Duru za Siasa: Awamu ya 5 - Uongozi na Yanayojiri

Duru za Siasa: Awamu ya 5 - Uongozi na Yanayojiri

Mkuu Nguruvi3

Sidhani kama wingi wa vyuo maana yake ni kuwa na vyuo visivyokidhi ubora. Unaweza kuwa na vyuo vingi na vyote vikakidhi ubora au unaweza kuwa na vyuo vichache lakini bado vikawa bogus vilevile.

Kuhusisha mambo haya mawili sidhani kama ni sahihi na kwa namna moja au nyingine ni upotoshwaji.
Mkuu upo sahihi, experience inaonyesha tulipokuwa na vyuo vichache ubora ulitiliwa maanani kuliko wingi.

Tangu tumeanza vyuo holela suala si ubora bali kufaulisha wanafunzi katika viwango vya chini
Chuo kinafundishwa na wahitimu wa degree ya kwanza. Hii si UPE nyingine kweli

Ukisoma vizuri hatukusema tuwe na vyuo vichache, tulichosema ni kuwa ni afadhali kuwa na vichache bora hata kama idadi itapungua kuliko kuwa na utitiri usiokidhi haja.

Hivyo jitihada za kuchuja vibovu ni nzuri hata kama tutabaki na viwili bora
Lakini pia milango haijafungwa kwa vile vtakavyomudu ushindani na kuonyesha Ubora

Pili, hatuna sababu za kuwa na chuo kikuu tunapoweza kufanya ''college' bila kuathiri idadi ya wanafunzi. Tuna maana kuwa ubora wa vyuo hutegemea uzoefu wake pia

Mkuu labda nikuulize, chuo kikuu Singida kinatoa wahitimu gani na future ya wahitimu hao ipo wapi? Bukoba University na Songea University nani anavitambua nchini na katika dunia hii?

Hivi navyo vinahitaji wanafunzi wa HESLB kwasababu tu kuna pesa, kinyume chake vinakufa
Kwanini wanafunzi walazimishwe kwenda kusoma 'highschool' halafu wapewe shahada za Chuo?

Hatua ya serikali kuhakikisha vina survive kwa ubora na si pesa za HESLB ni ya kupongezwa
Ni katika mambo mazuri sana wizara imeyaona.
 
Mkuu Mwalimu hili utaweza kunisaidia kuelewa

Siku za nyuma kulikuwa na JAB(Joint admission Board) ambayo iliweza kubaini mwanafunzi aliyeomba vyuo viwili au zaidi kwa wakati mmoja. Kwa maendeleo ya tech hili lisingekuwa tatizo licha ya idadi kubwa

Kwasasa TCU ndiyo imechukua jukumu la kupanga wanafunzi waende wapi. Kwanini?

Je, hapa hakuna 'ushirika' na wenye vyuo duni kupata wanafunzi?

Pili, kuna sababu gani za kuwa na SUA halafu ianzishwe Butiama Univ.?

Kwa mtazamo wa kawaida Butiama ikianza na wanafunzi 3,000 ni ghali kuliko ku upgrade SUA ifanye accommodation ya idadi hiyo. Je, Butiama inaanzishwa kwa sababu zipi za kielimu?

Tatu, kwanini Hospitali zilizofanywa za 'rufaa' kama Bombo ambazo zina infrastructure za kuanzia zisiimaarishwe eneo la afya kwa maana allied Health science wajifunzie huko ili kutoa nafasi kwa Muhimbili kuchukua idadi kubwa?

Inawezekanaje kukawa na Mkwawa College, Duce na ishindikane ku upgrade Marangu na Kigurunyembe ambazo zina infrastructure nzuri ili kutoa Walimu kwa 'specialty'?

Na mwisho, hadhi ya chuo pekee na ubora wake ni sehemu muhimu sana ya mafanikio ya wanafunzi
UDSM ina students exchange pamoja na walimu wao na vyuo vingi duniani.

Future ya wanafunzi ni pana kwasababu chuo tayari kina jina ndani na nje

Ndivyo ilivyokuwa kwa Mzumbe institute wakati huo ikitoa wanafunzi bora na kuwa na soko
Mabadiliko ya kukimbilia Univ yameathiri sana 'ubora' na kuwapa tabu wahitimu kwa siku za baadaye

Kwa msingi huo nakubaliana kabisa na serikali katika hatua za kuacha 'soko' liamue nani atoweke.

Hawa akina Songea n.k. muda si mrefu watatoweka, hawatakuwa na mapato.
Ilikuwa 'business' kwasababu ya ubora hovyo(wala siyo duni)

Wanaochechemea kama Mzumbe na MUHAS watabaki katika wakati mgumu labda kama wafanye mabadiliko ya kwenda na wakati hasa ubora katika research na 'product'

Kuna mahali nimesoma 'Kubira Univ. of Bukoba Univ. of Tumaini Univ. Makumira'' !!!
 
Mh WAZIRI NDALICHAKO
Umegusa 'watu' usirudi nyuma

Mh Waziri na serikali, kwa kugusa suala la TCU utakuwa umegusa maeneo 'nyeti' kwa baadhi
TCU kulazamisha wanafunzi kwenda vyuo fulani halikuwa jambo la bahati mbaya

Tangazo la kuruhusu wanafunzi kujiunga na vyuo wanavyotaka, ikiwa ni pamoja na kuimarisha vyuo vya Umma kama UDSM si jambo litakalofurahiwa na kila mtu

Tukisimamia ukweli, jitihada za ubora wa elimu pamoja na udahili ni za kuungwa mkono

Kwa miaka kadhaa elimu imedorora ngazi zote kiasi cha kufikiri kusomesha nje ya nchi

Ongezeko la vyuo halijakidhi ubora na kama tulivyosema, ongezeko hilo lina sehemu mbili

Kwanza, lilifanywa kisiasa. Tatizo lilianza na awamu ya 4 ambayo wizara ya elimu ilikuwa eneo la ''madudu'' kila uchao. Kubadilisha mitaala na vigezo vya mitihani ni baadhi tu ya ''madudu'' hayo

Kushusha viwango vya ufaulu ililenga haja ya kisiasa kwamba ongezeko la shule za sekondari na za msingi limewezesha wanafunzi wengi kujiunga na vyuo. Hakukuwa na maandalizi

Kilichofuata ni kutoa vibali kwa watu wenye majengo na mabango makubwa 'University'

Wanasiasa wakikimbilia majukwaani kutambia idadi ya vyuo kufikia 50 bila kujali ubora

Pili, wafanyabiashara wakaitumia fursa kufanya biashara ya elimu badala ya huduma
Elimu ni huduma inayoweza kufanywa kibiashara lakini kwanza iwe ni huduma halafu biashara

Hapo ndipo TCU nayo ikaendeshwa kisiasa ili kuakisi matakwa ya wanasiasa na si kitaalamu

Madudu anayohangaika nayo Waziri ni zao la utapeli wa kisiasa kwa kutumia ilani na watu wa CCM ambao leo wakiangalia nyuma wanaona mauza uza. Hilo tuwaambie,walikuwa kimya

Mh Waziri asitegemee hatua anazochukua zitapita bila upinzani.
Upinzani si wa kisiasa, ni wa wenye masilahi ya kibiashara ambayo sasa yanatishiwa

Kukata pesa za HESLB ni tangazo la 'kifo' la vyuo duni vya biashara tu

Vyovyote iwavyo, ubora wa elimu ni kitu muhimu kuliko wingi duni.

Vyuo duni vife kifo cha asili si kubebwa kwa pesa za umma vikizalisha wataalam duni

Tusemezane
 
MAANDAMANO YA WASANII

Sehemu ya I

-Kwanini viongozi wanarudia makosa yale yale kwa muda mfupi?
-Wasanii wanatambua nini wanapigania au wanatumika bila kujijua?
-Nini wanatakiwa kufanya

Wasanii Bongomovie wameandamana wakiunga mkono tangazo la RC aliyekataza usambazaji wa filamu kutoka nje. Hili ni kutaka mauzo ya filamu za ndani yaongezeke

Maandamano yanaonekana kuwa na baraka za serikali kinyume na tangazo la katazo la mikusanyiko

Kuna maoni kuhusu hili, wengi wakiliona kama marufuku isiyo na ulazima
Wanasema endapo ni hivyo marufuku zingeenezwa a kila mahali , jambo ambalo ni gumu kiuhalisia

Ujumbe waliotaka ni kuwa athari za vitu vya nje hazipo katika filamu tu bali maeneo yote

Kwa undani, suala ni kubwa kuliko kauli ya mtu.
Kuna mengi yaliyo nyuma yake tunayotakiwa kuyajadili kuelewa mantiki. Hayo ndiyo tutajadili hapa

TANGAZO LA RC

Serikali imegawanyika katika level kuanzia serikali za mitaa, vijiji, miji, manispaa , Majiji na serikali kuu. Kila ngazi ina ukomo ili kudhibiti mwingiliano wa majukumu 'overlap'

Ngazi za chini ya serikali kuu zina mamlaka kwa maeneo husika tu bila kuathiri maeneo mengine

Taasisi na vyama au club nazo zinafuata mfumo huo kwa ngazi zote kwa maana ile ile

Pamoja na mgawanyo, yapo yanayogusa Taifa na hushughulikiwa katika ngazi hiyo
Kuna wizara zenye viongozi wakiwemo makatibu wakuu na mawaziri kwa mambo ya kitaifa

Lipo tatizo la viongozi kutoelewa wigo wa mamlaka na bila kulitazama taifa kwa ujumla wake.
Hili limezua malalamiko na maamuzi yanayoonekana kuvuka mipaka

Dalili za awali za tatizo ni RC alipotoa tangazo la kupambana na madawa ya kulevya

Madawa ya kulevya ni tatizo la Taifa si la eneo fulani kama kipindu pindu au kuhara

Vipi kauli ya mkuu wa mkoa mmoja ingeweza kupambana na madawa mikoa yote?

Kauli hiyo ilitolewa na RC bila kujali ni kiongozi wa mkoa na si nchi na tatizo ni la nchi

Kwa kuelewa, serikali ikaingilia kati ikimshirikisha waziri mkuu na mkuu wa kitengo cha kuzuia madawa. Ilichofanya ni kusahihisha makosa ya RC aliyetaka kupambana na madawa kwa mkoa mmoja tu au aliyedhani tangazo lake ni la kitaifa

Inaendelea
 
Sehemu ya II
WASANII

Kosa la madawa ya kuelevya limejirudia kwa tangazo la bongomovie.

Sanaa ni suala la Kitaifa na mwenye dhamana nalo ni Baraza la sanaa na Waziri husika.

Walipokamatwa wasanii ilikuwa ni serikali hata wasanii kwa lugha ya 'wao na serikali'

Filamu za nje zinaweza kuingizwa kutokea Mbeya, Mwanza, K'njaro, Mara n.k.
Tangazo la kuzuia kwa mkoa wa Dar es Salaam halina mantiki wala maana

Unawezaje kuzuia filamu zisiuzwe Dar bila kufikiri zinauzwa Mkuranga, Kibaha AU Tanga?

Kauli ya RC ni ya mkoa wa Dar si ya kitaifa unless RC awe na mamlaka ambayo kikatiba hayajaanishwa kwa wadhifa wa 'RC wa Dar' kuwa na mamlaka kwingine

Katika nchi kama TZ yenye mipaka na mataifa 8, kauli haina lengo lolote la kusaidia wasanii

Kosa la madawa ni sawa na la kufanya kazi za Wizara na Basata
Kwanini watu hawajifunzi kutokana na makosa tena mengine yakiwa na miezi 2?

JE, KUNA SABABU?

Wiki mbili zilizopita kumekuwa na sintofahamu kati ya wasanii na mamlaka za serikali
Hilo limetishia uswahiba wao, kwa sehemu kubwa wasanii ni sehemu ya CCM/Serikali

Tumeona jitihada ikiwemo mialiko kama ule wa ufunguzi wa Hosteli

Kuna shaka tangazo limetoka kuwaridhisha wasanii wahisi wanathaminiwa na serikali

Endapo si hivyo, kwanini tangazo ''la kitaifa'' lifanywe kwa kundi moja na kwa baraka?
Je, kauli ya RC ililenga mkoa au ni kauli ya kitaifa?

Mamlaka yameanishwa wapi na sheria gani?Na wasanii wangenufaikaje mikoani ikiwa ni la Dar?

Kwa namna wasanii 'wametumika' pengine bila kujijua na kutojua sababu zinazoathiri tasani yao.

Hili nalo tunalijadili sehemu inayofuata

Inaendelea
 
Sehemu ya II

WASANII

Bongomovie wanaamini kuzuiwa filamu kutaongeza mapato kwa mauzo ya ndani
Kuna sababu za kuamini uwezo wao katika kupambanua ni wa kiwango duni

Ni duni kwasababu haionekani kama wametafakari au wamefanya utafiti wa wa tatizo

Dunia ya Tz ya leo si ya RTD, Uhuru, Mzalendo au muziki wa dansi.
Ni dunia ya soko huria. Hakuna sekta, tasnii au fani isiyoathirika. Hiyo ni kanuni ya asili

Tabia moja ya soko huria ni kuondoa ukiritimba, kuruhusu ushindani. Wenye nguvu husalimika

Ushindani una mengi ikiwemo ubora, soko, watumiaji au walaji n.k.

Wasdanii wangejiuliza kwanini Bongoflava inachanua katika soko kujali kanda za nje?

Kwanini Simba na Yanga zinasajili kutoka nje badala ya kung'ang'ana wa ndani?

Kwanini Nigeria na India zinauza filamu bongo tena kwa lugha za kigeni?

Wasanii wangejiuliza walaji wanataka nini bora filamu au ''filamu bora''

Maswali ni mengi na wangetafuta majibu sahihi kwanza, si majibu ya mkato yasiyo na maono

Kwa mantiki hiyo, wasanii hawaewi tatizo ambalo ni wao kwanza, hawaelewi dunia na mwelekeo ,chimbuko la matatizo hivyo kuwa 'vulnerable' kwa ''kutupiwa''bila kutafuta kiini cha matatizo yao

Tuwaeleza matatizo yao ni yapi, inaendelea....
 
Sehemu ya III

WASANII

Tatizo la wasanii ni uelewa na kuwaongoza waliofunguka(exposure)
Ni tofauti na Bongoflava, kwa kiasi uelewa wa wasanii na viongozi ni mpana kidogo

Tanzani imebadilika , enzi za kina mzee Kipara au smolo zimepitwa na wakati.
Watu wanataka kilicho bora kwa gharama, wapo tayari. Hayo ni mabadiliko yasiyoepukika

Filamu za bongo zina makosa mengi ya kifundi na na ubora hafifu usiouzika
Ubinafsi na kutokubali kushauriwa ni tatizo kubwa kuliko filamu za nje zinazoingia

Utengenezaji si rahisi, ni jambo la kuingia katika fikra za hadhira na kuishawishi ikubali kazi kwa thamani

Filamu hutengenezwa kwa kuanza na fikra, kuandika fikra, kuzitathmini, kuzifanyia marejeo , kuzipa uhalisia, kuangalia mazingira, kuangalia jamii na walaji n.k.

Fikra za filamu si za mapenzi au mambo ya kileo. Ukitazama filamu ya Kunta Kinte Kairaba, inaonyesha yaliyotokea miaka 100 iliyopita yenye hisia kali sana katika dunia ya leo

Script yake iliandikwa na watu wanojua historia, ikasimamiwa na mabingwa filamu
Utitiri wa wahusika ni mkubwa kila mmoja akiwa na wajibu

Kwa Bongo mtu anaamka na ku shoot bila kufanyia tathmini. Hakuna msanii anayewaza kufika idara au tasisi kwa ushauri, kuonana na manguli wa sanaa za filamu

Mtu mmoja, ni Director,Character, ni producer, ni mtu wa sound na kila kitu.
Unategemea kuna ubora gani katika hali kama hiyo? Ubinafsi tu wa kidogo na si bora

Filamu ikitengenezwa inatakiwa ifanyiwe review. Ni ngapi zinafanyiwa hivyo hapo Bongo?
Review ni critic na comment ili ikiingia sokoni imeiva. Hakuna hayo

Filamu zenu ni hafifu kwa ubora na ndilo tatizo ingawa tatizo halisi ni uelewa wenu

Mnatakiwa muangalie filamu za wenzenu, mjifunze kutoka kwao, mjifunze kutoka kwa wataalam na mushirikishe wataalam katika kazi zenu si kubeba kamera tu na kuachia movie

Kuthibitisha uduni wenu, mnataka mlindwe ili filamu ziuzwe mtendeni na Magomeni
Hamfikirii kuuza Kenya , Nigeria , India, Ulaya na kwingineko.

Ndiyo maana tamasha la Jahazi kule ZNZ haMna habari kwasababu mnategemea ulinzi sokoni

Sehemu ya mwisho inaendelea...
 
Sehemu ya IV

Bongmovie wasihadaike na hoja za wanasiasa wanaotaka kuwatumia baada ya 'wiki iliyopita'

Wasitafute kulindwa sokoni bali waingie sokoni kwa nguvu za ubora wa bidhaa

Wabadilike katika fikra, wakubali kukosolewa na waelewe vipaji vyao viambatane na mwongozo

Maadamano wanayofanya ni ya kupoteza muda tu, lazima wakae chini na kutafuta chanzo cha matatizo

Hakuna mwanasiasa anayeweza kuwasaidia, bali kuwatumia tu kisha kuwatekeleza

Tatizo la sanaa

Siyo Bongomovie tu, tatizo la sanaa limenea sehemu kubwa.

Wachekeshaji wanadhani ili mtu acheke lazima wapinde midomo.
Hawatambui kuwa unaweza kuongea kawaida na ukawa stand up comedian

Bongoflava wanadhani lazima 'biti' ziwe sawa na akina Rihana. Wanasahu Saida Karoli alivyoteka soko.

Sikiliza muziki huu
. Utaelewa hizo biti na lafudhi inatoka wapi.

Yaani ni south Africa lakini muziki ni wa majuu.
Kwanini sisi tusifikiri vitu kama hivyo kwa kutumia miziki yetu

Katika dunia ya sasa wasanii lazima mbadilike, msijifungie au kutegemea ziara za kampeni za uchaguzi

Wala msidhani kuna ulinzi wa soko, soko ni huria na nguvu inayoamua ni ushindani

Watu wana cable na masetilaiti yao unadhani watajali hata kama zitazuiwa kutoka nje
Watajali ikiwa kazi zenu ni bora na za viwango, zinazoshindana katika soko lililofurika

Badilikeni, msitumiwe bila kujua kwanini mnatumiwa.

Tusemezane
 
TUMEMWELEWA MZEE WARIOBA?

Katika kumbukizi ya kuzaliwa Mwl Nyerere, mmoja wa wazungumazaji ni mzee J. S Warioba
Mzee Warioba ametumikia awamu tatu na kuwa sehemu ya tume ya katiba awamu ya nne

Mzee Warioba ni waziri mkuu mstaafu na makamu wa kwanza wa Rais na nyadhifa kadhaa
Alikuwa waziri na mwanasheria mkuu, akawa mbunge pamoja na nyadhifa za kimataifa

Warioba alizungumzia alivyomfahamu Mwl Nyerere, moja ya hoja zake ni Mwl alikuwa msikivu
Alieleza kilichokuwa kinatokea wakati wanalumbana katika baraza la mawaziri

Katika hoja zake, alisema Mwl alikuwa msikivu kila walipokutana alimuliza 'mjini wanasemaje'
Mwl alitambua yupo katika uzio na zama zake hakukuwa na namna rahisi ya kuusikia umma

Tulikumbuka wakati wa uhaba wa sukari na unga kwa siku kadhaa.
Muda mfupi Mwl alihutubia Taifa na kulihakikishia hakukuwa na tatizo bali tatizo la usambazaji

Kila mtu alishtuka namna mwl alivyopata habari kwa usahihi kutoka katika foleni na majumbani

TukaKukumbuka ndege zetu zilipoangushwa Musoma, Mwl alihutubia Taifa kueleza kilichotokea
Pengine alifanya ni kutokana na maneno ya mitaani, na kama kiongozi akachukua nafasi yake

Zama za leo mawasiliano kati ya serikali, viongozi na umma ni suala la nukta za sekunde
Mitandao ya jamii na vyombo vya habari vinaeleza kwa undani nini hasa kinatokea nchini

Majadiliano mitandaoni yanatoa picha umma unasemaje, ungependa nini , unakereka wapi n.k.
Siku za karibuni mitandao ilihoji, ikiwa tuna Madaktari wa kupeleka Kenya iweje hawatoshi nchini

Ilichukua siku chache Mh Rais kutoa amri ya madaktari kuajiriwa.
Hii ni baada ya kusikia umma unasemaje kuhusu hilo, unaelewa nini na ungependa nini.

Hatuwezi kuendelea kama hatukubali kusikilizana, kukosoana na kupongezana ikibidi
Ni jambo baya kama watu hawatapenda kusikia mitaani kunazungumzwa nini na wananchi

Jitihada za kuziba sauti za vyombo vya habari au kuandamana mitandao hazina busara

Lau Mwl angekuwepo pengine angetumia mitandao kuliko kumuuliza Warioba mjini kuna ni.

Ujumbe wa mzee Warioba ulikuwa sahihi, kwamba, lazima kama taifa tusikilizane

Kusikilizana ni njia mbili, wanaouzungumza na wanaosikiliza kwa kupokezana

Katika kusikilizana kuna kukosoa , kufundishana , kuelekezana na kupingana ikibidi

Kupitia hayo, tunaweza kujenga hoja imara na madhubuti kwa ustawi wa jamii

Je, tulimwelewa Mzee Warioba katika mifano na hoja?Tulielewa ujumbe aliotaka kutuambia?

Tusemezane
 
TUSIFUTE HISTORIA, TUIENZI KAMA ILIVYO

UWANJA WA TAIFA DAR ES SALAAM NI 'MONUMENT'

Tangu uhuru wa Tanganyika, sherehe za maadhimisho zimefanyika uwanja wa Taifa
Na tangu muungano, sherehe hizo zimefanyika katika uwanja huo huo

Sherehe na maadhimisho mengine yamefanyika kwingine kwa wakati tofauti.

Uwanja wa Taifa 'shamba la bibi' ndipo matukio makubwa ya kitaifa yalipotokea.
Ni mahali bendera ya Tanganyika ilipandishwa ya mkoloni kushushwa kuashiria kujitawala

Kwa wenzetu uwanja wa Taifa ni 'monument' na ndiyo maana ule mpya umejengwa jirani bila kuvunjwa wa zamani. Ile ni thamani ya nchi ikiwa imebeba historia kubwa ya Taifa

Maadhimisho ya muungano na Uhuru ni kumbukumbu ya matukio kwa wakati muafaka

Kuhamishia sherehe Dodoma ni kufuta historia kwa vizazi vijavyo bila sababu
Sherehe zingeendelea kuwepo Dar kulinda historia bila kuathiri chochote

Kuzihamishia Dodoma hakufanyi Dodoma iwe kubwa, yapo yanayoweza kuipa Dodoma hadhi.
Upangaji mji, huduma za jamii, shughuli za biashara n.k. ni baadhi tu

Nchi nyingine ''monument'' hazihamishwi ila zinafuatwa pale zilipo iwe ni kijijini au mijini

Ipo siku vizazi vijavyo vitaamini siku ya uhuru tukio lilitokea Makutupora! tusivilaumu
Tunafuta historia kwasababu tusizoweza kuzitetea.

Tusemezane
 
SAKATA LA RC (Sehemu ya IV)

Mh Rais amemtaka RC kuendelea 'kuchapa kazi'yeye ndiye anajua ampange nani na wapi

Ni ukweli Rais ana mamlaka ya kisheria kabisa na katika kutekeleza anahaki ya kuchagua

Hata hivyo, Rais ni kiongozi wa umma ambao RC ni sehemu ya uwakilishi wake

Ni muhimu kusikiliza na kujibu hoja za umma hata kama hazipendezi

Rais hana sababu za kumuondoa RC katika wadhifa wake.

Kwa mamlaka yake na nafasi ya RC,Rais anasababu za kuutanabahisha umma nini kinaendelea ili aweze kuungwa mkono katika agenda zake

Moja ya agenda ni kuondoa 'wadanganyifu'' ambao umma umeonyesha shaka kwa RC

Kuliacha suala hilo na kuliita udaku, mbele ya safari kutakuwa na matatizo

1. Wananchi watavunjika moyo na kutokuwa na hamasa na wito utakaotolewa

2. Wananchi wataondoa imani (trust and credibility) kwa kauli za viongozi wao

3. RC Makonda atabaki reference . Watu wasiomtakia mafanikio Rais wataifanya agenda

a) Kila hatua atakayoifanya itaangaliwana kupimwa kwa jicho la RC.

Utenguzi wa RC Kilango ungeelezwa tofauti kama ungewekwa katika mizani na RC
b) Kutakuwa na tuhuma za upendeleo zinaweza kupata mashiko

Mbele ya safari kutakuwa na kulinganishwa hatua dhidi ya x kwa mizani ya RC Makonda

Watu wajinga ambao ni sehemu ya jamii wataingiza hisia chafu za ukabila, udini n.k.

Lakini pia kutakuwa na historia. RC aliwahi kuleta vurugu kwa tume ya Warioba.
Akaagiza watu wapigwe atajibu. Akaingia katika ugomvi na viongozi wa dini, na sasa kafanya baya la kuvamia vyombo vya habari kwa kutumia mamlaka na nguvu za dola.

Swali, kuna sheria ngapi na za akina nani ktk nchi hii? Kwanini mtu mwenye historia yenye utata anaendelea bila kuhoji busara na hekima zake? Maadili yanangaliwaje?

Clouds, inafuata
YANATOKEA
Katika mabandiko 4 na hilo hapo juu likiwemo tulieleza kwanini sakata la RC kuhusu vyeti linaigusa serikali. Tulisema kila kitakachofanywa 'reference' itakuwa RC

Tulisema kuwa serikali ''inajifunga mikono''. Ipo nafasi ya kujikwamua kwa kueleza sakata zima la RC kwa ukweli wake kama ulivyo

Leo katika kukabidhi majina ya walioghushi vyeti, suala hilo limeonekana ingawa si dhahiri. Kwamba, kuna maeneo hayakuguswa kwasababu yangegusa pasipotakiwa

Kwamba kuna nafasi za teuzi ambazo haziangalii sifa za kielimu.
Nafasi hizo ni kama za wakuu wa Wilaya, Mikoa n.k.

Ukifuatilia habari nzima, kulikuwa na 'kukwepesha' hoja kulikofanya zoezi zima 'kudorora'

Kuna hoja hapa. Kwamba uteuzi ni suala la madaraka , hilo ni kweli
Kuna kufoji vyeti ambalo ni kosa, halafu kuna kudanganya

Zoezi la vyeti feki linapoanza kuchagua na kubagua kwa kutumia 'hoja' zisizo na mashiko inatia shaka sana.

Zoezi ni jema lina lengo zuri, linafanywajwe ndilo tatizo.

Suala la RC litaendelea kuwa wingu hadi litakapopata majibu sahihi.
Majibu sahihi yatatoka kwa RC au vyombo husika katika ukweli

Hadi wakati huo, suala hilo lenye masilahi ya Taifa litakuwa 'rehani' kwa masilahi madogo. Kwanini?

Tusemezane
 
MIAKA 10 UDOM

Prof KIKULA ALIMAANISHA NINI? NANI ALIMWELEWA?

Katika uzinduzi wa sherehe za miaka 10 , makamu mkuu wa Chuo cha UDOM alizungumzia changamoto za chuo

Kati ya hizo ni kudaiwa fedha za ardhi na kumuomba Mh Rais aingilie kati

Prof alizungumzia uwepo wa ofisi za serikali katika majengo hayo
Kwa mujibu wa gazeti moja la habari, Prof alisema kuhamia kwa ofisi za serikali katika majengo ya UDOM hakujaathiri shughuli za kitaaluma

Kikula akasema kuhamias kumesaidia kwani kulikuwa na uharibifu wa majengo ikiwemo kung'olewa milango kwa majengo yasiyotumika.

Makamu akasema lengo la chuo ni kudahili wanafunzi 40,000 , kwasasa wapo 23,000

Prof Kikula akaeleza chuo kina kozi 186 na vyuo vya ndani kikiwa ni kikubwa nchini

Kwa upande wa matatizo alisema kuna uhaba wa majengo wa college tatu

Hoja:
Katika hali ya kuchanganya haieleweki kwanini kuwepo uhaba wa majengo ikiwa chuo kinadahili nusu ya idadi iliyokusudiwa

Kubwa zaidi ni kuhusu ofisi za serikali ambazo zipo chuoni bila kuathiri shughuli, wakati huo huo Prof Kikula akisema kuna college 3 zinahitaji msaada wa majengo

Majengo gani ikiwa serikali inatumia na hakuna athari?
Prof haoni uwepo wa serikali ndicho chanzo cha college 3 kutokuwa na majengo?

Haieleweki Prof alikusudia nini aliposema ofisi za serikali hazina athari, lakini anahitaji majengo kwa college tatu huku akiwa na nusu ya wanafunzi wa idadi iliyokusudiwa!

Kama ipo tafsiri tofauti Prof Kikula aieleze kwa umma, vinginevyo umma hautamwelewa

Je, Prof alifanya hivyo kukidhi haja za kisiasa? Je, anachosema kina mantiki?

Tusemezane
 
MIAKA 10 UDOM

Prof KIKULA ALIMAANISHA NINI? NANI ALIMWELEWA?

Katika uzinduzi wa sherehe za miaka 10 , makamu mkuu wa Chuo cha UDOM alizungumzia changamoto za chuo

Kati ya hizo ni kudaiwa fedha za ardhi na kumuomba Mh Rais aingilie kati

Prof alizungumzia uwepo wa ofisi za serikali katika majengo hayo
Kwa mujibu wa gazeti moja la habari, Prof alisema kuhamia kwa ofisi za serikali katika majengo ya UDOM hakujaathiri shughuli za kitaaluma

Kikula akasema kuhamias kumesaidia kwani kulikuwa na uharibifu wa majengo ikiwemo kung'olewa milango kwa majengo yasiyotumika.

Makamu akasema lengo la chuo ni kudahili wanafunzi 40,000 , kwasasa wapo 23,000

Prof Kikula akaeleza chuo kina kozi 186 na vyuo vya ndani kikiwa ni kikubwa nchini

Kwa upande wa matatizo alisema kuna uhaba wa majengo wa college tatu

Hoja:
Katika hali ya kuchanganya haieleweki kwanini kuwepo uhaba wa majengo ikiwa chuo kinadahili nusu ya idadi iliyokusudiwa

Kubwa zaidi ni kuhusu ofisi za serikali ambazo zipo chuoni bila kuathiri shughuli, wakati huo huo Prof Kikula akisema kuna college 3 zinahitaji msaada wa majengo

Majengo gani ikiwa serikali inatumia na hakuna athari?
Prof haoni uwepo wa serikali ndicho chanzo cha college 3 kutokuwa na majengo?

Haieleweki Prof alikusudia nini aliposema ofisi za serikali hazina athari, lakini anahitaji majengo kwa college tatu huku akiwa na nusu ya wanafunzi wa idadi iliyokusudiwa!

Kama ipo tafsiri tofauti Prof Kikula aieleze kwa umma, vinginevyo umma hautamwelewa

Je, Prof alifanya hivyo kukidhi haja za kisiasa? Je, anachosema kina mantiki?

Tusemezane


Mkuu, kwa bahati nzuri mimi nimepitapita hapo Udom. Anachosema Prof kinaeleweka vizuri tu kwa Structure nzima ya Chuo.

Ni kwamba kila college inapaswa kuwa na majengo yake binafsi kwa matumizi yake, ofisi, madarasa, maabara, hosteli, majengo ya utawala, n.k. Kilichopo ni hizo college 3 kubebwa ndani ya college nyingine, yaani kutumia majengo ya college nyingine.

Katika hali hiyo, majengo ya college hizo tatu yanahitajika.

Nafasi wazi zipo nyingi ndani ya baadhi ya college zilizokamilika, kwani hakuna iliyofikia lengo la mwisho la udahili, hivyo kutoa nafasi kwa college zilizokosa majengo kutumia nafasi hizo, na kwa sasa na serikali pia.

Linawezekana.
 
Mkuu, kwa bahati nzuri mimi nimepitapita hapo Udom. Anachosema Prof kinaeleweka vizuri tu kwa Structure nzima ya Chuo.

Ni kwamba kila college inapaswa kuwa na majengo yake binafsi kwa matumizi yake, ofisi, madarasa, maabara, hosteli, majengo ya utawala, n.k. Kilichopo ni hizo college 3 kubebwa ndani ya college nyingine, yaani kutumia majengo ya college nyingine.

Katika hali hiyo, majengo ya college hizo tatu yanahitajika.

Nafasi wazi zipo nyingi ndani ya baadhi ya college zilizokamilika, kwani hakuna iliyofikia lengo la mwisho la udahili, hivyo kutoa nafasi kwa college zilizokosa majengo kutumia nafasi hizo, na kwa sasa na serikali pia.

Linawezekana.
Bado haijajibu hoja ya kuwa na majengo yasiyotumika ambayo serikali inayatumia. Je, si muafaka majengo hayo yakapewa college zisizo nazo?

Kuna ulazima wa kujenga mapya ikiwa yapo yasiyotumika?
 
Bado haijajibu hoja ya kuwa na majengo yasiyotumika ambayo serikali inayatumia. Je, si muafaka majengo hayo yakapewa college zisizo nazo?

Kuna ulazima wa kujenga mapya ikiwa yapo yasiyotumika?

Ni muafaka kupewa, na wameshapewa, lakini lengo ni kudahili wanafunzi elfu 40, hilo lengo litakapofikiwa kila college inapaswa kuwa na majengo yake. Hata serikali italazimika kuhama chuoni.

Ukosefu wa majengo unaweza kuwa ni miongoni mwa changamoto za kufikia lengo la wanafunzi elfu 40.

Je, si sahihi kusema miongoni mwa changamoto za wizara zilizohamia Dodoma ni ukosefu wa majengo kwa sababu tu kuna nafasi chuoni?

Nafikiri kinachosemwa ni suluhisho la kudumu, si la siku moja kama zilivyobebwa wizara zetu. Majengo yanahitajika, yakamilike yote ili kuiachia management kuangalia mazingira mengine ya kufikia lengo la wanafunzi elfu 40.
Mimi nimeelewa hivyo nadhani.
 
Ni muafaka kupewa, na wameshapewa, lakini lengo ni kudahili wanafunzi elfu 40, hilo lengo litakapofikiwa kila college inapaswa kuwa na majengo yake. Hata serikali italazimika kuhama chuoni.

Ukosefu wa majengo unaweza kuwa ni miongoni mwa changamoto za kufikia lengo la wanafunzi elfu 40.

Je, si sahihi kusema miongoni mwa changamoto za wizara zilizohamia Dodoma ni ukosefu wa majengo kwa sababu tu kuna nafasi chuoni?

Nafikiri kinachosemwa ni suluhisho la kudumu, si la siku moja kama zilivyobebwa wizara zetu. Majengo yanahitajika, yakamilike yote ili kuiachia management kuangalia mazingira mengine ya kufikia lengo la wanafunzi elfu 40.
Mimi nimeelewa hivyo nadhani.
Rais alisema tatizo la kupangia wanafunzi vyuo ni chanzo cha vyuo kama UDOM kutokuwa na wanafunzi wa kutosha
VC capacity ya UDOM ni 40,000 hadi sasa ni 23,000

Hii ina maana moja, kwamba, hawana wanafunzi wa kutosha chuo na ndiyo maana majengo yapo wazi hadi wizara zinapewa kufanyia kazi

Kwa mantiki hiyo Kikula alipaswa kutumia kilichopo kwa kutoa majengo katika college halafu kujengewa mengine ni project lakini si tatizo la wakati huu

Anapo ji contradict ni kuonyesha chuo kina uhaba wa majengo, halafu kuna majengo yasiyotumika, na mwisho wametoa kwa wizara bila kuathiri shughuli, baada ya hapo anaomba msaada wa majengo ya college

Mjadala upo hapo, serikali inaingia tu kama kuonyesha contradictions zilizopo

Ningekuomba ufafanue hizo kauli nne, uhaba, ziada,kutoa, kuomba msaada.
 
Kama ulivyoisemea kauli ya Rais ya kutafuta ufumbuzi wa uhaba wa wanafunzi Udom, hii ni hatua ambayo uongozi wa chuo haipaswi kusubiri mfumuko wa wanafunzi ndio waandae mazingira. Wakiwa wana oversee matokeo ya hatua zinazochukuliwa ni jambo la wazi kabisa kuona Uhaba wa majengo.

Ziada iliyopo leo inatokana na uhaba wa wanafunzi chuoni. Majengo yaliyopo yanaweza ku-accomodate zaidi ya wanafunzi elfu 23, lakini si kufikia elfu 40.

Majengo yaliyotolewa serikalini ni yale yaliyobaki baada ya kukidhi kuwahudumia wanafunzi elfu 23, na yalibaki kwa kukosa wanafunzi, jambo ambalo linadhaniwa limesababishwa na mfumo wa udahili, na limeshachukuliwa hatua kama wanavyofikiri.

Wanaomba msaada ndio wa majengo mengine, lengo ni kujiandaa na hao wanafunzi watakaoongezeka, matokeo ya mfumo mpya wa udahili.

Katika jicho jingine ni kuiambia serikali sasa kuwa, ijiandae kuwaachia majengo yao maana yaliyopo hayawezi kutosha kiasi cha kuomba kujengwa mengine.

Ukamilifu wa Udom ni kila college iwe inajitegemea, katika kuzingatia hilo college 3 zina upungufu mkubwa kiasi cha kubebwa na college nyingine. Katika kuheshimu hilo, ni lazima kila college iwe na majengo yake. Vilevile ikumbukwe kuwa majengo yanayosemwa si hosteli tu, tukumbuke kuna hospitali, maabara, maktaba, utawala, madarasa, n.k. Tujaribu kufikiria ni kwa namna gani hayo yaliyoandaliwa kwa college moja, yanawezaje ku-serve college mbili au zaidi kwa wakati mmoja?

Bado nafikiri alichoongea si tatanishi kiasi hicho.
 
JingalaFalsafa

Kauli tata zinatokana na ukweli Prof aliongea kisiasa na si kitaalamu.
Tunasababu za kusema hivyo

Inaeleweka UDOM ina uwezo wa 40,000, kwahiyo kusema ni lengo lao la baadaye ni kunabatilisha sentensi zao kuhusu uwezo huo walio nao sasa

Pili, taarifa ya VC katika hali ya kawaida ilipaswa iongelee wakati uliopita, nini kimefikiwa wakati huu na nini ni matarajio ya chuo kwa siku za baadaye.

Laiti angesema matarajio ni kuwa na college 3 hivyo yanahitajika majengo kusingekuwa na utata
Alichosema ni UDOM kukabiliwa na uhaba wa majengo, hapa akimaanisha kwa sasa

Ndipo swali linazuka, ikiwa wana uhaba wa majengo , inakuwaje wanakuwa na majengo yasiyotumika hadi kutoa kwa serikali kutumia?

Kwa kutumia akili za kawaida tu, huwezi kuwa na ziada ukawa na pungufu.

Prof angesema serikali ikiondoka tutakuwa na upungufu wa college 2, ingeeleweka kuwa majengo ya college 1 yanatumiwa sasa

Pili, unaposema ilikuwa njia ya kuwaambia serikali waondoke, hapa si kweli.
Huwezi kuwaambia waondoke wakati unasifia uwepo wao wa kutumia majengo ili yasichakae!!!

Tatu, ni kweli mfumo wa udahili ulilazimisha wanafunzi kwenda vyuo vingine
Endapo wangekuja UDOM hali ingekuwaje ikiwa chuo hakina college 3?

Ukitazama kutoka kila angle hakuna utetezi unaokukidhi utata wa kauli za kisiasa za VC
Hakuongea kama mtaalam, bali mwanasiasa na kuvutika kumu 'impress' boss badala ya kuzungumzia hali halisi.

Kauli zake zina utata, hazieleweki zimejaa siasa na hazilingani na kiwango the least to say
 
Tukitazama kwa jicho la kisiasa, hakuna kauli ambayo itatolewa mbele ya wadau wa siasa halafu kusiwe na namna ya kuihusisha na siasa. Upo uwezekano Kikula kutumika kisiasa katika hili, lakini haiondoi uhalisia wa madai yake.

Mkuu Nguruvi3, UDOM HAIJAKAMILIKA KUJENGWA, kama zinavyokosekana nyumba za wafanyakazi wa chuo ndivyo yanavyokosekana majengo ya college 3.

Kosa lako ni kudhania Udom ina uwezo wa ku-accomodate 40,000 students leo, HAIKO HIVYO, ujenzi wa chuo HAUJAKAMILIKA, kinachodaiwa si New Project, ni umaliziwaji tu wa initial project.

Mkuu, nimesema hapa kuwa kwa matarajio ya huo mfumo mpya wa udahili, Serikali nayo inapaswa kujiandaa kuondoka chuoni. Lakini kwa sasa yale majengo kukaa bure ilikuwa ni upotevu wa resources tu.
Hao wanafunzi 40,000 wangekuja leo Udom tungeshuhudia kero zinazotokea Udsm, Mzumbe na vyuo vingine vinavyosumbuliwa na uhaba na majengo. Na kwa mazingira ya Dodoma hali ingekuwa mbaya zaidi.

Hata serikali ikiondoka leo, bado kutakuwa na uhaba wa majengo ya college 3, kwani wote kwa pamoja serikali na hizo college 3 zimepewa hifadhi ya muda tu kwenye hizo college zilizokamilika.

Bado ninafikiri hakuna utata mkubwa hivyo nje ya mtazamo wa kisiasa.
 
Nadhani Tusubiri ripoti ya tume ya pili, ndipo tutafanya mjadala mzuri juu ya sakata zima la Mchanga wenye madini kuzuiwa kusafirishwa kwenda nje.
 
Back
Top Bottom