Dunia ya utandawazi ni aidha waachwe wapumue au walishwe habari kwa wakati

Dunia ya utandawazi ni aidha waachwe wapumue au walishwe habari kwa wakati

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
761
Reaction score
6,985
Nilichojifunza kwa siku za hivi karibuni Duniani kote ni kwamba kila Jambo ni habari. Wanadamu wamekuwa wepesi sana kupokea habari na wazito sana kuzichuja habari.

Ili uweze kuwa na afya ya kiakili lazima ulishe ubongo habari mchanganyiko then ubongo nao achambue zipi uzihifadhi Kama maarifa na zipi usizihifadhi.

Mitandao inakuja wakati ambao binadamu bongo zao zimelemaa hazitaki kuchuja zinahifadhi kila kitu.

Kwa mantiki hii hakuna haja yakubishana nao Bali kuwa mwepesi kuwadhibiti kwa kuwapa habari nyingi iwezekanavyo.

Ukiwekeza kuwaziba masikio na mdomo unapoteza muda maana wanakwenda kupumulia kwenye fake IDentity na nje ya mipaka ya udhibiti.

Tusiwaache wananchi wetu wakilishwa uongo tukijiaminisha wanajua, tujikite kupambana na waongo na kuonyesha uongo wao adharani

Wapeni Uhuru wakupata habari na mjipe muda wakuwapelekea habari sahihi maana i vigumu kuwadhibiti, dunia siyo kisiwa tena.
 
Kwani kinachozuia mkuu asijitokeze nini? kama mzima hajazidiwa atoke tu hadharani dakika mbili arekodiwe na Millardayo kijana wa uvccm mambo mengine yaendelee
Kama ni mgonjwa sidhani anaweza kutoka kama Phillip Mpango huku ana kohoa hovyo, bali atasubiri apone kabisa.
 
'
20210313_103628.jpg
 
Kwani kinachozuia mkuu asijitokeze nini? kama mzima hajazidiwa atoke tu hadharani dakika mbili arekodiwe na Millard Ayo kijana wa uvccm mambo mengine yaendelee
Pengine ni mbinu, ni kupima mioyo ya raia wake
 
Information suffocation is a source of all speculations. What is happening now is entirely their (government's) own making. "Anaumwa. Kafa. Mzima mwenye afya."
 
Kwani kinachozuia mkuu asijitokeze nini? kama mzima hajazidiwa atoke tu hadharani dakika mbili arekodiwe na Millard Ayo kijana wa uvccm mambo mengine yaendelee
Kwani ni wapi ambapo alitakiwa kuonekana ila hakutokea na ndio iwe sababu ya huu uvumi?au ni miezi mingapi hadi sasa imepita toka kuonekana au kusikika kwa mara ya mwisho?
 
TULIPOFIKIA

Wanaostahili kutoa taarifa (Wanahabari & serikali) hatuwaamini

Tunawaamini watu ambao hata hawajulikani... hii ni mbaya sana kama taifa..

Fid Q alisema "Uongo ukiuzidisha, si mda mrefu utajikuta uko nje ya ukweli"
 
Tusiwaache wananchi wetu wakilishwa uongo tukijiaminisha wanajua, tujikite kupambana na waongo na kuonyesha uongo wao adharani
Bahati mbaya au nzuri,habari unazoziita za uongo ndio zimekuwa za kweli, na hizi unazoziita za ukweli ndio zimekuwa za uongo.
 
Back
Top Bottom