Mkuu Mkandara, talaka ipo kwa kadhi, kadhi kaingia mjini wanao omba hawaonekani.
Huko kwa kasisi wanadai huu ni mwili mmoja ingawa hawaamini wakiondoka hapo.
Huyo mwanamke mwenye funguo za nyumba anaomba afunguliwe mlango gani tena ili atoke?
Mkuu unasema Znz ni sehemu ya Tanzania basi iangaliwe katika fedha za maendeleo kama mikopo na misaada. Hoja yako imetumiwa vizuri sana na wanasiasa kupotosha umma na ni chanzo cha tunayoshuhudia.
Kule kwa Malikia wanasema 'blessing in disguise' kwa Tanganyika.
Kwa muda mrefu znz imejenga hoja ya kuonewa katika misaada. Hakuna ukweli katika hilo.
Tanganyika imelipa zaidi kuliko hiyo misaada inayosemwa. Tunasababu za kusema hivyo.
1. Kama misaada ingekuwa dawa kwa nchi ndogo, Burundi na Rwanda zisingetaka kuwa sehemu ya jumuiya ya Afrika mashariki. Kuna faida gani iliziona zaidi ya kudhani misaada ndio chimbuko la maendeleo yao?
2. Wznz wanaoishi Tanganyika ni nusu ya waliobaki Zanzibar. Hii imeongeza social strains katika huduma za jamii kama afya,ajira na elimu. Gharama hizo anazibeba Mtanganyika siyo SMZ.
3. Katika mambo 22 yaliyoongezwa na kupunguzwa hadi 7 na tume hakuna hata moja lililoiathiri au kumuathiri Mtanganyika. Mambo 15 yalikuwa kwa gharama za Mtanganyika kwa jina la Tanzania yakimfaidisha mzanzibar.
4. Special treatment
Wazanzibar wanapata huduma maalumu kwa sababu tu ni wazanzibar ndani ya Tanganyika
i) Kuna ajira maalumu kwa ajili ya wznz ambazo haziwekwi katika monetary value
ii) Kuna nafasi maalum kwa wanafunzi wa znz kwasababu tu ni wzn(hazina monetary value)
iii) Kuna mikopo isiyorudishwa inayotolewa kwa wznz kama wanafunzi (haina monetary value)
n.k. n.k. Hayo yote Mtanganyika aishie znz hapati kwakuwa hana kitambulisho cha ukaazi na huchuliwa kama raia wa kigeni. Hivi kama hupewi leseni ya udereva utapewa huduma gani znz?
5. Gharama za kuendesha muungano huu wa JMT ni gharama ya Mtanganyika
i) Gharama za watumishi na uendeshaji wa wizara anabeba mtanganyika
a) SMZ haina bajeti ya ulinzi na usalama ambayo peke yake tukigawana kwa ratio ya 1:8 bado ni mzito kwa znz. Mwenyekiti wa BLW kamati ya fedha kathibitisha hayo.
b) Gharama za wizara ya mambo ya ndani ni mzigo wa Mtanganyika, mznz hana wizara kama hiyo
c)Gharama za mashirika ya kimataifa ambayo znz imejitoa katika muungano inalipwa na Tanganyika
-ZMO ni shirika la SMZ likisajili meli kwa manufaa ya znz. Gharama za ZMO kule IMO zinalipwa na Mtanganyika kwa jina la Tanzania
a) Zanzibar ina civil aviation yake. Gharama za chombo hicho kimataifa zinalipwa na Mtanganyika
c)Gharama za taasisi, mashirika na hata balozi ni za Mtanganyika. Mchango wa znz ni kupata ajira
5. Bajeti ya 2012/13 JMT ambayo Zanzibar haitambui imeipa znz bilioni 32. Kiasi hicho ni kikubwa ukilinganisha na fedha za maendeleo zilizotolewa kwa mkoa wa Singida, Kigoma na Lindi kwa pamoja.
Kwa maneno mengine walipa kodi wa Tanganyika wanachangia maendeleo ya znz kuliko ya maeneo yao.
6.Fursa za kiuchumi kama soko la ajira na bidhaa kwa watu milioni 40 wa Tanganyika lipo wazi kwa wazanzibar. Fursa hizo haziwekwi katika monetary value ili kutoa picha kamili kwasababu kufanya hivyo kutaondoa hoja hafifu ya misaada.
7. Ikumbukwe znz inapata mgao wa asilimia 4 ya pato la taifa. Mchango wa znz ni chini ya asilimia 1.
Ukiweka katika mizani znz inanufaika zaidi kuliko misaada inayotolewa. Tataizo kubwa la upotoshaji ni kuangalia dollar bila kujali huduma na mambo yasiyoweza kuwekwa katika tahamani ya pesa.
Hayo yanatokea huku Mtanganyika akiwa mgeni katika JMT ambayo znz ni mshiriki pale inapomhitaji Mtanganyika tu,kinyume chake Mtanganyika ni mgeni kama raia wa Nigeria, Vietnam n.k.
Hili ni jambo jema kwa Watanganyika, linatoa picha ya huu muungano wanaolalamikiwa kuuhodhi.
Ni kukosa maadili ya kiroho Mtanganyika wa kidatu anapolazmika kulipa umeme zaidi ili kufidia gharama za mzanzibar asiyelipa kwasababu ni mzanzibar!
Ni kukosa maadili mzazi wa Tanganyika anapominywa pay cheque yake kwa kodi ili itumike kutoa elimu ya bure kwa mwanafunzi wa kizanzibar huku mwanafunzi wa Kitanganyika ima akinyimwa kabisa au arudishe
Ni kukosa maadili mznz anapokuwa katika bodi ya NECTA, bandari, anga, halmashauri, miji au wizara na kumnyima Mtanganyika fursa ndani ya nchi yake kuihudumia nchi yake
Ni kukosa maadili Mtanganyika atakapolipa fedha za mbunge kutoka znz akiwa Dodoma kujadili mambo ya Tanganyika yasiyomhusu kwa mujibu wa katiba ya znz ya mwaka 2010
Labda tujiulize, hivi kuna sababu gani kwa mbunge wa znz kuwa mjumbe wa kamati ya bunge la JMT ambalo katiba ya znz hailitambui. Mbunge wa znz anapkagua shughuli za maendeleo Ngara ni ili achangie nini ikiwa nchi yake haitambui uwepo wa JMT.
Ni kwa msingi huu tunasisitiza kuwa sasa muungano uwe wa kichumi zaidi ukilenga kuleta mafao kwa pande mbili bila kubeba au kubebwa. Usawa huo ambao ni muhimu na lazima hauwezi kupatikana ikiwaipo nchi kati ya mbili haionekani.
Leo nani ataongelea madhila haya kule Dodoma? Tanganyika inawakilishwa na nani?
Tanzania bara ya Pinda haiwezi kusimamia Tanganyika kwa kishikizo cha jina ZNI.
Inahitajika serikali ya Tanganyika, kwa watu wa Tanganyika na kwa mnufaa ya Tanganyika.
Mazingaombwe ya kuviziana kwa herufi za majina na kuwekeza kwa herufi sasa yafike mwisho.
Watanganyika tumeliona hili, akina Nape hawawezi kuzuia tena kimbunga.
Wanaweza kuahirisha kwa miaka 2 lakini hawatazuia.
Hatuwezi kutumia muda wetu kufikiri namna ya kuishi na wznz badala ya kufikiri umasikini na adha nyingine. Wznz wameukana muungano kwa ushahidi wa katiba ya 2010, ninyi wabunge wa Tanganyika Dodoma hamuoni hilo?Mkuu Mkandara, misaada ipi zaidi ya hiyo inayotolewa?
Nitakujibu moja baada ya jingine kwa sababu naelewa sisi tunatafuta sababu kama vile wao wanavyozitafuta sababu pasipo kutafuta ukweli japo ukweli upo wazi kabisa.
1. Swala la Misaada ya maendeleo kwa nchi halizihusu nchi za jumuiya ya EAC maaa kila nchi ina mipango yake na hulipa madeni yake. Hivyo, kama ingekuwa misaada hiyo inaombwa kwa ajili ya EAC kisha ni Kenya Uganda na tanzania tu ndio wenye kupanga matunmizi ya fedha hizo hapo ungesikia kero na lawama lakini sivyo.
2. Wazanzibar wanaoishi bara ni wengi hilo halina Ubishi na vile vile kumbuka wanalipa kodi bara vile vile, wanaijenga bara vile vile hivyo huwezi kuchukua hicho kama kipimo cha social strains ikiwa wao wamekuja bata kama wawekezaji zaidi ya Wataguta kazi. Pili, gharama za ulipaji madeni huwezi kuzipima pasipo kuzingatia asilimia hiyo hiyo unayoitumia maana Ikiwa deni ni bil. 3 bara ikalipa asilimia 95 na Znz asilimia 5, ifahamike pia kuwa hao waZnz mil. 2, ni asilimia 5 ya population ya nchi nzima hivyo mchango wao hauna tatizo.
3. Umezungumzia mabo 22 kuwa kati yake 15 yanamnufaisha Znz lakini je hujui kwamba jambo 1 tu linaweza nkubeba mambo madogo madogo 10. kwa mfano, Ujenzi wa Airpost au bandari bara inaweza kuwa sawa na mfuko mzima wa bajeti ya Znz. Je, kuna tatizo gani serikali ya Muungano kujenga bandari Znz au kituo cha kuzalisha umeme! isipokuwa kila kitu wategemee kutoka bara, halafu tuwanange kuwa pasipo Bara hawana kitu!
4. Mkuu wangu hili la nafasi maalum linatokana na Hulka za kibinadamu maana pasipo kufanya hivyo Wazanzibar wasingeweza kusoma Bara, wasingeweza kupata ajira bara kwa sababu sisi MIAFRIKA NDIVYO TULIVYO. Tuna mila na Utamaduni wa Ukabila, Udini na Jinsia haswa baada ya kuingia Ubepari. Nguvu kubwa ya madaraka na mamlaka imeshikwa na Bara na hata nisemavyo hivi leo pasipo kipengele maalum cha kusisitiza uongozi wa juu ktk Jamhuri uiweke Znz kama special treatment basi haitakuja siku rais, makamu wala waziri mkuu kutoka Zanzibar.
Bara tuna uchu sana wa madaraka kuondoka ktk umaskni na tunachofanya ni kugawana tu umaskini. Ebu nambie huo Uhaguzi wwa mwaka 2015 hakuna kingozi yeyote anayefikiriwa na wananchi atoke Zanzibar japo Mkapa na JK wote kwa awamu nne zilizopita marais na mawaziri wakuu wote wametoka bara. Ni bahati tu kifungu cha makamu ndicho kimeilinda nafasi hiyo laa sivyo zanzibar wasingekuwa na hata waziri.
Kwa kuongezea hili ebu tazama Wanawake, hadi leo hii miaka 50 baada ya Uhuru hatujawahi kuwa na waziri mkuu, makamu wala kmwanamke alokwisha fikiriwa kuchukua kiti cha Urais japo tunadai wanayo haki ya kugombea. Mind set zetu zimeshakuwa brain washed, haziruhusu kuongozwa na mwanamke, Hivyo Haki kama hizi zinatakiwa kulindwa japo mtasema ni special treatment.
5. Hizo gharama za uendeshaji serikali ya jamhuri linajibiwa tena na jibu langu ya kwamba lazima utazame asilimia ya watu kwanza kabla hujaweka madai kama haya. Ikiwa asilimia 90 ya Watanzania wanaishi Bara ulitegemea vipi Znz ilipe deni sawa na Bara wakati baba wa familia hii ni bara? sijui kama unanielewa!.
6. Fursa za Ajira ukitaka kuziweka wazi ndipo unaonyesha Utengano na kwamba tunashindwa kuelewa kuwa hatukuungana kuwa nchi moja isipokuwa tuna nchi mbili kuunda moja pasipo mke kupoteza nguvu zake na sababu ya kuolewa kama mke. Ni utaratibu unlojengwa kulinda haki za Zanzibar kama vile haki za Binadamu zinavyowalinda wanawake ktk ndoa. Hatuwezi sote kuwa midume kisha ukaita ndoa hiyo kuwa halali lakini hatutaki tuitwe mashoga.
Nitarudia kusema Muungano wa Tanzania ni special na one of its kind maana tumeunda Jamhuri inayotokana na mfumo wa Political Union. Na itambulike tu kwamba Znz ilikuwa nchi huru siku ya Mapinduzi kumuondoa Sultan na sii vinginevyo. Ule uhuru wa mwaka 1963 ilikuwa Uhuru wa bandia kama ule wa Ian Smith na Rhodesia hautambuliki.
Hivyo, Sisi bara kuingia gharama hizi kama baba mzazi wa Mapinduzi! na ikumbukwe kuwa CCM (Chama cha MAPINDUZI) kilichukua jina hilo tokana na Mapinduzi ya Znz. Hofu kubwa ilotangulia ni Znz kuwa chini ya Utawala wowote wa kigeni, iwe Sultan ama influence na mgeni yeyote ni tishio zima ktk usalama wa bara(Tanganyika), Afrika mashariki na Umoja wa nchi za Kiafrika. Hii ndio ilokuwa dream wa waasisi wetu wa UHURU kwa nchi zetu.
Hivyo sisi tulichukua jukumu na kiapo cha kuyalinda Mapinduzi yale kama vile baba anavyokubali kufunga ndoa akijua majukumu yatakayo mkabiri ktk ndoa, tena tumemuoa binamu yetu kwa lengo la kuhakikisha vizazi vyetu ndio watafaidika na Utajiri wa mali zetu na sii wageni.
Hatuwezi sema lazima mama pia achangie sawa na baba. Na mwisho, sisi watoto tulozaliwa na wazazi hawa hatuwezi kupanga utaratibu wowote wa ndoa ama talaka ya wazazi hawa, hilo sintoliafiki kabisa isipokuwa siku BLM na wala sii BLW linaloweza kuweka madai kuomba talaka - Huu ndio mtazamo wangu.
Na kuhusu bajeti ya Znz. Mkuu wangu wewe mwenyewe umekiri kwamba kuna Wazanzibar wengi bara kuliko Zanzibar hivyo kodi zao pia ni mchango ktk malipo ya gharama hizo. Hizo Bil.32 bila shaka ni katimaka maswala ya Muungano ambapo wao wanatazama sii tu kuyajenga majimbo bali ni kisu chao kama nchi ilojiunga.
Hata katika maisha ya kawaida huwezi kunambia tukiwa na Ubia na wewe basi mgao utatazama wewe una watoto wangapi badala ya wewe umeingia vipi ktk makubaliano ya kimkataba na yalisema nini ktk maswala ya Equity na ugawaji dividend. Umezungumzia tu faida lakini umesahau pia kwamba hasara zote zinazotokana na bara hata wao wanalipia wakati sisi ndio tumefanmya Ufisadi, Iwe EPA, Rada, wizi benki, IPTL,Richmond/Symbion na kadhalika. Na ukitazama kwa makini viongozi wetu wa bara ndio wana kesi na kulindana ktk Ufisadi kuliko tunavyowasikia Wazanzibar ktk serikali hii ya Muungano.
7. Ikiwa Zanzibar inapata asilimia 4 nwakati mchango wake ni asilimia 1 nadhani hapa tunakosea sana kwa sababu huwezi kumlipa mama fedha kutokana na mchango wake ktk familia. michango mingine haipimwi kwa fedha isipokuwa ushirika ulokuwepo baina ya nchi husika na mipango ya maendeleo ndio pekee inayoiwezesha Zanzibar kuchangia zaidi. Sasa ikiwa kila investment kubwa ya kitaifa itafanyika bara ulitegemea vipi zanzivar wachangie zaidi?... Kwa nini Muungano huu usihakikishe Zanzibar inapata investment za kutosha ili kuongeza mchango wake ktk mfuko wa Taifa!.
Swala hili hata sisi wananchi wa bara tunalo maana kila Investment kubwa hufanyika mkoa wa Dar es Salaam ikasahaulika mikoani. Leo gas imepatikana Mtwara lakini umeletwa Dar ili kuzalisha Umeme ambao ungeweza kabisa kuzalishwa kule kule.
Tutake tusitake pamoja na ujenzi wa bomba la gas bado nguzo za umeme zitahitajika kati ya Dar na Mtwara iwe kutoka upande wowote maana taifa haliwezi kuwa kizani isipokuwa mijini tu. Sasa kwa wale wanaosema Dar es salaam inahitaji fungu kubwa la maendeleo kuliko mikoa mingine ni kushindwa kuelewa kwamba mikoa hiyo ingeweza pia kuchangia zaidi ikiwa hizo investment zingewekwa huko.
Hao wabunge wa baraza la Katiba hawataweza kuijenga katiba mpya kwa sababu sisi wote ni wababaishaji tu. walafi na mafisadi kwa aina. Nilisema haitawezekana na kama itawezekana basi hakuna katiba mbadala. Sasa tazama hawa wabunge wanavuta laki 3 kwa siku, leo hii ni wiki ya 3 hawajamchagua hata mwenyekiti ina maana wameisha vuta zaidi ya mil. 5 kila mmoja wao kwa kazi isoonekana!, haya mazinmgaombwe gani? - Alamsiki.