Duru za Siasa: Awamu ya 5 - Uongozi na Yanayojiri

Duru za Siasa: Awamu ya 5 - Uongozi na Yanayojiri

Sehemu ya II

Mzanzibar anasema nje ya muungano znz itakuwa kama Dubai.
Ni kweli kwani kila Taifa hupigania kuwa bora lakini mchangiaji haukuelewa historia ya Zanzibar, jiografia ya dunia n.k. Kukua kwa znz zama hizo kulitokana na uwepo wa makoloni na biashara kutoka makoloni hayo

Hali ya sasa ni tofauti, biashara ya vipusa haipo, utalii ni jambo la kushindaniwa hivyo kuhisi kuwa znz inaweza kuwa ile ya mwaka 1900 au 1800 bila kuzingatia mabadiliko ya dunia ni hisia na si uhalisia

Zao la karafu linazalishwa duniani na nachi zenye maeneo na teknolojia kubwa.
Zama za karafu kutoka znz pekee hazipo tena kama ilivyokuwa kwa zao la Mkonge Tanganyika

Mbunge Zitto alieleza, mawese yalipelekwa Malaysia na mwingereza,Malaysia ndio mzalishaji wakubwa duniani

Nne, Jiorafia ya Dubai na ZNZ ni tofauti. Dubai inapowekeza katika biashara ya meli inapendelewa na jiografia Znz ipo neutical miles 90 kutoka Dar es Salaam, na karibu sana na Mombasa Kenya au Tanga

Disadvantage ya Znz katika ukanda huu ni soko. Ushindani wowote wa kibiashara utakumbana na nguvu ya soko
Makampuni yaliyowekeza znz yanahamia Tanzania bara kwasababu ya nguvu ya soko na ukubwa wa uchumi

Kudorora kwa bandari ya ZNZ ni kwasababu ya uwepo wa bandari zingine katika ukanda ambazo nguvu ya soko inatoa faida kwao. ZNZ iliwahi kutangaza uwepo wa bandari huru. Je, hilo limesaidia chochote?

Tano, kuhusu passport kutokuwa na picha ya karafuu, hili nalo linashangaza.
Passport ni hati ya kusafiria tu ambayo si kila mtu anaitumia. Hati hiyo haiwezi kuwakilisha kila kitu ndani ya nchi

Alichoshindwa kuelewa ni umuhimu wa jina la Tanzania. Kwamba mzanzibar mwenye passport ya Tanzania amefungua milango yake popote Tanzania, iwe Mtwara, Kigoma, Sumbawanga au Arusha

Utanzania unasaidia wazanzibar malaki wasioweza kusafiri kuliko wachache wanaosafiri na kuhitaji picha ya karafuu tu kwasababu ya kujitambulisha ni Wazanzibar

Hoja ya mwisho ilikuwa Utanzania na Uzanzibar, tutajadili sehemu inayofuata

Inaendele...
 
Sehemu ya III

Mchangiaji kutoka bara alikerwa na hulka ya Wazanzibar kutotaka utambulisho wa Tanzania bali Uzanzibar. Pengine hakuelewa kuwa Zanzibar wanataka kulinda hadhi yao ya Uzanzibar !!!

Ni kweli, wazanzibar nje ya nchi hupenda kujitambulisha kwa uzanzibar na siyo Utanzania
Utanzania wanauhitaji tu pale wanapokuwa na masilahi yao, na hilo ndilo huenda limemkera ''Mbara'' huyo

Kuna kitu ambacho wazanzibar pengine wa kizazi hiki hawaelewi.
Mgeni wa mjadala huo bwana Mkandara alieleza vema sana Znz ilivyoundwa na, washirazi, wachina, Watanganyika n.k. Huu ndio ukweli wa visiwa vingi duniani, si znz, Seychelles, Caribbean n.k.

Tatizo la kuukataa Utanzania ni kubwa kwa Wazanzibar kuliko Watanzania bara. Wznz wengi wanaishi bara.

Wazanzibar wanapojenga mbegu ya Uzanzibar, tayari wanapanda mbegu ya kubaguliwa wao wenyewe

Kwa mfano, fursa zote wanazopata ndani ya muungano ambazo si za muungano kama ajira za taasisi, mashirika au wizara za muungano,ardhi n.k. ni kwasababu ya Utanzania wao.

Pindi wakijiita Wznz, fursa wanazopata zitajadiliwa kwa muktadha huo.
Kwamba, kwanini Mzanzibar apate fursa abcd akiwa si Mtanzania au Mtanzania bara!

Pamoja na hoja, kuna kitu ambacho baadhi ya wazanzibar hawakioni.
Mwl Nyerere alisema nje ya muungano hakuna znz kuna wazanzibar na wazanzibar.
Maneno ya Mwali yanaishi na yanajitokeza kila siku

Mfano, mzanzibar anayetaka uwepo wa muungano anasemwa huyo si mzanzibar ni asili yake ni Tanganyika
Hata kama ana rangi gani, midhali anazungumzia muungano kwa kuupenda, huyo si Mzanzibar

Halikadhalika, ubinafsi huo umepelekea majibu ya 'machotara'
Kwamba, kama ni chotara, huyo si Mzanzibar, ni mgeni kutoka nje, na hajui maana ya Mapinduzi

Uzanzibar upo wapi?

Tuhitimishe kwa kusema, video ilikuwa na mjadala mwepesi na wa kawaida.
Kwa undani na kuitakari kuna jambo kubwa zaidi. Kero zinazosema ni sehemu tu ya tatizo si tatizo halisi

Kuna haja ya kueleza haya mambo kwa uwazi, na kwa mijadala ya ili kukiweka kizazi hiki katika kile kinachosemwa 'informed decision' ili watu waelewe faida na hasara na watakapoamua wawe na weledi

Mawazo ya wachangiaji katika video hiyo yanawakilisha jamii, siyo mapungufu ya mtu au watu

Viongozi husika, ''joint account'' haiwezi kuwa jibu, ongeeni na wananchi, wasikilizeni, muwajibu, mkubaliane nao au mpingane nao, waelimisheni n.k. Hiyo ni sehemu ya kutafuta majibu

Tusemezane
 
SWALI LA MABALOZI LINAJIRUDIA, HII NAYO NI KERO?

Ndani ya baraza la wawakilishi, kumeulizwa swali kuhusu teuzi za mabalozi na kwanini wapo ''9 katika balozi 41''
Waziri husika wa SMZ alilijibu ingawa hakueleza kwa kwa ufafanuzi na kina

Katika mabandiko yaiyopita tulizungumzia reja reja ya kutatua kero za muungano.
Moja ya kero hizo ni account ya pamoja 'joint account' kati ya JMT na SMZ.
Tulisema account si tatizo na haiwezi kuwa dawa ya jumla (panacea)

Kila uchao kutakuwa na madai mapya hasa kutoka Zanzibar ambayo kwa namna nyingine yanaleta fikra upande wa bara

Wakati swali lnaulizwa muulizaji pengine angejiuliza bajeti ya wizara ya mambo ya nje ipo wapi katika bajeti ya SMZ?

Uteuzi wa mabalozi ni kazi ya Rais wa JMT na wala hakuna vigezo vya kijamii ukiachilia vile vya kidiplomasia
Rais atateua mabalozi kwa mujibu na mamlaka aliyo nayo bila kujali, eneo, jinsia au chochote

Bajeti ya wizara ya mambo ya nje inapitishwa Dodoma ambako kuna wawakilishi kutoka Zanzibar

Kama kuna swali linalohusu uteuzi wa mabalozi, swali hilo linazua maswali mengine
Haki na wajibu ni vitu pacha , hivyo kudai haki tu hakutoshi ni muhimu wajibu ukaonekana pia

Kwa Wazanzibar kutaka uwiano wa mabalozi ni kuzua hoja kwa upande wa bara, kwamba, ikiwa wanahitaji uwiano huo basi fursa nyingine nje ya muungano zitazamwe ili kulinda maslahi iwe ya Tanganyika. ZNZ tayari wanasheria zao

Kuna sababu gani ya kudai mabalozi bila kujiuliza wazanzibar wangapi wanapata fursa Tanzania bara bila kujali uwiano?

