Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
Ota, Nigeria – Waumini katika ibada ya Jumapili walishuhudia tukio la kushangaza na lisilo la kawaida kanisani, baada ya mwanamke mmoja kuanza kuongea kwa sauti tano tofauti wakati wa ibada.
Mwanamke huyo aliletwa na ndugu zake kanisani hapo baada ya kuonyesha tabia zisizoeleweka kwa muda mrefu. Wakati Mchungaji alipoanza kumuombea, hali yake ilibadilika ghafla – macho yake yalitisha na sauti yake ikaanza kubadilika kwa haraka kutoka ya kike hadi ya kiume, na baadaye ikawa kana kwamba watu watano walikuwa wakizungumza kupitia kinywa chake kwa wakati mmoja.
Waumini walioshuhudia wanasema kuwa aliendelea kupiga kelele kwa nguvu huku akisema kwa sauti isiyo yake: "Hatutaki kutoka! Tumekaa humu kwa muda mrefu!" Mwanamke huyo aliendelea kuongea kwa lafudhi tofauti, maneno yasiyoeleweka, na mwili wake ulitikisika kwa namna isiyo ya kawaida!
Wakati hali hiyo ikiendelea, Mchungaji wa Kanisa hilo alikemea hali hiyo kwa Jina la Yesu Kristo, kisha mwanamke huyo alianguka chini. Alipoinuka, macho yake yalirejea katika hali ya kawaida. Akaanza kushuhudia hali aliyokuwa nayo kabla ya maombezi. Aliongea kwa sauti moja tu ya kawaida. Alikiri kwamba alikuwa anahisi kubeba mzigo mzito, lakini baada ya maombezi hayo uzito ulitoweka akajisikia mwepesi.
Tukio hili liliwaacha waumini wengi wakimtukuza Mungu kwa jinsi Jina la Yesu lilivyo na nguvu ya kuwafungua watu wanaoteswa na kuonewa na nguvu za giza.
Tukio hili lilitokea katika ibada ya kanisa la kipentekoste, Ota, Ogun State, Nigeria.