Duru za siasa: Bunge la Katiba, upotoshaji na kiwewe cha kuzinduka Tanganyika

Duru za siasa: Bunge la Katiba, upotoshaji na kiwewe cha kuzinduka Tanganyika

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Posts
15,773
Reaction score
32,431
MBINU ZIMEKWISHA, SASA NI UPOTOSHAJI
WALENGWA NI VIJANA NA WANANCHI WA KAWAIDA MITAANI NA VIJIJINI

Bunge la katiba linaendelea Dodoma kukiwa na msuguano mkubwa ndani ya CCM.
Nje ya CCM kuna upinzani dhidi ya wahafidhina wa CCM wanaotaka kulitekea bunge kwa masilahi yao

Msuguano wa CCM unatokana na chama kupungukiwa na udhibiti miongoni mwa wanachama.
Awali, CCM ilidhani mbinu za kuuteka zingefanikiwa kama tulivyoeleza mwaka jana.

Matumaini ya CCM yalikuwa udhibiti wa tume ya Warioba itekeleze matakwa yao, na matumizi ya wingi wa wabunge wakisaidiwa na Spika wa bunge la katiba

Udhibiti kwa njia hizo unaonekana kutokuwa na mafanikio kutokana na hali ya kisiasa nchini na mwamko wa wananchi katika baadhi ya mambo kama hili la katiba.

Baadhi ya wanaCCM hawakubaliani na chama hasa suala la muungano.
Mbinu za kupotosha rasimu kama kutumia hoja ya gharama za serikali 3 imeshindikana.
Na suala la kutumia kura ya wazi linaleta tatizo

Mbinu za kutumia rasimu mbadala ya Nape na Andrea haionekanani kuwa na matumaini.
Rasimu mbadala inaonyesha CCM wanaunga mkono serikali 3 kwa muundo wa Warioba. Wasichokubaliana nacho ni kupunguza nguvu za kisiasa

Nguvu ya hoja za kuizindua Tanganyika inazidi kushika kasi.
CCM imeanza kutumia mbinu za kuwatisha wabunge na wananchi

Mbinu za mwanzo ni ile ya Rais kubadili msimamo wa kuheshimu mawazo ya wananchi kupitia tume, ghafala akarudi katika serikali 2, na makamu wa rais kutumwa kuongea na vyama vya siasa akisistiza serikali 2

Wiki hii, Rais Shein wa SMZ akiwa na makamu wawili, Seif Hamad na Idd Seif walizundua logo na kauli mbiu za maazimisho ya miaka 50 ya muungano.

Katika hali ya kawaida hili halikuwahi kutokea siku za nyuma, ni wazi shinikizo la muungano linazidi.
Rais Shein amesema msimamo ni serikali 2 kinyume na matakwa ya wazanzibar ambao ndio hasa walioanzisha sakata la uzinduzi wa Tanganyika.

Katika hali ya kuchanganyikiwa ndani ya CCM hasa kuzinduka kwa Tanganyika, viongozi wameanza mbinu za kupotosha wananchi. Wanawalaghai vijana wadogo waliozaliwa nyakati za Tanzania, na wale wa mitaani ambao tofauti kati ya Tanzania na Tanganyika kwao haipo uwazi.

Waziri mkuu Pinda amenukuliwa akiuliza wanaotaka Tanganyika wanataka ipi ya 1961 hadi 1964 au ya Mkoloni? Hoja hii imelenga kupotosha umma,Tanganyikailiyokuwepo miaka ya 1800 na hadi leo

Kama umetusoma vema, hatutumii neno kurudisha Tanganyika kwasababu ipo,neno muafaka ni kuizundua. Kwa maneno ya kisayansi Tanganyika ni ‘recessive' ndani ya Tanzania.

Recessive ni kitu kilichopo ambacho hakionekani kwa uwazi.
Kinachotakiwa kufanywa ni kuifanya ionekane kwa uwazi na majukumu yake ‘dominant'.

Kabla hatujarudi kwenye historia kuonyesha uwepo wa Tanganyika moja bila kujali miaka, tungependa kuwaelewesha watu kuwa Tanganyika ipo ndani ya Tanzania hadi leo hii.

Kinachotakiwa ni kuizindua kutoka katika ‘nusu kaputi' ili itekeleze majukumu yake.
Pinda anapotosha kwa kile Mchambuzi anachokisema kuwa ‘even magician runs out of trick'
kwamba wacheza mazingaombwe kuna nyakati huishiwa mbinu.

Kwa Muktadha huo ni jambo la hatari kupuuza kauli za Pinda zilizolenga kuupotosha umma.
Duru tunauona ukumuhimu wa kukabiliana na hoja potofu

Ni makosa mgonjwa aliye katika dawa ya usingizi kumwita marehemu, Tanganyika si marehemu. Tutakuwa na mwendelezo wa kufafanua kuhusu Tanganyika, tofauti kati yake na Tanzania n.k.

Tutaeleza umuhimu wake kwa nyakati za sasa na kutemebelea hoja zinazoambantana na mada.

Tutaanza na sehemu ya I hadi ya V, tunaomba uvumilivu ili tuwe na mtiririko mzuri wakati tutakapoanza mjadala.

Sehemu ya kwanza inafuata


 
Sehemu I

Upotoshaji kuhusu Tanganyika umefikia kiwango cha kutisha. Majuzi waziri mkuu wa JMT mh Pinda aliuliza kuhusu Tanganyika. Katika maswali aliyouliza na hoja alizojenga Mizengo Pinda ameshindwa kutumia japo elimu kidogo katika udanganyifu. Pengine Pinda alielewa ufahamu wa kundi alilokuwa anaongea nalo na hivyo kutumia fursa hiyo kupotosha umma kwa kiwango kizuri tu. Tafadhali msome hapa chini kwanza kwa maneno yake
1) WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amekiri kuwa Bunge Maalumu la Katiba, limeanza na changamoto, huku akihoji wanaotaka Serikali ya Tanganyika, wanakusudia ipi ya mkoloni au ya baada ya uhuru ya miaka mitatu.

2) Mbali na hilo, amesisitiza yeye na chama chake cha Mapinduzi wanataka mfumo wa serikali mbili na si tatu kama Rasimu ya Katiba ilivyopendekeza.


3)Pinda aliyasema hayo jana wakati akifungua semina ya viongozi na watendaji wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwenye Makao Makuu ya chama hicho, White House mjini hapa.

Pinda ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, alisema zipo hoja nyingi za msingi katika mchakato huo wa kutunga Katiba, lakini kubwa na litakalochukua muda mwingi ni muundo wa Serikali. Hata hivyo, alisema wazi msimamo wake na ule wa CCM kuhusu pendekezo lao la kuwa na Serikali mbili, kinyume cha Rasimu ya Katiba inayopendekeza Serikali tatu.

4) "Hata ukiniamsha usingizini usiku wa manane, kwangu mimi bado Serikali mbili ni muundo mahsusi.

5) "Mwalimu Nyerere hata wakati ule alikaa na Tanganyika kwa kipindi kifupi, mwaka 1961 Tanganyika ikawa huru, 1962 tukawa Jamhuri, 1963 Zanzibar ikapata uhuru (baadaye alisema Uhuru wa bandia), mwaka 1964 ikazaliwa Tanzania.

6) "Tanganyika ya kikoloni ndiyo iliyokaa muda mrefu, hii nyingine ni kutoka mwaka 1961, 1962 na 1963. Ikazaliwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

7) Leo hii miaka 50 tuko ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunadai Tanganyika," alihoji Pinda na kuongeza:

8) "Tanganyika ipi? Nikadai ile ya mkoloni? Kipi kimo katika Tanganyika ya miaka mitatu?
Tanganyika wakati inazaliwa nilikuwa na miaka 13, Tanzania nilikuwa na miaka 16, naujua vizuri Muungano.

9) Kuanzia pale sijui chochote kingine, kama ilivyo wengi wetu humu.

10) "Au wale waliozaliwa miaka 50 iliyopita, wanaijua vizuri zaidi Tanzania. Tanganyika ipi mnazungumzia?
Maana haikuwapo zaidi ya ile ya kikoloni iliyokaa muda mrefu."

11) Alisema njia bora ni kukaa chini na kuzungumzia matatizo ya muundo wa Serikali mbili na kuyaboresha kwa nia ya kusonga mbele kuliko kudai Serikali ya Tanganyika.

Waziri Mkuu alisema si vyema kuanza sasa kujaribu muundo wa Shirikisho baada ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, huku akitolea mfano wa Shirikisho la Afrika Mashariki (EAC).

"Pale kuna Shirikisho la Afrika Mashariki, lakini angalia mambo yanavyokwenda sasa wakubwa wakikutana. Utasikia wanazungumzia ardhi, mara pasipoti.

12) "Haiwezekani miaka 50 baada ya Muungano tuanze majaribio ya Shirikisho. Aah, wapi tunataka kwenda. Tanzania Bara na Zanzibar wana historia ya udugu na ushirikiano. Ukaribu, lugha moja na kuoleana," alisema Pinda.

Huku akirejea kauli mbalimbali za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alisema hata hilo Shirikisho linalopendekezwa litakwama, kwa sababu Rais wake hatakuwa na ardhi, na kama nchi wanachama zitakataa kutoa ardhi, atafanyaje kazi zake.

13) Alisema tatizo lililopo ni utambulisho wa Zanzibar na suala la umiliki wa ardhi kwa Tanzania Bara wakiwa visiwani, ambayo alisema ni mambo yanayozungumzika.

14) "Suala hapa ni utambulisho wa Zanzibar ambalo hata hivyo si suala kubwa na tunaweza kulisahihisha.
Pia liko suala la ardhi Zanzibar. Lakini wanaotaka ardhi huko, lazima wajiulize je, kweli iko ardhi ya kutosha," alieleza

Kwa hisani ya Habari leo.
Wanaduru, ili kuweza kuelewa aina ya viongozi tulio nao na uwezo wao wa kuongoza, tumeweka namba katika hoja za mh Pinda zionyeshe kwa uwazi zilivyokosa mashiko na zilivyojaa upotoshaji

Hoja #9 , Pinda anasema tangu alipokuwa na miaka 16 Tanzania ilipoundwa hajui chochote tena kuhusu Tanganyika au Tanzania. Inawezekana anachoongea ni ukweli kama tutakavyoona.

