Duru: ' Utata wa Utatu', Katiba, Muungano na Kura ya Maoni

Duru: ' Utata wa Utatu', Katiba, Muungano na Kura ya Maoni

XX

PESA ZA MFUKO WA JIMBO KUTOKA BUNGE LA JMT KWENDA ZANZIBAR

Tukirejea bandiko I , II na III tumeona Bunge na idadi ya Wabunge ambao ni 393 akiwemo AG

Kwa upande wa Zanzibar yapo majimbo 50 ya Wabunge wa kuchaguliwa, Wabunge 5 wa Baraza la Wawakilishi, na Wabunge wa Kuteuliwa, na mwisho Wauteuliwa na Rais Kwa muktadha idadi ya Wabunge wa Zanzibar si chini ya 80.

Rejea gazeti la Serikali la Jan 5 2023.

Kwa mujibu wa Katiba ya JMT kama tulivyoonyesha, kuna mambo ya Muungano yanahitaji 2/3 ya kila upande.

Kwa minajili ya mjala ikiwa Wabunge wa Zanzibar ni 80, takribani inahitajika Wabunge 53 kupitisha jambo.

Pili, Wabunge wa Zanzibar wana KURA yenye nguvu sawa na Wabunge wengine wa Bunge la JMT.

Wabunge wa Zanzibar wana KURA kwa yasiyo ya Muungano kama Elimu, Afya, Utalii, Madini, Ujenzi, Uchukuzi, Mifugo, Kilimo , Ardhi n.k. wakiwa ndani ya Bunge. Haya ni mambo ya Tanganyika.

Mfano, Mswada unaohusu ARDHI unaweza kupita au kupingwa na kura za Wazanzibar.
Wazanzibar wana turufu ya kuamua mambo ya Tanganyika,yale yale wanayolalamika yasiwe ya Muungano.

Tuna suala la Bandari, Wabunge wa Zanzibar wamesema HALIWAHUSU lakini walipiga kura kuhusu suala hilo hilo.

Ikitokea Wabunge wa Zanzibar wana interest ya suala lisilo na masilahi na Tanganyika lakini lina masilahi yao, kura zao zinzaweza kuamua mustakabali wa Tanganyika.

Ukiacha nguvu ya TURUFU ya kura yao , kuna nguvu nyingine waliyo nayo.

Wabunge wa Zanzibar wanachaguliwa na idadi ndogo sana ya Wapiga kura.

Kwa mujibu wa Gazeti la Serikali la Jan 5, 2023 tutaonyesha idadi ya kura za Washindi tu katika kujenga hoja.
Hapa ni mifano michache

Mkoa wa kusini Pemba ( Zanzibar) - Mshindi alipata kura 4, 136.
Jimbo la Kawe Dar (Tanganyika )- Mshindi alipata kura 194, 833

Jimbo la Uchaguzi Konde (Zanzibar) - Mshindi alipata kura 1,552
Jimbo la Tanga mjini ( Tanganyika ) -Mshindi alipata kura 114,445

Mifano hiyo halisi ina maana .
Kwanza, Ikiwa kila Jimbo la Zanzibar litapewa wapiga kura 10,000 (idadi ya juu sana) itahitaji Wabunge 19 ili kupata idadi sawa ya wapiga kura wa Jimbo la KAWE.

Itahitajika Wabunge 11 kutoka Zanzibar ili idadi iwe sawa na iliyomchagua Mbunge wa TANGA MJINI.

Wabunge wa Zanzibar wanaochaguliwa na watu 1,500 kama yule wa KONDE wana haki ya kuzuia Bajeti ya Afya, Ardhi, Madini au Mifugo ya Tanganyika kinyume na Matakwa ya Wabunge wa Kawe na Tanga.

Wabunge wa Zanzibar wanapata pesa za Mfuko wa Jimbo sawa na Wabunge wengine wa Tanganyika.
Tunasisitiza Tanganyika kwasababu hakuna Mbunge aliyechaguliwa na Watu chini ya 20,000

Lakini pia pesa za Mfuko wa Jimbo zinatoka Mfuko wa Hazina Kuu Dar es Salaam ambao unakusanya fedha za Tanganyika peke yake na kuzifanya za Muungano.

Rais Mwinyi katoa ushuhuda kwamba Zanzibar haichangii chochote na kodi zote zinabaki huko.

Mfuko wa Jimbo la Kawe la walipa kodi 194,833 ni sawa na Mfuko wa Jimbo la Kusini pemba la watu 4,136( wasiolipa kodi Hazina Kuu Dar es Salaa) Kwa mujibu wa Rais Mwinyi ( Gazeti la Mwananchi December 11,2022).

Mfuko wa Jimbo la Mbunge wa Tanga Mjini aliyechaguliwa na walipa kodi 114,445 ni sawa na Mbunge wa Konde aliyechaguliwa na watu 1,552 (wasiolipa kodi Mfuko Mkuu wa Hazina Dar es Salaam) .

Wabunge wa Zanzibar wanapaswa kulipiwa gharama na SMZ kwasababu wanakuja kwa ajili ya Zanzibar, kinyume chake wanazawadiwa pesa kutoka Hazina Kuu Dar es Salaam kwenda kwenye majimbo ya Zanzibar.

Kama Zanzibar hawana Mchango Hazina Kuu Dar es Salaam kwa mujibu wa Rais Hussein Mwinyi na aliyekuwa gavana wa BoT Ndulu, kwanini kodi za Wapiga kura wa Kawe na Tanga mjini ziende majimbo Zanzibar?

Itaendelea
 
XX1

ACT Wazalendo WATHIBITISHA ALICHOSEMA RAIS H.MWINYI NA MARHUM GAV WA BoT
MAKAMO WA RAIS WA ZANZIBAR ''OMO'' ASEMA UKWELI MCHUNGU BILA KUTARAJIA.


View: https://www.youtube.com/watch?v=rSYpfltnuTI

Kwa miaka mingi kuna upotoshaji au elimu duni ya kuamini Tanganyika inainyonya Zanzibar kiuchumi
Kumekuwa na dhana mbovu kwamba Zanzibar inanyimwa misaada na kwamba inapaswa kupata 50/50

Kumekuwa na dhana ya kipuuzi ikienezwa na Viongozi wa chama cha ACT Wazalendo kwamba Tanganyika haitaki uwepo wa Tume ya pamoja ya Fedha ili kuendelea kuinyonya Zanzibar ambayo ni tajiri kiuchumi.

Dhana hizi ni matokeo ya hadithi za vijiweni au maskani watu wakipata kahawa ambazo baadhi ya watu wameizamini. Mzee mmoja alisikika mitandaoni akilalamikia misaada na kudai SSH sasa ameweka 1/3 kwa Zanzibar. Tulijiuliza ikiwa mtu huyu ni msomi akiwa nje ya nchi uelewa wake upo hivyo, vipi watu wa kawaida kule maskani !!

Kwamba anaamini nchi inaendelea kwa misaada na kwamba Zanzibar inapunjwa.
Mzee huyo hakijiuliza '' subsidy'' ya Bajeti ya SMZ inatoka wapi. 4.5% ya Pato la Tanganyika kwa Zanzibar ni kiasi gani. Na kwamba wapi Bajeti ya Ulinzi , mambo ya ndani na ya nje na mengine mengi ambayo Zanzibar haina bajeti zake.

Hili ikakumbusha kauli ya kiongozi wa ACT akidai Tanganyika haitaki Tume ya pamoja ya Fedha ili kuinyonya Zanzibar. Huyu ni kiongozi aliyewahi kushika madaraka makubwa katika SMZ.

Kiongozi huyu angejiuliza tu swali rahisi Bajeti ya Zanzibar ni kiasi gani ukilinganisha na Wizara kama ya Ulinzi

Rais H.Mwinyi kamaliza uongo wa ACT akisema 'wasiotaka Tume ni Zanzibar' kwasababu itabidi fedha ziingie akaunti ya pamoja kisha zigawanywe katika matumizi halafu zinazobaki ziende kwa washirika.

Ikiwa Bajeti ya Ulinzi ni 2.7 Trilioni na Bajeti ya Wizara ya Mambo ya ndani ni 1.2 T jumla ni 3.9 T.
Zanzibar ikipewa kulipa 10% ya Wizara mbili tu italipa 390 B. Zanzibar makusanyo kwa mwezi hayazidi Bilioni 120 B.

Ikiwa kila jambo la Muungano watapewa 10% bado Zanzibar hawatamudu.

Nani asiye na akili anayeweza kwenda kunyonya Zanzibar?
Mtaji wa NMB ni 11 Trilion, CRDB ni 10 T. Makusanyo ya Kariakoo ni Zaidi ya SMZ, sasa mtu anapodai Tanganyika inanyonya Zanzibar inafikirisha. Nani anaweza kumkamua Ndama akitegemea maziwa, huo si ujinga ni wendawazim

Majuzi katika Mkutano Mkuu wa ACT Zanzibar, kiongozi wa ACT Mh Othman Masoud Othman alitokwa na maneno bila kutarajia. OMO aliunga mkono Kauli ya Rais H. Mwinyi na Gavana wa BoT marhum Ndulu kwamba Zanzibar haina mchango katika Muungano na inapewa.

Katika Link hapo juu Dakika 45 OMO anasema kuna watu wanasema 'Unaona tunayofanya' akimaanisha CCM Zanzibar wanasema miradi inaendelea na wanafanya hili na lile.

Makamo wa Rais OMO anasema hizo ni Pesa za kupewa kutoka BoT kwasababu makusanyo ya Zanzibar 60% inakwenda kulipa mishahara na 40% inatumika kununua Karatasi n.k.

Bw Masoud anamaanisha Bajeti haijitoshelezi tena akisema ulizeni kama watu wanapewa pesa za maendeleo.

Bwana Masoud anaendelea kusema pesa zinatokana na Mikopo, na kwamba Wananchi waulize ikiwa Zanzibar inaweza kulipa mikopo hiyo. OMO anamaanisha mishahara ni 60% na matumizi ya kawaida ni 40% wapi Zanzibar itapata fedha za kulipia mikopo? Kasema walizeni CCM na Serikali yao.

Kauli inashadidia hoja yetu siku kwamba Mikopo inayopewa Zanzibar anayelipa ni Tanganyika kwa jina la Tanzania.

Makamo wa Rais OMO ambaye pia ni Kiongozi wa ACT Wazalendo amethibitisha pasi na shaka kwamba Zanzibar inapata pesa kutoka BoT kuendesha Miradi tunayoiona, na kwamba kama kuna mikopo anayelipa si Zanzibar bali mdhamini Tanzania ambaye ni Tanganyika. Rais H.Mwinyi katibitisha Zanzibar haichangii kodi Hazina Dar.

Kwa maneno yake, Mh Makamo wa Rais amesema ukweli .
Hatujui kama ni bahati mbaya au la, lakini hasira zake siku zote huishia kutamka maneno bila mpangilio.

Kwa hili amewasaidia Watanganyika kujua fedha na kodi zinakwenda Zanzibar kule kule wanakoita Tanganyika ni Wakoloni, ni maafriti na Majahilia kwa kauli za kiongozi wa ACT Bwana Jussa.

Inaendelea
 
XXII

GHARAMA ZA WATUMISHI NA WABUNGE ZINABEBWA NA 'WATANGANYIKA'

Tumerejea mara nyingi ya kauli ya Rais Hussein AH Mwinyi aliyoitoa desemba 11 2022 kuhusu mambo mawili.

Kwamba kodi za TRA Zanzibar zinabaki huko, hivyo hakuna mchango wowote Hazina Kuu Dar es Salaam.
Pili, Zanzibar haitaki Tume ya pamoja ya Fedha kwasababu italazimika kuchangia huduma za Muungano.

Tunarejea maneno ya aliyekuwa Gavana wa BoT Bw Ndullu kwamba zaidi ya miaka 40 Zanzibar haina mchango katika Hazina Kuu ya JMT. Kauli ya Gavana Ndullu haijawahi kukanushwa au kurekebishwa na kiongozi mwingine.

Makamo wa Rais na Kiongozi wa ACT Bw Masoud Othman Masoud akisema Zanzibar inapewa fedha za BoT.
Mishahara ni 60% na matumizi ya kawaida ya shughuli za serikali ni 40%.
Kwamba pesa za maendeleo zinatoka BoT. Bw Masoud kasema Zanzibar haina uwezo wa kukopa kwasababu haiwezi kulipa akimaanisha mikopo ya Zanzibar inalipwa na Tanzania au Tanganyika.

Kauli hizo zina maana kubwa kwa Tanganyika. Kwamba, mzigo wa Muungano umebebwa na Tanganyika peke yake.

Watumishi wa serikali 21% mgao mahususi wa Zanzibar gharama ikiwemo mishahara na mafao ya kustaafu ni mzigo atakaoubeba Mtanganyika. Wabunge wanaowachagua kwa ajili yao wanalipwa mishahara na masilahi ikiwemo viinua mgongo kwa fedha za Watanganyika kutoka Hazina Kuu Dar es Salaam

Fedha za Hazina Kuu ni za Watanganyika kupitia rasilimali na kodi. Katika Muungano ambao Zanzibar imelalamika kuonewa inasikitisha Mabilioni ya fedha yakielekezwa sehemu isiyo na mchango wowote na kuziacha sehemu zinazochangia Muungano bila huduma Muhimu.

Zanzibar , tofauti na Mkoa mwingine wa Tanganyika ina serikali na mifumo ya kukusanya kodi.
Kupitia SMZ Wazanzibar wameondoa hata kile kinachoweza kuwa cha pamoja wanapoona kina manufaa kwao

Mfano, wameondoa gesi na mafuta kwa maana kwamba kama yapo Tanganyika itabaidi inunue kana nchi jirani
Wameondoa Bandari kwasababu tu ya kudhani mafao ya Bandari yatainufaisha zaidi bila kuishirikisha Tanganyika

Wafanyakazi 21% , makatibu wakuu wa Wizara za Muungano na zisizo, Wakurugenzi hadi wa Halmashauri, Wabunge , Majaji wa Mahakama ya Rufani , kwa pamoja wanalipwa mishahara, marupu rupu na ya uzeeni kutoka mapato ya Gesi ya Mtwara, Bandari, Dhahabu, Tanzanite, Maliasili , Mifugo , Uvuvi, Kilimo na kodi za Watanganyika.

Hoja ya Wazanzibar ya kutaka Muungano wa Haki na Usawa ( Fair and Equitable) ipo wapi?
Hoja ya Zanzibar kuhujumiwa na Tanganyika ipo wapi?

Katika mazingira ya Haki na Usawa wanaodai Wazanzibar, tunahitaji Katiba Mpya.
Katiba itakayowapa Watanganyika Haki na Fursa ya rasilimali kwa maendeleo kama inavyofanya Zanzibar sasa

Tunahitaji Katiba mpya ili kama muungano utakuwepo Zanzibar ishiriki na iwajibike kwa hali na mali.
Zanzibar ishiriki na isiwe mzigo ndani ya Muungano ikidai fursa na upendeleo na kuchangia ZERO katika ustawi

Mfano, hivi kwanini Wazanzibar wadai Tume ya Pamoja ya Fedha ili kujadili namna ya kugawana fedha za Tanganyika? Zanzibar inapopata fedha za Tanganyika kwa jina la Tanzania ni HISANI si HAKI

Si muhimu kuwa na Katiba mpya ya Muungano, Wazanzibar waulizwe ikiwa wanautaka Muungano.

Kama hawautaki hakuna 'MBAO'. Vipi upande Jahazi Bure halafu ukishuka udai mbao za mwenye jahazi

Inaendelea
 
XXIII

KERO ZIWE ZA WAZANZIBAR ZINAPOITWA ZA MUUNGANO
ZA TANGANYIKA NANI ANASHUGHULIKIA ?

Kwa hisani ya Gazeti la Mwananchi August 24,2021


View: https://youtu.be/CVEbJf2qol8

Katika mtandao wa JF kuna mada iliyoisema 'Watanganyika hawatamsahau Waziri Mchengerwa''
Inafikirisha na kujiuliza kwanini mada ilimhusu Waziri wa kawaida tena akitajwa kwa jina.
Methali ya kiswahili inanena '' asiye machoni na moyoni hayupo'' . Waziri alikuwa moyoni mwamleta mada.

Waziri Mchengerwa alitoa taarifa za kuipendeza Zanzibar kuhusu 21% ya ajira za Muungano kwa Wazanzibar.
Alitoa taarifa hiyo kwa majigambo na kujifaragua kama 'achievement kubwa''

Waziri hakueleza 21% katika watu milioni 1.5 inapatikana kwa hesabu gani dhidi ya 79% kwa watu milioni 60
Waziri hakueleza ajira hizo za Muungano zinalipiwa na nani na kwa utaratibu gani.

Waziri hakueleza kero ya Tanganyika kuhusu mchango wa Zanzibar unaohudumia Muungano ni asilimia ngapi.
Kwa maana kwamba ajira 21 % lazima ziwe na chanzo cha pesa ambacho ni Tanganyika na Zbar.

Hali hiyo imemkuta Makamo wa Rais (VP) Phillipo Mpango na itamwandama kwa miaka mingi ijayo.
VP Mpango ameeleza kuhusu kikao kilikuwa cha kushughulikia kero za Muungano.

Kwanza, Makamo wa Rais hakuwa sahihi kwasababu hakuna kitu kinachoitwa kero za Muungano.

Muungano ni matokeo ya nchi mbili Tanganyika na Zanzibar kwa uthibitisho wake dakika ya 13.20 aliposema ' focus za watu ziwe kwa masilahi ya Wazanzibar na Focus iwe kwa masilahi ya Tanzania Bara''

Kabla ya kueleza kwanini hakuna kero za Muungano, tukumbushe pakiwa na Tanzania Bara kuna Tanzania Visiwani pia, lakini Makamo wa Rais kwa hofu isiyojulikana akaitaja Zanzibar pekee.

VP anatambua kwamba Tanzania Bara imetajwa katika Katiba ya JMT 1977 kama iliyokuwa Tanganyika.
Ilikuwa sahihi kwa VP Mpango kusema 'Focus na moyo iwe kwa masilahi ya Tanganyika na Zanzibar''

Kuita Tanzania Bara ni siasa maji na zilizopitwa na wakati na kizazi hiki kinalazimika kucheka bila sababu !
VP kama Mbunge , Waziri na Mtumishi wa Kimataifa allipaswa kuelewa hakuna Tanzania bila Zanzibar

Rais wa Marekani Abraham Lincoln aliwahi kusema '' You can fool all of the people some of the time, and some of the people all time, but you cannot fool all the people all the time.

Pili, tukirejea kero za Muungano hakuna kitu kama hicho. Muungano upo bila kero ya aina yoyote.
Kilichopo ni kero za Zanzibar kwasababu kero za Tanganyika hazizungumzwi ni 'taboo' na ni jinai.

M/Kiti wa Chadema alipotahadhrisha suala la Bandari pale Dodoma akawa hoja badala ya Hoja aiyotoa.
Wakati huo huo ACT Wazalendo si kwamba wanatoa hoja bali wanaporomosha mitusi hakuna wa kuwakemea

Kero za Zanzibar si kero kwasababu kero ni kitu kinachoudhi !
Kwa Zanzibar ni madai ya kupewa, huwezi kutaka kisicho chako ukasema ni kero.

Mfano, ajira za Muungano zinazozungumzwa ni ajira za Tanganyika kwa maana mbili.
Moja, Tanganyika ndiyo inalipia ajira hizo. Pili, Kuna zisizo za Muungano lakini zimefanywa za Muungano.

Zanzibar inapodai asilimia 21 ya ajira za Muungano hiyo siyo kero wala siyo madai bali bali kuomba Fadhila'
Kiungwana Wazanzibar wasitumie neno kero bali Fadhila tukifahamu katika muungano hawana mchango

Ikiwa Zanzibar ina madai lazima ionyeshe katika muungano inachangia nini! mali ya mtu inakuwaje kero?
Zbar haina mchango hata senti kwa ushahidi uliotolewa na Wazanzibar . Kero zinatoka wapi?

Ni kwa mantiki hiyo VP na kikao walizungumzia ' maombi ya Fadhila ya Wazanzibar' siyo kero za Muungano

Tunasema hivyo kwa ushahidi wa kutosha kwasababu VP katika kile alichokita ' kero 9' kwa kuogopa kuudhi Wazanzibar na katika kutetea nafasi yake, hakuna kero hata moja iliyo na masilahi na Tanganyika!

Mfano, Azam kuingiza maziwa Tanganyika inakuwaje kero yenye masilahi kwa Tanganyika.
Tanganyika haina upungufu wa maziwa na '' in fact'' Rais Magufuli alipiga marufuku kuingizwa maziwa yanayotoka nje kutoikosesha Tanganyika mapato yanayotokana na uchochoro wa kukwepa kodi Zanzibar

Hili lina masilahi gani na Tanganyika?
VP anatumia muda kushughulikia biashara za watu! ni kero ya Tanganyika??

VP Mpango anaposema ' focus iwe moyo wa Tanganyika' anawambia akina nani!
Historia ipo wazi, Wabunge wa Tanganyika wa miaka ya nyuma walisimama kidete kuitetea Tanganyika.

Tuna mifano ya suala la Passport na G55. Wabunge hao majina yao yapo na wengi wapo akina Jenerali Ulimwengu wakiwa na heshima katika Jamii .

Hawa wa sasa hawana moyo wa kutetea Tanganyika wana moyo wa kutetea masilahi yao kama VP.

VP na wanaojificha waelewe Tanganyika ipo mbioni iwe kwa heri au la
Mzee Wariobana Tume waliliona hilo na halikwepeki kwa kuzingatia haya wanayofanya akina VP na wenzake.

Wanayoyafanya yatahitimisha safari zao kisiasa au majina yao yatahukumu vizazi vyao kama tulivyoona 'bandiko la kumlaani Waziri Mchengerwa '' hata kama maamuzi yalikuwa ya Baraza la Mawaziri.

Je , VP alisema nini katika video hapo juu!
Tutafafanua hoja 11 kuona anachosema masilahi ya Tanganyika kipo wapi na kwa namna gani.

Kwa hisani ya DW pia Hoja 11 zinazoelezea kero za Muungano wa Tanzania – DW – 24.08.2021

Tutaangalia kama kero zipo au alikuwa anazungumzia FADHILA kwa Wazanzibar

Itaendelea
 
XXIV

VP : FAIDA ZA KERO ZA MUUNGANO KWA TANGANYIKA NA ZANZIBAR

Bandiko XXIII limeeleza tafsiri za kinachoitwa kero za Muungano ambayo kiuhalisia ni 'fadhila za Muungano'

Tukiangalia utatuzi wa kero, inashangaza kuwepo kwa HATI za makubaliano kati ya JMT na SMZ.

Viongozi wetu wanawaonaje Wananchi wao!!! . Hili halihitaji hata cheti cha Form IV kulibaini.

Rais wa JMT na VP wake si Viongozi wa Tanganyika. Ni viongozi waliopigiwa kura pande zote za Muungano.
Ni viongozi wanosimamia Muungano. Inakuwaje kuna Makubaliano kati ya Muungano na Zanzibar?

Kiongozi mwenye dhamana ya mambo ya Muungano ni VP Mpango kama alivyokuwa VP SSH wakati huo.
Ipo Wizara ya Mambo ya Muungano. Ofisi ya VP na Wizara zinaajiri watu wa pande zote za Muungano.

Ofisi hizi mbili zinapogeuzwa kuwa za Tanganyika wakati wa majadiliano ni utapeli na uhuni tu.

Yaani kuna Wazanzibar kutoka ofisi ya VP na Wizara ya Muungano wanaokaa upande wa pili kujadilina na Wazanzibar wanaotoka SMZ, bila haya kuna Viongozi wanatuaminisha kuna pande mbili zimejadiliana

Ukweli, hakuna pande mbili, Tanganyika haina uwakilishi wowote.
Uwakilishi wa Tanganyika unapatikana kwa uwepo wa viongozi na uongozi si majina ya Watanganyika

VP Mpango anawajibika kwa Rais wa JMT na kamwe hawezi kufanya 'subordination' ya namna yoyote.

Kwake maagizo ya Rais ni amri na atayatekeleza hata kama si sahihi hasa kwa viongozi wa Afriika
VP anasema kero zimetatuliwa kwa 'manufaa ' ya pande mbili, Tanzania ( Zanzibar ikiwemo) na Zanzibar!

1. Usimamizi wa Bahari Kuu :
Zanzibar hawataki mambo ya Bahari yawe ya Muungano kwa wanachosema kuna gesi na mafuta.
Hilo halina tatizo kuliondoa, kuna tatizo kwamba rasilimali zinazotoka Bahari kuu ya Tanganyika kama gesi zinatumika kuhudumia shughuli za Zanzibar kama Ulinzi, mambo ya ndani, nje, Taasisi za Bunge , Wizara na kuipa Zanzibar 4.5% ya pato la Tanganyika , na subsidy ya Bajeti ya SMZ.

Makubaliano aliyoingia VP hayana faida kwa Tanganyika kwa kutoa chote na Zanzibar kwa kubaki na chake.
Mbele ya safari hoja itarudi ikimzingira VP kwa maswali mengi na kubwa ni Uzalendo wake kwa Tanganyika

VP Mpango hataweza kusimama mbele ya Watanganyika na kuwaeleza makubaliano aliyosimamia yalikuwa na faida kwao! hataweza ! achilia mbali mengine yatakayoambatana na hilo. Muda utasema

VP alitakiwa kujiuliza, haya mambo yamefanyika kwa kutumia Hati, je Kikatiba yapo vipi?

2. Mgawanyo wa Ajira katika Taasisi za Muungao. VP anasema kuna faida kwa pande mbili.
Kutoa 21% ya ajira kwa watu 1.5M wa Zanzibar na kuacha 79% kwa watu 60M kuna faida kwa hao milioni 60!!

Watanganyika wangapi wenye weledi na akili wanaweza kumwelewa VP Mpango! kwa kauli hiyo

Ajira za Muungano hazina mpaka, zote za Tanganyika kwa jina la Tanzania ambalo Zanzibar inalitumia.

Mfano aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Muungano alihamishwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Mawasiliano na ndiye alisainii mkataba wa Bandari wenye matatizo akiwa na Waziri Mzanzibar aliyepewa mamlaka na Rais Mzanzibar. Ni nani amelinda masilahi ya Tanganyika katika jambo hili lisilo la Muungano?

VP anawaambia Watanganyika kuna faida kwa mgawanyo huo wa 21% bila kueleza ajira hzinalipiwa na nani.

Inajulikan Zanzibar haina Mchango katika Muungano, ajira 21% zinalipiwa na Hazina Kuu ya Tanganyika.
VP anaposema ajira za Muungano zinaleta faida pande mbili ni kuwatusi na kuwadhihaki Watanganyika.

Ajira za Muungano ni Fadhila kwa Wazanzibar wasio na gharama ya aina yoyote isipokuwa namba tu 21%.
Hata bila Muungano ajira hizo zitabaki katika kiwango hicho tu kwa Tanganyika. Faida anayosema VP ni ipi?

VP angeeleweka kama angeeleza 21% inapatikanaje kwa hesabu gani , na inalipiwa vipi na Zanzibar
Kuwabebesha Wtanganyika mzigo halafu kudai kuna faida ni kuzitukana akili za Watu milioni 60.

Hili, VP atabaki nalo na ipo siku Wananchi wa Tanganyika watahoji mantiki na kwanini aliitenda haya.

Itaendelea kero # 3 Mgawanyo wa mapato ya Uhamiaji
 
XXV

VP : KERO ZA MUUNGANO NA FAIDA KWA TANGANYIKA, KERO ZA MUUNGANO NA FADHILA KWA ZANZIBAR

Katika kero ya 3 aliyoitaja VP Mpango ni kuhusu mapato kutumika pale yanapokusanywa

Uhamiaji ni suala la Muungano na mapato yalikusanywa kutoka vyanzo vyote na kupelekwa makao makuu

Zanzibar ina vyanzo vichache vya uhamiaji si zaidi ya 4 ( port of entry) wanakokusanya mapato
Tanganyika ina vyanzo vingi vikubwa ikipakana na nchi 8 na maeneo mengi yanayoleta Wageni.

VP anasema vyanzo vya mapato vitumike pale vinapokusanywa

VP anamaanisha kero ya Zanzibar ni mapato kukusanywa na Uhamiaji Tanzania na sasa mapato yatabaki Zanzibar
na kuingia katika mfuko wa Hazina kuu Zanzibar. Hakuna fedha itakayovuka bahari kuingia mfuko Mkuu wa Hazina

Uhamiaji ni suala la Muungano, Wafanyakazi wa Uhamiaji pande zote za Muungano wapo bila kujali upande.
Hayo ni maagizo ya Rais SSH alipofunga mafunzo ya kwanza ya Uhamiaji kule Tanga.

Wafanyakazi wanalipwa mishahara na huduma za Ofisi zinahitaji fedha kama Taasisi nyingine

Kwav suala la Muungano fedha za kuendesha shughuli za Uhamiaji zitatoka Mfuko mkuu wa Jamhuri ya Muungano
Kwa maana fedha zitatoka vyanzo vya Uhamiaji na Hazina Kuu Tanganyika kuhudumia Uhamiaji Zanzibar

VP Phillipo Mpango anasema utaratibu huo utanufaisha na kuleta tija kwa Tanganyika na Zanzibar!
Yaani VP anamaanisha Watanganyika wanapobeba mzigo wa Uhamiaji peke yao ni faida kwao!!

Kauli za VP zinaacha maswali , kwamba, ima amewadharau Watanganyika katika weledi na uelewa kiasi kwamba anaweza kusimama mbele ya TV na kuwatwisha mzigo kisha kuwaambia ni faida kwa upande wao, au amefanya hivyo kuwapendeza Wazanzibar na pengine mkuu wake au hakuelewa madhara ya kauli yake katika Muungano.

Kwa hali yoyote ile mapato ya shughuli za Muungano yakibaki Zanzibar yanapaswa kuhudumia shughuli za Uhamiaji Zanzibar, na ya Tanganyika pia, VP hakueleza bali kuaminisha Watanganyika utaratibu huo una faida kwao

Tanganyika haina uwakilishi katika vikao vya kero za Muungano. VP anajiweka katika nafasi ngumu sana kwasababu inaonekana ana 'conflict of interest' kuhusu Uzalendo wake kwa Tanganyika na nafasi yake.

Kauli kama hizi zinawapa '' kauli' wale waliomtuhumu bila ithbati siku za mwanzo.

Kero inayofuata ni mgawanyo wa mapato
 
XXVI
VP : ''FAIDA'' KERO ZA MUUNGANO KWA TANGANYIKA, FADHILA ZA KERO ZA MUUNGANO KWA ZANZIBAR

Makamo wa Rais wa JMT (VP) aliendelea kuorodhesha alichokiita utatuzi wa kero za Muungano

Tuangalie kero ya Tatu

Mgawanyo wa mapato ya misaada kwa 'general budget support'
Wazanzibar wamepigia kelele ssuala la misaada bila kujadili misaada inayopata ambayo ni zaidi ya wanachodai

Waziri wa fedha Marhum Basil Mramba alisema wakati wa Salmin Amour na hata Amani Karume mishahara ya watumishi wa SMZ ilitoka Hazina kuu tena akisema katika kiwango cha 20M wakati huo.
Na aliyekuwa waziri wa masuala ya Muungano Bw Makamba alisema ''JMT ina support bajeti ya SMZ''

SMZ inapata 4.5% ya pato la Tanganyika kwa kinachosemwa ni shea za kuanzisha BoT.
Uwepo wa shea ni kweli, lakini ni nafuu kwa Tanganyika kulipa shea kwa SMZ kwa kuzingatia malipo ya miaka mingi kuliko kuendelea na utaratibu uliopo una maana kuchukua kisicho husiana na mtaji wa Bank Kuu.

Kila jiwe la dhahabu, Tanzanite, Almasi, Nickel , na kila kilo ya zao la chakula au biashara, kila cubic meter ya gesi , au kila senti inayotoka Bandari yoyoteTanganyika , kila senti ya kodi n.k. kuna 4.5% inakwenda Zanzibar

VP anasema italeta ufanisi katika miradi ya maendeleo. Kwa Tanganyika misaada inaingia katika shughuli za muungano kw kuhudumia maeneo kama Ulinzi, mambo ya ndani, nje na Taasisi zote za Muungano.

VP Mpango anaposema zitasaidia maendeleo kuna ukweli nusu.
Nusu ya ukweli ni kwamba misaada itasaidia 'general budget support' ya Zanzibar kwa kuelekeza katika shughuli za Zanzibar tu. Nusu ya pili General budget support ya Tanganyika ni ya Tanzania inayohusu mambo ya Muungano.

Ili kueleweka, tuchukue mfano wa Msaada unaotolewa kwa Wizara ya Mambo ya ndani wa Tsh 300.

Katika Tsh 300, Tsh 100 zitakwenda Zanzibar katika shughuli za maendeleo kama Afya, elimu , Uvuvi n.k. kwasababiu Bajeti ya SMZ haina Wizara ya mambo ya ndani.

Tsh 200 za Tanganyika zitakuwa za Tanzania na zitaenda katika eneo lililokusudiwa la Wizara ya mambo ya ndani ambayo pia inatoa huduma Zanzibar kama Taasisi ya Muungano.

Kwa maana kwamba, Zanzibar wanapata 1/3 halafu wanapata shea katika 2/3 ya Tanganyika.

Lakini pia kuna suala la hesabu, 1/3 ya watu milioni 1.5 na 2/3 ya watu milioni 60 ni hesabu ya wapi?

VP Mh Mpango ana furaha kumaliza kero ya kugawana misaada.
Furaha yake ni kwa kuona Wazanzibar wameridhika na Watanganyika wanaendelea kubeba mzigo.

VP hawatendei haki Tanganyika. Ikiwa kuna 'Formula' ya kugawana misaada 1/3 vs 2/3 kwa, iko wapi Formula ya kugawana gharama za kuendesha Taasisi za Muungano?

VP Mpango anaelewa kodi za TRA Zanzibar zinabaki huko, mapato ya Muungano kama Uhamiaji yanabaki Zanzibar na kwamba hakuna senti inayoingia Hazina kuu Dar es Salaam.

Ikiwa kuna formula iliyompendeza VP ya kugawana misaada, iko wapi formula ya kugawana majukumu ya Taasisi za Muungano!

Kikao cha VP na kero anazosema ni mambo ya kutoa fadhila za kero kwa Zanzibar si Tanganyika.

Kuna sababu za kutosha za kuamini kwamba VP anasimamia masilahi ya Zanzibar akiwatweza Watanganyika kwa kauli za Faida za utatuzi akijua fika Tanganyika haifadiki na chochote katika anayoyafanya.

Tanganyika itaendelea kubeba mzigo wa Muungano hadi pale itakapokuwa na serikali yake yenye viongozi Wazalendo na walio na uchungu nayo, wanaoitetea na si wale wanaoiuza wakitetea nafasi zao.

Katiba mpya ni muhimu

Inaendelea kero ya Simu
 
XXVII

MAPATO YASIMU YANAPOGAWANYWA KWA ZANZIBAR NA TANZANIA

Kuna malalamiko ya Wazanzibar kwamba country code ya simu ya Tanzania ambayo ni +255 haiwahusu wana yao isiyotumika +259, wamelalamika kukosa mapato yanayotokana na simu iwe kupiga, text au miamala

Nyakati za Muungano Posta na simu ilikuwa katika mkataba wa Muungano.
Posta na Simu ilikuwa shirika moja na eneo la usalama wa nchi kitoa huduma

Mabadiliko ya Teknolojia na soko huria yamesababisha uwepo wa mashirika huru ya ''posta' na Simu mengi na huria.
Hilo limeongeza ushindani na kulazimisha kuligawa shirika la Posta na Simu kuwa mashirika yanayojitegemea.

Serikali kuwa na mamlaka ya kusimamia shughuli za mawasiliano ( TCRA) ambalo uanzishwaji wake si suala la Muungano. Mfano kuna shirika la simu la Zantel lenye ubia na SMZ.

Kwa hali ya ushindani Zantel ilihamishia huduma Tanganyika kufaidika na soko la watu 60M dhidi ya laki- Zanzibar

SMZ ilikuwa na kila sababu na uwezo wa kuanzisha mamlaka yake ya kusimamia mawasiliano kama TCRA.
Kwa makusudi hawakuanzisha kwasbabu shirika hilo halitaipa SMZ mapato mengi kuliko kuvizia ya TCRA

Kero ya Muungano ni Wazanzibar kulalamika kwamba pesa za mawasiliano ya simu zinapaswa kutozwa kodi na SMZ kwasababu tunatumia 255. Hoja ikapelekea uwepo wa mgawanyo wa mapato yanayopatikana TCRA.

Katika mazingira ya kawaida Wazanzibar wanaoishi Tanganyika ni sawa au pengine zaidi ya wanaoishi Zanzibar, hivyo kupiga simu Zanzibar kutaingiza mapato zaidi kwa Tanganyika kuliko Zanzibar.

Ndivyo ilivyo kwamba Wazanzibar nje ya nchi watapigia simu Tanganyika kwa ndugu zao kuliko Zanzibar

Mabandiko ya nyuma tulionyesha idadi ya wamiliki wa simu wa mkoa wa Katavi ni sawa na wamiliki simu wa Zanzibar yote. Kwa maana simu za Tanganyika peke yake zinaingiza mapato TCRA bila kuitegemea Zanzibar.

Uwepo wa mgawanyo wa mapato ya TCRA ni kufanya ujahilia au uporaji kwa Watanganyika.
Kwamba, fedha zao zinakwenda Zanzibar kwa kusingizia Muungano lakini bila sababu ya msingi.

Tanganyika haitaathirika ikiwa Zanzibar watapewa ruhusa ya kutumia +259 au mamlaka yao ya Mawasiliano ''ZCRA''. Tanganyika haiathiriki kwasababu kuu mbili, idadi ya watumiaji wa simu ni kubwa na pili wanaohitaji simu za Tanganyika ni Wazanzibar kwasababu ya uwepo wao bara.

Kwa ilivyo, mtu akiwa Tanga na kumpigia nduguye aliyeko Dar es Salaam sehemu ya kodi inakwenda Zanzibar.

Mtu akiwa Musoma akatumia aka txt, miamala au simu kwenda Tabora kuna sehemu ya kodi inakwenda Zanzibar.

Vivyo hivyo Mwanafunzi aliyeko Mtwara akiwasilianana baba yake Kagera kuna sehemu ya kodi inakwenda Zanzibar.

Ukitaka kuthibitisha uporaji ni pale Wazanzibar wapo tayari kuunda taasisi zote zenye mbadala na za Tanganyika lakini hawataki kuunda ZCRA, wanafahamu upenyo wa kuchukua kodi za mawasiliano baina ya Watanganyika haupo

Katika kikao cha kero cha VP, anasema mgao limefanyika kwa faida ya pande mbili za Muungano.

Ukweli ni kwamba limefanyika kwa fadhila za upande mmoja yaani Zanzibar.

Inashangaza kwamba ukweli kama huu bado unapakwa rangi na VP. Uzalendo upo wapi?

Kwanini VP awafanye Watanganyika mazumbukuku kwa kejeli na dhihaka ? Tanganyika inafaidika na kitu gani?

Tunahitaji katiba mpya na Tanganyika yenye viongozi Wazalendo kwanza

Muungano uwawajibishe washirika si mmoja kubwebwa kwa gharama za mwingine. VP Mpango anaelewa hili!!! na hana sababu za kuwadhihaki Watanganyika. Kwamba wanapoteza yeye anasema wanafadika!

Inaendelea
 
XIX

KERO ZA MIKOPO KWA ZANZIBAR ITAKAYOLIPWA NA TANGANYIKA

Katika kumaliza eneo la kinachoitwa kero za Zanzibar tuangalie maeneo mawili ya mwisho ambayo VP alisema yana manufaa kwa Zanzibar na Tanganyika

Malalamiko ya Azam kuhusu maziwa
Kwamba Wazanzinzibar wanalalamika kuhudu kampuni ya Azam kuzuiliwa kuingiza maziwa Tanganyika
Tatizo lilianza wakati wa JPM alipozuia mianya ya uchochoro wa kukwepa kodi kupitia Zanzibar.

Kamati ya VP imeruhusu maziwa kutoka Zanzibar yaingizwe Tanganyika kutoka nje ya nchi kupitia Zanizibar

Hili lina maana moja kwamba maziwa ya Tanganyika yatakuwa ghali ukilinganisha na yanayoingizwa na kampuni ya Azam. Lakini jambo la kujiuliza ni kwamba kwanini biashara za mtu binafsi ziwe kero ya Kitaifa?
Nani yupo nyuma ya hili na kwamba kwanini serikali iingilie biashara binafsi! nani anaamuru haya

Kero zingine ni kuhusu mikopo ifuatayo;
Mkopo wa fedha za Hospitali ya Mnazi mmoja
Barabara za Chake Chake
Bandari ya mpiga duri

Kwamba serikali ya muungano idhamini mikopo ya maeneo hayo. Hii inakuwaje kero ya muungano?

SMZ inavyanzo vyake vya mapato na inawez kukopa na kulipia mikopo, kwanini ipitie JMT?

Jibu la maswali hayo ni rahisi, lengo ni kutaka mikopo ipitite JMT na Kisha ilipwe na Hazina Dar Es Salaam ambayo ni mali ya rasilimali za Tanganyika., Zanzibar haina mchango Hazina na kubebesha mzigo wa mikopo kwa Tanganyika

VP Mpango anaposema suluhu ni kwa manufaa ya nchi mbili inashangaza sana.
Kwamba kero hizo hapo juu, ni ipi ambayo Mtanganyika ana nufaika nayo?

Ni kwa mantiki hiyo tunasisitiza kinachoitwa kero za Muungano hakipo, zipo kero za Wazamzibar kutaka kufadhiliwa kwa kisingizio cha Muungano. Kwanini haya yanatokea wakati huu kwa kasi zaidi?

Kuna msukumo gani zaidi kuliko huko nyuma kwa nyakati za Magufuli, Kikwete, Mkapa au Mwinyi?

Tunahitaji Tanganyika itakayosimamia masilahi yake na siyo kutumika kwa koti la Muunganano.
Tunahitaji Tanganyika itakayokuwa na serkali ya Wazalendo wenye uchungu na nchi yao.

VP Mpango ameshindwa kusimamia masilahi ya nchi pengine kwa hofu ya nafasi yake, haya yapo katika rekodi na ipo siku ataulizwa Uzalendo wake kwa Tanganyika !!!
 
MKOPO WA MAGHALA YA KILIMO YA ''JAMHURI YA MUUNGANO'

Mkataba wa Muungano au nyongeza nyingine zilizofuata Kilimo hakijawahi kuwa suala la Muungano.

Shughuli za Wizara ya kilimo ni za JMT ni Tanganyika kama ilivyo katika katiba ya JMT 1977

Katika ziara yake Rais wa Jamhuri ya Muungano amefungua maghala ya kuhifadhi chakula kule Mtwara

Akitoa taarifa kwa Mh Rais, Mratibu wa mradi wa maghala alisema Serikali imejenga maghala 14 kwa fedha za mkopo kutoka Bank ya Afrika wa mabiloni ya Tsh.

Katika maghala 14 , 12 yapo Tanganyika na 2 yapo Zanzibar kwa maana ya Unguja na Pemba.

Kwa muda mrefu tumejaribu kuonyesha mambo kadhaa yanayohusu Muungano

1. Kwa mfano huu, Kilimo si jambo la Muungano, je, ni kwanini Maghala ya Kilimo yanayojengwa kwa fedha za mkopo wa Tanganyika ziende kujenga maghala Zanzibar ambako kuna Wizara ya Kilimo na Bajeti yake?

2. Mkopo wa Bank utalipwa kutoka katika Hazina Kuu Dar es Salaam ambayo ni Mali ya Tanganyika kwa asilimia 100.
Ni mali ya Tanganyika kwa vile Zanzibar haichangii kwa namna yoyote kama tulivyoeleza huko nyuma

Hivyo maghala mawili yaliyojengwa kwa pesa nyingi za mkopo yatalipiwa na fedha za Tanganyika.

Laiti serikali ya Tanganyika ingalikuwepo hili lisingetokea kwasababu maghala mawili yange elekezwa maeneo mengine ya Tanganyika yanayochangia katika mfuko wa hazina kuu ya Tanganyika.

Kulifanya jambo la Kilimo kama la Muungano ni njia ya kupora rasilimali za Tanganyika kwa jina la JMT
Haya yameanza wakati huu wa Rais Samia jambo linalozua maswali

3. Tunazidi kuona unafiki wa Wazanzibar. Kilimo si jambo la Muungano kama Bandari.
Vipi wanakubali kujengewa maghala kwa jambo wanalofaham fika si la Muungano. Huu ni unafiki usio na utetezi

Unafiki unazidi pale Wazanzibar wanapodai kugawana misaada lakini MIkopo kama huu wanasema ni Jukumu la Muungano ili kumtwisha mzigo Mtanganyika.

Ikiwa Zanzibar inapata fursa za JMT kama Misaada, fursa za ajira n.k. ni wakati Zanzibar iwajibike ;
1. Kuchangia mapato ya kuendesha Muungano
2. Ishiriki kulipia huduma kama Mikopo

Mambo yanayowakera Watanganyika ni kuona Zanzibar ikipewa fursa maalumu kuliko maeneo mengine ya nchi lakini Zanzibar ikiwa haiwajibiki katika Muungano kwa lolote au chochote kama kuchangia Muungano au kulipia madeni ya huduma inazopata, kwa maana kwamba inafaidika kuliko mikoa michanga au masikini ya Tanganyika lakini Zanzibar hairejeshi chochote kwa Tanganyika

Maswali ya lini Zanzibar itakuwa mshirikia na si mzigo katika Muungano yanazidi kila uchao, ndiyo maana wengi wanadai katiba mpya itakayoweka misingi ya Muungano katika ushirika zaidi ya kutoa na utegemezi
 
YATOKANAYO NA MKUTANO WA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA NA WADAU DEMOKRASIA YA NCHI
Hoja ya Miaka 3 ya elimu ya Katiba
Hoja ya umuhimu wa 'kijitabu' cha katiba

Mkutano wa Baraza la vyama vya siasa na wadau wa Demokrasia umemalizika kwa hoja tata na zenye mantiki

Hoja zinahitaji mjadala mpana na wa kina

Moja ya hoja mitandaoni ni kauli ya Rais SSH ya katiba ni ' Kijitabu' tu wakati anasisitiza hoja yake.
Kauli imeunganishwa na ile ya siku za nyuma iliyosema Katiba haiwezi kuleta chakula mezani.
Inaonekana ni marudio ya kauli ya 'Katiba isubiri ajenge uchumi kwanza'

Kauli ya ''kijitabu'' imewakera Wananchi na kufunika hoja muhimu. Ikiwa kauli ni ya hotuba aliyoandaliwa Rais , walioandaa hawakumtendea haki. Ikiwa ni kauli yake kutokana na ghadhabu Mh hajajitendea haki

Katiba ni muongozo mama wa sheria za na zana ya kwanza anayopewa Rais kwa kuapa akiingia madarakani.

Rais SSH hakuingia madarakani kwa kuchaguliwa bali kwa utaratibu wa kikatiba baada ya kufariki Rais JPM

Rais aliapa kwa Katiba kwanza kabla ya kufanya kazi yoyote ya Urais kisha ''kumwapisha'' Mwanasheria mkuu AG ili kuhakikisha anapata usaidizi wa kufuata taratibu zilizoanishwa katika katiba ikiwemo uteuzi wa wasaidizi.

Uwepo wa Rais katika mkutano wa Wadau wa Demokrasia si bahati mbaya.
Rais ni kiongozi wa Serikali na hivyo taratibu zote zinazogusa mambo ya Katiba zinamhusu moja kwa moja

Katiba ni muongozo wa namna tunavypata viongozi wa Serikali, Bunge na Mahakama

Serikali ina andaa miswada ya sheria, Bunge linajadili na kuidhinisha miswada, Rais anasaini na Mahakama inatafsiri
Rais ana nguvu ya ziada alizopewa na Katiba juu ya sheria za nchi.

Rais anaweza kukataa mswada na Bunge,anaweza kuvunja Bunge na ni mteuzi wa viongozi wa mahakama

Vyombo vya serikali vinaundwa na sheria zinazotokana na Katiba na sheria za nchi zinawafikia Wananchi

Rais anaweza kutanganza hali ya hatari na kuamua watu watembee , wakae au walale vipi
Anaweza kuingiza nchi katika vita akipeleka askari vitani

Waziri wa Kilimo akipiga marufuku uuzaji wa mazao anatumia mamlaka ya kisheria aliyopewa chini ya Katiba
Waziri wa Afya anapoongeza tozo ya Toto Bima anafanya hivyo kwa mujibu wa sheria chini ya Katiba.

TRA inapoongeza kodi, wanafanya hivyo kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha mamlaka chini ya Katiba

Wavuvi , wafugaji , na wakulima wanatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria chini ya Katiba
Matumizi ya ardhi, maji , misitu, makazi n.k. yanatokana na sheria zilizochini ya Katiba

Rais anaweza kumsamehe aliyehukumiwa kunyongwa au kusaini anyongwe kwa sheria chini ya Katiba ya nchi.

Rais ni mtumishi namba moja na mwajiri mkubwa wa Umma, anaweza kutoa au kupunguza ajira kwa mujibu wa sheria za nchi chini ya Katiba.

Walituhumiwa na vyeti feki waliondolewa kazini sasa wamelipwa mafao kwa amri ya Rais kwa kuzingatia mamlaka aliyopewa kisheria chini ya Katiba.

Wakulima na upatikanaji wa pembejeo ni zao la serikali kuidhinisha kwa sheria zilizotungwa chini ya Katiba ya nchi
Mfuga nyuki akitaka kusafirisha asali itabidi afuate tratibu zilizowekwa na mamlaka husika chini ya Katiba

Mikopo ya Wanafunzi inatokana na sheria za nchi zinazoipa serikali mamlaka ya kutoa au kutotoa.
Kiwango gani mtumishi anakatwa kurudisha mikopo ni kwa mujibu wa sheria za mamlaka husika chini ya Katiba

Mifano ni mingi sana, inatosha kusema kila tulipo tuwe hai au wafu Katiba ya nchi ndiyo muongozo wa kila siku.

Kuanzia tunapolala, kuamka kwa kifungua kinywa, kwenda kazini kwa boda boda au kwa basi au gari, kupata lunch , kurujea, kupata dinner, homework za watoto kwa umeme au vibatali yote ni chini ya sheria na miongozo ya Katiba

Watanzani wachache wanaelewe chombo cha kwenda mwezini, hawaelewi Kitabu cha rocket science, hawajui kitabu cha sheria au medicine n.k. , lakini asilimia ''70-90'' wanajua kitu kinachoitwa Katiba.

Wanaweza kutofahamu vifungu vya sheria lakini wanajua sheriaza nchi zipo katika Kitabu kianchoitwa KATIBA

KATIBA haiwezi kuwasawa na kijitabu cha mwanasesere.

Katiba ni kitabu kikubwa katika maktaba yoyote kwasababu kinaamua nani aishi nani asiishi na kwa namna gani.

Katiba ni ugali na maharage, katiba ni vitumbua na maandazi, katiba ni Hospitali na Madarasa, Katiba ni mifugo na nyuki na katiba ni V8 na Bajaji, katiba ni mama ntilie na mbeba Lumbesa, katiba ni Profesa na Mwanafunzi n.k.

Katiba inakuwaje KIJITABU?

Inaendelea .... Darsa adhimu la sheria ya Katiba la miaka 3! darasa la kipekee duniani.
 
2
YATOKANAYO NA MKUTANO WA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA NA WADAU DEMOKRASIA YA NCHI
Hoja ya Miaka 3 ya elimu ya Katiba
Hoja ya umuhimu wa 'kijitabu' cha katiba

miongoni mwa mambo aliyoeleza Mh Rais ni subira elimu ya katiba ikitolewa kwa miaka 3
Elimu ya katiba ni hoja iliyotolewa na aliyekuwa waziri wa sheria Mh Ndmbaro sas tunajua ilikuwa ya Baraza zima

Hakuna anaye eleza ni wapi elimu ya katiba iliwahi kutolewa duniani kabla ya kuandika Katiba.
Kwa utaratibu, elimu ya katiba hutolewa wakati wa 'rasimu' kama ilivyokuwa huko Kenya , Afrika kusini au tume ya Mzee Warioba. Ni kupitia elimu ya katiba wananchi hupata fursa ya kuitathmini katiba kwa kura ya maoni

Tuna historia ya Kuandika katiba ya Uhuru 1961, ya Jamhuri ya Tanganyika 1962, ya Mpito 1964 na ya kudumu 1977.
Hakuna wakati wowote elimu ya uraia ilitolewa kwanza.

Hata marekebisho ya Katiba ya Zanzibar ya 1984 toleo 2010 haikuwa na elimu ya katiba.

Hili la elimu ya Katiba linatoka wapi? Je, hii si sababu ya kupitisha muda?

Ikiwa tunadhani wananchi wanatakiwa kuielewa katiba, ukweli ni kwamba wanaielewa katiba..
Mzee Warioba na Tume yake walishangazwa na kiwango cha Wananchi kuelewa mambo ya Katiba.

Wananchi haielewi katiba kwa vifungu bali kwa hoja ndani yake.
Mfano, Wananchi wanaweza kutojua kifungu cha sheria kinachotupa idara ya Mahakama, lakini wanaelewa haki inatolewa na idara ya mahakama. Tunawezaje kusema wananchi hawajui katiba?

Na ikiwa tunahitaji maoni tayari tunayo ya Tume ya Nyalali, Jaji Kisanga na ya Warioba kwa uchache wa kuandika.

Tume hizi zilifanya kazi ya kukusanya maoni ya wananchi kwa kina na takwimu tofauti na Kikosi kazi cha Mkandala kilichohoji watu wachache na kaundika ripoti kama kilivyo agizwa

Hakuna kiongozi wa serikali anayeeleza kwanini maoni ya Tume ya Warioba hayafai.
Hakuna anayeeleza kwanini maoni ya Tume ya Kisanga au Nyalali hayafai.

Rais Samia alikuwa kiongozi wakati wa Bunge la Katiba. Ikiwa kuna tatizo kwanini haelezi anatafuta sababu zisizo na mashiko kama hii ya elimu ya Katiba!

Huko nyuma tuliwahi kujadili kwamba Kikosi kazi kililenga kuundoa Umma kwenye maoni ya Tume ya Warioba

Inasikitisha viongozi wa sACT Wazalendo wakiingia katika mkumbo wa kikosi kazi wakijua kwamba lengo si zuri.

ACT wanajua fika Kikosi kazi kiliundwa bila kufuata tartibu lakini wao wakaunga mkono.
Leo ACT wameacha hoja za Tume ya Mzee Warioba sasa wanazungumzia kikosi kazi ns tume huru ya uchaguzi

Kudai Tume huru ya uchaguzi wakati sheria kuu ni katiba haisaidii kitu. ACT wanatambua hali ya siasa lakini kwa makusudi, kutojua au usaliti wameungana na CCM kuhujumu agenda muhimu za nchi kama Katiba

ACT wameshiriki uchaguzi mdogo na kushindwa wakilalamikia rafu za CCM.
Hivi inschukua mambo mangapi kwa ACT kuelewa CCM haina nia njema na masuala yenye masilahi kama Katiba?

Kwa ushiriki na CCM, ACT inatoa uhalali kwa chama tawala kuendelea na ubabe.

Laiti kwa uzito wake ACT kule Zanzibar wangeungana na Chadema , nguvu ingaliwaleta CCM mezani, kinyume chake ni kutoa uhalali wa uhuni wa CCM kutamalaki

Inasikitisha zaidi pale viongozi wa juu kama Mh Duni wakitoka katika mkutano wa hujuma tena wakisifu kwamba Rais SSH amewafurahisha. Mkutano haukuwa na jambo lolote la kufurahisha na haijulikani ACT wanafurahia nini

ACT Wajitafakari kama wanachofanya kina maana na masilahi katika taifa letu.

Hadi hapo watakporudi upande wa wengi, ACT inabeba taswira ya USALITI
 
CHADEMA INAVYOJIVURUGA KWA MISIMAMO YA KATIBA
MWENYEKITI NA UONGOZI KIMYA! UCHAWA WATAWALA


Rejea bandiko XIX likieleza CHADEMA (CDM) inavyoyumba kwa misimamo kutokana na Ombwe la uongozi wa chama. Bandiko likaeleza kwanini viongozi wa Kamati kuu walaumiwe kwa mauza uza ya Mwneyekiti

Kuna 'taarifa' za Mwenyekiti Mbowe kuonekana katika vikao kwa kinachosema ' vya mashauriano' kwa mujibu wa mitandao ya jamii. Hakuna anayejua agenda wala kinachojadiliwa lakini kuna kila dalili CDM inashiriki vikao fulani

Kumekuwa na mtifuano kati ya CDM na Kundi lingine la Wanaharakati. Agenda ya kundi hili ni katiba mpya na kuna taarifa CDM walikataa kushirikisha kundi hilo katika mikutano. Akiongea katika mitandao kiongozi wa kamati kuu ya CDM Bw Mwaitenda alibainisha tatizo la mawasiliano . Hali si nzuri kukiwa na kushambuliana katika mitandao

Agenda ya kundi la Wanaharakati ni kutumia 'platform' za siasa kuendeleza harakati zao.
Huu ni ukweli kwasababu kwa sheria za nchi si rahisi raia kuanzisha mikutano nje ya utaratibu wa siasa

Mkutano wa Temeke ulihudhuriwa na makundi mbali mbali chini ya utayarishaji wa Chadema.

Ni ukweli usiopingika mchakato wa Katiba lazima uhusishe makundi ya siasa. Wanasiasa ni wadau muhimu kwa hadhi na platform. Mathalani Mwanaharakati na Mwanasiasa wana hadhi tofauti katika uwanda wa mhusiano ya Kimataifa.

Ikiwa CDM walizembea au walikusudia kutoshirikisha Wanaharakati, ni kosa la kisiasa.

Wanaharakati ni sehemu muhimu inayoandaa wapiga kura 'voting block' tukijua si kila mtu ni mwanasiasa au anaamini katika siasa. Nguvu ya Chama cha Siasa ni Wanachama kwavile ndio wapiga kura watoa rasilimali

Katika hali isiyo ya kawaida ujumbe wa Katiba mpya wa CDM unachanganywa na Tume Huru ya uchaguzi.
Ni jambo la kushangaza kwasababu Tume huru ni matokeo ya Katiba , iweje kuwe na madai ya aina mbili!

Msimamo wa CDM ni katiba mpya, lakini baada ya M/Kiti Mbowe kushirikia ' Maridhiano ' ya kupoteza muda sasa narudi kwa njia ya Tume Huru. Hili linawavuruga Wana CDM.

Ni dhahiri M/Kiti tangu atoke Magereza na kuitwa ikulu amekuwa '' Compromised'

Pengine ni kutokana na kuwa compromised, Mbowe hataki kujihusisha na Wanaharakati wanaodai Katiba Mpya.

Ikumbukwe Mbowe alisema '' Mama ana ni njema katika Majidiliano' na huenda nia hiyo ina compromized misimamo yake kisiasa

Kuna uwezekana mtifuano kati ya Wanaharakati na CDM unchochewa na CCM lakini kuna maswali ya kujiuliza
1. Kwanini Uongozi wa CDM upo kimya wakati baadhi ya washiriki wa mtifuano wakiwa viongozi wao?
2. Kwanini uongozi wa CDM unaruhusu mijadala inayolenga kuwagawa Wananchi badala ya kuwaunganisha?

Kutokana na M/Kiti kuwa '' compromised ' ni wakati wa Wanachama kuchukua hatua za kukinusuru Chama kilichowekewa matarajio na wananchi wengi.

1. Wanachama kushikiza M/kiti ajiuzulu kwasababu ameshindwa kuunganisha nguvu ya umma kwa ujumla
2. M/Kiti ajiuzulu kwasababu kuna kila dalili amekuwa 'compromised'
3. M/Kiti ajiuzulu kwasababu anakwenda kinyume na Msimamo wa CDM wa kutoshiriki Uchaguzi
4. Kamati kuu ya CDM ichukue hatua, Wajumbe wanaoona mwelekeo hasi wa chama chao wajiuzulu nafasi zao.

Bila kuchukua hatua za makusudi na za lazima Chama kinapoteza mwelekeo kwa kasi kubwa
 
WENDAWAZIMU (INSANE)
JAMII INACHOKA NA UPINZANI. TATIZO NI UPINZANI AU VIONGOZI WA UPINZANI?

Mabandiko yaliyotangulia tulieza wendawazimu wa Chama cha ACT Wazalendo wa kudai Tume Huru ya uchaguzi badala ya katiba mpya. Tulisema Tume ni matokeo ya Katiba na haiwezi kutengwa na madai ya Katiba mpya

ACT iliyosheheni viongozi wa CUF ya zamani walifanya ujinga wa kuamini mambo nusu.
CUF iliamini kubadili katiba ya Zanzibar kungetoa majibu ya tatizo ikiwemo uwepo wa Tume huru ya uchaguzi.

Serikali ya CCM ikawapa CUF tume huru yenye wajumbe sawa. Katiba ya 1984 marekebisho ya 2010 ikawapa Wazanzibar kichwa kikubwa, kwanza, kuamini Katiba imewapa ukuu juu ya katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na hivyo kutoingilia katika masuala yao.

CUF wakasahau Amiri Jeshi Mkuu ni Rais wa JMT, na Tume ya uchaguzi ya Zanzibar inaongozwa na sheria inayokataza matokeo kuhojiwa mahakamani.

Furaha ya CUF na Wazanzibar hadi kujisahau ni 'Euphoria' yaani raha inayopita kipimo na kuviza ufikiri.

Uchaguzi ulipofanyika na CUF kuelekea kushinda M/kiti wa ZEC alitoka katika eneo la kujumlisha matokea kwa msaada wa vyombo vya doal, akaenda kwenye TV na kufuta matokeo kwa msaada wa vyombo vya dola.

Hayo yaliwezekana kwasababu Rais wa JMT ni Amir jeshi mkuu. Mahakamani sheria inasema matokeo hayahojiwi.
CUF chali ! Wakaambuliwa mikwaju na Bakora na kila aina ya dhulma. Katiba ya Zanzibar haikuwasaidia kitu.

CUF kama ACT Wazalendo hawaelewi kwa makusudi , ujinga au kutojua kwamba Vyombo vya dola vina mvhango mkubwa katika kupindua matokeo, na kwamba kama hakuna kuhojia matokeo mahakamani ni balaa zaidi 'disaster'

ACT wanarudia jambo lile lile kwa namna ile ile ''insane' au Wendawazimu

CHADEMA katika hali ya kushangaza meingia mtego wa kudai Tume huru ya uchaguzi, wakiunga mkono wendawazimu 'insane' ya ACT.

Chadema wanasahau kwamba walikamata masaunduku ya kura na Polisi hawakufanya lolote na kwamba hakuna matokeo ya Tume yanayohojiwa mahakamani

Vyama vya Upinzani vingelikuwa makini vingesusia uchaguzi na kuendesha kampeni ya kudai katiba mpya.
Umma upo nyuma yao wakiwemo wanachama wa CCM wanaosema ni wakati wa kuwa na katiba.

Kampeni za CHADEMA kanda ya Magharibi , Serengeti na Ziwa inaonyesha kuungwa mkono na umma

Kwa bahati mbaya Mwenyekiti amechomeka hoja ya Tume huru bila kufikiri mazingira ya kisiasa katika Ujinga ule ule walioufanya CUF na unaoEndelezwa na ACT

Ubabaishaji wa Chadema umevuruga umma kiasi cha Wanaharakati kuhoji ikiwa tatizo ni upinzani au viongozi wa upinzani waliochoka na wanaofukuzia vyeo , Ubunge na Udiwani.

Hoja za Wanaharkati zina mantiki , kwamba, Umma umekuwa '' frustrated '' jinsi Chama kikuu cha Upinzani kilivyoshindwa kusimama katika misimamo yake, kuunganisha Umma na kutumia Umma kuleta mabadiliko.

Kuna nafasi ya kurejesha imani ya Umma kutoka Chama kikuu cha upinzani.

Nafasi hiyo ni kumtaka Mwenyekiti ambaye amekuwa ''severely compromised'' na kupoteza uwezo wa kuona mambo, kutafakati na maono ya baadaye kujiuzuku au taratibu za chama zitumike kumlazimisha ajiuzulu

M/Kiti wa Chadema amehshindwa kuunganisha umma, kutumia nguvu ya umma kuleta mabadiliko chaya.
Kinyume chaka ametumia nafasi yake kuyumbisha misimamo ya chama na kudumuza vugu vugu la Katiba.

Hakuna shaka M/Kiti amekuwa ''compromised'' na kuna kila sababu ya kuamini si kwamba analamba asali bali amepewa Kisado kwenda nacho nyumbani.

M/Kiti amechoka it is time to go! uwepo wake ni liability siyo asset. Uwepo wake unadumaza Upinzani.
 
KUTOKA MITANDAONI: Dr R NSHALLA ANENA

MBOWE ATIBUA ZAIDI, ASONONESHA WAFUASI WAKE


Katika mtandao wa X kulikuwa na mjadala wa Katiba. Moja ya wachangiaji alikuwa Mwanasheria Nguli na Wakili ambaye pia alikuwa Rais wa chqma cha mawakili Tanganyika Dr Nshalla.

Dr Nshalla alieleza nini kinahitajika katika mchakato wa kuandika katiba mpya.
Dr Nshalla hueleza mambo kwa upeo wa hali ya juu wa kisheria. Katika mjadala wa leo Dr Nshallah alieleza haya ;

Kwanza, kwamba mchakato wa katiba unapaswa kutanguliwa na kura ya maoni ikiwa Muungano uendelee au la!

