Duru za Siasa: Awamu ya 5 - Uongozi na Yanayojiri

Duru za Siasa: Awamu ya 5 - Uongozi na Yanayojiri

TATHMINI (iii)
Kuwachukulia hatua watu wanaoandika hisia zao ziwe sahihi au la ni kujinyima fursa

Hao ni wachache , haijulikani wangapi wana mtazamo huo. Njia nzuri ni kushinda nyoyo nyingi 'win the heart' ambapo fursa ipo kuliko kufukuzana na wachache

Mashirika kama CIA, FBI, M15, Scotland Yard, KGB n.k. yamo katika mitandao yakisoma hisia za wananchi ili kupata ufahamu wa nini kinaendelea katika jamii

Marekani ndio wenye ufunguo wa Internet na ndio wamekuwa waathirika katika harakati za kigaidi kwa kutumia internet na mitandao ya kijamii.

''Recruitment'' ya watu waouvu inafanyika kwa ugunduzi wao.

Marekani haizui au kuwachukulia hatua, inatumia mwanya kukabliana na hali mbali mbali

Wiki mbili zilizopita Marekani ilinusuru Taifa dakika za mwisho kwa taarifa za kigaidi
Taarifa za mhusika zilijulikna na taifa husika, lakini lini anatekeleza azma,ilitoka Marekani

Taarifa zilipatikana kupitia mitandao ya kijamii ambako walikuwa wanafuatilia nyendo

Huu ni mfano tu kuonyesha kuwa ili kuweza kubaini nini kilichopo nyuma ya mtu au watu ni lazima kuelewa hisia zilizopo na kuzifanyia kazi katika kupata matokeo chanya

Hasira haionyeshi uovu, ndani ya hasira inaweza kupatikana busara, na hiyo ndiyo inayotakiwa kufanyiwa kazi wala si kukabiliana na hasira

Lakini pia kuna somo kutoka Marekani. Katika miaka ya 90 wakati wa Bill Clinton, kulitokea shambulio katika mji wa Oklahama.

Vyombo vya habari vilijikita kuzungumzia ugaidi na kundi la Alqaeeda wakati huo.
Habari nzima ikafunikwa na jina la Ugaidi

Vyombo vya dola vilikuwa kimya vikifanya uchgunguzi.
Mwishowe, walimkamata Mmarekani Mweupe kwa jina la Tom McVeigh.

Tom alikuwa na hasira dhidi ya US kwa mambo Imani,akazihamishia kulipua jengo

Mwisho wa siku vyombo vya habari vikajifunza namna ya ku 'react' katika matukio.

Siku hizi vinazungumzia habari baada ya utibitisho.

Vyombo vya dola vya wenzetu havitoi taarifa za kuchanganya au 'reactions' tu

Kauli ya mkuu wa Operesheni ilitoka mapema, ilikuwa na viashiria vya hisia za tukio
Katika muda mfupi, kamanda alipataje habari kuhusu uhusiano wa wahalifu na siasa?

Marufuku ya mikutano ya ndani nanje, inahusianaje na tukio lilo katika uchunguzi?

Hivyo tukio zima limekuwa na kile kinachoitwa ''parti pris' au preconceived notion.
Kwamba kuna hali ya kisiasa hivyo tukio linahusiana na hali hiyo

Je, iwapo kuna wananchi wenye taarifa,katika mazingira ya kuwa na ''majibu'' watajitokeza?
Je, hili si kuwa linawagawa wananchi na hivyo kuinyima Polisi fursa nyingine?
Je,ikibainika ni sababu zingine nini itakuwa taswira ya jeshi mbele ya umma?
Je, uchunguzi ukibaini mengine tofauti utawezwaje kuwekwa mbele ya jamii?
Je, tukio la juzi linatofautianaje na mengine ya nyuma kiasi cha kuliekeleza pengine?
Hili ni tukio baya sana, lakini pia linaweza kutusaidia tusijepatwa na mengine tukijua yanajirudia. Swali ni je, Polisi wanatazamaje jinsi lilivyochukuliwa na jamii, na mazuri au mapungufu yanaeleza lolote la kujifunza kwa siku za mbaleni?

Inaendelea sehemu ya mwisho
 
Sehemu ya mwisho ([HASHTAG]#194[/HASHTAG])

MATARAJIO YA MVUTANO UNAOENDELEA
Hali ya mvutano ipo kama inavyoonekana katika habari na matamko

Upande wa Upinzani umesimama katika hoja ya kutumika kwa sheria
Kuachwa waendelee na mikutano kama sheria zinavyosema

Upande wa Serikali, hoja haipo wazi kama alivyosema Mh Wassira

TATIZO: Hata kama ni dogo sana, ukweli unabaki kuwa lipo tatizo

Matamko ya Viongozi wa mikoa na kwingineko yanaeleza hilo
Kauli za Viongozi wa dini na wengine zinaeleza hivyo
Kauli ya Polisi mara kwa mara inaeleza uwepo wa tatizo

Mwaka 2001 ilichukuliwa kirahisi tu kuwa ni baadhi au kundi la watu
Madhara yalikuwa makubwa kwa gharama za maisha ya wananchi

Serikali ikajikuta katika hali ya kujitetea mbele ya uso wa dunia
Tukazalisha Wakimbizi katika nchi inayopokea Wakimbizi

Hakuna aliyeshinda, sote tulishindwa kama nchi na Taifa, tukajitia doa

MSAJILI WA VYAMA
Kaitisha kikao 29/30. Msajili alishatoa kauli kuhusu maandamano na si chanzo cha tatizo. Kwamba haku address tatizo bali kutaka usitishwajwi tu

Hilo lilijenga kutoaminiana kwa mtazamo wa kutokuwa 'impartial'

LHRC(Utawala bora na haki za binadamu)
Waliitisha kikao, wadau wengine hawakuhudhuria bila matokeo chanya

Kikao cha 29/30 kina shaka.Ni dharura, kwanini tarehe zinazokaribia 'tukio'?

Msajili wa vyama katika mazingira yaliyojitokeza alipoteza ile 'trust'.
Busara angeshirikisha makundi mengine muhimu ya kijamii

Msajili na tume ya haki walishindwa,kipi ni tofauti safari hii?

Kikao cha 29/30 kisipotoa ufumbuzi kitakuwa kimechagiza hisia zaidi

Hili ni tatizo, bila kujali ukubwa au udogo wake, ni tatizo.

Linahitaji busara,weledi ujasiri, haki, sheria na kuliangalia Taifa kwanza.

Wadau wote waweke masilahi ya Taifa mbele, watazame nyuma na kujifunza

Tusemezane
Katika bandiko hili tulihoji sana mantiki ya kikao kuwa 29/30
Tukauliza kama ni jambo la muhimu nini kinashindikana kufanya mkutano mapema?

Tulihoji sana tarehe hizo kwasababu hazikuonekana kuwa katika 'nia' iliyothabiti

Leo msajili ameahirisha hadi tarehe 2 na 3. Kwamba wamealikwa watu maarufu n.k. na hivyo kupewa notisi ya muda mfupi wanaweza kushindwa kufika

Maoni yetu
Msajili ametoa raia hiyo baada ya kukutana na kamati ya uongozi ya vyama vya siasa
Ilikuwaje msajili akatangaza tarehe kabla ya kukutana na uongozi huo?

Hao wazee na watu maarufu wanahitaji muda na maandalizi gani?

Tarehe 2 na 3 zitakuwa zimesadia hali iliyopo?

Msajili wa vyama ana haki na uhuru wa kufanya yaliyo katika mamlaka yake.
Haki hiyo izingatie hali iliyopo na iwe katika dhamira inayoonyesha kupata suluhu

Haisadiii kunapokuwa hakuna kuamiana. Suluhu huanza na kuaminiana.

Tutaendelea na tathmini sehemu ya mwisho, hii ilikuwa by the way tu

Tusemezane
 
HALI YA SIASA ZA NCHI NA YANAYOJIRI

Sehemu ya I

Kwa takribani mwezi mmoja kumekuwa na 'tension' kuhusiana na maandamano ya kile kilichoitwa 'ukuta'.

Maandamano yameahirishwa na Chadema masaa
Kilichosemwa ni kutokana na maamuzi ya kamati kuu.

Mabandiko ya nyuma tulieleza kutokuwepo kwa ulazima wa tension kati ya wapinzani a serikali. Kwamba,ni jambo la taratibu na sheria tu

Hoja kubwa inayozungumzwa ni maandamano ya tarehe 1.
Uhalisia,hayo ni matokeo ya kukatazwa kwa mikutano ya siasa nchini

Pengine hoja ilipotoshwa makusudi ili kukwepa hoja nzito ya kikatiba

Kwamba, ni sheria gani ya nchi inayozuia shughuli za kisiasa ambazo mikutano ni sehemu yake? Nani mwenye mamlaka nayo?

Ni sheria gani inayozuia mikutano baada ya uchaguzi mkuu?
Sheria gani inayotoa ruhusa ya mikutano ikifika 2020?

Msajili wa vyama,mlezi na mtunza sheria hakuwahi kutoa ufafanuzi wa hilo.

Mwanasheria wa serikali (AG)kama walivyokuwa viongozi wa makundi ya jamii , wa dini, wastaafu, wanataaluma,vyama vya kitaaluma n.k. hakuna aliyesimama na kutetea , kufafanua au kueleza kwa mantiki na hoja

Hii inaeleza nini?
Inatueleza kuwa kilichoondoka ni maandamano, hoja ya msingi bado ipo miyoni mwa wenye malalamiko na hivyo tatizo lipo pale pale.

Pengine kilichotokea ni kuahirisha muda tu, mbele ya safari tatizo hili litajirudia kwa njia nyingine na hata tusizopenda zitokee

Ukweli wa kanuni, suluhisho la tatizo ni suluhu ya chanzo si dalili za tatizo
Kwa maana kuwa Asprin au Pandol zinatoa unafuu tu hazitibu maradhi halisi!

Je, tutaishi kwa dawa za maumivu au ni wakati wa kupata dawa ya tatizo kwa njia za sheria mezani na kwa haki?

Inaendelea...
 
Sehemu ya II

Ukinzani uliotokea umetoa mafunzo mengi tukisonga mbele kama Taifa

1. Hakuna mshindi katika hili na hakika serikali imetumia muda, nguvu nyingi na kupoteza fursa ilizokuwa nazo kusogeza mbele agenda zake

Ilikuwa kawaida kusoma wananchi wakifuatilia serikali inafanya nini katika shughuli za kila siku, hata kufuatilia teuzi za viongozi , sera n.k.

Kwa takribani miezi 2 hakuna anayejua nini kimetokea, focus kubwa ikiwa habari za kamata kamata, Polisi, matamko n.k.

Wangapi wanajua waziri mkuu alikuwa Kenya kwa shughuli gani? Makamu wa Rais yupo safarini kwasababu gani?waziri wa elimu anafanya nini elimu?wafanyakazi hewa, uhalifu, kwanini soko la pamoja linatuathiri Watz n.k.?

2. Kwamba, taasisi za umma zimepoteza mwelekeo na kuingiliwa kisiasa. Ofisi ya msajili wa vyama inaposhindwa kutafsiri sheria au kutoa ufafanuzi

Ni jambo la kutisha sana.Tulifika hapa kwasababu ofisi imepoteza ''huru''
Imefungwa na wanasiasa.

Kama kuna kiongozi anayepaswa kujiuzulu ni msajili wa vyama.
Huyu amelianguasha Taifa , haaminiwi the least to say

Hatujui mikutano aliyoandaa tarehe 2 na 3 itazaa nini tukijua ameshindwa kuzungumzia chanzo cha tatizo kisheria akiwa emebeba sheria mkononi !

3. Matumizi mabaya ya nguvu za dola

Tumeliongelea mabandiko yaliyopita. Kwamba, kumekuwa na kamata kamata za watu kwasababu ambazo hazielezeki kiurahisi au kisheria.

Funz ni kuwa sheria zinatoa nafasi ya baadhi kufanya 'abuse of power'

kwamba mtu akamatwe ijumaa ili alale mahabusu wikiendi!

Kwa nchi zingine mtuhumiwa huachiwa ikipita masaa 24 kabla ya kusomewa mashtaka, na wapo mahakimu wa zamu siku za wikiendi

Haki ya dhamana inaminywa bila sababu za msingi.
Kuna kiongozi alikataliwa haki eti usalama wake upo hatarini.

Huyu alikamatwa nyumbani kwake kwa kosa lisilohusiana na jamii, iweje Polisi wahofie usalama wake ikiwa wao ndio wenye kesi dhidi yake?

Inaendelea
 
Sehemu ya III

Mtumizi mabaya ya nguvu, kwamba kiongozi anaamua kutumia neno 'uchochezi' kufungia vyombo vya habari bila haki ya kuwasikiliza

Kwamba, sheria hazifuatwi bali matamko ya viongozi
Kiongozi anaamrisha watu waadhibiwe na Polisi atajibu yeye

Hakuna utawala wa sheria bali mwenye nguvu ndiye mwenye sheria

Matumizi mabaya ya nguvu kiasi taasisi zilizo na mamlaka zimebaki ofisi tu na kusikiliza watawala badala ya kutekeleza majukumu yao

Msajili wa vyama ni mfano mzuri sana. Kwamba hawezi kutafsiri sheria zake

Mgogoro huu wote ni kwasababu ofisi ya msajili haina kauli
Ni kama jumuiya ya chama chochote cha siasa.
Imeshindwa kusimama katika sheria kuzitafsiri kwa ukweli na haki! inatisha

Mamlaka ya utangazi imeporwa nguvu zake na waziri.
Je kuna umuhimu wa taasisi hizo kuwepo?

Vyombo vya dola kutozingatia haki katika kusimamia sheria
Watu wanakamatwa bila kufikishwa mahakamani kwa wakati

Matumizi mabaya ya kutumia kauli kama sheria za nchi.
Kama tulivyosema, hatujaonyeshwa sheria inayozuia mikutano hadi 2020?

Matumizi mbaya ya nguvu, CCM inapopewa favor katika sheria ile ile iliyokataza wengine. Hapa kuna discrimination, kwamba ni ubaguzi mkubwa

Lakini pia matumizi mabaya ya nguvu ni pamoja na kueneza habari ambazo umma umebaini hazikuwa sababu za kisheria kuzuia mikutano ya siasa

Swali linajitokeza, kwanini haya yanatokea?

Tutajadili
 
KWANINI HAYA YANATOKEA?

Mambo haya yanatokea kwasababu viongozi wamejisahau kuwa ni watumishi wa umma waliochaguliwa au kuteuliwa kutumikia umma.

