Duru za Siasa: Awamu ya 5 - Uongozi na Yanayojiri

Duru za Siasa: Awamu ya 5 - Uongozi na Yanayojiri

TUKIO LA TANGA SIYO USULUHISHI NI UPATANISHI (III)
MITANDAO ISIBADILI MAANA NA ASILI YA TUKIO

Kwa upande wa serikali, hili jambo ni la kufikirisha. Inapofikia mahali mkuu wa nchi anaingilia kati, ni dhahiri suala lilikuwa zito kuliko inavyodhaniwa.

Halikuwa zito kwa Media ni kwa mtendaji wa serikali aliyeichafua kuombewa msamaha

Uzito wake unaongezeka kwa kujiuliza, lini serikali itatoa uhakiki wa vyeti na majina ya RC mhusika ili kusafisha hali ya hewa!

Huko nyuma tulieleza, hoja zisipotolewa majibu kutajengeka utamaduni wa 'kuhifadhiana'.
Ni kwa utamaduni huo tulisema, zoezi la uhakiki wa vyeti litaingia doa.

Liliingia doa waziri alipolazimika kuondoa makundi ya watumishi kukwepa jina la mtu

Kiongozi huyo anailazimu serikali 'kumpatanisha' na wadau kwa makosa binafsi zaidi kuliko majukumu yake

Haipendezi kumweka Mh Rais katika wakati tusiotarajia kama ilivyotokea Tanga

Swali la kujiuliza, kuna ni, anayetenda na kupewa 'pass' hata panapoonekana wazi?

Je, kiongozi huyu ni Asset au ni Liability na anaisadiaje serikali?

Na kwanini serikali iendelee kulinda taswira kwa gharama ya mtu mmoja?

Kwa upande wa Media na hasa TEF, hili limekuwa funzo zuri kwa viongozi wengine wasioheshimu taaluma yenu 'rogue' na wanaotaka kuwatumia watavyo.

Ni funzo zuri mnaweza kulinda taaluma mkiamua, hatua mlizochukua bila kujali zimewaathiri vipi, zimefanikiwa kwa kiwango kikubwa sana.

Mumeitendea taaluma haki na heshima

Tusemezane
 
WAZIRI MKUU NA HOJA YA UTALII

TATIZO LETU SI RASILIMALI AU VIVUTIO. NI UVIVU WA KUFIKIRI

Sehemu ya I

Waziri mkuu yupo Cuba kwa ziara ya kiserkali na ametembelea mkoa unaoingiza Watalii wengi kuliko Tanzania. Rasilimali kubwa ya mkoa huo ni ufukwe wa bahari wa KM 22 wenye mahoteli 20,000

Mh Waziri mkuu ametoa wito kwa mamlaka ya utalii kuangalia namna ya kukuza utalii nchini
Waziri mkuu ana hoja, kwa kutambua kuwa mkoa mmoja wa Cuba unaingiza waalii kuliko nchi nzima
Ana hoja kwamba,rasilimali waliyo nayo ya ufukwe ni sawa tu na kile tulicho nacho

Pamoja na ukweli wa hoja zake, ni ukweli pia viongozi wengi wamesomea au wametembelea au kuishi maeneo yenye utalii hata bila kuwa na vivutio vya maana kama tulivyo navyo. Hivyo utalii na thamani zake wanaujua

Tumkumbushe mh Waziri mkuu ya kuwa pale anapoishi kuna ufukwe wa Coco ambao miaka nenda rudi umebaki na 'uoto' wake wa asili kukiwa hakuna huduma muhimu ingawa idadi ya watumiaji inaongezeka kila uchao

Hatuhitaji darubini kubaini kuwa uwezo wa viongozi wetu katika ngazi zote za Wilaya, mkoa na Taifa una mashaka makubwa kwa kuangalia tu Coco Beach na jinsi tulivyoshindwa. Je, tunaweza kutangaza utalii nje?

Mh Waziri mkuu anarudia kauli ya tangu zama za Rais Kikwete ya kutangaza vivutio vya utalii nje ya nchi
Utalii si suala la bahati nzuri, ni uwekazaji unaohitaji maarifa na 'sayansi' yakiwemo mahesabu

Na wala uwekezaji si kugawa mapesa kama tulivyowahi kuona mabasi ya east London wakati wa awamu ya nne
Nchi zilizofanikiwa zimewekeza kwa mkakati na mahesabu haswa tena kwa muda mrefu na sasa 'inalipa'

Utalii ungefanywa kwa njia za kitaalamu na kuacha siasa pembeni ungeweza kuliingizia taifa hili kipato kikubwa sana na pengine kutotegemea sekta nyingine zenye kuhitaji gharama kubwa

Tatizo letu si rasilimali, si vivutio na wala si hali ya hewa, ni uvivu wa kufikiri.
Uvivu haumaanishi tunaamka wachovu, ni uvuvi wa kuelekeza fikra zetu katika mambo yasiyolisaidia taifa

Tumekuwa washabiki wa mambo ya ajabu ajabu na kujinyima fursa ya ubunifu wa mambo ya maana

Mathalan, mkoa mama wa Utalii nchini ndio unaongoza kwa habari za kukamatana, mahubusu, kesi na vitu ambavyo mwisho wa siku haviliingizii taifa hili hata dollar moja

Viongozi wa maeneo kama hayo wana muda gani mwingine wa kufikiri namna ya kukuza utalii?

Hatuwezi kuwekeza kwenye fikra mbovu tukategemea kushindana na wale wenye fikra endelevu

Utalii ni hesabu ni sayansi ni sanaa, tutaeleza kwa undani bandiko lijalo

Inaendelea..
 
WAZIRI MKUU NA HOJA YA UTALII
TATIZO LETU SI RASILIMALI AU VIVUTIO. NI UVIVU WA KUFIKIRI

Sehemu ya II

Kabla ya kujadili hoja ya utalii kuwa uchumi, elimu, syansi, sanaa n.k. tujiulize maswali machache
Je, mlima Kilimanjaro ndio mlima pekee duniani? Kwanini mtu asiende milima mingine aje Kilimanjaro!

Je, wanyama wakiwemo 'rare' kama Faru na wengine wanapatikana Tanzania peke yake?
Je, Tanzania peke yake ndiyo yenye fukwe nzuri za kupumzika kuliko nchi nyingine?

Majibu ya maswali ni rahisi, kwamba kila kitu kinapatikana sehemu nyingine ya dunia
Tanzania si pekee, ina washindani katika biashara ya Utalii duniani

Ushindani wa biashara ya utalii si kama riadha, wakwanza ndiye mshindi atashangiliwa na watazamaji. Ushindani wa utalii ni katika mambo mengi, haulengi kukimbia mbele bali kuvutia 'watazamaji' au watalii

Unawavutiaje watalii? Kwanza, lazima uwe na elimu ya kuuza unachotaka kuwauzia.

Pili, si kuuza tu bali ubora 'quality' wa unachouza.
Haiishi hapo ubora ni pamoja na kucheza na 'Elimu, psychology na uchumi' wa mhusika

Psychology haimaanishi ghilibu,ni kuelewa walengwa wanataka nini na kwasababu zipi na gharama gani.

Mfano, msomi anayetaka kuona nyayo za Laitoli Arusha, ashawishiwe kufika mlima Kilimanjaro ukimweleza kwanini Kilimanjaro ni Unique duniani. Si lazima apande bali kufika tu eneo hilo ni muhimu

Lakini pia unatakiwa umweleza kuna Olduvai gorge sehemu ya elimu ya archaeology ukielewa interest yake ni katika eneo hilo, kuna wildbeast migration ya wanyama karibu na maeneo anayotaka na maeneo ya mapumziko n.k.

Hayo yanafungwa katika kapu la uchumi, kwamba ticket moja kuja Tanzania itamwezesha kufaidika na mengi kuliko haja yake ya Laitoli.

Hadi hapo umetoa elimu, ameelezwa ubora, uchumi umezingatiwa, 'value for money'

Kutangaza utalii si kuweka mabango, au TV tu, ni kutafsiri na kumshawishi mhusika kwanini aje Tanzania, si Kenya, Botswana, South Africa, Mali au Kathmandu

Swali la kujiuliza, tumejiandaa kwa hilo? Tuna watu wenye uwezo wa kielimu katika kushawishi, kuongoza, kupokea hadi mtalii anaporudi alikotoka salama?

Je, mtaali anapofika anapata huduma anazopaswa kwa usahihi?
Je, tuna vyuo vya utalii vyenye kushirikisha taaluma kama timu ili kuongoza watalii

Vyuo vya utalii hatumaanishi vya watoa huduma za malazi na kugawa chai.

Vyuo vya utalii ni vile vinavyotoa mafunzo kwa wataalamu wa fani mbali mbali washiriki Utalii kupitia taaluma zao kama Daktari wa wanyama , wataalam wa wanyama pori, archaeologist, watu wa mazingira na tabia nchi n.k.

Ukweli ni kuwa hatuna wataalam wa Utalii, tuna wahudumu wa utalii.

Katika hali hiyo tunakwendaje kushindana na wenzetu waliojizatiti tukidhani mabango yanajiuza yenyewe na sio sisi kuuza bidhaa zetu kitaalam!!!

Inaendelea..
 
WAZIRI MKUU NA HOJA YA UTALII
TATIZO LETU SI RASILIMALI AU VIVUTIO. NI UVIVU WA KUFIKIRI

Hoja rasha rasha tukiendelea na mjadala, 'on transit'

Ukiwa Cairo unaweza kwenda Giza Pyramid n.k.
Ukiwa London na kama ni 'eligible' kutoka unaweza kwenda London eye, Bridge, Buckingham place n.k.
Ukiwa Paris kama ni 'eligible' kutoka unaweza kufika Eiffel tower n.k.

Orodha inaendelea na ni ndefu. Kote unakopita unajikuta ukiacha 'dollar'
Kwa nchi za wenzetu hata connections za ndege zinatengenezwa kiwezekana uache dollar 1

Kwa msafiri aliyetua JNIA Dar asubuhi saa 2 kutokana nchi jirani au hata ndani ya nchi na anaunga ndege saa 5 usiku, kwa muda huo atakwenda wapi? Kuna kitu gani unachoweza kumshawishi atoke akatembelee?

Kuna nchi hazina vivutio vya asili, zimetengeneza tu na zinafanya vizuri kuliko sisi

Utalii si mabango ya faru na nyati, si mlima Kilimanjaro ni zaidi ya hapo.


Inaendelea..sehemu ya III
 
WAZIRI MKUU NA HOJA YA UTALII
TATIZO LETU SI RASILIMALI AU VIVUTIO, NI UVIVU WA KUFIKIRI

Sehemu ya III
Kuwekeza katika utalii si mabango ya matangazo au barabarani kuhubiri au mikutano

Zipo njia nyingi za kuwekeza. Kwanza, ni muhimu wananchi wakaelewa wana nini ndani ya nchi yao

Ili kuelewa ni lazima kuwe na utalii wa ndani kutoa elimu kwa wananchi kuziba pengo la mapato wakati msimu wa watalii wa nje unapopungua.

Katika hili kuna kutoa motisha ya gharama ikiwa ni pamoja na kwa kuhamisisha kuanzia mashuleni, vyuo na watu binafsi wanaotaka kupata mapumziko

Pili, kuna suala la kuwekeza katika infrastructure ili kurahisha safari za watalii wa nje. Kwa sasa kuna usafiri wa ndege za nje kufikia KIA moja kwa moja.
Hili limesaidia sana kupunguza gharama na muda kwa watalii

Ni wakati wa kujiuliza kwanini Nairobi inakuwa 'Hub' cha ndege za nje na si si kwetu?
Kuna haja ya kuangalia gharama kuvutia mashirika ya ndege tukizingatia nafasi ya Jiji kama Dar kijiografia

Mashirika kama Scandinavia airline, PIA, Lufthansa, Air France n.k kwanini yaliacha safari za moja kwa moja Tz?

Mashirika hayo yanahudumia kupitia Nairobi, kwanini si kwetu wenye hazina ya utalii

Tatu, kufanyike jitihada za makusudi kuhakikisha nchi inakuwa mgeni wa mikutano ya kikanda na kimataifa, wageni wapewe 'incentives' za utalii.
Huo ni uwekezaji katika kujitangaza kwa hali ya juu

Nne, sekta ya utalii iangalie kwa jicho la watalaam. Hatudhani kudorora kwetu ukilinaganisha na nchi kama South Africa au Kenya ni kwa bahati mbaya.

Kuna 'ombwe' la watalaam linalotokana na kukosa vyuo vinavyotambulika
Kuna tatizo la 'exposure' kwa watu wetu na kuwafanya 'incompetent' katika ushindani

Tano, kuwepo na aggressive advertisement kupitia balozi zetu.
Kwamba, zinaweza kuandaa siku maalum za kutangaza nchi na katika siku hizo kuwepo na uvutiaji wa watu kuja Tanzania.Hili ni pamoja na balozi kuwa na resources za kuwawezesha na si suala la kutoa visa tu

Sita, kupitia michezo na watu maarufu ambao katika zama za kiteknolojia huwa na wafuasi kwa mamilioni. Kupitia 'celebrity' ni rahisi kufikia mamilioni ya watu kuliko mabango ya matangazo yanayosomwa kwa nandra

Saba kutumia watalaam wetu kuandika habari katika magazeti maarufu kama The Geography au Discovery kufikia watu wenye interest mbali mbali na mambo ya asili

Haya ni kwa uchache sana, hoja kubwa njia za kutangaza utalii si jukumu la TTB tu, ni jukumu la serikali . Ongezeko la watalii lina manufaa kwa Taifa kwa ujumla

Mh Waziri mkuu kabla hajaeleza nini ameona fukwe za Cuba, labda timu yake ingemsaidia kuelewa tatizo letu li wapi ikiwa tuna kila kitu?
Kama hatuwezi Coco beach, Msasani au Barakuda tunashangaa kipi Cuba?

Hatuwezi kuona ukumbini kwetu tunawezaje kuwalaumu TTB?

Muhimu, TTB wanachaguliwa na nani kiasi kwamba wanayofanya hayawezi kupimwa au kutathminiwa?

Inaendelea...
 
