Duru za siasa: Bunge la Katiba, upotoshaji na kiwewe cha kuzinduka Tanganyika

Duru za siasa: Bunge la Katiba, upotoshaji na kiwewe cha kuzinduka Tanganyika

Mkuu wangu nina swali moja tu.. Hivi mkeo akiitwa Mrs.Nguruvi3 atakuwa amepoteza Ubinadamu wake? Kuna tofauti ipi baina ya kuitwa Mrs. au laa!
Mkuu Mkandara, mkeo akiitwa Mrs au kubaki na binti ABC haina taabu bado atakuwa mkeo.

Tatizo ni pale mkeo atakaposhindwa kuheshimu makubaliano ya ndoa yawe rasmi au mliokubaliana wawili.

Mkeo anapoamua kuondoka na kitanda,majiko na kuchukua funguo za nyumba na kukutaka umpigie simu ili akuruhusu kuingia ndani ya nyumba yako huyo si mke ni mhuni.

Tena uhuni wake ni zaidi ya changudoa maana yeye anakutumia kwa jina la mume akikuumiza zaidi kuliko kukusaidia.

Huyu mke anayesubiri ujaze friji aseme ni vyakula vyetu wakati chenji yake akinunua lip stick za wadogo zake si mke ni gubeli.

Huyu mke anayesema mna account ya pamoja wakati umechangia 100 amechangia sh 0 si mke.
Mke anyekupiga busu wakati mnaenda benki na mkishagawana hiyo 100 anakurushia matusi si mke ni tatizo.

Huyu mke anayeishi nyumbani kwako wakati anadai ana vitenge vyake, nyimbo za taarabu na sasa anataka balozi wa nyumba kumi amtambue kuwa ni mwenye nyumba yako, si mke ni baradhuli
 
Last edited by a moderator:
Na masema hivi kwa sababu imenishangaza sana kuona wajumbe waloteuliwa kuongoza kongamano hili la baraza la katiba hakuna hata mtu mmoja alovaa pini ya bendera ama ngao yetu kuonyesha Uzalendo wao kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sasa ikiwa hawa watu wameshindwa kuitukuza nchi yao kwa kuvaa pini tu ktk makoti yao, mashati yao leo wanabishaa juu ya mavazi sijui mashati gani yavaliwe utadhani kuna red carpet basi ujue huko bungeni kuna Ubinafsi na kupendeza zaidi ya Utaifa!
Mkandara nikushukuru kwa maneno haya ambayo nitayaeleza kama ifuatavyo.

Mwenyekiti wa muda kificho ana waraka unaoitaka serikali 3, akiwa ndani ya CCM anataka serikali 2.
Hivi kificho atavaa pini ya nembo gani? Tanzania, united republic of Tanganyika and Zanzibar au Republic of Zanzibar?

Wajumbe kutoka Zanzibar haiwatambui JMT, na hilo si kosa lao kwasababu katiba ya znz ya mwaka 2010 inawapa haki.

Znz ni nchi na pale Dodoma wamekuja kwa ajili ya posho na masufuru, mioyo yao ipo kwa Zanzibar.
Ndio maana ya maneno znz kwanza.

Kuwalazimisha kuvaa nembo ya JMT ni kuwatukana, katiba ya nchi yao haisemi hivyo.
Wala hiyo JMT hawaitambui kabisa isipokuwa pesa za posho zinapogawanywa.

Wajumbe wa Tanzania wamechanganyikiwa, hawajui wavae nembo ya nchi gani. Je wavae nembo ya taifa jipya la Tanzania bara aliliovumbua Nape na Pinda, au wavae nembo ya JMT ambayo hawajui imeungana na nchi gani kwasababu wao ndio JMT peke yao.
Hawajui ni nembo ile ya adam na hawa ya Tanganyika au watengeneze nembo nyingine haraka haraka.

Wabunge wa Tanganyika wengine wanajiuliza, endapo bunge la JMT linajadili miswada na kuidhinishwa na BLW kwa kukubali au kukataa, wavae nembo ipi ? Ya SMZ yenye BLW linaloongoza Tanzania au JMT inayoongozwa na BLW.

Mimi nawashauri Wabunge wa Tanganyika wasichangayikiwe, warudi na kujiuliza siku ile Nyerere alipokabidhiwa nchi na Malikia walikuwa na nembo ya nchi gani.

 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mkandara, mkeo akiitwa Mrs au kubaki na binti ABC haina taabu bado atakuwa mkeo.

Tatizo ni pale mkeo atakaposhindwa kuheshimu makubaliano ya ndoa yawe rasmi au mliokubaliana wawili.

Mkeo anapoamua kuondoka na kitanda,majiko na kuchukua funguo za nyumba na kukutaka umpigie simu ili akuruhusu kuingia ndani ya nyumba yako huyo si mke ni mhuni.

Tena uhuni wake ni zaidi ya changudoa maana yeye anakutumia kwa jina la mume akikuumiza zaidi kuliko kukusaidia.

Huyu mke anayesubiri ujaze friji aseme ni vyakula vyetu wakati chenji yake akinunua lip stick za wadogo zake si mke ni gubeli.

Huyu mke anayesema mna account ya pamoja wakati umechangia 100 amechangia sh 0 si mke.
Mke anyekupiga busu wakati mnaenda benki na mkishagawana hiyo 100 anakurushia matusi si mke ni tatizo.

Huyu mke anayeishi nyumbani kwako wakati anadai ana vitenge vyake, nyimbo za taarabu na sasa anataka balozi wa nyumba kumi amtambue kuwa ni mwenye nyumba yako, si mke ni baradhuli
Ahahahah! sasa ulipenda um[paramie tu meo upendavyo? Mkuu sisi waswahili mkeo unamuomba kwa mapenzi ya zawadi na kadhalika, unaomba kaa unaomba kazi na akifarajia ndipo unaingia ila wewe hutakiwi kumkatalia kwa sababu umechoka na kazi.

katika Utamaduni wetu anunuacho mkeo hutakiwi kujua wala kuuliza na ni jukumu lake kuwatazama bado familia yake kupitia utajiri wako, maana yeye hana mirathi mule. Na wakati uu hai nyumba ni ya mkeo, wewe ni kiongozi wa familia. Mkeo ndio anayepanga hadi kijiko kikae wapi, anayetandika kitanda, anafagia ukumbi na kadhalika wewe kazi yako iko shambani kalime mkuu. Hizo dhahabu tunazovuna tumpambe pia mke!

Na siku tutakapo fahamu na kuzingatia ya kwamba huyu mke tumeshindwa kumpamba hadi wamekuja Wazungu sijui Wataliani na Waarabu tena kwa mlango wa nyuma kumhudumia tuliposhindwa, sasa kwa nini asidai taraka?...
Nachowaomba Watanganyika, haswa sis Wadanganyika wa bara na visiwani, Tujirudi wakuu zangu. Kama kweli ni sehemu ya Tanzania na tunathamini huu muungano wetu hiyo bajeti yetu ya maendeleo itazame pia upande wa mama hasa pale tunapotegemea zaidi mikopo na misaada toka nje.

Hizo fedha zifike pia kumhudumia mama na sii kuwaachia wataliani na Waarabu wajirushe wakati sisi tunashinda bar halafu wakilaani Ulevi tunawatukana japo nazielewa hasira zenu watoto wa Tanzania ambo huku nyumbani pia baba mwenye nyumba hana malezi mazuri kwa wanawe kutokana na kilevi chajke (ufisadi)Tuisikie kilio cha mama zanzibar kama mama na hata siku moja tusiitazame Zanzibar kama mtoto tulivyo sisi watoto wazawa wa Muungano huo. Kosa kubwa tunaklofanya ni pale mke (BLW)wakisema kero zao, sisi wototo ndio tunadakia ya kwamba mama naye kazidi mbona hata sisi baba hatujali wote. Tukumbuke sisi tuna Urithi ktk mali za baba wakati huyo mama yetu hana lolote!

Umenisoma lakini! haha haha haha!
 
Last edited by a moderator:
Mkandara nikushukuru kwa maneno haya ambayo nitayaeleza kama ifuatavyo.

Mwenyekiti wa muda kificho ana waraka unaoitaka serikali 3, akiwa ndani ya CCM anataka serikali 2.
Hivi kificho atavaa pini ya nembo gani? Tanzania, united republic of Tanganyika and Zanzibar au Republic of Zanzibar?

Wajumbe kutoka Zanzibar haiwatambui JMT, na hilo si kosa lao kwasababu katiba ya znz ya mwaka 2010 inawapa haki.

Znz ni nchi na pale Dodoma wamekuja kwa ajili ya posho na masufuru, mioyo yao ipo kwa Zanzibar.
Ndio maana ya maneno znz kwanza.

Kuwalazimisha kuvaa nembo ya JMT ni kuwatukana, katiba ya nchi yao haisemi hivyo.
Wala hiyo JMT hawaitambui kabisa isipokuwa pesa za posho zinapogawanywa.

Wajumbe wa Tanzania wamechanganyikiwa, hawajui wavae nembo ya nchi gani. Je wavae nembo ya taifa jipya la Tanzania bara aliliovumbua Nape na Pinda, au wavae nembo ya JMT ambayo hawajui imeungana na nchi gani kwasababu wao ndio JMT peke yao.
Hawajui ni nembo ile ya adam na hawa ya Tanganyika au watengeneze nembo nyingine haraka haraka.

Wabunge wa Tanganyika wengine wanajiuliza, endapo bunge la JMT linajadili miswada na kuidhinishwa na BLW kwa kukubali au kukataa, wavae nembo ipi ? Ya SMZ yenye BLW linaloongoza Tanzania au JMT inayoongozwa na BLW.

Mimi nawashauri Wabunge wa Tanganyika wasichangayikiwe, warudi na kujiuliza siku ile Nyerere alipokabidhiwa nchi na Malikia walikuwa na nembo ya nchi gani.

Mkuu katika hili zanzibar wanaitambua tanzania vizuri sana. wanaitambua ndoa hii na ndio maana wanaitaka taraka kisheria laa sivyo wangeingia msituni. Hiyo katiba yao ni ya mambo ya kike ambayo umetokana na mume kushindwa kutimiza majukumu ya mume.

Hizi kero zote za Zanzibar ni kutokana na kuwepo wataliani na waarabu wanaojenga nyumba ya mzee, wanaosaidia kupeleka gunia la mchele wakati bara inaendekeza pombe na ulevi. kama kweli zanzibar hawaitambui Tanzania wasingekuja kabisa Dodoma kwa sababu wengi wao ni wabunge tayari na wanavuta kila mwezi.

Kuwepo kikao cha bunge ama hakuna wanavuta mshahara kila mwezi tena kwa kiasi sawa na mbunge wa bara japo jimbo lake lina watu wasiojaa mkononi. Hizi posho za kukaa utazisikia sana kwa wabunge wa bara maana sasa hivi huko Dodoma kumejaa machangudoa na hela ya mshahara haitoshi kujirusha! matatizo haya tunayo sana sisi kuliko wao.
 
Last edited by a moderator:
sijui kama nitakuwa sahihi sana ama kama nimekuelewa sijui, nafikiri NCHI ni eneo lenye mipaka yake (country =is a region legally identified as a distinct entity in political geography)
na TAIFA ni watu wenye tamaduni, lugha na historia katika eneo husika, (NATION =a large body of people united by common descent, history, culture, or language inhabiting a particular state or territory )
na serikali ni muundo

Uko sahihi. Ukisema COUNTRY unaongelea a geographic location, wakati ukisem NATION watu. Kwa kifupi nati wanaishi ndani ya country.
Skype
 
Last edited by a moderator:
Kuna haja ya kuelewa jinsi gani Tanganyika ilitutoka ili tuweze kujua tutaizinduaje. Nitajaribu kujadili suala hili.

Ningependa nianze mchango wangu kwa hoja za Nguruvi3 kwa kugusia kidogo hili la Pinda na Tanganyika ingawa nguruvi3 ameliweka katika muktadha wake vizuri sana.

Pinda amekuwa waziri mkuu kwa miaka sita sasa na kwa mtazamo wangu he's the worst prime minister our country eve had. Katika miaka yake sita kama waziri mkuu, amefanya nini la maana, hasa katika kutatua kero za muungano au for that matter, kuuboresha? Mwalimu nyerere alikerwa sana na kitendo cha waziri mkuu wa wakati ule (John Malecela) kumshauri vibaya rais wa JMT Ali Mwinyi juu ya sakata la G55 na Tanganyika. Hakika mwalimu angekuwepo leo, angekerwa sana na waziri mkuu kushindwa kumshauri vizuri rais wa sasa juu ya udhibiti wa zanzibar kuvunja katiba ya JMT.

Suala la pili nalopenda kujadili ni kwamba: mkataba wa muungano (1964) ndio nguzo kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kinyume na mkataba wa muungano na pia kinyume na katiba ya muda ya 1965, katiba ya JMT (1977) ambayo inatumika hadi leo haitoi kauli ya wazi ya kuunda serikali ya Tanganyika na haimpo madaraka rais wa muungano au kiongozi mwingine yoyote kuendesha na kusimamia mambo ndani ya Tanganyika (tanzania bara?), mambo ambayo hayapo ndani ya muungano. Nape na CCM wanataka kuendeleza tatizo hili au kasoro hii, na pengine tuwaulize kwamba je, kwanini mkataba wa muungano ulitamka juu ya uundwaji wa serikali ya Tanganyika? Kwanini hilo liliendelea kutamkwa ndani ya katiba ya muda (1965)? Je hili lilikuwa ni kosa la bahati mbaya? Ni dhahiri hili lilifanywa kwa makusudi kuiondoa Tanganyika for good. Kama alivyojadili nguruvi3, leo hii, Rais wa JMT na Serikali ya JMT ndio vyombo vinavyohusika na uendeshaji wa serikali ya Tanganyika na hali hii imekuwepo tangia siku muungano ulipozaliwa 1964. Wakati vyombo hivi viwili vilipewa madaraka kamili na mkataba wa muungano (1964) na Katiba ya muda ya JMT (1965) ili kutekeleza jukumu hili la msingi kabisa, katiba ya JMT ya mwaka 1977 haikutamka juu ya madaraka hayo ya kusimamia na kuendesha Tanganyika. Kwa maana hii, hatua na maamuzi yote yaliyochukuliwa na marais wa JMT na hata leo (Kikwete) kuhusu mambo yasiyokuwa ya muungano (ya Tanganyika au tuite Tanzania bara), hayana nguvu za kisheria, wala za kikatiba. Hili ni tatizo kubwa sana kwani ndio vimefanya Tanzania ionekane ni Tanganyika na Tanganyika ni Tanzania machoni mwa wananchi wengi. Mbaya zaidi, hali hii inachangia sana watu wengi kuja na hoja kwamba hakuna haja ya kuwa ba serikali zaidi ya moja kwa nchi nzima ya tanzania.

Tukiangalia sakata la G55 kidogo - hoja binafsi juu ya Tanganyika ililenga kurekebisha kosa hili na kulikuwa na hoja ya msingi na ndio maana bunge na rais walipitisha hoja hii kwa maslahi ya muungano na taifa kwa ujumla. Lakini kinyume chake, uamuzi huu ukapingwa na hoja kuwa watered down kwa maelezo kwamba chama hakikuwa kimebadilisha sera yake ya mfumo wa serikali mbili. Swali linalofuatia ni je- CCM kilipata wapi wapi madaraka ya kuingilia mambo ya kikatiba wakati mkataba wa muungano haukutaja chama chochote cha siasa? CCM ya leo ya kina nape inapata wapi madaraka ya kuingilia mambo ya kikatiba ya nchi wakati huu wa mfumo wa vyama vingi vya siasa? Taifa letu litaelekea wapi iwapo vyama vya kisiasa vitakuwa vinaingilia suala la katiba bila ya nguvu ya kisheria na kikatiba? CCM inataka kulipeleka wapi taifa letu?


JINSI KATIBA YA JMT ILIVYOKIUKA MKATABA WA MUUNGANO NA JINSI CCM ILIVYOSHIRIKI KUIZIKA TANGANYIKA.

Katiba ya 1977 ibara ya (1)
Inasema kwamba Tanzania ni jamhuri huru iliyoungana. Ikumbukwe kwamba awali katika mkataba wa muungano na pia katiba ya muda ya 1965, Tanzania haikutajwa, badala yake - Jamhuri ya Muungano Tanganyika na Zanzibar.

Ibara ya (2) juu ya nchi shiriki inataja nchi hizo kuwa ni Tanzanoa Bara na Zanzibar, again kinyume na mkataba wa muungano, na katiba ya muda 1965.

Tume ya warioba imejaribu kuja na ufumbuzi juu ya kasoro hii kubwa, tena sio kwa kubuni bali kwa kurudi kwenye legal foundation of the union - mkataba wa muungano, lakini badala ya kupongezwa, inatukanwa, wakiwepo makada wa ccm.

