Ogah, post: 20312497, member: 121"] Tumefikaje huku?
Kukosa uvumilivu kwa pande zote, na kila mtu kusahau (kwa makusudi au kutokujua) majukumu yake kisheria.Ukosefu wa busara ili kutumia njia muafaka wa kutatua matatizo yaliyojitokeza
Tumefika huku kwasababu utamaduni wa kuvumiliana, kusikilizana na kuelezana ukweli umetoweka
Tumejenga utamaduni mpya kama ambavyo tuliona askari aliyemzuia Nape.
Ukisikiliza, askari alifika na kumwambia Nape arudi ndani ya gari.
Nape akauliza wapi kitambulisho chako?
Ni kweli mwananchi ana haki ya kuonyeshwa kitambulisho na Polisi hasa ''askari kanzu''
Ukitazama mavazi ya askari waliokuwepo, kuna tshirt zinazofanana na chama kimoja cha siasa
Nape kama mwananchi mwingine ana haki ya kuonyeshwa kitambulisho na mtu aliyemzuia
Badala ya kutoa kitambulisho askari akatoa bastola!! Yaani jibu la kitambulisho ni bastola
Askari alizuiwa na mwenzake wa vazi jekundu akimwambia'utaharibu mambo'
Ni baada ya askari wa bastola kuondoka, ndipo hali ikatulia
Unaweza kuona tulipofika, kwamba utamaduni wa kuongea kiswahili na kusikilizana umekwisha, sasa ni rungu , bastola, makonde ilimradi tu kauli za kiungwana na matendo sahihi zimekwisha
Ubabe haushii hapo upo hadi bungeni ambako kauli za kibabe ni sehemu ya uongozi
Bungeni ni mahali pa kuunganisha wananchi ili kuisukuma serikali kutimiza majukumu yake
Kwasasa lugha ya bunge hakuna, baada ya kauli mbili tatu utaona askari wakiingia na kuzoa waheshimiwa mzobe mzobe, ukitafuta mkasa , jibu ni ubabe ubabe tu. Lugha ya staraha hakuna
Kwa bahati mabya haionekani kama tuna mwongozo wa wazee au viongozi, tumepoteza !!!
Katika mazingira hayo, wananchi wamechanganyikiwa kwani wapo kipindi cha mpito.
Hawajui ima waache utamaduni wa kitanzania waliozoea na kukumbatia utamaduni wa kibabe, au waukane wa kibabe wakumbatie ule wa kitanzania. Wapo katika mtanziko mkubwa
Tunahitaji nini?Leadership ili kuweza kumaliza haya matatizo....Walau Waziri Mkuu (baada ya kujadiliana na wakubwa zake) asimame na kutoa muongozo....kwani matukio haya ni vizuri yakawa solved once and for all
Hatuna tatizo na leadership, wapo na wanaongoza .
Tuna tatizo na kupata matokeo ya leadership. Kazi ya kuongoza ni ngumu .
Inahitaji hekima na busara kuliko uwezo wa akili,hapo tuna ombwe, chanzo cha hali iliyopo
Kuna tafsiri kuwa kuongoza ni kutangulia na wajao wafuate kama shurti
Kuongoza ni kuratibu shughuli au maoni ya watu.
Na si kuratibu ili watu wakubaliane, lakini pia wakubaliane hata wasipokubaliana.
Kuwe na lugha stara, kuvumiliana, kuambizana ukweli, kusifiana, kukosoana na kupongezana
Ukiongoza watu milioni milioni 10, 25 au 45 usitegemee kuwa na mtazamo sawa.
Kama utataka hao mamilioni waende pamoja, lazima utumie mjeledi.
kwa binadamu mjeledi hauwezekani, ni viumbe wenye akili na fahamu
Kinachotakiwa ni kusikiliza, wale walioamua kwenda, na wanaopiga kona au kurudi nyuma
Ukielewa kwanini tofauti, ukatafuta njia ya uelekeo sahihi bila kujali wengi au wachache, utafanya kazi ya uratibu na ndiko kuongoza
Nilishangaa RC alipoingia katika mtafaruku na Bunge, bosi wake waziri mkuu alikuwa kimya ingawa naye ni mmoja wa watu wa mjengoni waliodhihakiwa.
Hili la Clouds nalo kakaa kimya. Pengine katenda kupitia mtu au kakaa kimya, hatujui! tunachojua kunq ombwe, Nape alijaribu njia ya haraka akisubiri ya muda mrefu, imemgharimu
Gharama aliyolipa Nape inaonekana ni yake, lakini tufikiri zaidi
Hivi nani atasimama ili naye alipe gharama kama Nape huko serikalini?
Makapuku nani atanena kwa niaba ikiwa midomo imefungwa kwa makufuli au gundi ya mbao?
Hatujui tunaelekea wapi, lakini moja tulilo na uhakika nalo, kuna tatizo tukae kitako kwanza
Tusemezane