Anasema Tanganyika ilitoweka miaka 50 iliyopita na ni miaka 50 tupo ndani ya JMT # 7.
Wakati anadai Tanganyika ilitoweka miaka 50 na kupata JMT, Pinda anatuzalishia taifa lingine lisilojulikana Tanzania bara (# 12). Waziri mkuu hajui Tanganyika ilipotelea wapi na wala hajui Tanzania bara ni nchi ipi.

Pinda anasema tupo ndani ya JMT kwa miaka 50 na hatupaswi kudai Tanganyika (# 7) halafu anasema kinacholeta tatizo znz ni utambulisho wa znz (# 13).

Pinda amesahau kuwa hoja # 7 sisi ni JMT, kama ni hivyo kwanini znz ihitaji utambulisho, wakati Tanganyika ilikufa miaka 50?

JMT inaundwaje kama kuna utambulisho mmoja ili hali muungano ni wa nchi mbili.
Kwanini ashadidie kifo cha Tanganyika(#7) halafu atukuze utambulisho wa Zanzibar(# 13).

PM anasema Tanganyika ipi ya miaka mitatu baada ya uhuru au ya Mkoloni (# 1). Asichokielewa Pinda (#9) na hata akiamshwa usingizini (# 4) ni kuwa Tanganyika imekuwepo kwa karne.

Ilipotawaliwa na Mjerumani ilikuwa Tanganyika, ilipowekwa chini ya udhamini wa mwingereza ilikuwa Tanganyika.

Nyerere alisoma Tanganyika, akajiunga na Tanganyika African Asscoiation (TAA), wakaunda TANU ambayo herufi ya mwanzo ni Tanganyika.

TANU ilikufa mwaka 1977 ikiwa Tanganyika na wala si Tanzania African National Union.

Nyerere aliendesha harakati za kudai uhuru kwa kutumia TANU, akaenda UNO kuomba uhuru wa Tanganyika.

Tanganyika ikapewa serikali ya madaraka ya ndani na Waziri mkuu wa kwanza wa Tanganyika ni Nyerere.

Dec 9 1961 Bendera iliyopandishwa uwanja wa taifa ilikuwa ya Tanganyika. Mwaka 1962 tukawa Jamhuri ya Tanganyika.

Mkataba wa muungano na Zanzibar hausomeki kwa neno Tanzania bali Tanganyika. Katiba ya mpito ya kwanza ilikuwa ya Tanganyika.

Pinda anaposema Nyerere kaishi na Tanganyika kwa miaka 3 ni upotoshaji usio na hata chembe ya usomi. Pengine Nyerere amekaa na Tanganyika zaidi kuliko alivyoakaa na Tanzania.

Kwahesabu za haraka za elimu ndogo Nyerere ameishi Tanganyika kwa miaka 45 na Tanzania kwa miaka 32.

Sasa Pinda anamsingizia kwa lipi.
Kipi kipimo cha Tanganyika alichotumia ?(# 8)

Pengine kutokana na usingizi (# 4) Pinda anaamini kuwa yeye ni waziri mkuu wa JMT (# 6) na kwavile hajui lolote (# 9) Pinda hafahamu kuwa mamlaka yake hayavuki bahari. Je, JMT ipi anayoongelea mheshimiwa?

Pinda anasema njia bora ni kukaa na kuzungumzia serikali 2 (# 11).
Kwa vile haelewi kama alivyokiri ni wazi kuwa hakumbuki kuwa yeye ni waziri mkuu kwa miaka 5 na matatizo ya miaka 50 aliyoyakuta hajaweza kutatua hata moja zaidi ya kuongezeka.

PM anasema kuundwa kwa shirikisho kuna tatizo la Rais wa shirikisho kukosa ardhi endapo washirika watakaa kutoa.
Pinda amesahau kuwa hoja # 13 na #14 anadai znz haina ardhi ya kutosha.

Kama ni hivyo katika serikali 2 nani anatoa ardhi?
Na kwanini sisi kama JMT tubaguane kwa ardhi, kwamba znz ni kidogo na bara ni nyingi. Msukuma wa Shinyanga atakaposukumwa na Mpemba kutoka eneo lake hapo kuna udogo na haki?

Ni kwanini anadhani Mtanganyika hana sababu za kupata ardhi znz, na kwanini haki hiyo apewe mznz ambaye si kwamba ni mshirika tu bali ana utambulisho (# 13).

Endapo znz inataka utambulisho(#13) ni upi huo utakaovuka bara ? na kwanini Mtanganyika asipewe utambulisho wake kama ilivyo mznz ili kwa pamoja wakae na kujadili JMT?
Kwanini Pinda adhani JMT ni kitu cha pamoja na znz ni kitu pekee?

Wanaduru ukisoma hayo kwa uchache utagundua kuwa Pinda aliyasema ima kwa kutokujua (# 9) au kutoka usingizini (# 4) na nidhahiri hana ufahamu na anachokiongelea.
Pia kuna uwezekano anajua anaoongea nao (# 3).

Tutaendele na sehemu ya II kuonyesha upotoshaji wa mh Pinda na jinsi anavyojichanganya kwa kuangalia jinsi Tanganyika ilivyotoweka

Itaendelea sehemu ya II
 
Sehemu ya II

Tumeona kwa uchache jinsi waziri mkuu anavyoweza kuudanganya umma kuhusu Tanganyika. Pinda hafahamu Tanganyika ilikuwepo na ilipotezwa katika mazingira ya kutatanisha mwaka 1965-1967


Katiba ya mpito na ya muda sheria zilizotumika zilikuwa za Tanganyika.

Kwa mtu mwenye uwezo na nia njema hatasita kutambua Tanganyika imetengeneza sheria za muungano kama ilivyo article of union ya Tanganyika and Zanzibar.


Mh Pinda anaposema Tanganyika ya muda mrefu ni ile ya mkoloni na kwamba Nyerere alikuwa na Tanganyika kwa miaka 3 inasikitisha. Tanganyika haijawahi kubadilika kwa maana kuwa siku ya Uhuru hakukuwa na uchaguzi wa jina la Tanganyika.


Ni uzushi kusema kuna Tanganyika ya mkoloni au Tanganyika ya Nyerere.

Tanganyika ni ile ile daima na hata sasa ipo ingawa Pinda hakubali hilo.


Uwepo wa Tanganyika ni pale Pinda anapofanya kazi zake Tanganyika na haruhusiwi kuzungumza hata na sheha kule visiwani.


Kwamba sheha(balozi wa nyumba 10) ana nguvu za kisiasa kuliko Pinda akiwa visiwani. Pinda haelewi hilo na anaamini kuwa ni waziri mkuu wa JMT.


Kinachomchanganya mh ni ufahamu wa vitu vifuatavyo ambavyo hakika vinawachanganya wengi pia. Kuna taofauti ya mambo yafuatayo



  1. Nchi (country) 2. Taifa(nation) 3. serikali/state (government)

Mbele ya safari tutafanunua maana ya vitu hivyo ambavyo vinamchanganya waziri mkuu au anavichanganya ili kukidhi haja yake ya upotoshaji.


PM anasema suala ni serikali 2 ni watu wakae wazungumze matatizo yaliopo.

Mh Pinda is on the wrong side of history, Pinda is out of touch with society


Tumeuliza swali hili na ii ni mara ya 23, kwamba kwa miaka 50 CCM imeshindwa kutatua kero za muungano, ni dawa gani ambayo haikuwepo miaka 50 na sasa imepatikana?


Swali hili halijawahi kujibiwa na mCCM yoyote achilia mbali Pinda aliyekiri kutojua lolote kuhusu Tanganyika.


Tumeuliza, katika tume 5 zilizoundwa hakuna iliyokuja na mapendekezo ya serikali 2. Tume zote ziliundwa chini ya usimamizi wa CCM na viongozi wa CCM.


Labda mh Pinda hajui tume ya Nyalali, Kisanga na Warioba(siyo hii ya sasa) zilikuja na mapendekezo gani.


Kusema kuwa matatizo ya serikali 2 yanazungumzika ni intellectual abuse , na inatuacha tukijiuliuliza kama waziri mkuu hana ufahamu wa mambo mepesi kama haya, ni vipi tutaweza kuondoa umasikini nchi hii.


Hoja ya msingi hapa ni kuwa PM anapotosha.

Hakuna Tanganyika ya vipindi, Tanganyika imekuwepo kwa karne na hata kuondoka kwake kulikuwa kupitia sheria za mwaka 1967 ambayo haikutamka kuzikwa kwa Tanganyika bali kuibuka kwa nchi ya Tanzania.


Nchi ya Tanzania ina Tanganyika na Pinda ameonyesha wazi pale aliposema Znz inahitaji utambulisho.


Utambulisho wa znz ulitoweka kwa katiba ya mwaka 1977 ilipojulikana kama Tanzania visiwani. Hivyo ubara ulitokana na uwepo wa Tanzania visiwani.


Pinda kudai kuna nchi ya Tanzania bara si kweli, hakuna nchi hiyo!

Ni udanganyifu mkubwa wa kisiasa.


Unapoondoa znz katika JMT kwa utambulisho, tunabaki na Tanganyika ambayo Pinda hataki kuiita Tanganyika ili tu awe waziri mkuu ‘toy' wa JMT.


Lakini si hapo tu Pinda lazima aelewe jinsi muungano ulivyoundwa na kama vyama vya ASP na TANU vilishiriki. Lazima aelewe ushiriki wa wananchi ulikuwa kiwango gani. Kwa hayo Pinda ataweza kuelewa kama CCM ina mandate yoyote juu ya Tanganyika na muungano kwa ujumla.