Swali hilo nalo linatupleka kwingine, je, wale wazanzibar ndani ya taasisi, wizara na mashirika yasiyo ya muungano nafasi zao ziangaliweje? Madai kwasababu tu ya uzanzibar yanalazimisha upande mwingine uangalie maslahi yake.

Ikitokea kwa mfano , mabalozi 41 wakagawanywa sawa, halafu Tanganyika wakadai fursa nje ya muungano zisijadiliwe, ongezeko la mabalozi 12 kufikia 20 litafidiwaje na maelefu ya wznz wanaofaidika na ajira nje ya muungano?

Maswali hayo yakiachwa tu bila kuelezwa itafika mahali wazanzibar watadai kwanini hakuna uwiano wa ma-DC na RCs!

Rasim ya Jaji Warioba ilijaribu kutenga mamlaka kwa kuchelea mambo kama haya. Kwamba, yawepo mambo ya muungano na yawekwe wazi, yasiyo ya muungano Tanganyika iangalie masilahi yake kama ilivyo kwa Zanzibar

Tusemezane
 
MWAKILISHI AZUNGUMZIA KATIBA YA JMT na SMZ(2010)
ADAI KATIBA ILIYOPO IFANYIWE MAREKEBISHO KWANZA!

Mwakilishi wa jimbo la Tunguu ameonekana katika TV Zaima akitoa maoni yake kuhusu tofauti za katiba akilenga kuelezea nafasi ya Waziri kiongozi na Makamu wa pili wa Rais. Mwakilishi Simai Mohamed said anasema

''Mwaka 2010 Zanzibar ilifanya marekebisho ya vifungu vya katiba. Iliondoa nafasi ya Waziri kiongozi na kuweka Makamu wa pili wa Rais. Katiba ya JMT inamtambua Waziri kiongozi. Hivyo Marekebisho yafanywe ili inapotokea Makamu wa pili anahudhuria sherehe za muungano atambuliwe hivyo na si kama Waziri kiongozi kwa mujibu wa katiba ya JMT''

Simai amesema kuna umuhimu wa kurekebisha katiba ya muungano ili iakisi mabadiliko ya katiba ya Zanzibar 2010 wakati mchakato wa katiba ukisubiriwa.

Jambo hili linaonekana kama kero na kama alivyosema Simai ni muhimu kuendelea kutatua kero ili kuimarisha muungano

Kuna mambo Wazanzibar huyafanya kisha kulaumu muungano bila sababu yoyote. Hili ni mojawapo

Mwaka 2010 Zanzibar ilipofanya mabadiliko ya katiba haikushirikisha JMT. Kikubwa kilichochagiza mabadiliko ni kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa na kuondoa suala la mafuta katika mambo ya muungano!

Marekebisho yalifanywa haraka bila kutilia maanani uwepo wa katiba ya JMT ambayo kwa namna moja au nyingine ina mwingiliano na katiba ya Zanzibar. Tunakumbuka hili lilileta malalamiko ingawa Tanzania bara hawakulishikia bango.

Ndani ya bunge la JMT kuna wabunge kutoka Zanzibar na Wabunge kutoka baraza la wawakilishi.
Hawa ni kiungo cha sshughuli za pande mbili katika kuleta uwiano.
Kuna Baraza la wawakilishi lililojadili na kupitisha katiba ya ZNZ 2010

Mkaundi hayo matatu hakuna hata moja lililoona umuhimu wa kushirikisha mabadiliko ya katiba ya znz 2010 ndani ya JMT
Hoja ingepelekwa Bunge la JMT kusingekuwa na tatizo kurekebisha kifungu husika kwa kubadili mjina tu

Vipi leo muungano unalaumiwa na kuiita hii kama kero ikiwa ni tatizo lililotengenezwa na Zanzibar yenyewe?
Bunge la JMT lingejadili suala hili kwa kutumia kigezo gani ikiwa hakuna aliyetaka lijadiliwe kutoka ZNZ?

Pengine Bunge la JMT lingejadili wapo ambao wangesema ' ni kuingilia mambo ya Zanzibar'

Je, hiyo nayo ni kero kweli? Na ''joint account'' inayosemwa itatua vipi hoja reja reja kama hizi?

Tusemezane
 
KERO ZA MUUNGANO
MALALAMIKO MENGINE YANAWEZA KUJITATUA YENYEWE

Kuna msemo wa mitaani usemao 'hata mbuyu ulianza kumea kama mchicha'
Msemo huo unashabihiana sana na ule usemao 'mdharau mwiba guu huota tende'

Kuhoji muungano ni jambo lenye afya iwapo hoja zitolewazo zina mashiko na tafakuri
Tumeona hoja ambazo badala ya kujibiwa pengine kwa udhaifu wake, zinazua mengine

Wizara inayoshughulikia mambo ya muungano ipo chini ya ofisi ya Makamu wa Rais
Dhima kubwa ya wizara ni kutatua kero za muungano ikiwa kama msuluhishi

Swali, tunapongelea mfuko wa pamoja wa fedha, nani anawakilisha Tanzania bara?

Hoja ya nyingine ni ile ya Zanzibar kudai uwepo uwiano wa teuzi za mabalozi
Swali, je kuna uwiano wa idadi ya watu katika majimbo ya wabunge wa ZNZ na Bara?

Mbunge wa Bara anaweza kuwakilisha watu milioni 1, Waznz pengine laki moja
Uwiano gani unaoongelewa hapa? Kwanini uwiano wa mabalozi na si uwakilishi wa watu?

Yapo malalamiko yanayoweza kujitatua bila nguvu bali busara.
Wazanzibar wanalalamika mambo ya muungano kuongezwa '11 hadi zaidi ya 30'
Swali, katikati mambo hayo nani anayefaidika ?

Mfano, ipo wizara ya elimu ya Tanzania ambayo kimsingi ni ya bara. Ipo ya Zanzibar
Kuna baraza la mitihani la Tanzania, Zanzibar wanabaraza lao na mfumo wao
Kuna bodi ya mikopo ya elimu ya juu Tanzania HESLB na Zanzibar ZHESL

Ili kuondoa malalamiko kwanini shughuli za wizara elimu zisitengwe kwa kila upande?

Kinachotakiwa ni uwiano tu wa elimu, kwamba, mwanafunzi wa ZNZ anayedhaminiwa na ZHESL akitaka kujiunga na vyuo vya bara, akidhi mahitaji na Wabara pia wakidhi ya znz
Kufanya hivyo kutaondoa malalamiko ya pande zote

Malalamiko yataondoka kwasababu Bara itakuwa na mitaala yake ya elimu, itadhamini wanafunzi, mabaraza ya mitihani yatatathmini wanafunzi wa Tanzania bara tu

Zanzibar watakuwa na mitaala yao, watawatathmini kwa vigezo vyao

Bara hawana sababu ya kuhoji udhamini wa wanafunzi wa znz ikiwa ZNZ hawatoi udhamini kwa wanafunzi wao na kwamba hilo si jambo la muungano.

ZNZ hawatalazimika kuwa katika mambo yasiyo ya muungano yanayosemwa 'yameongezwa kinyemela' kama kero, na itakuwa imeojiondoa bila malalamiko

Kwa ufupi taasisi zenye mbadala znz zitenganishwe ili kupunguza malalamiko ya kuongeza mambo yasiyo ya muungano.