MUHIMU:
Muswada wa Katiba ulipelekwa bungeni april 25 1977 na kupitishwa siku hiyo hiyo kuwa katiba ya JMT bila hata kushirikisha umma. Katiba hii ikakiuka mkataba wa muungano kwa kila namna, lakini muhimu kuliko yote, kutoweka uendeshaji wa serikali ya Tanganyika kwa mujibu wa katiba. Kasoro hii inaweza kuonekana ni ndogo sana kama anavyojadili Pinda lakini sio suala dogo kwani linaonyesha dhahiri uingiliaji wa chama CCM katika katiba wakati kimsingi CCM sio mshiriki wa asili wa Muungano. Ndani ya katiba ya 1977, CCM ikajipa mamlaka ya "kuunda na kuvunja katiba". Kwa hali hii, CCM inahalalishia vyama vingine vikiingia madarakani vije na katiba zinazokidhi mahitaji ya vyama husika vya siasa. Hii ni hatari kwa muungano na taifa kwa ujumla.

Nirudie swali tena, kwanini Katiba ya 1977 haikutaja utawala wa Tanganyika, moja ya nchi shiriki za muungano? Mkataba wa muungano uliweka wazi kwamba hadi hapo katiba mpya ya JMT itakapokuwa tayari na kupitishwa na bunge:

*Katiba ya Tanganyike itumike kwa ajili ya JMT lakini irekebishwe ili ieleze uwepo wa serikali ya zanzibar.
*vile vile chini ya mkataba wa muungano, ikakubalika kwamba katika kipindi hicho cha mpito, Jamhurri ya muungano iwe inasimamia Tanganyika. Kipindi cha mpito kilikuwa ni mwaka mmoja ambapo mkataba wa muungano uliagiza kwamba mchakato wa Katiba mpya ya JMT uanze. Ibara ya 4 ya mkataba wa muungano inasema hivi:

...na hilo bunge lililotajwa na rais litakuwa na mamlaka juu ya mambo hayo kwa ajili ya jamhuri ya muungano, hii ni ziada juu ya mamlaka kuhusiana na mambo yote yanayohusiana na Tanganyika

Mwaka 1965, katiba ya muda iliweka wazi juu ya kipindi cha mpito (mwaka mmoja, sio 12) kwa kusema:

12(1) Mamlaka yote ya serikali juu ya mambo ya muungano kuhusu na mengine yote ndani ya tanganyika yamewekwa chini ya rais

Pia ibara ya 49 ya katiba ya muda (1965) inasema:

Mamlaka ya kutunga sheria juu ya mambo yote yalio ya muungano na mambo mengine yote ndani na juu ya Tanganyika yanawekwa chini ya bunge.

Ilitarajiwa kwamba sheria za kudumu juu ya masuala yote yasiyo ya muungano zingefuata muda sio mrefu. Tanganyika kama moja ya nchi shiriki za muungano ilitakiwa kupewa haki zake kuhusu masuala yasio ya muungano kama ilivyopewa zanzibar. Baada ya nchi kukaa na katiba ya muda kwa miaka karibia 13 badala ya mwaka mmoja tu kama mkataba ulivyoelekeza kiwe ni kipindi cha mpiti, Katiba ya 1977 ikaja na mambo ya ajabu kabisa. Katiba hii iliacha kabisa kuiweka Tanganyika, kwa mfano, juu ya serikali inasema
Mamlaka ya serikali ya jamhuri ya muungano kuhusiana na jamhuri ya muungano na mambo yote ya muungano yanawekwa mikononi mwa rais

Fananisha maneno haya na yale ya hapo juu kwenye katiba ya 1965 na mkataba wa muungano 1964.

Na kwa upande wa znz, katiba ya JMT 1977 ikatamka:
Kutakuwa na serikali ya zanzibar inayojulikana kama serikali ya mapinduzi ya zanziba ambayo itakuwa na mamlaka katika zanzibar juu ya mambo yote yasiyo mambo ya muungano kwa mujibu wa masharti ya katiba hii

Wapi mamlaka ya Tanganyika katika suala hili? Ndio nape na ccm wanakuja na hoja kwamba serikali mbili zitatatua mgogoro baada ya kushindwa kwa miaka 50? Kwa dawa gani, baraza la wawakilishi la Tanzania bara litakalozaa mabunge matatu ndani ya serikali mbili? How pathetic!

Ibara ya (3) ya katiba ya 1977 ilileta confusion kubwa sana, hasa kipengele kilichosema:
Chama ndicho chenye madaraka ya mwisho katika mambo yote kwa mujibu wa katiba hii na katiba ya chama.

Pia inasema:
Shughuli zote za vyombo vya serikali ya muungano zitatekelezwa kwa mujibu wa matakwa ya chama.

Tunabaki kujiuliza, je, chama kiliingiaje katika suala la muungano?

Kama alivyojadili nguruvi3, Sio tu ccm, bali hata ASP na TANU havikuhusika katika kuleta muungano 1964. Uamuzi huu ulikuwa ni wa marais wawili kwa kutumia mamlaka yao kama wawakilishi wa wananchi. Isitoshe, nchi ilikuwa bado ndani ya mfumo wa vyama vingi (vilifutwa 1965). Mkataba wa muungano ulifanya kwa makusudi kabisa kutohusisha vyama vya siasa na huu unatakiwa ndio uwe msingi wa katiba yoyote tutakayotunga (JMT na Tanganyika). Mkataba wa muungano haukuja na dhana ya kushika hatamu, dhana ambayo ccm ambayo sio tu kwamba haikutajwa kwenye mkataba, pia haikuwepo kama chama cha siasa lakini baadae kikaja kujichukulia mamlaka yote ya muungano kama vile kilihusika kwa namna yoyote. Swali linalojirudia ni je, kama mkataba haukutaja vyama, viliingia vipi?

Itaendelea...



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Kuhusu Nchi, Taifa, na Serikali.

  1. Serikali ni taasisi inayosimamia mwenendo wa maisha ya watu katika eneo fulani. Inaweka sheria na kusimamia sheria hizo sifuatwe. Kuna miundo mingi ya serikali, yote ikiwa na mamlaka ya kutunga na kusimamia sheria. Serikali inaweza kuamua kuwatoza raia wake kodi ili iwe na mapato ya kujiendsha. Serikali moja huweza kufanya kazi zake chini ya serikali nyigine; mifano mizuri sana ni zile serikali za miji, serikali za viji na serikali za mitaa. Kwa marekani kuna serikali za counties, serikali za miji, serikali za majibo na hata serikali za reservations za wahindi wekundu. Serikali inaweza kubadilishwa wakati wowote kwa njia mbaliambali ikiwa ni pamoja na mapinduzi ya nguvu.
  2. Nchi ni kipande cha ardhi kinachokaliwa na watu wanaotawaliwa na serikali moja. Mipaka ya nchi hujulikana kwa nchi majirani ili kujua mwisho wa mamlaka ya serikali husika.
  3. Taifa ni watu, nchi, pamoja na serikali yao kwa pamoja wakiwa wanajitoafutisha na watu wa nchi nyingine. Ingawa serikali moja inaweza kufanya kazi chini ya serikali nyingine, serikali ya taifa moja haifanyi kazi chini ya serikali nyingine. Yenyewe ndiyo yenye uamauzi wa mwisho katika nchi husika.
 
Ukisema COUNTRY unaongelea a geographic location, wakati ukisem NATION watu. Kwa kifupi nati wanaishi ndani ya country.
Skype

Shukrani kwa nyongeza mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Muundo wa serikali mbili ulikuwa uko skewed sana kuilea Zanzibar baada ya mapinduzi isionekane kuwa Tanganyika ndiyo iliyoendesha mapinduzi yale lakini ulikuwa ni transitional ili baadaye tufikie kuwa ni nchi moja yenye serikali moja. Miaka ya sabini kabla ya vita ya Kagera tulikuwa tumekaribia sana lengo hilo, hasa baada ya TANU na ASP kuanza kwa kuungana; lakini baada ya vita mambo yakaharibika sana.

Kwa dunia ya leo hii, nadhani ni ndoto ya alinacha kudhani kuwa lengo hilo litafikiwa tena hasa kwa vile tuna umma mkubwa sana wa wanasiasa wanaofikiria madaraka kuliko well being ya nchi. Kwa hali hiyo muundo wa serikali tatu utabaki ndiyo njia pekee ya kuendesha nchi hii. Kukosekana kwa viongozi wenye ushawishi wa kuunganisha nguvu ni ombwe ambalo linafungua chumba kikubwa sana kuwepo kwa muundo wa serikali tatu ambazo ndiyo njia pekee iliyobaki. Ni ama serikali moja au serikali tatu; ile transtional structure ya serikali mbili imeshindwa kabisa hasa wakati huu tunapofikia miaka hamsini bado kukiwa na friction za kimadaraka baina ya pande mbili za muungano.

