Duru: UKAWA njia panda, CCM maji ya shingo

Duru: UKAWA njia panda, CCM maji ya shingo

KATIBA: CCM YABANWA KULIA KUSHOTO

TAMKO LA JUMUIYA YAKIKISTO LINA WALAKINI

SERIKALI IMEFUNDISHA''WANAFUNZI WANAJIBU''

Sehemu ya I

Jumuiya za dini ya Waislam zilitoa matamko kuhusu katiba. Zilisemasuala la kadhi lisipokuwepo kikatiba, watahamasisha waumini wasusie kura yamaoni ya katiba ya Chenge

Jumuiya ya kikrsito imetoa tamko likihimiza kuikataa katibaya Chenge wakati wa kura za maoni
Wapo takaolaumu viongozi wa dini kuchanganya dini na siasa.

Serikali ndio iliyo asisi msemo huo. Ni makosa kuzilaumujumuiya za dini kutoa maoni.

Inapotokea waziri katika serikali yupo kanisaniakizungumzia katiba, hatutegemei waumini wakae kimya.

Tamko la jumuiya zakikristo ni majibu ya mafunzo yaliyotolewa kanisani na akina Lukuvi

CCM wanapotoa ahadi za mahakama ya kadhi ili kupata kura,hatutarajii waumini wakae kimya.

Matamko ya jumuiya za kiislam ni majibu kutokana na mafunzo ya CCM

Hivyo, ni vema kusema, serikali imewafundisha na sasawanafunzi wanajibu somo.

Waziri mkuu

Katika kuhaha ili katiba iungwe mkono, waziri mkuu amesema suala la mahakama ya kadhi linarudi tena bungeni.

Hii ni baada ya kubanwa upande mmoja. Kabla halijarudi bungeni wengine wanaona ni suala la kuligawa taifa.

Ni haki kusema, serikali imebanwa kulia na kushoto. Haina pakutokea na ujanja na ubabe wa katiba sasa unaiumiza. Imebanwa kulia na kushoto

TAMKO LA JUMUIYA ZA KIKRISTO

Tamko la jumuiya limekuja miezi mingi baada ya katiba yaChenge kusukumizwa kwa hila na mbinu.

Katika tamko, jumuiya zinasema hakukuwa na uadilifu, nchi imegawanyika hasa likisisitiza kuhusu mahakama ya kadhi.

Jumuiya inasema, serikali inalitumia suala hilo kama hongo na mchakato mzimaulikosa uadilifu

Tamko hilo linaendelea kusisitiza kuwa wananchiwajiandikishe, washiriki mchakato mzima, wasome katiba na kuielewa na mwisho wapige kura ya hapana

Kwa maoni ya duru za siasa, tamko la jumuiya za kikristo lina walakini.

Kwanza, jumuiya haikuunga mkono wapinzani wakati uhuni wa mswadawa sheria ya kuanzisha mchakato ilipoanza.

Wapinzani walisema, bunge la katibaliwe na wabunge watakaochaguliwa kutoka katika makundi ya jamii na si 201watakaoteuliwa na Rais

Lengo la wpinzani lilikuwa kuhakikisha makundi ya jamii yanachagua watu watakao simamia masilahi yao kwa upana Kilichotokea, sheria ikampa Rais kuchagua wabunge.

Kwa muda wote huo si jumuiya ya wakristo auwaislam walioonyesha kukerwa na hilo.

Kwa uoande wa waislam, walikuwepo masheikh wa jumuiya ziizonje ya Bakwata na wale wa Bakwata.
Kwa upande wa wakristo nako walikuwepo wa jumuiya kubwa yawakatoliki na wale wa kiprotestant

Makundi yote mawili hayana uadilifu wa kuhoji uadilifu wabunge wakati yalikaa kimya wakati uadilifu unachakachuliwa!

Makundi yote mawili yaliungana kuandika waraka wa kulaani UKAWA na kuunga mkono mchakato.

Hakuna taasisi ya nje si ya waislam au wakristo iliyowakemea kwa kununuliwa.

Leo matamko yanahusu nini? Hawa watu wa dini hawakuona ukosefu wa maadili kuanzia mwanzo

Inaendelea II
 
Sehemu ya II

Sitta alipoamuru kura za facebook, hakuna jumuiya(wakristo,waislam) iliyokemea uhuni huo.
Leo wanahoji vipi kuhusu uadilifu wakati uadilifu ukichakachuliwa walikuwa kimya?

Tamko la jumuiya ya wakristo linahimiza waumini wao wajiandikishe katika daftari la kura.
Hata pale tunapojua kuna tatizo lauandikishaji, duru tunahimiza wajiandikishe.

Tunachokiona kama kasoro ya tamko la wakristo ni kuhusu uadilifu. Wanasema mchakato wa katiba haukuwa na uadilifu.

Halafu wanasema wananchi washiriki hatua zote za mchakato kuelekea kura ya maoni na wapige kura ya hapana.

Hivi, kushiriki mchakato haramu, haitoshi kuwa ni kutoa uhalali kwa mchakato wakristo wanaosema hauna uadilifu?

Kwamba, kuna uchafu lakini wananchi washiriki kujadili uchafu huo. Huu ni walakini mkubwa sana watamko

Kisha wakristo wanasema, wananchi wasome na kuielewa vema katiba.
Sasa kama katiba ni zao la kukosa uadilifu, wananchi wasome kuelewa nini?

Kuelewa uadilifu ulivyokosekana au kuelewa katiba inasemaje? Walakini wapili

Na mwisho, wakristo wanasema ipigwe kura ya ‘hapana'.

Sasa ikiwa tamko la jumuiya linasema wananchi wasome na waelewe, inakuwaje waongozwe na tamko lililotokewa hata kabla ya kusoma.

Je, jumuiya haioni kufanya hivyo nikuwaburuza waumini? Walakni mkubwa

Na mwisho jumuiya inaelewa, kura ya maoni inaandaliwa na tume ya uchaguzi ya CCM.

Maaskofu hawaoni kukosekana uadilifu wa mchakato hakutatakaswa na matokeo ya tume ya uchaguzi ya CCM?
Na wala kura ya hapana haitashinda hata wakikesha. Walakini

Duru tunasema, mbegu mbaya iliyopandwa na CCM sasa inachanua.

Waacheni viongozi wa dhini wajibu hoja zenu mnazohubiri misikitini na makanisani

Ile kauli ya kuchanganya dini na siasa haina maana kwavile ninyi mnachanganya siasa na dini

Kwa jumuiya za dini zote,hili liwe funzo kuwa CCM haiaminiki na wala haiwezi tena kuongoza.

Ni busara kuziba ufa kuliko kujenga ukuta.

Waislam na Wakristo walioona Soni kukemea uovu mwanzoni, hawana tena mamlaka ya roho ya kukemea mchakato

Tuacheni tuliosema mapema tuendelee kusema. Ninyi rudini mlishashindwa kazi kwa pepo la CCM.

Mumeshindwa na kulegea.
Pepo hatoki hata mkinena na kudhikiri. Mlishakubali hongo za CCM

Tusemezane
 
HALI YA KATIBA NI TETE SANA

MAKUNDI YANAZIDI KUJITOKEZA

Tuliona makundi ya Bakwata na Baraza la taasisi za kiislam.
Kama tulivyoeleza hapo juu, yote yalikuwa na wawakilishi ndani ya bunge maalumu la katiba.
Misimamo yao inakinzana , kila kundi likiwa na msimamo wake

Juzi, kulikuwa na kikao cha jukwaa la wakristo lililotoa tamko kuhusu katiba ya Chenge.

Kikubwa ilikuwa kuhimiza watu kujiandikisha, kushiriki na kupiga kura ya hapana. Utata wa mambo hayo matatu tumeueleza hapo juu

Leo kadinali Pengo, kiongozi wa Wakatoliki amepingana na msimamo wa jukwaa la wakristo.

Alcihokisema ni kuwa jukwaa hilo halina mamlaka ya kuamua waumini wapige kura gani, bali wasome na kufikia maamuzi wenyewe.

Kauli ya Pengo, si ya kushangaza. Itaeleweka, Kadinali ni muumini wa serikali mbili.

Alipinga sana uwepo wa serikali tatu. Kiuchambuzi, si kuwa kadinali anataka serikali mbili kama njia ya kutatua mgogoro.

Kwa jinsi ilivyo, uwepo wa serikali mbili unatoa nafasi ya udhibiti wa Zanzibar kama tunavyoeleza kila siku

Hofu ya kadinali ni kuwa, znz itakapokuwa na serikali yake huru, pengine kanisa katoliki litakosa nafasi waliyo nayo sasa.

Hilo linafikiriwa na kadinali kwa kuzingatia kuwa SMZ inaweza kuzuia madhehebu mengine kufanya shughuli zao znz.

Ukisoma kauli zake, Kadinali hakupingana na maaskofu kuwa mchakato hauna uadilifu, umegubikwa na ubabe na umeligawa taifa.

Kadinali anaonekana kukubaliana na hayo, ingawa msimamo wake ni watu kuendelea kusoma katiba ya Chenge.

Kadinali Pengo hajatazama haki kwa ukweli na uhalisia wake.

Hakuna zao halali linalotoka katika mti haramu.
Mchakato mzima ulikuwa wa kibabe, rushwa, udanganyifu na kila aina ya dhambi.

Haieleweki ni kwanini kadinali hajaliona hilo, bali anasisitiza waumini wasome katiba ya Chenge, ambayo ni haramu ili waje na fikra zitakazokuwa halali.

Kauli ya Pengo inaonyesha jinsi taifa lilivyogawanyika.

Si kati ya vyama vya siasa, bali dini na dini, madhehebu moja na nyingine.

Hakika kuendelea na mchakato wa katiba ya Chenge ni kutengeneza hali tete siku za usoni.

Duru siku zote tumesisitiza kuwa, kilichotakiwa ni kuwa na mkutano wa kitaifa wenye agenda ya katiba.
Hata pale iliposhindikana, rasimu ingeweza kuja na suluhu afadhali kuliko katiba ya Chenge

Mkutano wa kitaifa ungeamua tunataka kujenga taifa gani, kwa njia zipi n.k.

Hizi changamoto zinaozonekana sasa hivi zingepata majibu na mchakato ungeelea na kuselelea bila matatizo.

Kuzuka kwa makundi hasa miongoni mwa dini kuu, yakipingana ndani na miongoni mwao, na njekati ya moja na jingine si jambo linaloashiria mwisho mwema hata kidogo

Kwa hali ilivyo hali ni tete hata kama haisemwi na haitakiwi kusemwa

Tusemezane
 
nguruvi 3 msimamo wa baraza la wakristo ambao unaundwa na makanisa yote ya kiprotestant na RC ulikuwa na lengo la kuhamasisha watu wapige kura ya hapana kwa sababu wanaelewa fika kwamba kutokujitokeza kwao kupiga kura ndicho kitakacho wamaliza watanzania.

kiukweli ikiwa wananchi wengi wwatajiandikisha na kupiga kura ya hapana ndio suluhu pekee ya kuhakikisha katiba ya Chenge haipiti. ikiwa watu hawatajitokeza kupiga kura basi ni wazi iyo katiba itapita.

utata unaligubika kanisa la RC kutoka kwa kiongozi wao mkuu ni wazi kwamba anayohofu ya kukosa nafasi ya kuwa na kanisa Z'BAR. lakin tujiulize ivi ikiwa tayari kunao wakristo zbar je watakataliwa kuwa wakristo kwasabbu tu ya kwamba ni serikali inayojitegemea?

na je sisi kama akisema huo sio msimamo wa wakristo inamaana anataka kusema kwenye hilo jukwaa la wakristo RC hawamo? ikumbukwe kabisa kanisa hili la RC tayari lilishakubali kuwa kwenye kashfa mbaya ambayo tena ni dhambi kwa taifa ya ESCROW ambapo benki ya Mkombozi imetumika kutakatisha fedha chafu. sasa sijui anashindwa kumudu hali na mwenendo wa taifa kwa sasa anaanza kujiuma uma??

muda mwingine nimewaza inawezekana kabisa pia ni njia yake ya kutafuta huruma ya serikali manake kwa kashfa iliyonayo ni wazi kwamba hata benki yake inatakiwa kuchukuliwa hatua na benk kuu.
 
Last edited by a moderator:
bppengo.jpg

Mwadhama Laureano Cardinali Rugambwa anakumbukwa kwa unyenyekevu na kuheshimu uwajibikaji wa pamoja
katika kanisa bila kuonyesha makuu wala kutoa kauli tatanishi zinazopingana na uwajibikaji wa pamoja kikanisa.

gfsonwin,
Pengo anadhalilisha kanisa Katoliki. Yeye si msemaji bali ni member katika barala la Maaskofu katoliki Tanzania chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye ni msemaji wa kanisa Katoliki na ni Mwenyekiti wa Baraza hilo Tanzania kwa sasa ni Askofu Tarsisius Ngalalekumtwa wa Jimbo Katoliki Iringa.

Pengo si mkuu wa kanisa katoliki Tanzania, ila cheo chake ni cha heshima kuwakilisha kwenye halmashauri ya Pope Vatican- Rome, na anachofanya Mwadhama Pengo ni sawa na mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM anayewakilisha wilaya kuchukua majukumu ya mwenyekiti wa CCM wa wilaya. Kila Jimbo katoliki duniani linawajibika moja kwa moja kwa Pope, Vatican. Kuna mwenyekiti wa baraza la Maaskofu kila nchi na ukanda anayekuwa msemaji baada ya maridhiano ya pamoja huwa ni kauli moja si kama upwayukaji wa Pengo anaharibu nafasi na heshima ya cheo chake katika kanisa.

Tunamkumbuka sasa hayati Laureano Cardinal Rugambwa ambaye aliheshimu sana maamuzi ya vikao tofauti na Pengo anayepwayuka ovyo ovyo nje ya vikao na kinyume cha makubaliano ya pamoja ya vikao. Pengo amevunja utaratibu wa uwajibikaji wa pamoja kikanisa kadiri ya mapokeo na utaratibu wa Kanisa Katoliki. Labda anasimama upande wa CCM na serikali kumkingia kifua Waziri Mkuu Pinda wanayetoka kabila moja?

Kauli ya kanisa Katoliki inatakiwa kutambuliwa inayotolewa na mwenyekiti wake, au makamu wake kwa niaba ya mwenyekiti kauli ambayo huwa inatokana na uwajibikaji wa pamoja kikanisa baada ya makubaliano katika vikao vyao, na hapo wapo walio kinyume lakini wengi wape na walio kinyume wanawajibika kwa pamoja kufuata ukubali wa wengi. Hapo ndipo Pengo anapoharibu na kujidhalilisha nafasi yake kama askofu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam bila kufuata uwajibikaji wa pamoja. Umeshaona Maaskofu kila mmoja anatoa kauli jimboni mwake? La hasha ila kinachosomwa ni waraka kutoka ofisi kuu ya TEC.
 
gfsonwin , ahsante sana na naomba nizipitie hoja zako katika sehemu kuu mbili

Sehemu ya I

Kuna mambo ya kuyaangalia kwa jicho lingiine.

Kwanza, CCM wameweka suala la kujiandikisha kama sehemu ya hatua za uchaguzi mkuu.

Kwa kuona katiba ya Chenge haiuziki na kwakutambua uhuni walioufanya Dodoma, kujiandikisha kwa kuambatanishwa na kura yao ya maoni

Lengo ni kuweka mtego kwa wananchi wa kawaida kuwa, bila kujiandikisha na kupiga kura ya maoni hakuna uwezekano wa kupiga kura uchaguzi mkuu.

Hapa ukweli wa kujiandikisha unachanganywa na haki ya kujiandikisha katika daftari kwa minajili ya kupiga kura.
Msisitizo wanaouweka ni kuwa kura ya maoni ndio ufunguo wa kupiga kura

Pili, CCM walijua kikwazo cha katiba ni BMLK. Ndio msingi wakusema, wapinzani walishiriki hata kama ni Mrema na Cheyo wakificha ukweli wapinzani zaidi ya 100 na wengine 200 na ushee hawakushiriki.

Walichotaka ni kupitisha katiba yao wakijua mbele ya safari hakuna wa kuwazuia wala cha kuwazuia.

Wanajua , vyombo vyote vya dola wanavyona hivyo kura ni ushahidi tu, matokeo wanayo hadi sasa.

Tatu, UKAWA kuondoka ni kutoridhika na mchakato.
Hakuna shaka UKAWA wanawakilisha sehemu kubwa sana ya jamii inayoona uhuni uliofanyikaDodoma.

Hivyo, katiba ya Chenge inakosa uhalali wa kisiasa, na hata kisheriakutokana na jinsi kanuni, na sharia zilivyokuwa zinabadilishwa ili kujenga mazingira ya CCM na si wananchi

(i)Kushiriki kura ya maoni ni kukubali kuwa kilichofanyika UKAWA wakiwa hawapo ni halali.
Kama unapiga kura ya hapana, tayari umesharidhia kila kitu na wananchi wawe tayari kukubaliana na matokeo.

(ii)Kura ya maoni inaondoa haki ya kudai katiba. Kwa maana watu walishiriki sasa wanadai nini?

Shemu ya II inaendelea..
 
Last edited by a moderator:
Sehemu ya II

Kura ya hapana au ndio ni maigizo ambayo CCM wanayajua vema.

Tulishazoe watu kushinda kwa asilimia 99 tena wakipangwa.
Hayo yametokea ndani ya halmashauri kuu na mkutano mkuu. Kwani si unakumbuka neno'kura hazijatimia?

Ndani ya BMLK Samwel Sitta amepata kura za watu wasiojulikana kwasababu hawakuwemo bungeni.

Sitta akakusanya kura za facebook, halijawahi kutokea tangu uhuru
Hesabu zikapigwa na wabunge wa NCCR wakajikuta wameiga kura za ndio ingawa hawakuwemo bungeni

Katika mazingira hayo, nani anaweza kuwazuia CCM huko Tandahimba, Nanyumbu, Mwandiga, Magoroto n.k.?

VYOMBO VYA DOLA
Tunafahamu kazi za wakuu wa wilaya na mikoa, Polisi, usalama wa taifa ni kutekeleza yale ya CCM
Nani anaweza kusimama na kuhoji matokeo yaliyopangwa na CCM kupitia tume ya uchaguzi NEC?

Hadi sasa hivi, tume ya uchaguzi imenyeng'anywa mamlaka.
Rais ndiye anatangaza ratiba za shughuli za tume.
Tume imebbaki kupewa maagizo mengine yakiwa hayatekelezeki.
Mwenyekiti wa CCM kasema pesa zitatoka ili mfumo wa BVR ufanyike

Mkoa wa Njombe ambao ni mpya umetumia zaidi ya wiki 2. Tuki assume kuwa tume inafanya kazi usiku na mchana, mkoa mmoja unaweza kutumia siku 7.

Hiyo ni assumption kuwa kila kitu kipo sawa sawa. Mikoa 26 iliyobaki iitatumia zaidi ya siku 125 ambazo ni sawa na miezi 4. Hapo hatujafikiria mikoa yenye population na mikubwa kama Morogoro na Kilimanjaro (idadi)

Hivyo kufikiria siku 7 ni ndoto, kazi haiwezi kukamilika ndani ya siku 45.

Tume ya uchaguzi inajua hilo, lakini wao ni watumishi wa chama Lumumba, hawawezi kukana kauli ya mwenyekiti. Wanaendelea na mzaingaombwe

Katika hali hiyo, hivi watu wanaamini kuwa tume inaweza kutangaza matokeo halali ya hapana?

Tunajua ya halali yapo, kinachoangaliwa ni asilimia ngapi.
Je, kuna umuhimu wa kuzuia gharika unaojua ni kubwa kuliko mlima?

Suala la kura ya hapana haliwezekani, ni njia rahisi sana ya kuhalalisha uhalifu.

Siku tume ikitangaza, ndio utakuwa mwisho wa mjadala wa katiba. Kwanini watu watupiwe kitanzi na kisha wakifunge shingoni?Kura ya hapana haitazaa matokeo ya aina yoyote ile ambayo CCM haiyataki. Hilo halitawezekana

KUSUSIA KUNA MAANA GANI
Kwamba, CCM watakuwa wameandika katiba yao, na wananchi waanze sasa kudai katiba ya nchi.

CCM wakilazimisha goli la mkono, hiyo haitaondoa uhalali wa madai ya wananchi na itakuwa ni chachu ya kudai mageuzi si ya katiba bali nchi kwa ujumla

Wananchi wanachotakiwa, kwanza kuwaadhibu wabunge wa CCM walioshiriki uhuni ule.

Wawaambie bila kificho kuwa hawahitaji tena na wala hawatarudi Dodoma. Wasiwasikilize kabisa
Wabunge wa CCM waende CCM kutumikia katiba yao ya kihuni.

Pili, wananchi waanze madai ya katiba sasa hivi, na wapuuze kabisa kura ya maoni.
Wajiandikishe lakini wasishiriki kura ya maoni

Tatu, wananchi wafanye maamuzi magumu ya kukomesha kiburi, dharau, kejeli ya CCM na viongozi wao.

Nne, wapinzani wameshapata agenda. Kwanza, kudai katiba mpya inayoliliwa na wananchi.
Halafu kuonyesha upuuzi na ubabe wa CCM. Kwamba, wezi walioibia wananchi ndio waliojiandikia katiba yao na kupuuza maoni ya wananchi. Katiba iliyoandikwa na wenye milioni za mboga na vijisenti haifa, haikubaliki wala kujadilika

Tano, wapinzani wawaambie wananchi, miaka 50 inatosha kudhalilishwa.

Ni kutokana na kiburi cha CCM siku hizi wanasema bila hata hofu.
Milioni 10 pesa za mchicha na sukuma wiki, bilioni 2 vijisenti vya unga, wananchi wanachoweza ni kuuza nyanya n.k.

CCM wanafanya ubabe kwasababu wanaelewa udhaifu wa Watanzania.
Kwamba, watawatupia mzoga kisha kuwaamuru wale watake wasitake.

Ndilo hili la katiba. Bila kuanza kuonyesha kuchoshwa na uhuni, kila siku wataiba pesa, bili watalipa wananchi.

Kisha wanasema ni pesa za kununua dagaa, furu, nguruka, vitoga na migebuka.

Kususia katiba ndilo jibu, kinyume chake wananchi watakuwa wametoa uhalali wa haramu.

Kuhusu suala la Pengo, nitakujibu na Candid scope kwa pamoja
 
KAULI YA PENGO
gfsonwin na Candid Scope

Kwanza, katika jukwaa lwa wakristo, wakatoliki wapo na wamewakilishwa.
Kauli ya Pengo inaonyesha ni yake na si msimamo wa pamoja.
Candid scope kaeleza vema taratibu za kutoa kauli kama kanisa kupitia majimbo.

Kauli ya Kadinali Pengo si kuwa imemdhalilisha Nagalalkumtwa, bali pia imejenga ufa kati ya wakatoliki na waprotestant.

Alikuwepo Mwalusasu na wenzake wengine. Wao watajisikia wamefedheheshwa na Pengo ambaye Candid Scope amemueleza ni 'ceremonial''

Pia nakubaliana na Candid kuwa Kadinali Pengo amekuwa na utofauti mkubwa sana na mzee Rugambwa.
Tangu alipoteuliwa, Kadinali amekuwa na kauli zenye utata na zingine zikiwa hazina kipimo sahihi kwa nafasi yake

Kadinali Pengo leo anasema waumini waachiwe waamue. Huko nyuma, alishawahi kutoa maoni kuwa yeye angependelea mfumo wa Serikali mbili. Hakuacha wananchi waamue kama anavyosema leo. Aliwapa msimamo wake na kanisa

Hakueleza kwanini, alichojaribu kusema ni kuwa S2 zinaleta umoja wa kitaifa.
Na kwamba S3 zitaligawa taifa. Huo ndio msimamo wa Ploycarp kadinali Pengo.

Kauli yake kuwa waumini waachwe waamue imekuja wakati maaskofu wakisema mchakato mzima uligubikwa na ubabe, kukosa uadilifu, na kila uovu.

Anachosema Pengo ni kuwa maaskofu hao ni waongo, mchakato ulikuwa sahihi, wananchi waachwe waamue.

Kwa maneno mengine, Pengo anatoa baraka kwa katiba ya Chenge, halafu anarudi madhabahuni kusema nchi imekosa maadili.

Kadinali, haiwezekani mchakato haramu uzae katiba halali.
Pengo anafahamu hilo, lakini kuna kinachomsukuma.

Yeye anataka S2 kwa hofu tu kuwa S3 zitaondoa udhibiti wa Zanzibar na hivyo kumpa nafasi zaidi kule visiwani.
Ana hofu ile ile aliyoisema waziri Lukuvi ndani ya kanisa.

Tena ukiangalia kwa umakini, kuna mahusiano sana ya kauli ya Lukuvi na msimamo wa Pengo.

Hivyo, yeye anaridhika na katiba ya Chenge kwavile tu ina kipengelea anachodhani ni muhimu kwake.

Hofu hii si ya lazima kwa mwanadamu. Pengo anatakiwa asome historia na aangalie nini kimetokea wapi na kwanini.

Msimamo wa Pengo wa S2 ndio unamsukuma kuwasuta, na kuwadhalilisha wenzake.

Msimo wake hauna jingine bali hofu yake juu ya znz kuwa ni eneo tofauti ambalo yeye anadhani litamkwaza katika harakati zake za kidini.

Ni hofu isiyokuwa na msingi kwasababu kanisa la kwanza EA lipo znz.

Na huu ni muungano, hata kama si S3, inaweza kuwa S2 na muungano ukafa kama inavyotarajiwa.
Je, Pengo atatamani znz ipigwe mabomu?
 
sasa hapa nimeelewa jambo jingine ambalo nilikuwa sijaliangali kwa mapana haya.
but wait, ivi inamaana kwamba ukivote hapana bado watalazimisha iwe katiba?
na je kama tusipokwenda kabisa bado wale walio na mapenzi mema ya serikali ya CCM hawata tu deceive?

kuna mtego ninao uona hapa kwamba tusipovote no wachache wataipitisha, lkn pia uwezekano wa kura kuibiwa tukaambiwa tulivote Yes ni mkubwa pia

na pia iwapo hatutaenda kabisa kupiga kura bado wana ccm wataenda na watapiga kura ya ndiyo na katiba itapita.

nafkiri tuchukue uamuzi mwingine hapa kabla hatujachelewa wa kwenda mahakamani kuweka zuio la kura ya maoni na this time sisi watanzania ndio twende na sio kundi fulan. mfano naamini tunaweza kusaini petition against iyo katiba tuko miliona 45 tukipata watu wazima robo ya idadi ya watu wote wazima basi tunaweza bila kuonyesha itikadi tukafungua kesi ya msingi dhidi ya katiba hii. ama hapa nimekosea??
naomba ufafanuzi
 
sijui kwanini nimejikuta namuonea huruma Ngalalakumtwa, lkn binafsi nilishiriki kwenye misa moja aliyokuwa anapongezwa askofu huyu kwa kutimiza miaka 25 ya uaskofu.

alichokiongea kuhusu mwenendo wa nchi kwa sasa alikuwa sahihi sna. najua serikali inamuona kama threat na Pendo naye amejikuta kwenye huu mkumbo wa kumuona threat na hivyo kutaka kumdefeat kwa nafasi yake ya ukadinali.

niseme wazi kwamba ishu ya dini ya RC kukosa mianya ya kujistawisha Z'bar bado ni ndogo sana ukilinganisha na uhitaj wa S3 ambao tunautaka.

hivi leo hii askofu ataona sawa kuona watanganyika tunapigwa bomu wote kisa tu dini?
 
sasa hapa nimeelewa jambo jingine ambalo nilikuwa sijaliangali kwa mapana haya.
but wait, ivi inamaana kwamba ukivote hapana bado watalazimisha iwe katiba?
na je kama tusipokwenda kabisa bado wale walio na mapenzi mema ya serikali ya CCM hawata tu deceive?

kuna mtego ninao uona hapa kwamba tusipovote no wachache wataipitisha, lkn pia uwezekano wa kura kuibiwa tukaambiwa tulivote Yes ni mkubwa pia

na pia iwapo hatutaenda kabisa kupiga kura bado wana ccm wataenda na watapiga kura ya ndiyo na katiba itapita.

nafkiri tuchukue uamuzi mwingine hapa kabla hatujachelewa wa kwenda mahakamani kuweka zuio la kura ya maoni na this time sisi watanzania ndio twende na sio kundi fulan. mfano naamini tunaweza kusaini petition against iyo katiba tuko miliona 45 tukipata watu wazima robo ya idadi ya watu wote wazima basi tunaweza bila kuonyesha itikadi tukafungua kesi ya msingi dhidi ya katiba hii. ama hapa nimekosea??
naomba ufafanuzi
gfsonwin sualawanalotaka CCM ni kuhalalisha haramu yao. Siyo matokeo.

Wamebadili vifungu vta sharia kama kile cha 2/3 na kufanya50.1 %

Hii maana yake ni kuwa hawatatakiwa ku-justify matokeo yao.
Wanachotakiwa kufanya ni kupata 50.1% ambayo inapatikana ‘maabara' na si vituovya kura

Katika kuhakikisha wanafanikiwa, hata hiyo kura yaoinapelekwa mbio bila kuzingatia sharia.

Sheria iliyoanzisha mchakato imeanisha wazi muda wakujiandikisha na elimu kwa umma.

Vyote vinahitaji ziaid ya miezi miwili. Hali ilivyo sharia ya mchakato itabidi ikiukwe waweze kupiga kura yakatiba ya Chenge

Hapa ndipo hoja yako ya kwenda mahakamani inapokuwa nanguvu.
Kuna sheria nyingi zimekiukwa, taratibu zimekiukwa n.k.

Tatizo linguine litazuka huko mahakamani. Nadhani unajua mahakimu siku hizi wana account Mkombozi.

Wakubwa zao ni wateuliwa wamwenyekiti wa CCM. Nako Imani haipo kabisa.

Hata hivyo hiyo ni moja ya silaha ,kubwa ikiwa kususa kabisa
 
sasa hapa tunaenda sawa, skiliza Nguruvi3 unajua tukisema watu wasuse nakuhakikishia wale ambao tayari miamala yao ya Mkombozi ishasoma some 10[SUP]6[/SUP] nakuendelea wataipigia kura tu hata kama watakuwa 20.

mbaya zaid ni kwamba wapo ambao wanaishi kwa mkumbo tuu ambao wao hawaelewi zaid ya kusoma upepo unaendaje hawa ndio ambao hata pasipo mshiko wanahadaika na ndio walo wengi zaid ya wote.

kundi pekee ambalo nalitegemea ni lile la watu wanaojitambua ambao hawahadaiki kwa mkumbo wala kwa mshiko zaid ya kuona haki inatendeka ama kilicho bora kinatekelezeka. aina hii ya watu ni wachache sana na hawa najua wako tayari hata kwenda mahakan kupinga hii kura ya maoni.

nafikiri ndg yangu hapa tuanze kutafuta watu robo ya mil 26 ambao ni kama watu mil 6 tu ambao watakubali kusain petition tuweeke zuio mahakamani kisha tufungue kesi ya msingi.

tukifanya hivyo tutakuwa tumetumia delay technique na ambayo pia itasababisha watu kupata kuipitia zaid hiyo katiba ili mwisho wa siku wawe wameshajua wanakwenda kutoa vote ya aina gani.

lakin pia ikiwa tutashirikiana vizuri na wanasheria wachache basi uwezo wa kuishinda serikali mahakaman ni mkubwa sana na hivyo kubatilisha mchakato mzima.

nakubaliana na wewe kwamba kususa ni silaha nzuri lkn usisahau kwambu ukisusa wenzi wala na wale wanaokula ndio watakao tutia kitanzini
 
Last edited by a moderator:
Sehemu ya II

Kura ya hapana au ndio ni maigizo ambayo CCM wanayajua vema.

Tulishazoe watu kushinda kwa asilimia 99 tena wakipangwa.
Hayo yametokea ndani ya halmashauri kuu na mkutano mkuu. Kwani si unakumbuka neno'kura hazijatimia?

Ndani ya BMLK Samwel Sitta amepata kura za watu wasiojulikana kwasababu hawakuwemo bungeni.

Sitta akakusanya kura za facebook, halijawahi kutokea tangu uhuru
Hesabu zikapigwa na wabunge wa NCCR wakajikuta wameiga kura za ndio ingawa hawakuwemo bungeni

Katika mazingira hayo, nani anaweza kuwazuia CCM huko Tandahimba, Nanyumbu, Mwandiga, Magoroto n.k.?

VYOMBO VYA DOLA
Tunafahamu kazi za wakuu wa wilaya na mikoa, Polisi, usalama wa taifa ni kutekeleza yale ya CCM
Nani anaweza kusimama na kuhoji matokeo yaliyopangwa na CCM kupitia tume ya uchaguzi NEC?

Hadi sasa hivi, tume ya uchaguzi imenyeng'anywa mamlaka.
Rais ndiye anatangaza ratiba za shughuli za tume.
Tume imebbaki kupewa maagizo mengine yakiwa hayatekelezeki.
Mwenyekiti wa CCM kasema pesa zitatoka ili mfumo wa BVR ufanyike

Mkoa wa Njombe ambao ni mpya umetumia zaidi ya wiki 2. Tuki assume kuwa tume inafanya kazi usiku na mchana, mkoa mmoja unaweza kutumia siku 7.

Hiyo ni assumption kuwa kila kitu kipo sawa sawa. Mikoa 26 iliyobaki iitatumia zaidi ya siku 125 ambazo ni sawa na miezi 4. Hapo hatujafikiria mikoa yenye population na mikubwa kama Morogoro na Kilimanjaro (idadi)

Hivyo kufikiria siku 7 ni ndoto, kazi haiwezi kukamilika ndani ya siku 45.

Tume ya uchaguzi inajua hilo, lakini wao ni watumishi wa chama Lumumba, hawawezi kukana kauli ya mwenyekiti. Wanaendelea na mzaingaombwe

Katika hali hiyo, hivi watu wanaamini kuwa tume inaweza kutangaza matokeo halali ya hapana?

Tunajua ya halali yapo, kinachoangaliwa ni asilimia ngapi.
Je, kuna umuhimu wa kuzuia gharika unaojua ni kubwa kuliko mlima?

Suala la kura ya hapana haliwezekani, ni njia rahisi sana ya kuhalalisha uhalifu.

Siku tume ikitangaza, ndio utakuwa mwisho wa mjadala wa katiba. Kwanini watu watupiwe kitanzi na kisha wakifunge shingoni?Kura ya hapana haitazaa matokeo ya aina yoyote ile ambayo CCM haiyataki. Hilo halitawezekana

KUSUSIA KUNA MAANA GANI
Kwamba, CCM watakuwa wameandika katiba yao, na wananchi waanze sasa kudai katiba ya nchi.

CCM wakilazimisha goli la mkono, hiyo haitaondoa uhalali wa madai ya wananchi na itakuwa ni chachu ya kudai mageuzi si ya katiba bali nchi kwa ujumla

Wananchi wanachotakiwa, kwanza kuwaadhibu wabunge wa CCM walioshiriki uhuni ule.

Wawaambie bila kificho kuwa hawahitaji tena na wala hawatarudi Dodoma. Wasiwasikilize kabisa
Wabunge wa CCM waende CCM kutumikia katiba yao ya kihuni.

Pili, wananchi waanze madai ya katiba sasa hivi, na wapuuze kabisa kura ya maoni.
Wajiandikishe lakini wasishiriki kura ya maoni

Tatu, wananchi wafanye maamuzi magumu ya kukomesha kiburi, dharau, kejeli ya CCM na viongozi wao.

Nne, wapinzani wameshapata agenda. Kwanza, kudai katiba mpya inayoliliwa na wananchi.
Halafu kuonyesha upuuzi na ubabe wa CCM. Kwamba, wezi walioibia wananchi ndio waliojiandikia katiba yao na kupuuza maoni ya wananchi. Katiba iliyoandikwa na wenye milioni za mboga na vijisenti haifa, haikubaliki wala kujadilika

Tano, wapinzani wawaambie wananchi, miaka 50 inatosha kudhalilishwa.

Ni kutokana na kiburi cha CCM siku hizi wanasema bila hata hofu.
Milioni 10 pesa za mchicha na sukuma wiki, bilioni 2 vijisenti vya unga, wananchi wanachoweza ni kuuza nyanya n.k.

CCM wanafanya ubabe kwasababu wanaelewa udhaifu wa Watanzania.
Kwamba, watawatupia mzoga kisha kuwaamuru wale watake wasitake.

Ndilo hili la katiba. Bila kuanza kuonyesha kuchoshwa na uhuni, kila siku wataiba pesa, bili watalipa wananchi.

Kisha wanasema ni pesa za kununua dagaa, furu, nguruka, vitoga na migebuka.

Kususia katiba ndilo jibu, kinyume chake wananchi watakuwa wametoa uhalali wa haramu.

Kuhusu suala la Pengo, nitakujibu na Candid scope kwa pamoja

ingekuwa vyema sana kama kuna viongozi wa upinzani na wale wafuasi wao wakalipitia bandiko hili na kulisoma kwa umakin kisha kwenda kulifanyia kazi.

ingekuwa wapinzania wetu nao sio watu wa kuwa bribed basi hili lingekuwa ni msingi wa wao kuiondoa hii serikali ya CCM madarakani.

shida inakuja pale ambapo hata hao wapinzani tunaambiwa ni mamluki kama sio vibaraka wa chama tawala. nachelea kusema kwamba wapinzani wetu bado sio imara sana wanaweza kununulika kirahisi sana kama ambavyo hata viongozi wa dini wengine wanavyonunulika kwasasa.

tukitaka tanzania huru yenye uwezo stahiki hatuna budi kuipa poo serikali ya CCM hata kwa miaka mi5 tu ili sasa tuanze kuijenga hii nchi upya. jana nilikuwa nawaza sana hivi JK anavyoondoka madarakan atakuwa ameacha ufa mkubwa kiasi gani? na je anayeachiwa kijiti ataikuta nchi na hali gani hasa kisiasa, kiuchumi na kijamii?

Leo hii kisiasa hatuko stable kabisa, katiba tunaburuzwa tuu, rushwa ndio iko juu ubabe ndo usiseme, hakuna mwenye uchungu na nchi kama nchi na kila mmoja amesha kamata chake mapema. hawa ndio viongozi ambao wanatoka madadrakan tayari wana mijengo ya maana US na Dubai, hawa ndio wenye kumiliki ardhi kubwa ukilinganisha na wanachi wotee, hawa ndio wanaomiliki uchumi wa nchi kwa sasa hivi kweli tuliwaweka wajineemeshe ama watuongoze?

leo hii ukitazama mauaji ya albino na vikongwe ndo hayo, achilia mbali watu kuuana kisa mapenzi, visasi, ukiwa kinyume na serikali ni shiidah manake kufa kuko mkononi sasa je tuko kwenye Tanzania ile ile ama nyingine?

nafkiri umefika wakati wa wananchi kutambua aina ya unyanyasaji na ubabe wa CCM na pia watambue kwamba ukombozi hauwez kuja ila isipokuwa kwa mapinduzi ya kweli. Mapinduzi ya kweli kwasasa ni kuipindua CCm na uozo wake wote bila huruma.

Hebu mwaka huu tujaribu tuone mbona inawezekana?
 
NENO LIMETIMIA

TULISEMA MCHAKATO UTATOA MATOKEO SIFURI

CCM WAOGOPA NGUVU YA UMMA

SAMWEL SITTA, LUBUVA YAKO WAPI

Sehemu ya I

Tume ya uchaguzi imeahirisha kura ya maoni ya katiba ya Chenge.

Katika mabandiko yetu hapa duru tumewahi kueleza mambo kadhaa

1. Kwamba, bunge la katiba lingevunjika wiki mbili baada ya kuanza
2. Tulieleza katiba haitengenezwi na wanasiasa bali wananchi
3. Tukashauri maridhiano yapatikane kwanza, hakuna mahali dola iliwahi kushinda nguvu ya umma
4. Tukaeleza wazi, umma haukubaliani na mchakato na umesusia

Yote yametokea. Hayakuwa utabiri wala hayakuhitaji akili, ni suala la kutazama ukweli na kuufuata

Wazee wa serikali na Chama wakadhani nchi imesimama kama walivyoikuta, leo tunawauliza yako wapi?

Tulishauri kuanzia wakati wa kutunga sheria, katiba haiandikwi na kundi la wanasiasa na wala si mali ya wanasiasa

Katiba huandikwa kwa maridhiano yanatokana na wananchi

Na kwamba ushirikishwaji wa wananchi ni muhimu kuliko jambo jingine

CCM wakatumia ubabe kupitisha sheria za mchakato.

Wakatumia demokrasia ya wingi wao bila kujua hatari iliyopo mbele

Ni vema kusema, mchakato mzima haukuwa na plan, hakufanyiwa tathmini na wala kutekelezwa kiufundi na kiuadilifu

Zaidi ya hayo, mchakato uliongozwa na ubabe, dharau na katiba kama mali ya mtu na si watu

Plani mbovu: Katiba ni dai la wananchi, wazo la mchakato likatolewa na mtu mmoja
Kimantiki tu, hapo kuna tatizoKwamba hakuna ushirikishaji wa wananchi, hakuna mipango n.k.

Hakukuwepo kukaa mezani kama wananchi na kupanga nini tunataka, kwa wakati gani na kwa njia zipi

Tathmini: Hakukuwa na tahmini ya zoezi zima kujua vikwazo na urahisi wa zoezi zima
Kilichotakiwa kuangliwa ni rasilimali'resource' muda wa zoezi, na njia za kukabiliana na matatizo katika safari

Matokeo yake, mipango ya zima moto kama aibu ya kwenda kuazima BVR ikajitokeza.
Hayo ni matokeo ya kutokuwa na tathmini ya jambo husika

Utekelezaji: Kwamba, viongozi walidhani utekelezaji wa zoezi ni kutoa pesa hazina, kuhonga watu na propaganda.

Ili kutekeleza zoezi kwa ufanisi ni lazima iwepo plan nzuri, tathmini, ushirikishaji wa watu n.k. hayakufanyika kwa kujua kuwa polisi na vitisho vilitosha kufikia azma yao mbaya

Ubabe: Tumeona akina Samwel Sitta wakibadilisha kanuni kama ile ya Rais kuja kujibu hotuba ya Warioba na si kuzindua bunge. Tuemoana Rais ''akiwashauri'' wenzake wafute vifungu vya rasimu kwa kutumia 'wingi wao'

Dharau: Tume ya Warioba ikadhalilishwa , wananchi wakadharauliwa maoni yao na sheria zikipindwa kulia na kushoto

Katiba mali ya kundi: Likabaki kundi la CCM, wakaandika katiba-Chenge wakitaka iwe ya umma bila umma kushiriki

Zoezi limeshindikana si kwasababu ni gumu, ni kwasababu tu ya kuwa na viongozi wasio na maono, wasiosikiliza wananchi, wanaodhani Tanzania ya 1960 ni ilele na waliolewa bwimbi la madaraka.

Ni viongozi wabinafsi na walafi ambao kwao posho zilikuwa muhimu kuliko taifa

Hakuna mtu mwenye akili timamu ambaye hukujua kuwa tangu Sitta achukue kiti ilikuwa dhahiri bunge limevunjika

Hakuna asiye na akili timamu aliyeshindwa kuona, hotuba ya Rais wakati wa kufungua bunge ilishaua mchakato mzima

Kuanzia hapo, ilitosha kuokoa pesa za wananchi kwa kusitisha shughuli nzima

Inaendelea..

Ingawa rais alitaka katiba iwe 'legacy yake' kuvunjika na kushindwa kwa mchakato ni donda litakaloumiza historia ya utawala wake kwa muda mrefu sana. Hili ni moja kati ya mambo aliyoshindwa, na si kushindwa tu bali kwa upana wake wa kushindwa kuliongoza taifa wakati wa majaribu

Inaendelea
 
Sehemu ya II

WAHANGA WA KUVUNJIKA KWA ZOEZI LA KATIBA

Kuvunjika kwa zoezi la kupata katiba mpya, kumetokea kukiwa na majeruhi wakubwa

Pamoja na ukweli kuwa mchakato haukuanza kwa kufuata taratibu za wananchi kuumiliki, kupanga na kuamua nini wanataka kupitia mkutano wa kitaifa, bado zoezi la rasimu ya Warioba lilikuwa katika mstari

Laiti tume ya Warioba isingaliingiliwa na kuvurugwa, uwezekano wa kupata katiba licha ya mapungufu ulikuwepo

Kwa bahatibaya, viongozi waliopaswa kusimamia mchakato mzima ndio hasa chanzo cha kuvunjika kwa zoezi

SERIKALI: Kazi ya serikali ni jenga mazingira salama, imara na yenye hekima ili mchakato uendelee kama ulivyopkuwa unakwenda. Tuliona msisimko wa Rasimu ya I na II ikiashiria wananchi kukubaliana na mchakato na kusahau mapungufu yaliyojitokeza kwa ujumla

Tulishangaa kuona mawaziri wakiwasilisha miswaada ya serikali katika kujenga mazingira ya kufanikisha ubabe kwa kutumia wingi
Hilo walifanikiwa kupitia akina Waziri Wasira, Lukuvi na wengineo.

Tukaona Rais akitumia sheria zilizopitishwa kilaghai kuidnisha mambo yenye migogoro.

Rais akizungumza na wapinzani neno moja na kesho kubadili msimamo.
Mfano, mzuri ni uteuzi wa wajumbe wa BMLK uliojaza makada wa chama ili kupata wingi na si ubora

BUNGE LA KATIBA

Mh Sitta, akaliendesha bunge la katiba kibabe, akishinikiza kubadili kanuni. Hakutaka maridhiano hadi mwisho.
Tulishuhudia akiiba kura, akiidhinisha kura za maruhani na zingine za face book ili tu kutimiza azma iliyoanishwa serikali

WAJUMBE
Tukawaona wajumbe waliojifungia na kuandika katiba yao. Hawa waliongozwa na Chenge na Asha Rose
Tuliwasikia wajumbe wakichangia katiba mpya kwa njia za matusi na kejeli na hata kujua uwezo wao wa kufikiri

Waziri mkuu, kama kiongozi ndani ya bunge na serikali, alishindwa kusimama katika ukweli.
Kauli zake siku zote zilikosa vionjo vya uongozi 'leadership''

TUME YA UCHAGUZI
Ilishangaza kuwa tume yenye mamlaka na inayoitwa huru, ilinyang'anywa mamlaka na serikali.
Rais akawa ana ratibu shughuli ambazo ni jukumu la tume.

Tume ikaamriwa ifanye kazi hata kama ilijua haiwezekani. Mzee Jaji Lubuva akachukua jukumu akijua wazi haiwezekani

Katika makundi hayo ya juu, wapo watakoathirika na zoezi lililoshindwa

Rais ataondoka madarakani akiwa na sifa ya kushindwa kuliongoza taifa kuandika mwongozo wake
Zaid ya hapo hana cha kupoteza

Waziri Wasira: Kwa kutumia nguvu nyingi na ubabe, kushindwa kwa zoezi kunahitimisha ndoto zake za Urais
Akiwa msaidizi na mshauri wa Rais, Wasira ameshiriki kuliongoza taifa kushindwa!

Samwel Sitta : Kwa mara nyingine , ameshindwa kusimama jambo hadi mwisho kama ilivyokuwa katika kashfa za Richmond na madudu mengine akiwa Spika. BML limetoa sura halisi ya Sitta, kama mbabe na si kiongozi, hilo imehitimisha safari ya magogoni

Waziri mkuu, huyu anaathirika kwa kushindwa kuongoza au kusihauri serikali.
Ameshindwa kuwaunganisha wabunge, na makundi ya jamii katika kutafuta muafaka.
Naye kama walivyo wenzake, ametia doa kubwa safari ya kwenda Ikulu

Waziri Lukuvi: Hana cha kupoteza

Waziri Asha Rose : Huyu ni mmoja wa wana Mama wanaotajwa sana katika kinyang'anyiro.

Pamoja na kuujua ukweli, AshaRose alilazimika kuzungumza, kugawa katiba n.k. jambo linalomweka katika wakati mgumu.

Asha Rose anaonekana kiongozi asiye na msimamo, anayesubiri kuambiwa.Heshima aliyokuwa nayo imengia dosari kubwa

Akiwa kama naibu katibu mkuu wa UN, Asha Rose alitakiwa awe kiungo muhimu na mtu mwenye maono zaidi ya uono wa CCM. Hakutumia nafasi hiyo vema, kosa la kisiasa!

JAJI LUBUVA
Hana cha kupoteza zaidi ya heshima tu. Naye kama Sitta, ni watu waliotumika vibaya.
Leo amekabidhiwa jukumu la kuahirisha mchakato. Huko nyuma majukumu yalipo onekana mazuri waliyafanya wenyewe

WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA WA CCM

Hapo lipo tatizo kwa idadi kubwa ya watu hasa waliokuwa mstari wa mbele wa katiba ya Chenge
Kundi kubwa litaathirika kwa kushindwa kwa mchakato

Lipo kundi la Tanganyika na la Zanzibar kiliongozwa na Vuai Shamsa.

Inaendelea ....
 
inaendelea

Spika Makinda: Hana cha kupoteza. Tatizo lake ni udhaifu wakusimama kama kama mfano wanawake.
Makinda anatueleza jinsia haijaweza kuwakigezo cha uongozi

Watakaosema ni zamu ya wanawake, swali litafuta, kama Makinda? Na kwasababu zipi?
Lipi la maana Makinda kama mwanamke amekuwa tofauti na watangulizi wake?

Job Ndugai: Kuna nyakati anasimama mwenyewe, kutokubalianana chama . Suala la Escrow ,pengine ana masilahi yasiyojulikana ndio maana alitaka uwazi.
Aliondolewa kwa muda bungeni
kuachia mijadala iliyoichoma serikali

Ndugai anakabiliwa na haya

1 CCM ikamtafutia ‘mbadala' jimboni, escrow ndio wenye maamuzi katika vikao hivyo.
2.Kujisalimisha CCM,itabidi afanye jambo kuwafurahisha. Uwezekano wa kuharibu kabisa pande mbili alizo nazo ni mkubwa
3. Hana mahusiano mazurina upinzani wala chama chake. Ndugai ni mmoja wa washabiki wa mchakato ulioshindwa.

Uwezekano wa kurudi bungeni ni mdogo. Ndugai haeleweki anasimamia wapi katika mambo ya kitaifa.
Ndani ya chama chake, anasubiriwa kwambele

Prof Mwandosya: Aliyejijengea heshima muda mrefu. Uzoefu na usomi vilimpa nafasi kubwa.
Kitendo cha kumkashifu mzee Warioba, na matokeo ya kiushindwakwa zoezi kuna tia shaka na uwezo wake wa kutawala.

Akiwa mtarajiwa, hili limemuondolea sehemu ya sifa ya uongozi.
Kauli zake ndani ya BMLK zinaeleza umma ni mtu wa aina gani. Amejiondolea sifa ya ''usomi''

Lowassa: Hakusema lolote kuhusiana na katiba, alitambua maoni ya wananchi na hakuwa tayari kusema dhidi ya CCM ili asitoneshe vidonda.

Alichofanya Lowassa ni kutochukua upande ili asiudhi eneo lolote.
Lowassa hakukemea uhuni , alishiriki kuhalalisha wizi na ulaghai alioufahamu, alishiriki vikao na kamati za jambo ovu, kama alivyoshiriki kuficha Richmond

Hakuna namna Lowassa anaweza kusimama na kuetetea hoja ya utaifa.
Yeye ni sehemu ya uovu tena akiwa na makovu makubwa

Tofauti ya Lowassa, Sitta, Mwandosya haionekani. Kujificha kunaeleza jambo moja, ni mtu asiye na msimamo au anayefanya mambo nyuma yapazia a.k.a mdanganyifu

Lowassa hakuonyesha uchapakazi unaosemwa. Tangu afukuzweuwaziri mkuu, hatumjasikia akiongea kama kiongozi. Haeleweki anasimama wapi kwa mambo kama katiba.

Haeleweki anasimama wapi kwa masuala ya bungeni nay a kitaifa.Swali watakalopamba nalo wapambe wake ni hili, katika miaka 6 elezeni uchapakazi wa Lowassa katika mambo ya kitaifa!

inaendelea...
 
VIJANA

Kundi lina akina Shamsa Vuai, January, Mwigulu, Kigwangalla,Ngeleja.Ilitegemewa suala la katiba liwe agenda ya kitaifa

Kwa uwezo wao,weledi na exposure, vijana wangetoa mtazamo tofauti
wakiangalia taifa, kulileta pamoja,kutafuta maridhiano na muafaka

Vijana hao watarajiwa wa Urais,hawakuonyesha uongozi. Nchemba alisikitikia upotevu wa mapesa akijua mchakato hautakamilika na wala hauna maridhiano. Ndani ya BMLK Nchemba alikuwa kiungo kizuri katika kamati

January alisimama kutetea S2 kwa hoja nyepesi. Ilikuwa wazi,hakuangalia maoni ya wananchi, alitaka kuwafurahisha CCM kama mtetezi wa sera za Mwalimu. Naye alikuwa kiungo kizuri katika kuandaa katiba ya Chenge

Ngeleja na Kigwangalla, nao pia kama wenzao, walikuwa viungo kizuri cha katiba ya Chenge

Shamsa Vuai: Kama mtu anayeangaliwa visiwani kugombea Urais,alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha hujuma zinafanyika katika BMLK ilikuwaridhisha CCM.

Hakuangalia masilahi mapana ya eneo analotaka na aina yasiasa zake. Hili la BMLK litamtafuna muda mrefu

Tatizo la vijana si misimamo yao, ni jinsi wasivyoweza kusimama wenyewe, wameonyesha udhaifu wa kujificha hata kuogopa kusema uovu.

Hesabu zilionyesha BMLK halitatoa majibu sahihi. Vijana wakakubali wizi, ulaghai, udanganyifu uliofanywa na akina Sitta tena wakiungana na Chenge kuandika nyaraka waliyojua si halali na imejaa uovu.

Walijua tume haiwezi kukamiisha zoezi na mchakato mzima ulishavurugwa.
Hawakusimama kutetea umma, walijificha nyuma ya CCM.

Hawa vijana wanawezaje kusimama na kutuambia, watakemea rushwa, hawapendi ufisadi, wanachukizwa na umasikini,wana maono n.k. ikiwa wao walishiriki yote hayo kwa vitendo?

Kwa fikra, mchato ulivurugwa na umefeli, nini tofauti yamitazamo ya Lusinde Kibajaji,Nchemba, Asumpta msham,Lowassa, Wasira, JanuaryMakamba, marehem Komba,Mwandosya, Ngeleja, Mrema n.k
 
WAHANGA

Inaendelea..

Waziri mkuu
Kiongozi wa serikali bungeni hakuonyesha ‘leadership'' miswada yote ya kubadili sharia ili kukidhi haja ya kushinikiza katiba waliyotaka wao. Wazri mkuu ahibiiha udhaifu mkubwa sana katika kupanga, kusimamia na utekelezaji

WAPINZANI

Wapinzani walionyesha udhaifu mkubwa wakati wa majadiliano

Hawakuwa tayari kuzungumza walichojadiliana katika vikao vya usuluhishi.
Waliamini maneno bila
maandishi hilo lilitoa nafasi ya Rais kuwageuka kila mara.

Matokeo ya kuahirishwa kwa mchakato yamewapa wapinzani nguvu kisiasa ya kisiasa

Kwanza, wananchi wanapata Imani kuwa wapinzani waliona mbali, wangesikilizwa taifa lisingeingia hasara

Pili,madai kuwa hakukuwa na maandalizi wala ushirikishwaji wa wananchi yamepta nguvu kuliko siku za nyuma

Tatu, Wananchi wanazidi kuuelewa upinzani ni jambo jema tofauti na vurugu

Nne, kususia BMLK kiuna maana,hawakushiriki tendo lisilo na maridhiano na kulitia taifa hasara iliyotokea

CCM

Hili ni tukio la kwanza lililowazi chama tawala na serikali yake vimeshindwa kulisimamia.

Ni dalili, nguvu ya ‘ziada' haikubaliki, mbinu za udanganyifu zimekwisha,CCM inakabaliana na nguvu ya umma

Matokeo ya chaguzi za serikali za mitaa ni kiashirio kwamba hamkani si shwari.

Baada ya matokeo, ulikuwa muda muafaka wa kufikiria hali ya mchakato. CCM hawakufanya hivyo!
Hili la katiba ni msumari wa moto juu ya kidonda

CCM ilijaribu kujiweka pembeni na mchakato . Hatukusikia viongozi wakipigia debe.

Hilo walifanya katika jitihada za kuinasua CCM na mchakato ulioonkena kufeli baada ya kuvurugwa BMLK

CCM walijiweka mbali ili kuepuka matatizo ya ndani. Wahafidhina walitaka katiba ya Chenge kwa udi na uvumba

Lipo kundi lililoona walakini,haikuwa sahihi kwa hatua zilizofikiwa.

Kundi la wahafidhina lina nguvu ndani ya chama na ndilo lilishinikiza kila mbinu kura ya maoni iendelee

Kwa namna yoyote, kushindwa kwa mchakato kuanzia BMLK ni zao la ubabe na uhuni wa CCM.

Wawakilishi wa CCM ndani ya BMLK hawawezi kujitenga na lawama au hasara zilizotokea, wala haiwezi kujitoa ili hali viongozi wa serikali ndio wa CCM.

Adhabu yoyote itakayotokana na hasira za wananchi itawashukia CCM bila kujali nani alishiriki nani alikuwa pembeni ingawa ‘wahanga' wataathirika Zaidi na hasa wabunge wao

CCM NA MAPIGO MAWILI

Uchaguzi wa serikali za mitaa ulipeleka ujumbe kwa CCM, hali ya kisiasa si nzuri kwa upande wao.
Kushindwa kwa katiba ni pigo jingine linalodhihirisha ubutu unaoikabili CCM

MBINU ZA KUJANASUA
Matokeo ya serikali za mitaa yalipeleka ubaridi mtaa wa Lumumba.

Ni dhahiri wananchi wamechoshwa na ubabaishaji, uhuni na ubabe wa chama tawala.
CCM wakaanda mbinu za kutoka katika sakata la katiba kisutaarabu

Mbinu za CCM, Inaendelea
 
MBINUZA CCM

Haikuwa muafaka kuacha mchakato UKAWA walipojitoa. Hilo lingewapa nguvu wapinzani kwa mtazamo wa CCM.

Wahafidhina waliamini matumizi ya vyombo vya dola yangeleta ‘mafanikio'

Tulishuhudia uhuni wa kura za maruhani,facebook, wajumbe wasiojulikana kupiga kura, wapinzani kupiga kura wakiwa hawamo bungeni, akina Zakhia Meghji kubadilishwa ukaazi n.k.

Hizo zote zilikuwa jitihada za kuokoa mchakato ili kutimiza matakwa ya wahafidhina na kuiepusha CCM na aibu

Baada ya kukamilika uhuni, haikuhitaji cheti au degree kubaini wananchi walisusia kila hatua iliyofuata

Katiba ya Chenge licha ya kutengewa mabilioni ilionekana kama hadithi za Abunuwasi.

CCM walitambua wananchi hawataki, walishasoma mazingira ya chaguzi zamitaa, walitafuta mahali pa kutokea.

Maji yalishakuwa ya shingoni!

TUME YA UCHAGUZI YATUMIKA

Tume ya uchaguzi ikapewa kazi bila nyenzo za kukamilisha zoezi. Bila elimu ya hesabu ni wazi zoezi liliandaliwaili lishindwe

WAPINZANI WAFANIKIWA , ‘WAIKOA CCM KIAINA'

Shinikizo la wapinzani Bungeni majuzi kutaka kupewa msimamo wa uandikishaji daftari la wapiga kura ulikuwa na lengo moja,kuilzimisha serikali kukubali zoezi limefeli.

Ulikuwa ni mkakati mzuri sana kwa upande wa upinzani.

Kitendo cha kugomea bunge lisiendelee hadi msimamo upatikane ni jambo sahihi kwa wakati sahihi na msimamo sahihi.

Kwa upande mwingine, shinikizo hilo limeisaidia CCM na serikali mahali pa kutokea.

Ilimlazimu mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kutoka hadharani na kukiri zoezi limeshindwa.

Mwenyekiti wa tume alilazimika kutoa kauli hata kama tunajua, siku za nyuma Rais ndiye aliyeratibu kura ya maoni

Ugumu ulitokea kwa serikali kutokana na ukweli kuwa muda mrefu Rais na waziri mkuu, na mawaziri wa utawala bora na sheria wamesisitiza kura ipo na zoezi litafanikiwa

Tunakumbuka Rais aliagiza hazina itoe pesa ili kukamilisha kazi.

Katika mazingira hayo ya kukomalia kura ya maoni, ni vipi Rais au waziri mkuu angesimama na kusema wamefeli?

Ndipo akatupiwa mzigo mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, mzigo unaoathiri taswira na heshima yake kwa muda mrefu

HOTUBA YA MWEZI

Kutokana na ugumu wa zoezi na jinsi gani serikali inaweza kueleza hasara iliyotokana na maamuzi hovyo, viongozi wanakwepa kuongelea suala hilo.

Ni kawaida Rais hutoa hotuba ya mwisho wa mwezi
Kwa mwezi huu ulioambatana na sherehe ya pasaka, haikutarajiwa hotuba ikosekane.

Tumeshuhudia hotuba zikirekodiwa hata anapokuwa safarini, vipi mwezi huu?

Haingewezekana Rais aliyesema kura ya maoni inawezekana, wiki moja baadaye arudi kwenye umma na kuuambia haiwezekani! Mzigo akakabidhiwa Jaji!

...Haingewezekana Rais aliyesema kura ya maoni inawezekana, wiki moja baadaye arudi kwenye umma na kuuambia haiwezekani! Mzigo akakabidhiwa Jaji!
Mzigo akakabidhiwa Jaji na Jaji akakubali kuubeba! Hapo ndipo lilipo chimbuko la matatizo ya nchi hii...tuna uhaba wa watu wenye weledi, maadili na ujasiri wa kuita koleo koleo. Badala yake tunao kibao watu kama Jaji Lubuva...wanafiki, wachumia tumbo na waoga wanaoongozwa na ulafi wao!

Jaji alipata nafasi nzuri sana ya kuchukua maamuzi ya kijasiri, kizalendo na kishujaa kwa kusema, hapana, kazi imenishinda...nabwaga manyanga. Tupo ambao tungemwelewa na kumsamehe lakini hapa katanguliza maslahi yake binafsi badala ya taifa ingawa tupo ambao tungesimama kumtetea.

Ni hapa namsifia japo Jaji Warioba, alionesha msimamo na akawa tayari kuutetea bila kujali matusi, kejeli na vurugu kutoka kwa wahuni kama Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni! Jaji Warioba alisimama kidete kutetea aliyoamini ni maslahi, maoni na matakwa ya wananchi bila kujali msimamo wa chama chake.
 
Back
Top Bottom