Pili, ikiwa Wananchi watasema uendelee, ni muungano wa serikali zenye muundo gani, serikali moja ambayo wengi hawaikubali, serikali mbili ambao ni muundo wa sasa au serikali tatu

Dr Nshalla akasema kwa hali itakavyokuwa kutakuwa na ulazima wa kuwa na serikali ya Tanganyika na hivyo kutahitajika pia kuunda katiba kwa kile alichosema iwe kwa jina lolote litakaloamuliwa na Wananchi.

Dr akasema ikiwa Wananchi wataamua muungano uendelee na uwe wa serikali 3 , kutahitaji kuangalia ukubwa wa serikali ya Muungano ikiwa kama itabaki kama ilivyoshauriwa na Tume ya Warioba au vinginevyo.

Katika hilo la Serikali ya Muungano, Dr kasema ni lazima pia uchangiaji uangaliwe kwasababu kutakuwa na nchi mbili zenye hadhi sawa na hivyo serikali ya Muungano itaendeshwa kwa msingi huo.

Na mwisho Dr Nshalla akaeleza taratibu zinazoweza kutumika katika kupata Bunge la Katiba.

Dr Nshalla alisisitiza kwamba tuna fursa ya kuangaliwa wenzetu wa nchi kama Kenya na South Africa kwa namna walivyoweza kupita katika vipindi vya mpito.

Dr Nshalla akaonya, Bunge la Katiba haliwezi kuchaguliwa na Rais bali kwa ushirikishwaji wa makundi ya jamii.

Akihitimisha hoja Dr Nshalla alisema Elimu ya Katiba hutolewa wakati wa RASIMU ili watu waweze kufanya maamuzi ya Katiba wanayoitaka na si elimu hii ya '' shahada ya miaka 3 '' kwa Taifa zima la Tanzania.

Hoja yetu ni kwamba kile kiliachoanzisha uzi huu na kukieleza kama ' utatu'' kinaelezwa kisheria na Wanasheria.

Ni kwa msingi huo tunasisitiza Katiba Mpya lazima itanguliwe na majibu ya maswali muhimu kuhusu Muungano.

Wanaodai TUme Huru ya Uchaguzi kama ilivyokuwa Zanzibar na iliyoshindwa ni wendawazimu (insane).
Tume Huru ni Mtoto wa Katiba na haiwezi kurekebishwa bila kugusa Katiba.

Ni kwa kupitia hoja hizo mzozo kati ya CHADEMA na Wanaharakati wa Sauti ya Tanzania umechukua sura mpya baada ya M/Kiti wa Chadema kutoa kauli. Kauli zenye utata.

Chadema kama chama kinahitaji Wafuasi. CDM imeaniwa na Wananchi kubeba agenda ya Katiba Mpya.
CDM lazima inapaswa ikubali heshima iliyopewa na Wananchi kwa unyenyekevu si dharau, kiburi au jeuri

CDM inahitaji Wanaharakati katika shughuli zake kama vile Wanaharakati wanavyoihitaji CDM kuufikia Umma.

Wanaharakati hawana chama na hawana cha ''kupoteza'' kisiasa. Chadema ina mengi ya kupoteza.

Mjadala unaoendelea una wagawa Wanachama wa CDM, wengine wakiunga mkono Wanaharakati.

Hoja za Wanaounga mkono kutoka CDM , kwanza, viongozi kuogopa kumwambia Mwenyekiti wao Ukweli kwamba wajibu wake ni Kuunganisha umma wa Watanzania kama Chama Mbadala.

Pili, wanadai agenda za chama zimegeuzwa kuwa za kikundi cha Viongozi wanaomnyenyekea Mwenyekiti kama ilivyo CCM na zidumu fikra.

Na mwisho wanasema agenda ya CDM ni Katiba mpya, haya ya Tume ya uchaguzi ni 'maridhiano ya Mbowe na SSH' jambo linalowakera kwasababu Chama kilisema hakuna kwenda uchaguzi bila Katiba.

Mbowe kama kawaida anaonekana kubadili gia angani kwa utashi wake na si Wanachama

Kwa ufupi, Mwenyekiti Mbowe anapoteza imani ya Wananchi na Wanachama.

Kama tulivyosema huko nyuma, njia bora kwakwe ni kuachia ngazi.

Mwenyekiti hawezi tena kufikiri au kutenda kwasababu maridhiano yame 'compromise his credibility and integrity' .

Chairman Mbowe is a Liability, no longer an asset, he must go ! if Chadema is to weather the public backlashl
 
KWANINI HAKUNA KERO YA KUCHANGIA MUUNGANO?
UBORA NJE YA MUUNGANO UKO WAPI KWA HAYA YA SIMBA NA YANGA!


Kila zinapotajwa kero za Muungano si kwa pande mbili bali upande mmoja wa Zanzibar ikilalamika jambo fulani.
Kwenye mikutano au mahojiano ya viongozi wa Zanzibar hoja kubwa ni kuonewa katika Muungano

Kero au kuonewa ni pale Wazanzibar wanahitaji jambo katika muungano. Kwa mfano, utawasikia wakitaka ajira za Muungano, wakitaka malipo ya BoT, Wakitaka ruzuku na kupewa fursa zote zinazopatikana Tanganyika.

Kero au 'uonevu' ambao kamwe hutawasikia Wazanzibar wakitamka ni endapo '' Wanachangia zaidi katika Muungano''. Htawasikia wakizungumzia mgawanyo wa kuchangia gharama za Muungano

Kero au uonevu ambao kamwe hutawasikia wakiusema ni namna ya kuendesha Taasisi za Muungano
Kero au uonevu ambao kamwe hutawasikia ni kuondoa mambo yenye gharama kutoka katika Muungano.

Katika 'mitandao' ya Wazanzibar ya kwao pekee kunajengeka hoja kwamba ' Watanganyika' wadai nchi yao ili Muungano uvunjike kila mtu kivyake halafu itafutwe namna ya kuwa na Muungano baada ya nchi hizi mbili kuwa na katiba zao. Hoja hii inayoenezwa na Wazanzibar haina elimu na ni ya kipuuzi.

Wazanzibar wanasahau kuna sababu kwanini kero au uonevu tulio ainisha kwa uchache hapo juu hawasusemi.

Nje ya Muungano hakutakuwa na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwasababu;
1. Tanganyika watajiuliza ni kipi wanachofadika nacho kwa kuungana na Zanzibar
2. Kuna sababu gani za kuungana na Zanzibar nje ya EAC, SADC n.k. ikiwa Jiografia inaipendelea Tanganyika.

Maswali hayo mawili yanaeleza umuhimu wa kuwa na kura ya maoni kwa Wazanzibar wakitafuta hatma ya nchi yao
Lakini pia maswali hayo mawili kwa sasa yanahitaji majibu kwa Watanganyika.

Na hapa tunapata hoja nyingine kuhusu Muungano, kwamba, lawama inayotupiwa Tanganyika hazina mantiki.

Mfano, kuna viongozi wawili waandishi wa habari walipiga sana kelele Zanzibar ijitoe katika Ligi ya Soka ya Tanzania.
Hoja ya Waandishi hawa mmoja ni kwamba nje ya Muungano Zanzibar itasonga mbele kwa soka na kwamba Tanganyika ndicho kikwazo chao katika maendeleo ya soka.

Zamani tuliziona club za Zanzibar kama KMKM, Miembeni, Small Simba , Jamhuri, Kikwajuni n.k zilizoshiri ligi kuu ya Tanzania zikipata nafasi za kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Kimataifa hususan barani Afrika.
Ushindani wa Ligi kuu ulizijenga club za Zanzibar katika viwango vya Juu sawa na vile vya Tanganyika.

Tangu Zanzibar ijitoe Ligi ya Muungano, hakuna athari yoyote kwa Ligi ya Tanganyika.
Ligi imeimarika kwa ubora ikifuatiliwa Africa. Ubora wa Ligi kuu umeziwezesha Club mbili kuingia katika mashindano makuba ya Soka Africa. Jana , orodha ya makundi imetoka Tanzania ikiwakilishwa na Timu mbili, Yanga na Simba.

Hayo yakijiri Ligi kuu ya Zanzibar imekuwa ya hovyo kwa mujibu wa FIFA na sasa haisikiki tena na wala hakuna vijana wanaojua Zanzibar kuna Timu gani za Mpira. Yale ya KMKM, Kikwajuni, Miembeni yamebaki katika makavazi.

Jambo hili linatupa uthibitisho wa mambo mawili, kwamba, kelele za kuituhumu Tanganyika kama kikwazo kwa Zanzibar hazina elimu na za kupuuza. Pili, kwamba, Tanganyika haiathiriki na chochote nje ya Muungano.
 
UTATA WA MUUNGANO HADI MIKATABA YA BANDARI
ZANZIBAR INAHUSIKA VIPI NA YASIYO YA MUUNGANO?


Rejea
View: https://youtu.be/F0gomkVedMg?t=1561

Wazanzibar ni wepesi wa kulalamika masilahi yao yanapoguswa, lakini ni wepesi wa kuhemea masilahi ya Tanganyika. Kwa muda mrefu na katika uzi huu tumeeleza wazi kile kinachoitwa kero za Muungano

Hoja yetu ipo wazi, kwamba, yale yasiyo ya Muungano Wazanzibar waachwe , wasishirikishwe ili wasilalamike.

Moja ya mambo waliyosema si ya muungano na yalikuwa katika hati ya Muungano ni Bandari.

Kwa kudhani kwamba Tanganyika inanufaika na bandari za Zanzibar na kwa fikra zisizo na elimu kwamba Bandari za Zanzibar zinaitoshelez, Zanzibar iliondoa Bandari kama suala la Muungano.

Bila mashauriano na mshirika Tanganyika, Zanzibar ikaondoa, mwenedelezo wa jeuri ndani ya Muungano.

Karibuni kuna mzozo wa ubinafsishaji wa Bandari ya Dar es Salaam na DP World kwa mapunufu ya mkataba ya kisheria na kiprotokali. Mathalan, mkataba unaohusu bandari za Tanganyika ulisainiwa na Waziri Mzanzibar kwa niaba ya Rais Mzanzibar akishirikiana na Katibu mkuu wa Wizara isiyo ya Muungano ambaye ni Mzanzibar

Wizara ya Ujenzi na uchukuzi (wakati huo) si suala la Muungano na haikupaswa kusimamiwa na Mzanzibar kwa mujibu wa Wazanzibar wenyewe kwasababu si suala la Muungano. Katibu mkuu wa Wizara isiyo ya Muungano ni Mzanzibar. Halikuwa sawa kwasababu nyingi, kwamba, malalamiko ya Wazanzibar wasishirikishwe mambo yasiyo ya Muungano HAYAKUZINGATIWA, lakini pia si kuwatendea haki Watanganyika !

Wazanzibar walsema suala la DP World halihusu Bandari za, hivyo kule visiwani na Bungeni.

Kwa maneno mengine Bandari za Tanganyika haziwahusu na wamekana hilo kwa vinywa vyao.

Wazanzibar wamesani mkataba wa Bandari zao na kampuni ya Ufaransa, tunasoma magazetini.
Hakuna kiongozi yoyote wa JMT au Tanganyika aliyekwenda kushuhudia utiaji saini mikataba hiyo.

Tazama video hapo juu. Katika viongozi waliohudhuria hafla ya kutia saini kile kinachoitwa mikataba ya Bandari za Tanganyika ni Rais wa Zanzibar H. Mwinyi , Makamu wa Pili SMZ H.A. Suleiman. Spika wa Baraza la Wawakilishi Bw. Zuber Maulid

Hivi viongozi hawa wa Zanzibar wamehudhuria mikataba inayohusu Tanganyika kwasababu gani?
Si hawa Wazanzibar waliosema na kutenga bandari zao kwa hoja ya kwamba si jambo la Muungano!

Kuna sababu kwanini Rais wa SMZ, Makamu wake wa Pili na Spika wamehudhuria jambo lisilo la Muungano

1. Dakika ya 14.54 katika video, Rais SSH anawashukuru Watanzania wote.
Hapa si Tanganyika au Tanzania bara kama wanvyosema bali Watanzaia wote wakiwemo Wazanzibar.

2. Dakika 17.22 Rais SSH anawashukuru wote waliofanikisha majadiliano kati ya Serikali ya JMT na DP World.
Rais SSH analihalalisha jambo hili kuwa la JMT ambayo Zanzibar ipo si la Tanganyika tena

3. Halafu anamshukuru Waziri Mbarawa kwa kufanikisha majadiliano.
Hapa anaonyesha Wazanzibar wameshiriki katika majadiliano ya Bandari za JMT si Tanganyika

Hivyo, baada ya Rais SSH kuwaruhusu Wazanzibar waondoe Bandari zao na waingine mikataba yao, Wazanzibar hao hao wasiotaka mambo ya Muungano kama Bandari wanaingia kwa mlango wa JMT.

Kwamba chochote kinachotokana na Bandari za Tanganyika ni cha JMT na Zanzibar ina haki
Hivi ndivyo Zanzibar impewa nafasi ya kufuja na ku 'abuse' Muungano ikiwa na impunity.

Hoja ya kwamba mambo yasiyo ya Muungano na ya Muungano ni ya KINAFIKI.
Wazanzibar hawana sababu za kukataa jambo kwamba si la muungano halafu wanashiriki jambo hilo kwenye masilahi ya Tanganyika.

''Nguruwe haiwezi kuwa haramu lakini mchuzi wake ni halali''

Kwa Watanganyika, hoja kubwa ni kudai Wazanzibar wapewe haki ya KURA YA MAONI ikiwa wanataka Muungano au la ilia kumaliza mzozo na unafiki kwa Wazanzibar.

Pili, ikiwa wanataka basi yaanishwe mambo kama ilivyo rasimu ya Warioba.

Lakini pia Watanganyika wanataka kuona mchango wa Zanzibar katika muungano ( assets) na wasiwe mzigo kwa Tanganyika (liability) kama ilivyo sasa hivi, kwamba wao ni kuvuna tu
 
Waziri hakueleza 21% katika watu milioni 1.5 inapatikana kwa hesabu gani dhidi ya 79% kwa watu milioni 60
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema juu ya suala la idadi ya watu katika Muungano.

Kwa maelezo yasiyo rasmi alisema,

"Tanganyika na Zanzibar zilipoungana, ziliungana kama nchi mbili kamili. Katika Muungano huo hakukuwa na suala ukubwa wa ardhi ama wingi wa idadi ya watu. Pale ziliungana nchi kamili zilizosawa." Mwisho wa maelezo.

Kwa hiyo, kama katika makubaliano ya Muungano ilisemwa 21% ikamilike. Hakuna namna lazima ikamilike. Vinginevyo, uandaliwe utaratibu wa kupunguza kiwango hicho cha asilimia.

Kwa hiyo, tukijadili suala la Muungano tujadili Muungano wa nchi mbili zilizo sawa. Sasa ili kupunguza manung'uniko...ni suala la Wazanzibari kuisikiliza kero za watanzania wanaoishi Tanzania bara na kuzitafutia ufumbuzi. Vile vile na Watanzania bara kuisikiliza kero za Watanzania wanaoishi Tanzania Visiwani/ Tanzania Zanzibar na kuzitafutia ufumbuzi.

Na usikilizaji huu wa kero kwa pande mbili ufanywe objectively bila mihemuko.

Binafsi, Sipendi Muungano uvunjike, lakini nitafurahi zaidi tukiungana na kuwa na nchi Moja na serikali moja.
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema juu ya suala la idadi ya watu katika Muungano.

Kwa maelezo yasiyo rasmi alisema,

"Tanganyika na Zanzibar zilipoungana, ziliungana kama nchi mbili kamili. Katika Muungano huo hakukuwa na suala ukubwa wa ardhi ama wingi wa idadi ya watu. Pale ziliungana nchi kamili zilizosawa." Mwisho wa maelezo.

Kwa hiyo, kama katika makubaliano ya Muungano ilisemwa 21% ikamilike. Hakuna namna lazima ikamilike. Vinginevyo, uandaliwe utaratibu wa kupunguza kiwango hicho cha asilimia.

Kwa hiyo, tukijadili suala la Muungano tujadili Muungano wa nchi mbili zilizo sawa. Sasa ili kupunguza manung'uniko...ni suala la Wazanzibari kuisikiliza kero za watanzania wanaoishi Tanzania bara na kuzitafutia ufumbuzi. Vile vile na Watanzania bara kuisikiliza kero za Watanzania wanaoishi Tanzania Visiwani/ Tanzania Zanzibar na kuzitafutia ufumbuzi.

Na usikilizaji huu wa kero kwa pande mbili ufanywe objectively bila mihemuko.

Binafsi, Sipendi Muungano uvunjike, lakini nitafurahi zaidi tukiungana na kuwa na nchi Moja na serikali moja.
Nakubaliana nawe kwamba hayo ni maneno ya Mwalim Nyerere lakini maneno yake yanachukuliwa ''out of context'

Mwalimu alimaanisha zilizoungana ni nchi mbili huru ''sovereign states' bila kujali ukubwa wa eneo au idadi ya watu. Hapa key word ni ''sovereign ''. Kuna vi nchi vidogo kuliko Zanzibar vyenye watu 120,000 lakini ile 'sovereignty ' inavipa haki sawa katika UN kwa kura moja sawa na China USA, , India na Urusi.

pamoja na kiti kimoja UN, bado idadi ya watu ina determine baadhi ya mambo. Mfano, US inachangia zaidi ya Vanuata , Fiji au Tonga.

Ninachosema hapa Mwalimu alikuwa sahihi in the context of sovereignty.

Pili, makubaliano ya Muungano hakuna sehemu inayosema ajira za Muungano zitagawanywa vipi.
Hakuna ! Kwasababu sisi ni nchi moja Raia wana haki ya ajira kwa mujibu wa Mwalimu.

Tatizo limeanza Wazanzibar walipodai wanahitaji ''mgao rasmi' wa ajira za Muungano, yakazua haya
1. Ajira za Muungano ni zipi? ni zile za mambo ya mkataba wa Muungano au zile za nyongeza?
2. Ni mgao upi unaotumia na kwa formula gani ?

Ukisema ni zile mkataba formula inayotumika ni ya mambo 11 tu.
Ukisema ni zile za JMT formula inayotumika ni ya kila jambo la Tanganyika na Muungano.

Kumbuka hakukuwepo formula hiyo wakati wa Nyerere, Mwinyi, Mkapa. Haya yamezuka wakati wa Kikwete kwasababu aliendekeza kuwapendeza badala ya kutafuta suluhu. SSH kupitia Mchengerwa kapigilia Msumari kabisa na kuongeza kila kitu hadi formula ya mikopo ingawa hakuna formula ya kulipa

Ghafla tukasikia Wazanzibar wanapewa 21% ya ajira za Muungano bila kufafanua ni zipi.
Kikubwa zaidi hapa ni kwamba hiyo 21% imepatikana kwa formula gani?

Hakuna document yoyote inayoonyesha uwepo wa hiyo 21% kabla ya mwaka 2005-hadi leo.

Swali linalozuka katika hiyo 21% wanayopewa Wazanzibar ni je wanalipa mishahara ?
Ukweli usio na shaka ni kwamba 21% inalipiwa mishahara na Tanganyika siyo SMZ

Watanganyika wanahoji tena kwa nguvu sana. Inakuwaje kuna formula za kugawana yale mazuri kama mgao wa BoT na Ajira za Muungano lakini hakuna formula ya kuchangia Muungano, hakuna formula ya kulipia madeni ya nje.

Tukubaliane kwa hoja yako kwamba ni nchi mbili sawa na hivyo zina usawa.
Nikuulize ikiwa kuna mgao wa ajira 21% , je Zanzibar inalipa Wafanyakazi hao?
kama hakuna formula, kipi inahalalisha hilo.

Labda utujibu akina Makame Mbarawa na Katibu mkuu wake na Wazanzibar lukuki waliojaa Tamisemi kama akina Shaka, wizara ya elimu, Wizara ya utalii, Maliasili, mifugo, madini n.k. wanaingia huko kwa formula gani?

Unapodai '' fair and equitable'' inahusu kila jambo si kuchagua pale penye mafao halafu mzigo unabebwa na Watanganyika. Ukidai haki lazima uwajibike, Zanzibar ni wazuri sana wa kudai tu hatuoni mchango wao.

Mwisho umesema unapenda Muungani uendelee, hebu mshawishi Mtanganyika wa kawaida tu kule Sumbawanga, Msoma, Tunduru, Singida n.k. kwamba anahitaji Muungano!
 
Pili, makubaliano ya Muungano hakuna sehemu inayosema ajira za Muungano zitagawanywa vipi.
Hiki kipengele kimenistua sana!!

Kumbuka hakukuwepo formula hiyo wakati wa Nyerere, Mwinyi, Mkapa. Haya yamezuka wakati wa Kikwete kwasababu aliendekeza kuwapendeza badala ya kutafuta suluhu. SSH kupitia Mchengerwa kapigilia Msumari kabisa na kuongeza kila kitu hadi formula ya mikopo ingawa hakuna formula ya kulipa
Kweli Kuna tatizo Mahali!!! Elimu uliyoitoa hapa. Inatakiwa iwafikie wengi ili tuwe kwenye ukurasa mmoja wakati wa mjadala.


Mwisho umesema unapenda Muungani uendelee, hebu mshawishi Mtanganyika wa kawaida tu kule Sumbawanga, Msoma, Tunduru, Singida n.k. kwamba anahitaji Muungano!
Ni kweli naunga Mkono Muungano uendelee kwa mazingira Yale niliyoeleza. Nchi moja, serikali moja kwa maana hiyo, tutakuwa na uraia wa aina moja hakutakuwa urai wa ukaazi bali raia wa Tanzania.

Ni kwa nchi moja, serikali moja migogoro yote hii ya changamoto za Wazanzibari na changamoto za watanzania waishio Tanzania bara itakwisha.
 
Back
Top Bottom