Effort yoyote ya kuendelea kutuacha kwenye transitional system ni matumizi mabaya ya raslimali zetu
 
Mkuu Kichuguu kwa upambanuzi wako hapo juu sasa nimepata maana halisi ya nchi, taifa na serikali.

Naomba mjadala uendelee ila kwa uelewa wangu mdogo ningependa Zanzibar na Tanganyika zipotezwe kabisa tubaki na nchi, taifa na serikali moja tu ya Tanzania. Hii itasaidia kupunguza mzigo wa gharama za uendeshaji wa serikali kwa wananchi ama sivyo basi kuwe na Tanganyika na Zanzibar kama nchi/mataifa huru kwa kuvunja na kuutupilia mbali mkataba wa muungano na kubaki na ushirikiano ktk baadhi tu ya mambo.
 
Last edited by a moderator:
Inaendelea toka #28

Katika bandiko #28 nilimalizia na swali kwamba je, kama mkataba wa muungano (1964) haukutaja vyama vya siasa, vyama, hasa TANU na baadae CCM viliingia vipi?

Kutajwa kwa vyama vya siasa kulianza ndani ya katiba ya muda ya 1965, na hatua hii ilitokea Tanganyika kwani Zanzibar haikushirikishwa katika maamuzi ya kuingiza vyama vya siasa katika suala la muungano. Kutoihusisha znz ilikuwa ni kinyume na katiba. Wapo walio ona kwamba kuingizwa kwa vyama vya siasa ilikuwa ni kwa lengo la muda mfupi tu hasa kipindi cha mpito na kwamba kosa hili lingerekebishwa, lakini muda sio mrefu wakabaini kwamba ilifanywa makusudi na kusudio lilikuwa ni la kudumu. Katiba ya muda ya JMT (1965) ikasema hivi (kinyume na mkataba wa muungano):

3 (1) Kutakuwa na chama kimoja cha siasa katika Tanzania.
(2) Mpaka hapo TANU itakapoungana na ASP na kuunda chama kimoja cha siasa, chama hicho kwa Tanganyika kitakuwa ni TANU na kwa zanzibar kitakuwa ni ASP.

(4) Katiba iliyoonyeshwa katika nyongeza ya kwanza ya katiba hii itakuwa katiba ya TANU na katiba inaweza kurekebishwa wakati wowote (na masharti yaliyomo ndani yake ba baada ya muungano wa TANU na ASP kwa mujibu wa masharti yaliyopo ndani ya katiba hiyo

Kama tunavyoona, Tanzania ilisemwa kama nchi yenye chama kimoja wakati ukweli ni kwamba kulikuwa na chama kingine cha ASP. Kwa miaka 13 ya kipindi cha katiba ya muda ya JMT (1965-77), basically, TANU ndio iliyokuwa inaendesha nchi kwa kujipa hatamu.

Kama tunavyoelewa, hatamu za chama huwa chama hakijipi chenyewe bali hatamu hizi huwa zipo kwenye nguvu za wananchi/umma. Kwa maana nyingine, hatamu hutokana na nguvu ya umma na sio nguvu za serikali, bila hivyo, TANU na ASP visingeweza kumtimua mkoloni kwani vyama hivi nguvu zake zilitokana na kukubalika sana ndani ya jamii husika. Lakini cha ajabu ni kwamba TANU ikasahau haya, miaka 13 baadae ikafanikisha ndoa na ASP bila ya ridhaa wa wanachama wa pande zote mbili na kuanza upishi wa Katiba ya JMT 1977. Chama kikateua makada wake na kuwaweka kwenye kamati, kamati ambayo basically ilichukua nafasi ya baraza la kutunga katiba na bunge likachukua nafasu ya baraza la kutunga katiba. Mkataba wa muungano ulielekeza marais wa pande mbili wateue tume ya katiba, haikusema TANU iteue tume hiyo. Tukumbuke kwamba masharti haya ya mkataba wa muungano juu ya uteuzi wa tume ya katiba na baraza la kutunga katiba yalikuja kuchakachuliwa na sheria ya baraza la kutunga katiba ya mwaka 1965. Kupitia sheria hii, TANU ilijinyakulia mamlaka ya wananchi kutoka bunge na BLW zanzibar na kuziweka chini ya mamlaka ya chama. Hali hii ilikuwa inajenga mazingira hatarishi kwa siku za usoni iwapo mfumo wa vyama vingi ungerudi kwani kila chama madarakani kingeiga tabia ya TANU/CCM na kuzaa mgogoro wa kikatiba usiokwisha. Tunayaona haya leo.

Ujanja uliotokea ni kwamba - wakati kwa upande mmoja Tanganyika ikawa imedai kusalimisha mamlaka yake ndani ya muungano kwa kuifuta serikali ya Tanganyika, kwa upande mwingine Tanganyika ilikuwa imejipanga kisiasa zaidi kupitia chama (TANU) badala ya serikali ili kuhodhi muungano.

Suala la muhimu hapa ni kwamba TANU iliingia katika muungano kinyemela na zanzibar na chama chake cha asp hakikushirikishwa katika maamuzi hayo. Kwa maana nyingine, katiba ya mida ya JMT 1965 ilichapishwa ikiwa na elements za katiba ya TANU. Na hili halikuishirikisha zanzibar kimaamuzi, mshirika mwingine wa muungano. Kitendo cha katiba ya chama cha siasa (TANU) kuwekwa ndani ya katiba ya nchi (kinyume na mkataba wa muungano) maana yake ni kwamba kuanzia tarehe ya katiba ya JMT 1965, kazi za tanu pamoja na katiba yake zikafanywa kuwa ni sehemu ya sheria za jamhuri ya muungano wa Tanzania. Kwahiyo kuiondoa serikali ya Tanganyika ikawa ni danganya toto tu kwani bado Tanganyika ilikuwa inahodhi muungano kupitia chama chake cha siasa (tanu).

Katiba ya muda ya jmt 1965 pia ikasema katika ibara ya 3(3)
Shughuli zote za kisiasa zaidi ya zile zilizo chini ya serikali ya muungano, vyombo vya serikali na vya kutunga sheria zanzibar au serikali za mitaa zilizoanzishwa kwa au chini ya sheria zilizopo, zitaendeshwa na kusimamiwa na serikali

Maswali muhimu hapa ni je:

*ilikuwa ni sahihi kwa bunge kupitisha sheria iliyokipa chama cha TANU nguvu kwa Tanzania nzima wakati zanzibar kulikuwa na ASP?
*je ilikuwa ni sahihi wa bunge kulifanya suala la TANU kuwa ni suala la muungano?
*je kwanini wananchi hawakushirikishwa katika maamuzi juu ya kuifanya TANU kuwa ndio chama pekee ndani ya muungano?

Tukirudi nyuma kwenye katiba ya katiba ambayo ilikubalika iwe ya mpito, hakuna sehemu ilisema juu ya chama kushika hatamu lakini cha ajabu, katiba ya TANU ikaja kuingizwa katika katiba ya nchi. Baada ya muungano wa tanu na asp na kuzaa ccm, katiba ya JMT 1977 ikasema kwamba ccm itakuwa ni chama pekee cha kisiasa katika jmt. Ibara ya 3 inasema:

a)chini ya masharti ya katiba yake yenyewe, ccm itakuwa na maamuzi ya mwisho juu ya mambo yote ya muungano na yasiyokuwa ya muungano.
b) shughuli zote za kisiasa zitafanywa chini ya maelekezo na udhibiti wa chama.
c) shughuli zote za mashirika ya serikali katika jamhuri ya muungano zitafanywa chini ya maelekezo ya chama.

Matokeo yake ni kwamba, baada ya TANU kuifuta serikali ya Tanganyika mwaka 1967, CCM kupitia katiba ya JMT 1977 ikaibatiza rasmi Tanganyika kuwa Tanzania Bara. Ibara ya 2(1) ya katiba ya jmt 1977 ikasema:
Eneo la jamhuri ya muungani ni eneo lote la Tanzanua bara na eneo lote la zanzibar pamoja na eneo la bahari

Ikaachwa ibara ya 94(1) kueleza kwamba Tanzania bara maana yake ni eneo lote la jamhuri ya muungano ambalo kabla lilikuwa ni eneo la jamhuri ya tanganyika.