Tutaangalia hayo sehemu inayofuata.


Itaendelea…


 
Inaendelea.....

Kwa wasomaji pamoja na Pinda, mkataba wa muungano wa mwaka 1964 haukutaja Tanzania hata sehemu moja.

An Act to ratify the Article s of Union between the Republic of Tanganyika and the People 's Republic of Zanzibar..........

Kwa tafsiri isiyo rasmi kwa minajili ya mjadala(Naomba radhi kwa upungufu wa tafsiri, maneno hayo yana maana ya 'Sheria ya kuridhia muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar'
The Republic of Tanganyika and the People 's Republic of Zanzibar shall, upon Union Day and ever after, be united into one Sovereign Republic by the name of the United Republic of Tanganyika and Zanzibar.

Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar wakati na baada ya muungano watakuwa Jamhuri huru kwa jina la Jamhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Tutambue kuwa muungano ulikuwa wa Jamhuri mbili, Tanganyika na Zanzibar.
Ili kumuonyesha zaidi mheshimiwa kuwa Tanganyika haijafa, sheria zilianza kujengwa kwa kutumia katiba ya Tanganyika


Subject to the provisions of this section and to any Act of the Parliament of the United Republic whereby the provisions of the interim Constitution of the United Republic may be altered, the United Republic shall begoverned during the interim period in a ccordance with the provisions of the Constitution of the Republic of Tanganyika a s so modified a s to provide ...

Kwa mujibu wa vifungu vya ibara hii na mswada wowote wa bunge la jamhuri ya muungano
ambao vifungu vya katiba ya mpito vyaweza kubadilishwa, jamhuri ya muungano itaendeshwa katika kipindi cha mpito kufuatana na vifungu vya katiba ya Tanganyika kama vilivyorekebishwa kukidhi yafuatayo

(i) the Constitution and government of the United Republic,(Katiba ya Jamhuri ya muungano)
(ii) Exter rna l Affa irs ;(Mambo ya nje)
(iii) Defence ;(Ulinzi)
(iv) Police ; (Polisi)
(v) Emergency Powers ; (Hali ya hatari/dharura)
(vi) Citizenship; (Uraia)
(vii) Immigra tion;(Uhamiaji)
(viii) Exte rna l trade and borrowing;(Biashara ya nje na mikopo
(ix) the Public Se rvice of the United Republic;( Utumishi wa jamhuri ya muungano)
(x) Income ta x, corpora tion tax, cus toms and excise duties ;(kodi, ushuru na maduhuli)
(xi) Harbours , civil avia tion, posts and te legraphs ;(Bandari, mambo ya anga, posta)
and for the exclusive authority of the said Parliament and
Executive in such matters throughout and for the United Republic
and in a ll other matters in and for Tanganyika;
Na kwa mamlaka pekee ya bunge na watawala katika mambo ya jamhuri ya muungano na yote kwa Tanganyika

Tunaona Tanganyika ilivyoshiriki kuandaa katiba ya mpito hadi pale bunge litakapoitishwa.

Na kwa mujibu wa vifungu hivyo, hakuna mahali imetajwa Tanzania au Jamhuri ya muungano wa Tanzania, vilivyotajwa ni Jamhuri ya muungano tu kwa maana ya nchi mbili.

Mh Pinda anakosea anaposema Tanganyika ya mwaka 1961,1962,1963.
Tanganyika ilikuwepo kabla kama nchi na kupita mwaka 1964 sheria zake zikigeuzwa kuwa za Muungano. Bunge lililoifuta Tanganyika halikutokea mwaka 1963 au 1964 kama inavyopotoshwa

Mkataba ulitoa idhini ya mambo 11 lakini baadaye yaliongezeka.
Nguvu za kuongeza mambo hayo ilianza kidogo kidogo kama inavyoonekana hapa

The modifications to the Constitution of Tanganyika provided for in subsection (1) of this section sha ll be made by Decree of the President of the United Republic and the power of the said President in that behalf ma y be exercised from time to time ; and such Decrees , and any amendments , variations or substitutions thereof made in the like manner, shall have effect for the modification of the Constitution of Tanganyika for the purposes of this section and for the alteration, of the interim Constitution of the United Republic

Marekebisho ya katiba ya Tanganyika kwa mujibu wa kifungu kidogo cha kifungu cha (1) yatafanywa kwa amri ya rais wa jamhuri ya muungano na kwa mamlaka yake kwa nyakati mbali mbali, na amri za marekebisho, mabadiliko yakayofanywa, yakakuwa na nguvu za kubadili katiba ya Tanganyika na ya mpito na kwa mujibu wa kifungu kubadilisha katiba ya mpito ya jamhuri ya muungano.

Wana duru, muungano uliopo haukujengwa kwa nguvu za chama chochote cha siasa.

Hakuna mahali TANU au ASP imetajwa katika mtiririko mzima.

Inashangaza wana CCM wanaposema msimamo wa chama chao ni serikali 2 tangu miaka 50 iliyopita.

Mabadiliko yaliyofanywa ya katiba ya Tanzania mwaka 1977 baada ya Tanganyika kumezwa kiaina na bunge la mwaka 1967 ndiyo yaliyoipoteza Zanzibar na kuwa Tanzania visiwani.

Ni mabadiliko hayo ndiyo yalikuwa na uCCM kwasababu kilikuwa chama kimoja kilichoshika hatamu.

Zanzibar ikaandika katiba yake 1979 na kuirejesha hadhi ya Zanzibar badala ya Tanzania visiwani.
Jumbe aliandika waraka wa kutaka uwepo wa serikali 3 kama mkataba wa muungano ulivyokuwa.

Wengi wanapotosha hoja inayomhusu Jumbe. Wajumbe wa BLM akiwemo Nasor Moyo wamesema tatizo la Jumbe ni kufanya mambo kwa siri jambo lililopelekea kuonekana kama njama za uhaini.

Kumbuka wakati huo tulikuwa JMT.

Kitendo cha Znz kuandika katiba yake na kuukana Utanzania visiwani kiliamsha hisia kwa Watanganyika na kuchangia curiosity ya muungano.

Hoja ya kujiunga na OIC bila kuwasiliana na serikali ya JMT ilionekana kama uvunjaji wa katiba.
Hilo nalo likachangia kuanzishwa kwa kundi la G55 katika bunge la JMT likitaka Tanganyika.

Hoja ya G55 haikukataliwa na Nyerere kwasababu ya serikali 3. Alichomaanisha Nyerere ni kuwa kwa wakati huo hiyo haikuwa sera ya CCM ambayo ilishika hatamu. Hivyo waliotaka hoja hiyo wajiondoe kwanza ili waitetee nje ya chama.


Lakini kibaya zaidi ni pale watu wachache kwa jina la wabunge wanapokaa mahali na kutaka kuamua mustakabali wa nchi bila kuwauliza wananchi.

Kosa la kutouliza watu kuhusu muungano Nyerere aliliona baada ya muda mrefu na alitaka lisijirudie tena pengine kwa kuangalia na mabadiliko ya nchi, kijamii, kisiasa na kiuchumi.
Kwa bahati mbaya Kikwete hakuweza kujifunza kutokana na makosa ya nyuma na amerudia kosa lile lile.

Na hata sasa hivi JK anaposisitiza serikali 2, katiba si suala la chama. Hii aliyoapa kulinda haikutenegenezwa na chama cha siasa kwa asili yake.

Wabunge wa CCM kukaa Dodoma na kutaka kushinikiza hoja zao ni makosa yale yale ya G55 kutaka kuamua mustakabali wan chi na kuwaacha wananchi nje ya maamuzi ya mustakabali wao.

Kwa uchache sana unaweza kuona kuwa suala la Tanganyika si la leo na wala si la tume ya Warioba. Tanganyika ipo lakini imefichwa kwa kivuli cha Tanzania, tena ikiwa yenyewe bila mshirika wake.

Mshirika wa Tanzania ni znz ambaye hugeuka kuwa Mtanzania pale anapoihitaji Tanganyika.


Tutarejea kuonyesha jinsi mambo 11 hapo juu yalivyoongezeka kufikia 22, yaliongezwa vipi na kwa faida ya nani na jinsi yalivyoondolewa nusu nusu kwa ujanja na faida ya mzanzibar kwa gharama za Mtanganyika na hapa tutagusia mabadiliko ya katiba ya znz ya 2010 pia.

Itaendelea......
 
SEHEMU YA II
Tunaelekea kujadili mambo yenye utata kwa pande zote mbili.
Duru tunasisitiza Tanganyika imekuwepo kabla ya uhuru na baada ya uhuru.

Tanganyika imefutwa na sheria namba 24 ya 1967 iliyoibadilisha na kuwa Tanzania bara.
Pinda Anaposema miaka 50 iliyopita si kweli.
Pinda anapouliza Tanganyika ipi, jibu ni Tanganyika ile kabla hajazaliwa na alipokuwa na umri wa miaka 18 ilipofutwa

Katiba ya muda ilikusudiwa kuwa ya mwaka mmoja, ikaenda hadi miaka 10.
1977 katiba ya kudumu ikaandikwa na kuanzisha Tanzania bara nchi mpya ya Pinda na Tanzania visiwani.

Mwaka 1979 Znz ikaandika katiba ya kulikataa jina la Tanzania zanzibar au visiwani.
Pinda aelewe tayari znz ina utambulisho wake kwa katiba ya 1979, hakuna haja ya utambulisho zaidi. Utambulisho wa znz umefanyika kwa nguvu za kisheria mara nyingine ukikiuka katiba ya JMT mwaka 2010 na kujipa uwezo mkubwa zaidi ya ule wa JMT

Katiba ya 2010 imeipa hadhi znz kuwa nchi. Ni kwa muktadha huo JMT imebaki na Tanzania bara ya Pinda ambayo ni Tanganyika.

Kwasasa Pinda anatakiwa aongelee utambulisho wa Tanganyika ambao haujulikani upo wapi kwasababu Tanzania si Tanganyika ingawa Tanganyika imebaki kuwa Tanzania.

Suala la kurudi kwa serikali ya Tanganyika si la leo au jana, limefukuta miaka mingi, Pinda akisoma, akiwa ofisi ya mwanasheria mkuu, afisa wa Ikulu, mbunge na waziri mkuu.
Tume zote zilizoundwa Pinda anazifahamu kuliko mtu mwingine.

Mh Pinda anaposema hajui Tanganyika ipi ni upotoshaji wa umma kwa kuelewa vijana wengi watababaika na pengine kumuona ana hoja ya maana.
Ukweli ni kuwa Pinda anababisha na hana hoja wala ushahidi wa kile anachokisema.

Sheria za Tanganyika zilibailishwa kuwa za Jamhuri ya Muungano na kisha JMT.
Mkataba wa muungano ndio ulianza kumpa rais wa Tanganyika kuongeza, kubadili na kurekebisha baadhi ya mambo kwa kutumia bunge.mambo yakaongezwa hadi kufikia 22.

Kuna nadharia mbili juu ya kuongezwa mambo hayo.
Kwanza, wapo wanaosema Nyerere alitaka kuimeza znz kiaina hivyo kuchukua kila kitu kudhibiti

Nadharia ya pili ni kuwa Nyerere alitaka kuwa na taifa moja Tanzania kama alivyotaka kuwa na East Africa federation mwaka 1963 kabla ya mapinduzi ya znz

Nadharia ya pili kwa ina mantiki. Nyerere aliona yapo mambo ambayo Znz inahitaji msaada. Mathalani, suala la elimu na elimu ya juu, ilikuwa ni vema kuwa na watu wenye elimu zinazolingana kuelekea taifa moja.

Asilimia 95 ya viongozi wa SMZ ni wafaidika wa elimu ya Nyerere iliyotoa fursa kwa wote.
Znz iliwezeshwa kwa nafasi maalumu na kwa gharama za JMT ambayo basically ni Tanganyika. bahati mbaya viongozi waliofadika na mfumo huo ndio vinara wa kumtukana katika majukwaa.

Muungano wa kwanza ulikuwa wa kisiasa ambao haukushirikisha vyama vya siasa.
Hata ushiriki wa wananchi ulikuwa mdogo.
Nyerere aliliona hilo na kulikemea katika Jumbe na masakata yaliyofuata kama G55.

Mabadiliko ya nchi na dunia hayatoi nafasi kwa muungano w
:A S 27:kisiasa.
Nchi zinazoungana kwa sasa zinalenga katika masuala ya siasa za uchumi na siyo uchumia tumbo.

Duru tukubaliane kidogo na Pinda kuwa muungano wa Tanganyika na znz upo karne nyingi kutokana na mategemezi ya kijiografia, miingiliano ya kijamii na kiuchumi.

Uhusiano huo haukusimamishwa au kusimamiwa na majeshi, vyama vya siasa au viongozi wa makundi, ni muungano uliotokea kiasili.

Lakini kwa mahitaji ya dunia ya sasa muungano wa kiuchumi na kwa siasa za uchumi hauepukiki. Viongozi wa pande zote wameshindwa kuliangalia hili kama tatizo,wamejikita katika mambo ya kisiasa wakitumia takwimu za kiuchumi kuchochea jamii zisizoweza kubaini ukweli.

Wananchi walipaswa kuulizwa ili waridhie kama upo umuhimu wa mahusiano ya karne kubororeshwa zaidi au yabaki kama majirani wema.

Hilo lingejeka msingi wa majadiliano ya aina ya ushirikiano unaohitajika. Na wala vyama vya siasa havipaswi kuongelea suala hili kwasababu msingi wa muungano haukuwa katika vyama.

Makundi yaliyojitokeza hasa upande wa znz yanatumia takwimu hafifu zisizo na mashiko katika kueleza malalamiko dhidi ya muungano.

Uhafifu wa takwimu na hoja umepotosha mambo 11 ya muungano kwa faida za kisiasa. Umepotosha ongezeko la mambo hadi 22 kwa faida ya Zanzibar.
Na umeamsha hisia za kujitambua kwa Watanganyika.

Sehemu inayoendelea tunajadili kwa kina matatizo yaliyopo na hatima ya muungano.

Inaendelea......
 
SEHEMU YA III

Wapo wasemao kurejea Tanganyika kutaua muungano.
Hoja hafifu sana, hadi sasa Tanganyika ipo baada ya Znz kujiondoa katika JMT.
Tanganyika imebaki ikiwa na sura mbili, kwanza, Tanganyika iliyojificha,pili ni Tanganyika ya JMT.

Mtanganyika serikali yake ndiyo ya muungano, mzanzibar anaihitaji penye manufaa.
Mwenyekiti wa kamati ya fedha BLW amekaririwa katika semina akisema' Znz haiwezi kuchangia sawa katika serikali ya shrikisho kwavile haina uwezo'
Maneno haya yana maana Tanganyika ndiye mchangiaji wa muungano.

Uthibitisho wa Tanganyika kuchangia zaidi muungano umetolewa na Samuel Sitta aliokuwa kiongozi wa shughuli za serikali bungeni akimkaimu Pinda.

Sitta alinukuliwa July 9 2011 akisema, He said:"Now if we allow a three Government system, the Union will automatically die because the Tanganyika government might refuses to share running costs of the Union government which will be by then a toothless bulldog'

He said if the Tanganyika and the Union governments are to be formed Zanzibar will be required to share the costs hence more competition on the Isles part

Mwaka 2013 Rais Sheni wa SMZalikaririwa akiuliza kwanini wznz waseme wanaonewa bila kujiuliza gharama za ulinzi na usalama na elimu ya juu znz wanachangia nini katika muungano.

Aliyekuwa waziri kiongozi Shamsa Vuai, wakati wakiwa waziri wa ulinzi wa JMT naye alikaririwa akisema muungano una faida kubwa kwa znz akitolea mifano ya ulinzi, elimu, usalama n.k.

Katika mambo 11 yaliyoongezwa kufikia 22 hakuna hata moja ambalo Tanganyika ni mnufaika.
Wanasisa uchwara wanatumia takwimu za misaada na mikopo kupotosha ukweli.

Wanawaaminisha watu, Tanganyika kwa jina la Tanzania inanufaika na misaada wakiacha mambo yanayogharamiwa na Tanganyika ikiwemo serikali ya JMT kama ushahidi unavyosomeka hapo juu.

Wamefika mahali wanadai nafasi za ubalozi ambazo si zaidi ya 40 kama ni tatizo linalowakwaza kiuchumi. Fursa za uchumi wanazozipata malaki ndani ya muungano ikiwemo free movement hawaziweki katika thamani bali kutumia hoja dhaifu, kipuuzi kupumbaza jamii

Mlolongo wa malalamiko hayo umepelekea Watanganyika kujiuliza maswali mengi.
1. Ni nani Tanzania na nani anagharamia Tanzania.

Kama ipo znz yenye malalamiko Tanzania ambayo znz imo inasimamia malalamiko dhidi ya nani. Jibu, Tanganyika haina mtetezi dhidi ya malalamiko ya znz ambayo msulushishi ni Tanzania.

Katiba ya znz ya mwaka 2010 ndiyo imevuruga zaidi. Znz ni nchi yenye mamlaka kamili.
Ina uwezo wa kufanya lolote bila kuulizwa, na katiba ya JMT ni dhalili mbele ya BLW

Udhalili wa katiba ya JMT ni wa kusikitisha sana. Imefika mahali Mtanganyika hawezi kupitisha mswada au sheria inayohusu mambo ya Mtanganyika bila watu 50 wanaojiita BLW kukubali.
Wajumbe wa BLW znz wanawakilisha majimbo madogo kuliko diwani wa Tanganyika.

Leo wamepewa nguvu kubwa na kiburi, jeuri kuamua kama Watanganyika wanataka sheria ya mambo yanayowahusu wao. Kwamba watu 50, wananguvu kuliko bunge la Tanganyika lenye watu 320. Hii ni dhalili wanayoishi nayo Watanganyika. Lakini hawajiulizi ni kwasababu gani za msingi

Wznz si kwamba wamevunja katiba ya JMT tu, bali wamekiuka mambo 11 ya mkataba wa muungano kama yalivyo katika bandiko namba 2 .

Wamefanya kwa kiburi na jeuri kuwa uwezo wanao na kwamba Tanzania haina uwezo juu ya mambo ya znz. Aliyepaswa kuwauliza ni Tanganyika ambaye hayupo ingawa anatumiwa na wzn katika mambo yao kwa jina la Tanzania

Mfano, wznz wamekiuka mkataba wa muungano wa mwaka 1964
Wameondoa bandari na kuunda chombo chao(ZMO).
Gharama za ZMO kule International Martitime organization(IMO)zinalipwa na JMT ambayo ni Tanganyika. Makusanyo ya bandari na usajili wa meli ni mali ya SMZ. Tatizo la meli za Iran ni mfano mzuri sana

ZNZ imeanzisha Civil aviation(mambo ya anga) wakati katika jumuiya ya kimataifa Tanzania ndiyo inayolipa gharama za ushiriki na dhamana zingine. Znz inaendesha chombo kwa gharama za Tanganyika.

Suala la gesi na mafuta halikuwemo katika mkataba wa awali, znz imekimbilia kuliondoa katika kwa kujua itafadika bila kuishirikisha Tanganyika.

Hao wanaofanya hivyo ni viongozi waliosoma kwa hisani, nafasi za upendeleo na kodi ya Mtanganyika kwa jina la Tanzania. Kwamba, wznz walikuwa Watazania bila mafuta, yalipopatikana ni wznz siyo Watanzania.

Na katika kuhakikisha kuwa wanaitumia Tanganyika vema, wznz hawathubutu kuongelea suala la afya, elimu na elimu ya juu, utumishi au ulinzi na usalama. Hayo wanategemea Tanganyika ili waweze kuendesha mambo yao bila gharama.