Mathalani,kuna sheria na wizara ya ardhi ZNZ, Wizara ya ardhi ya JMT ishughulike na mambo ya bara tu. Hili lisiwe jambo la muungano na kila upande ushughulike na yake

Wabunge kutoka Znz wasishiriki katika kamati za kisekta za bunge kwa mambo yasiyo ya muungano. Hili litasaidia kupunguza idadi ya yale yanayosemwa yameongezwa kinyemela

Swali kubwa tunaloliacha leo ni hili, kwa ongezeko la mambo ya muungano Tanzania bara wananufaika vipi na Zanzibar wanadhulumika vipi?

Tusemezane
 
MALALAMIKO YANAYOWEZA KUJITATUA
Sehemu ya II

Kwa mujibu wa katiba ya JMT ya 1977,nyongeza ya kwanza, imetaja mambo ya muungano
Miongoni mwake ni ; Takwimu, utafiti, utafiti wa hali ya hewa, usafiri na usafirishaji wa anga,elimu ya juu,leseni ya viwanda na Takwimu, baraza la taifa la mitihani, mikopo na biashara za nje'' na mengine

Tumeeleza kuhusu elimu ya juu inayoweza kuondolewa na kuondoa manung'uniko
Tanzania bara na Zanzibar kila mmoja ina vyombo vinavyoweza kushugulikia hilo
Je, hii si kero inayoweza kujitatua yenyewe?

Utafiti, utafiti wa hali ya hewa ni huduma kwa jamii na hutegemea ruzuku kujiendesha
Kuwepo katika mambo ya muungano kuna faida ipi kwa Bara kiasi cha znz kuona yameingizwa kinyemela na huenda kuwanyima fursa?

Kuhusu leseni za viwanda na takwimu. Je, hili nalo haliwezi kuijitatua kwa kuacha kila upande uendelee na mipango yake?Kuna upande upi unaofadika kwa kulifanya jambo la pamoja?

Kuna taasisi mbadala, mfano TFDA na ZFDB, TBS na ZBS, Zanzibar Maritime Authority na Tanzania Maritime Authority na mengi orodha inaendelea

Ikiwa ni hivyo, mambo yanayolalamikiwa na Zanzibar ni ya 'kinyemela' ni yapi?
Na kwanini yasiwekwe bayana kuwa haya ni ya Bara na haya ni ya Zanzibar?

Ingekuwa vema Wazanzibar wakaanisha manung'uniko yao kwa maelezo ya kina ili tuone wapi kuna tatizo. Kusema tu 'yameongezwa kinyemela' bila kuonyesha yanaathiri vipi si haki.

Swali, elimu ya juu na mikopo ya wanafunzi kupitia HESLB inaathiri vipi ustawi wa Zanzibar?

Tunayajadili haya kwa sababu hizi;
kwanza, kuonyesha kuwa malalamiko yanayoelezwa kuhusu nyongeza ya mambo ya muungano yanapaswa kutolewa na Bara kwa kuzingatia uzito wa kuyasimamia!

Pili, malalamiko ya Zanzibar kutokuwa na maamuzi yana shaka.Ni kwa vipi ikiwa mabadiliko ya katiba ya znz 2010 hayakuzingatia Katiba ya JMT katika baadhi ya vipengele?

Hoja kuwa ZNZ inanyimwa fursa ndani ya muungano inahitaji maelezo mengine ya kina vinginevyo hoja hiyo ni dhaifu. Kama yupo mchangiaji atueleze ni fursa zipi wanazonyimwa

Tatu,kunaandaliwa mfuko wa pamoja, mambo yasiyoeleweka yanasimama vipi yataleta tatizo. Mfuko kama ulivyoelezwa kikatiba utakuwa wa mgawanyo wa mapato, na madeni.
Bila kujua kipi kipo upande upi formula itazua tatizo mbeleni

Mfano, Wazanzibar wakisema TBS au TFDA si vyombo vya pamoja,wana vyao, je, huduma za vyombo hivyo zitapata mgao kutoka wapi au vitachangia eneo gani ikiwa vina mapato?

Tusemezane
 
TAASISI MBADALA NA 'KERO'

Tumeeleza kuhusu taasisi mbadala za Tanzania bara na Zanzibar.
Miongoni ni shirika la umeme Tanzania bara (TANESCO) na shirika la umeme Zanzibar (ZECO)

Kwa upande wa Bara kuna taasisi inayoangalia bei za nishati (EWURA) bila kuingia Zanzibar

Bajeti ya Serikali ya mapinduzi ZNZ 2017/2018 imeeleza deni la umeme linalodaiwa
Waziri wa fedha SMZ anasema kutOlipwa kikamilifu au kabisa kunatokana na sababu kadhaa(uk 27) kama;

1. Madeni ya ndani ya ndani ya wateja ikiwemo SMZ
2. Kutokubaliana TANESCO na ZECO na wakati mwingine msimamizi wa bei bara (EWURA)

Waziri alisema deni la kibiashara linalokubalika ni Tzs Bilioni 65 zinazopaswa kulipwa
Katika kupunguza deni SMZ imeomba JMT kulipa bilioni 18 kutoka PAY kwenda SMZ

Pili, JMT ilipe TANESCO Bilioni 2.2 ZECO kwa taasisi za Muungano ziliopo Zanzibar

Tukiangalia hoja hizo tunaweza kuona matatizo ya taasisi mbadala na jinsi zinavyokuwa kero

1. Biashara kati ya TANESCO na ZECO ni huduma na makubaliano ya kibiashara
ZECO inaposhindwa kukusanya madeni ya wateja/SMZ kwanini liwe tatizo la TANESCO?

Gharama zinazotokana na kushindwa kwa ZECO zinafidiwaje katika kuendesha Tanesco ?

2. Ni kwa vipi bei zinazopangwa na EWURA kwa Tanzania bara zinaathiri mkataba wa biashara kati ya TANESCO na ZECO?

EWURA si taasisi ya muungano na haiwezi kuingia katika makubaliano kati ya taasisi mbili tofauti za muungano zinazofanya biashara.

Kwanini itumike kwa 'bargaining'! Zanzibar inaitambua EWURA? Jibu ni hapa, EWURA inagiaje!

3. Hoja ya kwamba PAYE ya SMZ inayoidai JMT ilipwe Tanesco nayo inachanganya
PAYE inayosemwa ni ipi? Ile ya wafanyakazi kutoka Znz ndani ya muungano (21%)?

4. Ikiwa ZECO wanadai taasisi za muungano zilizopo ZNZ, nini wajibu wa SMZ katika kugharamia shughuli za muungano?
Taasisi zilizopo bara zinahudumiwa kutoka mfuko upi kati ya JMT na zile za bara pekee?

Hoja si uwepo wa taasisi tofauti, kwa hakika ni sehemu ya kumaliza kero.

Kinachotatiza ni pale pasipokuwepo na uwazi au mpaka wa taasisi za muungan

Mfano, ZNZ wanaiona 'Tanesco na Ewura' kama taasisi za muungano penye masilahi yao
Wakati huo huo ZNZ ina taasisi zake nje ya muungano!

Ni kwa msingi huo, kuainisha taasisi za muungano na zile za Bara na ZNZ kwa uwazi kutasaidia kuepuka matatizo yasiyo ya lazima na kupunguza kinachoitwa kero

Lakini pia tunaona ugumu wa mfuko wa pamoja maana haieleweki mchango wa bara ni upi wa ZNZ ni upi na wapi sehemu mbili zinakutana kuendesha JMT

Swali la leo, wanaouliza uwiano wa teuzi za mabalozi, wanasemaje kuhusu uwiano wa gharama kama za umeme kwa taasisi za muungano?

Tusemezane
 
TAASISI YA EWURA NA ZURA!

