Dunia yakaribia kuondoa kero ya plastiki huku mkataba mpya ukisainiwa na UNEP

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
1.jpg

Na Ronald Mutie

Takwimu zilizotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kulinda Mazingira UNEP kwenye mkutano wa tano mkuu wa Mazingira UNEA-5, zinaonyesha kuwa takriban tani milioni 11 za taka za plastiki hutiririka katika bahari kila mwaka, na kutishia maisha ya viumbe vya baharini, usalama wa chakula na maisha ya jamii za pwani.

Takwimu kutoka UNEP zinaonyesha kuwa uzalishaji wa plastiki ulipanda kutoka tani milioni 2 mwaka 1950 hadi tani milioni 348 mwaka 2017, na kuifanya biashara ya plastiki kuwa sekta kubwa yenye thamani ya dola bilioni 522.6 za Marekani.

Licha ya kuwa baadhi ya nchi duniani zimeondoa matumizi ya plastiki ya mara moja lakini sheri ya kimataifa ya kuthibiti uchafuzi wa aina hiyo ni vigumu kusafisha bahari zetu.

Lakini sasa kufuatia azimio lililoidhinishwa kwenye mkutano huo nchi zote wanachama wa Umoja wa Matifa zitakuwa na hadi mwaka 2024 kukomesha uchafuzi wa plastiki.

Azimio hilo ambalo lilipendekezwa na Rwanda, Peru, Japan na India, ndio lilichukua sehemu kubwa ya mjadala wakati wa mkutano huo wa Nairobi ulioleta pamoja wajumbe 3,400 huku wengine 1,500 wakifuatilia kupitia mtandaoni.

Huku azimio hilo likiwa ndio hatua muhimu zaidi ya kimataifa ya kulinda mazingira tangu makubaliano ya hali ya hewa ya Paris ya 2015, linatarajiwa kufungua ukurasa mpya wa juhudi za kusaifisha njia za maji.

Rais anayemaliza muda wake wa UNEA-5 ambaye ni waziri wa mazingira wa Norway Espen Barth Eide, alipongeza kupitishwa kwa azimio la hilo kuondoa uchafuzi wa plastiki, na kusema kuwa ni hatua muhimu ambayo inaahidi ajira, usafi wa ikolojia na kuimarika kwa afya.

"Uchafuzi wa plastiki umeongezeka na kuwa janga. Kupitia azimio la leo tuko kwenye mkondo rasmi wa kupata tiba," Eide alisema, akiongeza kuwa mkataba huo utashughulikia uchafuzi wa plastiki kutoka kwa chanzo hadi watumiaji wa mwisho.

Kwa kuidhinishwa kwa mkataba wa kimataifa unaolindwa kisheria, nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zitapewa jukumu la kushughulikia mzunguko kamili wa plastiki, muundo wa bidhaa na nyenzo zinazoweza kutumika zaidi ya mara moja, lakini pia na hata kama zinavyohimiza uhamishaji wa kutumia teknolojia ili kukutana njia mbadala zinazofaa mazingira.

Mkurugenzi wa (UNEP) Inger Andersen, alisema kuidhinishwa kwa azimio hilo ni ushindi wa umoja wa pande nyingi na azma ya wanadamu kuishi katika sayari safi na yenye afya.

"Leo ni ushindi kwa sayari ya dunia dhidi ya plastiki zinazotumika mara moja. Huu ni mkataba muhimu zaidi wa kimazingira wa kimataifa tangu mkataba wa Paris," Andersen alisema.

Andersen anasema kuwa wakati mazungumzo yatakayopelekea kuanzishwa kwa mkataba wa kimataifa wa kukomesha uchafuzi wa plastiki yanazidi kupamba moto, taasisi za kimataifa zitashirikiana na serikali na viwanda kutafuta ufadhili na teknolojia ambazo zinaweza kuharakisha mpito kuelekea uchumi usio na uchafuzi wa plastiki kwa njia endelevu.

Kutekelezwa kwa azimio hilo kutapunguza plastiki zinazoingia baharini kwa zaidi ya asilimia 80 ifikapo 2040, kupunguza uzalishaji wa plastiki kwa asilimia 55 na kuokoa dola bilioni 70 kwa serikali husika ifikapo 2040.

UNEP inasema, kuondoa plastiki kutapunguza uzalishaji wa gesi chafuzi kwa asilimia 25 kando na kuunda nafasi za ziada za ajira 700,000 kwa nchi zilizoko kanda ya kusini mwa dunia.
 
View attachment 2138240

good move
 
Back
Top Bottom