Katika hatua tuliyofikia sasa, mjadala unaounga mkono mfumo wa serikali mbili umetawaliwa na hoja za wanasiasa wachumia tumbo na wachumi "uchwara" wenye kupinga serikali tatu kwa hoja za gharama kwa walipa kodi lakini pia kwamba zanzibar haina uwezo wa kuchangia gharama za muungano kwa usawa na Tanganyika. Kwa upande wa serikali tatu, mjadala huu umetawaliwa na wanasiasa wanaotanguliza siasa safi, wachumi wanaojadili na kuchambua faidi za serikali tatu kwa muungano, nchi shiriki na wananchi kwa ujumla, lakini pia wapo wanaharakati. Kwa mazingira haya, tutarajie mjadala mkali ndani ya bunge la katiba vifungu juu ya muundo wa muungano vitakapofikiwa.
Hoja za wanasiasa wa serikali mbili tayari inaeleweka ni hoja zinazoweka mbele madaraka na nia ya kuendeleza control of the people badala ya control of the territory kwa wanasiasa wa CCM, hivyo kutokuwa na uchungu na Tanganyika ambayo ndio asili yao. Tukumbuke kwamba mataifa yaliyoendelea yanajali zaidi kudhibiti territory zake kuliko kuthibiti watu. Zama za mataifa kuthibiti watu zimepitwa na wakati. Tutajadili hili siku nyingine kwa undani zaidi. Kwa upande wa hoja za kiuchumi ambazo wana ccm wanaotetea serikali mbili hutumia, mbali ya hoja ya gharama ambayo ni dhaifu sana, pia wapo wanaojadili kwamba serikali tatu hazifai kwani zanzibar haina uwezo wa kuchangia sawa na bara/Tanganyika.
Profesa wa uchumi kutoka UDMS, humphrey moshi hivi majuzi alinukuliwa na vyomba vya habari akisema kwamba - tangia muuungano uanze mwaka 1964, zanzibar wamechangia mara tatu tu: 1964/5, gharama ya kuendesha muungano katika masuala yale yaliyokubaliwa chini ya mkataba wa muungano zilikuwa ni shillingi milioni 107.Kati ya hizi, znz ilichangia shillingi milioni 10, sawa na 9% ya gharama zote. Mwaka 1965/66, gharama za kuendesha muungano zilifikia sh. Milioni 153, na znz walichangia milioni 12, sawa na 8%; Mwaka wa mwisho kwa znz kuchangia kwa mujibu wa profesa mushi ilikuwa ni 1966/67, ambapo gharama zilikuwa ni milioni 176 huku znz wakichangia sh. Milioni 8.1, sawa na 5% ya gharaa zote za muungano. Kutokana na haya, profesa mushi na wengine wanajadili kwamba zanzibarr haitakuwa na uwezo wa kuchangia kwa usawa na Tanganyika chini ya serikali tatu.
Kuna ukweli katika hoja hii lakini wanachosahau aidha kwa bahati mbaya au makusudi watu wa upande huu wa hoja ni kwamba kuna two factors zilizochangia hali hiyo ya zanzibar ijitokeze:
1. Orodha ya muungano ilianza kuongezwa kinyume na mkataba wa muungano na bila ya kuishirikisha serikali ya znz katika maamuzi haya. Katika hali hii, zanzibar ikaanza kuona kwamba inalazimishwa kuendelea kuingia gharama kulipia mambo ambayo wao walitegemea kwamba yangekuwa yana gharamiwa na nchi shiriki peke yake. Kwa maana nyingine, nyongeza ya orodha ya muungano kwa zanzibar waliona ni mzigo na ni kinyume cha mkataba wa muungano.
2. Factor ya pili ni kwamba mara tu baada ya mkataba wa muungano kusainiwa, ilipitishwa sheria ya muungano ambayo nia yake ilikuwa ni kupunguza makali na relevance ya mkataba wa muungano. Moja ya sheria hizi zilipelekea zanzobar kupata kilema cha uchumi. Tukumbuke kwamba kipindi cha nyuma kabla ya muungano, znz ilikuwa na uchumi bora kuliko Tanganyika. Tutaangalia hili kwa undani baadae.
Kuna maswali muhimu ya kuyachambua:
1. Je, chini ya mfumo wa serikali tatu kuna ukweli kiasi gani kwamba znz haitaweza kuchangia katika masuala saba ya muungano kwa mujibu wa rasimu ya katiba?
Nguruvi3 aliwahi kujadili hili, tunaomba utusaidie tena.
2. Je, kipi ni ukweli kati ya haya - znz haitakuwa na uwezo wa kifedha kuchangia muungano wa serikali tatu au ni kwamba tu znz hawataki kuchangia kwa sababu za kihistoria? (Rejea madhara ya nyongeza ya mambo ya muungano kwa znz).
Vinginevyo ima iwe znz hawana uwezo kiukweli au uwezo utakuwepo chini ya utaratibu ulioanishwa na rasimu lakini wanakwepa tu ukweli, hali hii ni sababu tosha ya kuvunja muungano kwani hatukuungana ili mshirika mmoja aje kumbeba mshirika mwingine, unless kufanya hivyo ilikuwa ni kwa lengo la kwenda serikali moja. Lakini hakuna ushahidi katika mkataba wa muungano kwamba kulikuwa na lengo la serikali moja. All that said and done, iwapo znz hawana uwezo (kiukweli au kwa visingizio), huu ni wakati muafaka kwa Tanganyika kuanza kujiendesha kivyake.
Muungano wa znz na tanganyika ulikuwa ni muungano wa hiyari, sio wa lazima, na hata mkataba wa muungano uliweka hilo wazi huku pakiwa na provision za nchi washirika kujitoa iwapo wataona muungano hauna faida. Ni katika mazingira haya, mwaka 1968 nyerere alitamka mbele ya mwandishi wa gazeti la observer la uingereza kwamba hatowapiga mabomu wazanzibari iwapo wataona muungano hauna faida kwao na kuongeza kwamba muungano ambao washirika hawautaki ni muungano usiokuwa na maana, ikiwa na maana kwamba hata Tanganyika nao wakiuchoka, solution si mabomu. Swali linalojirudia ni je:
*iwapo muungano ulikuwa ni wa hiyari, ikiwa mshirika mmoja wa muungano anashindwa kuchangia gharama za muungano, kwanini muungano huo uendelee kuwepo?
Vile vile:
*Mapinduzi ya zanzibar ya mwaka 1963/64 yalilenga nini kwa wazanzibari?
Ni dhahiri kwamba mapinduzi yalilenga wazanzibari kujipatia mamlaka kamili na itokanayo na wananchi wa znz, lakini muhimu zaidi - uhuru wa kujiendeshea mambo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Kwa maana nyingine, wazanzibari hawakufanya mapinduzi ili waje kuitegema Tanganyika kujiendesha kiuchumi (kisiasa inaonekana wanazidi kurudhika na mamlaka wanayopewa). Iwapo nipo sahihi, sasa hizi hoja kwamba zanzibar hawatakuwa na uwezo wa kuchangia muungano wa serikali tatu ni hoja za kina nani na zina ukweli gani na kwa maana hiyo huu muungano wa hiyari una maana gani kuwepo wakati moja hana uwezo wa kuchangia gharama za kuuendesha?
Hapo awali niliahidi kujadili kidogo sheria za muungano ambazo zilipitisha mara tu baada ya muungano kusainiwa 1964. Sheria hizi zilipitishwa bila ya kumshirikisha mshirika mwingine wa muungano (znz) kwani ni upande wa Tanganyika ndio ulikuja na sheria hizo na kuzipitisha kimya kimya tena wakati huo Serikali ya Tanganyika ikiwa bado ipo na ikifanya kazi zake kwa mujibu wa mkataba wa muungano. Hii ilikuwa ni katika kipindi cha mpito ambacho kwa mujibu wa mkataba wa muungano, kilikuwa ni cha mwaka mmoja tu ambapo rais wa JMT na wa Znz ambae alikuwa ni makamo katika kipindi cha mpito, wangeshirikiana kuteua tume ya katiba na baraza la kutunga katiba vyombo ambavyo vingesimamia mchakato wa katiba mpya ya JMT. Katika kipindi cha mpito, katiba ya Tanganyika (kwa mujibu wa mkataba wa muungano) ikafanyiwa marekebisho machache ili iweze kutumika kwa muungano, ile ya tanganyika (original) iendelee kutumika tanganyika huku znz wao pia wakifanyia kazi utaratibu wa katiba yao ya taifa shiriki la muungano, ikizingatiwa kwamba hawakuwa na katiba kwani mapinduzi ndio kwanza yalikuwa yamefanikiwa.
Baada ya muungano kutiwa tu saini na kuingiza taifa jipya katika kipindi cha mpito kuelekea katiba mpya kwa mujibu wa mkataba wa muungano (1964), matukio kadhaa yakajitokeza. Moja wapo ilikuwa ni ujio wa sheria za muungano za mwaka 1964, siku chache baada ya mkataba kutiwa saini, na hii ilikuwa kinyume kabisa na mkataba wa muungano, sheria ambazo zililenga kuufunika mkataba wa muungano usiwe na makali kuelekea katiba mpya ya JMT. Katika sheria hizi, ipo ile ya kifungu cha tisa cha sheria za mUungano (1964) ambacho kimsingi ndio sheria iliyoipa kilema cha kudumu uchumi zanzibar. sheria hii ilipitishwa kimya kimya bila ya kushirikisha serikali ya znz. Sheria hii (1/Mei/1964), siku tano baada ya kusainiwa muuungano inasema hivi:
Mali na Mikataba: Mali zote na haki juu ya mali za jamhuri ya muungano wa Tanganyika, na haki zote juu ya mali za jamhuri ya watu wa zanzibar zilizokuwa zinamilikiwa au kutumiwa au zilizomilikiwa au kutumiwa kimsingi kuhusiana na mambo ya muungano, zitakuwa kuanzia siku ya muungano, chini ya jamhuri ya muungano
Muhimu:
*Sheria hii ni moja ya sheria kadhaa zilizopitishwa kinyemela baada ya mkataba wa muungano kusainiwa, na kupitishwa kimya kimya, lengo ikiwa ni kuanza kuuzunguka mkataba wa muungano ili huko mbele iwe rahisi kuhalalisha uchakachuaji.
Kitendawili juu ya kwanini zanzibar iliacha kuchangia gharama za muungano 1967 kinaweza teguliwa na sheria hii, na hii ni mbali ya sababu za ongezeko la masuala ya muungano ambayo znz haikushirikishwa na haikuona ni haki kuyachangia wakati ingeweza yaendesha yenyewe. Ikumbukwe pia kwamba ni mwaka huohuo (1967)serikali ya Tanganyika ilizikwa rasmi kupitia sheria namba 24 ambayo ilizaa tanzania bara.
Ili zanzibar iwe na haki kuchangia sawa na Tanganyika chini ya mfumo wa serikali tatu, suala la assets za zanzibar zilizotaifishwa na Tanganyika kwa koti la muungano ni lazima litaibuka. Na tutake tusitake, ipo hoja ya kisheria katika hili, hasa iwapo mkataba wa muungano utakuwa ndio the legal foundation of the union.
Tutaiangalia sheria hii namba tisa ya mwaka 1964 kwa undani zaidi baadae.
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums