wako kua ulikua wa kwanza darasani kumbe kubwa LA viraza shubaaamit
 
Mkuu...ndio maana saa zingine wanapigwaga hawa marefa,yani ukiangalia kwenye orodha ya red-cards za jamaa hiyo ya 19 na ata kama unaikumbuka ile mechi...ni Neymar tu alicheza na akili ya referee na referee hakuliona hilo...alichofanya ni kumtolea tu RED Ramos...ila ile card ilikuwa ina Doubt sana ata kweny bodi ya ligi huko laliga waliireview ile action a day after that game...ila ndo vile haikuwa na impact kwa kuwa match ilishachezwa na barca walishapata matokeo yao!
kabsa mkuu,hata wanatusiwa sababu
Ya ujinga wao, kosa la kumpa mtu
Onyo wao wanatoa card yan hata
Huruma hawana
 
Umaarufu my foot!!.Yaani mtu hadi sasa ana UEFA 2 halafu unamwambia mambo ya cjui umaarufu akiwa Spurs?..Hata mwenyewe Luke akikuskia atakuona fala sana.
Sasa kati yangu mimi na wewe nani fala...soma vizuri mada iliyo ubaoni sio unakurupuka tu.
Mwandishi anasema dunia impe heshima ya soka Luka akimaanisha anajituma kwa kipaji alichonacho lakini haonekani kupewa stahiki ya kazi yake ipasavyo
Sababu kubwa ni kucheza timu
amabayo haimtegemei sana yeye kufanya vizuri so anaonekana wa kawaida tu...kitu ambacho ni tofautia na alipokuwa Spurs
 
Ha ha ha hii ni sawa na Aguero Pale Man City,,,ukicheza timu ya kawaida hata delle Ali anakuzidi...kule kuna benzema,ronaldo,bale halafu Umfikirie Modric ha ha ha kwel mkali ila ni wakawaida kwa waliomzunguka ,,Shikamoo Marcelo
Najaribu kuwaelewesha watu kitu kama hiki lakini hawaelewi kabisa yani
 
Hapana mm simkubali kivile bora isco ndo machine na ingine pia ya madrid
 
Ushukuriwe mtoa mada kwa kuliona hili,Luka huwa ananikuna sana kwa pasi na krosi zake matata.
hakika mrembo ukiomba ucheze GAME moja na luka modric utafunga BAO nying sana, maana si kwa pasi zile za jamaa na yale makrosi yake.
 
Timu bora ya FIFA(fifa's first eleven) ni miaka 3 mfululizo nadhan yupo. Labda haandikwi sana ila wataalamu wanajua mchango wake ndio maana anapigiwa kura na kuwepo kikosini siku zote. Pia,ameshinda tuzo za kiungo bora wa Laliga mara nyingi tu. Tafuteni rekodi zake kwanza
 
Modric ni mzuri ila sio lazima apewe tuzo sababu kuna viungo bora kuliko yeye na hawajawai kupewa tuzo.

Aliyekuwa maestro pale Barcelona Xavi Hernandez, amemaliza soka lake la ulaya bila tuzo. Andre Iniesta Lujan pamoja na mchango wake mkubwa kwa Barcelona na timu ya taifa bado huyu jamaa hajapewa tuzo.

Kwa sasa kuna viungo wazuri kuliko modric lakini lakini hutasikia wamepewa tuzo. Ambaye amepata ni Kante. Wakati mimi naona kabisa kante hajafikia kiwango cha Victor Wanyama na Mussa Dembele wanaocheza pale spurs. Mara nyingi viungo huwa hawapewi tuzo wanapewa washambuliaji.
 
Una hisa nini pale Man utd?apo utakua umeniingilia uhuru wangu wa kuongea/kusema chochote la msingi sivunji sheria.

Kwa kifupi ni Shabiki mzuri tu Man utd ila hakuna game iliniuma kama ile hasa yule refa toka uturuki kumpa kadi Nyekundu Nani.

Kati ya viungo bora kuwahi kutokea Modric naye yupo tena sasa Zidane kampa uhuru zaidi baada ya Casemiro kuwa kiungo mlinzi na Modric kupewa jukumu la kucheza huru akizungukwa na Kroos anajua kulinda sana mpira ukiwa miguuni mwake kuuchukua labda umchezee rafu kariba ya akina Iniesta,Xavi
Sure man. PAMOJA
 
68ea157c686d956c5a382ac27be9819f.jpg
 
Bila kumung'unya maneno wanazi na wazandiki wa soka duniani hawamtendei haki Luka Modric. Wamekuwa wakimu-underrate na kumuona mchezaji wa kawaida.

Lakini kwa misimu kama mitatu Luka yupo katika ubora wa kipekee aking'arisha vilivyo safu ya kiungo ya Real Madrid.

Ila bahati mbaya, wazandiki wa soka wanawasifia viungo wa kawaida kama Pogba, Fabregas, Kroos, na Rakitic.

kikosini Real Madrid, wachezaji wanaosujudikiwa ni Ronaldo, Marcelo, Sergio Ramos na Casemiro. Wanamsahau mtu ambaye yuko nyuma ya pazia ya mafanikio ya hao wengine.

Kwanini dunia ya soka haimpi heshima yake Luka?
Imekua ni kawaida ulaya kuwapa sifa wasiostahili na kuwaacha wale wanaostahili.
 
Back
Top Bottom