Elimu ya juu: Hili halipo katika mambo 11 ya awali. Kama ilivyo gesi na mafuta nalo liliingizwa baadaye. Znz wameondoa gesi na mafuta kwa kisingizo cha kuingizwa kinyemela, lakini hawathibutubu kuondoa elimu ya juu kwasababu ni wafaidika.

Kwa mwaka 2012 Tanganyika (Tanzania) ilitoa nafasi za upendeleo kwa znz na pesa za kusomesha wanafunzi 1000 huku SMZ ikisomesha 800. Hakuna mwanafunzi wa Tanganyika aliyefaidika na mkopo au msaada wa aina yoyote kutoka SMZ.

Gharama za kuendesha bunge ni za JMT ambayo znz hina ushiriki mwingine zaidi ya jina. Mtanganyika ndiye anayelipa gharama zote za wabunge wa znz ambao huja kujadili mambo ya Tanganyika bila kuwa na Mtanganyika ndani ya BLW.

Katika mchakato wa katiba waznz wamekataa kulipa gharama kwa kisingizoio hilo ni suala la muungano 'Serikali ya Mapinduz ya zanzibar imesema kamwe haitachangia gharama za mchakato wa kuunda katiba mpya,imedai kuwa jukumu la kugharamia ni la Serikali ya Jamhuri ya Muungano
sosi:NIPASHE,25 N0VEMBER,2011''

Jeuri hiyo inatokana na mwendelezo wa kukiuka mambo mengi bila kuchukuliwa hatua.
Na ukitaka kuona jinsi ambavyo muungano huu una matatizo ni pale ambapo Znz ilipitisha mswada wa sheria ya usajili wa mzanzibar 7 ya 2005 inayomtambua raia kutoka bara kama rai wa kigeni na anyehitaji kitambulisho cha ugeni.

Kifungu 6(A) kinaeleza kila asiye mzanzibari (siyo Mtanzania) ajisajili wakiwemo Watanganyika. 6(A)(3) kimetaja aina ya Wageni ambao Mtanganyika ni mmoja wapo.
Sababu za kutunga sheria hiyo ni kuzuia watu kupata huduma za jamii wasizo stahili.

Tunajiuliza kama ni hivyo, iweje wazanzibar takriban 400,000 waishi Tanganyika bila kitambulisho?
Je huduma za jamii haziathiriki kwa kiwango hicho cha raia kutoka nchi ya Zanzibar?

Ubaguzi huu umeendele hadi katika ngazi za utumishi. Ni kituko kwa Mtanganyika kupata fursa ndani ya SMZ. Ipo sheria iliyopiga marufuku Watanganyika kufanya shughuli za mahakama au uwakili n.k. Kwa upande mwingine malaki ya wznz wapo Tanganyika wakipata fursa sawa kama Mtanganyika.

Ubaguzi wa aina hiyo umeendelea katika maeneo kama ardhi n.k. bila kuathiri wazanzibar wanaoishi Tanganyika na kubanana na Watanganyika katika fursa za Tanganyika kwa jina la Tanzania.

Wana duru, labda nitoe mifano rahisi muelewe vioja vilivyopo. Kwa kutumia katiba ya 2010 na jeuri Znz imeondoa baraza la mitihani ambalo lililiongezwa katika mambo 11 na kuunda baraza lake.

Kwamba, watatahini watoto wao kwa standard zao wenyewe. Wanapotaka kujiunga na elimu ya juu katika vyuo vya serikali Tanganyika, wznz wanakuja kwa jina la Watanzania.
1. Wanaomba nafasi za upendeleo kwasababu ni wznz
2. Wanapata mikopo wasiorudisha ambazo ni kodi za Mtanganyika kwasababu ni wznz.

Halafu, katika bodi ya NECTA wznz wapo. Sasa jiulize kama wana baraza lao kwasababu hawana imani na NECTA, ndani ya bodi ya NECTA wanafanya kitu gani.

Wapo ndani ya bodi ya mamlaka ya anga ambayo wameunda yao, bodi za mashirika kama bandari wakiwa na bodi zao n.k

Ndivyo ilivyo katika kamati za bunge, ambapo wznz wanakwenda kukagua maendeleo ya halmashauri za Tanganyika, lakini ni mwiko na dhambi kubwa Mtanganyika kushiriki shughuli za BLW. Hawa wznz wanafanya nini katika mambo ya Tanganyika.

Mheshimiwa Pinda anapsimama na kusema kero ni suala la ardhi, hakika haitendei haki nchi yake.
Yeye mwenyewe kutokuwa na uwezo kama waziri mkuu wa Tanzania kufanya kazi znz ni kero kwa kuanzia. Kuchagua suala moja na kuaminisha ni kero ni udanganyifu wa kiwango kizuri sana!

Mh Pinda, kama unatusoma elewa kuwa znz imevunja mambo ya mkataba wa muungano wa mwaka 1964 na kuacha yenye mafao kwao kwa gharama za Mtanzania. Imevunja katiba ya JMT kwa katiba ya znz ya 2010 inayoipa mamlaka makubwa dhidi ya JMT.

Hapo hakuna muungano kwa kuanzia achilia mbali kero za maana ambazo hukizitaja ili kupumbaza kundi ulilokuwa unaongea nalo.

Kwa ufupi, Tanzania ni Tanganyika hivyo suala lililopo mbele ni Tanganyika wala si utambulisho wa znz.

Nini mwonekano wa bunge la katiba?
Watanganyika wafanye nini?
Nini hoja zetu kuhusu serikali ya Tanganyika

Tutaendelea sehemu inayofuata.......
 
Wakuu Nguruvi3 Mchambuzi Mzee Mwanakijiji Pasco Mkandara na wengine wengi...

Kwa sasa wengine tumeelekeza akili zetu kwenye ibara ya kwanza ya rasimu ya katiba, muundo wa muungano..lakini kuna jambo lingine muhimu sana, may be muhimu zaidi hata kuliko suala la muundo wa muugano.

Sina hakika kama ni sheria ya usalama wa taifa ya mwaka 1970 ndiyo inatumika sasa, au sheria ya mwaka 1996.

Kuna lolote linaendelea kuhusu suala hili, kwa maoni yangu kama hakutakuwa na mabadiliko ya maana ya kipengele hiki matatizo yote makubwa yanayoikabili Tanzania na udhaifu wa systems zinazoshiriki kwenye uongozi na utawala wa Tanzania zitaendelea kuwa lame..
 
Last edited by a moderator:
Wakuu Nguruvi3 Mchambuzi Mzee Mwanakijiji Pasco Mkandara na wengine wengi...

Kwa sasa wengine tumeelekeza akili zetu kwenye ibara ya kwanza ya rasimu ya katiba, muundo wa muungano..lakini kuna jambo lingine muhimu sana, may be muhimu zaidi hata kuliko suala la muundo wa muugano.

Sina hakika kama ni sheria ya usalama wa taifa ya mwaka 1970 ndiyo inatumika sasa, au sheria ya mwaka 1996.

Kuna lolote linaendelea kuhusu suala hili, kwa maoni yangu kama hakutakuwa na mabadiliko ya maana ya kipengele hiki matatizo yote makubwa yanayoikabili Tanzania na udhaifu wa systems zinazoshiriki kwenye uongozi na utawala wa Tanzania zitaendelea kuwa lame..
Kwa muono wangu tatizo kubwa la Watanzania sio yapo ktk maandishi yaani msahafu wetu, bali watu wenyewe hawana imani na msahafu huo. Ni kama kina sisi tunaojiita waislaam wakati maisha yetu hayalingani na matakwa ya dini, au wakristu wanaoishi kinyume cha Biblia lakini ukiwauliza wapo tayari hata kwa vita kutetea imani zao. Dini ni way of life na usipofuata maandishi haijalishi hata ukijiita Muislaam au Mkristu na kuvaa vibaraghashia au msalaba wewe ni huna tofauti na Kafir (Pagan)

Binafsi yangu nimezisoma katiba zetu iwe za chama, ama ya Taifa na kujaribu kutazama mangapi kweli yanafuatwa na wale walokula kiapo kuifuata! Ni aibu tupu!..Kwa hiyo bado siamini kabisa kama kupatikana kwa Katiba mpya kutabadilisha ama kudhoofisha lolote zaidi ya udhoofu ulokuwepo ktk imani za watu wenyewe. Uzalendo hatuna kabisa na hauji kwa mmaandishi mapya!

Kuzaliwa kwa TISS ama chombo kingine chochote leo hii ni kwa maslahi ya watu iwe kundi ama wenye nguvu ya kiutawala. Usalama wa Taifa wakati wa mwalimu ulikuwa usalama kweli wa Taifa na acha mbali kutojulikana kwa watendaji wake, leo hii kila mtu anaona sifa kuitwa usalama wa Taifa kwa sababu usipojulikana huwezi kuvuta za mafisadi. TISS kiana ni Cartel vile vile inayotekeleza interest za watu maana kitaifa sisi hatuna Interest zetu nje zaidi ya humu ndani, na waliwao ni wananchi wenyewe.

Hivyo binafsi nina mashaka sana na uboreshaji wa kariba hasa hii mpya kutokana na kwamba zile sababu hasa zinazotakiwa ama zilizo sababisha kutakiwa katiba mpya zinapuuzwa na nyingi nyinginezo zenye kulindana ama kugawana umaskini ndizo zinawekewa mkazo zaidi kwa sababu katiba hii ni sawa na wafiwa wanaosubiri sinia la palau msibani, watu wameisha nawa wanasubiri tu lishuke mkekani wengine wamebeba ndizi mifukoni. sasa itokee pilau halikuja umeletwa ugali utasikia cha moto.. Hakuna maslahi ya Taifa.