Tumeona japo kidogo jinsi gani mkataba wa muungano ulivyokiukwa na ccm kwa ccm kujichukulia mamlaka ambayo hayakuwepo ndani ya mkataba wa muungano wa 1964. Baadae tutaona pia jinsi gani mkatana wa muungano ulidhamiria mfumo wa serikali tatu kabla ya TANU na baadae CCM kukiuka mkataba huo na kulazimisha sera ya serikali mbili. Kimsingi, mkataba wa muungano ulilenga serikali tatu au mamlaka ambao zinatajwa wazi kama tanganyika, zanzibar na muungano. CCM haikutajwa pahala popte kama mmoja wa mamlaka hizo hivyo kuingiza TANU/CCM kuwa mshiriki wa mkataba wa muungano ilikuwa ni kosa. Kwa maana hii:

1. CCM haina uwezo wowote wa kisheria (locus standi) wa kujiingiza kisheria na kulazimisha haki na wajibu wa muungano kwa upande wa zanzibar, Tanganyika au jamhuri ya muungano wa Tanzania.

2. CCM haikuwa sehemu ya mkataba wa muungano kwahiyo haiwezi kisheria kudai kupata manufaa yoyote chini ya mkataba wa 1964 kwa kuzinyonya, kuzilalia au kwa hasara ya Tanganyika na zanzibar ambazo ni sehemu ya mkataba wa muungano. Hata mahakama ya kimataifa itakubali kwamba huu ni ukiukwaji wa wazi wa mkataba wa kimataifa.

Itaendelea...



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Wakuu
Tunazidi kuona ambavyo muungano ulivyoundwa bila kushirikisha vyama vya siasa.
Ushirikishwaji wa wananchi haukuwa timilifu kwa kupitia wabunge wa mabunge.
Mabunge yalijigeuza na kuwa mabunge ya katiba.

Wazo la kuanza kwa mchakato uliopo halikutoka katika vyama vya siasa. Akina Nape na Pinda wameshtukizwa kama wananchi wengine. Bunge la wakati huu lililenga kuwa la wananchi. Bahati mbaya sana baada ya kuingia interest za kisiasa bunge limebeba uchama zaidi ya Uananchi.

Hao wabunge wananowakilisha wananchi badala ya kuangalia nchi wanasikiliza vyama.
Vyama vinapita nchi ipo kila siku.
 
Muundo wa serikali mbili ulikuwa uko skewed sana kuilea Zanzibar baada ya mapinduzi isionekane kuwa Tanganyika ndiyo iliyoendesha mapinduzi yale lakini ulikuwa ni transitional ili baadaye tufikie kuwa ni nchi moja yenye serikali moja. Miaka ya sabini kabla ya vita ya Kagera tulikuwa tumekaribia sana lengo hilo, hasa baada ya TANU na ASP kuanza kwa kuungana; lakini baada ya vita mambo yakaharibika sana.

Kwa dunia ya leo hii, nadhani ni ndoto ya alinacha kudhani kuwa lengo hilo litafikiwa tena hasa kwa vile tuna umma mkubwa sana wa wanasiasa wanaofikiria madaraka kuliko well being ya nchi. Kwa hali hiyo muundo wa serikali tatu utabaki ndiyo njia pekee ya kuendesha nchi hii. Kukosekana kwa viongozi wenye ushawishi wa kuunganisha nguvu ni ombwe ambalo linafungua chumba kikubwa sana kuwepo kwa muundo wa serikali tatu ambazo ndiyo njia pekee iliyobaki. Ni ama serikali moja au serikali tatu; ile transtional structure ya serikali mbili imeshindwa kabisa hasa wakati huu tunapofikia miaka hamsini bado kukiwa na friction za kimadaraka baina ya pande mbili za muungano.

Effort yoyote ya kuendelea kutuacha kwenye transitional system ni matumizi mabaya ya raslimali zetu
Transition kwenda serikali moja imeshindikana kwasababu, kwanza ulafi wa viongozi kimadaraka.Inashangaza CCM wameacha kuongelea masilahi ya wakulima, wafanya, akina mama na watoto wamekwenda kujifungia kuandika kurasa 22 za kuboresha kile walichoshindwa kwa miaka 20 iliyopita.
Nani anajua tume ya kuondoa kero aliyounda JK imetoa matokeo gani.

Pili, hakuna viongozi wa kuongoza. Tuna kundi la viongozi wababishaji, waongo, wazushi na wahuni.
Hivi kiongozi anayesema faida za muungano ni kuoleana huyo anaelewa maana ya muungano kweli.
Kiongozi kama Nape ameshindwa kueleza hata mara moja kwa mantiki kwanini anataka serikali 2.
Na wala hajaweza kutoa majibu hizo kero zitashughulikiwa vipi.

Kiongozi mkuu kama Pinda anasema malalamiko ya Tanganyika ni kupewa ardhi znz.
Anajaribu kubadilisha mada na kuacha concern halisi za Watanganyika ikiwemo kukiukwa kwa katiba, znz kuendesha mambo bila kuulizwa huku ikitaka bila kuuliza.

Unapokuwa na kundi la viongozi kama hawa ambao hawawezi kukabiliana na hoja kwa uaminifu na udhati muungano ni ndoto.

Tatu, kuna asili ya majivuno yasiyo na msingi. wznz wanadhani kuwa ni taifa lenye utofauti na mataifa mengine.
Muungano na Tanganyika katika mambo ya kiuchumi na kijamii kwao si priority, muhimu ni kuwa na logo, nembo na utambulisho walioahidiwa na Pinda.

Nne, kukosa maono na kuwa nyuma ya wakati. Pinda anapotengeneza taifa la Tanzania bara na kufuta Tanganyika ambayo yeye ni waziri mkuu wake ni kukosa maono na kuwa nyuma ya wakati.

Pinda anafahamu kuwa yeye ni waziri mkuu wa Tanganyika, lakini kwa makusudi anajitoa ufahamu na kudhani anaweza kuongea na sheha wa znz.

Nape anadhani muungano unajengwa kwa uzushi, uongo na bla bla, amesahau kuwa kizazi kilichopo kina watu wenye uewezo wa kufikiri, kuona na kutambua kuliko yeye katika mizania yoyote.

Tano, Ombwe la uongozi.
Uongozi wa taifa haujui nini wananchi wanataka, haupewi habari za nini kinaendelea mitaani.
Uongozi unadhani mabomu na risasi ni njia muhimu sana na bora katika kuimarisha muungano.
Uongozi hautambui nini tofauti ya nchi, wananchi, vyama na wanchama.

Tukifika hapo ni wazi hakuna nahodha au mabahari wa kuliongoza jahazi kuelekea lilipokusudia.

Kuna njia mbili tu zilizobaki
1. Kuliacha jahazi lizame, au kulipeka ufukweni ili tupasue na kugawana mbao
2. Kutia nanga yenye pembe tatu (serikali 3) ili kuangalia kama mawimbi yatatulia na safari kuendelea.

Kujidanganya kuwa jahazi linaweza kuendelea kama lilivyo huku maji yakiingia na mabahari wahuni wakituaminisha wanachota maji na kuziba nyufa tukijua km 50 zilizopita hawakuwa na dawa ya kuzuia maji au kuziba ni kulitakia jahazi safari njema chini ya bahari. Kitakachofuata ni jahazi kuzama na injini kubwa ya CCM huko baharini.
 
Na siku tutakapo fahamu na kuzingatia ya kwamba huyu mke tumeshindwa kumpamba hadi wamekuja Wazungu sijui Wataliani na Waarabu tena kwa mlango wa nyuma kumhudumia tuliposhindwa, sasa kwa nini asidai taraka?...
Nachowaomba Watanganyika, haswa sis Wadanganyika wa bara na visiwani, Tujirudi wakuu zangu. Kama kweli ni sehemu ya Tanzania na tunathamini huu muungano wetu hiyo bajeti yetu ya maendeleo itazame pia upande wa mama hasa pale tunapotegemea zaidi mikopo na misaada toka nje
Mkuu Mkandara, talaka ipo kwa kadhi, kadhi kaingia mjini wanao omba hawaonekani.
Huko kwa kasisi wanadai huu ni mwili mmoja ingawa hawaamini wakiondoka hapo.
Huyo mwanamke mwenye funguo za nyumba anaomba afunguliwe mlango gani tena ili atoke?

Mkuu unasema Znz ni sehemu ya Tanzania basi iangaliwe katika fedha za maendeleo kama mikopo na misaada. Hoja yako imetumiwa vizuri sana na wanasiasa kupotosha umma na ni chanzo cha tunayoshuhudia.

Kule kwa Malikia wanasema 'blessing in disguise' kwa Tanganyika.

Kwa muda mrefu znz imejenga hoja ya kuonewa katika misaada. Hakuna ukweli katika hilo.
Tanganyika imelipa zaidi kuliko hiyo misaada inayosemwa. Tunasababu za kusema hivyo.

1. Kama misaada ingekuwa dawa kwa nchi ndogo, Burundi na Rwanda zisingetaka kuwa sehemu ya jumuiya ya Afrika mashariki. Kuna faida gani iliziona zaidi ya kudhani misaada ndio chimbuko la maendeleo yao?

2. Wznz wanaoishi Tanganyika ni nusu ya waliobaki Zanzibar. Hii imeongeza social strains katika huduma za jamii kama afya,ajira na elimu. Gharama hizo anazibeba Mtanganyika siyo SMZ.

3. Katika mambo 22 yaliyoongezwa na kupunguzwa hadi 7 na tume hakuna hata moja lililoiathiri au kumuathiri Mtanganyika. Mambo 15 yalikuwa kwa gharama za Mtanganyika kwa jina la Tanzania yakimfaidisha mzanzibar.

4. Special treatment
Wazanzibar wanapata huduma maalumu kwa sababu tu ni wazanzibar ndani ya Tanganyika
i) Kuna ajira maalumu kwa ajili ya wznz ambazo haziwekwi katika monetary value
ii) Kuna nafasi maalum kwa wanafunzi wa znz kwasababu tu ni wzn(hazina monetary value)
iii) Kuna mikopo isiyorudishwa inayotolewa kwa wznz kama wanafunzi (haina monetary value)
n.k. n.k. Hayo yote Mtanganyika aishie znz hapati kwakuwa hana kitambulisho cha ukaazi na huchuliwa kama raia wa kigeni. Hivi kama hupewi leseni ya udereva utapewa huduma gani znz?

5. Gharama za kuendesha muungano huu wa JMT ni gharama ya Mtanganyika
i) Gharama za watumishi na uendeshaji wa wizara anabeba mtanganyika
a) SMZ haina bajeti ya ulinzi na usalama ambayo peke yake tukigawana kwa ratio ya 1:8 bado ni mzito kwa znz. Mwenyekiti wa BLW kamati ya fedha kathibitisha hayo.

b) Gharama za wizara ya mambo ya ndani ni mzigo wa Mtanganyika, mznz hana wizara kama hiyo
c)Gharama za mashirika ya kimataifa ambayo znz imejitoa katika muungano inalipwa na Tanganyika
-ZMO ni shirika la SMZ likisajili meli kwa manufaa ya znz. Gharama za ZMO kule IMO zinalipwa na Mtanganyika kwa jina la Tanzania

a) Zanzibar ina civil aviation yake. Gharama za chombo hicho kimataifa zinalipwa na Mtanganyika
c)Gharama za taasisi, mashirika na hata balozi ni za Mtanganyika. Mchango wa znz ni kupata ajira

5. Bajeti ya 2012/13 JMT ambayo Zanzibar haitambui imeipa znz bilioni 32. Kiasi hicho ni kikubwa ukilinganisha na fedha za maendeleo zilizotolewa kwa mkoa wa Singida, Kigoma na Lindi kwa pamoja.
Kwa maneno mengine walipa kodi wa Tanganyika wanachangia maendeleo ya znz kuliko ya maeneo yao.

6.Fursa za kiuchumi kama soko la ajira na bidhaa kwa watu milioni 40 wa Tanganyika lipo wazi kwa wazanzibar. Fursa hizo haziwekwi katika monetary value ili kutoa picha kamili kwasababu kufanya hivyo kutaondoa hoja hafifu ya misaada.

7. Ikumbukwe znz inapata mgao wa asilimia 4 ya pato la taifa. Mchango wa znz ni chini ya asilimia 1.

Ukiweka katika mizani znz inanufaika zaidi kuliko misaada inayotolewa. Tataizo kubwa la upotoshaji ni kuangalia dollar bila kujali huduma na mambo yasiyoweza kuwekwa katika tahamani ya pesa.

Hayo yanatokea huku Mtanganyika akiwa mgeni katika JMT ambayo znz ni mshiriki pale inapomhitaji Mtanganyika tu,kinyume chake Mtanganyika ni mgeni kama raia wa Nigeria, Vietnam n.k.

Hili ni jambo jema kwa Watanganyika, linatoa picha ya huu muungano wanaolalamikiwa kuuhodhi.
Ni kukosa maadili ya kiroho Mtanganyika wa kidatu anapolazmika kulipa umeme zaidi ili kufidia gharama za mzanzibar asiyelipa kwasababu ni mzanzibar!

Ni kukosa maadili mzazi wa Tanganyika anapominywa pay cheque yake kwa kodi ili itumike kutoa elimu ya bure kwa mwanafunzi wa kizanzibar huku mwanafunzi wa Kitanganyika ima akinyimwa kabisa au arudishe

Ni kukosa maadili mznz anapokuwa katika bodi ya NECTA, bandari, anga, halmashauri, miji au wizara na kumnyima Mtanganyika fursa ndani ya nchi yake kuihudumia nchi yake

Ni kukosa maadili Mtanganyika atakapolipa fedha za mbunge kutoka znz akiwa Dodoma kujadili mambo ya Tanganyika yasiyomhusu kwa mujibu wa katiba ya znz ya mwaka 2010

Labda tujiulize, hivi kuna sababu gani kwa mbunge wa znz kuwa mjumbe wa kamati ya bunge la JMT ambalo katiba ya znz hailitambui. Mbunge wa znz anapkagua shughuli za maendeleo Ngara ni ili achangie nini ikiwa nchi yake haitambui uwepo wa JMT.

Ni kwa msingi huu tunasisitiza kuwa sasa muungano uwe wa kichumi zaidi ukilenga kuleta mafao kwa pande mbili bila kubeba au kubebwa. Usawa huo ambao ni muhimu na lazima hauwezi kupatikana ikiwaipo nchi kati ya mbili haionekani.

Leo nani ataongelea madhila haya kule Dodoma? Tanganyika inawakilishwa na nani?
Tanzania bara ya Pinda haiwezi kusimamia Tanganyika kwa kishikizo cha jina ZNI.

Inahitajika serikali ya Tanganyika, kwa watu wa Tanganyika na kwa mnufaa ya Tanganyika.
Mazingaombwe ya kuviziana kwa herufi za majina na kuwekeza kwa herufi sasa yafike mwisho.

Watanganyika tumeliona hili, akina Nape hawawezi kuzuia tena kimbunga.
Wanaweza kuahirisha kwa miaka 2 lakini hawatazuia.

Hatuwezi kutumia muda wetu kufikiri namna ya kuishi na wznz badala ya kufikiri umasikini na adha nyingine. Wznz wameukana muungano kwa ushahidi wa katiba ya 2010, ninyi wabunge wa Tanganyika Dodoma hamuoni hilo?Mkuu Mkandara, misaada ipi zaidi ya hiyo inayotolewa?
 
1. CCM haina uwezo wowote wa kisheria (locus standi) wa kujiingiza kisheria na kulazimisha haki na wajibu wa muungano kwa upande wa zanzibar, Tanganyika au jamhuri ya muungano wa Tanzania.

2. CCM haikuwa sehemu ya mkataba wa muungano kwahiyo haiwezi kisheria kudai kupata manufaa yoyote chini ya mkataba wa 1964 kwa kuzinyonya, kuzilalia au kwa hasara ya Tanganyika na zanzibar ambazo ni sehemu ya mkataba wa muungano. Hata mahakama ya kimataifa itakubali kwamba huu ni ukiukwaji wa wazi wa mkataba wa kimataifa.
Na katiba ni mali ya kila mwananchi. Katiba ya nchi si mali ya Chama.
CCM haikuwepo wakati wa muungano, wala wazazi wake TANU na ASP hawakushirikishwa.

Hata mchakato uliopo CCM haina ufahamu nao. Mchakato haukupitia ngazi yoyote ya chama na wala hakukuwa na uhalali kwa mali ya wananchi kuhodhiwa na kundi la watu katika vyama

Nape na Pinda kwa miaka 8 hawana cha kutuonyesha kuhusu suluhu ya kero za muungano.
Leo wanakuja na hadithi za kufikirika wakitegemea Tanzania ya Nnauye ndiyo ya leo.

Ndio mna vyombo vya dola na mnaweza kuvitumia kuhujumu jambo lolote.
Ninachowakumbusha ni kuwa historia haiandikwi inanukuliwa baada ya kujiandika.
Ipo siku mtashindwa kusimama mitaani kwasababu historia itawatenga, matakuwa on the wrong side of the history.

Labda mtueleze, ni wapi na lini duniani nguvu ya umma iliwahi kushindwa na dola?


 
Nadhani kuna haja ya kujadili mapendekezo ya ccm ambayo lengo lake ni kuboresha mfumo wa serikali mbili, mapendekezo haya yatajadiliwa na wajumbe wa ccm kwa lengo la kuamminisha umma kwamba mfumo wa serikali mbili ndio unaofaa.

Tuanze na suala alilojadili Nguruvi3 hapo juu - gharama za kuendesha muungano. CCM imependekeza kufunguliwa kwa akaunti ya fedha ya pamoja ambazo zitatokana na mapato ya vyanzo vya muungano na kwamba kuwekwe utaratibu wa kisheria ambao utatekeleza uendeshaji wa akaunti hiyo na kuweka mgawanyo wa mapato kwa pande mbili za muungano. Kwanza kwa sentensi hii tu, maana yake ni kwamba ccm imekubali serikali tatu kwani inataja muungano na inataja pande mbili za muungano. Swali linalofuata ni je kuna uwezekano wa kuwepo kwa pande mbili za muungano bila kuwepo kwa serikali ya Tanganyika? jibu ni hapana, vinginevyo ni muendelezo wa mazingaombwe ya chama.

Nikirudi kwenye pendekezo hili la ccm, suala la "kufunguliwa kwa akaunti ya pamoja ya fedha zitokanazo na mapato ya vyanzo vya muungano" ni suala ambalo halitekelezeki chini ya mfumo wa serikali mbili. Isitoshe akaunti hiyo imekuwepo kwa miaka ishirini sasa lakini malalamiko juu ya mgawanyiko wa mapato ya fedha hayajaisha. Swali la kumuuliza Nape Nnauye na Ccm ni je:
*Hayo mapato ya muungano yapo wapi chini ya serikali mbili wakati chombo cha kusimammia mapato tajwa kwa nchi inayoitwa Tanzania bara, chombo hicho hakipo? kutakuwa na ZRA, TRA na chombo gani?

Ni vigumu kuelewa kwanini kina nape na ccm wanafanya watanzania ni wajinga. Lakini pengine wanadhania kwamba legitimacy ya serikali ya ccm bado chanzo chake ni masuala nje ya katiba kama nilivyojadili elsewhere kwani mapendekezo kama haya yatatekelezeka iwapo tu umma wa watanzania utakiamini ccm na kukipa uhalali wa kuendelea kuongoza nchi bila ya kujalisha constitutionalism.

Pengine kina nape hawaelewi (pengine) kwamba chini ya mfumo wa serikali mbili hakuna kitu kinachoitwa mapato ya nchi mbili kwani kuna mmapato ya zanzibar na mapato ya muungano. Kwa hili tu, tunaona jinsi gani kwa hoja za nguruvi3 hapo juu, pengine ni kwa miaka miwili tu kina nape na ccm watafanikisha malengo yao haya ya ajabu ajabu kwani muda sio mrefu "raia" wa "Tanzania Bara" watawazuia "raia wa Zanzibar" wasitumie kisichowahusu. Kwa upande wa zanzibar, wao wataendelea na malalamiko yao kwamba wanadhulumiwa mapato yao, kisa? Kukosekana kwa chombo cha kusimamia mapato ya "Tanzania bara".

Lakini nadhani ccm wanaelewa kabisa kwamba kuunda chombo cha kusimamia mapato ya Tanzania bara haiwezekani kwa sababu kufanya hivyo kutahitaji uundwaji wa serikali ya Tanzania bara (Tanganyika).

Kuna hoja nyingine ya ccm inayojadiliwa sana na makada wake na inatarajiwa kubeba wingu kubwa la mjadala BLK litakapofikia kwenye article ya mfumo wa muungano, na suala hili ni kwamba - serikali tatu ni gharama kwa mlipa kodi. Huko nyuma tulijadili kwa kina kwanini mfumo wa shirikisho una gharama ndogo, na pia huu, nguruvi3 amefafanua kwanini mapendekezo ya rasimu ya katiba yatamwondolea mtanganyika gharama asizostahili.

Hoja ya makada wa ccm wanaodandia uwongo na upotoshaji wa gharama ni kwamba - gharama za kuendesha serikali tatu zitakuwa kubwa sana kutokana na nchi kuwa na marais watatu - rais wa zanzibar, tanganyika na muungano. Swali kwa nape na ccm ni je:

*Nani kasema kutakuwa na marais watatu? Kwanini hili linajengewa hoja wakati hata katiba mpya bado haijaandikwa? Je, ccm imeshaamua aina ya uongozi utakaukuwepo chini ya serikali tat iwapo itatokea hivyo? Ili to prove nini, failure ya serikali tatu na kurudi kwa wananchi na kuwaambia "tuliwaambia ni gharama"?

Wapo makada wa ccm wanaojenga hoja pia kwamba tutakuwa kituko kwa dunia kwa kuwa nchi moja yenye marais watatu. Hii hoja haina mashiko kwani mfumo wa serikali mbili tayari umewachekesha wenzetu wa nje kwa miaka mingi, lakini hili la katiba ya JMT kuvunjwa na zanzibar 2010 ndio limewamaliza kabisa mbavu.

Fine, tuseme basi kiongozi wa Tanganyika ataitwa Rais, ni cha ajabu hapo? Kwa miaka 50 nchi yetu imekuwa na marais wawili, sasa ajabu ya marais watatu itakuwa ni ipi, tena bila ya kiini macho bali mfumo wa shirikisho? Kama alivyojadili nguruvi3, rais wa zanzibar kwa miaka mingi ameleta tu usanii ndani ya muungano, na kuanzia 2010 baada ya katiba mpya rais wa zanzibar ataleta balaa ndani ya muungano wa serikali mbili, kwanini ccm haisemi rais wa tatu ataleta balaa lipi? Kama mmoja wa washirika wa muungano, zanzibar kwa sasa ina rais, na makamo wawili wa rais, na kama mshirika mwingine wa muungano (Tanzania bara) ipo chini ya Rais wa muungano ambae yeye pia ana makamu wake na pia yupo waziri mkuu, jamani, mbali ya gharama kubwa, hatuoni kwamba tunafanya michezo ya kitoto?

MUHIMU
CCM imekuwa ni chama cha ajabu sana, na marehemu kolimba aliona hili kwa kusema kimekosa dira na mwelekeo, na kauli ya Kolimba inakiandama CCM leo kwa mfano ufuatao:

CCM kwani kwa upande mmoja, kinahubiri suala la gharama kubwa zitazotokana na serikali tatu na marais watatu, pia ni chama kinachohubiri kwamba mfumo huu utaleta mgongano wa madaraka. Lakini kwa upande mwingine, CCM hii hii ndio iliyoamuru zanzibar iwe na makamu wawiwli wa rais na ndicho chama kilichoamuru uwepo wa marais watatu leo - rais wa jmt, makamo wa rais na rais wa zanzibar.

Itaendelea...



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Na katiba ni mali ya kila mwananchi. Katiba ya nchi si mali ya Chama.
CCM haikuwepo wakati wa muungano, wala wazazi wake TANU na ASP hawakushirikishwa.

Hata mchakato uliopo CCM haina ufahamu nao. Mchakato haukupitia ngazi yoyote ya chama na wala hakukuwa na uhalali kwa mali ya wananchi kuhodhiwa na kundi la watu katika vyama

Nape na Pinda kwa miaka 8 hawana cha kutuonyesha kuhusu suluhu ya kero za muungano.
Leo wanakuja na hadithi za kufikirika wakitegemea Tanzania ya Nnauye ndiyo ya leo.

Ndio mna vyombo vya dola na mnaweza kuvitumia kuhujumu jambo lolote.
Ninachowakumbusha ni kuwa historia haiandikwi inanukuliwa baada ya kujiandika.
Ipo siku mtashindwa kusimama mitaani kwasababu historia itawatenga, matakuwa on the wrong side of the history.

Labda mtueleze, ni wapi na lini duniani nguvu ya umma iliwahi kushindwa na dola?

Mkuu Nguruvi3, tatizo la CCM wanaamini kuwa wanachopenda wao basi kina wafaa watanzania na kinaifaa Tanzania, kitu ambacho si kweli.

Ukiangalia CCM ina wanachama milioni 5 hivi, lakini watanzania wako wengi zaidi ya idadi hiyo, haiwezekani interests za watu hao ndio ziwe interest za tanzania

Mimi binafsi si muumini wa serikali tatu, lakini naamini kuwa waliotoa maoni kwa tume ya Mzee Warioba wanawakilisha maoni ya watanzania, si ya wanaCCM tu. Kwa hiyo CCM ikifunika maoni yao, matokeo yake yatakuwa mabaya.

Ni rahisi kuwazuga watu kwa muda, lakini wakistuka wanageuka na wakigeuka ni issue sana.
 
[
Tuanze na suala alilojadili Nguruvi3 hapo juu - gharama za kuendesha muungano. CCM imependekeza kufunguliwa kwa akaunti ya fedha ya pamoja ambazo zitatokana na mapato ya vyanzo vya muungano na kwamba kuwekwe utaratibu wa kisheria ambao utatekeleza uendeshaji wa akaunti hiyo na kuweka mgawanyo wa mapato kwa pande mbili za muungano.

Kwanza kwa sentensi hii tu, maana yake ni kwamba ccm imekubali serikali tatu kwani inataja muungano na inataja pande mbili za muungano.

Swali linalofuata ni je kuna uwezekano wa kuwepo kwa pande mbili za muungano bila kuwepo kwa serikali ya Tanganyika? jibu ni hapana, vinginevyo ni muendelezo wa mazingaombwe ya chama.

Nikirudi kwenye pendekezo hili la ccm, suala la "kufunguliwa kwa akaunti ya pamoja ya fedha zitokanazo na mapato ya vyanzo vya muungano" ni suala ambalo halitekelezeki chini ya mfumo wa serikali mbili. Isitoshe akaunti hiyo imekuwepo kwa miaka ishirini sasa lakini malalamiko juu ya mgawanyiko wa mapato ya fedha hayajaisha. Swali la kumuuliza Nape Nnauye na Ccm ni je:
*Hayo mapato ya muungano yapo wapi chini ya serikali mbili wakati chombo cha kusimammia mapato tajwa kwa nchi inayoitwa Tanzania bara, chombo hicho hakipo? kutakuwa na ZRA, TRA na chombo gani?

Ni vigumu kuelewa kwanini kina nape na ccm wanafanya watanzania ni wajinga.
Lakini pengine wanadhania kwamba legitimacy ya serikali ya ccm bado chanzo chake ni masuala nje ya katiba kama nilivyojadili elsewhere kwani mapendekezo kama haya yatatekelezeka iwapo tu umma wa watanzania utakiamini ccm na kukipa uhalali wa kuendelea kuongoza nchi bila ya kujalisha constitutionalism.

Pengine kina nape hawaelewi (pengine) kwamba chini ya mfumo wa serikali mbili hakuna kitu kinachoitwa mapato ya nchi mbili kwani kuna mmapato ya zanzibar na mapato ya muungano. Kwa hili tu, tunaona jinsi gani kwa hoja za nguruvi3 hapo juu, pengine ni kwa miaka miwili tu kina nape na ccm watafanikisha malengo yao haya ya ajabu ajabu kwani muda sio mrefu "raia" wa "Tanzania Bara" watawazuia "raia wa Zanzibar" wasitumie kisichowahusu. Kwa upande wa zanzibar, wao wataendelea na malalamiko yao kwamba wanadhulumiwa mapato yao, kisa? Kukosekana kwa chombo cha kusimamia mapato ya "Tanzania bara".

Lakini nadhani ccm wanaelewa kabisa kwamba kuunda chombo cha kusimamia mapato ya Tanzania bara haiwezekani kwa sababu kufanya hivyo kutahitaji uundwaji wa serikali ya Tanzania bara (Tanganyika).
Kabla sijachangia hoja niliyoinukuu, niwarudishe wanajamvi nyuma kidogo kuhusu upotoshaji wa Pinda. Waziri mkuu anasema rais wa shirikisho atakuwa hana ardhi katika mfumo wa serikali 3.

Pinda amesahau kuwa katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010 imempa rais wa znz mamlaka ya kugawa maeneo bila consultation na rais wa JMT.

Kwa kwenda solo maana yake ni kumuondolea Rais wa JMT kipande cha ardhi ya znz.
Kipande alichobaki nacho ni cha 'Tanzania bara ya Pinda'. Sijui mantiki ya hoja ya Pinda ipo wapi.

Mantiki rahisi ni kuwa ardhi ya Tanganyika ndiyo ya muungano ikiwa na haki pande zote.
Hili ni kuwanyima Watanganyika haki na kuwapa wznz haki wasiostahili.

Nikirudi katika hoja ya Mchambuzi kuhusu mgawanyo wa mapato, hivi tunavyoongea kuna tatizo tayari. Zanzibar hawataki makusanyo yao yaingie katika serikali kuu, wameanzisha ZRA na TRA ambayo kimsingi mapato yake yanabaki znz.

Aslimia 4 ya pato la taifa inakwenda SMZ kutoka katika vyanzo ikiwemo TRA wasiochangia

Uwepo wa chombo cha pamoja una maana znz iendelee kuwa na ZRA halafu TRA iendelee kuwa ya JMT na kutoa haki kwa znz kushiriki katika mgao bila kushiriki katika makusanyo.

Mapendekezo ya rasimu ya CCM yanamaanisha uwepo wa ZRA na TRA.
Hapa ni gharama na maumivu kwa Mtanganyika.

Kama akina Pinda na Nape wamelenga huko ni sawa, kwa Watanaganyika huo ni usaliti na kuuza taifa


Mfano mzuri ni ule wa tume ya Warioba. Wazanzibar kupitia SMZ wamekataa kulipa gharama za tume ingawa waling'ang'ania uwepo sawa wa wajumbe wa tume.

Hoja yao kubwa ni kuwa gharama za tume ya Warioba zibebwe na JMT kwasababu hilo ni suala la JMT nao wao ni sehemu ya JMT. In other words gharama za tume ya Warioba amezibeba Mtanganyika 100%


Hili akina Nape na Pinda hawalioni kwasababu tu nyadhifa zao zipo hatarini kama hawatauza Tanganyika. Kwao Heshima na mtumbo yao mbele nchi baadaye.
Sisi tunawaambia, no no! mpo katika upande mbovu wa historia na tutawauliza siku moja mbele ya safari.


Ujanja wa kutumia Tanganyika unaendelea kpitia vitambulisho vya taifa.
Zoezi linaelekea znz kwasasa badala ya kusitishwa kwanza ili mustakabali wa taifa upatikane.


Nitoe mfano mwingine, Maalim Seifa anayetaka muungano uvunjike anacho kitambulisho cha Tanzania (Tanganyika). Kitambulisho hicho kitampa haki zote akiwa Tanganyika.

Mtanganyika wa kawaida hawezi kupata fursa za maalimu akienda znz kwasababu znz wana kitambulisho cha uzanzibar ambacho kinamtambua Mtanganyika kama Mcameroun, Nigerian au Congolese.

Hayo yanatokana na ukweli kuwa kuna znz na JMT. Kwa maneno mengine znz ni ya wznz na Tanzania ni ya wote. Lakini hiyo Tanzania inayosemwa ni Tanganyika.

Akina Nape na Pinda wanataka kutuaminisha kuwa upo uwezekano Znz huru na Tanzania bila tatizo.

Mchambuzi amesema ipo siku Tanzania bara ya Pinda itaanza kuwabagua wznz kwasababu itaona inaonewa. Niseme tayari yameshaanza kutokea katika ngazi za juu na huo moto unateremeka hadi katika mabweni ya shule. Kwa mara ya kwanza Watanganyika wamedai SMZ igharamie wajumbe wake katika BLK.

Haitaishia hapo kwasababu tutaanza kuhoji wale wabunge wa utalii kutoka znz wanaokuja Dodoma wanakuja kumwakilisha nani na kwa gharama za nani.

Katika bunge la katiba watu wanaangalia kwa macho ya wale na sisi, rejea kauli ya Ndugai.
Hali hiyo itakapofika katika ngazi za chini kutakuwa hakuna control, tutasikia wznz wametimuliwa shule au makazini katika hali za kusikitisha na kutisha.

Ikumbukwe kuwa Watanganyika wameficha hisia zao kwa muda mrefu sana, na wamezieleza kwa kutumia tume ya Warioba. Kuwakaidi ni kuwapa mbadala kitu tusichohitaji kutokana na matokeo yake.


Yes, akina Nape wanaamini wanavyombo vya dola, wasichotambua ni kuwa hawana dola.
Dola anayo mwananchi na siku ikifika kutakuwa hakuna nafasi ya majdiliano tena.

Mathalan, wznz walipoonyesha hisia zao kuwa hataki muungano hawakusikilizwa.
Walichokifanya ni kutafuta mbadala wa kuwasaka Watanganyika na kuwachoma moto kwa maguduria ya petrol mchana. Wahalifu wakaachiwa huru na SMZ kama njia ya kuonyesha sympathy kwa watu wao.

Hii ni kutokana na kutosikiliza wananchi na control inaposkosekana chochote kilicho mbele ni suluhisho.

Akina Nape na Pinda ndiko wanapolielekeza taifa huko, tusipowakemea na kuwakatalia mbinu za kulinda matumbo yao ipo siku tutakuwa tumeimana tukitokwa na machozi.
 
Back
Top Bottom