MATUKIO YA MELI ZENYE BENDERA
TAMKO LA SERIKALI NI JEMA, HATUA ZAIDI ZINAHITAJIKA YASIJIRUDIE

Sehemu ya I

Juzi Makamu wa Rais alitoa tamko kuhusu sakata la meli zenye bendera ya Tanzania kukamatwa zikiwa na shehena zisizokubalika kimataifa

Taarifa ya Makamu imekuliwa na magazeti likiwemo la The citizen lililoeza asili ya meli

Ni tukio lenye usumbufu kwa serikali na nchi kulitolea ufafanuzi
Usumbufu ni pale jumuiya ya kimataifa inapotaka serikali kufafanua tukio isilolijua

Si mara ya kwanza, huko nyuma meli nyingine ilikamatwa ikikiuka vikwazo vya kimataifa

Katika matukio hayo matatu kuna kitu ''common'' kwamba meli hizo zimesajiliwa Zanzibar

Zanzibar wana mamlaka inayosimamia vyombo vya baharini (ZMA) chini ya SMZ
Chombo cha kimataifa cha usafiri wa majini (IMO) Tanzania ni mwanachana-United Republic of TZ

Ni kwa mantiki hiyo, uanachama wa Tanzania katika IMO (1974) unasimamiwa na Jamhuri ya muungano ikiwemo haki za unachama na wajibu kama ada n.k.
ZMA kupitia SMZ si mwanachama

Meli ziwe zimasajiliwa bara au Zanzibar hupeperusha bendera ya JMT
Tatizo linapotokea anayewajibika ni JMT na hapa ni serikali

Ni haki kwa jumuiya ya kimataifa kuitaka JMT kutoa maelezo ya matatizo yaliyojitokeza kwa chombo chenye bendera ,ni haki JMT kutoa maelezo,ndiyo mmiliki wa bendera

Hakuna shaka matukio ya meli ya karibuni na yaliyopita yameiweka wizara na serikali katika wakati mgumu kwa namna mbili;
kwanza, kuchafuliwa jina la nchi, pili kutoa maelezo kwa jambo linalofedhehesha

Kwa kutambua unyeti wa masuala ya muungano, na kwamba suala imehusu serikali mbili, Makamu wa Rais, kiongozi wa masuala ya muungano ikabidi alitolee maelezo

Hilo imefanyika kwa weledi, ni rahisi kwa baadhi ya watu kutuhumu Zanzibar kuingiliwa endapo tamko lingetolewa na kiongozi asiye na jukumu la muungano na pengine asiyetoka Zanzibar

Pamoja na tamko hilo, kuna kila sababu za kuliangalia tatizo hilo kwa kina lisijirudie na kuifedhehesha nchi achilia mbali kuiweka serikali katika mazingira magumu pasi na sababu

Nini tatizo na nini kifanyike? Inaendelea sehemu ya II
 
MATUKIO YA MELI ZENYE BENDERA
Sehemu ya II

Kuna maswali yakujiuliza ya a meli zinazokamatwa kwa kukiuka sheria na taratibu

Kwanza, kwanini meli hizo zinakuwa zimesajiliwa Zanzibar?

2.Je, ZMA inauangalizi gani kiasi kwamba matukio hayo yamekuwa yanajirudia?

3.Kuna sababu gani za kuwa na ZMA,chombo chini ya SMZ na JMT haina udhibiti?

4.Kwanini matukio yanayotokana na SMZ yapelekee upande mwingine kuingia matatizo?

5.Je, mapato ya ZMA yanachangia vipi uendeshaji wa Tanzania Maritime Authority?

6.Kwanini SMZ imeshindwa kudhibiti matukio haya kujirudia?

7.Kwanini Znz isipewe fursa ya ushiriki 'associate' kama baadhi ya nchi ndani ya IMO?

8.Je, usafiri wa majini na bandari ni mambo ya muungano au siyo?

Maswali yanaweza kuwa na majibu mepesi, mbele ya safari yanaweza kukosa majibu

Ni mambo yanayolihusu Taifa kwa muktadha wa muungano na ushiriki wa nchi kimataifa
Endapo hayataangaliwa, ipo siku yataiweka nchi katika wakati usiotarajiwa

Kulikuwa na sababu gani ya SMZ kuwa na ZMA ikiwa chombo hicho kinatumia bendera ya JMT na sheria iliyoanzisha ni ile ya SMZ?

Katika matatizo yaliyojitokeza, SMZ ilikuwa wapi na kwanini 'hawakujitokeza' kuzungumzia meli walizosajili, wanazochukua ada kupitia ZMA?

Upana wa jambo hili unazigusa taasisi nyingine za Zanzibar nje ya muungano.
Matukio haya yanaondoa 'umanifu' (credibility) ya taasisi hizo zinapoingia katika JMT

Zanzibar ilipoanzisha taasisi zake ilitegemewa ziwe katika viwango kwa kuelewa muingiliano wa muungano

Mathalani, atakayetilia shaka baraza la mitihani la Zanzibar, au shirika la viwango au taasisi nyingine ataekosea kwa namna gani kwa kuangalia ZMA na utendaji wake?

Hatua ya serikali za kuzifutia meli usajili ni nzuri kwa mantiki ya kuisafisha nchi kutokana na uchafu uliotokea eneo jingine. Hatua hiyo ni ya kuanzia na dharura, kuna umuhimu wa kuchukua hatua zaidi

JMT iangalie uwezekano wa kuipa fursa SMZ kuwa mwanachama mshiriki 'associate' IMO

Pili,kuna kila sababu ya kuangalia iwapo ipo haja ya kuwa na taasisi pande mbili zikibeba majukumu sawa ikiwemo bendera, zikiwajibika tofauti na pengine kuwa tatizo upande mwingine

Tatu, kuna haja ya JMT kuangalia viwango vya taasisi nje ya muungano ili kuleta uwiano.
Isichukuliwe kirahisi,kwavile ni JMT basi taasisi kutoka nje ya JMT zinakubalika kwa jina

Kushindwa kwa ZMA kudhibiti hali inayojirudia ni kielelezo cha uwepo wa tatizo

Inawezekana udhaifu wa ZMA ni dalili yaya udhaifu wa taasisi zinazoingia katika muungano kwa jina- JMT

Kwa hili la meli za Zanzibar, hatua ya serikali ni ya kupongezwa, hata hivyo hiyo ni dawa ya 'kutuliza maumivu'. Ni muhimu kutafuta dawa ya kuponya, vinginevyo mchezo unaweza kuiweka nchi katika wakati mgumu .

Hivi Tanzania ingeingia matatani mbele ya jumuiya ya kimataifa, mwananchi wa Kigoma, Mtwara au Ruvuma anahusika vipi na tatizo la taasisi isiyo ya muungano, iliyoanzishwa na sheria nje ya muungano na kusainiwa na kiongozi nje ya muungano kwa ajili ya shughuli nje ya muungano?

Je, tunajifunza lolote kuhusu changamoto za muungano na jinsi zinavyoweza kuwa tatizo siku za mbeleni?

Tusemezane
 
Duniani kuna biashara za aina nyingi. Yaani watu 'wanakodi bendera ya nchi' kwa ajiri ya kuweka juu ya meli zao!
====
Je, tunajifunza lolote kuhusu changamoto za muungano na jinsi zinavyoweza kuwa tatizo siku za mbeleni?
Mkuu, hapa nikutafuta suluhu sahihi ya kutatua tatizo hili na mengine yanayofanana na hili ili yasitokee siku nyingine. Nadhani hakuna haja ya kulalamika tena wala kuhojiana. Tutafute, tupendekeze nini cha kumaliza hili tatizo sisi kama wananchi kupitia serikali yetu (zetu) inayo(zinazo)husika na usimamizi.

Bila kuchelewa mimi naanza na mapendekezo yangu namna ya kumaliza tatizo hili.

Mkuu biashara ya 'kukodisha bendera yetu' iangaliwe upya. Iwe inasimamia ZMA ama taasisi yoyote ya JMT, ili kuondokana na kadhia hii siku nyingine, lazima meli zote zitakazosajiriwa zipewe sharti la kuhakikisha msajiri anapata uhakiki wa meli hizo zinasafirisha nini na kwa nani. Uhakiki huo ujikite katika kuhakikisha meli hizo hazisafirishi ama kufanya biashara haramu ama kuvunja mikataba ama kuvuruga makubaliano tuliyoridhia ya kimataifa. Kwa hili, itafutwe namna bora ya kuhakikisha hili linafanyika kwa usahihi kabisa.
 
"TUJITEGEMEE, post: 25429808, member: 31026"]Duniani kuna biashara za aina nyingi. Yaani watu 'wanakodi bendera ya nchi' kwa ajiri ya kuweka juu ya meli zao!
Unaweza kusimama mbele ya mataifa ukatoa sababu hii ukaeleweka?
Mkuu, hapa nikutafuta suluhu sahihi ya kutatua tatizo hili na mengine yanayofanana na hili ili yasitokee siku nyingine. Nadhani hakuna haja ya kulalamika tena wala kuhojiana.
Sijui malalamiko ni yapi uliyoyaona, I wish ungesoma vizuri bandiko 407 na 408
Huwezi kutafuta suluhu kwa jambo usilolifanyia analysis kujua chimbuko na huenda tatizo lipo wapi
Mkuu biashara ya 'kukodisha bendera yetu' iangaliwe upya.
Una maana biashara hii inajulikana na kama inajulikana inafanyika vipi na akina nani wanahusika?
Iwe inasimamia ZMA ama taasisi yoyote ya JMT, ili kuondokana na kadhia hii siku nyingine, lazima meli zote zitakazosajiriwa zipewe sharti la kuhakikisha msajiri anapata uhakiki wa meli hizo zinasafirisha nini na kwa nani.
Umewahi kusoma sheria zinazoidhinisha usajili wa meli?
Uhakiki huo ujikite katika kuhakikisha meli hizo hazisafirishi ama kufanya biashara haramu ama kuvunja mikataba ama kuvuruga makubaliano tuliyoridhia ya kimataifa.
Pitia sheria zilizoanzisha mamlaka husika ujiridhidhishe unachosema hakipo au sicho kinachofanyika!

Kwa taarifa ya gazeti la mwananchi ZMA imesajili meli zaidi ya 400 na SUMATRA 88

Jiulize kwanini meli zisajiliwe kwa wingi Zanzibar?
Kuna incentive gani, na kwa wingi huo udhibiti unakuwaje. Jiulize, kwanini tatizo linajirudia eneo lile lile!

Bandiko 409 umenukuu hoja ya muungano pengine kwa kutotambua hili linaugusa muungano

Ukitazama wiki hii utaona Makamu wa Rais na Waziri anayehusika na muungano wakiwa pamoja
Gazeti la mwananchi limeeleza kuundwa kwa kamati na upande wa ZNZ atakuwa makamu wa pili wa Rais

Tazama mambo ya muungano, utaona kuna usafiri na usafiri wa anga, Bandari, posta , Mambo ya nje, Mambo ya ndani, Uhamiaji, biashara na mikopo ya nje, Mambo ya nje n.k.

Kwa mtazamo wa hayo machache, kuna Tanzania Maritime Authority (TMA) ambayo kwa uwepo ZMA inabaki kuwa ya bara na ZMA ya visiwani. Katika IMO inayojulikana ni United Republic of Tanzania

Tatizo la meli limegusa muungano kwasababu inayotoa maelezo ni Tanzania si SMZ au ZMA

Ukiviangalia vyote kwa jicho angavu na weledi utaiona hoja ya muungano na changamoto zake

Siyo suala jepesi la kupendekeza nini kifanyike, ni suala linalohitaji mtazamo mpana

Kwa uzito wake ndiyo maana imeundwa kamati kwa mujibu wa taarifa ya gazeti la Mwananchi
 
Sijakosea uamuzi wangu wa kukutambulisha kuwa mwalimu mkuu wangu hapa JF, Nguruvi3 .
====
Wahusika wazipitie hoja zako.
 
MWANASHERIA MAARUFU ZANZIBAR, JE, UMELITAZAMA HILI?

Katika bandiko [HASHTAG]#408[/HASHTAG] tulieleza suala la meli linavyoweza kuwa na hisia ndani yake katika mambo ya muungano
Tulihitimisha kwa kusema ' Je, kwa tukio la meli na bendera, Watanzania hatujajifunza matatizo mbeleni?

Imechukua siku chache kauli ya waziri wa sheria kuibua mjadala mzito.
Hili halitokani na kauli bali 'reservations' yaani manung'uniko yaliyokuwa yanatafuta mahali pa kutokea

Mmoja wa walioguswa na suala hilo ni mwanasheria Bwana Saidi kutoka Zanzibar

Saidi amekunukuliwa akisema ' Tanzania kuna wapiga kura milioni 50 na Zanzibar lakini tano, hivyo Rais anaweza kuchaguliwa bila kura kutoka Zanzibar na anaweza asifanye kampeni na bado akashinda'

Mwanasheria huyo anahitimisha kwa kusema 'Aliyechaguliwa na wenzetu ana mamlaka juu yetu''

Anachosema ni sahihi kabisa kuwa hivyo ndivyo inavyoweza kutokea.

Alichosahau ni historia
Kwamba ' Rais wa Zanzibar aingie katika baraza la mawaziri kama makamu wa pili wa Rais'
Ndivyo ilivyokuwa siku za nyuma tukiwa na makamu wa kwanza na wa pili, nalo ni jambo la kweli

Malalamiko anayosema mwanasheria huyo yalikuwepo upande wa bara.

Kwamba, Rais wa ZNZ anawezaje kuwa Makamu wa kwanza na kuwa na madaraka Rais asipokuwepo ikiwa hakuchaguliwa na watu wa bara ambao ni mamilioni akiwa amechaguliwa na wachache kutoka Zanzibar?

Lakini mwanasheria hakueleza makamu wa Rais wa JMT anatoka Zanzibar bila kupigiwa kura na upande wowote.

Pengine watu wa bara wangehoji zaidi, kwanini awe na mamlaka juu yao kwa jina la Uzanzibar?

Mwanasheria hakueleza kiini cha tatizo. Kwamba, meli zimesajiliwa na mamlaka za ZNZ kwa bendera ya JMT.

Mtunzaji 'custodian' wa bendera ya Tanzania ni Rais wa JMT

Ndiyo maana vyombo vya kmataifa viliitaka serikali ya Tanzania(JMT) yenye bendera kujibu tuhuma za meli .

Malalamiko kidiplomasia yatapitia wizara ya mambo ya nje ya JMT ambayo ipo chini ya Rais wa JMT

Masuala ya muungano yana mkanganyiko na yakiangaliwa kwa jicho la Uzanzibar na Ubara, yanazua maswali

Mathalani, kwanini Wazanzibar wadhani Rais wa JMT hana mamlaka kwa waziri wa SMZ ikiwa Wazanzibar wabunge wanaokuja Dodoma wanagharamiwa na serikali ya JMT inayoongozwa na Rais JMT na si SMZ

Mwanasheria pia angejiuliza. Inakuwaje Wabunge wa Zanzibar washiriki shughuli zisizo za muungano hata kuwa viongozi katika kamati za Bunge la JMT ambalo sehemu kubwa ya shughuli si za Muungano?

Kwanini wabunge kutoka znz wawe na mamlaka kwa mambo yasiyohusu Zanzibar pale Dodoma?

Ikiwa wazanzibar wanaingia kamati za bunge za mambo yasiyo ya muungano, kwa tafsiri ya kazi za Bunge ni kusimamia serikali ya JMT inayoongozwa na Rais wa JMT.

Vipi wao waweza ku 'overlap ' katika kusimamia serikali ya JMT wakati huo huo Rais wa JMT asiweze ku overlap pale masilahi ya JMT yanapoguswa hata kama ni kutoka ZNZ?

Hoja iliyopo ni kuwa suala la muungano liangaliwe kwa jicho pana na la muda mrefu SI ''kero'' ambazo hazijulikani zinaanishwa kwa kigezo gani na kutoka kwa nani

Je, kwa haya hatujifunzi kitu kuhusu muungano na pengine miongozo yetu ya kikatiba?

Tusemezane
 
MIAKA 54 YA MUUNGANO
TUMEFANIKIWA KUONDOA 'KERO' ZA MUUNGANO

Sehemu ya I

Tarehe 26 April ilikuwa sherehe ya muungano kuadhimisha miaka 54 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Nusu karne ni muda mrefu wa kutathmini muungano katika nyakati tulizo nazo, tulikotoka na twendako

Gazeti moja liliorodhesha tume(zaidi ya 15) zilizoundwa kushughulikiwa kinachoitwa kero za muungano
Kero za muungano ni lugha ya kisiasa inayolenga kubadili maana ya matatizo ya muungano

Ndani ya Bunge (JMT)hali ilikuwa tata, kukiwa kuna kutuhumiana kutoka kila pande hasa Zanzibar
Hakuna muungano uliokamilika kwa asilimia zote, hivyo kero si tatizo kubwa kama inavyoonekana

Tatizo kubwa ni hali ya mwiko 'taboo' ya kuongelea kwa uwazi matatizo ya muungano
Tatizo la pili ni muungano kufanywa kama suala la kundi na si la wananchi, maamuzi yakitengenezwa bila kuzingatia utashi , maoni au weledi na upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya watu

Tume zote zimefanya kazi kwa hadidu za rejea zinazotengenezwa bila kupata maoni ya wananchi kama wadau
Matokeo yake hakuna tume iliyokuja na mwarobaini wa matatizo

Hata kama kila tume ingepewa suala moja tu, kila uchao kuna tatizo linalojitokeza
Sababu kubwa ni ya kutokuwa na ujumla wa majibu 'holistic approach'

Tume ya Jaji Warioba kupitia maoni ya wananchi ilijaribu kwenda mbali ya zaidi ya tume nyingine
Tume ilitafuta jawabu la matatizo ya sasa na yanayoweza kujitokeza siku za baadaye

Kwa bahati mbaya, mchakato ukaingiliwa na wanaodhani muungano ni 'haki' yao zaidi ya wananchi

Matokeo ya kuvurugika kwa mchakato yameturudisha kule kule kwa kutafuta majibu ya reja reja
Majibu yanayotokana na kikundi cha watu wanaohisi wana majibu na si wadau ambao ni wananchi

Makosa hayo ndiyo yanayofanywa kwa sasa na waziri mwenye dhamana kwa kushughulikia kero akishirikiana na watu wa pande zote ambao hakuna anayeweza kujua wanatoa maoni kwa kuzingatia maoni ya watu gani

Kwa kuangalia hayo hapo juu, tutakuwa na mfululizo wa mabandiko kuhusu muungano na yanayojitokeza

Mabandiko yamelenga kujadili kwa uchache wapi tulipo na wapi tunakwenda

Bila kuwa na mjadala wa masuala haya kwa uwazi, ni kulea tatizo
Madhara yake, wasioutakia muungano wanasikika na hoja za kupotosha kuliko wenye nia ya muungano

Kuna uwezekano hakuna tatizo kubwa kama inavyodhaniwa, hata hivyo sauti chache za wapotoshaji zinasikika kwa nguvu na upotoshaji wao unaonekana kama ukweli, kwasababu hakuna anayesema ukweli kama mbadala

Inaendelea....II
 
TUMEFANIKIWA KUONDOA KERO ZA MUUNGANO?

Tumeeleza bandiko la awali kuwa hakuna 'holistic approach' kwa maana njia ya kutafuta majibu ya jumla
Kinachoendelea kwa sasa ni kutafuta majibu ya reja reja kwa kila kinachojitokeza
Ni njia dhaifu sana kwa kuzingatia mabadiliko yanayojitokeza kila siku duniani na katika jamii yetu

Udhaifu mkubwa zaidi ni ule wa kusikiliza kero zinazozuka tu kila wakati kwa vile hakuna formula ya kudumu
Kwa sehemu kubwa kero zimechakuliwa kama tatizo la Wazanzibar bila kujali hali ya Watanganyika

Kwa kutumia reja reja ya majibu, hisia ziliingia vichwani mwa Watanganyika wakitaka kuhoji, iweje wao waonekane kuwadhulumu au kuwaonea wenzao bila hoja zao kusikilizwa?

Tume ya Warioba iliona tatizo na kuweka kero za pande zote wazi
Kushindwa kwa tume ya Warioba kumeturejesha kule kule kwa hoja reja reja

Tunapoongelea hoja reja reja mkazo unakuwa kwa hoja za Wazanzibar na kusahau hoja za Watanganyika

Hata katika vikao, ni nani anayesimama kuzungumzia hoja za Watanganyika ikiwa wao ni JMT?
Waziri wa Muungano hawezi kuzungumzia kero za Tanganyika, hivyo kero zinazozungumzwa ni za Zanzibar

Hili linaweza kufanikiwa kwa muda mfupi, kwa muda mrefu litazua tatizo.Kero zitabadilika kutoka za Wazanzibar na itakuwa zamu ya Watanganyika. Hapo hali itakuwa ngumu kushughulikia reja reja zinazowahusu

Tuna mifano ya majibu reja reja yasivyojibu hoja za leo, kesho na keshokutwa

Rais wa awamu ya nne, alitangaza kutoa fursa kwa Zanzibar kufanya biashara za nje bila kushirikisha JMT ikiwa ni pamoja na uwezo wa kukopa. Akaondoa mafuta kama jambo la muungano

Swali, je hilo limeondoa kero? Jibu ni hapana na limekuza tatizo zaidi

Kwavile Znz inaweza kufanya biashara kimataifa,haki ya kupata soko la Bara inaangaliwa tofauti, kwamba, fursa ya hiyo inaweza kujenga 'uchochoro' utakaoinyima Tanganyika (Bara) mapato

Limeshazua mtafaruku, Wzn wakisema ni sehemu ya JMT(Tanzania bara) wakiangalia maslahi yao kwa upana

Uwezo wa kukopa; Fursa ni kuwapa Wazanzibar haki na uwezo wa kukopa bila kupitia JMT
Kutokana na hali ya kiuchumi, ni rahisi Zanzibar wanapokuwa na 'mdhamini'. Wao wanasema JMT iwe

Tanzania bara wanahoji, iweje waingie katika udhamini na 'mikopo na madeni' yaliyofanya nje ya muungano?

Kuondoa mafuta; Wznz wanalilia kuondoa mafuta katika mambo ya muungano kwa hoja ya rasilimali ya asili
Tanganyika wanasema, ikiwa ni hivyo kwanini gesi iwe sehemu ya JMT ambayo mapato yake yanakwenda znz?

Ugumu ni pale bomba la mafuta la km chache kwenda znz linapokuwa nje ya mjadala
Ikiwa mafuta ni ya wznz na si JMT, kwanini gesi ya Tanganyika iwe ya JMT?

Mifano hiyo michache ni kuonyesha jinsi majibu reja reja yanavyoacha maswali yasiyo na majibu

Inaendelea
 
Tatizo la msingi la muungano wetu ni kuujadili kama wazanzibar au watanganyika na siyo watanzania. Tunaujadili kwa watu tusiungana…tuajadili tukiwek moyoni uwezekano Wa kuuvunja.. Ni saws na watu wawili wanajadili amani huku akificha jambia mgongoni kwake
Pili muungano umetekwa na wanasiasa kama kitu chao… kauli kama tutaulinda muungano kwa nguvu zote.Unaulinda dhidi ya nani? Wananchi sasa wamekuwa adui wa muungano badala ya kuwa kitu chao cha kujivunia
 
TUMEFANIKIWA KUONDOA KERO?

Sehemu ya III
Kwasababu masuala ya muungano hayaangaliwi au kujadiliwa kwa upana , ukweli na uwazi, yanaacha nafasi ya wapotoshaji kuendeleza sauti na hata kufanya muungano kama kadhia na si faraja

Upotoshaji unafanywa na baadhi ya viongozi kwa makusudi au kwa kutoelewa hali ya muungano

Tuangalie hoja zilizoibuka bungeni siku za karibuni

1. Mbunge(ZNZ) na waziri mwandamizi wa zamani wa JMT alisema ''.....Sisi wabunge tunaowakilisha znz tunaonekana daraja la pili'' kama amenukuliwa sahihi

Hoja, mtu aliyekuwa waziri wa JMT na Mbunge wa JMT kusema anawakilisha ZNZ si sahihi

Wabunge ni wawakilishi wa Tanzania katika bunge la JMT. Hoja na masilahi yao wanalipwa kwa kodi za Watanzania. Hakuna Mbunge anayelipwa kwa pesa kutoka kanda, mkoa au jimbo lake

Kauli ya Mbunge na waziri huyo wa zamani inachochea hisia. Tanzania bara watahoji
a) Ikiwa uwakilishi wao unatokana na Uzanzibar, je, masilahi yao yanalipwa na SMZ?
b) Ikiwa wapo kwa Uzanzibar, iweje wachangie mijadala isiyo Znz au mambo ya muungano?
c)Ikiwa wapo kwa Uznz, kwanini wanakuwa katika kamati zinazoamua mambo ya bara yasiyowahusu?

2. Mbunge(ZNZ) kauliza ' Kuna wzn wangapi mabalozi na kwanini wapelekwe nchi za Kiarabu'

Hoja; mabalozi ni haki ya uteuzi ya Rais wa JMT, hakuna kigezo cha atoke eneo gani
Dr Salim Ahmed Salim ni Mznz aliyekuwa balozi hadi kugombea ukatibu mkuu wa UN
Aliporudi nyumbani alihudumia kama waziri wa mambo ya nje, ulinzi na waziri mkuu kabla ya kwenda AU

Muda wote aliungwa mkono kama balozi wa Tanzania na kupewa fursa kama Mtanzania na si Uzanzibar wake
Hoja ya mabalozi wangapi wanatoka ZNZ haina maana kwa mantiki yoyote, ni kujengea hisia kwa kukosa weledi

Lakini pia Mbunge huyo hapaswi kuongelea idadi ya mabalozi, anapaswa kuuliza ni balozi ngapi zinazohudumiwa na ZNZ? Kudai haki ni jambo jema, lakini haki inakuja na wajibu. Je, amejiuliza hilo?

3. Mbunge wa tatu akaja na hoja, kwanini wznz wanapelekwa nchi za kiarabu tu
Mabalozi ni wawakilishi wa nchi katika mataifa na si kanda au eneo
Ikiwa wznz wanafanya vema katika nchi hizo tukiangalia mazingira ya kiutamaduni n.k, kuna tatizo gani?

4. Mfuko wa pamoja: Hii ni hoja inayopotoshwa na italeta matatizo makubwa mbele ya safari
Wznz wanasema kuwepo na mfuko wa pamoja wa JMT. Kwamba, misaada na mikopo iweze kugawanya kwa haki

Kwa kuangalia hiyo 'joint account' kutakuja hoja nyingi kutoka bara kuliko mfuko huo

a) Unapozungumzia mfuko wa pamoja unaongelea kuweka na kutoa. Je, uchumi wa ZNZ unaweza kuleta usawa?
b) Kugawana misaada, hivi muungano wetu umejengwa kwa misaada? Isipokuwepo kitatokea nini?
c) Mfuko wa pamoja unahusu madeni, je, SMZ ipo tayari kuchukua dhima ya madeni na mikopo hiyo?

Hoja kubwa ya WZN ni misaada. Itakawepowekwa 'Formula' ni formula hiyo itatumika katika mikopo na madeni
Wabara hawawezi kukubali katika mioyo yao Formula ya misaada tu, mikopo na madeni itatakiwa pia

Katika kutengeneza formula ya misaada, mikopo na madeni, kutahitajika kuangalia mambo mengine ili kuleta uwiano.Mfano, formula gani inatumika katika kuhudumia taasisi za Muungano zikiwemo wizara na mashirika?

5. Kuna hoja wizara za muungano ziwe na ofisi bara na Zanzibar. Hili ni jema kwa jicho potofu
Kuendesha wizara ni gharama kubwa. Mfano, wizara ya ulinzi , mambo ya ndani, nje, na taasisi zingine
Kwa wakati huu, kodi za kuendesha wizara na taasisi zinatoka wapi? Je, SMZ ipo tayari kuhudumia ofisi nyingine

Hoja hii imelenga kuongeza gharama, lakini wanaoitaka hawaelezi gharama zinatoka wapi na kwa formula gani

Tumeyaeleza haya kwa ufupi kuonyesha upotoshaji unaowachanganya wananchi bila sababu zozote za maana
Na kwamba kazi ya kutatua kero kwa reja reja inazaa matatizo na kuwapa hoja wasioutaka muungano

Kama alivyochangia bantulile ,kujadili muungano ni suala la Tanzania na Watanzania
Kwa sasa inaonekana ni suala la kufariji na hivyo kuendelea kuwagawa Watanzania

Hatuwezi kukwepa mjadala kwa vikao vya watu wachache tena kwa kusikiliza upande mmoja
Hatuwezi kupata suluhu kwa suluhu za reja reja na siyo ujumla 'holistic approach'

Inaendelea..
 
TUMEFANIKIWA KUONDOA KERO ZA MUUNGANO?

Sehemu ya IV

Miaka 54 ya muungano imekuwa na misuko suko.
Waliozaliwa baada ya muungano wamerithi kero zilizoachwa na kizazi kilichotangulia

Haionekani kama kuna jitihada za kumaliza kero ili kuimarisha na kuuacha kwa vizazi vijavyo

Tukitaka tujenge muungano imara, ni vema kuurudisha kwa wananchi, wadau na walinzi
Kamati na tume zaidi ya 10 zimejaribu hazikufanikiwa,tunadhani njia hiyo itatupa majibu tofauti!!

Swali muhimu kwa wahusika. Kamati ya kero inawashirikisha akina nani, wamechaguliwa au kuteuliwa kwa mwongozo upi, wamepata maoni wapi na wanawashirikishaje wananchi

Kero hazitatuliki kwa kuchagua na njia ya reja reja. Kuunda mfuko wa pamoja si suluhu, kutazaa matatizo.

Mfuko huo utakuwa na formula,wananchi watahitaji formula maeneo mengine tena kwa uwazi

Bila uwazi, kutaamsha hisia kwa washirik
Mfano, suala la sukari limevuta hisia za uonevu-znz, kwa kupazwa tu na propganda
Mbunge wa bara alipojibu kwa hisia kama waleta hoja, ulizuka mtafaruku

Muungano unaweza kutokuwa na matatizo kama inavyoaminishwa na wapotoshaji
Bahati mbaya,wanaoeneza ubaya wana fursa kuliko wanoeleza faida

Hili limezidi kupotosha wenye ufahamu kidogo. Mfano, ni rahisi kusikia muungano ni jambo baya
Ukiuliza ubaya upo wapi, hoja utakazosikia ni za kufikirika, zinazojengwa kwa hisia na kusikia tu

Inawezekana kulinda muungano kwa namna zozote, hata hivyo kama hakuna dhamira na maridhiano manung'uniko yataendelea. Kitakachofuata ni kurithisha matatizo kwa kizazi kijacho

Itafikia wakati walalamikaji watachoka, wanaolalamikiwa watachoka
Kuita wachovu katika meza kutafuta muafaka ni jambo lisilo na matokeo mazuri. Wamechoka, watajadili nini?

Kuna mambo yanayoweza kufanywa kwa uchache, kuulinda muungano bila kauli bali kwa kanuni

1. Mjadala wa muungano uwe wazi tuachane na 'taboo', kwamba muungano haujadiliwi
Bila kujadili, tutafahamu vipi nini kilichomo mioyoni mwa wananchi?

2. Kupitia mjadala kutakuwa na elimu ikayobainisha changamoto, matatizo na faida zake

3. Mambo ya muungano yashirikishe wananchi ili kupata uthabiti wa hoja.
Ni kundi gani linaloweza kujua fikra za wananchi milioni takribani 50 bila kuzungumza?

4. Matatizo ya muungano yatafutiwe kanuni 'Formula' ya ujumla na siyo reja reja kama ilivyo

5. Kuna umuhimu wa kusoma taarifa ya Jaji Warioba tena na tena, kuna hoja nzito ndani yake

Muungano unaonekana kuwa imara na thabiti kijamii hasa kwa maingiliano na mahusiano ya wananchi. Ni jambo gumu kujadili utengano katika ngazi hiyo ya chini

Hata hivyo, ni vema kukumbuka kuwa muungano umeingia katika hatua nyingine ya udhaifu
Tulizoe kusikia malalamiko ya upande mmoja ambayo yameamsha sana fikra za upande wa pili

Udhaifu uliopo sasa ni manung'uniko ya pande zote hata kama hayasemwi hadharani kwa kuogopa 'taboo'
Hakuna ajuaye, ikiwa mmoja atasema ''nimechoka'' na mwingine akasema ni 'heri' nini hatma?

Tusemezane
 
REJA REJA YA KERO INAWEZA KUZAA KERO ZAIDI

Katika mabandiko ya nyuma tumeeleza utaratibu unaozungumziwa wa kumaliza kero

Imesemwa bungeni, kero zimeshughulikiwa na sasa imebaki moja ya mfuko wa pamoja 'joint account'
Huu ni mfuko wa sehemu mbili, yaani Tanzania bara na Zanzibar. Hao ndio wamiliki

Katika kutafuta kanuni ya mfuko 'Formula' kuna idadi ya mambo yatakayojadiliwa. mfano tu wa mjadala
a) Misaada: Hapa ni muhimu kanuni ikaanisha misaada ya nje na misaada ya ndani na kanuni inasemaje
b) Mikopo na madeni; Ni muhimu kuwa na kanuni ya kusimamia hayo. Ukikopa utalipa na ni jukumu ka wakopaji
c)Mapato: Endapo kuna mapato ya pamoja katika mfuko, kanuni ieleze ni kwa uwiano gani
d)Gharama na matumizi; Nayo pia yaonyeshwe, ni gharama zipi za muungano na kanuni inazigawa vipi

Mifano hiyo hapa juu inaweza kuonekana si muhimu na itatafuta njia rahisi ya kuridhishana

Hebu tuangalie huko nyuma ilikuwaje na tatizo liitatuliwa vipi

Kuna tume iliwahi kupendekeza kuwa malalamiko ya Zanzibar kuhusu ajira ndani ya muungano yajadiliwe
Ikapendekezwa ajira za muungano zigawanywe kwa 21% Zanzibar na 79% bara, (kama takwimu ni sahihi)

Kanuni(Formula) hiyo ilionekana kuondoa malalamiko yanayoitwa kero kwa Zanzibar
Kwa vile Formula haikuwa ya ujumla na ilitekelezwa katika kuridhishana si kutafuta ufumbuzi, tatizo bado lipo

Tanzania bara kuna hoja

Ikiwa kuna Formula ya kugawana ajira za muungano, iko wapi Formula ya kuonyesha jinsi gani Tanganyika na Zanzibar zinagawana gharama za
a)Kuendesha muungano
b) Kugharamia asilimia 21 na 79 za wafanyakazi waliopatikana kwa kanuni iliyotengenezwa

Kwa mfano huo, je, kero ya ajira imetoa jibu au imezua swali zito kuliko lililokuwepo?

Hoja hapa, mambo ya muungano yakiangaliwa haraka haraka na reja reja, yanaleta tatizo kuliko tatizo lililopo.

Ndio maana kuna swali, je, Formula ya joint account itahusu nini na kama itakuwa wazi kwa wananchi kuona bila kusikia tu kwa dhana

Tusemezane
 
HOJA YA MBUNGE WA SUMBAWANGA INA MANTIKI
TATIZO LA SUKARI LINAELEZA KITU ZAIDI YA 'KUONEWA'

Mbunge Ali Kessy alijibu hoja zinazohusu sukari kwa kutoa mifano.
Kwa minajili ya mjadala namba alizosema zinaweza kutokuwa sahihi, kama upo pungufu tunaomba radhi

Mh. alisema kontena la pikipiki linalipiwa 'milioni 40' bandarini Dar na ''milioni 5 likiteremsha Zanzibar'
Alionyesha kuwa endapo hakutakuwepo na ulinganifu upande mmoja utapoteza mapato yanaoendesha nchi

Tanzania bara ina watu takribani milioni '45' na soko kubwa kwa bidhaa za Afrika mashariki, Zanzibar ikiwemo
Kwa mazingira ya kijiografia Znz ni wanufaika wa soko hilo kwa kupitia muungano

Lakini pia znz ina mfumo wa kukusanya kodi unaohusisha TRA na ZRB. Moja ya vyanzo vya mapato ni TRA

Hoja ya Wazanzibar, sisi ni nchi moja na hivyo bidhaa zinaweza kusafiri eneo hadi jingine bila kodi ni mfu
Kwa kufanya hivyo na kwa viwango vya kodi tofauti, wakwepa kulipa kodi watatumia upenyo wa znz

Mbunge aliongea kwa hoja ya kujenga, kwamba, lazima uwepo uwiano wa biashara na kuziba mianya

Hata hivyo, kwa kutumia kigezo cha nchi moja, Znz itakuwa na wakati mgumu kuliko hoja wanayodai

Mfano tu kwa ajili ya mjadala. Ikiwa kodi ya kontena itakuwa ni 10% Tanzania bara na 5% Zanzibar, Bara wakipunguza kodi hadi 5%, hakuna atakayetumia Zanzibar na itaathiri uchumi wake

Bara watakuwa na haki hiyo kwa kigezo cha sisi ni nchi moja, tuwe na viwango sawa vya kodi ili bidhaa zikiteremka ZNZ au Bara ziingie sehemu nyingine ya nchi bila kikwazo

Kwa kutumia 5% kila upande,bidhaa zitapitishiwa bara, tayari ina soko la ''milioni 45''
Hoja ya wznz kuwa ni nchi moja ina ukweli na nzuri kwa kutumia kigezo kama cha sukari
Hata hivyo, hoja hiyo ikitumiwa na Tanzania bara , Zanzibar itakwama

Hoja ya sukari inajibu hoja za kupotosha katika muungano. Je, hakuna la kujifunza kwa hilo?

Je, soko la watu takribani milioni 45 ambalo znz ina access kuliko nchi nyingine si jambo jema?
Je, soko la ajira lililowaajiri wazanzibar nje/ndani ya mambo ya muungano bara si jambo jema?
Je, soko la ardhi lililohuru kwa wazanzibar kuliko watu wa taifa jingine si jambo jema kwao?

Kati ya njia za kuondoa malalamiko ya uonevu kutoka pande zote ni suluhu ya jumla'holistic approach' na kanuni zitakazoongoza 'Formula'.
Mambo ya muungano yaanishwe na yasiyo ya muungano yaanishwe pia

Lau ingeeleweka, na kwa kutambua Zanzibar wana uwezo wa kufanya biashara nje bila kupitia muungano, ingelikuwa rahisi kuwashauri kuhusu sukari.

Kwasasa ni ngumu, hoja ya wazanzibar sisi ni nchi moja ina mantiki
Hoja ya kwamba wanaweza kufanya biashara bila kupitia muungano ina mantiki?

Hoja ya Mh. Mbunge ina mantiki zaidi, tushirikiane kubeba muungano kwa hali na mali bila kuumizana na kwamba, ni wakati tuwe na kanuni 'formula' kuondoa manung'uniko ya pande zote

Tusemezane
 
TAASISI NDANI YA MUUNGANO

Yapo mambo yanayotajwa kuwa ya muungano kwa maana ya kuwa ya pamoja.
Mfano ni wizara ya ulinzi, mambo ya ndani, nje na ya muungano.
Katika hili kuna eneo moja tu linalokutanisha pande mbili
Kuna mashirika ya muungano mfano shirika la Posta. Hili linahudumia pande zote

Kuna taasisi za muungano, katika eneo hili kumekuwa na taasisi za Tanzania na za Zanzibar.
Eneo hili ni moja ya mambo yasiojadiliwa lakini mbele ya safari yanaweza kuleta 'kero' nyingine

Mfano,kuna bodi ya mikopo ya wanafunzi ya elimu ya juu (HESLB) ya Tanzania na Zanzibar(ZHESLB)
HESLB inashughulikiwa wanafunzi wote, ZHESLB ni ya wanafunzi wa Zanzibar tu
Gharama za kuendesha HESLB ambazo ni kodi za wananchi zinatoka eneo gani ?

Kuna Tanzania bureau of standards(TBS) na Zanzibar bureau of standards. Haya ni mashirika mawili ya viwango katika nchi moja. Inawezekana kabisa kukawa na uratibu wa shughuli za pande zote kwa pamoja
Je, siku ikitokea ZBS wakatofautiana na TBS katika viwango, mtafaruku unatatuliwaje?

Lipo shirika la umeme la Tanzania , kuna shirika la umeme Zanzibar.Ikiwa mashirika haya yanatoa huduma kwa njia za biashara, Tanesco na Zesco zinapaswa kufanya kazi kwa kutoa huduma na biashara zenyewe
Hata hivyo haya ni mashirika ya umma ya JMT na SMZ,ikitokea kuhitilifiana maana yake ni hitilafu ya serikali 2!

Kuna shirika la meli Tanzania na shirika la meli Zanzibar. Tunakumbuka mtafaruku wa meli zilizokuwa na bendera ya Tanzania zikiwa na 'kashfa' nje ya nchi. Utatuzi wa suala hilo ulihusu mamlaka za juu
Wazanzibar wakasema kulikuwa na 'kuonewa' kwa kufanya uhakiki wa meli zinazosajiliwa Zanzibar

Hili linaonyesha uzito unaoweza kutokea siku za mbeleni kuhusu taasisi zinazofanya kazi ndani ya muungano katika sehemu mbili tofauti zikiwa zimeundwa na vyombo tofauti na mamlaka tofauti.

Maswali ya kujiuliza. Kwanini baadhi taasisi za muungano ambazo zina mwenza kule Zanzibar ziwe na sharti la kuajiri watumishi kutoka Zanzibar ikiwa majukumu yana ukomo bara?

Hoja hapa ni kuwa rejareja ya utatuzi wa kero haiwezi kuwa na majibu ya jumla.
Kuna umuhimu wa kuwa na kanuni za jumla zitakazopambanua matatizo rejareja.

Tusemezane
 
VIDEO INAYOELEZA ZAIDI YA KILICHOZUNGUMZIWA
FIKRA ZA KIZAZI CHA SASA JUU YA MUUNGANO

Wazee waioasisi muungano walikuwa na malengo ya wakati huo ya muda mfupi na mrefu
Walitambua uhusiano wa karibu wa kijamii , kitamaduni, kisiasa na kijiografia baina ya Tanganyika na Zanzibar

Miaka zaidi ya 50 kizazi cha sasa hakielewi chanzo na madhumuni ya muungano achilia mbali faida zake
Kinachoelezwa ni matatizo ya muungano ambayo kwa ulinganifu ni machache kuliko faida zitokazonazo

Kuna kundi tulilosema linapotosha kuhusu muungano kwa hoja rahisi lakini zinazosikika na hasa kizazi hiki

Kulikuwa na video inayoonyesha watu watatu wakiwa nje ya nchi wakijadili masuala ya muungano
Alikuwepo aliyejitamulisha kama Mzanzibar (Mznz) na Mtanganyika (Mtg) na katikati akiwa mgeni(Mg)

Ukiitizama video hoja zinazozungumzwa ni za kawaida tu, lakini ndani yake zinaeleza kitu kikubwa hasa kwa kizazi cha sasa. Tuujadili mjadala huo katika Video ya 'karibu chai' kama kuna tunalojifunza

Kwanza, kuna makosa yanayofanywa na viongozi kwa kudhani kuwa kukaa peke yao na kujadili muungano ili kutafuta suluhu ya kero kutatoa majibu ya tatizo. Ni vema viongozi wakaangali jamii ina mtazamo gani na nini hasa chanzo cha matatizo badala ya kudhania tu kisha kutafuta suluhu peke yao bila kuijua jamii inasema nini

Mgeni(Mg) wa mjadala alisimama kati kueleza asili ya muungano na nini kinaweza kutokea iwapo hautakuwepo
Alieleza kwa nini uhusiano wa kihistoria baina ya pande mbili kabla ya uhuru
Alihoji, waliozaliwa nje ya maeneo yao asili watakwenda wapi ikiwa muungano hautakuwepo?

Mbara (mtg)akasema yeye angependa kwenda ZNZ kutembea tu . Aliita znz kama 'kitongoji'
Ukitafakari mchangiaji alimaanisha hana sababu za kwenda kuishi znz pengine kutokana na hali ya kiuchumi, ukubwa wa soko, ajira , ardhi na fursa zinginezo

Mznz alisema, Tanganyika inainyima znz fursa ya maamuzi. Baraza la wawakilishi lazima yapite Tanzania bara. Ingalikuwa si hivyo, ZNZ ingekuwa kama Dubai.

Alionyesha kero moja ya kutokuwepo kwa picha ya karafuu katika passport mpya zilizotolewa
Akasema muungano usipokuwepo waliozaliwa nje ya maeneo ya asili wataamua wapi wabaki

Ukimsikiliza kwa makini,utabaini hoja zake zimejengwa kwa kusikia na si kwa uhalisia.
Kwanza, si kweli kuwa maamuzi ya BLW lazima yapelekwe bara

Mwaka 2010 BLW lilifanyia marekebisho ya katiba yake bila kujali uwepo wa JMT.
Athari za mabadiliko hayo tunazifahamu na ulikuwa ukiukwaji wa katiba

Pili, BLW lina bajeti na wizara zake nje ya muungano na mipango hufanywa bila kushirikisha JMT
Tatu, uwepo wa kura ya maoni iliyotengeneza serikali ya umoja wa kitaifa (GNU) haikushirikisha JMT

Hoja ya kuingiliwa inajengwa kwa hisia na si uhalisia kama ambavyo mzanzibar huyo alivyoeleza

Inaendelea....
 
Back
Top Bottom