Na masema hivi kwa sababu imenishangaza sana kuona wajumbe waloteuliwa kuongoza kongamano hili la baraza la katiba hakuna hata mtu mmoja alovaa pini ya bendera ama ngao yetu kuonyesha Uzalendo wao kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sasa ikiwa hawa watu wameshindwa kuitukuza nchi yao kwa kuvaa pini tu ktk makoti yao, mashati yao leo wanabishaa juu ya mavazi sijui mashati gani yavaliwe utadhani kuna red carpet basi ujue huko bungeni kuna Ubinafsi na kupendeza zaidi ya Utaifa!
 
Sina hakika kama ni sheria ya usalama wa taifa ya mwaka 1970 ndiyo inatumika sasa, au sheria ya mwaka 1996.

Sheria hizi ni sheria mbili tofauti; moja ni ya Usalama wa Taifa na hiyo ya pili ililunda tu taasisi ya Usalama wa Taifa; haikugusia kwa kiasi kikubwa yaliyomo kwenye sheria ya 1970 au kuibatilisha.
 
SEHEMU YA V

Tumalizie kuwa kusema yafutayo.

Tanganyika imekuwepo katika muungano wa sasa ikiwa imefichwa.
Tanganyika iliungana na Zanzibar kwa mkataba wa muungano wa nchi mbili.

Hakuna chama cha siasa kilichoshiriki. Wananchi hawakushirikishwa moja kwa moja.
Tanganyika ilitoweka utajwa wake kwa sheria ya 24 ya 1967.

Katiba ya muda ikawa miaka 10, ikazaa Tanzania bara na visiwani. Katiba ya znz 1979 ikaondoa visiwani na kubaki zanzibar, Tanganyika ikiitwa bara kama anavyoamini Pinda.

Katiba ya 2010 ikaiondoa znz mabaki katika muungano. Muungano haupo isipokuwa kwa wapotofu kama Pinda na Nape

Tanganyika na znz zina mahusiano ya karne yaisyohitaji siasa.
Wanasiasa ndicho chanzo cha matatizo yaliyopo. Wasomi na wanasiasa wanatumia elimu kulaghai umma bila kueleza faida za muungano. Tunaweza kubaki kama mataifa huru na wala kuoeleana halitakuwa tatizo kama anavyodai Pinda.

Muungano umebebwa na Tanganyika baada ya kuachwa njia panda na mshirika wake.
Tanganyika haina cha kupoteza muungano ukitoweka.

Znz itazame nafasi yake kichumi bila kusahau kivuli ilichojengewa ndani ya muungano itakapokuwa katika ushirika wa kikanda na kimataifa.

Jitithada za kuunusuru muungano siku za nyuma ilikuwa kusimamia katiba.
Muungano upo taabani kwa udhaifu wa viongozi kusimamia katiba za nchi na
kuwasikiliza wananchi, kudhani muungano utalindwa kwa silaha na mabomu.

Kibaya zaidi ni udhaifu wa viongozi kama Pinda na Nape kuzua, kupotosha na kulaghai umma wakidhani wananchi wa leo ni wale wa mwaka 1950.

Kwa miaka 50 CCM imeshindwa kupata ufumbuzi wa tatizo la muungano.
Imekuwa inatoa dawa za kutuliza maumivu kwa muda.

Hakuna mbinu ambayo CCM imebaki nayo kibondoni.
Tume 5 za watu maarufu na mshuhuri zimekuja na jibu lile lie kutoka kwa wananchi.

Lazima tuangalie tunaelekea wapi!
CCM kulazimisha kinyume na matakwa ya wananchi ni kujitafutia mauti.
Ingawa ipo taabani hili la muungano litaipeleka katika maktaba za historia kama ilivyo kwa UNIP na KANU.

Wananchi hawakusikilizwa na CCM kwa tume 5 na miaka zaidi ya 50.
Hii itakuwa fursa yao kutafuta mbadala.

CCM itaweza kulinda muungano kwa upanga, lakini haitachukua muda katiba mpya itaandikwa tena pale serikali mpya itakapoingia madarakani. Serikali hiyo itaingizwa kwa hasira za wananchi.

Njia iiliyobaki ya kunusuru muungano ni moja, serikali 3 kila mmoja ashughulike na mtatizo yake.
Yale tutakayokubalina tukubaliane kwa kuwajibika kuyahudumia kwa haki bila kubeba au kubebwa.

Ima hilo haliwezekani basi hatuwezi kuwa na muungano unaosimamiwa na askari.
Yale ya 2001 znz yatajirudia na safari hii kwa nguvu kubwa kutoka pande.

Jitihada za kuzuia malalamiko ya kuzindua Tanganyika zimeshindwa, kuanzia mwanzo wa muungano miaka ya 80 na kwa makundi mbali mbali.

Uhalifu wa kukiuka katiba, ubabe wa kujiamulia na ufidhuli wa kujivuna hauwezi kuvumilika tena.

Tanganyika ilikuwa nchi huru kabla ya znz. Kukasimu madaraka yake kwa BLW ni kuwasaliti wazalendo walioipigania nchi hii kwa damu, hali na mali.

Ni aibu na fedheha kwa taifa la watu milioni 40 kupangiwa mipango ya maendeleo na wawakilishi 50 wa BLW. Ni aibu watu kudai uwepo, muungano haupo tena.

Ni kuwadhalilisha walipa kodi wa Tanganyika pale kodi zao zinapohudumia chombo kinachotumiwa na nchi ya jirani. Kodi za Mtanganyika ndizo muungano! sasa basi inatosha

Tanganyika si taifa jipya, na wala kurejea kwakwe hakuwezi kuwekwa katika mizania ya yale ya Timor, Eritrea au South Sudan.

Tanganyika ilikuwepo kama nchi na taifa pamoja na serikali yake.
Kilichofichwa ni serikali ya Tanganyika, kilichopo ni nchi na taifa chini ya kivuli kingine.

Jaribio la kukataa matakwa ya Watanganyika kudai seerikali yao ni usaliti wa nchi.
Wote wanaoisaliti nchi hii wanapaswa kuonekana kwa macho ili historia iandikwe vema.

Hii ni nguvu ya umma inayoita, hakuna wa kuizuia nguvu ya wananchi na wala haijatokea duniani nguvu ya serikali kuizima ya wananchi.

Majaribio yote yalishindwa kwa wananchi kuwa kidedea.
Hilo ndilo bomu linalosubiri kulipuka siku si nyingi kama mchezo mchafu wa CCM unaoendelea.

Muungano umeshakufa, ipeni Tanganyika hadhi na haki yake isimamie watu na mali zake bila kuomba kibali kutoka taifa jingine.

Wabunge wa Tanganyika, nchi yenu inawaita, amkeni kwa pamoja, wekeni siasa pembeni simamie masilahi ya wananchi wenu.

Tumerithi matatizo ni aibu kuyapeleka kwa watoto wetu.
Sisi kama taifa tunahitaji muda wa kufikiri na kutafuta suluhu za matatizo ya Tanganyika wala si kufikiria namna tutakavyobemebeleza majirani zetu.

Hatuhitaji kibali kutoka BLW znz kujenga vyoo vya shule zetu.
Hatuhitaji kibali cha BLW znz kuwasaidia akina mama wanaozalia juu ya matenga.
Hauthitaji kibali cha BLW kukarababti hospitali zetu mbovu.

Ninyi wabunge kwa dhalili ni hii ya sisi kuwatuma nanyi kuomba kibali cha kutuhudimia kutoka Zanzibar hamuioni, jitokezeni mtueleze uhalali wa BLW kuitawala Tanganyika.

Tunapoteza muda wetu kulumbana na wzn, huu uwe wakati Tanganyika irudi na tulumbane kuhusu matatizo ya Tanganyika!

Tutaishi maisha haya ya mashaka hadi lini? Kwani sisi Tanganyika tunapoteza nini muungano huu ukifika tamati kama si serikali 3?


 
SEHEMU YA V

Tumalizie kuwa kusema yafutayo.

Tanganyika imekuwepo katika muungano wa sasa ikiwa imefichwa.
Tanganyika iliungana na Zanzibar kwa mkataba wa muungano wa nchi mbili.

Hakuna chama cha siasa kilichoshiriki. Wananchi hawakushirikishwa moja kwa moja.
Tanganyika ilitoweka utajwa wake kwa sheria ya 24 ya 1967.

Katiba ya muda ikawa miaka 10, ikazaa Tanzania bara na visiwani. Katiba ya znz 1979 ikaondoa visiwani na kubaki zanzibar, Tanganyika ikiitwa bara kama anavyoamini Pinda.

Katiba ya 2010 ikaiondoa znz mabaki katika muungano. Muungano haupo isipokuwa kwa wapotofu kama Pinda na Nape

Tanganyika na znz zina mahusiano ya karne yaisyohitaji siasa. Wanasiasa ndicho chanzo cha matatizo yaliyopo. Wasomi na wanasiasa wanatumia elimu kulaghai umma bila kueleza faida za muungano. Tunaweza kubaki kama mataifa huru na wala kuoeleana halitakuwa tatizo kama anavyodanya Pinda.

Muungano umebebwa na Tanganyika baada ya kuachwa njia panda na mshirika wake.
Tanganyika haina cha kupoteza muungano ukitoweka.

Znz itazame nafasi yake kichumi bila kusahau kivuli ilichojengewa ndani ya muungano itakapokuwa katika ushirika wa kikanda na kimataifa.

Jitithada za kuunusuru muungano siku za nyuma ilikuwa kusimamia katiba.
Muungano upo taabani kwa udhaifu wa viongozi kusimamia katiba za nchi.
Kwa udhaifu wa kuwasikiliza wananchi na kudhani muungano utalindwa kwa silaha na mabomu.

Kibaya zaidi ni udhaifu wa viongozi kama Pinda na Nape kuzua, kupotosha na kulaghai umma wakidhani wananchi wa leo ni wale wa mwaka 1950.

Kwa miaka 50 CCM imeshindwa kupata ufumbuzi wa tatizo la muungano.
Imekuwa unatoa dawa za kutuliza maumivu kwa muda.

Hakuna mbinu CCM imebaki nayo kibondoni. Tume 5 za watu maarufu na mshuhuri zimekuja na jibu lile lie kutoka kwa wananchi.

Lazima tuangalie tunaelekea wapi! CCM kulazimisha kinyume na matakwa ya wananchi ni kujitafutia mauti.
Ingawa ipo taabani hili la muungano litaipeleka katika maktaba za historia kama ilivyo kwa UNIP na KANU.

Wananchi hawakusikilizwa na CCM kwa tume 5 na miaka zaidi ya 50.Hii itakuwa fursa yao kutafuta mbadala.

CCM itaweza kulinda muungano kwa upanga, lakini haitachukua muda katiba mpya itaandikwa tena pale serikali mpya itakapoingia madarakani. Serikali hiyo itaingizwa kwa hasira za wananchi.

Njia ilizobaki za kunusuru muungano ni moja, serikali 3 kila mmoja ashughulike na mtatizo yake.
Yale tutakayokubalina tukubaliane kwa kuwajibika kuyahudumia kwa haki bila kubeba au kubebwa.

Ima hilo haliwezekani basi hatuwezi kuwa na muungano unaosimamiwa na askari.
Yale ya 2001 znz yatajirudia na safari hii kwa nguvu kubwa kutoka pande.

Jitihada za kuzuia malalamiko ya kuzindua Tanganyika zimeshindwa, kuanzia mwanzo wa muungano miaka ya 80 na kwa makundi mbali mbali.

Uhalifu wa kukiuka katiba, ubabe wa kujiamulia na ufidhuli wa kujivuna hauwezi kuvumilika tena.
Tanganyika ilikuwa nchi huru kabla ya znz.
Kukasimu madaraka yake kwa BLW ni kuwasaliti wazalendo walioipigania nchi hii kwa damu, hali na mali.

Ni aibu na fedheha na aibu kwa taifa la watu milioni 40 kupangiwa mipango ya maendeleo na wawakilishi 50 wa BLW. Ni aibu watu kudai uwepo wa muungano kwasababu ya pili haipo katika muungano tena.

Ni kuwadhalilisha walipa kodi wa Tanganyika pale kodi zao zinapohudumia chombo kinachotumiwa na nchi ya jirani.

Tanganyika si taifa jipya, na wala kurejea kwakwe hakuwezi kuwekwa katika mizani na yale ya Timor, Eritrea au South Sudan.

Tanganyika ilikuwepo kama nchi na taifa pamoja na serikali yake.
Kilichofichwa ni serikali ya Tanganyika, kilichopo ni nchi na taifa chini ya kivuli kingine.

Jaribio la kukataa matakwa ya Watanganyika kudai seerikali yao ni usaliti wa nchi.
Wote wanaoisaliti nchi hii wanapaswa kuonekana kwa macho ili historia iandikwe vema.

Hii ni nguvu ya umma inayoita, hakuna wa kuizuia nguvu ya wananchi na wala haijatokea dunia nguvu ya serikali kuizima ya wananchi.

Majaribio yote yalishindwa kwa wananchi kuwa kidedea.
Hilo ndilo bomu linalosubiri kulipuka siku si nyingi kama mchezo mchafu wa CCM unaendelea.

Muungano umeshakufa, ipeni Tanganyika hadhi na haki yake isimamie watu na mali zake bila kuomba kibali kutoka taifa jingine.

Wabunge wa Tanganyika, nchi yenu inawaita, amkeni kwa pamoja, wekeni siasa pembeni simamie masilahi ya wananchi wenu.

Tumerithi matatizo ni aibu kuyapelekeza kwa watoto wetu.
Sisi kama taifa tunahitaji muda wa kufikiri na kutafuta suluhu wala si kufikiria namna tutakavyobemebeleza majirani zetu.

Hatuhitaji kibali kutoka BLZ wzn kujenga vyoo vya shule zetu.
Hatuhitaji kibali cha BLW znz kuwasaidia akina mama wanaozalia juu ya matenga.
Hauthitaji kibali cha BLW kukarababti hospitali zetu mbovu.

Ninyi wabunge kama dhalili ni hii ya sisi kuwatuma nanyi kuomba kibali cha kutuhudimia kutoka Zanzibar hamuioni, jitokezeni mtueleze

Tunapoteza muda wetu kulumbana na wzn, huu uwe wakati Tanganyika inarudi na tulumbane kuhusu matatizo ya Tanganyika!

Tutaishi maisha haya ya mashaka hadi lini? Kwani sisi Tanganyika tunapoteza nini muungano huu ukifika tamati kama si serikali 3?


Wanajamvi sasa Tusemezane
 
Sheria hizi ni sheria mbili tofauti; moja ni ya Usalama wa Taifa na hiyo ya pili ililunda tu taasisi ya Usalama wa Taifa; haikugusia kwa kiasi kikubwa yaliyomo kwenye sheria ya 1970 au kuibatilisha.


Mkuu kwanini tuna sheria mbili zinazohusu kitu kimoja na zinashughulikia kitu kimoja. Kwa nini isiwe sheria moja? Lakini kimisngi hapa ni kuwa, kwa mazingira ya sasa inaonekana kuwa sheria hizo ndio ni tatizo kwa usalama na hata kwa maendeleo ya Tanzania. Kama hakutakuwa na mabadiliko ya maana kwenye sheria hizo, sidhani kama kutakuwa na lolote la maana kwenye katiba mpya.
 
SEHEMU YA V

Tumalizie kuwa kusema yafutayo.
Muungano umeshakufa, ipeni Tanganyika hadhi na haki yake isimamie watu na mali zake bila kuomba kibali kutoka taifa jingine.

Wabunge wa Tanganyika, nchi yenu inawaita, amkeni kwa pamoja, wekeni siasa pembeni simamie masilahi ya wananchi wenu.

Tumerithi matatizo ni aibu kuyapelekeza kwa watoto wetu.
Sisi kama taifa tunahitaji muda wa kufikiri na kutafuta suluhu wala si kufikiria namna tutakavyobemebeleza majirani zetu.

Hatuhitaji kibali kutoka BLZ wzn kujenga vyoo vya shule zetu.
Hatuhitaji kibali cha BLW znz kuwasaidia akina mama wanaozalia juu ya matenga.
Hauthitaji kibali cha BLW kukarababti hospitali zetu mbovu.

Ninyi wabunge kama dhalili ni hii ya sisi kuwatuma nanyi kuomba kibali cha kutuhudimia kutoka Zanzibar hamuioni, jitokezeni mtueleze

Tunapoteza muda wetu kulumbana na wzn, huu uwe wakati Tanganyika inarudi na tulumbane kuhusu matatizo ya Tanganyika!

Tutaishi maisha haya ya mashaka hadi lini? Kwani sisi Tanganyika tunapoteza nini muungano huu ukifika tamati kama si serikali 3?


Wanajamvi sasa Tusemezane


asante sana kwa mchango wako wa kusisimuwa (wabeja sana) wenye kisikia na wasikie
 
Nguruvi3 samahani kama niko nje ya mjadala wako ila naomba urejee hapa na unifafanulie maana ya nchi (country), taifa (nation) na serikali (government) kama ulivyodokeza mwanzo wa mjadala. Napenda zaidi kujifunza.
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3 samahani kama niko nje ya mjadala wako ila naomba urejee hapa na unifafanulie maana ya nchi (country), taifa (nation) na serikali (government) kama ulivyodokeza mwanzo wa mjadala. Napenda zaidi kujifunza.
sijui kama nitakuwa sahihi sana ama kama nimekuelewa sijui, nafikiri NCHI ni eneo lenye mipaka yake (country =is a region legally identified as a distinct entity in political geography)
na TAIFA ni watu wenye tamaduni, lugha na historia katika eneo husika, (NATION =a large body of people united by common descent, history, culture, or language inhabiting a particular state or territory )
na serikali ni muundo
 
sijui kama nitakuwa sahihi sana ama kama nimekuelewa sijui, nafikiri NCHI ni eneo lenye mipaka yake (country =is a region legally identified as a distinct entity in political geography)
na TAIFA ni watu wenye tamaduni, lugha na historia katika eneo husika, (NATION =a large body of people united by common descent, history, culture, or language inhabiting a particular state or territory )
na serikali ni muundo

Asante sana mkuu zumbemkuu, ni kweli ulielewa swali langu na nimeelewa ulichokieleza.
 
Last edited by a moderator:
Kwa ndugu zetu wazanzibar
Hakuna haja ya kuomba mamlaka kamili, tayari mnayo. Mnachopaswa kufanya ni kutekeleza mamlaka hayo. Mkataba wa 1964 una mambo kama ya anga, bandari na mambo ya nje (rejea bandiko # ) ambayo mumeweza kuyaondoa katika muungano.

Mumeweza kuiondoa katiba ya Jamhuri katika mambo ya muungano kwa kuwa juu yake. Mnatakiwa mtangaze wizara yenu ya mambo ya nje. Tayari mna wimbo wa taifa na bendera, kilichobaki ni kumpeleka balozi UN na kupandisha bendera.

Kwa upande wa Watanganyika, ni wakati mfikirie na si kujiuliza. Hivi kuna nini mnachopata kwa kutoa rasilimali, hali na mali katika muungano huu ambao basically haupo na hauongezi chochote zaidi ya kuwa chanzo cha migogoro.

Leo tungekuwa tunaongelea katiba itakayobadili mwelekeo wa Tanganyika. Kinyume chake tunajadili namna gani tutawashawishi wznz waweze kukubali miswada na sheria zinazotumika nchini kwetu.
Huu utumwa hadi lini, na kwa sababu zipi hasa znz inaweza kuwa juu ya Tanganyika.


