Duru: UKAWA njia panda, CCM maji ya shingo

Duru: UKAWA njia panda, CCM maji ya shingo

Mag3,

Tatizo lililopo ni Kwamba Mwenyekiti wa Hilo bunge haweki maslahi ya taifa Mbele Bali maslahi binafsi ya posho na ya urais 2015. Kwa mfano, kwa Mujibu wa vyanzo vya uhakika, posho ya Sitta kwa siku 84 za bunge la katiba zitakuwa jumla ya shillingi milioni 150. Je unatarajia nini kwa kiongozi ambae Ana rekodi ya kujenga ofisi ndogo ya uspika jimboni kwake kwa gharama za walipa kodi shillingi milioni 500, ofisi ambayo sio Anna Makinda Wala maspika wajao wataitumia?

Sitta anaishi kwenye nyumba oysterbay inayogharamiwa na walipa kodi zaidi ya shillingi milioni kumi kwa mwezi Kama kodi, nyumba ambayo ilitakiwa ampishe spika Makinda lakini akagoma, sasa tutarajie nini kwa kiongozi wa aina hii Huko Dodoma ambako posho Ndio habari ya Mjini?

Pia tunajua uzoefu wake wa siasa za ubabe na kupinda mambo, mfano alivyowasha na kuzima hoja ya Richmond bungeni pre maturely. Majuzi ametishia ITV kwa sababu inasimamia upande wa wananchi. Anasahau Kwamba Wakati wa Sakata lake na the so called mafisadi, hakuna media org iliyompa air time Kama itv, kuanzia kipindi cha Dakika 45 hadi Sakata la mwakyembe kulishwa sumu.

Leo Sitta anaenda Mbali na kuamuru masuala ya Tanzania bara yaingizwe kwenye katiba ya muungano ili kuua hoja ya tanganyika. Kuna taarifa Kwamba anapita Kamati hadi Kamati na kuamuru nini cha kuwekwa. Kiongozi wa aina hii hatufai, ataipasua nchi vipande vipande kwani ameonyesha wazi Kwamba:

1. Hajali matakwa ya wananchi.
2. Hajali Sheria - amekiuka Sheria ya mabadiliko ya katiba (2011).
3. Hana hulka ya kuheshimu katiba ya nchi.
4. Mkandamizaji wa vyombo vya habari.
5. Hana nia ya Dhati ya kupambana na ufisadi na ubadhirifu wa Mali ya umma kwani Mbali ya Mifano hai hapo juu, pia amebariki ubadhirifu wa kulipana posho bungeni Katika suala ambalo mwisho wake tayari unajulikana - katiba ya wananchi haitopatikana.

Mamlaka ya mchakato husika yapo mikononi kwa wananchi kwa Mujibu wa Sheria ya mabadiliko ya katiba(2011), mamlaka ambayo Sitta Ameamua kuyapora. Huu ni uhalifu Kama aina nyingine zote za uhalifu.


Sent from my iPhone using JamiiForums
Pamoja na hayo, pia kuna suala la credibility.
Sitta anafahamu kuwa tayari mbio za Urais zimeshamuacha.

Akiondoka bungeni utakuwa msumari wa mwisho katika 'jeneza' la kisiasa. Hivyo wakati anavizia milioni 150, pia anajaribu kuangalia kama kutatokea bahati mbaya itakayo okoa heshima yake.

Kwa maana hiyo ndio maana ameamua kuunda tume yake ya kukusanya maoni akiwa hapo bungeni.
Jana alikutana na Wafugaji, leo akakutana na wahairiri waliohongwa, wiki inayokuja anakutana na Wazanzibar.
Sitta amepewa wapi mamlaka ya kuunda tume yake mwenyewe na kujikusanyia maoni

Halafu hataki watu wazungumze wala vyombo vya habari viandike. Hoja kubwa huu mchakato ni mali yake na familia yake.


Sitta kaamua kuchukua mchakato na kuufanya mali yake.
Anasema tume ya warioba haikuzingatia suala la ardhi. Sitta ni mtu wa ajabu sana, katika masuala ambayo tume imeyaonyesha wazi na kyawakea mkazo kama chanzo cha mgogoro ni ardhi. Tena kukiwa na randama maalumu.

Leo anaingiza suala hilo katika muungano ili kuwafurahisha wazanzibar ambao wana miliki yao na Mtanganyika hana manufaa nayo.

Sitta anatengeneza mazingira mazuri sana ya chuki na hasira.

Atakuwa ameshachukua milioni 150 akishuhudia taifa linavyoparaganyika na waznz wakilipa gharama ambazo zingeweza kuepukika.

Sitta hatasalimika na madhara on the making na historia itamhukumu bila wakili au mwendesha mashitaka.

Sitta ni mtu hatari sana na adui mkubwa wa ustawi wa demokrasia na maendeleo ya nchi hii.
 
Mchambuzi,

Tatizo kubwa la viongozi wengi ndani ya CCM ni kwamba wananunulika tena kirahisi sana; wananunulika kirahisi kwa sababu hawana weledi na hii ni kwa sababu wanakokota mizigo ya kashfa. Mtu kama Sitta, hana namna kwani historia haiko upande wake; akikohoa tu wanamlipua...the hapless, miserable and poor soul has no way out, he is wedged between a rock and a hard place, he has no choice but to toe the line or else!

Viongozi wetu wengi wanaotafuta madaraka wanaweza kuonekana wasafi kwa nje lakini wanapofanikiwa tu kuyapata madaraka, wanajikuta uso kwa uso na madhambi yao huko nyuma. Mara nyingi wananchi huwa tunajidanganya tukidhani tunachagua viongozi lakini ukweli ni kwamba liko genge linatuchagulia viongozi. Siku ya kwanza tu ofisini, mafisadi haoo wanapiga hodi and immediately they are making you offers you cannot refuse!

Kinachosikitisha ni kwamba ndani ya CCM wenye ujasiri wa kuwatolea nje kama wapo ni wachache sana; wengi ni wachafu wachafu wachafu. Wanaoonekana angalau watanyamazishwa kwa njia mbali mbali hata ikibidi kuwatoa roho... hawana huruma na mtu. Yuko kiongozi moja tu aliwahi kuwatolea nje naye ni Hayati Mwalimu Nyerere na aliweza kufanya hivyo tu kwani hakuwa na bei, hakuweza kununulika; the man had nothing to hide!

Matokeo yake tumejenga taifa la wanafiki la watu wanaotetea hata yale wasiokubaliana nayo mradi posho ipo, cheo kipo, ajira ipo, maslahi binafsi yapo...to hell with principle! Katika watu hao Sitta is one of the leading figures. He'd sacrifice his own mother for a piece of silver! Aliwasaliti wenzake CCJ kwa ahadi ya Uwaziri na leo anawasaliti Watanzania kwa ndoto ya Uraisi; trouble is, times have changed...the dude is in for a rude awakening!
 
Mag3

Unamkumbuka kiongozi aliyesema 'Wana CCM wajiandae kwa mabadiliko ya muundo wa serikali (S3)
Alikumbana na genge lenyewe, ghafla akarudi na kusema 'S3 jeshi litapindua nchi''

Sitta anajua nguvu ya genge hilo. Anachokifanya sasa hivi ni kuomba msamaha ili afikiriwe tena.
Kwa bahati mbaya sana credibility yake katika jamii is second to none.

Anasubiri bahati nzuri itokee na kuokoa sura yake.
Kwasasa yeye ni 'public enemy number 1''

Ukisoma alama za nyakati utaona hata CCM wamemuacha kama yatima akizidi kukwangua hata ka-heshima kadogo kailikobaki mtaani kwake. Shame on him!
 
Mchambuzi;10317077]Nguruvi3,Iwapo CCM itafanikiwa kuleta serikali Mbili zilizoboreshwa, hii itakuwa ni kwa faida ya Zanzibar na kwa hasara ya Tanganyika. Hali hii itapelekea wananchi wa Tanzania bara kudai Tanganyika kwa Nguvu Kama alivyoeleza professor Kabudi. Kwa maana nyingine, jinsi CCM inavyoZidi kuboresha serikali Mbili ndivyo jinsi watanzania bara wanavyozidi kukosa Haki zao za kisiasa, kijamii, na kiuchumi (political, social and economic justice) ambazo zitakuja leta vurugu na vita. Kwahiyo serikali Mbili zilizoboreshwa ni "timing bomb" ambalo ni wajibu wa ukawa kuwaelezea wananchi Kwamba wajibu wa kulitegua ni wananchi wenyewe.
Matumaini yao ni kulinda muungano kwa kutumia FFU, kukamata watu na kuwasingizia makosa.

Wasichokumbuka , Sha wa Iran, Fernandos Marcos walikuwa na FFU wengi wenye zana bora sana. Wote wamejikuta wanafia ughaibuni. Nguvu ya umma haizuiliwi kwa rasha sha, magrunedi au virungu.

CCM hawafahamu kuwa Watanganyika wamebaini mambo mengi yanayowatia hasira. Katika kumfurahisha mzanzibar lazima utamuudhi Mtanganyika. Ndio maana tunasema kila siku na kuonekana tuna chuki, atakayelipa gharama si Mtanganyika. Yeye ana kazi moja tu kutoa ya kifuani.
 
chambuzi;10317077] Wananchi wengi wa upande wa bara Hawaelewi athari za katiba ya Zanzibar (2010) kwa Tanganyika na kwa muungano kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Kisiasa, rais wa muungano ambae ndiye rais wa Tanganyika ni rais boya. Rais wa muungano ambae pia ni rais wa Tanganyika hatokuwa na uwezo wa kuilinda na kuitetea Tanganyika chini ya katiba iliyoboreshwa. Kiuchumi, chini ya serikali Mbili zilizoboreshwa, muungano utamhudumia mzanzibari kuliko mtanzania bara. Na kijamii, utambulisho wa mtanzania utafifia zaidi chini ya nchi Mbili Zenye serikali Mbili kuliko uzanzibari. Matokeo yake ni Kwamba Kama taifa, tutajenga Kizazi ambacho hakitaweza jitambua Huko Mbeleni.

Kwa mtazamo wangu, hayo Ni baadhi ya maeneo ambayo ukawa wanatakiwa kuyazingatia in their dialogue na wananchi.
Labda nitoe mfano hai kwa hoja yako hii. Leo wazanzibar wapo Dodoma wanajadili ufugaji. Hivi hili linawahusu nini tukijua kuwa mzanzibar anaogopa hata kumshika ng'ombe. Leo wanajadili mambo ya Monduli ili iweje.
Wanajdili kilimo, wakati hilo haliwahusu n.k.

Hata Wabunge wa CCM na wa kundi maalumu hawaoni jinsi gani kuna hasara kwa Mtanganyika.
Ni kwamba unapokuwa na JMT tayari umeshamnyan'nganya Mtanganyika haki zake na kuzifanya za muungano.
Kama haki za Mtanganyika ni za muungano, kwanini zile za Mzanzibar ziwe zake? Muungano gani hapo?

Hawa wabunge waliofungwa akili, hawaelewi kubwa idadi ya wabunge wa majimbo ya uchaguzi 100 tu ya uchaguzi ya Tanganyika yanahudumiwa na kiasi kidogo cha rasilimali za wananchi wao kuliko zile zinazokwenda nchi jirani ya ZNZ.

Yaani inafika mahali unaona kabisa jinsi watu wanavyouza nchi yao, uzalendo na utaifa na kujiuliza, hivi watu kama wale wabunge wa CCM wana watoto kweli? Kama wanao wanadhani watawarithisha nini siku zijazo, bongofleva!

Kama yupo asiyeona social, economic and poilitical dhuluma inayofanyiwa Tanganyika, mtu huyo badala ya kuwa Bungeni angekuwa jirani na hospitali ya pale Dodoma.

Mnawasikiliza akina Sitta, hao baada ya kifo cha Nyerere ndio madalali waliobaki wa kuinadi nchi hii.

Watanganyika, tutawasha karabai na fanusi muone kile msichokiona, maana siku mtakapokiona bila kuambiwa patachimbika.
 
Mag3,

Tatizo lililopo ni Kwamba Mwenyekiti wa Hilo bunge haweki maslahi ya taifa Mbele Bali maslahi binafsi ya posho na ya urais 2015. Kwa mfano, kwa Mujibu wa vyanzo vya uhakika, posho ya Sitta kwa siku 84 za bunge la katiba zitakuwa jumla ya shillingi milioni 150. Je unatarajia nini kwa kiongozi ambae Ana rekodi ya kujenga ofisi ndogo ya uspika jimboni kwake kwa gharama za walipa kodi shillingi milioni 500, ofisi ambayo sio Anna Makinda Wala maspika wajao wataitumia?

Sitta anaishi kwenye nyumba oysterbay inayogharamiwa na walipa kodi zaidi ya shillingi milioni kumi kwa mwezi Kama kodi, nyumba ambayo ilitakiwa ampishe spika Makinda lakini akagoma, sasa tutarajie nini kwa kiongozi wa aina hii Huko Dodoma ambako posho Ndio habari ya Mjini?

Pia tunajua uzoefu wake wa siasa za ubabe na kupinda mambo, mfano alivyowasha na kuzima hoja ya Richmond bungeni pre maturely. Majuzi ametishia ITV kwa sababu inasimamia upande wa wananchi. Anasahau Kwamba Wakati wa Sakata lake na the so called mafisadi, hakuna media org iliyompa air time Kama itv, kuanzia kipindi cha Dakika 45 hadi Sakata la mwakyembe kulishwa sumu.

Leo Sitta anaenda Mbali na kuamuru masuala ya Tanzania bara yaingizwe kwenye katiba ya muungano ili kuua hoja ya tanganyika. Kuna taarifa Kwamba anapita Kamati hadi Kamati na kuamuru nini cha kuwekwa. Kiongozi wa aina hii hatufai, ataipasua nchi vipande vipande kwani ameonyesha wazi Kwamba:

1. Hajali matakwa ya wananchi.
2. Hajali Sheria - amekiuka Sheria ya mabadiliko ya katiba (2011).
3. Hana hulka ya kuheshimu katiba ya nchi.
4. Mkandamizaji wa vyombo vya habari.
5. Hana nia ya Dhati ya kupambana na ufisadi na ubadhirifu wa Mali ya umma kwani Mbali ya Mifano hai hapo juu, pia amebariki ubadhirifu wa kulipana posho bungeni Katika suala ambalo mwisho wake tayari unajulikana - katiba ya wananchi haitopatikana.

Mamlaka ya mchakato husika yapo mikononi kwa wananchi kwa Mujibu wa Sheria ya mabadiliko ya katiba(2011), mamlaka ambayo Sitta Ameamua kuyapora. Huu ni uhalifu Kama aina nyingine zote za uhalifu.

Sent from my iPhone using JamiiForums

Mchambuzi if you read carefully in his mind, i can only say that Mzee Sitta is not himself. He tried, and he was very close to move to Chadema, lakini kwa sababu ambazo nadhani umezitaja kiasi hakuwa na jeuri ya kuhama CCM. Nadhani amekubali kabisa kuwa "if you can not beat them, join them". Yote uliyo ya-attribute kwa mzee Sitta, kimsingi si yake tu, bali pia ni ya CCM.

Uliyotaja hayo, ya kujenga ofisi ya Spika Tabora, kung'ang'ania nyumba ya Spika Dar, hana njia ya kuyalipa isipokuwa kulipa kwa kuwatumikia. CCM wanapenda sana watu wenye maovu, kwa kuwa uovu ambao ungewapeleka gerezani, unatumiwa na CCM kuwafanya watu hao waitumikie kwa uoga na kwa unafiki. Hicho ndio anakifanya Sitta.
 
Labda nitoe mfano hai kwa hoja yako hii. Leo wazanzibar wapo Dodoma wanajadili ufugaji. Hivi hili linawahusu nini tukijua kuwa mzanzibar anaogopa hata kumshika ng'ombe. Leo wanajadili mambo ya Monduli ili iweje.
Wanajdili kilimo, wakati hilo haliwahusu n.k.

Hata Wabunge wa CCM na wa kundi maalumu hawaoni jinsi gani kuna hasara kwa Mtanganyika.
Ni kwamba unapokuwa na JMT tayari umeshamnyan'nganya Mtanganyika haki zake na kuzifanya za muungano.
Kama haki za Mtanganyika ni za muungano, kwanini zile za Mzanzibar ziwe zake? Muungano gani hapo?

Hawa wabunge waliofungwa akili, hawaelewi kubwa idadi ya wabunge wa majimbo ya uchaguzi 100 tu ya uchaguzi ya Tanganyika yanahudumiwa na kiasi kidogo cha rasilimali za wananchi wao kuliko zile zinazokwenda nchi jirani ya ZNZ.

Yaani inafika mahali unaona kabisa jinsi watu wanavyouza nchi yao, uzalendo na utaifa na kujiuliza, hivi watu kama wale wabunge wa CCM wana watoto kweli? Kama wanao wanadhani watawarithisha nini siku zijazo, bongofleva!

Kama yupo asiyeona social, economic and poilitical dhuluma inayofanyiwa Tanganyika, mtu huyo badala ya kuwa Bungeni angekuwa jirani na hospitali ya pale Dodoma.

Mnawasikiliza akina Sitta, hao baada ya kifo cha Nyerere ndio madalali waliobaki wa kuinadi nchi hii.

Watanganyika, tutawasha karabai na fanusi muone kile msichokiona, maana siku mtakapokiona bila kuambiwa patachimbika.

To the contrary, wale wanaobariki dhuluma hiyo ndio wanaokena watu wa maana. Nguruvi3 kwa mtu yoyote anayetumia akili, busara na uelewa rahisi, serikali mbili ni wizi, ujinga na ujuha. Ni hatari sana kwa muungano wetu na usalama wa nchi yetu. I am telling you, when we talk of building strong institutions, constitution is one of them. If we get a sloppy one through this shabby process of alienating UKAWA and Jaji warioba, ni mwanzo mbaya sana kwa TZ.
 
To the contrary, wale wanaobariki dhuluma hiyo ndio wanaokena watu wa maana. Nguruvi3 kwa mtu yoyote anayetumia akili, busara na uelewa rahisi, serikali mbili ni wizi, ujinga na ujuha.

Ni hatari sana kwa muungano wetu na usalama wa nchi yetu. I am telling you, when we talk of building strong institutions, constitution is one of them. If we get a sloppy one through this shabby process of alienating UKAWA and Jaji warioba, ni mwanzo mbaya sana kwa TZ.
Hakika haukna nchi yoyote iliyowahi kucheza na katiba ikabaki salama.
Katiba ndio 'grisi' ya kila raia wa nchi husika. Kunapokuwa na mtafaruku, katiba ndio mwongozo unaotoa majibu.

Matatizo yaliyopo ya kijamii na kisiasa ni matokeo ya katiba kuwa na matatizo au kupitwa na wakati.
Prof Kabudi katika darsa lake alisema katiba tuliyokuwa nayoilikuwa instrumental. Miaka 50 hakuhitajiki tena kwasababu mazingira ya sasa ynahitaji katiba ya maendeleo na matendo ''pragmatic'

Hakuna katiba iliyoandikwa bila kuwa na mivutano. Kenya tuliona Wacko commission na kisha Boma
Kutokana na watu wachache kuchezea katiba kama Mzee Sitta anavuyofanya, damu ilimwagika Kenya.

Mwisho wa siku kukawa na muafaka ambao makundi yaliridhia na kwenda kushindana kwa hoja. Kura ya maoni ilikuwa wazi tena ikipigiwa upatu na kila kundi kupinga au kukubali. Kenya imerudi katika maridhiano na sasa ipo salama.

Katika muungano wetu, kuna kila kiashiria kuwa hali si nzuri. Tunakumbu kumbu za mswada kuchomwa moto mbele ya Sitta, Watanganyika kubaguliwa na hata kuchomwa moto na kwa upande mwingine sentiment kubwa dhidi ya wazanzibar wanaoishi bara. Chuki tunaanza kuiona mitaani akina Mzee Sitta wakiamini FFU wapo kila nyumba, ofisi na shule.

Kundi linalotetea dhulma ya muungano ni la akina Sitta. Mzee huyu akiwa Spika alishuhudia matatizo makubwa sana mbele yake kuhusiana na muungano. Na yupo katika rekodi akionyesha sentiment za Watanganyika.

Kiuchumi: Tanganyika imebeba 100% ya muungano, Znz ikinufaika 100% na mzigo huo wa Tanganyika
Kijamii: Zanzibar inanufaika na muungano 100% Tanganyika ikinufaika 0%
Kisiasa: Nako kama kiuchumi na kijamii ni hivyo hivyo.

Tatizo halikuanzia kwa Watanganyika, ni wazanzibar waliooonyesha Watanganyika dhulma wanayofanyiwa.
Madai ya wznz kuhusu muungano, na jinsi wanavyopewa yanaamsha hisia kali sana kwa Watanganyika.

Muda wa majadiliano ukipita, kitakachofuata ni muungano kuvunjika kama glass.
Mzee Sitta anadhani yeye ndiye gundi ya muungano, hajui muungano ni wananchi.
Mbele ya Safari Sitta atajilaumu sana maana kutakuwa hakuna muungano kabisa.

Historia haitakamilika kama Sitta hatatajwa miongoni wa watu walioshiriki kikamilifu, kuzua vurugu anazotengeneza sasa hivi, kuvunja muungano na zaidi kuwa msaliti wa Taifa lake.
 
CCM MAJI YA SHINGO

Mwanasheria Werema kasema lipo tatizo mbele ya safari ya BMK. Kwamba, uwezekano wa kupata akidi ya kupitisha rasimu ya Samwel Sitta ni mdogo sana. Werema amewataka UKAWA warudi, katiba inayokusudiwa ya Sitta na CCM ipate uhalali wa kisiasa.

UKAWA walimtaka Rais asimamishe mchakato kwasababu ili kuokoa fedha za wananchi.
Ikulu imejibu, Rais hana mamlaka ya kuvunja bunge.

Ukiangalia kauli mbili, ya Ikulu na Werema, hakuna shaka mambo ni magumu sana kwa upande wa CCM.

Ikulu imetumia lugha yake ya 'kawaida ya kutoonekana wabaya' Wanasema Rais hana mamlaka, halafu wanawasihi UKAWA warudi. In other words, wanamwambia Samwel Sitta aangalie failure iliyopo.

Bongolander alisema neno '' Sitta is not hinself'' na hakika mzee Kachanganyikiwa.

Mzee Sitta kabaki mwenyewe akihangaika kuunda tume na kutumia fedha kualika wafugaji na mambo mengine ya aibu. Asichokitambua kwasababu ya ubabe wake ni kuwa sasa hivi amebeba mzigo wote wa lawama na laana za katiba

Kama litatokea lisilotarajiwa, mtu wa kwanza kunyooshewa kidole ni Samwel Sitta.
Huyu ndiye aliita wapinzani vichwa ngumu na kuendesha bunge kwa ubabe akidhani ni mali yake

SITTA ANAWEZA KUOKOA PESA

Sheria iliyoanzisha mchakato na BMK haikueleza Rais kuwa na uwezo wa kuvunja Bunge.

Watu wengi akiwemo mwanasheria wanashindwa kuelewa jambo moja, kuna technical means zinazoweza kutumika kuokoa pesa za wakulima na wagfanyakazi zinazoendelea kufujwa na CCM Dodoma, bila huruma

SITTA AHIRISHA BUNGE, USIVUNJE

Mwezi wa sita Sitta aliahirisha bunge, kupisha bunge la bajeti liendelee.
Nafasi hiyo anayo ya kuahirisha bunge ili kupisha maridhiano.
Si kuvunja, ni kuahirisha kama ilivyowahi kutokea mara nyingin tu.

Njia ya pili, ni kutumia mbinu za kiufundi, kwa kushirikiana na CCM ili akidi isitoshe na kuwa sababu ya kuahirisha bunge

Haya ni machache, kuna mengi kisheria yanayoweza kuzungukwa na sheria isivunjwe na kuokoa pesa.

Hata hivyo, hivi kuna sheria gani inayoogopwa kuvunjwa nchini?
Kama hawatambui tume ya Warioba waliyounda wenyewe kuna sheria gani wanayoogopa hawa.

Samwel Sitta, pesa za wakulima zinateketea, hasira za wananchi juu ya katiba zipo juu, hasira za kudharauliwa maoni yao zipo juu, na hasira za uhuni unaoendelea wa kujali matumbo yenu zinaongezeka.

Hasira zote hizo zimeashaondoka kwa wahusika, na sasa zipo mabegani mwa Samwel John Sitta.

Wenzako Ikulu na ofisi ya mwanasheria wanaanza kujiosha, umebaki wewe na tume yako ya kushughulikia matatizo ya wafugaji.

Kumbuka yule mwanasheria wa Kenya, Kivuitu na Rais Kibaki hawakwenda the Hague.

Tusemezane
 
CCM MAJI YA SHINGO

Mwanasheria Werema kasema lipo tatizo mbele ya safari ya BMK. Kwamba, uwezekano wa kupata akidi ya kupitisha rasimu ya Samwel Sitta ni mdogo sana. Werema amewataka UKAWA warudi, katiba inayokusudiwa ya Sitta na CCM ipate uhalali wa kisiasa.

UKAWA walimtaka Rais asimamishe mchakato kwasababu ili kuokoa fedha za wananchi.
Ikulu imejibu, Rais hana mamlaka ya kuvunja bunge.

Ukiangalia kauli mbili, ya Ikulu na Werema, hakuna shaka mambo ni magumu sana kwa upande wa CCM.

Ikulu imetumia lugha yake ya 'kawaida ya kutoonekana wabaya' Wanasema Rais hana mamlaka, halafu wanawasihi UKAWA warudi. In other words, wanamwambia Samwel Sitta aangalie failure iliyopo.

Bongolander alisema neno '' Sitta is not hinself'' na hakika mzee Kachanganyikiwa.

Mzee Sitta kabaki mwenyewe akihangaika kuunda tume na kutumia fedha kualika wafugaji na mambo mengine ya aibu. Asichokitambua kwasababu ya ubabe wake ni kuwa sasa hivi amebeba mzigo wote wa lawama na laana za katiba

Kama litatokea lisilotarajiwa, mtu wa kwanza kunyooshewa kidole ni Samwel Sitta.
Huyu ndiye aliita wapinzani vichwa ngumu na kuendesha bunge kwa ubabe akidhani ni mali yake

SITTA ANAWEZA KUOKOA PESA

Sheria iliyoanzisha mchakato na BMK haikueleza Rais kuwa na uwezo wa kuvunja Bunge.

Watu wengi akiwemo mwanasheria wanashindwa kuelewa jambo moja, kuna technical means zinazoweza kutumika kuokoa pesa za wakulima na wagfanyakazi zinazoendelea kufujwa na CCM Dodoma, bila huruma

SITTA AHIRISHA BUNGE, USIVUNJE

Mwezi wa sita Sitta aliahirisha bunge, kupisha bunge la bajeti liendelee.
Nafasi hiyo anayo ya kuahirisha bunge ili kupisha maridhiano.
Si kuvunja, ni kuahirisha kama ilivyowahi kutokea mara nyingin tu.

Njia ya pili, ni kutumia mbinu za kiufundi, kwa kushirikiana na CCM ili akidi isitoshe na kuwa sababu ya kuahirisha bunge

Haya ni machache, kuna mengi kisheria yanayoweza kuzungukwa na sheria isivunjwe na kuokoa pesa.

Hata hivyo, hivi kuna sheria gani inayoogopwa kuvunjwa nchini?
Kama hawatambui tume ya Warioba waliyounda wenyewe kuna sheria gani wanayoogopa hawa.

Samwel Sitta, pesa za wakulima zinateketea, hasira za wananchi juu ya katiba zipo juu, hasira za kudharauliwa maoni yao zipo juu, na hasira za uhuni unaoendelea wa kujali matumbo yenu zinaongezeka.

Hasira zote hizo zimeashaondoka kwa wahusika, na sasa zipo mabegani mwa Samwel John Sitta.

Wenzako Ikulu na ofisi ya mwanasheria wanaanza kujiosha, umebaki wewe na tume yako ya kushughulikia matatizo ya wafugaji.

Kumbuka yule mwanasheria wa Kenya, Kivuitu na Rais Kibaki hawakwenda the Hague.

Tusemezane

Mkuu Nguruvi3,

Una mtazamo gani kuhusu kufutwa Kabisa kwa Sheria ya mabadiliko ya Katiba (2011) na bunge la JMT? Kama rais Hana mamlaka ya kuvunjwa bunge lililopo kwa Mujibu wa Sheria, je bunge halina uwezo wa kuifutilia Mbali Sheria husika? Mimi nadhani kuvunjwa au kuhairishwa hakutakuwa na maana ikiwa bunge litakaporejea litaendeshwa kwa Sheria Ile Ile. Just thinking out loud.




Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Nguruvi3,

Una mtazamo gani kuhusu kufutwa Kabisa kwa Sheria ya mabadiliko ya Katiba (2011) na bunge la JMT? Kama rais Hana mamlaka ya kuvunjwa bunge lililopo kwa Mujibu wa Sheria, je bunge halina uwezo wa kuifutilia Mbali Sheria husika? Mimi nadhani kuvunjwa au kuhairishwa hakutakuwa na maana ikiwa bunge litakaporejea litaendeshwa kwa Sheria Ile Ile. Just thinking out loud.
Mkuu Mchambuzi , silaha wanayotaka kuitumia CCM ni kuhusu kutokuwepo kwa sheria inayoruhusu bunge la katiba kuvunjwa na Rais. Hivyo wanaendelea ili kupora pesa tu wakijua matokeo yake ni kukosekana kwa wanachokitaka. Hoja yao ni kuwa BMK litavunjwa na nani? Kama ni hivyo UKAWA warudi.
Hiyo ndiyo arguement yao.

Katika bandiko langu nimeshauri kuwepo na kuahirishwa kwa bunge na si kuvunjwa kwa sababu hizi.
1. Kuahirisha bunge ni rahisi zaidi kuliko kuvunja ambako tayari wanasimama katika sheria wakisema hairuhusu.
2. Kuahirisha bunge maana yake ni kuzuia wezi wasiendelee kupora pesa za walipa kodi.
3. Hiyo itatoa nafasi ya kwenda katika bunge la JMT kufuta sheria husika. Hivyo ilikuwa ni hatua kuelekea huko.
4. Na mwisho Bunge la JMT ambalo litakaa Oct lijadili uwezekano wa sheria itakayovunja BMK.

Hata hivyo hilo litakuwa double edge sword.
1. Kwa upande mmoja litwezesha mchakato kuanza upya. Sidhani sheria inaweza kufutwa na kuacha mambo ya tume.
2. CCM watafurahia kwa kuelewa huenda mwiba mchungu wa Warioba watauepuka kwa kuunda ''tume makini''

Hata hivyo kuna njia ya kuepuka hilo, kama kutaka mchakato mzima uanze bungeni.
Ninapata tabu kidogo kwa hili.

Una mtazamo gani
 
Last edited by a moderator:
KATIBA YACHENGE YADODA
MBINU ZA CCM ZA KUJIKWAMUA ZAPANGWA
ESCROW NA MAFISADI, VIFO VYA WAPIGA DEBE, PIGO LINGINE

Katiba yaChenge imedoda, haina mvuto, mjadala wala haiuzungumzwi.
Rais ameamua kuendeleana mchakato licha ya matatizo yanayoonekana kutokea.
Kwa muda sasa, CCM na serikali yake wamekuwa kimyakuhusu katiba kutokana na mambo kadhaa


Kwanza,mchakato mzima uligubikwa na mazonge zonge mengine yakiwa ya aibu katika nchi yenyewasomi kwa zama hizi kuliko huko nyuma. Kuvunjika kwa bunge baada ya UKAWA kutoka ni ushahidi mzuri wa mchakato kukwama.
Kubadili sheria, kanuni na taratibu ili kukidhi matakwa ya CCM ni sehemu nyingine ya dhalili


Njia mufaka ni CCM kukaa kimya ili upepo wa mambo hayo usahaulike vichwani mwa Watanzania.
Kimya hicho ni pamoja na wananchi kusahau suala la Escrow lililowatia kiwewe CCM katika chaguzi za serikali za mitaa


Escrow ni mwiba kwasababu walioandika katiba ya Chenge ndio wahusika wakuu.
Uhusiano wa katiba ya Chenge na ufisadi wa Escrow haviwezi kutengwa.

Mafisadi walitaka mfumo uliopo unaowapa unafuu uendelee na ndio maana walijitoa sana kuandikakatiba ya Chenge.


Ili kujitakasana mafisadi na kuitenga katiba ya Chenge na ufisadi, CCM imewasimimisha baadhi ya wanachama wake katika vkao. Jambo la kushangaza mkakati wa kupitisha katiba hiyo unahusisha mafisadi wale wale waliosimimishwa kuhudhuria vikao. Hii nidanganya tu ili kuifanya katiba ya Chenge isionekane katika sura ya ufisadi.

Pili, CCMwamekumbwa na madhila ya asili. Kifo cha mbunge na msanii Komba kimetokea na kuumiza mkakati wa CCM.
Si kwamba Komba ni msanii, bali kifo chake kimeamsha hisia na hasira za ubabe na kauli mbaya za CCM ndani ya bunge la katiba, jambo ambalo CCM hawakulitaka, walitaka ukimya utawale watu wasahau uhuni uliofanyika ndani ya bunge la katiba


Mazungumzo mengi yamehusisha kifo cha Komba na bunge la katiba na kuamsha hasira za wananchi.

Mnadhimu wa CCM Zanzibar naye alikutwa na mauti akiwa anajiandaa kupeleka mswada wa kuvunja serikali ya umoja wa kitaifa. Lengo la CCM ni kuondoa GNU ambayo ni kikwazo katika kupitisha mambo yao kibabe.

Inaendelea…
 
Sehemu ya II

Kuvunjwa kwa GNU kungesaidia mabadiliko ya katiba ya Zanzibar ambayo ni kikwazo kwa katibaya Chenge.
Lengo ni kuondoa 2/3 BLW na 2/3 kura yamaoni ya wananchi, mambo yanayotishia kukwama kwa katiba ya Chenge


Lengo la katiba ya Chenge ni kuhakikisha inapata uhalali kwanza znz kwa kuvunja GNU nakufanya ubabe wa kupitisha.

Njia hii inatumika kwasababu kipindi cha mapito walichoiga kutoka rasimu ya Warioba hakiwezi kufanya kazi ikiwa katiba ya znz haijafanyiwa marekebisho. Na bila kuua GNU hilo haliwezekani.


Tatu, tumeya uchaguzi imekuwa tawi la CCM ikipokea maagizo ya mwenyekiti wa CCM.
Tume imelazimika kutumia mfumo wa kuandikisha kutumia BVR.

Mfumo huo kwa nchi masikini kama yetu hauwezi kufanya kazi kikamilifu kutokanana katika haraka zilizopo


Tume imeagizwa kukamilisha zoezi hilo kwa njia yoyote hata kama ni ya kipuuzi ilikulinda masilahi ya CCM.
Tunashuhudia mwenyekiti wa CCM akitoa ratiba za kazi za tume, kutangaza taratibu za kura ya maoni n.k.


Lengo ni kuhakikisha CCM inawachanganya wananchi. Kwamba, ni lazima wajiandikishe kwaBVR ili waweze kupiga kura ya maoni ya katiba ya Chenge na uchaguzi mkuu.

Mambo hayo yamewekwa pamoja ili kuwadanganya wananchi wa vijijini kuwa ni muhimu kupigia kura katiba ya Chenge.


Tume imegawa katiba ya Chenge bila kuwa na utaratibu wa elimu ya umma kwavile sharia inawazuia kutokana na muda. Vitabu vimegawiwa kama ushahidi tu, hakuna la maana litakalopatikana, wananchi wamesusa hawaelewi katiba ya Chenge. Wanaojaribu kuelewa hawaelewi tofauti na katiba ya 1977

Nne, CCMinaelewa, ili kupata uhalali ni lazima uwepo upande wa hapana katika kudanganya umma.

Kazi ya kuhonga viongozi baadhi wapinge katiba ya Chenge inaendelea na muda litaokea kundi linalofadhiliwa na CCM likijinasibu kupinga katiba yaChenge


Tano, ilikuipa katiba uhalali, CCM inataka kushutukiza wananchi kwa kutambua wamesahau uhuni uliofanyika Dodoma.

CCM inataka kufanaya shamra shamra wa kuamsha hisia,kutumia muda mfupi wananchi wasihoji, kuwanyima elimu ya katiba ili mambo ya chenge na mafisadi wengine walioandika katiba yasahaulike japo kwa muda


Kwa hali ya mambo ilivyo, katiba ya Chenge imedoda, imesusiwa, haina maana na inatengeneza mazingira mazuri ya vurugu. Hakuna namna katiba ya Chenge itapata uhalali wa wananchi.

Kwa wapinzani na watanzania kwa ujumla, kosa wanaloweza kulifanya lenye gharama kubwa ni kuongelea katiba ya Chenge.

Wananchi na vyama vya siasa vikae mbali nakimya. Kuongelea tu ni kuijengea katiba ya Chenge iliyoandikwa na mafisadi kwa njia za ufisadi uhalali.


Tusemezane
 
Nguruvi3.

Nikianza na hitimisho lako kwamba wananchi, vyama vya upinzani na wadau mbalimbali wanatakiwa kutoizungumzia kabisa katiba ya CHENGE kwa sababu itakuwa ni kuipa promo, kwa upande wangu natofautiana kabisa na wewe.
Moja unapaswa kukumbuka kwamba kuna mambo mengi tu ambayo upinzani ambao ni ndio twaweza sema wanasauti kubwa zaidi katika taifa hili ukiacha mbali serikali tawala umesusia lakini mwisho wa siku yakapita tena bila matatizo yeyote Katiba ya Chenge ikiwa ni mfano tu wa mambo hayo. CCM haihitaji wananchi wanaoilewa ni nini katiba na inamaana gani hasa kwa taifa lao na maisha yao. Inatakiwa kujulikana kwamba katiba hii ili ipite inaitaji wananchi ima wajinga, waliohongwa au wenye vyeo kuipitisha lakini sio wananchi wenye akili zao timamu na hili linajulikana vizuri na CCM. Kwa maana kuipotezea ni sawa na kuwapa nafasi nzuri ya kuipitisha kimagumashi. Lakini pia wakati unaposema wananchi wasusie kumbuka sio wananchi wote ni wa upinzani au wanaelewa katiba ni nini kwa mustakabali wa taifa lao la kesho. Watanzania weng bado wanaiamini serikali ya CCM pamoja na yote yanayopita chini ya mikono yake kama ufisadi,rushwa na mengineyo.

Angalau ungeshauri wapinzani kuendelea kutumia nguvu kubwa kuwaelezea wananchi ukiukwaji wa taratibu nzima za upatikanaji wa katiba na kwamba hata waliohusika katika undikaji wa katiba ni waovu ambao hawakustahili kufanya kazi hiyo nzito.

Jambo la msingi la kujulikana katika mchakato huu ni kwamba kwa bara katiba hii inaweza kupita bila kipingamizi tatizo na sehemu ya kuitilia mkazo ni Baraza la wawakilishi ZNZ na wananchi wa ZNZ. Hao ndio wanaoweza kuamua ipite au isipe hasa sheria ikiwa haijabadilishwa.
 
Nguruvi3.

Nikianza na hitimisho lako kwamba wananchi, vyama vya upinzani na wadau mbalimbali wanatakiwa kutoizungumzia kabisa katiba ya CHENGE kwa sababu itakuwa ni kuipa promo, kwa upande wangu natofautiana kabisa na wewe.

Moja unapaswa kukumbuka kwamba kuna mambo mengi tu ambayo upinzani ambao ni ndio twaweza sema wanasauti kubwa zaidi katika taifa hili ukiacha mbali serikali tawala umesusia lakini mwisho wa siku yakapita tena bila matatizo yeyote Katiba ya Chenge ikiwa ni mfano tu wa mambo hayo.

CCM haihitaji wananchi wanaoilewa ni nini katiba na inamaana gani hasa kwa taifa lao na maisha yao.

Inatakiwa kujulikana kwamba katiba hii ili ipite inaitaji wananchi ima wajinga, waliohongwa au wenye vyeo kuipitisha lakini sio wananchi wenye akili zao timamu na hili linajulikana vizuri na CCM.

Kwa maana kuipotezea ni sawa na kuwapa nafasi nzuri ya kuipitisha kimagumashi. Lakini pia wakati unaposema wananchi wasusie kumbuka sio wananchi wote ni wa upinzani au wanaelewa katiba ni nini kwa mustakabali wa taifa lao la kesho. Watanzania weng bado wanaiamini serikali ya CCM pamoja na yote yanayopita chini ya mikono yake kama ufisadi,rushwa na mengineyo.

Angalau ungeshauriwapinzani kuendelea kutumia nguvu kubwa kuwaelezea wananchi ukiukwaji wataratibu nzima za upatikanaji wa katiba na kwamba hata waliohusika katikaundikaji wa katiba ni waovu ambao hawakustahili kufanya kazi hiyo nzito.

Jambo la msingi la kujulikana katika mchakato huu ni kwamba kwa bara katiba hii inaweza kupita bila kipingamizi tatizo na sehemu ya kuitilia mkazo ni Baraza la wawakilishi ZNZ na wananchi wa ZNZ. Hao ndio wanaoweza kuamua ipite au isipe hasa sheria ikiwa haijabadilishwa.
Hakika umeongea jambo tulilokusudia kwa namna tofauti.
Nilidhani kuwa tunaposema wananchi wasusie ingeeleweka kwavilenimeliongelea sana suala hili.

Naomba tufafanue

Tnaposema wananchi wasiongelee kabisa, nina maana wasijaribu kuongelea katiba ya Chenge.

Kufanya hivyo kutaipa katiba hiyo uhalali kwav ile itakuwa inajadiliwa.
Hakuna uhalali wakati wa kuujadili mzoga. Mzoga ni mzoga, haufai kujadiliwa.


Tuunganenawe kwa kusema kuwa, mara zote tumewaasa wapinzani na Watanzania wote kuwa ni muhimu kuacha mchakato wa katiba ya Chenge uendelee ili CCM waweze kupata katiba yao.

Wananchi na wapinzani, wazungumzie mchakato wa katiba mpya kama agenda yao ya uchaguzi.Hilio ndilo kusudio.

Kama ulivyosema, hakuna haja ya kuzungumzia katiba ya Chenge. Kwa namna yoyoteitapita tu.

Wananchi wameshuhudia tume ya Uchaguzi ikwa katika hadhi naUVCCM, UWT au Wazazi.

Tume imeporwa nguvu zake na JK ambaye ni mwenyekiti waCCM.
Sasa hivi ndiye anazungumza kama msemaji wa tume, anapanga na kutekeleza kila kitu


Tume itaambiwa tu asilimia ngapi itangazwe kama ushindi. Katika mazingira hayo, hakuna hata sababu ya kusema ‘hapana'.

Zipo sababu za kususia kuongelea kabisa katiba ya Chenge, lakini madai ya katiba mpya yaongelewe kama ulivyosema


Ni kwabahati mbaya tu wapinzani nao wana matatizo. Kazi ya kudai katiba mpya ilitakiwa iwe imeshaanza siku nyingi.

Kudai katiba mpya si kuongelea ya Chenge,ni kueleza umma kuwa iliopo ni ya tume ya kukusanya maoni ya Samwel Sitta iliyokusanya maoni ya watu 38, na kuandikwa na Chenge


Chenge/Ngeleja/Tibaijuka na wengine ndio washiriki wa escrow.

Tumewahi kueleza kuwa jitihada za akinaWerema na mafisadi zilikuwa kupitisha katiba iyakayolinda masilahi yao,itakayowafurahisha CCM katika jitihada za kufunikwa escrow.

Kwa bahati mbaya azma haikutumia kama walivyokusudia.


Hii si katiba ya wananchi, ni ya mafisadi na kuijadili tu ni kuipa uhalali.
Ndio maana Salva Rweyemam alishatenga 2.5Bilioni kununua wasomi, waandishi, viongozi wadini n.k.


Kisichoonekanani ugumu kule znz. Katiba ya Chenge imetenga miaka 4 kama kipindi cha mpito.

Hili ni katika kufanya hithada za kuiwezesha katiba husika kufanya kazi znz, nakuoanisha mambo kati ya ile ya znz na hiii ya Chenge. Shida ni kuwa katiba yaznz haitoi nafasi hiyo na hapo ndipo CCM walipokwama.


Jitihada zakumtumia marehemu Salimin Awad kupeleka mswada wa kuvunja GNU ilikuwa nikuondoa kikwazo.

Ni ngumu sana kwavile ile GNU ivunjwe lazima kuwe na 2/3 yakura ya maoni ya wananchi.

Hali ya kisiasa znz hairuhusu 2/3 kwa upande wowoteule. CCM watakuwa wamekwama sana na vurugu kuwa zinalinyelea taifa.
 
WABUNGE NAWAGOMBE URAIS WATARAJIWAMAJI YA SHINGO
WATAPEWA ZIGO LITAKALO WAANGAMIZA
JK HANA CHAKUPOTEZA TENA, ANAJENGA JINA

Jaribio lakushtukiza na kushambulia katiba ya Chenge linaratibiwa na CCM
CCM inawakati mgumu sana wa kupata wapiga debe licha ya pesa wanazomwaga

Chama,kimebuni mkakati wa kuwatumia wasomi hasa wa fani ya sharia katika kupiga debe.
Hilo linatokana na hali dororo ilivyo na utata wa uchaguzi mkuu wa 2015.


Utata ni wananchi wanaonekana kuwa na hasira na chuki dhidi ya katiba ya Chenge

Chenge mwenye katiba yake amezuiliwa katika vikao vya chama.
Je,ataendelea kuwa nje ya mkakati wa katiba ili hali yeye ndiye mjuzi na mwenyekatiba?

Kuondolewa kwa Chenge ni jitihada za kuitenga katiba na ufisadi


CCM inataraji kuwatumia mkada, ambao wengi ni wabunge wanaotarajia kuwania tena
Katiba yaChenge inawafungamanisha wapiga debe hao watarajiwa na ufisadi.

Atakayekubali kuwa mpiga debe, mbele ya safari atakuwa na wakati mgumu kuwaeleza wananch ikuhusu katiba wasioiafiki na isiyowakilisha maoni yao

Wagombea Urais nao wana wakati mgumu. Kupigia debe katiba ya Chenge ni kujifungamanishana katiba ya kifisadi ,kukaribisha hoja ya uwezo wao kuongoza.

Mbele yasafari wataulizwa maswali yanayohusiana na katiba.
Kwa vile watakuwa wapiga debe, majibu yao yanaweza kuwa kitanzi kizuri

Njia ya tatu ni CCM kuwatumia wajumbe wa bunge maalumu la katiba kama wapiga debe.
Swali watakaloulizwa wajumbe hao ni jinsi gani walishiriki katika BMLK.


Je,walikwenda kama wawakilishi wa makundi ya jamii au walikwenda kwa kutumia jamii wakiwa ni waumini wa CCM.

Hilo litafungua maswali mengi Zaidi kuhusu mchakato na uhuni uliofanyika.

Mpango wanne ni kuwatumia wapinzani ‘feki' waliobaki bungeni.

Hao nao wanataka nafasi kama za ubunge, na upigaji debe unawaondolea hata kile kidogo walichonacho

Lakini,suala zito kabisa ni namna gani CCM itaweza kuleta hamasa ili yawepo makundimawili, lile la ‘ndiyo CCM' na lile la ‘feki hapana'?

Ili kuweza kuleta hamasa ni lazima wawepo watu wenye ushawishi kwa jamii.

CCM itawapata wapi ikiwa tayari imeshanunua ‘wapinzani feki"?

Na hata ikitumia pesa kununua wasomi, ni wapi hao wanaojulikana na wenye ushawishi kwa jamii?

CCM na tawi lao la tume ya uchaguzi watatumia ubabe kufanikisha ushindi wa kishindo.

Kwa bahati mbaya, katiba ya Chenge itakosa uhalali wa kisiasa'political legitimacy' kablaya matokeo hayatangazwa na CCM-tume ya uchaguzi.

Kuelekea2015, huo unaweza kuwa mwiba mkali.
Uwezekano wa CCM kupoteza mhimili mmoja kati ya miwili( Bunge au Serikali) unazidi kuongezeka.

Lakini pia itategemea wapinzani wanatumia vipi fursa zinazoelekea kwao kwa sasa kama hii la katiba.


Tusemezane
 
WABABAISHAJI WAITAIWEKA UKAWA NJIA PANDA

CCM INATAFUTA KOSA MOJA TU LA UKAWA, IJENGE UHALALI WA KATIBA YA CHENGE

Siku za karibuni yamekuwepo maoni kuwa, UKAWA washiriki mchakato wa kura ya maoni

Shinikizo hilo linatoka sehemu mbili.
Kwanza, ndani ya UKAWA ambako baadhi wanaamini kuwa nguvu ya UKAWA inaweza kuzuia kura ya maoni (hapana)

Pili, 'wapinzani' walionunuliwa na msingi wa hoja yao ni huo huo.
Hawa lengo lao ni kutaka katiba ya Chenge ipewe sura ya kitaifa na kukubalika kwa kushiriki

Kwanini UKAWA walisusia bunge
Baada ya kuwapa maonyo mengi kuhusu mchakato na kudharau, mwishowe UKAWA walibaini kinachofanyika si bunge la katiba bali la CCM lenye katiba ya CCM iliyoandikwa na Sitta na Chenge. Wakatoka kususia mchakato mzima

Kususia maana yake ni kutokubaliana na mchakato mzima uliogubikwa na hila, na pia kujiondoa katika mchakato ambao mwisho wa siku ungetoa katiba haramu.

UKAWA hawakutaka kuwa sehemu ya uovu huo wakati huo na siku za mbeleni.
Mantiki hii inaeleza bila shaka, kwanini UKAWA hawapaswi,si kushiriki bali kuzungumzia katiba ya Chenge

Katika makundi mawili yaliyotajwa aya ya kwanza hapo juu, kundi la UKAWA wanaoamini wanaweza kushawishi kura ya hapana linakosa maono, halijifunzi kutokana na makosa na lina ufinyu mdogo wa kuelewa.

UKAWA walishindwa kuzuia uhuni kuanzia mchakato hadi walipotoka bungeni.

Haiwezekani wakazuia mchakato ukiwa uraiani ambako CCM wanajua mchezo vizuri sana. Tuangalie haya kwa ufupi

1. Matokeo ya uchaguzi wa 2010 hadi leo matokeo kamili hayapo. Tume ya uchaguzi ilipoulizwa kuhusu usahihi wa matokeo, haikuwa na jibu bali kusema matokeo yasingebadilisha chochote.

Je, kura ya kila mtu ilihesabiwa? Na kama tume ilikuja na hoja za kipuuzi kama hizo, nini kinawashinda kuja na hoja kama hiyo wakati wa kura ya maoni?

2. Matokeo ya serikali za mitaa yanaonyesha jinsi ambavyo CCM na vyombo vyake wanavyoweza kutumia kila mbinu kupata ushindi, halali haramu.

3.Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu ametenga bilioni 2.5 kama kianzio cha kampeni.
Nini kitawashinda kuchota mipesa zaidi hazina ili kuhakikisha kura ya maoni inapita?

Na kwanini Ikulu ihangaike kughilibu umma kwa nyaraka ya umma?
Nani anaweza kuzuia vyombo vya dola,vitende haki ikiwa mwenye umiliki wa vyombo hivyo anagawa rushwa kama njugu?

4. Mwenyekiti wa CCM ndiye amekuwa msemaji wa tume ya uchaguzi, akitoa ratiba, taratibu na maelekezo.

Tume ya uchaguzi ambayo ni tawi la ''Uchaguzi-CCM'' litakuwa na uwezo gani wa kutamka jambo kinyume na maelekezo ya mwenyekiti wa CCM aliyechukua jukumu la kura ya maoni kwasasa?

5. UKAWA wameshuhudia CCM wakijiibia kura pale Dodoma chini ya Sitta, wakiruhusu kura ya maruhani wasiojulikana, wakihesabu kura za face book n.k.

Yote yamefanyika wakiwa wenyewe bila aibu na dunia ikaona, leo UKAWA wanapata wapi nguvu za kuzuia kura ya maoni ya hapana, ikiwa dunia imeshuhudia na wahusika hawana mtima wa aibu!

8. UKAWA waliona tume ya Warioba ilivyonyanyaswa, dharauliwa na kudhalilishwa.

Hiyo ni tume iliyowekwa kisheria ikisheni watu wenye heshima zao katika taifa hili.
CCM hawakujali, walitenda yao.
Leo UKAWA wanawezaje kuzuia katiba ya Chenge kwa kura ya hapana!

Orodha ni ndefu, inatosha kusema kuwa kazi kubwa iliyokuwa nayo CCM ni kuhakikisha katiba yao inapita ndani ya bunge la katiba. Huko mitaani hata aje malaika CCM itashinda.

Iwe kwa asilimia 90 au 99 lazima zitapatikana. Hivyo, anayedhani anaweza kupiga kura ya hapana ikahesabiwa ni mwendawazimu. Zile za mwaka 2010 hazikuhesabiwa zote seuse hizi zinazosimamiwa na Ikulu yenyewe. Tume ya uchaguzi imebaki kuwa kamati ya BVR ikipoteza maana yake halisi na kuwa kibaraka wa serikali

Kundi la pili, ni la watu walionunuliwa kama wapinzani.
Hawa nao watawababisha ukawa kwa hoja laini za kuvutia.
Tumeshuhudia wasomi, viongozi wa dini, wanahabari n.k. wakipangiwa bei zao hadharani.

Hivyo, UKAWA lazima wajihadhari na ''wapinzani wenye uchungu'' ambao tayari wamepata mafao yao.

UKAWA wafanye nini!
Msimamo uliowatoa bungeni ndio msingi wa hoja yao. Mchakato ulivurugwa, katiba ya Chenge haikutokana na wananchi na madai ya katiba mpya hayajatekelezwa.

Huo ndio msimamo utakaojenga hoja mpya ya kudai katiba kama agenda ya uchaguzi.

Ukawa watumie agenda hiyo kupata wabunge wengi, wakisimama katika kuhesabu wabunge wa CCM walioshiriki uovu kwa majina, majimbo na michango yao ndani ya BMLK, katika mikutano na wananchi mijini na vijijini.

UKAWA wasishiriki au kuongelea katiba ya Chenge. Kufanya hivyo ni kuipa uhalali ambao CCM ina utafuta.

Katiba ya Chenge ambayo ni ya CCM iachwe ipigiwe kura na CCM na hilo litajenga uhalali wa madai ya katiba mpya ya wananchi. Madai hayo yaanze sasa kuelekea October 2015 na katiba mpya ni sehemu ya agenda za uchaguzi wa 2015

Kama kuna makosa UKAWA watakayorudia kama kawaida yao, ni kuyasikiliza makundi mawili yaliyojadiliwa hapo juu.

Hoja za makundi hayo zisifikiriwe kabisa, zidharauliwe na zipewe kisogo.

UKAWA wasifanye kosa la kujadili hata mstari mmoja wa katiba ya Chenge.
Kosa hilo litajenga uhalali katika haramu ya katiba ya Chenge.

Na mwisho, UKAWA wahimize watu wao kujiandikisha kwa uchaguzi, wakifafanua si kwa kura ya maoni, na wakati huo huo wakiwaelimisha wananchi kususia zoezi zima la kura ya maoni kwa vile katiba iinayoandaliwa ni ya CCM.

Ya wananchi ipo mbioni

Tusemezane
 
Nakuheshimu mkuu,lakini kuna vitu umejaribu kuwa mtabiri,jambo ambalo si kweli,unaposema wananchi wameisusa,wananchi gani hao,mtaa gani,Kata gani,wilaya,mkoa,vinginevyo itabaki kua Hisia
 
Nakuheshimu mkuu,lakini kuna vitu umejaribu kuwa mtabiri,jambo ambalo si kweli,unaposema wananchi wameisusa,wananchi gani hao,mtaa gani,Kata gani,wilaya,mkoa,vinginevyo itabaki kua Hisia
Adharusi
Nadhani unaweza kuona tofauti ya msisimko wa rasimu I &II, ukilinganisha na katiba pendekezwa.

Kwa uchache, ilitarajiwa katiba -Chenge iwe na msisimko mkubwa Zaidi.


Kwa hali iliyopo, rasimu ya kwanza ilikuwa na msisimko Zaidiya katiba ya Chenge

Pili, angalia vyombo vya habari rasmi na vile vya kijamii.Ni wangapi wanaongelea katiba-Chege?
Hakuna mwenye interest ya kukijadili.


Tatu, unakumbuka rasimu ilivyokuwa inajadiliwa katika vituovya TV?
Endapo unadhani ni utabiri, muulize mkurugenzi wamawasiliano Ikulu.

Warakawake unaonyesha kutenga mafungu ya kuhonga wanahabari na wasomi kuletamsisimko.

Kulikuwa na haja gani ya kutenga mabilioni kwa nyaraka ya wananchi?


Hilo halina maana katiba chenge haijadiliwi, kinachotokea,waliohongwa wanapiga debe kwa nguvu.
Wenye katiba ambao ni wananchi wapo baridi kabisa.
 
KATIBA: CCM YABANWAKULIA KUSHOTO
TAMKO LA JUMUIYA YAKIKISTO LINA WALAKINI
SERIKALI IMEFUNDISHA,WANAFUNZI WANAJIBU

Sehemu ya I


Jumuiya za dini ya Waislam zilitoa matamko kuhusu katiba. Zilisema suala la kadhi lisipokuwepo kikatiba, watahamasisha waumini wasusie kura yamaoni ya katiba ya Chenge

Jumuiya ya kikrsito imetoa tamko likihimiza kuikataa katiba ya Chenge wakati wa kura za maoni

Wapo watakaolaumu viongozi wa dini kuchanganya dini na siasa.

Serikali ndio iliyo asisi msemo huo. Ni makosa kuzilaumujumuiya za dini kutoa maoni.

Inapotokea waziri katika serikali yupo kanisaniakizungumzia katiba, hatutegemei waumini wakae kimya.

Tamko la jumuiya zakikristo ni majibu ya mafunzo yaliyotolewa kanisani.


CCM wanapotoa ahadi za mahakama ya kadhi ili kupata kura,hatutarajii waumini wakae kimya.
Matamko ya jumuiya za kiislam ni majibukutokana na mafunzo ya CCM


Hivyo, ni vema kusema, serikali imewafundisha na sasawanafunzi wanajibu somo.

Waziri mkuu

Katika kuhaha ili katiba iungwe mkono, waziri mkuu amesema suala la mahakama ya kadhi linarudi tena bungeni.

Hii ni baada ya kubanwaupande mmoja. Kabla halijarudi bungeni wengine wanaona ni suala la kuligawa taifa.


Ni haki kusema, serikali imebanwa kulia na kushoto. Haina pakutokea. Imebanwa kulia na kushoto

TAMKO LA JUMUIYA ZA KIKRISTO

Tamko la jumuiya limekuja miezi mingi baada ya katiba yaChenge kusukumizwa kwa hila na mbinu.

Jumuiya zinasema hakukuwana uadilifu, nchi imegawanyika, likisisitiza kuhusu mahakama ya kadhi.

Na kwamba, serikali inalitumia suala hilo kama hongo na mchakato mzimaulikosa uadilifu


Tamko hilo linaendelea kusisitiza kuwa wananchi wajiandikishe, washiriki mchakato mzima, wasome katiba na kuielewa na mwisho wapige kura ya hapana

Kwa maoni ya duru za siasa, tamko lina walakini.

Kwanza, jumuiya haikuunga mkono wapinzani wakati uhuni wa mswadawa sharia ya kuanzisha mchakato ilipoanza.

Wapinzani walisema, bunge la katibaliwe na wabunge watakaochaguliwa kutoka katika makundi ya jamii na si 201watakaoteuliwa na Rais


Lengo la wpinzani lilikuwa kuhakikisha makundi ya jamii yanachagua watu watakaosimia masilahi yao kwa upana na weledi. Kilichotokea, sheria ikampa Rais kuchagua wabunge.

Kwa muda wote huo si jumuiya ya wakristo auwaislam walioonyesha kukerwa na hilo.


Inaendelea...

Seemu ya II
 
Back
Top Bottom