Katika kutekeleza wajibu wanapswa kufuata sheria kama zilivyoandikwa

Chanzo cha tatizo si maandamano, ni ukiukwaji wa sheria zilizoanishwa na sheria mama(katiba) na zitokanazo (derived) katika sheria mama

Tatizo ni ukikukwaji wa haki ya msingi ya wananchi na vyama vya siasa kukutana na kujadiliana yanayohusu Taifa kwa kufuata taratibu zilizopo

Soko la wanasiasa ni jamii na huwafikia kwa mikutano iwe ya ndani au ya nje. Haki hiyo ipo katika katiba ya 1977.

Katika kuiimarisha, msajili wa vyama ana sheria zinazoongoza mikutano
Haki ya wananchi kukutana imeanishwa katika sheria za Jeshi la Polisi

Kupiga marufuku mikutano inapaswa kuambatana na sababu zilizo katika sheria. Mfano, hali ya usalama imeelezwa na jinsi inavyotekelezwa kikatiba

Kutokana na kutofautwa kwa sheria mama; mamlaka, taasisi na viongozi wanalazimika kuvunja sheria kwasababu msingi wa sheria umevunjika

Pamoja na mapungufu ya katiba yetu ya 1977, lau kama ingefuatwa kama ilivyo, hili la leo lisingekuwa tatizo hatya kidogo.

Katiba ya 1977 imeeleza kwa uwazi haki za wananchi na mihimili mingine
Ni kwa kutumia katiba hiyo, hakuna kiongozi yoyote, mtaalamu au wanataaluma aliyetokea hadharani na kubainisha uhalali wa marufuku

Hatuna majibu ya: Sheria ipi inazuia mikutano ya kisiasa hbaada ya uchaguzi mkuu. Sheria ipi inatamka siasa ni hadi 2020 na imeanishwa wapi tarehe , mwezi na mwaka huo 2020?

Hakuna sharia ya CCM wafanye mikutano,ni chama tawala vingine vikae pembeni.

Hivyo kutozingatia katiba ya 1977 ndilo chimbuko la tatizo na suluhu yake inapatikana hapo hapo si kwa vikao vingine.
 
KUAHIRISHWA MAANDAMANO

Baada ya kuona chimbuko na athari zinazotokana na matumizi ya nguvu mengine yakivuka mipaka, tuangalie kwa ufupi kuahirishwa kwa maandamano ya Sept 1

Kwa mwezi kumekuwepo na harakati za kutaka maandamano yasitishwe.

Serikali na vyombo vyake ikisema ni haramu na nguvu itatumika.

Makundi mengine kama Msajili wa vyama yakiunga mkono bila kueleza chimbuko.

Kubadili tarehe za vikao vyake ni sehemu tu ya jitihada za kuhakikisha hayafanyiki.

Na hapa ukweli usemwe, msajili ''amechukua upande'' na kuacha nafasi yake ya asili

Viongozi wa dini wakitumia nafasi yao na wengine wakitumika.

Mwisho ikafuata kamata ya viongozi nchini. Hatimaye ilikuwa viongozi wa Chadema wakiwa katika kikao cha kamati kuu wakitakiwa kuripoti siku ya maandamano.

Kubwa ni lile la taasisi nyingine kufanya mazoezi siku hiyo.
Hili linaonekana kuwa katika muda muafaka kwani ni wakati wa tukio.

Kwa upande mwingine taarifa za mazoezi kutolewa na kiongozi wa kisiasa inashaka. Kwanini kiongozi wa siasa awe ''msemaji'' wa taasisi nyeti za usalama wa nchi?

Ilikuwa dhahiri maandamano yangeleta matatizo makubwa.
Kuna sintofahamu kati ya vyombo kama Polisi na wananchi.

Laiti yangalikuwepo, uwepo wa shughuli za taasisi nyeti siku hiyo iingekuwa tatizo kubwa

Hivyo wapinzani walikuwa na mengi ya kufikiri.
Moja, viongozi wao waandamizi ima wapo mahabusu au wana kesi.

Pili, kuendelea nayo kungeweza kuleta matatizo makubwa tusiyoyatarajia.

Tatu, kuna makundi kadhaa ya jamii yaliyokuwa tayari si kwasababu ya mikutano, bali kutafuta mwanya wa kuonyesha hasira zao

(i) Hali za maisha mitaani si za kuridhisha
(ii) Kuna wenye hasira za mambo yaliyopita kama kufukuzwa vyuoni
(iii) Wapo wanaolifikiria suala la Zanzibar na hao si huko tu wapo kila mahali
(iv)Kuna kundi la wanasiasa ambao wanaona 'kituo' chao cha kazi kimefungwa
(v)Wapo wananchi wanaoona nchi inaendeshwa bila sharia zilizopo
(vi)Lipo kundi linaloona linadhalilishwa na matumizi mabaya ya nguvu za dola
n.k.

Uzito wa makundi hayo hauonekani dhahiri, hayana platform kama wanasiasa.

Hata hivyo watu wanaposhangilia maafa dhidi ya wanadamu wengine, kuna tatizo kubwa

Kwamba chuki imefika mahali utaifa unapotea, na inaonyeshwa dhahiri. Kuna tatizo

Kama tulivyosema, katika hili serikali imepoteza sana.
Ile nguvu iliyokuwa nyuma yake bila kujali itikadi imetoweka.

Hamasa ya wananchi kufuatilia nini serikali yao inafanya imepotea.
Nguvu ya serikali kueleza mipango na utakeleza imefutika katika habari

Kibaya Zaidi chuki imetawala, kati ya makundi ya siasa kwa uchama, taasisi na wananchi, wananchi na mamlaka n.k

Haya yote yanapoteza nguvu ya serikali iliyokuwa nayo mieizi 2 au 3 iliyopita

Kwa wapinzani, kuna sura kuu nne za tukio hili

Tutazijadili
 
KWANINI TUMEFIKA HAPA

Kabla hatujajadili sura za wapinzani, tuangalie kwanini yanatokea haya

1. Katiba haiheshimiwi. Hakuna chombo kinachosimamia kingine.

Mfano, Seneti ya Brazil imepiga kura kumwondoa Rais madarakani na 'impeachement'

Kwetu na kwa katiba iliyopo, Bunge ndilo linaloweza. Je, Bunge linaweza?

Kwa katiba ya 1977 ndiyo inawezekana, lakini lazima wawepo wabunge wa kutosha
Mlolongo ni mrefu ambao si rahisi kuchukua hatua katiba inapokiukwa

2. Kutokuwa na vyombo huru
Katiba(1977) inatoa madaraka makubwa kwa mtu mmoja kuliko mamlaka nyingine
Ni kuanzia teuzi wakuu wa taasisi, bodi n.k.

Mfano, Msajili wa vyama ni mteuliwa na Rais(mwenyekiti wa CCM)

Msajili atamwambiaje Rais umekosea? au chama chake kimekosea?
Kiuhalisia msajili hawajibiki pengine,utendaji una conflict of interest ya ''masilahi na majukumu''

Hili tunaliona katika sakata hili , msajili ameshindwa kufafanua sheria alizo nazo

Hakueleza marufuku ya mikutano hadi 2020 yapo katika sheria gani ndani ya ofisi yake
Hakueleza sheria ya kuzuia mikutano baada ya uchaguzi ipo wapi katika sheria alizo nazo

Alichokifanya ni kutupa lawama kwa wapinzani bila kujali chanzo cha tatizo
Ni kutumia baraza la vyama kukwepa jukumu lake. Baraza la vya halina 'meno'

Mfano wa pili ni wa kiongozi aliyetoa agizo Polisi kuadhibu'watuhumiwa' kabla ya sheria
Kiongozi yupo madarakani licha ya kosa alilotenda.
Mamlaka ya kumwajibisha ipo kwa aliyemteua kwa mujibu wa katiba

Mifano hiyo ipo sehemu zote ikilindwa na katiba

CCM walilalamikia rasimu ya Warioba kumpunguzia Rais madaraka
Walijua 'Matatizo' pindi nguvu hizo zinapopungua

Kwamba, Rais atakuwa na 'watch dog' , mamlaka za utezi nje ya Rais
Teuzi zitathibitishwa na kuwajibika kwa vyombo vingine

CCM waliona uwanja wa ushindani utakuwa sawa, tatizo kwao!
Wakavuruga mchakato makusudi ili kuenedeleza 'status quo'

Muda umebadilika, hili lina ashiria katiba iliyopo itatuletea matatizo

Ni wakati turudi kuandika katiba itakayoendana na mazingira ya sasa

Ni funzo zuri kuwa 'business as usual' huenda isifanikiwe katika kizazi kilichopo

Tusemezane
 
DANA DANA ZA MSIJILI WA VYAMA

Mtakumbuka tulionyesha hofu na nia ya msajili wa vyama kwa majukumu na uwajibikaji

Tukumbushe kwa ufupi
Mwenyekiti wa tume ya utawala bora na haki za binadamu aliitisha kikao
Walihudhuria Chadema . Polisi, serikali hawakuhudhuri kwa 'udhuru'

Msajili wa vyama
Akaita press conference kufafanunua marukufu ya mikutano. Alisema ''kauli ya Rais ilitafsiriwa vibaya, alimaanisha kuwaalika wapinzani katika kujenga nchi''

Msajili akaitisha kikao tarehe 29 na 30 kujadili suala la maandamano ya Ukuta

Kikao kikaahirishwa siku chache kabla. Msajili kasema 'kuna wazee na watu maarufu walioalikwa, haraka wasingeweza kujiandaa''kikaahirishwa hadi tarehe 2 na 3

Leo taarifa inatolewa na Naibu mwenyekiti wa baraza la vyama vya siasa.
Taarifa inasema suala hilo limeahirishwa bila kutoa ufafanunuzi hadi lini

Mlolongo huu ni kutoa feedback ya hali ilivyo na kujiuliza maswali, je, ipo nia ya dhati ya kujadili suala hili katika kiwango cha msajili wa vyama na baraza?

Je, naibu mwenyekiti ana nafasi gani kutoa taarifa ya shughuli za msajili wa vyama ?

Kwa ufahamu mdogo, msajili anateuliwa na Rais, anaongozwa sheria ya vyama vya siasa

Wajibu wa mwenyekiti au naibu wa baraza ni kusimamia vikao vya baraza hilo.

Aliyeitisha kikao ni msajili wa vyama kwa mamlaka aliyopewa na sheria.
Iweje agenda ya msajili ifafanuliwe na baraza la vyama?

Msajili ana orodha na ya vyama, na anayesimamia shughuli za vyama
Inakuwaje anatoa nafasi za shughuli zlizoitisha kutangazwa na mtu mwingine?

Tunaweza kuona jinsi msajili alivyoshindwa kutumia sheria kutafuta ufumbuzi
Nguvu za kisheria anazo hata kufuta vyama vya siasa.

Tujiulize laiti chama kingine nje ya CCM kingetoa matamshi hatarishi, msajili angeita baraza la vyama kujadili hilo?

Ni mara ngapi tumemsikia akitishia kufuta vyama vya siasa?
Iweje basi katika hili sakata nafasi yake haionekani kinyume chake anatumia baraza?

Tunarudi katika bandiko la awali, mfumo umetengenezwa kwamba vyombo huru vimefungwa na kusababisha mambo madogo kuleta taharuki na sintofahamu

Wakati wananchi walipendekeza kuondoa mamlaka ya baadhi ya vyombo kutoka 'serikali' ili kuvipa uhuru , CCM waliona hilo kama tishio la uwepo wao

CCM wanaamini ili mambo yawaendee vizuri, serikali iwe na udhibiti wa vyombo.
Bunge la katiba likavurugwa

Wakati umma ukitaka baadhi ya mamlaka ziwe na checks and balance, kama tume ya uchaguzi, ni muhimu kufikiria nafasi kama msajili wa vyama, Jaji mkuu, tume ya maadili, tume ya utumishi n.k. kuwajibika kwa chombo kingine.

Kuendelea na katiba ya CCM (Pendekezwa) tutarudi hapa tulipo.

Wakati wa kuangalia katiba mpya ni sasa kuliko wakati mwingine.

Hii ya CCM ikaachwa iendelee, tunyayoyaona yataongezeka

Tusemezane
 
Mh VUA ALI AVUAI ASADIA UFAFANUZI

'AWEKA WAZI UWEZO WA BARAZA'

Baada ya tamko la baraza la vyama vya siasa kuahirisha kikao cha tarehe 2 na 3 bila sababu, yametokea majadiliano katika mitandao kwa namna tofauti

Wapo wanaohoji ikiwa dhamira ya vikao hivyo ilikuwepo?
Wengine wakiohoji tu umuhimu wa baraza katika mazungumzo ya siasa
Na wapo waliohoji utendaji wa msajili hasa baada ya tamko kutolewa na Vua A Vuai

Vua ni naibu katibu mkuu wa CCM ZNZ, na naibu m/kiti wa baraza la vyama vya siasa

Katika mkutano wa Unguja ambao si rahisi kujua ulikuwa wa kiserikali au kichama kwa 'message' kubeba uchama na userikali, Vua alipewa nafasi ya kuwasilimu wananchi

aliongelea baraza la vyama kwamba lipo kwa mujibu wa sheria, video ya pili dakika 1.50

Ziara ya Rais Magufuli Unguja: Asema hakuna mpinzani atakayekanyaga kwenye serikali yake

Vuai anasema baraza la vyama lipo kisheria chini ya kifungu 258, 21(b na C) cha sharia ya msajili wa vyama iliyolipa baraza uwezo wa KUSHAURI serikali kupitia MSAJILI wa vyama kuhusu mambo ya kisiasa katika mustakabali wa nchi

Mh Vua amerudia mara mbili,kazi ya baraza ni kuishauri Serikali kupitia msajili wa vyama

HOJA
Hakuna anayekataa uwepo wa baraza la vyama vya siasa kisheria.
Uwepo ni kama alivyoanisha Mh Vuai kama ilivyo katika sheria ya msajili wa vyama

Pili, shughuli za baraza (Vuai) ni kuishauri serikali kuhusu mambo ya siasa nchini

Vuai anaeleza kwa uwazi si kazi ya baraza kuwasiliana na serikali au umma isipokuwa kupitia msajili wa vyama vya siasa

Tatu,Msajili wa vyama ndiye mwenye sheria inayotambua uwepo wa baraza, na baraza lenyewe halina sheria zake labda kama lina kanuni.

Hivyo uwepo wa baraza ni kutokana na uwepo wa sheria ya msajili ambayo mhusika mkuu ni msajili wa vyama vya siasa kama kiungo cha vyama vya siasa, serikali na umma

Nne, ni kutokana na tangazo la Msajili kuhusu mkutano wa tarehe 29 na 30 ulioahirishwa, na ule wa tarehe 2 na 3 uliosubiri wazee na watu maarufu ilikuwa katika jukumu la msingi la Msajili wa vyama.

Kwasababu zozote zile, Msajili bado ana uhalali wa kisheria kuwa kiungo akibeba sheria

Tano, tangazo la Naibu mwenyekiti wa baraza la vyama kusistisha kikao cha tarehe 2 na 3 kwa sababu yoyote halikuwa katika muundo sahihi.

Vuai alipaswa kumshauri msajili kuhusu jambo hilo na si yeye kutoa tangazo.

Sheria anayosema inamruhusu kushauri serikali kupitia Msajili na si kuwasiliana na umma. Mwenye dhamana hiyo ni Msajili wa vyama ambaye ndiye mwenye 'act'

Sita, Vua katika nafasi yake alipaswa kumuandikia Msajili (mwenye nguvu za kisheria na mwenye sheria inayojumuisha baraza) kuhusu kuahirishwa kikao, ili Msajili aishauri serikali na umma

Kwa kuangalia hoja hizo, naibu mwenyekiti wa baraza la vyama, na naibu katibu mkuu CCM ZNZ ametupa habari kuhusu ''udhaifu'' wa Ofisi ya Msajili na baraza la vyama.

Ameitumbukiza CCM na Serikali katika hali isiyotarajiwa

Inaendelea
 
''AITUMBUKIZA'' CCM KATIKA MGOGORO

AONYESHA UDHAIFU WA OFISI YA MSAJILI

AICHONGANISHA SERIKALI NA VYAMA/UMMA

Kama tulivyoona na kwa mujibu wa Vuai, suala la yeye kutoa taarifa lina utata

Tafsiri inayopatikana ni Ofisi ya Msajili,iliacha jukumu lao kwa baraza la vyama.

Baraza halina sheria, lipo kisheria na kazi yake ni kuishauri serikali kupitia Msajili(Vuai)

Taarifa ya kuahirishwa kikao cha 2 na 3 kwa mtazamo uliopo na kwa maelezo ya Mh Vuai yanaonyesha msajili hakutimiza wajibu wake wa kupokea ushauri kutoka baraza la vyama, kuishauri serikali na kuwasiliana na umma wakati ndiye mwenye agenda

Ni sababu zipi zilizopelekea Msajili 'kuacha' jukumu lake kuchukuliwa na baraza?

Ile dhana kuwa ofisi ya Msajili haina 'uhuru' itaondokaje vichwani mwa wananchi?

Mh Vuai alipaswa kuelewa huu ni mgogoro kati ya serikali na Upinzania (Chadema).

Msajili wa vyama alichukua jukumu la asili kwavile ndiye mwenye sheria

Tendo la Vuai kutoa taarifa zilizopaswa kutolewa na Msajili, na akiwa naibu katibu mkuu CCM anakiweka CCM katika mgogoro usio wa lazima.

Picha ya Vuai inaonekana ki CCM Zaidi kuliko unaibu Mwenyekiti wa baraza la vyama.

Wapo watakaotumia hoja hiyo kutafsiri kuwa Ofisi ya Msajili imeingiliwa na CCM.

Mh Vuai ameiweka ofisi ya Msajili pagumu, ameitumbukiza CCM katika mgogoro usioihusu

Kati ya Msajili wa vyama na baraza la vyama, ni nani mwenye kauli thabiti?

Haya, yanauchanganya umma bila sababu na kupoteza Imani ya ofisi za umma

Kuna 'overlap' ya kazi baina ya msajili na baraza CCM ikiwa katikati bila kutarajiwa

Je, baraza litabeba Imani katika siku za usoni likitokea lingine linalohitaji ushauri?

Je,wangapi watatenganisha nafasi nyakati tofauti?(Vuai wa baraza na wa CCM)?

USHAURI
CCM wachukue hatua za haraka na za dhati kutenganisha kauli za Vuai wa baraza na Vuai naibu katibu mkuu ili wasiingie katika mgogoro wa CDM na Serikali

Kwa kuelewa conflict of interest na sheria Vuai hakupaswa kubeba jukumu ambao:

1. Ni la msajili wa vyama, kwani yeye alipaswa kumshauri na si kutoa 'press release'
2. Kutoa tamko akiwa na kofia mbili,ya CCM inaonekana Zaidi kuliko ya baraza

Hivyo, hakuna namna CCM watajitenga na mgogoro huu kama hawaatajitakasa

Kwa upande wa Msajili, ofisi pengine ina nafasi ya kufafanunua ilikuwaje hatua za awali ilihusika na hatua zilizofuata imeacha baraza lihusike.

Kwamba,ni nani mwenye sheria na agenda za vikao vilivyoahirishwa

Kama hakuna ufafanunuzi, ofisi itapoteza dhamana katika Taifa.

Je, itakuwa na hadhi na Imani kama ilivyoanishwa katika sheria?

Tusemezane
 
TAARIFA MBILI ZA WIKI HII

MAKAMU WA RAIS

Kuna habari mitandaoni na magazetini zilizopewa uzito wa juu kuhusu Makamu wa Rais kutaka kujiuzulu nafasi hiyo

Habari hizo zinasema sababu kubwa ni 'kutokuwa ' na masikilizano kati ya mabosi wawili

Muda haukupita, taarifa hiyo ikakanushwa na ofisi ya Makamu wa pili wa Rais

Taarifa ilisema huo ni uzushi uliolenga kuleta taharuki katika jamii

HOJA
Hizi ni taarifa tu zilizosambaa mitandaoni. Kukanushwa kwake haraka kunazua maswali

Pengine zingekanushwa baada ya siku kadhaa, huo ungebaki uzushi usio na kichwa wala miguu. Haieleweki ni kwanini taarifa zilikanushwa kwa haraka kiasi hicho

Pamoja na hayo na kwa kuzingatia hali ya mambo ilivyo, 'uzushi' huo umeleta usumbufu

Kwanini imetokea hivyo kwa VP? Linabaki swali tu miongoni mwa vichwa vya wananchi

TAARIFA YA WAZEE WA CHADEMA

Habari nyingine ni ya wazee wa Chadema 'wakikemea' kauli za ziara ya Rais ZNZ

Katika taarifa hiyo, msajili wa vyama ametajwa kwa namna inayofikirisha

Wazee hao wanahoji 'kutokuwa' na mawasiliano ya barua kati ya chama na Msajili

Kuahirishwa kwa vikao wakimtuhumu Msajili 'kula' njama za kuitega Chadema ifutwe

Hayo ni madai tu yanayotolewa na upande mmoja.
Huenda upande wa Msajili ukawa na maoni na mtazamo tofauti. Muda ukifika tutafahamu

Hata hivyo katika mfululizo wa mabandiko tumeeleza kuhusu Msajili.
Inaonekana kuna kutoaminiana kati yake na baadhi ya vyama vya siasa( Mistrust)

Kutuhumiwa kula njama za kufuta chama kikuu cha upinzani, ni tuhuma nzito
Msajili hapaswi kukaa kimya.

Ni vema akajitokeza yeye na si viongozi wa baraza kuweka mambo sawa.
Msajili anapotuhumiwa kutumika na serikali ina maana anatumika na ''CCM'' pia

Ieleweke, uchaguzi uliopita kwa mujibu wa NEC, Chadema ilipata kura milioni 6 za Urais CCM ikiwa na kura milioni 8. Tofauti hiyo ni 'significant' katika mustakabali wa siasa

Kundi hili la milioni 6 linapoaminishwa kwa tuhuma nzito kwa Msajili kama ilivyotokea ni jambo la hatari kuliko maandamano.

Ni hatari kwasababu mtu anayeweza kusimama kati na kati anapokosa Imani kwa upande mmoja , atasimama vipi wakati akihitajika?

Tumesikia viongozi wote wa dini na siasa na jamii wakizungumzia Amani.

Kama tujuavyo Amani ni tunda la haki na usawa.
Katika mazingira ya kundi moja kuhisi halitendewi haki, Amani tunaohubiri ni ipi?

Amani haivurugwi tu na wananchi, tuhuma zinazomkabili Msajili si kiashiria kizuri.

Wanaodhani kutotendewa haki wakikata tamaa hali inaweza kuwa isiyotarajiwa

Msajili ajitokeze azungumzie tuhuma alizotupiwa. Hili litalinda Amani ya nchi

Tusemezane
 
MATUKIO KATIKA SIKU JUMA

MEYA WA KINODONI NA MALALAMIKO

Jana Meya wa kinondoni alikuwa na mkutano na waandishi wa habari.
Kwa mujibu wake, Meya alikutana na watu wa usalama kuhojiwa kwanza!!!

Mazungumzo yake yanafutia ziara ya Rais katika Wilaya ya Kinondoni

Katika malalamiko yake, Meya Jacob amezungumzia kutengwa kiprotokali na kukataliwa ombi la msamaha wa kodi za kuingiza mashine za kuchakata taka

HOJA ZETU
Hii si mara ya kwanza wapinzani kutopewa nafasi yao katika mikusanyiko inayohusu shughuli za serikali. Rais alikwenda Kinondoni kama kiongozi wa serikali.

Kuifanya ziara ichukue sura za chama hakuna mantiki au busara
Mameya huchaguliwa na wakazi, ni viongozi wa wiote si chama

Katika majukumu, hawapaswi kutenga wananchi kisiasa.
Vivyo hivyo kwa viongozi wa serikali

Kiitifaki Meya ndiye mwenyeji wa Rais anapoongea na wananchi.
Si lazima aongee lakini itifaki inalazimu uwepo wake utambuliwe

Mara nyingi tumesikia kauli za 'uchaguzi umekwisha sasa kazi'
Kauli ina maana moja, muda wa siasa umepita ni muda wa utumishi kwa umma.

Inapotokea kutengwa, au kutopewa heshima kiongozi yoyote kutokana na itikadi za kisiasa, kauli nzima inapoteza maana na kuwa 'lip service'

Utengano unazidisha ufa usio na ulazima katika Taifa.
Hayo yanafanywa makusudi bila kujali masilahi mapana ya wananchi

Kwa hili serikali iliangalie kwani si kuwa linagawa taifa.
Linakinzana na kauli ya uchaguzi umekwisha na dhana '' kuwaletea maendeleo wananchi'

Maendeleo yanapatikanaje bila kuheshiamiana?
Chuki ,dharau na kutoaminiana zina masilahi gani kwa wananchi?

Tuliwahi andika, ni vema serikali ifuate kauli maarufu ya 'WALK THE TALK'
kinachosemwa kifanyike, tafsiri ya kinyume ni unafiki

Meya na sakata la Kodi

Inaendele
 
MEYA NA MSAMAHA WA KODI

Hoja ya Pili ya Meya wa Kinondoni ni kukataliwa msamaha wa kodi wa vifaa vya kuchakata uchafu vilivyolewa na shirika la Ujerumani kwa takribani Bilioni 3+

Katika barua alizopelekewa, zinaonyesha viongozi wa wamekataa ombi lake.
Hivyo, vifaa vinapaswa kulipiwa kodi ya takribani milioni 900

HOJA
Hili jambo lina maeneo mawili.
Wapo wasemao ni sheria na wanaosema kuna ''kuzuia'' miradi tu bila sababu za msingi

Misamaha ya kodi si jambo geni na imezoeleka kusika katika taasisi za dini.
Kuna ushahidi baadhi ya taasisi zimetumia misamaha kinyume na sheria

Hivyo si suala la sheria tu bali sheria kufuatwa kwa ukweli wake, ikisemwa 'to the letter'

Taasisi za dini zimeendelea kupata misamaha kwa kinachosema 'zinasaidia' au kuchangia huduma za jamii kama shule, mahospitali n.k

Hii maana yake,serikali inatambua michango katika huduma za jamii ni jambo la kuungwa mkono, linasaidia kufikia malengo iwe katika elimu au afya n.k.

Mantiki ya kusamehe kodi ni moja, kwamba vifaa vinavyoingizwa vinatumiwa na walipa kodi ambao pengine wangelazimika kulipa kodi au serikali kutumia kodi kwa jambo hilo

Ni kwa msingi huo , malalamiko ya Meya wa kinondoni yana mantiki na mashiko.
Mashine ya kuchakata uchafu ni kwa ajili ya manispaa kulinda afya na mazingira

Mashine hiyo haikukusudiwi kibiashara au huduma kwa mrengo wa siasa
Imetolewa kama msaada na wenzetu wanaopenda 'kutuletea maendeleo'

Ni jambo la ajabu na la kusikitisha wafadhili watakaposikia vifaa wanavyotoa vinalipiwa kodi kuingia nchini kwa ajili ya wananchi wasio na huduma hiyo

Hatujui wafadhili wamepataje bilioni 3 ,tujiulize kwanini serikali haikuwahi kutoa kiasi hicho? Hivi wenzetu wanatuonaje tunapotoza kodi pesa zao za kujitolea ?

Tujiulize ni lini viongozi wetu wameendesha harambee ya bilioni 3 mara moja?

Hatuoni mantiki ya kutoza kodi vifaa hivyo,hatuoni kwanini kuwe na viwango tofauti katika huduma za jamii!

Je, kuna tofuati gani ya kujenga zahanati ya dini au kuzoa taka kuzuia maradhi?

Ile kauli ya 'kuwaletea wananchi maendeleo' inayotumika ina mantiki gani ikiwa serikali yenyewe haioni umuhimu wa maendeleo yanayoletwa?

Hili jambo linachukua sura ya kisiasa ambayo ni kuwagawa wananchi
Linaipaka serikali matope,mantiki ya kutoza kodi ni hafifu kuliko kuruhusu viingie

Kwa mwendo huu, sisi kama Taifa tutafeli muda si mrefu.
Tukishindwa kushikamana kwasababu za ajabu ni mwanzo wa kuanguka.

Hili ni la kuangalia kwa upande wa serikali, lina mantiki na Meya asikilizwe

Tusemezane
 
'MADARAKA YANALEVYA'

HAYA YA Dr MWAKYEMBE TUYAELEWEJE?

Imezoeleka kusikia neon 'corrupt' kama tendo linalohusisha pesa. Maana ya neno hilo ni pana sana
Ni kweli kuwa kununua au kuuza haki ni sehemu ya 'corruption ' hasa pesa inapokuwa katikati

Hata hivyo, 'corruption' inaelezwa kwa maana nyingine kuwa ni kitendo cha kukosa uaminifu (dishonestly) kwa maana ile ile ya ima kufaidika kifedha au kupata masilahi binafsi

Ndipo tunapata msemo wa kiingereza usamao 'power corrupts' ukiwa na maana kuwa nguvu ziwe za madaraka au kuitawala huwa na tabia ya kuvunja uaminifu na uadilifu (lessen moral character)

Kwa waswahili msemo huo una maana ile ya 'madaraka hulevya' kwamba, madaraka huondoa sehemu ya ufahamu au utu au weledi au busara ya mhusika kama kilevi kifanyavyo

Mwingereza Lord Acton kaogelea power au madaraka kwa muktadha mkubwa zaid. Acto alisema 'absolute power corrupts absolutely' . Ndipo msemo wa 'power corrupts, absolute power corrupts absolutely' unaokuwa na maana

Tunaysema hayo baada ya kusoma habari za Mh Dr Mwakyembe, MB na waziri wa sharia akiachangia katika Bunge. Mh waziri anasema endapo Wapinzani wanaona Rais akavunja sharia, waende mahakamani. ''Akawasuta'' Wapinzani kuhusu Mh Lowass

Mh ni msomi aliyobeba katika sharia, alifanya kazi katika vyombo vya habari na mhadhiri maarufu wa Chuo kikuu. Ni mbunge wa siku nyingi ambaye si tu kuwa ana uzoefu katika Bunge bali pia amaeshiriki katika masuala mazito ya Bunge kama sakata la Richmond

Tulitegemea uzoefu wake katika mambo ya kitaifa ungekuwa na majibu tofauti ya hoja za kitaifa na si kauli kama tunazosikia mitaani zikiwaambia wapinzani waende mahakamani.

MARUFUKU YA MIKUTANO
Hili ndilo limezaa matatizo mengine kama maandamano yaliyoahirishwa kwa mujibu wa wapinzani

Hoja ya wapinzani ni kuwa 'Hakuna sharia inayozuia mikutano ya siasa ambayo ni kama kuzuia shughuli za siasa, wala sharia inayosema baada ya uchaguzi hakuna mikutano, au wananchi waachwe wafanye kazi.

Mheshimiwa waziri anapowaambia wapinzani kama hawaridhiki waende mahakamani, anafungua ukurusa mpya wa majadiliano, anafungua maswali na hoja Zaidi juu ya suala hilo

Tuangalie sura 3 zinazohusiana na hoja ya waziri Mwakyembe

Inaendelea....
 
Inaendelea
SURA TATU ZA HOJA YA WAZIRI MWAKYEMBE

1. Wapinzani wametaka kuonyeshwa sheria inayouzia mikutano ya siasa.

Kwa mujibu wao sheria haipo na kilichofanyika ni maamuzi ya mtu au watu kinyume na haki za shughuli za siasa kama zilivyoanishwa katika katiba, sheria ya vyama vya siasa, jeshi la Polisi .k.

2.Wapinzani kwenda Mahakamani 'kudai' kuvunjwa kwa sheria

3. Uwepo au kutokuwepo kwa 'kanuni' za asili (natural justice)

Tathmini

Hoja ya 1, ya wapinzani haikuwa tuhuma, walitaka waonyeshwe sheria iwe mwongozo

Ikiwa sheria ilikuwepo kwanini wahusika kama msajili wa vyama, tume ya haki na utawala bora, vyama vya siasa vinavyounga mkono serikali, watu wenye hekma katika jamii, watu wanaoheshimika katika jamii n.k. hakuna aliyeweza kuweka sheria hiyo hadharani?

Waziri wa sheria ana fursa nzuri sana ya kueleza uwepo wa sheria, kwanini hakufanya hivyo?

Hoja ya 2, Waziri anapowaambia waende mahakamani, waende kwasababu gani ikiwa wana sheria inayowaruhusu wao kufanya mikutano?

Ni kwa muktadha huo, waziri Mwakyembe 'kakwepa' jukumu lake la kufafanua uwepo wa sheria, iwe yeye au mwanasheria mkuu au msajili wa vyama

Wapinzani wanasema sheria za nchi zinawaruhusu kisiasa, waende mahakamani kudai nini?

Anayetakiwa kujibu hoja za upotofu wa Wapinzani ni waziri, iwe kwa mamlaka yake , usaidizi wa AG n.k. Na ana fursa ya kwenda mahakamani ku prove kuwa wapinzani wametafsiri sheria (kama ipo) vibaya au hawakuielewa na ipo.

La hawezi na hana sheria, hana wajibu wa kuwawelekeza mahakamani kudai 'kilichopo'

Jibu la kwamba wapinzani waende mahakamani ni kielelezo kuwa madai ya wapinzani hayana jibu

Hoja ya 3. kanuni za asili

Mh waziri anafahamu moja ya kazi za mahakama ni kutafsiri sheria

Ikiwa hakuna utata wa sheria wapinzani waende kuomba tafsiri ya kitu gani? Kwamba, waombe mahakama iwaruhusu watumie sheria zilizopo tayari na zinazotumika miaka takribani 25!

Hata kama watakwenda mahakamani , je, kanuni za asili zitakuwa zimefuata mkondo wa haki?

Mashahidi wataweza kusimama katika sheria dhidi yao wenyewe?

Waziri wa sheria- Mteuliwa wa Rais
Mwanasheria mkuu-Mteuliwa wa Rais
Mkurugenzi wa mashtaka-Mteuliwa wa Rais
Msajili wa vyama-mteuliwa wa Rais

Swali analotakiwa ajiulize mh ni kuwa, ni nani kati ya hao wachache anayeweza kusimama dhidi ya serikali iliyopiga marufuku mikutano?

Tusemezane
 
HILI LA TETEMEKO NI LA KUFIKIRI

WOGA NA NIDHAMU VINAPOSIGISHANA

Awali, tuwape pole waliofikwa na janga la asili la tetemeko
Wapo waliopoteza maisha, ndugu, wana familia n.k.

Wapo walio katika adha ya maumivu ya majereha, wasio na makazi n.k.

Ni tukio linalotugusa, Tanzania ni ya watu walioingiliana
Inatugusa hapa nyumbani na walio nje ya nchi.

Tuwaombe wepesi , faraja na maisha walionusurika, na waliotangulia.

Tukio lilianza kusikika katika vyombo vya habari vya kijamii kwanza
Kisha mashirika ya nje, halafu vyombo vya nyumbani

Ilichukua muda mrefu kwa serikali kutoa taarifa kamili kupitia vyombo husika

Tunazo idara za hali ya hewa, maafa, habari n.k. zilizotakiwa kuhabarisha

Kukosekana kwa taarifa za awali kulizua taharuki kwa wenye ndugu, jamaa , marafiki n.k. ndani na nje. Hivyo, kulikuwa na ombwe la habari

Hili ni janga kubwa la kitaifa, tulitegemea japo kiongozi mmoja wa kitaifa kuzungumza na wananchi kwa minajili ya kuwahabarisha, kuwatuliza, kuwaelekeza na hata kuwaonya kuhusiana na tukio.

Vyombo vya habari vilisuasa sua kana kwamba vilisubiri 'ruhusa' badala ya kuwa mstari wa mbele kutafuta habari na kuziweka bayana

Laiti ingekuwa tukio la kisiasa, tungesikia kila kauli za heri au za shari
Tungeona vyombo vya habari vikiwa na kazi nzito ya picha na habari

Hili la maafa kuna kuvuta miguu kana kwamba hakuna ajuaye nani afanye nini, mwenye wajibu ni nani. Hakuna anayejua katika taharuki kipi cha kufanya

Katika majanga kama haya tunaweza kuona tofauti tulizowahi kusema
Kwamba, kuna woga na nidhamu ambavyo ni ngumu kuvitenga ''thin line'

Kisichoweza kuonekana mapema ni je, tupo tayari kwa majanga ya asili au tupo tayari lakini hatupo tayari kifikra na kisaikolojia?