Ninyi wabunge wa Tanganyika, heshima na hadhi yenu ya kututumikia Watanganyika ipo wapi kama haumuwezi kufanya maamuzi yanayotuhusu hadi Unguja na Pemba kupitia BLW wakubali. Huu ndio uhuru Nyerere na wenzake walioutafuta.
Ni kwanini mnaiweka Tanganyika rehani kwa vipande viwili. Ndicho mlichokusudia kuwaachia watoto na wajukuu zenu
 
Mkuu Nguruvi3, shukrani kwa kuja na mada muhimu na inayohitajika sana katika kipindi cha sasa. Umejadili vizuri sana maeneo yote muhimu na hitimisho lako deserves a salute. Kabla sijachangia hoja zako, ningependa kujadili kidogo hoja ya Skype juu ya tofauti baina ya state, nation and government. Nadhani kuna umuhimu mkubwa wa kueleweshana maana ya dhana hizi kisha tuweze ku-relate na hoja juu ya Tanganyika.

Tukianza na serikali:
Hii ni taasisi, na jukumu lake kubwa ni kutunga na kutekeleza sheria na sera mbalimbali ndani ya jamii husika. Taasisi hii ina nguvu na pia mamlaka ya kutawala eneo husika la kijiohrafia pamoja na wakazi wanaoishi katika eneo hilo. Mamlaka na nguvu hii ya serikali imegawanyika katika maeneo makuu matatu:

1. Bunge (lenye mamlaka ya kutunga sheria mbalimbali).
2. Executive - yenye mamlaka ya kushurutisha? (Enforce) utiifu wa sheria.
3. Judiciary - yenye mamlaka ya kufafanua au kuainisha sheria mbalimbali ili kuongoza shughuli za kila siku katika uendeshaji wa serikali - kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Hadi hapa nadhani tunaelewa hoja ya Nguruvi3 pale anapohoji baraza la wawakilishi la Tanzania bara litafanya kazi chini ya serikali ipi? Nitalijadili hiki kwa undani zaidi baadae, lakini kwa sasa tuendelee kuangalia kwa undani dhana hii ya serikali.

Kuna aina nyingi za serikali lakini zinazotambulika zaidi ni pamoja na hizi zifuatazo:

1. A monarchy (absolute monarchy)-huu ni utawala wa serikali hii unatokana na haki za kurithi- basically ni hereditary rights ambapo mfalme au malkia anakuwa na absolute power, hakuna katiba inayomzuia kufanya lolote.

2. Constitutional monarchy - hapa kunakuwepo na katiba ambayo inaanisha na kuamua madaraka ya malkia/mfalme ni yepi na mipaka ya madaraka husika.

3. Theocracy - utawala wa serikali ya aina hii hufuata imani fulani ya dinim

4. Oligarchy - utawala wa serikali ya aina hii unahodhiwa na watu wachache sana ndani ya jamii.

5. Dictatorship - utawala wa serikali ya aina hii haujali katiba, sheria na hauruhusu mawazo mbadala hasa upinzani.

6. Constitutional republic - hapa supreme power ipo mikononi mwa wananchi ambao huchagua viongozi wao wa kuwawakilisha katika ngazi mbalimbali.

7. Anarchism - utawala wa aina hii hautambui dhana ya "serikali".

Mpaka hapa nadhani tunaona jinsi gani mchakato wa katiba mpya ulivyokuwa muhimu, hasa ikizingatiwa kwamba serikali ya ccm haijawahi kupata mamlaka ya kutawala kutokana na katiba itokanayo na wananchi. Kwa maana nyingine, we became a constitutional republic in 1962 lakini in practice, legitimacy ya serikali ya Mwalimu Nyerere haikutokana na katiba bali vyanzo vingine nilivyojadili elsewhere - ujamaa/azimio la arusha, historia na TANU kutetea wanyonge ndani na nje ya nchi na charisma, integrity na patriotism ya Mwalimu nyerere. Chini ya mazingira haya, wananchi walikuwa na imani kubwa sana na serikali ya TANU/CCM na kutojali umuhimu wa katiba ya nchi. Kina Nape Nnauye na CCM ya leo wanadhani kwamba wanaweza cheza na suala la katiba na kuendelea kuwa na legitimacy kwa sababu tu ni CCM. Sources of legitimacy alizokuwa nazo mwalimu are long gone, na ccm ikicheza badala ya kutafuta legitimacy yake kupitia katiba itokanayo na wananchi, itaishia kwenye archives za kina KANU, UNIP na wengine kama alivyojadili Nguruvi3.

Sasa tuhamie kwenye dhana ya "state":

State basically ni a geographic entity ambayo ina mambo makuu na muhimu yafuatayo:

1. Its fiscal system.
2. Its own constitution.
3. Its own sovereignty (freedom from external control).

Je Zanzibar ya sasa na Tanzania Bara zinafanana na haya kwa kiasi gani? That's open to discussion lakini nguruvi3 amefafanua sana suala hili, na nikipata muda na mimi ntatupia maono yangu.

Tuendelee kuichambua dhana ya state:

Ili "state" husika iweze kujiunga na mfumo wa kimataifa kiuchumi, kisiasa, ni lazima itambulike na states nyenzake duniani kwamba its a sovereign state. Swali: Je, hii ina husiana vipi na Zanzibar ya leo na Tanzania bara? Nguruvi3 kajadili hili pia, na mimi baadae ntatupia maoni yangu.

Tuendelee:

A state ina sifa kuu zifuatazo:

1. Ina watu wa aina mbalimbali bila ya kujalisha idadi/wingi wao au utofauti wao kijinsia, kidini, kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni n.k.

2. Huwa na eneo lake la ardhi bila ya kujalisha ukubwa eneo husika ili mradi eneo hilo lina uwezo wa kukidhi "mahitaji ya makazi" kwa watu wake.

3. Huwa na uhuru wa kutekeleza sera na sheria mbalimbali bila ya kuingiliwa na mataifa ya nje.

4. Na mwisho - a state uendeshwa na a government/serikali.

MUHIMU:

*Serikali haiwezi kuwepo bila ya state kuwepo na state haiwezi kuendesha shughuli zake bila ya kuwepo kwa government.

*Ingawa jukumu kubwa la serikali ni kusimamia, kuratibu na kuongoza the state, the government inaweza kubadilika kila baada ya muda fulani kufuatana na utaratibu wa kidemokrasia ambapo umma anaoujadili Nguruvi3 unakuwa na maamuzi ya juu kabisa juu ya nani au chama gani cha siasa ndio kiunde serikali ili isimamie, iratibu na iongoze the state.

Kwahiyo tofauti na serikali ambayo inaweza kubadilishwa kwa mujibu wa matakwa ya umma, a state kwa kawaida huwa haibadiliki, bila ya kujalisha mabadiliko ya serikali yanayofanywa na UMMA. Kwa maana nyingine, serikali ya CCM, Chadema, CUF etc zinaweza kuja na kuondoka, na hata vyama hivi kufa lakini the state itabakia pale pale.

Swali linalofuata ni je, Tanganyika kabla ya muungano wa 1964 ilikuwa ni a state? Jibu ni ndio na hata mkataba wa muungano unaitambulisha hivyo, kama inavyofanya kwa zanzibar.

Swali lingine, je, Tanganyika kabla ya muungano wa 1964 ilikuwa na serikali? Jibu ni ndio, na nguruvi3 kajadili hili kwa kina.

Swali lingine: baada ya muungano, nini kilitokea to Tanganyika as a state and a government? Nguruvi3 kajadili hili, hasa juu ya sheria ya serikali ya mwaka 1967, sheria namba 24 iliyopitishwa na bunge la Tanganyika - bunge hili lilikaa kama bunge la Tanganyika kuifuta Tanganyika na kuzalisha jina la Tanzania Bara. Baadae na mimi ntatupia maoni yangu zaidi juu ya hili la kupotea kwa Tanganyika.

Swali linalofuatia, je waziri mkuu pinda ana hojipo akadai Tanganyika ipi, ile ya mkoloni iliyokaa kwa muda mrefu au ile ya uhuru? Kipi kimo katika Tanganyika ya miaka mitatu (1961-64), pinda ana hoja? Nguruvi3 kamjadili vizuri tayari. Lakini hapa niseme tu kwamba hata hiyo state anayozungumzia Pinda haijawahi kuwa consistent na malengo yake:

Mwaka 1961-1966 Tanzania was a party STATE ambayo lengo lake kuu lilikuwa to create and sustain new order. Kwa vile nyerere as a nationalistic leader of Tanganyika hakuwa na experience of exercising power, alihitaji to secure his position at the helm of the state.

Mwaka 1967-1985- baada ya kuona order has been created and secured to reasonable level, Tanzania ikahama from PARTY STATE politics na kwenda into DEVELOPMENTAL STATE. Hapa main objective ikahama toka order na kwende kwenye development. Nyerere alilazimika kutekeleza ahadi za TANU wakati wa harakati za uhuru, hivyo kulikuwa na haja ya kuonyesha kwamba serikali ilikuwa na nia ya kuondoa kila aina ya matabaka na pia kuletea wananchi maendeleo hasa kwenye suala zima la basic needs.

1986- hadi leo (2014), kipindi kimekuwa ni cha CONTRACTING STATE, ambapo supremacy ya politics katika kuendesha nchi imepunguzwa, lakini kwa bahati mbaya, punguzo hilo limeenda sambamba na ongezeko la wageni to control rasilimali za nchi na kugeuza Haki ya Mungu Kuwa Haki ya Mzungu.

Mh Pinda anasifia Tanzania as state which has never been consistent juu ya nini inataka kufanyia wananchi wake. Mgogoro wa kikatiba unaweka wazi jinsi gani Tanzaniaya Pinda is problematic state and it is in the brink of becoming a failed state.

Kwa kumalizia niseme tu kwamba "a state" hujitokeza in response to needs ambazo makundi mbalimbali ndani ya jamii huwa nayo. Mahitaji haya yanaweza kuja kutokana na matatizo ya security, welfare au kutatua conflicting demands on scarce resources. Chini ya serikali mbili, CCM imeshindwa kusimamia, kuatibu na kuongoza the state kwa maslahi ya wengi. Nitalijadili hili kwa undani zaidi nikiwa natoa maoni yangu kwa hoja za nguruvi3.



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom