Duru: UKAWA njia panda, CCM maji ya shingo

Duru: UKAWA njia panda, CCM maji ya shingo

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Posts
15,773
Reaction score
32,431
Wanajamvi
Katika mabandiko 4 yajayo tutangaalia hali ya kisiasa mbali na BMK

Tutajadili mbinu na mikakati inayotarajiwa siku za karibuni

Namna CCM wanavyohaingaika kujinusuru

Na namna UKAWA walipo, njia panda na mitego inayowakabili.

Huu ni mwendelezo wa nyuzi hizi
https://www.jamiiforums.com/great-t...ji-na-kiwewe-cha-kuzinduka-tanganyika-25.html

https://www.jamiiforums.com/great-t...historia-ya-juisi-ya-maembe-kujirudia-13.html
Tumeonelea umuhumi wa kuwa na bandiko mahususi kufuatilia tahmini ya mambo yanayoendelea, mbele na nyuma ya pazia.

Sehemu ya I

UKAWA

Ukawa ni ushirika ulioundwa wa vyama kukabliana na nguvu kubwa nay a kibabe ya CCM
Kwa miaka 20 vyama vya upinzani vimejaribu kupigana na CCM kila mmoja kivyake bila mafanikio

CCM imetumia udhaifu wa vyama kutawala kwa hila au halali.
Udhaifu upo miongoni mwa wapinzani zaidi ya hasimu wao CCM.

Uundwaji wa vyama ni matokeo ya mafarakano ndani ya wapinzani.
Hilo lilisaidwa na uwepo wa mapandikizi katika upinzani.

Imefika mahali katibu mkuu wa chama au Mbunge anaporudi CCM ni kuonyesha
Kukamilika kwa kazi aliyotumwa.

Kila ulipotokea mzozo, matokeo ni kuacha udhaifu mkubwa. Mifano ni NCCR vs TLP, CUF.

Uhasama umeondoa maridhiano ya pamoja.Mifano ni mzozo wa CDM vs CUF bungeni ulioleta mapasuko.
Chanzo cha mzozo ni udhaifu uliotumiwa na CCM baada ya kuundwa ndoa ya GNU Zanzibar

CDM waliona CUF kama CCM-b, CUF wakiwaona CDM kama wapiga kelele wasiowatakia mema.
NCCR nao wakilalamika kuwa nje ya kambi ya upinzani.

Mvurugano ukawa mkubwa,kwamba ni rahisi Cuf kuunga mkono CCM au CDM kuungana
na CCM katika mazingira ya kukomoana.

Kambi ya upinzani ikagawanyika vipande, CCM wakatumia udhifu huo katika miswada ukiwemo wa kuandika katiba mpya.

Wapinzani wakirushiana maneno CCM walipanga mbinu zao kwa amani.
Sheria ya katiba ilifanyiwa marekebisho upinzani ukiwa ni CDM na kwa mbali NCCR

Mwenyekiti wa CCM akatumia udhaifu kuwaita kwa mafungu, na mwisho wa siku kuwapiga chenga,akitumia maneno baadhi yao wamekubali baadhi hawataki.

Wapinzani wakaelekea bunge la katiba(BMK) wakiwa na agenda zao binafsi dhidi ya CCM.
Uhuni wa CCM ukaanza kuuma kila upande na wapinzani kubaini tatizo si wao Mbaya wao ni CCM.

Ndipo ikazaliwa UKAWA, nguvu za kudai haki ya kuandika katiba ya nchi.
Muda mfupi wakabaini wamebeba agenda ya wananchi mamilioni nyuma yao.

Kuundwa kwa ukawa ni makubaliano ya viongozi wa vyama vya siasa.
Walichogundua ‘mbaya' wao ni CCM anayewatumia kutimiza azma ya hila na mbinu zake.

Na katika kuendeleza maridhiano, viongozi wakakubaliana kuunda kambi ya pamoja ya upinzani ili ushirika uwe endelevu ndani ya BMK na baada ya hapo.

Umoja huo unaungwa mkono na sehemu kubwa sana ya jamii.
Hata hivyo, jamii imekuja nyuma ya viongozi hao kwa vile agenda ya wananchi imekuwa ni moja, kumaliza ubabaishaji wa miaka 50 na kuweka agenda mpya.

UKAWA ni matokeo ya maridhiano ya viongozi si wananchi.
Kinachowaunganisha wananchi na UKAWA ni agenda ya kitaifa iliyopo mbele, katiba mpya.

Ni kwa muktadha huo UKAWA wana fursa iliyopataikana ya kuwaunganisha kwa kutumia
agenda ya katiba mpya.

Lakini hilo ni suala la muda, bado wana changamoto(challenges) wanazohitaji kuzifanyia kazi sasa na siku za baadaye.

Katiba mpya imetengeneza tanuru(template) ya agenda kubwa na wala katiba si agenda yenyewe kwa mtazamo wa wananchi.

Na wala UKAWA wasidhani CCM wanafarijika na umoja huo. UKAWA ni mwiba unaoangaliwa na CCM na kila mbinu itafanyika kuhakikisha, ima inatibua mipango yao au ina wavuruga.

Tuangalie changamoto zinazoikabili UKAWA

Inaendelea
 
Sehemu ya II

CHANGAMOTO ZINAZO IKABILI UKAWA

Kwa vile UKAWA haina ridhaa ya wananchi, kwanza, ni muhimu iwafikie wananchi katika ngazi
zote ili kuepuka kuwa ushirika wa viongozi. Hili ni kujenga mshikamano ngazi zote za kitaifa hadi vijijini.

Pili, UKAWA ni ushirika, sera zao zinatofautiana. Hata hivyo ni muhimu wawe na agenda ya pamoja itakayohusu sera, dira na mamlaka za kiutawala ili kwenda kwa wananchi wakiwa na agenda moja muhimu kwa taifa hata kama kutakuwa na sera tofauti. Kinyume chake wananchi watachanganyikiwa.

Kutumia agenda ya katiba mpya peke yake si suluhu ya muda mrefu ‘sustainable solution''

Tatu, UKAWA wawe mbele ya matazamio (pro-active) kwa kuelewa nini kinapangwa na kwasababu zipi.
Waelewe jamii ya Watanzania inapenda utulivu na woga na hivyo mbinu zao zinapaswa kwenda na wakati.

Suala liwe kujua wanakwenda kujadili nini ikibidi, na si kwenda kujadili kisha kurudi katika kususa au kugoma.
Hili ni muhimu kwasababu uwezekano wa kuchokwa kwa silaha hizo za migomo na kususa ni mkubwa na unaweza kutumiwa kinyume na kuwa tatizo mbele ya safari yao.

CHANGAMOTO ZA DHARURA ZA MUDA MFUPI

BMK limekosa msisimko, uhalali wa kisiasa na kidemokrasia. Linapingwa na sehemu muhimu sana za jamii wakiwemo wasomi waliobobea, wananchi wa kawaida,Katika miji mikuu, wanafunzi wa taasisi na vyu,makundi huru n.k

CCM inatambua bila UKAWA katiba inaweza kupatikana. Tatizo litakuwa uhalali wake kisiasa
na hasa mbele ya jjicho la kimataifa.

Wanatambua katiba itapingwa na yatatokea mambo haya

1. UKAWA kufanya suala la katiba kama sehemu ya ilani.

Kutokana na hasira walizo nazoWananchi, hoja itaungwa mkono na CCM kupoteza sehemu kubwa sana ya utawala.
Eneo wanaloweza kuathirika mapema ni Bunge, na CCM yawezapoteza majority

2. Tuhuma za kuvuruga mchakato zinaiumiza CCM mbele ya umma.
Njia muhimu ni kutoka katika mchakato huu wakiwa salama.

Mazingira hayo hapo juu yanailazimu CCM kufanya mbinu ili kujinusuru.

MBINU ZA CCM KUJINUSURU

Japo mchakato unaendelea, kinachotazamwa na CCM ni namna ya kutoka ''safe exit' katika njia salama, na itakayowamaliza UKAWA mbele ya safari.

Bunge linaloendelea ni kuvuta muda ili nafasi ya kutoka ikipatikana, hilo litimizwe

Mtego waliowekewa UKAWA

1.Kuendelea na majadiliano yakishikirisha watu wazito na wazee

UKAWA wataombwa mambo mawili
a) Kurudi bungeni ili kuendelea na mchakato
b) Kuahirisha bunge hadi muafaka utakapopatikana
c) Kukukbali kufanyia marekebisho katiba iliyopo muafaka ukitafutwa

HOJA
Kurudi bungeni:
UKAWA wakikubali kurudi bungeni watakuwa wamewasaliti wananchi walio nyuma yao na kupoteza imani.
Huo utakuwa mwisho wa kuaminiwa.

Ndani ya Bunge itabidi waridhie kanuni zilizobadilishwa wakiwa hawapo na hata kupoteza nguvu za ushawishi walizokuwa nazo. Hili litakuwa kosa kubwa katika siasa za nchi hii

Ukawa wakikubali kuahirishwa kwa bunge, CCM watatumia mbinu za kuwashirikisha ili
Suala hilo lionekane ni muafaka wa pamoja. UKAWA watakuwa wamepoteza kwasababu

i)CCM itajikwamua kutoka hoja ya kukwamisha mchakato kwa kauli ya ‘tumeamua sote'
ii)UKAWA haitakuwa na nguvu za kuinyoshea kkidole CCM nje ya bunge-'tumeamua'
iii)UKAWA haitaweza kutumia katiba kama agenda au ilani ya uchaguzi-'tumeamua sote'

Kukukabali kufanyiwa marekebisho ya katiba

CCM watawapoza UKAWA kwa ahadi za kukubali katiba iliyopo ifanyiwe maekebisho ili kukidhi haja ya uchaguzi mkuu ujao. Wata ahidiwa tume huru ya uchaguzi na mambo mengine. Hili litafanyika katika bunge la JMT ambako CCM ndio wenye ukanda.

Mbinu inayotarajiwa ni kuwashauri warudi katika bunge la JMT.

CCM watakuja na marekebisho yao, na hapo UKAWA watakuwa mtegoni
a) Wakubali marekebisho hayo hata kama hayana manufaa kwao
b) Wakatae na kususa ili watoke nje ya bunge

HOJA
UKAWA wakikubali marekebisho, basi wamekubali yaishe na huo ndio utakuwa mwisho wao
CCM itatumia nafasi hiyo kuonyesha kuwa kususa kwao BMK ilikuwa ni vurugu tu.
CCM watajinasibu kuwa wao si tatizo na wapo tayari kuafikiana, tatizo ni UKAWA

UKAWA wakisusa na kugoma umma hautawaelewa. Wananchi watahoji ni eneo gani ambalo
UKAWA wanadhani masuala ya kitaifa yanaweza kujadiliwa.

Na kwamba, migomo itaendelea hadi lini na nini matokeo yake.
UKAWA watakuwa wameuza silaha na kupoteza mbele ya CCM

Inaendelea
 
Sehemu ya III

KWANINI UKAWA NI WAHANGA (VICTIMS) WA CCM KILA MARA

Tatizo la UKAWA ni kutotaka kuweka mambo bayana na kutokuwa na mipango kabla ya hatua ni mara nyingi UKAWA hulalamika baada ya kuingia mkenge.

Kwa mfano, mazungumzo ya kurudi bungeni yakishindikana,CCM watatoa taarifa kuhusu hilo watatumia nafasi hiyo kuwashirikisha UKAWA watake wasitake.

Ndivyo mazungumzo ya Ikulu ya wapinzani na Rais yalivyofanywa.
UKAWA wakadanganywa na ikatolewa kauli ya pamoja (joint statement) kuwa kumekuwa na maridhiano kuhusu idadi ya wajumbe wa BMK, uteuzi n.k.

Kauli hiyo hadi leo inatumika kuwahukumu. Ndivyo walivyodanganywa kuandika kanuni za bunge
Bila kuziwekea uzio. CCM wakatumia utata kukwamisha mchakato.

Leo wanawahukumu UKAWA Kwa kusema walikuwa sehemu ya Mchakato wa kanuni za BMK

Usuluhishi unaoendelea kichini chini nao utazaa hali kama hiyo.
Katika wiki moja au mbili, tunaweza kusikia kauli ya pamoja kama tulivyoeleza hapo juu

Hilo likishindikana, UKAWA wataingizwa kingi kwa kukubali marekebisho ya katiba.

UKAWA WAEPUKE VIPI MITEGO INAYOWAKABILI

Ni lazima makubliano yote na CCM yaweke bayana kabla ya muafaka, yaeleweke,
yafungike na yaafikiwe kukiwa na upande huru wa tatu ‘third party'

Makubaliano husika yawekwe bayana mbele ya wananchi ili itakapotokea matatizo iwe rahisi kwa UKAWA kuwa na ushahidi wa kutosha machoni mwa wananchi.

Lakini pia ni muhimu wajue kila neno na namna linavyoweza kutumiwa kubadilisha maana.

UKAWA wachukue hatua za haraka za kukabiliana na changamoto tulizoeleza hapo juu.

Inaendelea...
 
Sehemu ya IV

UKAWA WACHUKUE UONGOZI(LEADERSHIP)

Kwa bahati nzuri UKAWA wanaungwa mkono na sehemu ya wasomi wa jamii yetu.

Kundi la wananchi ni kubwa kuliko wasomi, na hivyo UKAWA wanajukumu la kuchukua Uongozi wa mada, mijadala na elimu ya umma.

Kwa mfano, haitoshi tu kusema tunahitaji katiba mpya.
Ni lazima mwananchi aelezwe kwa kina katiba tunayoihitaji nini umuhimu wake kwa mwananchi na kwanini tunahitaji sasa.

UKAWA wafafanue agenda zao zieleweke kwa wananchi. Waeleze, rasimu ya Warioba imesema nini, sheria ya nchi ilitaka iweje na CCM wamechakachua eneo gani na kwanini.

UKAWA ieleze, msimamo wa serikali tatu unatokana na ukweli gani(facts) wakitumia nyaraka za tume na tume zilizopita za akina Kisanga, Nyalali n.k na kuonyesha ni kwanini mfumo unashauriwa hivyo.

UKAWA waeleze faida na hasara za serikali 2 au 3 kwa lugha rahisi na nyepesi kwa mwananchi.

Waeleze matakwa yao yamelenga nini katika maendeleo ya wananchi na nchi kwa ujumla.

Waonyeshe mfumo uliopo, jinsi ulivyoshindwa na athari zake kwa wananchi

Kwa lugha ya kigeni, ni wakati UKAWA wachukue leadership (uongozi) na si kuvizia nafasi au matamko ya makosa ya watu. Wao watangulie umma uwafuate na si kujificha.

Bila kuwa na leadership, nado umma utachangikiwa. Ukawa hawazwezi kudumu kwa kutaka kufurahisha kundi au watu fulani. Ni lazima wasiamame katika ukweli na waonyeshe nini halali na nini haramu.

Kuongoza ni uonyesha njia, katika nyakati hizi ambapo hakuna kiongozi, UKAWA wana fursa hiyo.
Ni lazima waonyeshe wapo tayari kwa prime time. Si muda wa kuibua kashfa, bali muda wa kuonyesha dira na mwelekeo wa nchi.

Inaendelea...
 
Sehemu ya V

MAJUMUISHO

Hali ya CCM ni ngumu kwa sasa.
UKAWA waijidanganye kudhani kuwa CCM imekaa kimya katika mazingira iliyo nayo au inaelekea kupoteza bila jitihada.

Sasa hivi wana mikakati mikubwa sana dhidi ya UKAWA

1. Kuua hoja ya katiba na kusukuma mzigo kwa UKAWA

2. Kuendelea na mbinu za udanganyifu ili kubaki madarakani

3. Kuudhofisha UKAWA kwa gharama zozote zile.

Katika mazingira tuliyoyaangalia hapo juu ni wazi kabisa, UKAWA wapo katika mtego mkubwa.

Kwa hali yoyote iwe kurudi BMK, kuahirisha mchakato au kurekebisha Katinba ya sasa, UKAWA
hawawezi kufaidika na lolote.

Kilio cha muda mrefu cha katiba kililenga kubadili mwelekeo na dira ya taifa.Itakuwa ni kushindwa kwa hali ya juu ikiwa UKAWA watakubali chochote katika nusu glasi watakayopewa.

Hakuna sababu zozote za kuharakisha mambo kwasababu taifa lipo na litaendelea kuwepo.

Tume ya Warioba imechukua miaka 2 tuliyodhani ni mingi leo tunaona kama mwezi mmoja.

Kwa kuzingatia hali halisi, mapambano ya CCM kujinasua na uzoefu katika udanganyifu ni muhimu UKAWA wakafikia hitimisho hili.

1. Kupatikana kwa katiba mpya ni suala muhimu kwa mwelekeo na dira ya taifa.
Taifa lipo tayari kusubiri katiba mpya kwa muda wa mwaka au miwili ijayo.

2. Uchaguzi mkuu wa mwakani uahirishwe hadi katiba mpya itakapopatikana

3 Hakuna sababu za kuwekea viraka katiba mbovu iliyopo.
Na wala hakuna uhakika wa kuwa na mabadiliko ya maana katika wingi wa CCM walio nao.

Ni lazima tuwe na muafaka kuelekea uchaguzi. Kama CCM wataenda uchaguzi kwa kiburi, basi UKAWA wajitoe na waendelee na jitihada za kutafuta katiba mpya.

Duru za siasa tunasisitiza kuwa, upo mkakati mkubwa na mzito unaoandaliwa kuhujumu jitihada zote za UKAWA.

UKAWA lazima wajipange vizuri, wasidhani Simba aliyenyeshewa na mvua ni sawa na nyani.

Mwendo wanaokwenda nao, kama hawatakuwa na uangalifu historia ya nyuma itajirudia kwa nguvu.
Vikao vinavyoandaliwa si vya maridhiano, ni mitego ya kujinasua na kuwatega. Hapo ndipo duru tunapoingiwa na hofu kama kweli UKAWA wanatambua hilo

Hakuna haraka ya uchaguzi wala katiba. Ni lazima muafaka ufikiwe. Uma upo nyuma yao na CCM sasa maji ya shingo.
UKAWA wakishindwa kutumia nafasi hiyo, basi wajisalimishe kwa CCM haraka maana dhahma kubwa itawaangukia.

TUSEMEZANE
 
Nguruvi3,

Asante kwa kuleta mjadala muhimu. Kuna mambo muhimu Sana ambayo Umejadili, nitajadili maeneo yote muhimu kwa kadri mjadala utakavyoendelea. Kwa sasa ningependa kujadili eneo moja muhimu - nalo ni kuhusiana na haja ya ukawa sasa kuchukua leadership role na kuzungumza na wananchi kwa lengo la kuwatolea ufafanuzi juu ya mengi ambayo bado yana wachanganya. Kwa vile wananchi walio wengi wamependekeza serikali Tatu badala ya Mbili au moja, approach ya ukawa sasa iwe kuwaelezea wananchi kwanini walichochagua kupitia tume ndicho kitawaweka on the right side of history hata Kama ni miaka 100 kutoka sasa. Yapo masuala kadhaa ambayo ningependa kuyawasilisha kwa mtindo wa nadharia tete ili kuchokoza mjadala na maeneo hayo in my humble view Ndio Yale ambayo ukawa wanatakiwa kuyafanyia kazi as they engage na wananchi kuanzia sasa:

1. Wananchi wengi wa upande waTanzania bara bado wanaona Kwamba haja ya serikali Tatu is more of a matter of retaliation on Zanzibar kuliko the fact Kwamba suala la establishment and existence of Tanganyika is a matter of principle. Kwa maana nyingine, kwa wananchi walio wengi bara, bado Hawana uelewa wa kutosha Kwamba Haiwezekani kuwepo serikali Mbili ndani ya nchi Mbili. Ndani ya nchi Mbili kunakuwepo na serikali moja au serikali Tatu, basi".

2. Mwalimu aliweka wazi mwaka 1994 Kwamba Tanganyika sio sera ya CCM, badala yake, sera ya CCM ni serikali Mbili, kuelekea moja. Katika Hali ya sasa, hata tume ya warioba imejiridhisha Kwamba Tanzania haiwezi tena kuwa na serikali moja. Malengo ya serikali Mbili kwa nchi moja yalishakufa na kuzikwa na waasisi wa muungano - mwalimu Nyerere na sheikh karume.

3. Wananchi wengi wa upande wa Tanzania bara Hawaelewi Kwamba Zanzibar hawawezi kurudi tena nyuma kikatiba na kujitambulisha tena Kama ni "Zanzibar sehemu ya jamhuri ya muungano wa Tanzania", Kama ilivyo kwenye katiba ya sasa ya JMT (1977) Toleo la 1995. Zanzibar itaendelea kuwa nchi, na CCM itaendelea kuwapa Zanzibar kila wanachotaka ili mradi sera ya CCM ya serikali Mbili iendelee kuwepo, huku wananchi wa Tanzania bara wakibebeshwa gharama za kuwabembeleza Zanzibar.

4. Mgogoro juu ya Mgawanyo wa Mapato ya muungano na uchangiaji wa gharama za kuendesha muungano Kati ya serikali ya muungano na serikali ya mapinduzi ya zanzibar hauwezi kumalizwa kwa kuruhusu wazanzibari kuagiza bidhaa kutoka nje, kukopa nje, na kuendesha uchumi wa Zanzibar bila ya kupitia au kudhaminiwa na Tanzania bara. Vyama vya CCM na ACT vina mtazamo huu Kama sehemu ya suluhisho la mgogoro wa muungano, mtazamo ambao haupo sahihi.

5. Mfumo we Serikali Mbili zilizoboreshwa na CCM ambazo zinalenga kuipa Zanzibar mamlaka kamili bado utaibua Madai mapya ya Zanzibar juu ya kuwa nchi kamili. Hakuna mamlaka kamili Zanzibar bila ya uwepo wa Tanganyika.

6. Iwapo CCM itafanikiwa kuleta serikali Mbili zilizoboreshwa, hii itakuwa ni kwa faida ya Zanzibar na kwa hasara ya Tanganyika. Hali hii itapelekea wananchi wa Tanzania bara kudai Tanganyika kwa Nguvu Kama alivyoeleza professor Kabudi. Kwa maana nyingine, jinsi CCM inavyoZidi kuboresha serikali Mbili ndivyo jinsi watanzania bara wanavyozidi kukosa Haki zao za kisiasa, kijamii, na kiuchumi (political, social and economic justice) ambazo zitakuja leta vurugu na vita. Kwahiyo serikali Mbili zilizoboreshwa ni "timing bomb" ambalo ni wajibu wa ukawa kuwaelezea wananchi Kwamba wajibu wa kulitegua ni wananchi wenyewe.

7. Wananchi wengi wa upande wa bara Hawaelewi athari za katiba ya Zanzibar (2010) kwa Tanganyika na kwa muungano kisiasa, kiuchumi na kijamii. Kisiasa, rais wa muungano ambae ndiye rais wa Tanganyika ni rais boya. Rais wa muungano ambae pia ni rais wa Tanganyika hatokuwa na uwezo wa kuilinda na kuitetea Tanganyika chini ya katiba iliyoboreshwa. Kiuchumi, chini ya serikali Mbili zilizoboreshwa, muungano utamhudumia mzanzibari kuliko mtanzania bara. Na kijamii, utambulisho wa mtanzania utafifia zaidi chini ya nchi Mbili Zenye serikali Mbili kuliko uzanzibari. Matokeo yake ni Kwamba Kama taifa, tutajenga Kizazi ambacho hakitaweza jitambua Huko Mbeleni.

Kwa mtazamo wangu, hayo Ni baadhi ya maeneo ambayo ukawa wanatakiwa kuyazingatia in their dialogue na wananchi.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mchambuzi
Ahsante kwa maoni yako. Nidonoe sehemu chache miongoni mwa ulizojadili.

1. Kwamba, S1 kama walivyosema waasisi ni ndoto.
Hili hata CCM wanalifahamu isipokuwa kwa kujitoa akili wanasema ndio lengo la waanzilishi.

Ndio la Tanzania nchi ya ujamaa katika katiba wakati tunaelekea miaka 30 ya kumbukumbu za kifo cha ujamaa kilichotokea Zanzibar

2. UKAWA watumie lugha nyepesi na inayoeleweka.
Kwa mfano, wananchi wanasema 'mbili zinatosha''hawaelewi ni kwa faida au hasara ya nani.

Sidhani kama UKAWA wanafanya jitihada za kutosha katika eneo hili.

3. Umezungumzia kuhusu mbinu hafifu za kuwafaraji wznz kama sehemu ya kubaki na mfumo wa S2.

Hili limefanyika miaka mingi sana, wznz hawaridhiki na wala hawataridhika.

JK amejaribu sana kuwafariji. Kwa bahati nzuri, wznz wamemuonyesha sura halisi.

Kuvunja katiba ni kosa kubwa kisheria.Makosa ya kukaa kimya katiba ikivunjwa ilitosha kubisa kuwa impeachment kwa nchi za wenzetu. Hilo lilifanyika katika jitihada za kulinda S2 kwa kuwafariji wnz.

Jitihada zimeendelea katika maeneno ya makongamano, wageni kutemebelea znz n.k.
Sasa ni kuruhusu tu chochote hata kama kina athari kwa taifa ili kuwafariji wznz na kulinda S2.

CCM haifahamu tatizo si kuwafariji baadhi, ni social and economic injustice inayoyohitaji suluhu
Hata kama yatakuwepo mabadiliko ya kutoa fursa zaidi kwa wznz katika kuwafariji hilo litazaa tatizo kubwa sana kwa upande wa pili.

Tanganyika ambao hawana mtetezi kwa sasa watatafuta utetezi nje ya JMT.
Hilo tu linaweza kupelekea social unrest ya hali juu na huenda likazaa mambo yasiyotarajiwa.

Kutakuwa na kuvunjika kwa nguzo zinazotushikilia kama taifa.
Hili ni tatizo on the making ambalo CCM hawalioni kwa sasa.

Kwa hali ilivyo, tuna utaifa wa aina mbili, Watanzania na wazanzibar.
Wananchi watakapoachiwa wa-define utaifa kwa misingi iliyopo tutaishia kuvunja uzalendo taifa.

Bongolander katika uzi mwingine ameeleza kitu kilichonisisimua sana.
Kasema, G55 ilidai Tanganyika katika misingi miwili, principle and retaliations

Sasa hivi madai ya Utanganyika yamevuka hapo na kuhusisha economy and injustice.

Ni kwa mtazamo huo wa Bongolander, S2 zinazoambiwa zimepatiwa majawabu zinajikuta na maswali mengi zaidi ya ilivyokuwa wakati wa G55.

1. Tanganyika iwepo as matter of principle kama anavyosema Mchambuzi
2. Kuna element za retaliations(Mchambuzi)
3. Kuna suala la uchumi kama tunavyosema kila siku
4. Kuna suala la injustice kutoka Tanganyika.

Hayo hayawezi kutatuliwa kwa kualika makamu wa Rais afungue maonyesho
na makongamano ,Kuwapeleka marais wanaotembelea nchi huko znz
Kuongeza nafasi za ajira, Kuongeza fursa kama kwa wznz n.k

Badala ya kutoa suluhu, CCM wanachochea hasira upande mwingine wakiweka 'band aid'
Huwezi ku-balance scale kwa kuongeza uzito upande mmoja.

Haya ndiyo UKAWA wanapaswa kuyaeleza na athari zake katika jamii ikiwa ni pamoja na kuondoa utaifa, kuvunja uzalendo na kuparaganyika kwa taifa.

Apparently inaonekana zanzibar imeshikilia muungano, in reality Tanganyika ndiyo ina turufu katika hatima ya taifa hili.

Ni lini na kwa njia ipi Watanganyika wataamua kutumia turufu yao ni intriguing question. Nini matokeo ya turufu hiyo ni jambo linalotisha.

Tuendelee kujadiliana
 
Sehemu ya IV

UKAWA WACHUKUE UONGOZI(LEADERSHIP).......Kwa mfano, haitoshi tu kusema tunahitaji katiba mpya.
Ni lazima mwananchi aelezwe kwa kina katiba tunayoihitaji nini umuhimu wake kwa mwananchi na kwanini tunahitaji sasa.

UKAWA wafafanue agenda zao zieleweke kwa wananchi. Waeleze, rasimu ya Warioba imesema nini, sheria ya nchi ilitaka iweje na CCM wamechakachua eneo gani na kwanini.

UKAWA ieleze, msimamo wa serikali tatu unatokana na ukweli gani(facts) wakitumia nyaraka za tume na tume zilizopita za akina Kisanga, Nyalali n.k na kuonyesha ni kwanini mfumo unashauriwa hivyo.

UKAWA waeleze faida na hasara za serikali 2 au 3 kwa lugha rahisi na nyepesi kwa mwananchi.

Waeleze matakwa yao yamelenga nini katika maendeleo ya wananchi na nchi kwa ujumla.

Waonyeshe mfumo uliopo, jinsi ulivyoshindwa na athari zake kwa wananchi

Kwa lugha ya kigeni, ni wakati UKAWA wachukue leadership (uongozi) na si kuvizia nafasi au matamko ya makosa ya watu. Wao watangulie umma uwafuate na si kujificha.
....................

Ahsante sana Nguruvi3 kwa uchambuzi unafuata misingi ya udadisi makini (serious curiosity principles) huku ukianisha uchambuzi wako kwa kutumia miongozo yakilojiki (logical guidance).

Nikirudi kwenye mada:

Kama tunawavika jukumu hili zito UKAWA juu ya kuwaelezea wananchi faida na hasara za serikali mbili ama tatu (jambo ambalo ni jema), huku tukikubali kuvuta subira ya kupata Katiba Bora; naona nivyema tuwaongezee majukumu katika hili.

Majukumu ninayoyapendekeza yanalenga kukusanya taarifa zitakazo saidia kuondoa kasoro zilizojitokeza wakati wa kukusanya maoni, kuandika rasimu ya kwanza na ya pili, kuwasilisha rasimu kwenye bunge la katiba, kufungua bunge la katiba, na kujadili rasimu ya katiba ndani ya bunge la katiba.

Majukumu ninayopendekeza kwa Ukawa ni kuwa watuelezee faida na hasara hasa kwa kuwalenga wananchi wa kawaida, viongozi walioko madaraka, viongozi wanaotarajia kuingia madarakani na taifa kwa ujumla wake yafuatayo:

1. Kuwa na Muungano wa serikali ya Tanganyika na serikali ya Zanzibar (Raisi mmoja mawaziri wakuu wawili wakiongoza serikali hizo)

2. Kutokuwa na Muungano wa serikali ya Tanganyika na serikali ya Zanzibar (kuvunja muungano yaani kila serikali ijitegemee)

3. Kuwa na Muungano wa Mtakaba wa serikali ya Tanganyika na serikali ya Zanzibar (uliopendekezwa na Seif kama sijakosea na baadhi ya wazanzibar)

4. Kuwa na Muungano wa serikali ya Tanganyika na serikali ya Zanzibar wenye serikali moja ya JMT( rais mmoja na waziri mkuu mmoja)

5. Kuwa na Muungano wa serikali ya Tanganyika na serikali ya Zanzibar wenye serikali mbili,serikali ya JMT na serikali ya Zanzibar (mfumo tulionao sasa)

6. Kuwa na Muungano wa serikali ya Tanganyika na serikali ya Zanzibar wenye serikali tatu, serikali ya JMT , serikali ya Zanzibar na serikali ya Tanganyika(mfumo uliopendekezwa kwenye rasimu ya Tume iliyoongozwa na Jaji Warioba)

7.Kuwa na Muungano wa serikali ya Tanganyika na serikali ya Zanzibar wenye serikali nne, yaani serikali ya JMT , serikali ya Unguja, serikali ya serikali ya Tanganyika, na serikali ya Jamhuri ya Pemba.

Sisi wananchi wa kawaida tukisha kuelezwa kwa lugha rahisi juu ya faida na hasara ya muundo wa Muungano na serikali zake; nina imani tutakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuchagua muundo wa muungano na serikali zake bila kubabaishwa. Hivyo tukija kuombwa maoni juu ya katiba itakuwa rahisi kutoa maon yetu.

Jukumu hili ni zito sana na shauri (kama tutasogeza mbele uchaguzi, jambo linalopigiwa upatu na mkuu wa kaya, ) basi wakae si chini ya miezi kumi na tano, watuletee ripoti hiyo. Baada ya hapo masuala ya kutunga katiba mpya ndo yaendelee.
 
Hili la kuahirisha uchaguzi haliwezi kufanyika mpaka katiba ya sasa ibadirishwe ili kuongeza possibilibility ya raisi kuongoza katika circumstance za aina hii. Isitoshe kama unaweza kuextend Utawala wa CCM bila kulazimika kupigiwa kura ni sawa sawa na umempa Fisi bucha akulindie, kwa sababu bila ya uchaguzi mpya CCM watabaki na wingi wao, na still nao wakiamua kukwamisha katiba mpya wanaweza, na kwa kuwa hutaki uchaguzi unakuwa huna leverage yoyote dhidi yao kwa kuwa CCM watakuwa hawana cha kuogopa!!

Tukiangalia trend ya taasisi za kijamii kati ya wale 201 ambao wengi miongoni mwao waliobaki bungeni, na pia tukiangalia viongozi wa madhehebu yenye watu wengi ikiwemo Bakwata, Catholics, Lutheran na wengineo, wapo Upande wa CCM. hawa nyuma yao wana watu wanaowasikiliza sana na ni base nzuri sana ya kura kwa CCM iwapo Ukawa wataendelea na siasa zao za kimatukio katika suala hili la katiba.

Lakini kitu kingine ulichokiacha, kwa nini husuggest Ukawa waende mahakamani kzuia mchakato iwapo wana msingi wa kisheria wa kufanya hivyo?- ninachokiona ni kwamba wanaleta Siasa katika mchakato huuu na kwa kuwa hawana wingi wa kura za kufanya maamuzi jamii itawaona kama watu wanaotaka kuvuruga tu. KAMA WANA HOJA NZITO ZA KISHERIA NI RAHISI KUKUSANYA NGUVU ZA KISIASA KWA NINI HAWATAKI OPTION HII KAMA WANA NIA NJEMA?
 
Kwahiyo unashauri heri nusu glass ya maziwa?

Kuhusu kuungwa mkono, nadhani taasisi nyingi hasa za wasomi hazikubaliani na CCM hata kidogo.
Hakuna msomi aliyesimama na kusema wazi anaunga mkono CCM, I mean mwanazuoni siyo wachumia tumbo.

Pili, hili la taasisi za kidini nadhani umeliangalia tofauti. Hao ndio wanasema maoni ya wananchi yaheshimiwe sasa sijui hapo wana maannisha nini. Na pia utambue hao ni viongozi, hakuna taasisi iliyowahi kupitisha kura ya maoni kuhusu mchakato kwa waumini wake.

Hap pia kuna tatizo, kwamba CCM wanapojaribu kuungwa mkono na taasisi za dini tunatengeneza fertile environment kwa matatizo siku za baadaye. Sijui 'Yehova na wajahidini' watakapokuwa na mtizamo tofauti na Cathloic na Bakwata tutaelekea wapi. Hii ni sehemu ya hatari ambazo CCM kwa kutaka madaraka inazitumia bila kujua ni tatizo.

Kuahirisha uchaguzi kwa kubadili kipengele cha kumuongezea muda rais sidhani kama ni tatizo kama kipengele ni hicho.

Jambo ambalo CCM hawalioni ni ongezeko la nguvu la nguvu ya umma. Ipo siku huenda wakaenda Dodoma wakiwa ndani ya Costa. Hivyo suala la kukabidhi bucha ni la mantiki tu.

Moi, Kibaki walijaribu na leo wapo maktaba wakijikumbusha enzi za KANU.

Kuhusu CCM na wingi wao, nasema kuwa kwasasa inaonekana ni wengi kwasababu wapo 'mahabusu ya kisiasa'
Ipo siku watataka uhuru wa kusema, kunene na kutamka na hali itakuwa tofauti.
Wingi wa CCM ni kutokana na kutiwa gerezani na akina Nape, Wasira, Kinana n.k.

Hata hivyo ndani ya CCM kuna sentiment kubwa tu inajengeka.

Ukitazama na kutembea mitaani na sehemu za wananchi, wengi hawakubaliani na CCM katika suala la katiba.
Hivyo UKAWA Iinaungwa mkono na sehemu muhimu ya jamii ambayo CCM can't do without.
 
Hili la kuahirisha uchaguzi haliwezi kufanyika mpaka katiba ya sasa ibadirishwe ili kuongeza possibilibility ya raisi kuongoza katika circumstance za aina hii. Isitoshe kama unaweza kuextend Utawala wa CCM bila kulazimika kupigiwa kura ni sawa sawa na umempa Fisi bucha akulindie, kwa sababu bila ya uchaguzi mpya CCM watabaki na wingi wao, na still nao wakiamua kukwamisha katiba mpya wanaweza, na kwa kuwa hutaki uchaguzi unakuwa huna leverage yoyote dhidi yao kwa kuwa CCM watakuwa hawana cha kuogopa!!

Tukiangalia trend ya taasisi za kijamii kati ya wale 201 ambao wengi miongoni mwao waliobaki bungeni, na pia tukiangalia viongozi wa madhehebu yenye watu wengi ikiwemo Bakwata, Catholics, Lutheran na wengineo, wapo Upande wa CCM. hawa nyuma yao wana watu wanaowasikiliza sana na ni base nzuri sana ya kura kwa CCM iwapo Ukawa wataendelea na siasa zao za kimatukio katika suala hili la katiba.

Kama alivyojadili Nguruvi3 Hapa na kwingineko,Katiba iliyopo haina uhalali tena kisheria na kisiasa. Katiba iliyopo inaendelea kuitambua Zanzibar kama "sehemu ya jamhuri ya muungano". Katiba hiyo pia inaelekeza serikali ya mapinduzi ya zanzibar kutekeleza kazi na majukumu yake kwa mujibu wa masharti ya katiba hiyo ya JMT (1977) pamoja na katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984. Tukizidi angalia kwa undani, katika ibara ya 103(2) ya katiba hii ya Jamhuri ya Muungano inasema hivi:

"Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kabla ya kushika madaraka yake ataapa mbele ya Jaji Mkuu wa Zanzibar kiapo cha kulinda Katiba ya JAMHURI YA MUUNGANO na kiapo kingine kingine chochote kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar kinachohusika na uutendaji wake.

Kiongozi wa Zanzibar atashika na kutekeleza madaraka hayo kwa mujibu wa masharti ya katiba hii na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984."

Ni katiba hii hii Kinana na Nape miezi kadhaa iliyopita Walisema Kwamba haina haja ya kubadilishwa. Tunashangaa kinana anatafuta nini Dodoma kwenye vikao vya maridhiano. Katiba Aliyosema kinana Kwamba haina haja ya kubadilishwa, haina ubavu tena mbele ya Katiba ya Zanzibar.

Kinana na nape baadae wakaenda znZ Kujibu mapigo ya ukawa waliotoka bungeni. Umati wa wananchi waliojitokeza kuwasikiliza akina kinana na nape uliwaona viongozi Hawa sio lolote zaidinyabwageni kutoka nchi jirani ya Tanganyika. Kwani Katiba ya Zanzibar, ambayo katiba ya kina Nape (JMT 1977) inasema kwamba Zanzibar ni "sehemu ya jamhuri ya muungano", inatamka wazi kwamba "Zanzibar ni Nchi". Katiba ya Zanzibar (tofauti na ile iliyopigiwa debe na kinana na nape) inasema kwamba "Mipaka ya taifa la zanzibar ni eneo lote la visiwa vya unguja na pemba, pamoja na visiwa vidogo vilivyoizunguka, bahari yake ambayo kabla ya kuundwa kwa jamhuri ya muungano, ikiitwa Jamhuri ya watu wa Zanzibar". Ibara ya kwanza ya Katiba ya Zanzibar inaweka wazi kwamba:

"Zanzibar ni miongoni mwa nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania."

Nchi ya pili ni ipi? Akina Nape, Wassira, Sitta na kinana hadi leo hawana majibu.

Tukiangalia masharti haya ya katiba ya zanzibar, tunaona wazi kwamba yanaenda kinyume na matakwa ya katiba ya kina nape (JMT 1977), katika ibara yake kwa kwanza ambayo inaendelea kutamka wazi kwamba:

"Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano"

Tukienda kwenye ibara ya 33(2) ya katiba ya kina nape (JMT 1977) inasema kwamba:

"Rais wa Jamhuri ya Muungano Ndiye Mkuu wa nchi, Kiongozi wa serikali na Amiri Jeshi Mkuu."

Kifungu hiki kinapingana na ibara ya 26 ya katiba ya zanzibar ambacho kinatamka kwamba:

"Rais wa Zanzibar ni mkuu wa nchi ya Zanzibar".

Tukienda kwenye ibara ya 2(A) ya katiba ya Zanzibar, inatamkwa kwamba, kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za serikali, rais aweza kuigawa Zanzibar katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.

Masharti haya yanaenda kinyume na katiba ya kina Nape ambayo katika ibara ya 2(2) inasema kwamba:

"kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za serikali ya Jamhuri ya Muungano au Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, rais aweza kuigawa Jmahuri ya Muungano katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria iliyotungwa na Bunge"

Maswali kwenu nyinyi CCM conservatives:

• Tutaingia vipi Katika uchaguzi mkuu mwakani na Madudu haya?

• Je kutakuwa maridhiano mapema baina ya ukawa na CCM lakini pia baina ya CCM na waandaaji wa katiba ya Zanzibar 2010?

Rais Kikwete miezi kadhaa iliyopita Alitamka Kwamba kuba uwezekano wa katiba ya sasa kuendelea kutumika katika uchaguzi mkuu ujao (2015). Sina uhakika Kama chama cha mapinduzi kinajua au Kinajali Kwamba iwapo uchaguzi utafanyika chini ya katiba ambayo itaendelea kupingana na katiba ya znZ,Rais ajaye (2015) ataingia madarakani huku madaraka yake yakiwa yameporwa na katiba ya zanzibar (2010).

Tatizo lililopo ambalo Wanasiasa wababe ndani ya CCM - Wassira, nape, Sitta aidha hawalijui au wanalipuuza ni kwamba - Katiba ya JMT na Katiba ya Zanzibar zina hadhi zinazopishana. Katiba ya JMT inatakiwa isomwe na kuendana pamoja na katiba ya Zanzibar, sio vinginevyo. Hivyo ndivyo muungano baina ya Zanzibar na Tanganyika unapotimia. Lakini kwa hali ya sasa, Ni kama vile katiba ya muungano haipo tena. Katiba hii imevunjwa, imefukiwa, hivyo kutubakisha na muungano wa maneno na mazoea tu. Vinginevyo muungano umeshatoweka.

Conservatives na wababe ndani ya CCM wanasahau jambo moja muhimu sana, nalo ni kwamba, tukiingia katika uchaguzi mkuu ujao chini ya katiba ya JMT inayopingana na Ile ya znZ, uwezekano wa kutokea mgogoro wa kikatiba na hata machafuko ni mkubwa.
Upo uwezekano wa serikali ya Jamhuri ya Muungano kushindwa kufanya uchaguzi mwakani (2015). Hii ni kwa sababu Rais ajaye bila ya kujalisha atatokea chama gani cha siasa, hatoweza kula kiapo kuilinda katiba ambayo tayari inakinzana na katiba ya nchi jirani ya Zanzibar.

Kwa mfano - Rais wa Muungano atatakiwa kuapa kuilinda katiba kwa sababu yeye ndiye mkuu wa nchi, Kiongozi wa serikali na amiri jeshi mkuu, lakini kwa upande wa zanzibar pia, Katiba yake inamtambua Rais wa Zanzibar kama mkuu wa "nchi" ya Zanziba na mkuu wa majeshi ya serikali ya mapinduzi.

Kutokana na mkinzano huu, itakuwa ni vigumu sana kwa uchaguzi mkuu ujao kufanyika bila ya aidha katiba ya
Zanzibar kufanyiwa marekebisho irudi katika hali yake ya kabla ya 2010, au Katiba ya JMT (1977) ifanyiwa marekebisho kukidhi haja za Zanzibar.

Lakini sote tunajua kwamba: Hakuna kiongozi yoyote wa CCM ambaye anaweza irudisha zanzibar nyuma. Hii ni kwasababu wazanzibari walishaamua kupitia kura ya maoni. Na ili zanzibar iweze kufanyia katiba yake mabadiliko itahitaji tena theluthi mbili ya kura ya maoni jambo ambalo halitatokea.

Lakini vilevile, kuirekebisha katiba ya JMT iendane na mabadiliko ya katiba ya zanzibar (2010) ni kuvunja muungano kwa mlango wa nyuma. Hii ni kwa sababu serikali mbili "zilizoboreshwa" ni suala ambalo halita tekelezeka, sana sana litazidisa migogoro na kero kwa pande zote mbili za muungano, na hatimaye kuvunja muungano.

CCM inaweza kufanikiwa kuwa at an advantage iwapo bunge la katiba litavunjwa, lakini mafanikio hayo yatakuwa "short lived" kwani hayatajibu sehemu kubwa ya kero za muungano za zaidi ya miaka 30 zinazotishia uhai wake. Sana sana, CCM kupitia kina Kinana, Wassira, lukuvi, Sitta, Nape watatumia fedha za walipa kodi wa Tanganyika kuwapa zanzibar kila watachotaka ili mradi tu waridhie serikali mbili zilizoboreshwa kuelekea uchaguzi mkuu ujao. Lakini Ukweli ni Kwamba Serikali hizi zitaishia kuzidi kuwaamsha watanganyika kutoka usingizini na kupelekea watanganyika kutambua jinsi gani serikali mbili zinavyowanyima haki yao kama mshirika wa pili wa muungano. Hali hii itajenga chuki kubwa baina ya wananchi wa pande zote mbili ambapo kwa upande wa zanzibar, serikali mbili zilizoboreshwa zitawapa mamlaka kwa mkono wa kulia na kuwapokonya kwa mkono wa kushoto na kwa upande wa watanganyika, gharama za kubeba nchi jirani badala ya kodi zao kutumika katika huduma za kijamii na kiuchumi kupitia Tanganyika as a subnational government kama ilivyo kwa SMZ ni suala ambalo litawasukuma wananchi wa upande wa bara kudai Tanganyika yao. Kitendo cha ccm kuwakatalia Haki yao hii ya kikatiba kitapelekea muungano kuvunjika.

Mwisho - ingawa Mkinzano uliopo kikatiba utaweza pelekea kutofanyika kwa uchaguzi wa serikali ya Jamhuri ya Muungano, chini ya katiba ya zanzibar (2010), nchi hii jirani haita athirika na hali hii. Kwa maana nyingine, uchaguzi wa Serikali ya muungano unaweza kukwama iwapo mabadiliko ya kikatiba hayata tokea, lakini hali hii haitazuia nchi jirani ya zanzibar kufanya uchaguzi wake mwakani (2015). Hii ni kwa sababu, ukitazama katiba ya Zanzibar katika ukurusa wa 17-18, inajadili ukomo wa rais na sababu za kushindwa kufanyika kwa uchaguzi mkuu zanzibar. Ibara ya 29 ya katiba hiyo inatamka kwamba:

"Ikiwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imo katika VITA na ikiwa Rais anaona kuwa ni muhimu kuzuia uchaguzi, baraza la wawakilishi linaweza kupitisha azimio, kuzidisha muda wa miaka mitano uliotajwa kwenye kijifungu (2) cha 28 katika kipindi hadi kipindi lakini hakutakwa na kipindi kitakachozidi miezi sita mfululizo.".

Kwa maana hii, iwapo uchaguzi wa serikali ya muungano utakwama mwakani kwa sababu tulizojadili awali, Zanzibar wataendelea na uchaguzi wao, vinginevyo kukwama kwa uchaguzi wa serikali ya muungano kuambatane na "vita". Ukawa wajiadhari na kusingiziwa Kwamba ni chanzo cha vita na machafuko.
]

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Lakini kitu kingine ulichokiacha, kwa nini husuggest Ukawa waende mahakamani kzuia mchakato iwapo wana msingi wa kisheria wa kufanya hivyo?- ninachokiona ni kwamba wanaleta Siasa katika mchakato huuu na kwa kuwa hawana wingi wa kura za kufanya maamuzi jamii itawaona kama watu wanaotaka kuvuruga tu. KAMA WANA HOJA NZITO ZA KISHERIA NI RAHISI KUKUSANYA NGUVU ZA KISIASA KWA NINI HAWATAKI OPTION HII KAMA WANA NIA NJEMA?

UKAWA wanastahili kwenda Mahakamani kufungua Kesi inayohusiana na uchakachuaji wa Sheria ya mabadiliko ya katiba. kumekuwepo mjadala mkali unaohoji mamlaka ya bunge hilo juu ya rasimu ya katiba iliyowasilishwa na tume. Katika mijadala hii, wapo waliojadili kwamba bunge hili lina mamlaka ya kubadilisha na hata kuondoa chochote itakachoridhia, huku upande mwingine wa hoja ukijadili kwamba hilo haliwezekani. Makada wengi wa ccm wamekuwa kwenye upande unaojenga hoja kwamba bunge hili lina uwezo wa kubadilisha na hata kuondoa vifungu mbalimbali vitakavyo ridhiwa; nadhani Kikwete atagusia hili, huku akiegemea kwenye hoja ya makada wa ccm;

Ukweli unabakia wazi kwamba bunge la katiba halina mamlaka ya kubadili rasimu kama ilivyowasilishwa na tume ya mabadiliko ya katiba. Kuna tatizo moja kubwa:

Kifungu cha 25(2) kikisomwa kwa kiingereza kinaweka suala hili la bunge kutokuwa na mamlaka hiyo lakini tafsiri yake kwa kiswahili ndio imetoa upenyo kwa wavurugaji kuingiza siasa zao. Pamoja na haya, ujumbe wa kifungu hiki kisheria ni kwamba- rasimu hii, kama itakavyowasilishwa na tume ya mabadiliko ya katiba ndiyo itakuwa msingi wa utekelezaji wa madaraka ya bunge katika kutengeneza/kuandika katiba mpya; kwa maana hii:

Kitu ambacho BLK lina uwezo wa kufanya ni kuboresha au kuongeza hapa na pale lakini bila ya kuathiri msingi mkuu wa rasimu hiyo. Hivyo rasimu inabakia kuwa ndiyo mhimili mkuu wa katiba mpya inayotarajiwa; professor Lumumba aliweka wazi Kwamba tutakuwa ni taifa la kwanza kufanya hivyo in the region.

Nimejaribu verify uelewa wangu huu na wataalam wa sheria, wanasema nachojadili ni sahihi na kuongeza kwamba-bunge la JMT lilitunga sheria ambayo haikulipa bunge la katiba mamlaka ya kubadili vifungu vya rasimu kwa jinsi inavyofaa; na iwapo bunge la JMT lingekuwa limetunga sheria hiyo, basi ingesemwa wazi kwani sheria huwa haipindi pindi mambo bali hunyoosha mambo, hivyo sheria ingetungwa na bunge la JMT kusema kitu kama vile:

"Bunge la katiba halitafungwa kwa namna yoyote ile na rasimu ya katiba."

Au sheria ingetumia maneno yanayofanania na haya; hatujaona haya; vinginevyo kwa jinsi sheria inavyotamka hivi leo, ukweli ambao hauepukiki ni kwamba rasimu ya katiba ilikusudiwa kuwa mhimili na msingi mkuu; tatizo lililojitokeza ni kwamba tume iliamua kutojifunga na matakwa ya chama, na huu ndio msingi wa porojo za sasa za kulitafutia bunge la katiba nguvu ambazo haizistahili;

Kuna hoja pia inayojadiliwa kwamba bunge la katiba kupitia kifungu 25(1) cha sheria husika kinalipa bunge hili mamlaka yasiyo na mipaka katika kujadili na hata kubadilisha vifungu vyote vya rasimu; kifungu hiki kinasema kwamba:

"Bunge la katiba litakuwa na mamlaka ya kutengeneza katiba mpya na kutengeneza vifungu vitakavyohusiana na ufanyaji kazi wa katiba hiyo."

Katika hili, nimepata nafasi ya kumsoma wakili peter kibatala ambae anasema:

["Namna bora ya kutafsiri vifungu vya 25(1) na (2) ni kuvipa uhai vifungu vyote viwili bila ya kuathiri kimojawapo kiasi kwamba kisiwe na maana kabisa. Hii ina maana kwamba ilikuwa lazima kifungu cha 25(1) kiwepo ili kulipa bunge mamlaka kujadili rasimu na kuliongezea nyama inapobidi - kisheria tunaita enabling provision au substantive provision."

Kifungu cha 25(2) unaweza sema ni kifungu elekezi cha namna ya bunge kutekeleza mamlaka yake (procedural provision) - maelekezo yanayojumuisha mipaka ya mamlaka hiyo.

Mipaka na mamlaka ni sehemu muhimu ya mamlaka ya chombo chochote cha kisheria kwani huelezea wapi uhalali wa mamlaka husika huishia.

Kifungu hiki cha 25(2) kitashirikiana a kanuni za bunge katika kuweka misingi ya bunge kufanya kazi zake za kujadili rasimu ya katiba.

Ukiacha tafsiri ya kifungu husika ambacho kinaweza kubishaniwa, namna nyingine ya kutafsiri sheria ni kuangalia mazingira yaliyozunguka kifungu cha sheria husika.

Mchakato wa kuandaa rasimu ulianza kwa tume kukusanya maoni ya wananchi na kisha kuandaa rasimu ya kwanza. Rasimu hiyo ikafanyiwa kazi kwa njia ya kupatiwa mabaraza ya katiba na njia nyingine na kisha tume ikachukua maoni kutoka huko na kuandaa rasimu ya pili ambayo ndiyo hii iliyopelekea bunge kujumuika tayari kuijadili. Swali kuu la msingi ni:

Je, michakato yote hii ya awali iliyojumuisha wananchi moja kwa moja ilikuwa na maana gani iwapo tena kila kitu kinaweza kufumuliwa kwa kadri ya utashi wa bunge la katiba?

Hapa siyo sahihi kusema kwamba michakato yote miwili inapumuliana na kubebana (complement each other).

Na pengine ni mchakato upi unaowapa wananchi sauti ya moja kwa moja katika katiba mpya kati ya rasimu iliyosheheni maoni yao na bunge la katiba ambalo halijachaguliwa moka kwa moja na wananchi; na wala wananchi hawana namna yoyote ile ya kulidhibiti?

Mtu anaweza kuja na hoja kwamba bunge la katiba linajumuisha wabunge waliochaguliwa moja kwa moja na wananchi, na hivyo wanawakilisha maoni yao;

Hoja hii ingekuwa na nguvu iwapo maelekezo ya mchakato mzima kwa mujibu wa sheria yangekuwa kwa tume kukusanya maoni na kuandaa rasimu na kisha kuyawasilisha katika bunge la JMT na baraza la wawakilishi ili yajadiliwe na kisha kupelekwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura ya maoni.

Mchakato wa namna hii ambao binafsi ningeupendelea zaidi ungebakisha umiliki wa mchakato mzima na hasa rasimu yenyewe na hatimaye katiba, moja kwa moja kwa wananchi;

Huu ungefanana na njia ambayo wenzetu wa Kenya walipitia, ambapo ile rasimu maarufu kama rasimu ya Bomas (Bomas Draft) ndio ulikuwa msingi mkuu wa majadiliano bungeni (bunge la kawaida) kabla ya kufikishwa kwa wananchi kwa kura ya maoni."]

Kuna suala lingine muhimu kibatala anajadili kuhusiana na sintofahamu kubwa inayoweza tokea iwapo BLK litafanya kosa linalopigiwa debe na makada wa CCM ambapo Anasema Kwamba:

"Tufikirie tu kwa mfano bunge la katiba linaamua kwamba linaweza kubadilisha vitu vyote vya msingi katika rasimu na katiba inapelekwa kwenye kura ya maoni na kupitishwa na baadae mahakama inasema tafsiri sahihi ya sheria ni kwamba rasimu haikutakiwa kubadilishwa na bunge la katiba."

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nguruvi3,

Asante kwa kuleta mjadala muhimu. Kuna mambo muhimu Sana ambayo Umejadili, nitajadili maeneo yote muhimu kwa kadri mjadala utakavyoendelea. Kwa sasa ningependa kujadili eneo moja muhimu - nalo ni kuhusiana na haja ya ukawa sasa kuchukua leadership role na kuzungumza na wananchi kwa lengo la kuwatolea ufafanuzi juu ya mengi ambayo bado yana wachanganya. Kwa vile wananchi walio wengi wamependekeza serikali Tatu badala ya Mbili au moja, approach ya ukawa sasa iwe kuwaelezea wananchi kwanini walichochagua kupitia tume ndicho kitawaweka on the right side of history hata Kama ni miaka 100 kutoka sasa. Yapo masuala kadhaa ambayo ningependa kuyawasilisha kwa mtindo wa nadharia tete ili kuchokoza mjadala na maeneo hayo in my humble view Ndio Yale ambayo ukawa wanatakiwa kuyafanyia kazi as they engage na wananchi kuanzia sasa:

1. Wananchi wengi wa upande waTanzania bara bado wanaona Kwamba haja ya serikali Tatu is more of a matter of retaliation on Zanzibar kuliko the fact Kwamba suala la establishment and existence of Tanganyika is a matter of principle. Kwa maana nyingine, kwa wananchi walio wengi bara, bado Hawana uelewa wa kutosha Kwamba Haiwezekani kuwepo serikali Mbili ndani ya nchi Mbili. Ndani ya nchi Mbili kunakuwepo na serikali moja au serikali Tatu, basi".

2. Mwalimu aliweka wazi mwaka 1994 Kwamba Tanganyika sio sera ya CCM, badala yake, sera ya CCM ni serikali Mbili, kuelekea moja. Katika Hali ya sasa, hata tume ya warioba imejiridhisha Kwamba Tanzania haiwezi tena kuwa na serikali moja. Malengo ya serikali Mbili kwa nchi moja yalishakufa na kuzikwa na waasisi wa muungano - mwalimu Nyerere na sheikh karume.

3. Wananchi wengi wa upande wa Tanzania bara Hawaelewi Kwamba Zanzibar hawawezi kurudi tena nyuma kikatiba na kujitambulisha tena Kama ni "Zanzibar sehemu ya jamhuri ya muungano wa Tanzania", Kama ilivyo kwenye katiba ya sasa ya JMT (1977) Toleo la 1995. Zanzibar itaendelea kuwa nchi, na CCM itaendelea kuwapa Zanzibar kila wanachotaka ili mradi sera ya CCM ya serikali Mbili iendelee kuwepo, huku wananchi wa Tanzania bara wakibebeshwa gharama za kuwabembeleza Zanzibar.

4. Mgogoro juu ya Mgawanyo wa Mapato ya muungano na uchangiaji wa gharama za kuendesha muungano Kati ya serikali ya muungano na serikali ya mapinduzi ya zanzibar hauwezi kumalizwa kwa kuruhusu wazanzibari kuagiza bidhaa kutoka nje, kukopa nje, na kuendesha uchumi wa Zanzibar bila ya kupitia au kudhaminiwa na Tanzania bara. Vyama vya CCM na ACT vina mtazamo huu Kama sehemu ya suluhisho la mgogoro wa muungano, mtazamo ambao haupo sahihi.

5. Mfumo we Serikali Mbili zilizoboreshwa na CCM ambazo zinalenga kuipa Zanzibar mamlaka kamili bado utaibua Madai mapya ya Zanzibar juu ya kuwa nchi kamili. Hakuna mamlaka kamili Zanzibar bila ya uwepo wa Tanganyika.

6. Iwapo CCM itafanikiwa kuleta serikali Mbili zilizoboreshwa, hii itakuwa ni kwa faida ya Zanzibar na kwa hasara ya Tanganyika. Hali hii itapelekea wananchi wa Tanzania bara kudai Tanganyika kwa Nguvu Kama alivyoeleza professor Kabudi. Kwa maana nyingine, jinsi CCM inavyoZidi kuboresha serikali Mbili ndivyo jinsi watanzania bara wanavyozidi kukosa Haki zao za kisiasa, kijamii, na kiuchumi (political, social and economic justice) ambazo zitakuja leta vurugu na vita. Kwahiyo serikali Mbili zilizoboreshwa ni "timing bomb" ambalo ni wajibu wa ukawa kuwaelezea wananchi Kwamba wajibu wa kulitegua ni wananchi wenyewe.

7. Wananchi wengi wa upande wa bara Hawaelewi athari za katiba ya Zanzibar (2010) kwa Tanganyika na kwa muungano kisiasa, kiuchumi na kijamii. Kisiasa, rais wa muungano ambae ndiye rais wa Tanganyika ni rais boya. Rais wa muungano ambae pia ni rais wa Tanganyika hatokuwa na uwezo wa kuilinda na kuitetea Tanganyika chini ya katiba iliyoboreshwa. Kiuchumi, chini ya serikali Mbili zilizoboreshwa, muungano utamhudumia mzanzibari kuliko mtanzania bara. Na kijamii, utambulisho wa mtanzania utafifia zaidi chini ya nchi Mbili Zenye serikali Mbili kuliko uzanzibari. Matokeo yake ni Kwamba Kama taifa, tutajenga Kizazi ambacho hakitaweza jitambua Huko Mbeleni.

Kwa mtazamo wangu, hayo Ni baadhi ya maeneo ambayo ukawa wanatakiwa kuyazingatia in their dialogue na wananchi.

Sent from my iPhone using JamiiForums

Mchambuzi kwa hali ya sasa naweza kusema tukiangalia sababu zote kisiasa, kiuchumi na hata kijamii, naweza kusema CCM iko kwenye upande usio sahihi kabisa wa hoja na wa historia. Economic injustice inayofanywa na Zanzibar kwa bara imekuwa chungu kutokana na kauli za kejeli na matusi kutoka Zanzibar. Wabara wana sababu za msingi kutaka serikali, kwa kuwa serikali ya JMT imeshindwa kabisa kuaddress economic injustice.