Katika mwendelezo ule ule wa taasisi mbadala lakini moja ikiwa ya Tanzania, kuna EWURA na kule Zanzibar kuna ZURA iliyoanzishwa kwa sheria 7/2013

Tulihoji iweje mkataba wa TANESCO na ZECO uhusishe bei zinazopangwa na EWURA?
Je kuna uwezekano bei zikaathirika kutokana na bei za ZURA?

Vyombo hivi ni tofauti na mashirika ya umeme, mikataba haiathiriwa na vyombo hivyo
Zanzibar kudai bei irekebishwa kwa kuangalia bei zinazopangwa na EWURA haina mantiki

Kwa mujibu wa bajeti ya SMZ iliyotolewa na waziri, deni la umeme la 2.2 Bilioni la taasisi za muungano zilizopo Zanzibar linapaswa kulipwa na Jamhuri ya muungano
Je pande mbili zinachangiaje muungano?

Hazina inatengaje' kodi' kuhakikisha Bara na Znz zinachangia gharama za muungano?

Biashara kati ya Tanesco na Zeco inaingiaje katika mambo ya muungano?

Uwepo wa mfuko wa pamoja ni jambo jema kabisa hasa kwa Tanzania bara.
Tatizo ni itakaposhindikana kutenga shughuli za muungano na gharama kwa kila upande

Kwavile shughuli za muungano zitakuwa za pamoja, zile zisizo za muungano ni vema zikaangaliwa na kutengwa ili kutobebesha upande mwingine gharama zisizo na tija

Kwa mfano, shughuli za kamati za Bunge ziangaliwe kwa jicho hilo.
Kuna sababu gani za kamati zisizo za muungano kuwa na wajumbe kutoka Zanzibar?
Kamati kama( kilimo , mifugo na maji)( hesabu-serikali za mitaa)(ardhi, maliasisi na utalii)

Katika hilo suala la ajira nalo litazamwe kwa kutenga za muungano na zile za washirika

Huo ndio uwiano mzuri ambao Zanzibar wanautaka na hakika una unafuu kwa pande zote

Mfuko wa pamoja ni jambo la kuungwa mkono na hasa Tanzania bara.

Mfuko utasiaidia kuanisha kipi cha muungano na kigharamiwe vipi na si 'misaada' tu

Mfuko huo kama hautaweka mambo kwa uwazi na haki, kutakuwa na malalamiko mbeleni

Tusemezane
 
VIDEO HII!

Mwakilishi Wa CCM Aukosoa Vikali Muungano Wa Tanganyika Na Z'bar- Muungano Wa Aina Gani Huu - Mzalendo.net

Tupitie hoja za mwakilishi (BLW) katika video tujiridhishe na maudhui yaliyomo.

Kama tunavyosema mara nyingi, muungano hauna tatizo kama inavyosemwa.
Kuna tatizo katika kuelewa dhana yake na ujenzi wa hoja pale penye tatizo

Ujenzi wa hoja ni wa kishabiki ukibeba mantiki dhaifu na mihemuko
Kuna nyakati kutoelewa au mihemuko inafichwa chini ya 'zulia' la kero za muungano

1. Mwakilishi katika video ameongelea suala la biashara kati ya ZNZ na Tanzani Bara.

Kwa wazanzibar, Tanzania si jina zuri na hata kutaka wanaoupenda utanzania wao waitwe Watanganyika ili kuhalalisha hoja ya kejeli ya 'Ukoloni'. Tukubaliane na lugha hiyo

Hoja: Kwa wazanzibar kuukataa Utanzania ni kujibagua kwa gharama zao

Ni vipi mwakilishia anahoji 'muungano gani' ikiwa alishaukataa kwa Uznz na Utanganyika!

Uwepo wa pande mbili unajenga anachokiona si sahihi kwa watu wa nchi moja.
Ni muhimu akubali Utanzania ili hoja ya biashara ndani ya nchi moja ijadiliwe, kinyume chake tutaongelea Tanganyika na ZNZ na si muungano.

2. Mwakilishi anasema ZNZ ni chuo, vyama vingi na matumizi ya dola yameanzia huko na kwamba ZNZ ni kitovu cha biashara tangu enzi.
Anasema, ukiacha karafuu na utalii kingine kilichobaki Zanzibar ni biashara

Hoja: Mwakilishi anaishi katika zama za historia.
Zama za dunia ya leo historia inabaki kuwa somo na haiwezi kuwa dira.

Ni hoja kama zile za Zanzibar kuwa nchi ya kwanza kuwa na TV ya rangi! Kwahiyo?

Ni kweli ZNZ ilikuwa kitovu cha biashara karne iliyopita
Biashara a utumwa, vipusa na pembe haipo tena. Zama za karafu kutoka hazipo.

Biashara imefunguka kwa kila wajasiriamali eneo zima la A.Mashariki
Kilichoonekana kwa mwakilishi ni kuwa 'disorganized' kwa kutojua ajenge vipi hoja

3. Mwakilishi anasema bandari D'salaam mafuta yanatozwa dola 3 kwa nchi za jirani,Znz inayotozwa dola 10, anahoji sukari imekataliwa kuingizwa,huu ni '' muungano gani'' !
Hatuna uhakikiki wa madai hayo lakini tuyaangalie kama alivyoyaleta

Kama ni kweli , mwakilishi angeuliza ni sababu zipi zilizopelekea tofauti anayosema.
Mambo hayatokei tu! alijikita katika kubabaika na historia ya znz bila kuanisha sababu

Mwakilishi anahubiri Utanganyika na Uzanzibar akitaka fadhila za muungano wa Tanzania. Ukishajitenga tayari umepunguza nguvu ya muungano na hapa kuna pande 2

ZNZ wana mamlaka za leseni, viwanda na biashara kwa masilahi yake, Tanganyika pia
Huwezi kuwa na mamlaka tofauti halafu ukabaki na muungano pale tu unapoutaka

Leseni za biashara na viwanda ni jambo lililopo katika mambo ya muungano.
Zanzibar waliliondoa bila hata kutaka marekebisho ya katiba kwavile tu walitaka

Leo tatizo la sukari na mafuta linashughulikiwaje kama suala la muungano ?
Kwanini mafuta na sukari liwe jambo la muungano na si leseni za viwanda na biashara?

Ni kutokana na hali hiyo ya Utanganyika na Uzanzibar iliyojengwa na Wazanzibar tena wakiita ukoloni, inalazimu kila upande ulinde malasilahi yake

Haiwezekani viwango tofauti vya kodi, tozo za bandari, leseni na biashara ziwe tofauti halafu utofauti huo utumike kama uchochoro wa kusingizia muungano

Bidhaa haziwezi kuingizwa znz na kuletwa bara katika viwango tofauti vya gharama.

Kukubali hilo ni kuua biashara za bandari na kodi ambazo kwa Tanzania bara ndizo zinaendesha muungano. Muungano si kero, bali matumizi yake ni kero

Mbunge Ali Kessy alitoa hoja Bungeni akisema kontena la spea za pikipiki linagharimu milioni 5 znz na milioni 40 bara. Nani atashusha mzigo bara? Ushindani utakuwaje?

Inaendelea....
 
VIDEO-MWAKILISHI
Sehemu ya II

3.Mwakilishi anasema , kutoruhusiwa kuingiza mafuta na sukari kutoka ZNZ kunafunga soko la Afrika mashariki tena kwa ndugu wa damu

Hoja: Mwakilishi atambue ZNZ ilishapewa 'ruksa' ya biashara za nje na mikopo n.k
Na kwamba, ZNZ inaweza kufanya biashara na nchi yoyote zikiwemo za Afrika mashariki.

Hakuna soko lililofungwa, bado wanaweza kuuza sukari na mafuta popote

Wakati wakiita Tanganyika mkoloni, bado wanataka kupata fadhila za muungano
Inakuwaje znz wamtake 'mkoloni' Tanganyika katika soko na si kujinasua kutoka kwake?

4. Mwakilishia anasema, ikiwa bidhaa za ZNZ zinazuiwa, basi bidhaa kama bia, saruji na nondo kutoka Bara nazo zizuiwe kuingia ZNZ

Hoja: Tunasisitiza, muungano hauna tatizo pengine kuna tatizo katika weledi

Kwa hali ya kijiografia znz ipo katika kivuli cha Tanganyika ndani au nje ya muungano. Huo ni ukweli isipokuwa kwa waliogoma kuukubali

Kivuli kinatengenezwa na mambo ya kijamii, biashara, utamaduni na idadi ya watu
Soko la ZNZ linategemea Tanganyika si nchi nyingine katika uchumi , ajira n.k.

ZNZ ni soko dogo kwa bara , watu 1.8 Milioni ukilinganisha ni 45 milioni

Mwakilishi anaweza kumshawishi waziri wa SMZ kuzuia bidhaa za Tanganyika kama hatua za kulipa kisasi kama anavyosema 'nipe nikupe, jaza ujazwe'

Hilo litafanyika kwa gharama ya Wazanzibar bila athari kwa Tanganyika
Wazanzibar watanunua bidhaa hizo kutoka kwingine kwa gharama kubwa

Mkoa mdogo Tanganyika kama K'njaro una watu zaidi ya milioni 2 na nguvu ya kiuchumi. D'Salaam ni takribani 5 milioni, Mwanza karibia na idadi hiyo kama ilivyo Arusha au Mbeya

Hivyo mwakilishi haelewi bidhaa za kwenda znz ni kwa faida yao na kwamba kuzuia kutawalazimu tu wanunue kwingine pengine kwa bei ya juu bila athari kwa Tanganyika

Tishio la mwakilishi likimataka waziri wa biashara na viwanda znz aangalie uwezekano wa kuzuia bidhaa kutoka bara halikuzingatia weledi wa biashara, jiografia na nguvu ya soko

Inaendelea....
 
VIDEO YA MWAKILISHI

Baada ya kujadili hoja za mwakilishi zilizojengwa kwa hisia na hamasa tuangalie tatizo linaanzia wapi. Kero zinasemwa hazina uhusiano na suala la muungano, ni za kuumba tu

Taasisi za muungano na ambazo zimefanya kazi katika muundo huo zinapotengenezewa mbadala zinapoteza nguvu ya muungano na kubaki za Tan Bara na Zanzibar

Tatizo linapotokea likihusisha mbadala wa taasisi si tatizo la muungano na si kero

Linakuwa ni tatizo la mashirikiano nje ya muungano. Tuangalie mifano michache

Wizara ya biashara znz na T.bara.
Hizi ni mamlaka mbili tofauti zikiwa na majukumu tofauti kuzingatia uanzishwaji wake.
Suala la mafuta na sukari ni mfano mzuri

Tungalikuwa na wizara moja, waziri wa JMT angelishughulikia kama tatizo ndani ya wizara
Kwavile linahusu wizara mbili tofauti, kila waziri atatekeleza majukumu ya mamlaka yake

Waziri wa znz ata promote interest za znz na wa Tanzania bara ata defend interest za Bara
Katika hali hiyo hakuna mwenye makosa wala kero, ni utaratibu unaofanya kazi

Mfano wa pili
NECTA ni baraza la mitihani Tanzania. Zanzibar wana council yao na mitaala yao ya elimu
Mifumo ya elimu kwa Tan Bara na Zanzibar ni tofauti.

Kuundwa kwa baraza znz kunaacha NECTA iwe ya Tanzania bara. Tayari kuna pande mbili

NECTA ndiyo yenye jukumu la kutathmini viwango vya wanafunzi kujiunga na vyuo

Jukumu la NECTA linaelekeza wanafunzi kutoka znz na bara watahiniwe sawa kuleta uwiano wa viwango kwani mbele ya safari wote watatahiniwa na vyuo kwa usawa

Hivyo NECTA hawalazimiki kutathmini wanafunzi wa znz, kinachotokea ni znz kutaka kutathminiwa na NECTA ili kukidhi vigezo vya kujiunga na vyuo Tanzania bara

Ikitokea wanafunzi wa znz kufeli na kuilamu NECTA si sahihi.
Wanafunzi hao wana hiari ya kutahiniwa na baraza la znz, wakijua ili wakubaliwe bara, lazima wakidhi viwango vya NECTA. Hapa 'ukoloni' au kuonewa kunatoka wapi ikiwa hiari ipo?

Ndivyo ilivyo kwa TBS Vs ZBS.
Kuundwa kwa ZBS kunaifanya TBS iwe mamlaka ya bara
Zote zimeanzishwa na mamlaka tofauti na majukumu yake kulingana na sheria iliyoanzisha. Kuwepo kwa tofauti ya utendaji si kero ya muungano

Kimantiki, viwango vya TFDA au TBS au NECTA vinaweza kukataliwa znz bila hisia za uonevu
Ndivyo ilivyo kwa bara pia kwani mamlaka zina haki sawa katika kulinda na kutetea masilahi

Orodha ya taasisi ni ndefu, hizo chache ni kwa minajili ya mjadala tu

Badala ya kubeba hoja na kuzipachika jina la kero za muungano, watu wajiulize, wajiridhishe na waelewe nini tatizo. Muungano unafanya kazi pale penye muunganiko, kinyume chake kunakuwa na pande mbili zinazoweza kushirikiana au la

Masuala ya muungano yasichanganywe na mashirikiano.
Mambo ya muungano yanatekelezwa kisheria, nje ya hapo ni mashirikiano tu ambayo ni makubaliano ya kuridhiana ikiwa yana masilahi kwa wahusika


Tusemezane
 
HOJA YA MWAKILISHI KUHUSU TV
Katika video iliyotangulia, mwakilishi wa BLW anadai, ''mtu akiteremka na TV moja bandarini analipishwa kodi na kwamba ya lakini moja anaweza kulipishwa mara mbili''

Hii ameiita kero ya muungano na kumpelekea kuhoji ni aina ''gani ya muungano''

Kazi ya serikali ni kukusanya kodi kuhakikisha wanunuzi iwe wa ndani au nje wanalipa kodi. Kulipa kodi ni wajibu wa raia mwema

Tatizo ni pale ambapo kodi haitachukuliwa kwa baadhi ya watu,wengine wakitozwa

Kwa wasafiri wanaoteremka bandari au viwanja vya ndege bara, suala la kodi za mizigo limekuwa ni 'kero' baadhi wakisema kuna vitu hutozwa kodi ikiwa ima thamani ni ndogo au ni vya kawaida kwa matumizi au zawadi. Haya ni malalamiko ya wananchi wote si wazanzibae tu

Malalamiko ni ya wasafiri waliobahatika kutoka nje na yanayotokea kila siku katika maeneo ya kuingia nchini 'port of entry'. Hiyo si kero ya muungano hata kidogo

Mtu anaposafiri na TV kutoka Mwanza kwenda Arusha, au D'Salaam kwenda Mbeya hatozwi kodi kwasababu alishalipia katika mamlaka husika na hapa tuseme TRA kwa bara

Mtu huyo huyo akiingiza TV kutoka Kenya, Mbeya, Kigoma au Mtwara atalipia kodi kwasababu inaingia nchini kwa mara ya kwanza, kama yule aliyenunua Samora avenue

Zanzibar wana TRA na Zanzibar revenue Board(ZRB) zinazokusanya mapato kwa SMZ
Ikiruhusiwa mtu kuingiza TV kutoka Zanzibar kama yule anayetoka Mbeya kuja Dar kuna tatizo

Maana yake ni kwamba TV zitaagizwa kupitia Zanzibar na mtu anaweza kuvusha moja moja kila siku, mchana na jioni na kuweka dukani
Zipo TV zinazogharimu hadi milioni 4 au 6 kutegemeana na model na Technology

Mtu akiingiza TV moja, mchana na jioni kila siku kutoka Znz, kwa mwezi ni TV 60 bila kodi
Kodi zote atakuwa amelipa Zanzibar ambayo ina mamlaka zake, si TRA Bara

Kutakuwa na uwiano gani wa biashara kati ya muuzaji aliyeingiza kupitia bandari au viwanja vya ndege vya Tanzania bara na kulipia kodi na huyu aliyeingiza kwa njia 'bubu'?

Leo gazeti moja la kila siku limemnukuu kamishna wa mapato ZRB akisema mapato yanaathirika kutokana na uwepo wa bandari bubu. Je ububu huo hauwezi kuathiri TRA bara?

Mwakilishi aelewe, tunapokuwa na mamlaka tofauti kila upande uta promote na ku defend interest zake kwa faida ya watu wa eneo husika.

Muungano hauwezi kutoa mwanya au uchochoro wa kuathiri biashara na mapato ya upande mwingine. muungano haujawa tatizo na hili si kero kama mwakilishi anavyotaka umma uamini


Tusemezane
 
SAKATA LA BIASHARA
WAZIRI(ZNZ), MAKAMU II(ZNZ), MAKAMU WA RAIS (JMT)
IMTENGENEZWA 'HOTLINE' YA KUSAIDIA WAFANYABIASHARA ZNZ

The Guardian tarehe 4 2018 limemnukuu waziri wa viwanda na biashara Zanzibar, balozi Amina akisema ' SMZ inashirikiana na mshauri (consultant) Trade mark East Africa kuangalia sababu za kushuka mauzo ya bidhaa za Znz kuingia Tanzania bara

Waziri kasema mauzo yameshuka kutoka Bilioni 87.4 hadi 36.4 katika mwaka 2017
Mauzo ya bidhaa kutoka bara yameongezeka kutoka Bilioni 134 hadi 206.4 mwaka

Bidhaa zinazouzwa bara kutoka visiwani ni marashi, maji, maziwa na MAGARI
Kutoka bara ni nafaka, vinywaji na dawa

Ushauri unaotafutwa ni kuhusu NTBs (Non tariff barriers), vikwazo visivyohusiana na tozo (kwa tafsiri isiyo rasmi) vinavyokwaza biashara kati ya JMT na ZNZ!!!

Waziri anasema kumetengenezwa 'hotline' kati ya ofisi ya Makamu wa pili wa Rais Znz na Makamu wa pili wa JMT, kwamba,wanaokwazika wafikishe taarifa

Taarifa ya TCCIA imeeleza vikwazo (NTBs) kwa nchi zote za EA na si Zanzibar pekee

Tuzipitie hoja hizo za bandiko linalofuata

Inaendelea II
 
HOTLINE YA KUSAIDIA WAFANYABIASHARA WA ZNZ
Sehemu ya II

Hoja:

Kwanza, Kwa mujibu wa chama cha wenye viwanda na biashara (TCCIA) tatizo la NTBs si la ZNZ linaonekana kulalamikiwa na Ea
TCCIA imeeleza kwa kina maeneo husikaVipi Zanzibar wadhani wanalengwa wao?

Pili,Zanzibar wanasema Muungano unawatia umasikini, vipi waone Tanzania bara kama eneo muhimu la biashara?Je,kufanya hivyo si kumwendekeza 'Mkoloni' na umasikini ?

Tatu, Zanzibar imeruhusiwa kufanya biashara za nje( ingawa katiba haijarekebishwa).
Ni kwa vipi soko la T.Bara ndilo linawakwamisha ikiwa wanaweza kuuza EA yote?

Nne, Zanzibar haina kiwanda cha magari, haya yanaoingia bara yanatoka wapi na kwanini yaingie Zanzibar kisha bara? Kwanini yasoteremeshe sokoni Bara?

Tano, tumeeleza huko nyuma uwepo wa waziri wa viwanda na biashara Znz unamfanya waziri wa biashara wa muungano awe waziri wa biashara na viwanda Tanzania bara

i) Kwanini wafanyabiashara wapewe hotline kati ya Makamu wa pili wa Rais Zanzibar na Makamu wa pili JMT. Je, nani anatetea masilahi ya 'Tanganyika'?

ii)Kwanini hotline isimhusishe waziri wa viwanda Tanzania?
Kwanini waziri ofisi ya Makamu wa pili anayeshughulikia muungano hakuhusishwa ?

iii)Kwanini hotline itengenezwe kutoka BLW na Si Bunge la JMT ambalo wznz wamo?

Kama ulifuatilia mjadala ndani ya BLW, wawakilishi ''walimshambulia'' waziri wa viwanda na biashara Mh. Mwijage na kumfanya kama kikwazo cha biashara za Zanzibar.

Hii inatokana na Mh Waziri kufanya kazi nzuri ya kuziba mianya ya uchochoro wa kwa kisingizio cha muungano na kukwepa kodi hata kulinyima taifa mapato

Kinadharia, ''kumetengenezwa'' utaratibu kwamba, waziri wa viwanda znz atapokea malalamiko ya wznz na kuyafikisha kwa makamu ZNZ na kisha makamu JMT

Ikitokea hivyo, Waziri wa viwanda na biashara Tanzania bara, au Kamishana wa mapato watakuwa na sauti gani kwa kauli itakayotoka juu kwa Bosi?

Kama kunatakiwa ufumbuzi, suala lifikishwe bungeni na wabunge wa znz
Hoja ijadiliwe na wabunge wote ili kupata muafaka kama lipo tatizo kwa pande zote

Hili la kumwacha waziri Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais Muungano, na Waziri wa viwanda na biashara Tan. bara, linatengeneza mazingira ya kuhojiwa 'motive' yake na halipo sawa

Nani anawatetea wafanyabiasha wa Tanzania bara katika mazingira haya ya 'hotline' inayowahusu Wazanzibar pekee kwa biashara inayohusu Tanzania bara?

Hotline ya wafanyabiasha wa bara ni ipi, nani anashughulikia?

Zanzibar undertaking study to identifying non tariff barriers kwa hisani ya The Guardian

Tusemezane
 
Mh. DUNI HAJI WA CUF NA HOJA ZA KUDIDIMIZWA ZNZ

Video dakika 3.05
Video [HASHTAG]#436[/HASHTAG] Mh Duni anaanza kwa kusema lengo la muungano ni kuididimiza Zanzibar
Hoja hiyo ameirudia mara nyingi hata pale anaposhindwa kuweka ukweli unaomgusa

Lengo la mbandiko si kushawishi umma kuhusu kupenda au kutopenda muungano

Lengo ni kuweka rekodi, umma uweze kutafakari wakati unapozungumzia muungano

Dak 8.09 Duni anazungumzia kuundwa kwa tume ya pamoja ya fedha.
Anasema lengo ni kuweza kubaini mchango unaoingia katika shughuli za muungano tu

Dak 12.35 anasema tume ni kwa faida Zanzibar, ndiyo maana haijatekelezwa

Dak 14.35 anasema tume inapaswa kuanisha mapato ya muungano, mikopo na misaada zikiwemo taasisi za muungano

HOJA 1
Kama lengo ni kuididimiza ZNZ Duni alipaswa kuwaeleza watu ni kwa sababu zipi
Kuhusu tume ya pamoja, ni kweli hili ni jambo zuri si kwa znz bali Tanganyika

Ukisoma uzi tulioweka bandiko # 436 kuhusu hoja za Mh Zitto zinazohusiana na malipo ya 1.5 Trilioni ambayo ameeleza, kuna hoja nzuri sana kuhusu muungano

Kwamba mapato yanayokusanywa ZNZ kwa mujibu wake hayavuki bahari.
Hapa Zitto anatueleza mapato ya TRA ZNZ yanabaki kwa SMZ na hayaingi JMT

Lakini pia kwa mujibu wa aliyekuwa mjumbe wa tume ya Warioba ambaye sasa ni katibu mwenezi wa CCM Humphrey Pole pole aliandika katika gazeti la Mwananchi haya

Polepole anasema utafiti ulionyesha kwa miaka 30 znz haikuchangia katika muungano

Na kumbukumbu zinaonyesha aliyekuwa waziri wa fedha wakati wa Mh Mkapa aliwahi kusema kuna wakati mishahara ya wafanyakazi wa SMZ ilitoka hazina Dar es Salaam

Kuna kitu kinaitwa budge support ambayo SMZ imekuwa inapewa kutoka Hazina Dar

Kwa mantiki hiyo, duni anaposema tume haijatekeleza majukumu yake yupo sahihi.
Kwa upande mwingine, tume ingetekeleza vipi ikiwa ZNZ haichangii katika muungano?

Mh Duni anapaswa kueleza mchango za ZNZ katika muungano kabla ya kulalamika ZNZ inadidimizwa. Ni kama vile anasema ZNZ inachangia na kunyimwa, si kweli

Ukweli wa hoja ya tume ya pamoja ni mzuri kwa Tanganyika, kwasababu utawezesha kuona misaada inagawanywaje, mapato yanatoka wapi na kiasi gani, na tunagawana vipi gharama za uendeshaji wa muungano.

Na kupitia tume ya pamoja tutaweza kuondoa mambo kama elimu ya juu ambayo Tanganyika inagharamia wanafunzi wa znz zaidi kuliko SMZ inavyowadhamini
Tutaondoa mambo ya ajira yasiyo ya muungano, ardhi na kero zingine

Tume ya pamoja ni nzuri iungwe mkono na Wabunge wa Tanganyika ili ifanye kazi vema

Inaendelea.....
 
DUNI HAJI...
Sehemu ya II

Video# 436 Dakika ya 16.30 Mh Duni anatoa mfano ' Kama kuna sh 100, matumizi ya muungano hayazidi asilimia 35. Asilimia zilizobaki (65 ni kwa mambo ya Tanganyika)

HOJA 2
Mh Duni anapotosha, alitakiwa aeleze taasisi za muungano zinagharama kiasi gani

Kwa mfano, bajeti ya ulinzi na usalama ni zaidi ya Tsh ni pungufu kidogo ya Trilioni 1
Kiasi hicho ni karibu na bajeti nzima ya SMZ ambayo ni Trilioni 1 na kidogo.

Kuna wizara ya Mambo ya ndani, nje, taasisi za muungano n.k. ambazo kwa pamoja zina bajeti zaidi ya Trilioni 2. Kwa maneno mengine ni Zaidi ya Bajeti ya ZNZ

Mh Duni anaweza kutueleza ni kiasi gani ZNZ inachangia katika muungano ikiwa tumeelezwa mapato ya ZNZ yanabaki huko.

Kwa maneno mengine mapato hayaingii hazina ya JMT ndiyo maana, kwa mujibu wa Mh Zitto hayaonekani katika ukaguzi. Kwa mantiki hiyo mchango wa ZNZ haupo

Pengine Mh Duni angesema, katika sh 100, zote ni mapato ya Tanganyika, hivyo asilimia 35 anayosema inamegwa kutoka Tanganyika. Anayepaswa kulalamika ni Tanganyika

Lau kama si kweli, Mh Duni aeleze kwa Bajeti ya ZNZ 2017/2018 ambayo ni 1.081.4 ni kiasi gani kimetumika katika shughuli za muungano?

Lakini pia tukichukulia maneno ya Duni kuwa ni asilimia 35 ndiyo inayotumika katika muungano, kwa Bajeti ya 1081.4 Trilioni ZNZ inaweza kuchangia kiasi gani katika kuendesha taasisi au wizara za muungano?

Mh Duni, asilimia 35 anaweza kuiona ni ndogo kwa namba. Hebu tufikirie kuwa asilimia 35 itatoka katika bajeti ya Trilioni 20(Namba kwa minajili ya mjadala), kiasi hicho ni 7.5 Trilioni

Mathalan tukiweka 7.5 Trilioni kama gharama za muungano, tukatoa misaada na mikopo n.k. tukabaki na Trilioni 3, Zanzibar ikiwa na bajeti ya Trilioni 1 itachangia kiasi gani?

Mh Duni ni muhimu aangalie namba kwa uhalisia na si hisia.

Kwa uchumi wa ZNZ hata kama matumizi ya muungano ni asilimia 20 bado Tanganyika itabeba mzigo mkubwa na si kufaidika kama anavyosema

Inaendelea...
 
YA Mh. DUNI HAJI

Sehemu ya II

Video [HASHTAG]#436[/HASHTAG] Dakika ya 19.21 Mh Duni anasema kila jambo la ZNZ linapelekwa bara
Katika Dak ya 20.20 Mh anasema matumizi ya Tanganyika 80% ni mapato ya Muungano

HOJA 3
Mh Duni anaposema kila jambo la ZNZ linapelekwa bara ana hoja ya nguvu na mantiki

Hatuoni sababu za baadhi ya mambo kama Ardhi, Ajira, Elimu ya Juu, Mikopo ya wanafunzi HESLB, Biashara, Bandari, Afya, Utalii, Usafiri wa Anga n.k. kuwa ya muungano

Yote na mengine ni kuwabebesha mzigo Watanganyika, kwani Wazanzibar hawahitaji

Kuyaondoa katika muungano ni kumtua mzigo Mtanganyika, mzigo usiomsaidia
Kwahili, Mh ana hoja na ni muhimu Wabunge wa JMT kutafakari kuyaondoa kabisa

Kwa upande mwingine, Mh Duni hana ufahamu wa mambo yalivyo licha ya kuwa kiongozi.

Hakuna taasisi ya muungano isiyo na mbadala Zanzibar. Hapa tumkumbushe kidogo

Bunge JMT-BLW, TRA-ZRA, TFDA-ZFDB, TBS-ZBS, TMA-ZMA, NECTA-ZEC, TMO-ZMO, EWURA-ZURA. Hizi ni taasisi chache kumwezesha Mh kupata ufahamu kabla ya kuongea

Anayepaswa kulalamika kuhusu taasisi ni Tanzania bara. Katika taasisi ambazo sasa ni za Bara pekee kuna Wazanzibar wanaingia kama taasisi za muungano japo si za muungano
Ni vema Mh akaelewa, mambo ya Tanganyika ndiyo ya muungano , ya znz ni ya znz

Ushahidi ni pale mapato ya TRA hayavuki bahari kuja hazina, sasa Duni anaposema kila la ZNZ linapelekwa katika muungano, ni lipi au yapi hayo?

Mfano mzuri,Wabunge kutoka BLW wanoingia Bunge la JMT kwa gharama za muungano
Hakuna Mbunge wa bara anayeingia Baraza la wawakilishi hata kwa bahati mbaya

Wabunge kutoka ZNZ wanashiriki shughuli za Bunge zinazohusu mambo ya bara pekee.

Ni kwavipi Mbunge wa ZNZ achangie wizara ya Kilimo, Afya,Serikali za mitaa, Mifugo na Maji, Utalii. Elimu na Elimu ya juu ikiwa si ya muungano na hayawahusu?

Ni kwanini Wabunge wa ZNZ wanaingia kwenye kamati za Bunge kukagua shughuli za Tanzania bara zisizo wahusu kwavile si za Muungano?

Ni kwanini Wabunge kutoka ZNZ walipwe kwa kukaa Dodoma,ikiwa yapo yasiyowahusu?

Duni anaweza kuonyesha SMZ inagharamia shughuli za Wabunge kutoka ZNZ wa JMT kwa kiasi gani na kama hakuna pesa hizo zinatoka wapi?

Hoja yake kuwa matumizi 80% ya Tanganyika yanatoka muungano ni ya kweli.
Ukweli ni kuwa kwa miaka 30 kutokana na tafiti ' kwa mujibu wa mwandishi ZNZ haijachangia muungano. Mh Zitto katueleza, mapato ya TRA ZNZ hayavuki bahari

Asilimia 100 ya uendeshaji wa muungano ni jukumu la Tanganyika kwa mujibu wa Duni
Kuna ubaya gani Tanganyika ikichukua asilimia 80% ya kipato chake na kutoa 20% kwa mujibu wa Duni kwa Muungano?

Hapa pia Mh Duni anazidi kujichanganya tu, awali alisema gharama za muungano ni 35%. Kwa mantiki ya 80% kwenda Tanganyika gharama za muungano ni 20%.
Yaania anababisha takwimu ili kuhadaa umma

Inaendelea...
 
HOJA ZA Mh Duni wa CUF

Tunaendelea tulipoishia katika mkipindi cha wiki tatu. Kwa muda huo, mengi yametokea hasa kuhusiana na mbandiko ya taasisi za Muungano na malalamiko ya Zanzibar. Tutajadili mbeleni

Tukimalizia hoja za Mh Duni, tungependa tumsikie akitoa takwimu kuhusu mambo yafuatayo
1. Ni kiasi gani Zanzibar inachangia kuendesha muungano ili kupata picha halisi dhidi ya malalamiko yake

2. Ni kiasi gani anapendekeza misaada inayopewa Tanzania igawanywe, na kwa kigezo gani?

3. (a)Ni kiasi gani Zanzibar inachangia katika kulipa deni la Taifa linalotokana na mikopo
(b) Nini kinazuia ZNZ isikope ikiwa tayari imeruhusiwa kufanya hivyo
(c)Kwanini JMT iwe mdhamini wa mikopo ya ZNZ na si Zanzibar yenyewe?

4. Kiasi gani cha VAT kinakusanywa Zanzibar na kuletwa hazina Dar es Salaam

5. (a)Kwanini BLW lisipitishe sheria ya kukataa wanafunzi wa ZNZ kupewa mikopo na HESLB
(b) Ni wanafunzi wangapi wa bara wanadhaminiwa na ZHESLB? na kama hakuna, kwanini

6. Ikiwa ZNZ imeondoa mafuata na gesi yanayotoka ardhini katika muungano, ni kwanini Wazanzibar wasipewe madharti ya umiliki wa ardhi kama wageni wengine katika ardhi ya Tanganyika ambayo kwa mujibu wa Duni si ya muungano?

7. Ikiwa ZNZ inapata 21% ya ajira za muungano, ni kiasi gani SMZ inachangia katika gharama za wafanyakazi wa muungano kutoka Zanzibar

8. Ni kwanini Wazanzibar wanaoteuliwa katika taasisi za muungano zilizobeba sura ya Bara pekee wanakubali teuzi hizo na hao Wazanzibar wanamwakilisha nani?

9. Kwanini Wabunge wanaowakilisha ZNZ hawagharamiwi na SMZ ikiwa tunataka kugawana mikopo, gawio la BoT na ZNZ inakusanya kodi zake bila kuleta katika muungano?

Hayo ni machache tunayodhani Mh Duni anapaswa kuyaeleza kwanza. Kutanguliza hisia za kuonewa kwa takwimu za kupikwa ni kuwadhulumu Wazanzibar haki ya kuelewa

Lakini pia hoja za Mh Duni zingine zina mantiki zizingatiwe.
a. Ajira zisizo za muungano ziachwe kwa Watanganyika kama ilivyo kwa Wazanzibar
b. Mambo kama umiliki wa ardhi yaondolewa kila upande uwe na sheria zake
c. Taasisi kama za mikopo ya wanafunzi HESLB zisiwe za muungano
d. Zanzibar ibebe jukumu la kuhudumia taasisi kama wabunge wanaokuja Dodoma

Hoja nyingi za Mh Duni zinamanufaa kwa Tanganyika na zitazamwe kwa jicho mujarabu

Tusemezane
 
YAMETIMIA, ZANZIBAR WAOMBA KUSAMEHEWA VAT!

Kwa wanaofuatilia mabandiko, hivi karibuni tumeeleza kuhusu taasisi mbadala za Zanzibar
Moja ya taasisi hizo ni ZEC ambayo kwa bara ni TANESCO

Tulieleza kuhusu deni la umeme ambalo waziri wa ZNZ anasema limelipwa sehemu ikiwa ni marejesho ya kodi za wafanyakazi.Imechukua mwaka na bado kukamilika

Majuzi bungeni kulikuwa na kizaazaa,Wabunge wa Zanzibar kulalamikia kuhusu VAT

Kwamba ZNZ inatozwa VAT mara mbili kwa maana ya umeme Tanesco na ZECO
Wanasema hilo limeogeza gharama na hata Mahoteli kutumia majenereta

Suala zima limerudishwa kujadiliwa na serikali za Muungano na ile ya Mapinduzi Zanziabar

Kwa mtazamo wetu, tatizo limesababishwa na Wazanzibar ingawa wanalalamika ni muungano. Tulieleza, uwepo wa Taasisi mbadala ni tatizo kwa znz wala si muungano

ZECO ikishanunua umeme , Tanesco hawana biashara nao.
ZECO hutoza VAT kwa mujibu wa sheria za SMZ, na imeelezwa VAT ya ZNZ haivuki bahari. Kwa mantiki hiyo ZECO na SMZ ndio wanaotoza VAT si muungano wateja wao

Hoja ya kuondoa VAT kwa umeme wa Tanesco ni kutaka umeme uende Zanzibar bila kodi
Mwanasheria mkuu kasema VAT si jambo la muungano, na hilo wazanzibar walielewe

Kupeleka umeme bila VAT ina maana kwamba, ZECO watatoza VAT wateja wa Zanzibar na VAT hiyo itaingia katika mapato ya SMZ siyo ya muungano.

Kupungua kwa mapato ya serikali ya muungano kunamaanisha jambo moja, kwamba kutatafutwa vyanzo vingine vya mapato na hapa mlipaji ni Mtanganyika.

Wakati Tanganyika ikibeba jukumu la kuendesha muungano, kuinyima mapato ni kuwabebesha Watanganyika mzigo unaopswa kubebwa na SMZ na ZECO

Kuna jambo moja Serikali ya mapinduzi inaweza kufanya.
ZECO waondoe VAT kwa wateja ili kuwapunguzia gharama si kutegemea Tanesco

Tanesco haina uhusiano na Znz zaidi ya kuuzia umeme.
Umeme ukifika Znz ndio mwisho wa kazi ya Tanesco

Zanzibar pia ifikirie nani anahudumia miundo mbinu ya kupeleka umeme huko na kama hakuna makusanyo ya kodi, ni vipi umeme utakuwa sustainable bila kodi

Tatizo la bei ya umeme ZNZ ni la SMZ na ZECO

Wakae pamoja wamalize tatizo lao bila kusingizia muungano na bila kumbebesha Mtanganyika mzigo kwani Tanesco inapohudumia miundo mbinu ni gharama za bara

Jambo moja zuri lililojitokeza katika mjadala huo ni Wazanzibar kuomba kusamehewa VAT, hawakudai au kutaka kwavile wanajua hawana haki katika hilo

Hili si kero na iwapo znz wanadhani umeme ni ghali, wana nafasi ya kutumia jenereta
Hakuna sheria inayowalazimisha kununua umeme wa Tanesco

Kwa mujibu wa AG sheria inasema umeme ukitoka nje ya Tanzania unalipiwa kodi
Wazanzibar hawataki utanzania na wana taasisi zao kama ZECO, umeme ushatoka nje

Uwepo wa ZECO umewasaidiaje? Wangekubali Tanesco haya yangetokea?

Tusemezane
 
Back
Top Bottom