Duru za biashara za mtandao: Kuna dalili za watu kulizwa huko kwenye soko la forex, wajuzi wa haya masuala njooni huku

Anarudi kivingine kufungua local broker yake bila partnership, ila broker wa wanyonge ni templer tu hizi brokerage za SA ni wapigaji hatari, watu wanataka kutrade kwa kuishi maisha yao ila sasa unakuta mtu anajilipua kana kwamba anataka kustaafu mwezi ujao,mwishowe anaunguza acc, hakuna kitu kigumu kama human behavior ktk trade yani upambane na normal behavior zako uweke za soko linavyo hitaji ni mziki ambao wengi wanafeli, jifunzeni forex taratibu ikikushinda achana nayo ila usiwaonee wivu madogo wanaotoboa, jua wamepambana sana tu,
 
Shida kubwa ya Sirjeff ni "egoism" kwanini uwabebe watanzania vichwa uji kwenye biashara ambayo 95% ya wawekezaji hupoteza mitaji yao ndani ya wiki 4 tu! Kwanini asifanye peke yake? Ujinga wa kuvuna commission za broker kwamba kila kichwa utakachokileta kwangu nakupa dola 100.. miaka yote kwenye fx Ontario hawezi kubaini broker wabovu??!

Kanuni kubwa ya forex: wapo watu tunawafahamu wanapiga hadi milioni 40 tsh kwa mwezi ila huwezi kuwaona kwenye social media, wale tu ambao biashara imewashinda ndio hao wamekuwa wauza signal, mawakala wa kuvuta watu kwenye magroup na kuwauza kwa unregistered brokers, nk
Soko la pesa lipo na watu wanawekeza, ila hakuna SHORT CUT...
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Hakuna broker nimewahi kumtumia na akawa solution ya changamoto zote sokoni kama Just forex wakuu.

Kwanza deposits zinafanyika ndani ya dakika chache hata kwa Mobile wallets bila kutumia wakala, na unaweza kuwithdraw ndani ya muda mchache pia.

 
Mkuu, hakuna siku ambayo umemchambua vzuri huyu bwana mdogo kama katika bandiko hli, binafsi nikiri kuwa huyu dogo nilianza kumfuatilia toka enz hzo akija na story zake za matrekta hapa jf, na mpaka huko instagram.

Ambacho nilichomgundua nikwamba kwanza anamajigambo ya kishamba sana, then ni TAPELI ambaye mamlaka zinamlea mpaka leo hii..,, huyu alipaswa kuwa Jela hadi tunavyozungumza sasa.

Mimi huwa ninawaambia vijana forex sio lelemama, forex inahitaji ujifunze haswa na uwesmart sana manake in forex you compete with expert on financial market, people who are skilled at every aspect on finacial market, ujinga wa jeff na masomo yake uchwara ya forex can' t make you to be a successfull trader, vijana wakawa hawaelewi wakamfanya bwana mdogo kama ndio Massihi wao katika ukombozi wa kiuchumi kumbe ni mwizi ambaye anaendelea kuwanyonya.

Vijana wengi hawaijui internet vzuri wengi, wanaitumia internet katika social medias., ila internet ni weupe kabisa, ndio maana wanaingia kichwakichwa, wanapigwa katika stubid scheams kama vile ponzi scheam, cryptocurrencies, stock market na hata forex.

Financial market sio elimu ya siku moja au mbili ukawa gwiji sokoni serious financial marketers wameinvest muda mwingi usiopungua miaka mitano na pesa ya kutosha, ndio maana duniani smart traders wapowachache sana na huwezi kuwakuta mitaani huwa wameajiriwa na taasisi kubwa kubwa kufanya hyo kazi.

Vijana mjifunze, narudia tena forex sio lelemama, inahitaji utulivu jifunzeni kwa watu sahihi na tumieni internet vzuri na mnunue vitabu vpo huko amazon vitabu bei zake zinafika mpaka dola 50, hvyo vitabu vya bure mnavyopewa vina maarifa madogo sana na haviwezi kukufanya kuwa smart traders.
 
Ni kweli kuna watu wanapiga hela za forex ila hutakaa kuwaona mtandaoni wakijitangaza kwasababu kwenye fursa hatualikani.

Ukiona "fursa" inatangazwa sana kuwa makini maana huchelewi kuingizwa mjini.

"Forex" na "Kijiji cha Vanilla" zitawanyoosha wabongo wanaopenda short cuts.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…