Tusemezane
 
MAJANGA YA ASILI NA MAAFA

TUTAJIFUNZA LINI?

Kama nchi na Taifa la dunia, Tanzania haina kinga dhidi ya majanga ya asili na maafa
Tumekubwa na majanga kama ya mafuriko , kiangazi, matetemeko n.k kila mara

Ni kutokana na hilo, kulionekana umuhimu wa kuwa na kitengo cha maafa ofisi ya waziri mkuu
Kitengo cha maafa popote duniani ni kikosi maalaumu kilichoandali wa maafa na majanga

Katika nchi za wenzetu, kitengo hicho huwa na bajeti yake kikiwa kimesheheni wataalam
Hao ni Wahandishi, madaktari, wagani, watu wa logistic , habari n.k.

Tukio la juzi kama tulivyoeleza limetisha na kuleta kiwewe kwa watz popote walipo duniani
Kiwewe kinatokana na kutokuwa na mfumo mzuri wa habari wala kuona maendeleo ya uokozi

Mathalan, watu walio nje ya nchi, walikuwa na limited information kutoka serikalini
Walioko mbali na eneo la janga, mikoani na kwingineko nao pia walipatwa na taharuki

Yanapotokea majanga kama haya, ni muhimu kuwa na press conference za kuhabarisha umma nini kinatokea, na nini kinafanyika. Hayo yatasaidia kuondoa 'panic' kwa walio mbali

Tulitegemea kuwa na press conference kila baada ya masaa kadhaa ili kupata habari za serikali

Kilichotokea ni habari kupatikana kupitia mitandao ya jamii

Vyombo vya habari navyo havijatoa uzito ukilinganisha na wiki zilizopita. Tunaelewa, huenda ni hofu iliyojengwa ya vyombo hivyo kufungiwa na hivyo vinajaribu kujiweka 'salama'

Kuna uwezekano kikosi cha maafa kilikwenda(?) hata hivyo ni muhimu wananchi wakajua
Tumeona watu wamelala sakafuni ikiwa ni dalili ya kukosa organization

Kikosi cha maafa kingekuwa na nafasi nzuri ya kushauri nini kifanyike
Hatuna uhakika wa majengo kama ya Hopsitali na kwingine. Hiyo ni kazi ya kikosi cha maafa

Tunarudia, kutangazwa au kuonekana kwa kikosi cha maafa si kwasababu ya kujitangaza.
Ni katika kupunguza kimuhe muhe kwa walio mbali na kutoa matumaini penye hofu

Ni katika kuratibu shughuli pamoja na huduma kwa kuzingatia uwepo wa vifaa
Inaendelea
 
TUTAJIFUNZA LINI?

Sehemu ya II

Kikosi cha maafa kikiwa na wataalam na vifaa kilitakiwa kuwa eneo la tukio haraka iwezakanavyo

Kulihitajika mahema, mahema ya wodi za dharura, makazi kwa walionusurika na huduma nyingine

Kikosi kilitakiwa kiwe katika eneo tukijua upo usafiri wa dharura. Je, ilikuwa hivyo?

Ingalikuwa muhimu kwa 'drill' kama tulizoona za polisi kufanywa katika vikosi kama hivi

Swali, ni je, tunatambua vipaumbele katika mambo kama haya ya maafa?

Kwavyovyote iwavyo, ni lazima tukiri , katika eneo la habari na kikosi cha maafa hatujajifunza

Siku tatu baada ya tukio na kwa kuangalia wenzetu wengine duniani tukiri kuwa tuna tatizo

Kwa upande mwingine, kuna kukosekana kwa washauri katika ngazi za juu

Suala la tetemeko haikupaswa kusubiri dakika za mwisho na kelele mitandaoni kugusa viongozi

Kwa ukubwa wa tukio kama lilivyoripotiwa, viongozi wangeshauriwa mapema

Hili pengine linalandana na yale tunayosema, woga au nidhamu ya waoga ya kushauri

Tumalizie kwa kusema
Haionekani kama tunajifunza kutokana na matatizo yaliyowahi kutupata
Tuna tatizo katika utoa habari, ukusanyaji na usambazaji
Tuna tatizo katika kujiandaa kwa maafa 'preparedness'
Hatuna viapumbele katika mipango yetu inayohusu jamii

Haitoshi kuonekana katika majonzi, tunapaswa kufikiria namna ya kukabiliana na majanga kitaalam, kufuatilia hali baada ya maafa, kujitathmini wapi tumefaulu na wapi tumefeli ili makosa ya haya yasiendelee kutokea. Hii ni aibu kwa Taifa lililojitawala nusu karne

Endapo hatutajifunza kwa hili kama tulivyoshindwa nyuma, tutajifunza lini?

Tusemezane
 
JITIHADA HIZI ZIMELENGA NINI?

Sehemu ya I

Katika siku za karibuni kumekuwa na jitihada za taasisi, na mamlaka mbali mbali kueleza mambo kama uchumi

Idara ya Takwimu imeeleza uchumi kukua 7.9% ikilinganishwa na 5 za kipindi kama hicho 2015

Gavana wa bank kuu akatplea maelezo mara mbili, kwanza kuhusu kile kilichoitwa mdororo wa uchumi
Na majuzi kaeleza kuhusu uchumi akionyesha kukua uchangaiji wa pato la taifa na deni la ndani na nje

Halafu tukapata utafifiti wa taasisi ya Twaweza ukizungumzia mambo kadhaa nchini.

Ukitazama harakati zilizopo ni kama jitihada ima za kusafisha, kukuza au kuondoa hofu ya jambo Fulani

Tunaamini ,wananchi wa sababu za kufahamu nini kinaendelea katika serikali yao.
Serikali ina wajibu wa kueleza nini kinafanyika. Kwa hali zote,muhimu ni kutumika kwa ukweli na ukweli mtupu

Idara ya takwimu inasema ongezeko la uchumi kwa 7.9 karibia na 8% limechangiwa na sekta ya madini, utengenezaji na nishati. Inasema ongezeko la gesi asili limeongeza upatikanaji wa nishati

Hoja katika mchanganuo huu ipo katika 'manufacturing'. Je, ni vitu gani tunatengeneza na vimeongeza pato la Taifa tukijua mpango wa Tanzania ya viwanda haujaanza kutekelezwa?

Je mchango wa madini ni katika eneo gani, uuzaji,mauzo au kodi?

Gavana wa BOT alizungumzia sekta zilizochangia ukuaji wa pato la Taifa.
Alitaja maeneo kadhaa, moja likiwa ni upande wa mawasiliano. Kwamba eneo hilo limechangia asilimia 13.

Asichotueleza Gavana ni upana wa eneo la mwasiliano na ni eneo gani limechangia Zaidi.

Je, ni kodi za watumiaji huduma kama simu? Je, ni kodi za mashirika? Hayo yalibaki gizani

TWAWEZA nao wakaja na utafiti ambao hatuwezi kujua ni research au ni survey.

Hii ni taasisi ambayo tafiti zake zimetiliwa shaka kwa nyakati, maeneo wanayofanyia na ithibati ya taarifa zake

Inaendelea....
 
Back
Top Bottom