Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
- Thread starter
- #21
Pamoja na hayo, pia kuna suala la credibility.Mag3,
Tatizo lililopo ni Kwamba Mwenyekiti wa Hilo bunge haweki maslahi ya taifa Mbele Bali maslahi binafsi ya posho na ya urais 2015. Kwa mfano, kwa Mujibu wa vyanzo vya uhakika, posho ya Sitta kwa siku 84 za bunge la katiba zitakuwa jumla ya shillingi milioni 150. Je unatarajia nini kwa kiongozi ambae Ana rekodi ya kujenga ofisi ndogo ya uspika jimboni kwake kwa gharama za walipa kodi shillingi milioni 500, ofisi ambayo sio Anna Makinda Wala maspika wajao wataitumia?
Sitta anaishi kwenye nyumba oysterbay inayogharamiwa na walipa kodi zaidi ya shillingi milioni kumi kwa mwezi Kama kodi, nyumba ambayo ilitakiwa ampishe spika Makinda lakini akagoma, sasa tutarajie nini kwa kiongozi wa aina hii Huko Dodoma ambako posho Ndio habari ya Mjini?
Pia tunajua uzoefu wake wa siasa za ubabe na kupinda mambo, mfano alivyowasha na kuzima hoja ya Richmond bungeni pre maturely. Majuzi ametishia ITV kwa sababu inasimamia upande wa wananchi. Anasahau Kwamba Wakati wa Sakata lake na the so called mafisadi, hakuna media org iliyompa air time Kama itv, kuanzia kipindi cha Dakika 45 hadi Sakata la mwakyembe kulishwa sumu.
Leo Sitta anaenda Mbali na kuamuru masuala ya Tanzania bara yaingizwe kwenye katiba ya muungano ili kuua hoja ya tanganyika. Kuna taarifa Kwamba anapita Kamati hadi Kamati na kuamuru nini cha kuwekwa. Kiongozi wa aina hii hatufai, ataipasua nchi vipande vipande kwani ameonyesha wazi Kwamba:
1. Hajali matakwa ya wananchi.
2. Hajali Sheria - amekiuka Sheria ya mabadiliko ya katiba (2011).
3. Hana hulka ya kuheshimu katiba ya nchi.
4. Mkandamizaji wa vyombo vya habari.
5. Hana nia ya Dhati ya kupambana na ufisadi na ubadhirifu wa Mali ya umma kwani Mbali ya Mifano hai hapo juu, pia amebariki ubadhirifu wa kulipana posho bungeni Katika suala ambalo mwisho wake tayari unajulikana - katiba ya wananchi haitopatikana.
Mamlaka ya mchakato husika yapo mikononi kwa wananchi kwa Mujibu wa Sheria ya mabadiliko ya katiba(2011), mamlaka ambayo Sitta Ameamua kuyapora. Huu ni uhalifu Kama aina nyingine zote za uhalifu.
Sent from my iPhone using JamiiForums
Sitta anafahamu kuwa tayari mbio za Urais zimeshamuacha.
Akiondoka bungeni utakuwa msumari wa mwisho katika 'jeneza' la kisiasa. Hivyo wakati anavizia milioni 150, pia anajaribu kuangalia kama kutatokea bahati mbaya itakayo okoa heshima yake.
Kwa maana hiyo ndio maana ameamua kuunda tume yake ya kukusanya maoni akiwa hapo bungeni.
Jana alikutana na Wafugaji, leo akakutana na wahairiri waliohongwa, wiki inayokuja anakutana na Wazanzibar.
Sitta amepewa wapi mamlaka ya kuunda tume yake mwenyewe na kujikusanyia maoni
Halafu hataki watu wazungumze wala vyombo vya habari viandike. Hoja kubwa huu mchakato ni mali yake na familia yake.
Sitta kaamua kuchukua mchakato na kuufanya mali yake.
Anasema tume ya warioba haikuzingatia suala la ardhi. Sitta ni mtu wa ajabu sana, katika masuala ambayo tume imeyaonyesha wazi na kyawakea mkazo kama chanzo cha mgogoro ni ardhi. Tena kukiwa na randama maalumu.
Leo anaingiza suala hilo katika muungano ili kuwafurahisha wazanzibar ambao wana miliki yao na Mtanganyika hana manufaa nayo.
Sitta anatengeneza mazingira mazuri sana ya chuki na hasira.
Atakuwa ameshachukua milioni 150 akishuhudia taifa linavyoparaganyika na waznz wakilipa gharama ambazo zingeweza kuepukika.
Sitta hatasalimika na madhara on the making na historia itamhukumu bila wakili au mwendesha mashitaka.
Sitta ni mtu hatari sana na adui mkubwa wa ustawi wa demokrasia na maendeleo ya nchi hii.