Lakini naweza kuungana na Profesa Kabudi kuwa kama CCM ikiwa ni chama tawala itashindwa kuleta serikali ya Tanganyika in any acceptable form, watanganyika wataitafuta wenyewe, by hooks and crooks. wanaweza kuzuga na kukwepa sasa lakini kesho hawatakwepa.

As i see it, for Tanganyikans S3 is not only a matter of necessity, but also a matter of principal, for CCM is a matter of opportunity. By embracing S3, CCM will be doing a first major step in reversing its irrelevance among Tanzanians, bara na visiwani.
 
Nguruvi3 et al,
Nakuelewa na kuafikiana nawe... Swali ni kwamba njia sahihi ya kuidai Tanganyika unadhani ni ipi? Unadhani msimamo wa UKAWA (which is a misnomer) kususia bunge utatusaidia kupata Tanganyika yetu? Isingekuwa vema kuteta hoja humo humo bngeni kwa uwazi na umahiri na sisi watazamaji tushawishike kupigia kura S3 na si S2?
Swali la huyu ndugu ni zuri sana kwasababu kuu moja, watu wengi hawaelewi mantiki ya UKAWA kutoka. Wanadhani UKAWA wamekimbia tu, bado walikuwa na nafasi ya kujenga hoja kwa kulumbana na wenzao.

Kwanza, Mwanagenzi ningalikuomba sana usome bandiko# 12 la Mchambuzi hapo juu.
Lina majibu ya swali lako kimantiki sana. Nitajaribu kushadidia majibu hayo kwa uchache tuelewane na kufahamishana.

Ukisoma sheria, zinasema kuwa rasimu ndio msingi wa uandikwaji wa katiba.
Maana yake ni kuwa umeshanunua kiwanja, umechimba msingi, umeshajenga msingi hadi magotini.
Kila mtu anafahamu nyumba yako itakuwa na vyumba vingapi n.k.

Fundi anayekuja kujenga juu ya ule msingi anaweza kuamua aina ya matofali bila kuathiri uzito wa msingi au kubadilisha.

Anaweza kuboresha muundo wa vumba bila kuathiri msingi. Mfano, anaweza kuweka partition ndogo za kugawa vyumba, anaweza au jiko kwa kutumia mbao n.k. ili mradi tu ongezeko au punguzo la maboresho hayo halitaathiri msingi wa nyumba

BMK lilipokaa lilikusudiwa kujadili rasimu katika msingi wake. Lina uwezo wa kufanya maboresho bila kuathiri msingi wa rasimu.

Kumbuka rasimu yote imeandikwa kwa kuzingatia maoni ya wananchi waliotaka muundo wa S3.
Hivyo msingi wa majadiliano na vifungu vyote ni S3 na maboresho yanaruhusiwa si kuharibu msingi bali kuboresha juu ya msingi.

Kilichopaswa kufanya ni kufanyia maboresho na kisha kuipeleka kwa wananchi kuikubali au kuikataa kwa kura ya maoni.

Wananchi wangekataa, option ilikuwa kurudi na kuangalia mifumo ya S1,S2,Mkataba n.k.

Katika hali ya kushangaza, CCM hawakujadili msingi, walileta maoni ya S2.

Hii maana yake ni kuwa rasimu nzima msingi wake umeharibiwa.
Nani aliwaambia wapendekeze mfumo? Mfumo ulishapendekezwa, walichotakiwa kufanyia kazi ni maboresho ya msingi.

Kuingiza S2 kulimaanisha CCM wamebadilisha msingi halafu wanataka kutumia wingi wao kupitisha msingi ambao wananchi hawakuupendekeza.

Hivyo kuendelea kupambana kwa hoja ilikuwa kujidanganya, na ndio sababu ya UKAWA kuondoka.
UKAWA hawakatai kujadiliana kuhusu katiba, wasichotaka ni kuingiza mambo nje ya rasimu.

Mfano wa nyumba niliokuambia una maana hii. Wewe umempa ramani fundi ikiwa na msingi.

Kesho unakwenda fundi anasema tumebomoa msingi na kujenga mwingine, sasa si vyumba 3 ni vyumba 2.

Fundi uliye mwajiri anakuambia, amebomoa msingi wote wa ramani ya nyumba yako, hivyo rudi ukamuulize mkeo kama anakubaliana na hili.

Huyo mkeo mliyekuwa naye wakati msingi wa vyumba 3 ukijengwa, si kuwa atakuona mwendawazimu ana haki ya kukutaliki maana wewe ni bogus.
 
Mchambuzi# 12
Nikumbushe kidogo kuwa hata kanuni za awali za BMK ziliweka wazi kuhusu mjadala.
UKAWA walipoondoka kanuni (sina uhakika, 33?) ikabadilishwa na kuingiza kifungu kinachowezesha ubadilishaji wa rasimu

Kitendo kile kilimaanisha kuwa CCM walikuwa wanatafuta namna ya kubadilisha rasimu tu.

Lakini pia CCM hawawelezi kwanini S2 na si S1 au mkataba ili kukidhi haja ya kila kundi?

Cha muhimu hapa ni kuwa kama CCM wanajadili rasimu ya maoni ya wananchi, watarudi kuwaeleza wananchi wapigie kura kitu gani?

Wananchi walisema S3, wanapopelekewa S2 hapo ina maana gani? Kwamba maoni yao hayakusikilizwa au?

Endapo hayakusikilizwa, yale ya mkataba je kwanini hayakupewa kipaumbele ili hali yalikuwa na wingi kuliko S2?

BMK likibidalisha wanachosema wananchi, kulikuwa na sababu gani za kuunda tume?
Kwanini liitwe bunge na kuamua hatima ya katiba? Na kama wananchi walisikilizwa, ni jambo gani walilosikilizwa?
 
Gamba la Nyoka,
Mbali ya UKAWA kuwa na uwezo wa kufungua Kesi Mahakamani Kama nilivyojadili na pia Kama Nguruvi3 alivyotoa ufafanuzi hapo juu, sisi wananchi pia tunaweza fanya hivyo. Kumbuka Kwamba sura ya 83 ya Sheria ya mabadiliko ya katiba inatupa sisi wananchi mamlaka. Kwahiyo mamlaka tuliyonayo ni kwa Mujibu wa Sheria. Kitendo cha CCM kuondoa maidhui ya rasimu yaliyojadiliwa na nguruvi3 hapo juu na kuingiza rasimu ya mafichoni ni kupora mamlaka na madaraka ya wananchi ambayo yapo kwa Mujibu wa Sheria ya mabadiliko ya katiba (2011).

Kwahiyo Kama BLK Mjini Dodoma linaendelea kujadili rasimu ya mafichoni badala ya rasimu ya tume ya warioba, wanachofanya Hawa Watu Dodoma ni kukusanya tu posho kitu ambacho kimsingi ni kupora fedha wa walipa kodi. Huu ni uhalifu Kama uhalifu mwingine wowote na hatua za haraka ni lazima zichukuliwe.

Cc chama, MwanaDiwani, Nape Nnauye, Mwigulu Nchemba, Ritz, Simiyu Yetu, Happy Feet, HKigwangalla, zomba, Jasusi, JokaKuu, Kobello, Mag3 Pasco, Dingswayo, MTAZAMO Mimibaba, Ezekiel Maige, Mzee Mwanakijiji, ASHA dii, EMT, Bongolander, Mtanganyika tpaul, Fue Fue

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Kuna ushahidi wa kutosha wa Kauli za wajumbe wa Tume na pia wa data unaoonyesha wazi kwamba Conclusions za Serikali tatu zilifikiwa SI KWA SABABU WANANCHI WALISEMA TATU MOJA KWA MOJA, BALI MCHANGANUO WA HOJA ZA WANANCHI KWA KUTUMIA "BUSARA NA HEKIMA NA UFAHAMU NA UTAALAMU" WA TUME NDIYO WAKAFIKIA HIYO CONCLUSION YA KWAMBA "WANANCHI WANATAKA SERIKALI TATU".

Nimemsikiliza mjumbe mmoja wa Tume (ndugu PolePole) wakati akihojiwa na kituo kimoja cha television cha Clouds Tv, akisema, Suala la serikali tatu kimsingi halikutokana na Takwimu, bali lilitokana na Hoja na Sababu, Then Tume walipoona Sababu na Hoja za serikali Tatu ni nzito kuliko nyinginezo TUME IKAAMUA KUPENDEKEZA SERIKALI TATU.
PolePole alisema, wakati mwingine mtu anataja serikali mbili, lakini ukimuuliza anakwambia mambo ya muungano yawe mengi!, kwa msingi huu tume inaconclude kwamba huyu basically ANATAKA TATU!!!.

Hivyo basi, Vyombo viwili vilivyobaki katika kutengeneza mchakato huu yaani , Bunge Maalum la Katiba na Kura za maoni ya Wananchi hawana budi kujiridhisha kwa kuangalia Methodology zote zilizotumiwa na Tume zilizoifanya Tume Iseme Wananchi wanataka tatu!!!. Kama tume wako honest, au mdau yoyote hana haja ya kuogopa jambo hili, kwa sababu Randama ipo, Video tapes za mahojiano na wananchi zipo. HUENDA CONCLUSION MPYA YA WANANCHI WANATAKA EXACTLY SERIKALI YA AINA GANI IKAPATIKANA!!!. SHERIA HAIJAKATAZA KUICHAMBUACHAMBUA RASIMU KWA MUKTADHA HUU .
Itakuwa ni jambo la ajabu, tume ituambie 1+1 ni 3 halafu tuseme eti kwa kuwa Tume imekusanya maoni ya wananchi basi hilo jibu ni jibu la wananchi na halitakiwi kupingwa!!. HAPA NAMAANISHA KAMA TUME IMEZITAFSIRI VIBAYA HOJA NA TAKWIMU ZA WANANCHI THEN BUNGE MAALUM LA KATIBA LINA HAKI NA WAJIBU WA KUSAHIHISHA HILO!!, NDIYO MAANA NINASEMA WABUNGE WA BMT WANA HAKI YA KUICHIMBA RASIMU NA KUJA NA CONCLUSIONS MPYA KAMA KWELI ZINA MASHIKO YANAYOSAPOTIWA NA MAONI HAYO YA WANANCHI!
Lakini Wait a minute!!: Kwa hoja hii sisi wengine tuna wasiwasi kwamba Busara na Hekima za tume inaweza zisitoshe, na Kwa kuwa wao ni binadamu Huenda analysis yao na conclusion yao Ikawa Wamekosea!, kwa kauli ya PolePole ni uthibitisho tosha kwamba kumbe katika Mapendekezo ya hizo tatu huenda wamewasemea wananchi badala ya wananchi kujisemea wao wenyewe!!

