Duniani Kuna vituko: Awashtaki wazazi wake Kwa kumzaa

...Amepanga kuwafikisha Wazazi wake Mahakamani... Kichwa Cha Uzi wako kinamaanisha Ameisha Wafikisha tayari??
 
kuna kipindi katika maisha yangu nilikuwa mtu wa kutumia logic sana, mungu wangu kumbe logic na maisha ni kama Russia na Ukraine.

..yatosha, acha kesi zao zijisumbukie zenyewe, kwani una nini nao!?
 
Hapa mtatoa povu ila yuko sahihi, unajijua maisha yako ya kuunga si uvae condom? Kwa nini ulete kiumbe duniani kukitesa bure? Yuko sahihi kabisa na mahakama itowe haki
Nimesikia hospitali ya mirembe wameanza kuwasaka wenye matatizo ya afya ya akili mitaani. Hivi hawana wawakilishi humu JF?
 
Nimesikia hospitali ya mirembe wameanza kuwasaka wenye matatizo ya afya ya akili mitaani. Hivi hawana wawakilishi humu JF?
Pelekwa wewe mirembe, binafsi siwezi ruhusu zaa mtoto kama sina uakika wa mkumlea.
 
Rukiacha masuala ya Imani,hapa kuna hoja.
Wengi kesi hii wataihusisha na urukwaji wa akili,Sidhani!

Kwani hizi njia za uzazi wa mpango si ni kama zinamwelekeo wa bwana Raphael? Au mi pia nimerukwa??

Ikiwa ng'ombe tu tunaambiwa tufuge wale tunaoweza kuwamudu,iweje kwa kiumbe chenye mahitaji lukuki(binadamu).Hapa ukweli usemwe KAMA HUNA UWEZO USIZAE,SUBIRI!
Mbona ukinunua gari alafu uanze kugongea pesa ya kiwese unaonekana hujielewi?

Imani ipo ila isitupofushe kufanya vitu hata tusivyonauwezo navyo!

HII KESI IENDESHWE BILA MZAHA ILI IWE FUNZO KWA WAZAZI WATARAJIWA WASIO NA MALENGO KTK NZAO ZAO!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…