Duru za biashara za mtandao: Kuna dalili za watu kulizwa huko kwenye soko la forex, wajuzi wa haya masuala njooni huku

Hivi bado hamjui tu kwamba hakuna hela rahisi, hela lazima uparangane kuipata....Sasa vijana mnataka hela za kudownload tu..
Forex is not easy, is not for everyone 😆
 
Mkuu wangu Sina lakusema kuhusu forex kama ni kamali au laa?. Lakini nachojiuliza kwa nini serikali haimchukulii hatua, kama namna inavyochukulia matapeli wengine?. Kama anaiba na bado sheria za nchi hazimtii hatiani basi Mimi nampongeza.
 
Nimecheka hapo kwenye meseji za malalamiko kuna jamaa mmoja eti anasema ''wasipokuwa serious watapoteza wateja sana'' Wawe serious nmana gani tena na u-serious wao ni kula vichwa vya watu? Ukiona umeliwa kichwa ujue wako serious!
 
Sirjeff ni tapeli mmoja very smart, yaani ni yapeli wa level ya kimataifa.Mimi nilishatrade na 360capital nikakumbana na ishu ya slippage... nilimfuata dm instagram akasema linashughulikiwa soon ila ikawa sio. Hii ishu ya slippage pekee inampa uhakika wa kuunguza accounts za traders wadogo hivyo yeye kupata faida kwa kuongeza freequncy ya deposits. Narudia tena Sirjef Denis ni tapeli atakae na asikie.
 
Kwa nini Serikali haimchukulii hatua?.
 
Muda si mrefu wata deactivate accnt zao za kwenye mitandao yote hiyo itakua kama ndo ishara ya kwaheri ya kuonana
Mm nilishawahi kujiunga na haya mambo ya sarafu za kimtandao nikapiga hela ndefu kidogo kwa level ya uchumi wangu Hadi leo huwa sitaki kukumbuka kabisa na wala sijawahi kumsimulia mtu yoyote niliona ndo itakua njia sahihi ya kusahau
 
Hii slippage unaigunduaje?
 
Forex haina shida kabisa ukiijua... Ila waswahili kama hao akina Jeff ndio wanafanya mambo yanakuwa magumu...

Mimi binafsi nilishaapa sitakaa nifanye biashara na Broker ambaye hana review ya kueleweka kwenye site ya Forex Peace Army (FPA)



Nipo zangu na Fusion market mambo ni mserereko....

Shida ya wabongo ni wapenda vitonga sana.
 
Ngoja wapigwe kwa kuwa vichwa vyao vimejaa makamasi maana forex ni biashara huria isiyo kuwa tied kabisa na huyo tapeli wa ONTARIO kwann watu wanaendelea kumfata kwa viproject vyake uchwara??
Imagine... yaani mazwazwa wengi kweli
 
Mkuu unafanya vibaya kumtetea huyu jamaa. Pesa siyo rahisi kutoka ndio maana majambazi wanatumia vitu vya ziada kama shaba. Sasa huyu anakutoa hela bila hata kukunyooshea mtutu yani dume zima tena una familiar unatoa hela hivihivi na kumkabidhi dume lingine. Inauma Aisee.

Na kinachouma zaid watu hawasikii na hawajifunzi bado tu wanaingizwa mkenge.

Fak!
 
Mkuu simtetei Jamaa lakini pia nashangaa kama anatapeli watu vyombo vya dola kutomchukulia hatua stahiki, au anashirikiana na wakubwa?.
 
Wonzur huko mwanza na shinyanga pia imeliza Watu....Watu waumizwa ni hatari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…