Mimi ninasema, kama ile Rasimu imetokana na maoni ya wananchi, then ninaamini kama wananchi wataletewa Katiba iliyopendekezwa isiyokuwa na maoni yao WATAIKATAA! na kutokana na hoja hii Ukawa hawana budi kupambana ndani ya bunge ili wananchi waone wana watetezi wao! na hii ina faida zifuatazo
1. Pesa nyingi hazitapotea kwa kuendelea na vikao ambavyo huenda mchakato ukakwama baadae
2. Ukawa kwa kutokushiriki vikao watajiweka katika hali ngumu kisiasa ikiwa CCM itafanikiwa kuipitisha katiba, HALAFU WANANCHI WAKAAMUA KUIKUBALI.
3.Ukawa watakuwa na Mtaji wa Kisiasa wa Kuzunguuka kupiga Campaign ya kuikataa Katiba iliyopendekezwa, wasiposhiriki katika vikao halafu wakashiriki katika campaign ya kuikataa katiba itakayopendekezwa na bunge la CCM watahesabika pia kwamba WAMESHIRIKI KATIKA MCHAKATO WA KATIBA ANYWAY! na hapa watakuwa weak mno kuelekea katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015
 
Gamba , tena hapa iunatusaidia sana kujenga hoja ya S3. Ahsante.

1. Tambua tume ilikutana na wananchi wa aina mbali mbali. Mwananchi anaposema 'na sisi tunataka yetu kama wenzetu wa znz'' ni wajibu wa tume kufafanua kauli ililenga nini.

Mwananchi anaposema serikali zetu za Tanganyika na znz ziunde chombo cha pamoja cha muungano, ni wajibu wa tume kuchambua na kufahamu alikusudia nini.
Hivyo takwimu ni sehemu ya, muhimu ni uchambuzi (analysis) ya mantiki hali.

2. Rasimu ilikuwa na awamu mbili, ya kwanza ilikuja na pendekezo la S3.
Hakuna aliyehoji takwimu au uchambuzi na conclusion.
Awamu iliyofuata ni mabaraza ya kata, hakuna aliyehoji S3 isipokuwa kujenga juu ya msingi uliokuwepo.
Kitendo cha CCM kuhoji katika final draft ya tume, kwanza kinamdhalilisha Rais.

Rais alipokeaji kitu asichojua kilikusudia nini na akasifu uadilifu na kazi ngumu.
Rais alisaini vipio nyaraka iliyolenga 'kupotosha' umma kitakwimu na uchambuzi

3. CCM walifahamu tume ya Warioba eti 'imechakachua''.
Well , walichopaswa kufanya ni kuagiza mwenyekiti wa CCM ambaye ni Rais, kusimamisha mchakato ili wananchi watendewe haki, au kufuta tume kabisa. CCM hawakufanya hivyo

4. CCM wanajadili maoni ya tume ambayo wanasema imechakachua takwimu. Hapa ndipo unaona wendawazimu fulani.Hivi unawezaje kufanyia kazi nyaraka ambayo huamini uhalali wake?
Leo wapo Dodoma wanafanyia kazi nyaraka ambayo Gamba anasema imefojiwa?

Kuhusu UKAWA, nadhani lengo ni kupinga udhalimu kwa njia yoyote. Hivyo sioni wapi wata loose.
Hata hivyo naungana nawe kuwa encourage wafanye kazi haraka sana ya kuelimisha umma.

Katiba inaweza kupita tu hata kuiba kura za maoni. Jambo moja ambalo wewe na wengine wetu hatuwezi kulikwepa ni kuwa hiyo itakuwa ni template nzuri sana ya vurugu nchini.

1. Watanganyika wataidai Tanganyika yao katika njia ambazo ni nje ya majadiliano
2. Wazanzibar watakuwa wahanga wa katiba hiyo, na pengine wakajikuta katika wakati mgumu sana kimaisha
3. Rais ajae awe wa CCM au Upinzani atakuwa na kazi ya kutumia FFU na si kupanga maendeleo.

Kumbuka mwaka 1965 Nyerere alipiga marufuku vyama vingi. Mfumo huo ukarudi akishuhudia kwa macho yake.
Nyerere alikataa tusiwe mawe, akashuhudia tukigeuka na kuwa minara ya chumvi.
Nyerere aliwazima G55. hoja ya Tanganyika haijawahi kufutikana leo ina nguvu kuliko miaka 20 iliyopita

CCM wanaweza kubadili katiba yao na kuwa ya nchi na kutumia bunge kupitisha.

Je, hilo unadhani lina afya kwa ustawi wa taifa na kila mmoja wetu?

Tafakari

Wanajamvi hakika nimebaki nimeduwaa, najaribu kujiuliza ni kitu gani kinaendela ndani ya hicho kikao anachokiongoza Samwel Sitta, sipati jibu. Sura ya sita ya rasimu ya Katiba kama ilivyowakilishwa bungeni na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ndiyo msingi unaotakiwa ubebe misingi mikuu ya taifa, uweke malengo ya Taifa, ulinde Haki na Usawa kwa Wananchi, utetee Uraia wa Wananchi, uheshimu Alama na Sikukuu za Taifa, utunze Tunu za Taifa, uhimize Maadili ya Viongozi na Miiko ya Uongozi...na inasema hivi, nanukuu;
Rasimu 12.11 Muundo wa Muungano said:
Muundo wa Muungano ni moja ya mambo muhimu ya kikatiba. Kuwepo kwa Jamhuri ya Muungano ni moja ya mambo ambayo Sheria ya Mabadiliko ya Katiba imeyaweka katika masuala ya kuzingatiwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mapendekezo yake. Tume inapendekeza kuendelea kuwepo kwa Jamhuri ya Muungano ambayo ni nchi moja yenye Muundo wa Shirikisho lenye Serikali tatu ambazo ni:

  1. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
  2. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; na
  3. Serikali ya Tanganyika.
Rasimu inapendekeza kwamba, Serikali ya Jamhuri ya Muungano ndiyo iwe na mamlaka ya kutekeleza Mambo ya Muungano. Aidha, Rasimu ya Katiba inapendekeza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano inaweza kutekeleza mambo yasiyo ya Muungano yanaohusu Serikali ya Zanzibar au Serikali ya Tanganyika endapo kutokana na makubaliano na masharti maalum. Kwa hiyo, kwa mujibu wa Rasimu ya Katiba mamlaka ya Serikali ya Tanganyika au Serikali ya Zanzibar ni kwa mambo yasiyo ya Muungano tu na siyo vinginevyo.

Mfumo wa serikali tatu kwenye rasimu ndio dira kuu ya mchakato wa katiba mpya na hivyo mpango wowote wenye lengo la kubatilisha kifungu hicho unafuta uhalali wa rasimu nzima. Bunge la Katiba kuendelea na vikao vyake vinavyohusu vifungu vingine vya rasimu, ni ulaghai na utafunaji tu wa pesa za walipa kodi wa nchi na ni vizuri lisitishwe mara moja. Kama hilo halitafanyika, hao wanafiki na walafi wajue iko siku watawajibika kwa walipa kodi wa nchi hii.

Ni wazi kumefanyika jitihada kubwa kuficha baadhi ya nyaraka za Tume ambazo kwa kiasi kikubwa ziliisaidia Tume kufikia pendekezo la serikali tatu. Katika hizo nyaraka, zipo zenye maoni yaliyorekodiwa ama kwa video au kwa sauti ya Maofisa wa serikali na Viongozi wa CCM wakipendekeza mfumo wa serikali tatu...leo watu hao hao, ama kwa uoga, unafiki, au ulafi wa pesa wako ndani ya BMLK wakilamba matapishi yao bila soni wala haya, shame on them!
 
Mag3,

Tatizo lililopo ni Kwamba Mwenyekiti wa Hilo bunge haweki maslahi ya taifa Mbele Bali maslahi binafsi ya posho na ya urais 2015. Kwa mfano, kwa Mujibu wa vyanzo vya uhakika, posho ya Sitta kwa siku 84 za bunge la katiba zitakuwa jumla ya shillingi milioni 150. Je unatarajia nini kwa kiongozi ambae Ana rekodi ya kujenga ofisi ndogo ya uspika jimboni kwake kwa gharama za walipa kodi shillingi milioni 500, ofisi ambayo sio Anna Makinda Wala maspika wajao wataitumia?

Sitta anaishi kwenye nyumba oysterbay inayogharamiwa na walipa kodi zaidi ya shillingi milioni kumi kwa mwezi Kama kodi, nyumba ambayo ilitakiwa ampishe spika Makinda lakini akagoma, sasa tutarajie nini kwa kiongozi wa aina hii Huko Dodoma ambako posho Ndio habari ya Mjini?

Pia tunajua uzoefu wake wa siasa za ubabe na kupinda mambo, mfano alivyowasha na kuzima hoja ya Richmond bungeni pre maturely. Majuzi ametishia ITV kwa sababu inasimamia upande wa wananchi. Anasahau Kwamba Wakati wa Sakata lake na the so called mafisadi, hakuna media org iliyompa air time Kama itv, kuanzia kipindi cha Dakika 45 hadi Sakata la mwakyembe kulishwa sumu.

Leo Sitta anaenda Mbali na kuamuru masuala ya Tanzania bara yaingizwe kwenye katiba ya muungano ili kuua hoja ya tanganyika. Kuna taarifa Kwamba anapita Kamati hadi Kamati na kuamuru nini cha kuwekwa. Kiongozi wa aina hii hatufai, ataipasua nchi vipande vipande kwani ameonyesha wazi Kwamba:

1. Hajali matakwa ya wananchi.
2. Hajali Sheria - amekiuka Sheria ya mabadiliko ya katiba (2011).
3. Hana hulka ya kuheshimu katiba ya nchi.
4. Mkandamizaji wa vyombo vya habari.
5. Hana nia ya Dhati ya kupambana na ufisadi na ubadhirifu wa Mali ya umma kwani Mbali ya Mifano hai hapo juu, pia amebariki ubadhirifu wa kulipana posho bungeni Katika suala ambalo mwisho wake tayari unajulikana - katiba ya wananchi haitopatikana.

Mamlaka ya mchakato husika yapo mikononi kwa wananchi kwa Mujibu wa Sheria ya mabadiliko ya katiba(2011), mamlaka ambayo Sitta Ameamua kuyapora. Huu ni uhalifu Kama aina nyingine zote za uhalifu.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom