Duru za siasa: Bunge la Katiba, upotoshaji na kiwewe cha kuzinduka Tanganyika

Duru za siasa: Bunge la Katiba, upotoshaji na kiwewe cha kuzinduka Tanganyika

Mkuu Mkandara
Bado hujajibu maswali niliyouliza ba hasa la la mwisho,wewe unapendekeza mfumo gani, kwanini na uendeshweje.
Mkuu labda hunisomi vizuri, Nimesema mundo uliopo hauna tatizo kabisa na wala sii sababu ya kuandikwa katiba mpya. Katiba mpya inatakiwa kutokana na transition yetu kutoka Ujamaa kwenda Ubepari (Economic liberalization) ili kuuboresha MWONGOZO wa nchi kulingana na wakati na sio utunzi wa sheria za makundi(constitution law) ambazo zinaweza kufanyiwa amendments wakati wowote pasipo kuandika katiba mpya.

Kama utafiti ungedhihirisha kuwa kero za muungano ndio sababu ya utunzi wa katiba mpya basi wasomi wangekuja na suluhisho kabla hata ya kuunda tume ya katiba. Naamini katika serikali 2 kama ilivyoasisiwa na viongozi wetu ambao walipitia kila sababu ya kutokuwa na serikali 1, au 3 maana msifikiri hawakuyatazama haya. Walielewa mabaya ya serikali moja, au 3 na tungevuna kitu gani.

Hakuna kati yetu alofanya utafiti isipokuwa mapenzi yake, Ukabila wake, Udini wake na kundi lake. hakuna kati yetu aopenda kuwa Mtanganyika au Mtanzania, alopenda kuzaliwa bara au visiwani isipokuwa ni mazingira ya Utaifa yalotufikisha kuwa na umoja huo. Sasa tunapowapa wananchi jukumu la kutoa maoni ya muungano wa nchi zetu ina maana tunataka katiba itutumikie sisi na sio sisi kuitumikia katiba. Yale yale ya kiimani ya binadamu kuandika Biblia/Kuruan ukitegemea mchungaji awaogope kondoo anaowaongoza na sio Biblia inayomfunga kila muumini!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mkandara

Kwanza niseme kuwa sababu za kutaka Tanganyika izundiliwe ni nyingi, nijadili chache



  1. Mkataba wa 1964 ulikuwa wa nchi mbili Tanganyika na Zanzibar
Kuondoka kwa Tanzania hakukuwa na sababu za kisayansi zaidi ya za kisiasa.
Tumejadili namna Tanganyika ilivyofutika bila ridhaa ya wananchi isipokuwa amri ya Rais na sheria 24 ya 1967



  1. Katiba ya 1977 iliunda taifa moja la Tanzania.
  2. Katiba ya Zanzibar 1984 ikaunda taifa la Znz nje ya lile la Tanzania
  3. Katiba ya 1984 iliyofanyiwa marekebisho 2010 ikarudisha taifa la znz

Hadi hapo unaona jinsi malalamiko ya wznz kuwa Tanganyika ndiyo Tanzania yalivyokuwa mazito. Malalamiko yametumiwa na znz kuumiza Tanganyika ambayo ipo kwa jina la Tanzania bara. Hakuna mahali Tanzania bara imekuwepo


JMT imebakia Tanganyika, znz wanaihitaji wakiwa na dhiki zao, baada ya hapo hawajali uendeshaji wakiendelea kuomba haki wasizostahili kwa jina la Tanzania.


Huu ni uhuni wa hali ya juu. Hawalipi bill kwasababu ni Tanzania, na hawachangii kwasababu ni znz kama nchi ya nje


Pili, Tanganyika inahitaji nafasi bila kubeba zigo isilojua lina nini na maana gani ndani yake kwa sababu za kiuchumi. Muungano wa dunia ya leo is all about economy


Tatu: Tume zilizoundwa zimeonyesha umuhimu wa kuzinduka kwa Tanganyika.


Nne, muungano wa serikali 2 umekuwa na kero miaka 50 na hakuna jibu. Inashangaza Mkandara anaposema hakuna tatizo.


-Serikali 2 anazoongela Mkandara ni ya znz na Tanzania. Sijui hesabu gani hizo zinazoweza kuwa na seti ya namna hiyo, sina uhakika.


Huwezi kuwa na nchi moja mara mbili, znz pekee na znz ndani ya muungano. Halafu ukawa na Tanzania isiyokuwa na mshirika wa znz ambaye ni Tanganyika


-Matokeo yake znz wamekuwa na kiburi na sasa BLW linaendesha JMT.

Kwamba Znz inaweza kuamua Tanganyika ifanye nini.


Huo ndio muungano Mkuu Mkandara anasema hauna tatizo kabisa.

Kwamba, tukitaka kutumia pesa zetu kwa ajili ya watu wetu lazima tuvuke bahari kwenda kuomba watu 50 wa BLW ruhusa kwa kile Mkandara anchosema ni asilimi 5 muhimu sana katika maisha ya Mtanganyika.


Mkanadara ukumbuke Nyerere alisema kama znz hawataki muungano hatawapiga mabomu. Na sasa kwa kutumia takwimu, katiba na majukwaa ya kisiasa inaonekana hawataki. Kwanini tuwalazimishe ili hali hatuna cha kupoteza.


Sisi ndio tunawabeba, wao wanataka kutembea njia ni moja tu, wakae mgongoni kwa aadabu na heshima au wavae viatu watembee wenyewe.


Hili la kutaka kugawana vyeo, madaraka, ubaguzi wa kizanzibar tumechoka nalo bila kujua gharama zake sasa basi. Sisi ni nchi iliyokamilika na wazee wetu walipigania uhuru si kwasababu ya kumfurahisha mzanzibar asiye na shukran au heshima, ni kwa ajili ya Watanganyika


Siku 22 tunajadili namna ya kuishi na wznz badala ya kujadili umasikini wa Mtanganyika na jinsi tunavyodhamiria kusaidia jamii yetu.


Tunakosa nini wznz wasipokuwepo na tutaendelea kuendeshwa na kundi hili la watu laki 5 hadi lini.


Mkandara kwa kutumia katiba ya znz 1984 na marekebisho 2010 nionyeshe sehemu moja tu ambayo mznz anajitambulisha kama Mtanzania.


Nadhani unahitaji wajitambulishe hivyo ili waendelee kunufaika na Tanganyika.


Kwasasa Tanganyika hatuna muda huo, we need our country ili tujadili ufisadi, umasikini, ujinga na maradhi na si jinsi yaku appease wznz kwa gaharama zetu wakitulipa matusi, kashfa na kejeli.


Unless una hoja nyingine, hoja za kisiasa, kiuchumi na kijamii zote tunaziona zikielekeza kuzinduliwa kwa Tanganyika hata wewe unakubali hilo.


Unless you have another reservation which I hope and I see you got it, there is absolute no reason to defend the failed status quo.


Tanzania ipi unaongelea wakati wznz hawataki kuitwa Watanzania Mkandara?


It is time we recall Tanganyika for Tanganyikans

 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3,

Mkuu sikuelewi kabisa maana unaposema Katiba ya mwaka 1977 ni katiba ya JMT na sio kinyume cha kutoitambua zanzibar kama nchi. hata kesho tukiunda serikali 3 bado katiba ya JMT itazungumzia tu yaliyomo ktk JMT pasipo kuelezea kikatiba maswala yasiyokuwa ya muungano ama mfumo wa serikali ya Tanganyika au Zanzibar.

Katiba ya Jamhuri itazungumzia muundo wa serikali ya JMT hiyo ya Muungano wakati huo huo serikali za Tanganyika na Zanzibar pia zitakuwa na katiba zao zinayozungumzia muundo wake na ktk maswala yasokuwa ya Muungano. Katiba ya mwaka 1977 haipingi kuwepo kwa serikali ya Zanzibar na kama ulivyosema serikali ndio huunda nchi. Kumbuka tu tulikuwa tukisafiri kwenda Zanzibar tumebeba passport zetu hapo zamani.

Kusema kweli sikupati kabisa hasa unapotumia katiba ya Muungano ama serikali ya JMT kwa kuitambulisha bara peke yake.
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3,

Mkuu sikuelewi kabisa maana unaposema Katiba ya mwaka 1977 ni katiba ya JMT na sio kinyume cha kutoitambua zanzibar kama nchi. hata kesho tukiunda serikali 3 bado katiba ya JMT itazungumzia tu yaliyomo ktk JMT pasipo kuelezea kikatiba maswala yasiyokuwa ya muungano ama mfumo wa serikali ya Tanganyika au Zanzibar.

Katiba ya Jamhuri itazungumzia muundo wa serikali ya JMT hiyo ya Muungano wakati huo huo serikali za Tanganyika na Zanzibar pia zitakuwa na katiba zao zinayozungumzia muundo wake na ktk maswala yasokuwa ya Muungano. Katiba ya mwaka 1977 haipingi kuwepo kwa serikali ya Zanzibar na kama ulivyosema serikali ndio huunda nchi. Kumbuka tu tulikuwa tukisafiri kwenda Zanzibar tumebeba passport zetu hapo zamani.

Kusema kweli sikupati kabisa hasa unapotumia katiba ya Muungano ama serikali ya JMT kwa kuitambulisha bara peke yake.
Katiba ya mwaka 1977 ilitambua Tanzania bara na Tanzania visiwani au Tanzania Zanzibar. Haikutambua Zanzibar. SMZ ilikuwepo halina halina tatizo.

Katiba ya 1984 iliyokuwa prompted kuandikwa kwasababu tu znz imeitwa visiwani ndiyo iliondoa nenovisiwani na kusisitiza Znz. Ndio maana inasomeka katiba ya Zanzibar ya 1984.

Katiba ya 1984 ikafanyiwa marekebisho na kuweka mipaka ya znz kama nchi. Ikamtambua rais wake na kuweka vyombo vya ulinzi ilivyoita vikosi maalumu. Ikampa rais wa zanzibar mamlaka ya kugawa nchi (ambayo kwa mujibu wa katiba ya 1977 ni Tanzania)
Marekebisho hayo yakalipa BLW kuhoji, kukubali au kukataa maamuzi ya bunge la JMT

Hadi hapo utaona znz inajiondoa kwenye muungano yenyewe na wala haikuondolewa na mimi au awaye.
Unachopigania wewe ni kuwa Tanzania ina jina la zn ndani yake. Upo sawa sawa kimaandishi, kimantiki hilo halipo kwasababu tayari znz ni nchi na ina serikali yake iliyoungana na nchi nyingine ambayo hatuijui kuunda JMT.

Niweke sawa rekodi, siku zote ninasema nchi inakuwepo halafu serikali inafuata na si kinyume chake.
Serikali ni chombo kinachoundwa kwa ajili ya kuendesha nchi. Kuna uwezekano serikali isiwepo na nchi ikabaki ilivyo lakini nchi haiwezi kutowepo kukawa na serikali.

Ninapokuelewa ni kuwa hata ikiundwa serikali ya shirikisho bado Znz itatumbuliwa kama nchi. Ni kwa mantiki hiyo Tanganyika iliyofichwa izunduke ili tuwe na Tanganyika pia halafu wakae pamoja na kuangalia eneo gani wanaweza kufanya kazi pamoja kwa faida ya pande zote( siyo kubebana tena).
 
Mkuu Mkandara
Labda unisaidie tena kuhusu serikali 2
Kwa maiaka 50 kero zimekuwepo, nini unadhani kinakosekana au kinahitaji kufanyika ili kuondoa hizo kero kwa sasa so that we can abandone the idea of Tanganyika.
 
Na mkuu hapa tulipofika kuna sitauation zifuatazo
1. ZNZ hairidhiki na muungano kwa kuona inaonewa 'nataka siataki inaikwaza'
2. Watanganyika wameachwa katika muungano na wanataka waendelee na safari yao

Serikali 1 kama taifa analotaka Mkandara haiwezekani kwasababu znz ni bora na haiwezi kupoteza utaifa kama Tanganyika ilivyofanya miaka 50 iliyopita.
Serikali 1 ni myth

Serikali 2 haziwekani, kuna reseravations za wznz, na Watanganyika wameona walichokuwa hawajui nao wana reservation zao tena genuine and serious.

Miaka 50 haikutoa jibu it is unlikely kuna dawa iliyobaki unless Mkandara atufungue akili tena.

Machaguo ni mawili 2
1. Serikali 3 tukiwa na mambo machache sana tena kwa kushirikiana(si kubebana)
2. Vunja jahazi tugawane mbao.

Kuendelea kulazimisha muungano kwa mabomu ya machozi ni kujidanganya.

Tume ya shelukindo ya 1977, doubt kama mfumo unafanya kazi
Aboud Jumbe akaja na lake,ni 3
G55 ikaibuka, ni 3
Tume ya Nyalali ikaja na hoja, ni 3
Tume ya Kisanga ikapigilia Msumari, ni 3
Tume ya warioba ikawasikiliza wananchi, ni 3

Kote huko kumeonyesha bila doubt kuwa the status quo haiwezekani.

CCM wana uwezo wa kutumia Samwel Sitta, Mabomu ya machozi, risasi za moto na kila kitisho.

Hilo litafanikiwa kwa muda mfupi, baada ya hapa we will return to the drawing board

Tatizo ninaloliona ni kuwa serikali ikikosa control ni jambo la hatari sana.
Wananchi watachukua hatua mikononi, wanaotaka Tanganyika watafanya hivyo, wasiotaka muungano watafanya hivyo.

Tension and sentiment zilizopo zitakuwa heighten na hapo si madole ya macho huenda ikawa mashoka vichwani(mungu pishilia mbali).
Huko ndiko tunakwenda na haitachukua miaka 3 kuanzia sasa hayo kutokea kama CCM watalazimisha muungano.
 
Katika hatua tuliyofikia sasa, mjadala unaounga mkono mfumo wa serikali mbili umetawaliwa na hoja za wanasiasa wachumia tumbo na wachumi "uchwara" wenye kupinga serikali tatu kwa hoja za gharama kwa walipa kodi lakini pia kwamba zanzibar haina uwezo wa kuchangia gharama za muungano kwa usawa na Tanganyika. Kwa upande wa serikali tatu, mjadala huu umetawaliwa na wanasiasa wanaotanguliza siasa safi, wachumi wanaojadili na kuchambua faidi za serikali tatu kwa muungano, nchi shiriki na wananchi kwa ujumla, lakini pia wapo wanaharakati. Kwa mazingira haya, tutarajie mjadala mkali ndani ya bunge la katiba vifungu juu ya muundo wa muungano vitakapofikiwa.

Hoja za wanasiasa wa serikali mbili tayari inaeleweka ni hoja zinazoweka mbele madaraka na nia ya kuendeleza control of the people badala ya control of the territory kwa wanasiasa wa CCM, hivyo kutokuwa na uchungu na Tanganyika ambayo ndio asili yao. Tukumbuke kwamba mataifa yaliyoendelea yanajali zaidi kudhibiti territory zake kuliko kuthibiti watu. Zama za mataifa kuthibiti watu zimepitwa na wakati. Tutajadili hili siku nyingine kwa undani zaidi. Kwa upande wa hoja za kiuchumi ambazo wana ccm wanaotetea serikali mbili hutumia, mbali ya hoja ya gharama ambayo ni dhaifu sana, pia wapo wanaojadili kwamba serikali tatu hazifai kwani zanzibar haina uwezo wa kuchangia sawa na bara/Tanganyika.

Profesa wa uchumi kutoka UDMS, humphrey moshi hivi majuzi alinukuliwa na vyomba vya habari akisema kwamba - tangia muuungano uanze mwaka 1964, zanzibar wamechangia mara tatu tu: 1964/5, gharama ya kuendesha muungano katika masuala yale yaliyokubaliwa chini ya mkataba wa muungano zilikuwa ni shillingi milioni 107.Kati ya hizi, znz ilichangia shillingi milioni 10, sawa na 9% ya gharama zote. Mwaka 1965/66, gharama za kuendesha muungano zilifikia sh. Milioni 153, na znz walichangia milioni 12, sawa na 8%; Mwaka wa mwisho kwa znz kuchangia kwa mujibu wa profesa mushi ilikuwa ni 1966/67, ambapo gharama zilikuwa ni milioni 176 huku znz wakichangia sh. Milioni 8.1, sawa na 5% ya gharaa zote za muungano. Kutokana na haya, profesa mushi na wengine wanajadili kwamba zanzibarr haitakuwa na uwezo wa kuchangia kwa usawa na Tanganyika chini ya serikali tatu.

Kuna ukweli katika hoja hii lakini wanachosahau aidha kwa bahati mbaya au makusudi watu wa upande huu wa hoja ni kwamba kuna two factors zilizochangia hali hiyo ya zanzibar ijitokeze:

1. Orodha ya muungano ilianza kuongezwa kinyume na mkataba wa muungano na bila ya kuishirikisha serikali ya znz katika maamuzi haya. Katika hali hii, zanzibar ikaanza kuona kwamba inalazimishwa kuendelea kuingia gharama kulipia mambo ambayo wao walitegemea kwamba yangekuwa yana gharamiwa na nchi shiriki peke yake. Kwa maana nyingine, nyongeza ya orodha ya muungano kwa zanzibar waliona ni mzigo na ni kinyume cha mkataba wa muungano.

2. Factor ya pili ni kwamba mara tu baada ya mkataba wa muungano kusainiwa, ilipitishwa sheria ya muungano ambayo nia yake ilikuwa ni kupunguza makali na relevance ya mkataba wa muungano. Moja ya sheria hizi zilipelekea zanzobar kupata kilema cha uchumi. Tukumbuke kwamba kipindi cha nyuma kabla ya muungano, znz ilikuwa na uchumi bora kuliko Tanganyika. Tutaangalia hili kwa undani baadae.

Kuna maswali muhimu ya kuyachambua:
1. Je, chini ya mfumo wa serikali tatu kuna ukweli kiasi gani kwamba znz haitaweza kuchangia katika masuala saba ya muungano kwa mujibu wa rasimu ya katiba? Nguruvi3 aliwahi kujadili hili, tunaomba utusaidie tena.

2. Je, kipi ni ukweli kati ya haya - znz haitakuwa na uwezo wa kifedha kuchangia muungano wa serikali tatu au ni kwamba tu znz hawataki kuchangia kwa sababu za kihistoria? (Rejea madhara ya nyongeza ya mambo ya muungano kwa znz).

Vinginevyo ima iwe znz hawana uwezo kiukweli au uwezo utakuwepo chini ya utaratibu ulioanishwa na rasimu lakini wanakwepa tu ukweli, hali hii ni sababu tosha ya kuvunja muungano kwani hatukuungana ili mshirika mmoja aje kumbeba mshirika mwingine, unless kufanya hivyo ilikuwa ni kwa lengo la kwenda serikali moja. Lakini hakuna ushahidi katika mkataba wa muungano kwamba kulikuwa na lengo la serikali moja. All that said and done, iwapo znz hawana uwezo (kiukweli au kwa visingizio), huu ni wakati muafaka kwa Tanganyika kuanza kujiendesha kivyake.

Muungano wa znz na tanganyika ulikuwa ni muungano wa hiyari, sio wa lazima, na hata mkataba wa muungano uliweka hilo wazi huku pakiwa na provision za nchi washirika kujitoa iwapo wataona muungano hauna faida. Ni katika mazingira haya, mwaka 1968 nyerere alitamka mbele ya mwandishi wa gazeti la observer la uingereza kwamba hatowapiga mabomu wazanzibari iwapo wataona muungano hauna faida kwao na kuongeza kwamba muungano ambao washirika hawautaki ni muungano usiokuwa na maana, ikiwa na maana kwamba hata Tanganyika nao wakiuchoka, solution si mabomu. Swali linalojirudia ni je:

*iwapo muungano ulikuwa ni wa hiyari, ikiwa mshirika mmoja wa muungano anashindwa kuchangia gharama za muungano, kwanini muungano huo uendelee kuwepo?

Vile vile:

*Mapinduzi ya zanzibar ya mwaka 1963/64 yalilenga nini kwa wazanzibari?

Ni dhahiri kwamba mapinduzi yalilenga wazanzibari kujipatia mamlaka kamili na itokanayo na wananchi wa znz, lakini muhimu zaidi - uhuru wa kujiendeshea mambo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Kwa maana nyingine, wazanzibari hawakufanya mapinduzi ili waje kuitegema Tanganyika kujiendesha kiuchumi (kisiasa inaonekana wanazidi kurudhika na mamlaka wanayopewa). Iwapo nipo sahihi, sasa hizi hoja kwamba zanzibar hawatakuwa na uwezo wa kuchangia muungano wa serikali tatu ni hoja za kina nani na zina ukweli gani na kwa maana hiyo huu muungano wa hiyari una maana gani kuwepo wakati moja hana uwezo wa kuchangia gharama za kuuendesha?

Hapo awali niliahidi kujadili kidogo sheria za muungano ambazo zilipitisha mara tu baada ya muungano kusainiwa 1964. Sheria hizi zilipitishwa bila ya kumshirikisha mshirika mwingine wa muungano (znz) kwani ni upande wa Tanganyika ndio ulikuja na sheria hizo na kuzipitisha kimya kimya tena wakati huo Serikali ya Tanganyika ikiwa bado ipo na ikifanya kazi zake kwa mujibu wa mkataba wa muungano. Hii ilikuwa ni katika kipindi cha mpito ambacho kwa mujibu wa mkataba wa muungano, kilikuwa ni cha mwaka mmoja tu ambapo rais wa JMT na wa Znz ambae alikuwa ni makamo katika kipindi cha mpito, wangeshirikiana kuteua tume ya katiba na baraza la kutunga katiba vyombo ambavyo vingesimamia mchakato wa katiba mpya ya JMT. Katika kipindi cha mpito, katiba ya Tanganyika (kwa mujibu wa mkataba wa muungano) ikafanyiwa marekebisho machache ili iweze kutumika kwa muungano, ile ya tanganyika (original) iendelee kutumika tanganyika huku znz wao pia wakifanyia kazi utaratibu wa katiba yao ya taifa shiriki la muungano, ikizingatiwa kwamba hawakuwa na katiba kwani mapinduzi ndio kwanza yalikuwa yamefanikiwa.

Baada ya muungano kutiwa tu saini na kuingiza taifa jipya katika kipindi cha mpito kuelekea katiba mpya kwa mujibu wa mkataba wa muungano (1964), matukio kadhaa yakajitokeza. Moja wapo ilikuwa ni ujio wa sheria za muungano za mwaka 1964, siku chache baada ya mkataba kutiwa saini, na hii ilikuwa kinyume kabisa na mkataba wa muungano, sheria ambazo zililenga kuufunika mkataba wa muungano usiwe na makali kuelekea katiba mpya ya JMT. Katika sheria hizi, ipo ile ya kifungu cha tisa cha sheria za mUungano (1964) ambacho kimsingi ndio sheria iliyoipa kilema cha kudumu uchumi zanzibar. sheria hii ilipitishwa kimya kimya bila ya kushirikisha serikali ya znz. Sheria hii (1/Mei/1964), siku tano baada ya kusainiwa muuungano inasema hivi:

Mali na Mikataba: Mali zote na haki juu ya mali za jamhuri ya muungano wa Tanganyika, na haki zote juu ya mali za jamhuri ya watu wa zanzibar zilizokuwa zinamilikiwa au kutumiwa au zilizomilikiwa au kutumiwa kimsingi kuhusiana na mambo ya muungano, zitakuwa kuanzia siku ya muungano, chini ya jamhuri ya muungano

Muhimu:
*Sheria hii ni moja ya sheria kadhaa zilizopitishwa kinyemela baada ya mkataba wa muungano kusainiwa, na kupitishwa kimya kimya, lengo ikiwa ni kuanza kuuzunguka mkataba wa muungano ili huko mbele iwe rahisi kuhalalisha uchakachuaji.
Kitendawili juu ya kwanini zanzibar iliacha kuchangia gharama za muungano 1967 kinaweza teguliwa na sheria hii, na hii ni mbali ya sababu za ongezeko la masuala ya muungano ambayo znz haikushirikishwa na haikuona ni haki kuyachangia wakati ingeweza yaendesha yenyewe. Ikumbukwe pia kwamba ni mwaka huohuo (1967)serikali ya Tanganyika ilizikwa rasmi kupitia sheria namba 24 ambayo ilizaa tanzania bara.

Ili zanzibar iwe na haki kuchangia sawa na Tanganyika chini ya mfumo wa serikali tatu, suala la assets za zanzibar zilizotaifishwa na Tanganyika kwa koti la muungano ni lazima litaibuka. Na tutake tusitake, ipo hoja ya kisheria katika hili, hasa iwapo mkataba wa muungano utakuwa ndio the legal foundation of the union.

Tutaiangalia sheria hii namba tisa ya mwaka 1964 kwa undani zaidi baadae.



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mchambuzi
Nichangie kidogo bandiko lako #67 lenye maswali kadhaa. Kabla ya hapo niweke sawa kauli ya waziri Wasira aliyotoa jana. Waziri anasema uwepo wa serikali 3 utaongeza gharama kwa Tanganyika kwasababu italipia shirikisho.

Upo ukweli kuwa Tanganyika italipia shirikisho pengine kwa kiasi kikubwa.
Kuna uongo wa kuongezeka gharama. Wasira hakueleza muungano uliopo nani anagharamia.

Swali la mchambizi, je zanzibar haitaki kulipa bill za muungano kwasababu haitaki tu kwasababu za kihistoria au hawana fedha.
Jibu: Znz haitaki tu kwasababu inatumia muungano vibaya. Prof humphrey ameeleza katika kitabu chake kuwa hakuna siku SMZ iliwahi kuulizwa kwanini haichangii muungano.
Znz imetumia kutishia kuvunja muungano na hilo wamelitumia kukwepa wajibu wa kuchangi.

Uwezo wa kuchangia wanao. Imedhihirika kuwa Znz ilikusanya kiasi cha dollar laki tano kutokana na usajili wa meli kupitia ZMO. Hakuna hata senti tano iliyokwenda muungano ili kuchangia ada za Tanzania kule IMO. Znz ilikuwa na uwezo hata wa kuchangia ikaamu kugoma kwavile kuulizwa watavunja muungano.

Mfano w pili, Znz wamekataa kuchangia tume ya Warioba kwa vile tu wakilazimishwa watavunja muungano. Baada ya tume kuja na mapendekezo, wajumbe wa BMLK kutoka Znz wanagharamiwa na SMZ. Uwezekano huo ulikuwepo endapo ingeamua kulipia wajumbe wa tume 15.

Inaendelea swali la pili.....
 
Inaendelea.....

Swali la kwanza , je kwa muundo wa serikali 3 ZNZ itashindwa kuchangia mambo 7 ya muungano kwa mujibu wa rasimu?

Jibu: Kwanza watu waelewe mfumo uliopo sasa kifedha umeelemewa na mwingilio wa mambo ya siasa.

Kwamba, kunatakiwa kuwe na balance inayoondoa fiscal responsibility kwa serikali ya muungano

Mfumo wa serikali 3 katika mambo 7 unaleta fiscal responsibility kwa washirika wa muungano.

Mathalani, mfumo uliopo unalazimu wabunge kutoka Znz katika bunge la JMT kuongoza watu 5,000-10,000 ili kupata idadi inayokusudiwa kisiasa na hulipwa kama mwingine mwenye uwakilishi wa watu Milioni 1.

Mfumo wa serikali 3 umeweka wazi bunge la shirikisho liwe na wabunge 75 ambao ni wachache kuliko wabunge wa WZN kwasasa wanaofikia 110 (wakiwemo wa kuteuliwa na makundi ya mama)

Bunge lenye wajumbe 320 la sasa litakuwa na wabunge 245(320-75). Tanganyika itaamua inataka bunge lenye ukubwa gani, na znz wataamua pia wanataka BLW lenye ukubwa gani kulingana na mapato ya kila mshirika. Hii maana yake gharama zitakuwa kwa wabunge 75 kwa kuchangia.

Pili, hadi sasa kuna wizara ya muungano na wizara zipatazo zote za muungano. Maana yake kuna wizara maalumu halafu zipo za mambo yote. Zanzibar ina wizara zote isipokuwa 2, mambo ya ndani, ulinzi na usalama. Mfano, wizara 2 za elimu, 2 za kilimo, 2 za afya n.k.
Gharama za kuziendesha ni kubwa mmno hasa kwa Tanganyika inayolipia bila kuchangiwa na znz

Kwa mfumo wa serikali 3, mambo 22 yamepunguzwa hadi 7.
1.Katiba
2.Uhamiaji na Uraia
3. Mambo ya nje
4.Ulinzi na usalama
5.Sarafu na Benki kuu
6.Usajili wa vyama
7.Ushuru wa bidhaa na mapato yasiyotokana na kodi

Ukiangalia kimantiki mambo hayo ni 4 tu yenye gharama baada ya kuondoa haya:
Ushuru wa bidhaa na mapato ni income.
Usajili wa vyama vya siasa gharama zake ni ndogo sana
Katiba (Taasisi na mamlaka) nayo ni ndogo kutokana na udogo wa serikali.

Mambo 4 yaliyobaki yenye gharama
Ulinzi na Uslama
Mambo ya nje
Uhamiaji na uraia
Sarafu na benki kuu

Haya 7 na hasa 4 yapo katika uwezo wa washirika. Hata kama hakuna muungano bado washirika watahitaji kuyagharamia, hayakwepi na ndivyo inatakiwa iwepo formula ya kuyagaharamikia.

Kila mshirika atashughulikia wizara, idara na taasisi zake mwenyewe kutokana na mapato ambayo hayapo katika mambo ya muungano.

Hii maana yake ni kuwa mzigo unaobebwa na Tanganyika wa mambo 22 na taasisi zisizo na idadi utapungua na kuwa 7 na basically 4.
Itakuwa ni wajibu wa kila mshirika kula urefu wa kamba yake.

Na kwavile ni kula kwa urefu wa kamba, fiscal responsibility itakuwepo tofauti na sasa ambapio vyeo na taasisi zinaundwa kuongeza gharama ili kukidhi haja za kisiasa na si kiuchumi.

Kuna sababu gani kuwa na wabunge 100 kutoka znz katika bunge la JMT? Kwanini BLW liwe na wajumbe 50? Jibu ni rahisi, ili kuleta uwiano wa kisiasa bila kuangalia gharama.

Katika shirikisho wale wabunge 100 wanaokuja Dodoma itabidi wakabanane znz kwa gharama zao wenyewe. Kwa Mtanganyika hilo limeondoa gharama kubwa sana inayobeba bila sababu.

Kama wapo watu wa kulilia serikali 3 basi ni Watanganyika kwasababu watakuwa wamepunguza gharama kubwa sana. Kwasasa wana mambo 22 ambao ni mzigo wao wenyewe.

Na kwa znz hii ni fursa ya kuunda vyombo vyao na kuvidhibiti bila kuingiliwa.
 
Serikali moja huru ama mbili huru ndiyo Suluhu ya matatizo yote hayo.

Watanzania tupewe fursa ya kuchagua kama tunataka muungano ama la...na kama tunataka muungao uwe wa serikali moja.

Nakuhakikishia wanaotaka serikali tatu ni ama wana uchu wa madaraka ama lengo lao wanataka kuvunja muungano kwa njia ndefu badala ya njia fupi. Serikali tatu haziendesheki. Kwa uchache angalia kizungumkuti cha vipengele hivi hapa https://www.jamiiforums.com/katiba-...atiba-vinachochea-kuvunjika-kwa-muungano.html

Mpaka sasa sijapata majibu ya kwa nini wale wanopenda muungano wa serikali tatu, nne au mbili, kwa nini hawataki serikali moja (tuwe ka Germany ilivyo sasa). Kama hatutaki moja basi tuwe kama Senegal na Gambia.
 
Serikali moja huru ama mbili huru ndiyo Suluhu ya matatizo yote hayo.

Watanzania tupewe fursa ya kuchagua kama tunataka muungano ama la...na kama tunataka muungao uwe wa serikali moja.

Nakuhakikishia wanaotaka serikali tatu ni ama wana uchu wa madaraka ama lengo lao wanataka kuvunja muungano kwa njia ndefu badala ya njia fupi. Serikali tatu haziendesheki. Kwa uchache angalia kizungumkuti cha vipengele hivi hapa
https://www.jamiiforums.com/katiba-mpya/614369-vipengele-vya-60-1-a-c-na-60-2-a-c-katika-rasimu-ya-katiba-vinachochea-kuvunjika-kwa-muungano.html

Mpaka sasa sijapata majibu ya kwa nini wale wanopenda muungano wa serikali tatu, nne au mbili, kwa nini hawataki serikali moja (tuwe ka Germany ilivyo sasa).
Kama hatutaki moja basi tuwe kama Senegal na Gambia.

Katiba ya mwaka 1977 ilikuwa ni preamble ya kuelekea serikali 1.
Kuanganisha vyama vya siasa ilikuwa ni hatua kuelekea serikali moja.

Mwaka 1984 Zanzibar ikaandika katiba yake ikikataa uwepo wa Tanzania viswani kwa mujibu wa katiba ya 1977.

Mwaka 2010 katiba ya znz ikafanyiwa marekebisho na kuifanya znz iwe nchi, rais wake, wimbo wa taifa, bendera na mamlaka ya rais kuigawa nchi akiwa na vyombo vya ulinzi vinavyooitwa vikosi maalum.

Katiba hiyo ikaifuta znz katika muungano isipokuwa kwa jina na baadhi ya mafao tu.

Hivyo serikali 1 haiwezekani, unless uniambie kuna mabomu na risasi za kuwalazimisha wznz kukana yote niliyoyaeleza halafu watu wakae chini kama taifa moja.

Tanganyika ilikubali na kupoteza utaifa ndani ya Tanzania kuelekea taifa moja.
Sasa imeachwa njia panda peke yake.

Serikali 3 ni option inayozuia kuvunjika muungano ambao tayari umeshavunjwa na znz.
Kosa la kwanza lilikuwa kutouliza wananchi, lilifanyika makusudi kuzia hicho kidogo kilichobaki.
1. Serikali 3 za mambo machache na kudumisha legacy ya muungano
2. Vunja jahazi tugawane mbao.

Kitu ambacho wengi hawakitambui ni kuwa znz wanataka kuwa na mamlaka kamili wakati huo huo wanasita kuwa wenyewe kwasababu wanazozijua na tunazozijua.
Vinginevyo mbona muungano wameshavunja siku nyingi sana!

Hivi kuna muungano gani wakati katiba ya znz ni zaidi ya katiba ya JMT?



 
....
Mwaka 1984 Zanzibar ikaandika katiba yake ikikataa uwepo wa Tanzania viswani kwa mujibu wa katiba ya 1977.

Mwaka 2010 katiba ya znz ikafanyiwa marekebisho na kuifanya znz iwe nchi, rais wake, wimbo wa taifa, bendera na mamlaka ya rais kuigawa nchi akiwa na vyombo vya ulinzi vinavyooitwa vikosi maalum.
........



Mkuu nashukuru sana kwa ufafanuzi wako huu. "Umenifumbua macho" juu ya maswala ya katiba ndiyo maana sasa nina kiri kuwa sina ujuzi wa kutosha kuhusu masuala ya katiba.

Ila kuna jambo ambalo naona umenionyesha hapa limenistua kidogo. Mwaka 1984, Baba wa taifa alikuwa bado ni Rais wa Jamhuriya muungano wa Tanzania. Wakati Zanzibar inapuuza matakwa ya katiba ya 1977 alikuwa bado yuko ikulu, akiwa na zana zote za kulinda Katiba. Mwaka 2010, rais Kikwete alikuwa bado yuko madarakani tena mapaka sasa. Zanzibar ikaendelea kupuuza katiba ya 1977 pamoja na marekebisho mengine ambayo ilikuwa imefanyiwa. Rais wa sasa bado ana zana zote za kulinda katiba hiyo ambalo ni jukumu muhimu sana kwa rais yeyote halali wa nchi.

Sasa je. Mosi, Mkuu, nitakuwa sahihi nikisema Baba wa Taifa alishidwa kulinda katiba isipuuzwe/isivunjwe na Watanzania visiwani akiwa madarakani, hivyo kuchochea vurugu za kutikisa muungano? Nitakuwa sahihi kumulaumu Baba wa Taifa kwa hili kwa kuiingiza JMT kwenye msukosuko wa kikatiba?

Pili, Mkuu nitakuwa sahihi, kusema Rais Kikwete naye ameshidwa kulinda katiba ya Tanzania ya 1977 pamoja na maboresho yake, mwaka 2010 akiwa madarakani kwa kuruhusu watanzania Visiwani kuendelea kuidhihaki katiba ya JMT ya 1977 kwa kukusudia/kuanzia nchi ndani ya nchi (watanziana visiwani hawa waliendeleza uhaini waliounzisha 1984)?Nitakuwa sahihi kumulaumu Rais Kikwete kwa hili kwa kuendelea kushabikia kuingiza JMT kwenye sukosuko wa kikatiba na kiutawala ulionzishwa na Baba wa Taifa 1984?

Tatu, Je. nitakuwa sahihi pia kuendelea kumlaumu Rais Kikwete, pamoja na kugundua tatizo la kushidwa kulinda katiba ya 1977, bado ametoa mwanya wa kutungwa katiba mpya ambayo haina mwelekeo wakuleta serikali moja kama Katiba ya JMT ya 1977 ilivyokuwa inakusudua?

Nakuuliza , mkuu, niko sahihi...!?
 
Mkuu nashukuru sana kwa ufafanuzi wako huu. "Umenifumbua macho" juu ya maswala ya katiba ndiyo maana sasa nina kiri kuwa sina ujuzi wa kutosha kuhusu masuala ya katiba.

Ila kuna jambo ambalo naona umenionyesha hapa limenistua kidogo. Mwaka 1984, Baba wa taifa alikuwa bado ni Rais wa Jamhuriya muungano wa Tanzania. Wakati Zanzibar inapuuza matakwa ya katiba ya 1977 alikuwa bado yuko ikulu, akiwa na zana zote za kulinda Katiba. Mwaka 2010, rais Kikwete alikuwa bado yuko madarakani tena mapaka sasa. Zanzibar ikaendelea kupuuza katiba ya 1977 pamoja na marekebisho mengine ambayo ilikuwa imefanyiwa. Rais wa sasa bado ana zana zote za kulinda katiba hiyo ambalo ni jukumu muhimu sana kwa rais yeyote halali wa nchi.

Sasa je. Mosi, Mkuu, nitakuwa sahihi nikisema Baba wa Taifa alishidwa kulinda katiba isipuuzwe/isivunjwe na Watanzania visiwani akiwa madarakani, hivyo kuchochea vurugu za kutikisa muungano? Nitakuwa sahihi kumulaumu Baba wa Taifa kwa hili kwa kuiingiza JMT kwenye msukosuko wa kikatiba?

Pili, Mkuu nitakuwa sahihi, kusema Rais Kikwete naye ameshidwa kulinda katiba ya Tanzania ya 1977 pamoja na maboresho yake, mwaka 2010 akiwa madarakani kwa kuruhusu watanzania Visiwani kuendelea kuidhihaki katiba ya JMT ya 1977 kwa kukusudia/kuanzia nchi ndani ya nchi (watanziana visiwani hawa waliendeleza uhaini waliounzisha 1984)?Nitakuwa sahihi kumulaumu Rais Kikwete kwa hili kwa kuendelea kushabikia kuingiza JMT kwenye sukosuko wa kikatiba na kiutawala ulionzishwa na Baba wa Taifa 1984?

Tatu, Je. nitakuwa sahihi pia kuendelea kumlaumu Rais Kikwete, pamoja na kugundua tatizo la kushidwa kulinda katiba ya 1977, bado ametoa mwanya wa kutungwa katiba mpya ambayo haina mwelekeo wakuleta serikali moja kama Katiba ya JMT ya 1977 ilivyokuwa inakusudua? Nakuuliza , mkuu, niko sahihi...!?
Kuna mambo mawili kuhusu Nyerere na muungano. Kwanza, Nyerere alisema haitakuwa vema Tanganyika kuimeza znz kwa kuelewa kuwa bado wznz walikuwa na post mapinduzi euphoria na hawakautaka kusikia jambo lingine. Nyerere inaonekana aliamini kuwenda mbele kizazi kitabadilika na kuona umuhimu wa Utanzania zaidi kuliko uzanzibar.
Moja kati ya jitihaza zake ilikuwa kuwachukua wznz waje kuishi nakufanya kazi bara hata kuwapa elimu ya bure.
95-98% ya viongozi wa znz wa sasa ni zao la muungano, wamesoma na wamefanya kazi Tanzania bara akiwemo Maalim Seif, Jusa n.k Swali linakuja kwanini kizazi kinaona muungano mbaya? Well ni pamoja na mambo mengi lakini madaraka ni moja ya kati ya hayo, na uduni wa ufahamu kwa sehemu ya jamii n.k.

Pili, Nyerere alizuia kuvunjwa muungano au alichochea? Jibu ni kuwa alizuia. Znz kuanzisha katiba ilikuwa ni kuijengea uwezo wa kuwa na taratibu za uendeshaji wa nchi. Tangia 1964 hadi 1984 znz ilikuwa inaongozwa na baraza la mapinduzi(BLM) ambalo halikuwa na katiba. Nyerere aliona hilo ni muhimu ili kuanza kujenga taasisi kwa ajili ya mawasiliano zaidi ya kuwa na genge la wababe 12 kwa jina la BLM.

Katiba ya 1984 haikusema znz ni nchi bali ilijitambulisha kama Zanzibar na taratibu kuondoa neno Tanzania. Bado ilivumilika kwasababu ya kulinda identity kama alivyowahi kusema 'Isemezwe'

Aboud Jumbe aliondolewa madarakani kwasababu za muungano. Hiyo ilikuwa jitihada za kulinda muungano.
Dr Salimin alijaribu naye akaitwa Dodoma na kuanzia hapo hadi leo kimya.

Mwaka 2010 Karume Amani ndiye alianzisha mabadiliko ya katiba. Mabadiliko hayo yakaifanya znz iwe nchi ikiwa na rais, serikali na kutoa mamlaka zaidi kama kugawa nchi, vikosi vya usalama maalum, bendera na wimbo wa taifa.
Kibaya zaidi katiba hiyo ikamuondolea rais wa JMT mamlaka kama rais wa nchi huku ikiifanya katiba ya znz kuwa juu ya JMT na kutoa uwezo kwa BLW kukubali au kukataa shauri lililopitishwa na bunge la JMT.

Kumbuka bunge la JMT lina wawakilishi kutoka znz wa makundi maatatu
1. Waliochaguliwa na wananchi
2/ Kutoka baraza la wawakilishi
3. Walioteuliwa na vyama vya siasa kutokana na uwiano wa matokeo ya kura.

Kwa pamoja ni wabunge takribani 100. Lakini jambo likifanywa na bunge la JMT ambalo lina uwakilishi wa znz bado linaweza kugomewa na BLW lenye watu 50 tu. Hapo ndipo muungano ulipovunjika ingawa wanasema bado.
Lini mtoto akawa mkuu wa nyumba na baba amsikilize kabla ya kutoa maamuzi?

Yote hayo yalifanyika wakati Kikwete yupo madarakani akaiongoza serikali na chama. Kwa vile ni mtu asiyetaka kuudhi watu aliona ni jambo dogo na litapita kama upepo. Leo anangalia nyuma na kutambua kuwa alichokifanya ilikuwa kuchochea kuni na sasa tuna option mbili tu
1. Serikali 3 ili kuendelea kuwa kishikizo cha muungano uliovunjwa tayari na znz
2. Kuvunja jahazi tugawane mbao na misumari.

Hivyo udhaifu wa JK umechangia sana katika kuamsha hisia hasa kwa Tanzania bara. Ndicho chanzo cha kujiuliza hivi inakuwaje muungano uvunjwe na ZNZ na bado tuwe taifa moja? Na je Tanganyika ipo wapi maana mshirika wake znz keshajitoa kiani ingawa ki jina na maandishi bado yupo.

Kwahiyo kuzinduka kwa Tanganyika ni matokeo ya kuachwa njia panda, kutengwa na kubaguliwa na kudharauliwa kwa muungano kiasi cha znz kuuvunja viongozi wakishuhudia na kudhani mabomu ya machozi ni suluhisho.

Historia itamwelezea vema sana JK kama watu watajutia siku moja. Kwa hapa tulipo ni 'tia maji tia maji' muungano upo mahututi sana.
 
Mkuu Mkandara
Labda unisaidie tena kuhusu serikali 2
Kwa maiaka 50 kero zimekuwepo, nini unadhani kinakosekana au kinahitaji kufanyika ili kuondoa hizo kero kwa sasa so that we can abadone the idea of Tanganyika.
Kwanza kabisa tunachotakiwa ni kuelewa hizo kero zimetokana na nini na sii kero zenyewe. Watu wana react kutokana na kero tu pasi kujua hizo kero chanzo chake nini..

Unajua muundo wa serikali yetu ya Muungano inazijumuisha nchi mbili hivyo kwanz ausiseme Zanzibar sio nchi kwa sababu tu Tanganyika sio nchi. Na hivyo kuna serikali ya Zanzibar inayosimamia mambo yao yasokuwa ya Muungano. Kisha tuna serikali ya Muungano ambayo Tanganyika na Zanzibar wamo, yaani wala huku na huku na wanachangia ktk mapato na matumizi japo kwa asilimia ndogo sana ukilinganisha na Bara.

Hivyo, kuwepo kwa kero za Muungano kumetokana na mambo matatu muhimu sana.
1. Kwanza ni Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, siasa hii ilipigwa vita na pande zote mbili japo Zanzbar waliichukulia kama siasa ya Nyerere na sio Karume. Utaifishaji wa mali na kadhalika ulileta mzozo mkubwa japo Zanzibar yenyewe ingekuwa nchi ya Kijamaa mbele yetu kutokana na Mapinduzi. Hii ni kati ya mwaka 1977 hadi 1984.

2. Ujio wa mageuzi ya kiuchumi (Economic liberalization) 1984, kulizua kero mpya na ndio kina Jumbe wakaibuka. Kumbuka kwamba ktk maswala ya serikali ya Muungano, Zanzibar kama nchi ina mkono wake ndani, lakini kwa jinsi tulivyoendesha serikali hii ilikuwa kama vile yale maswala yasokuwa ya Muungano, bara ama niseme Tanganyika isoonekana nayo ndio ilokuwa na mamlaka kamili, Zanzibar haihusiki japo wana wabunge na wawakilishi wake ilikuwa kama vile mama kabeba mimba.

Kilichofanyika ni kutengeneza safu ya Uongozi kuunda serikali ya Muungano kufurahisha na kupendezesha viongozi lakini yale maswala yasokuwa ya Muungano, bara bado ilikuwa na sauti kubwa kuliko Zanzibar maana yamo ktk serikali ya muungano. Mfano Elimu, inapofika ktk serikali ya JMT Zanzibar walitengwa kiana kwa sababu ipo ktkmaswala yasokuwa ya muungano japo wao pia mkono ndani ya serikali ya JMT.
Pili, wakasahau mageuzi ya uchumi sio swala la uongozi na siasa pekee bali ni swala la kiuchumi zaidi. Kilichotakiwa ni mfumo bora wa kimamlaka ktk ukusanyaji kodi, Uraia, mipango ya maendeleo (miundombinu) kwa Taifa zima.

Ndio yakazuka maswala ya OIC, uwekezaji na kadhalika yakawa na picha mbili zinazokinzana. Hili ni swala la serikali ya Zanzibar yenye mamlaka au ni swala la JMT. Viongozi wetu wakaonyesha sura zao, walovaa ngozi ya kondoo wakajitokeza na ikadhihirika kuwa hapa kuna Zanzibar na Tanganyika kwa maana ya kwamba serikali ya Muungano ilisimamia zaidi maslahi ya Tanganyika.

Usalama wa Taifa dhidi ya nani anaruhusiwa ku invest Zanzibar japo Investments zao hazikuwa ktk makubaliano. Mgao wa pato la taifa haukuwa na mfumo maalum zaidi ya kukatiana kishikaji kiasi kwamba Tanganyika imenufaika zaidi ktk mikopo na uwekezaji kwa kutumia jina la serikali ya Muungano. Hivyo, picha ikazidi kuharibika.

3. Mwaka 2010, ni siku ambayo Kiongozi wetu Mh. Pinda aliposema Zanzibar sio nchi ndipo alipoasha kero mpya juu ya zile zilizokuwepo. Na kama ulivyokwisha sema palipo na serikali kuna nchi, sasa iweje Zanzibar sio nchi ilihali wana serikali yao?. Kama Pinda angejibu kirahisi kabisa ya kwamba - Zanzibar ni nchi ndani ya JMT isingeleta taabu maana walichokuwa wakizungumzia Wazanzibar ni pale walipoona maswala yasokuwa ya Muungano yaliingizwa kinyemela ktk bunge la JMT na kuwanyima mamlaka kamili. Pinda kama waziri mkuu alitoa picha kuwa ni waziri mkuu anayeitazama serikali ya JMT kama nchi moja yenye serikali moja.

wakatokea kina Jussa walokuwa wakisubiri tu makosa haya yafanyike. wakautumia mwanya huio kuonyesha Wazanzibar hawana serikali na wala yale maswala yasokuwa ya Muungano hayapo mikononi mwao isipokuwa kwa idhini ya Tanganyika. ndipo walipofikiria kuunda umoja wao ambao ndio umetufikisha hapa tulipo. Kifupi hizo ammendments zilizofanywa ktk katiba ya Jamhuri pasipo ridhaa ya Wananchi haswa Wazanzibar ndizo sababu kubwa za mgogoro uliopo.

Mwisho kuwa na serikali 3 haiwezi kundoa kero hizo maana bado maswala ya JMT yatahusu nchi 2 zote, na nani mwenye mamlaka kamili haitajulikana! ama laa hiyo serikali ya 3 itakuwa na majukumu gani ikiwa hatukubaliani ktk hizi 2.
 
Mkuu Mkandara kabala sijadadavua badiko lako na kuonyesha wapi unajichanganya na wapi unapotosha ningependa kukuuliza tena swali hili ambalo hujalibu kama walsivyolijibu wanajamvi, Nape, Pinda, Wasira na wengine.

Swali: Kwa vile unapendelea mfumo wa serikali 2 uliodumu kwa miaka 50, na kwa vile kuna kero katika kipindi hicho cha miaka 50 zilizoundiwa tume, kamati n.k. bila, Je, unadhani nini kinahitajika kufanyika ili mfumo huo uendelee ambacho miaka 50 hakikufanyika?
 
Mkandara;8955954]Unajua muundo wa serikali yetu ya Muungano inazijumuisha nchi mbili hivyo kwanz ausiseme Zanzibar sio nchi kwa sababu tu Tanganyika sio nchi.
Sijasema hivyo, nilichosema znz wamejiondoa katika muungano kwa kuvunja taratibu na kanuni.

Nimeonyesha wapi wamevunja kanuni. Nikasema ni sehemu ya JMT kwa jina lakini kwa imani ambayo wznz wanayo wao siyo Watanzania na wala hawana sababu za kuchangia Tanzania. Nimeonyesha kwa takwimu za prof Humphrey.
Nikasema katiba yao inayokuwa juu ya katiba ya JMT ni ushahidi kuwa katiba ya JMT hawaitambui.
Na hivyo kuna serikali ya Zanzibar inayosimamia mambo yao yasokuwa ya Muungano. Kisha tuna serikali ya Muungano ambayo Tanganyika na Zanzibar wamo, yaani wala huku na huku na wanachangia ktk mapato na matumizi japo kwa asilimia ndogo sana ukilinganisha na Bara.
Kuna justification gani znz kula huku na huku?
Kwanini Tanganyika iwe ndani ya muungano na znz iwe mguunje mwingine ndani.
Pili, tumekubaliana kwa bandiko lako kuwa ni nchi mbili Tanganyika na znz.
Hilo ukumbuke.
2. Ujio wa mageuzi ya kiuchumi (Economic liberalization) 1984, kulizua kero mpya na ndio kina Jumbe wakaibuka. Kumbuka kwamba ktk maswala ya serikali ya Muungano, Zanzibar kama nchi ina mkono wake ndani, lakini kwa jinsi tulivyoendesha serikali hii ilikuwa kama vile yale maswala yasokuwa ya Muungano, bara ama niseme Tanganyika isoonekana nayo ndio ilokuwa na mamlaka kamili, Zanzibar haihusiki japo wana wabunge na wawakilishi wake ilikuwa kama vile mama kabeba mimba
Kumbuka mambo yasiyo ya muungano yaliongezeka kutoka 11 hadi 22.
Nitajie moja tu ambalo unadhani Tanganyika ilinufaika nalo kwa kuiminya Zanzibar.
Kilichofanyika ni kutengeneza safu ya Uongozi kuunda serikali ya Muungano kufurahisha na kupendezesha viongozi lakini yale maswala yasokuwa ya Muungano, bara bado ilikuwa na sauti kubwa kuliko Zanzibar maana yamo ktk serikali ya muungano.
Umesema yasiyo ya muungano, hivyo bara ina uhalali wa kuyashughulikia kwasababu si ya muungano.

Kumbuka huko nyuma umetoa uhalali wa znz kuwa sehemu mbili, znz na muungano. Uhalali huo haupo kwa Tanganyika, je yale yasiyo ya muungano Tanganyika ingeyapeleka wapi?
Mfano Elimu, inapofika ktk serikali ya JMT Zanzibar walitengwa kiana kwa sababu ipo ktkmaswala yasokuwa ya muungano japo wao pia mkono ndani ya serikali ya JMT.
Mkuu Mkandara unaongozwa kwa hisia sana zaidi ya ukweli.
Unaongozwa na prejudice badala ya ukweli.

Kwanza kabisa kumbuka elimu si suala la muungano, halipo katika yale 11. Limeongezwa kinyemela kama unavyodai.

Umesahau kuwa nyuma umelalamika mambo yasiyo ya muungano kuingizwa katika muungano. Hapa unakuja na hoja kuwa jambo lile ulilosema ni haramu wznz walinyimwa. Walinyimwa vipi haramu?
Mkuu huoni unavyojichanganya hapa! mkuu!

Pili, Zanzibar ina wizara ya elimu kwa wazanzibar.
Kutoka katika muungano, znz imepokea msaada wa elimu.

Kwa mfano kuna nafasi za upendeleo kwa wznz bila kujali ufaulu katika vyuo vya chini, kati na juu. Kwamba sifa ni kuwa mznz siyo paper waliyofanya. Hilo limewanyima Watanganyika fursa nyingi kwasababu wao wanashindana kwa nafasi.
Chuko kikuu ni mfano mzuri.

Wafanyakazi karibu asilimia 96-98 wa SMZ na viongozi wao wamesoma na kufanya kazi Tanganyika.

Katika elimu ya juu mwaka 2012 wznz 1000 walipewa zawadi za elimu wakati wenzao wa Tanganyika ambao baba zao ndio walipa kodi kwa jambo lisilo la muungano wamepewa mikopo ya kurudisha na wengi kunyimwa kwasababu hawana div II. Kwa mzanzibar yeye anapaa tu kwasababu ni mznz baasi.

Mwaka jana wizara ya elimu ya juu imetoa bilioni 5 kwa SMZ kwa ajili ya elimu ya juu. Elimu ya juu siyo suala la muungano, lakini Mkandara na wznz wanapotaka mafao basi haramu wanaisomea dua haraka inakuwa halali hapo hapo.

Huwezi kulaani jambo kuingizwa kinyemela halafu ukaligeuza kuwa haki mbele ya safari. Mkuu kuna hisia hapa naomba zisikuongoze bali ukweli ukuongoze
Ndio yakazuka maswala ya OIC, uwekezaji na kadhalika yakawa na picha mbili zinazokinzana. Hili ni swala la serikali ya Zanzibar yenye mamlaka au ni swala la JMT. Viongozi wetu wakaonyesha sura zao, walovaa ngozi ya kondoo wakajitokeza na ikadhihirika kuwa hapa kuna Zanzibar na Tanganyika kwa maana ya kwamba serikali ya Muungano ilisimamia zaidi maslahi ya Tanganyika.
Kumbuka mambo ya nje kwa mujibu wa mkataba ni suala la muungano.
Usalama wa Taifa dhidi ya nani anaruhusiwa ku invest Zanzibar japo Investments zao hazikuwa ktk makubaliano. Mgao wa pato la taifa haukuwa na mfumo maalum zaidi ya kukatiana kishikaji kiasi kwamba Tanganyika imenufaika
Unaongelea mgao kwasababu ni mafao, huongelei ukweli kuwa tangu mwaka 1967 znz haijachangia chochote katika muungano.

Mgao wao wanapata na ni 4% ya pato la taifa. Tuonyeshe kwa namba na asilimi mchango wao katika pato hilo ni kiasi gani.Hivyo suala si mgao, suala ni mgao na kuchangia, huwezi kutenganisha vitu hivyo.
3. Mwaka 2010, ni siku ambayo Kiongozi wetu Mh. Pinda aliposema Zanzibar sio nchi ndipo alipoasha kero mpya juu ya zile zilizokuwepo. Na kama ulivyokwisha sema palipo na serikali kuna nchi, sasa iweje Zanzibar sio nchi ilihali wana serikali yao?. Kama Pinda angejibu kirahisi kabisa ya kwamba - Zanzibar ni nchi ndani ya JMT isingeleta taabu maana walichokuwa wakizungumzia Wazanzibar ni pale walipoona maswala yasokuwa ya Muungano yaliingizwa kinyemela ktk bunge la JMT na kuwanyima mamlaka kamili. Pinda kama waziri mkuu alitoa picha kuwa ni waziri mkuu anayeitazama serikali ya JMT kama nchi moja yenye serikali moja.
Mkandara, kama suala si la muungano linawakeraje likiingizwa katika bunge la JMT.
Na kwavile Tanganyika haipo ulitarajia masuala yasiyo ya muungano yapelekwe wapi?
Akina Jusa wakautumia mwanya huio kuonyesha Wazanzibar hawana serikali na wala yale maswala yasokuwa ya Muungano hayapo mikononi mwao isipokuwa kwa idhini ya Tanganyika. ndipo walipofikiria kuunda umoja wao ambao ndio umetufikisha hapa tulipo. Kifupi hizo ammendments zilizofanywa ktk katiba ya Jamhuri pasipo ridhaa ya Wananchi haswa Wazanzibar ndizo sababu kubwa za mgogoro uliopo.
Again suala si la muungano akina Jusa walitaka liwe mikoni mwao kwa vipi.
Na hayo yasiyo ya muungano yangepelekwa wapi wakati Tanganyika haipo
Mwisho kuwa na serikali 3 haiwezi kundoa kero hizo maana bado maswala ya JMT yatahusu nchi 2 zote, na nani mwenye mamlaka kamili haitajulikana! ama laa hiyo serikali ya 3 itakuwa na majukumu gani ikiwa hatukubaliani ktk hizi 2.
Kwa maelezo yako hapo juu serikali 3 zitaondoa kero.
Zitasaidia yale yasiyo ya muungano yasishughulikiwe na akina Jusa na wenzao.
Ya Tanganyika yabaki huko na znz yabaki huko.

Kuhusu mikopo, hilo ndilo linawasumbua wznz na Mkandara.
Huko nyuma nimeeleza kuwa kuangalia mikopo ni rahisi sana, je unaangalia ulinzi na usalama, mambo ya nje, mambo ya ndani na faida ambazo znz inazipata ambazo huziweki katika monetary values?

Mkuu unapokuwa na prejudice au pre conceived notion una compromise sana hoja.
I believe Mkandara I know and respect will not be driven by other motives rather than facts on the table.

Ukisoma ulichoandika, hakika unatetea serikali 3 zaidi kukiko kuponda.
Unaposema mambo yasiyo ya muungano, kwa ufupi unasema kuwepo na mstari wa mambo ya Tanganyika na mambo ya znz halafu mambo ya pamoja.

Hapo unataka serikali 3 bila ubishi, kwa hoja zako na mantiki unless useme wakati unaandika ulighafilikiwa.

Ni kwa msingi huo ndiyo maana tunataka serikali ya Tanganyika izinduke ili yasiyo ya muungano ambayo sasa ni 7 na practically ni 5 yabaki hivyo.
Kama hilo litashindikana tuvunje jahazi tugawane mbao.

Hatuwezi kuitwa Tanzania halafu tukalaumiwa kwanini ni Tanganyika wakati hakuna Tanganyika.Hatuwezi kuwa na ndumila kuwili znz na Tanzania, ni lazima mstari uchorwe
 
Mkuu Mkandara kabala sijadadavua badiko lako na kuonyesha wapi unajichanganya na wapi unapotosha ningependa kukuuliza tena swali hili ambalo hujalibu kama walsivyolijibu wanajamvi, Nape, Pinda, Wasira na wengine.

Swali: Kwa vile unapendelea mfumo wa serikali 2 uliodumu kwa miaka 50, na kwa vile kuna kero katika kipindi hicho cha miaka 50 zilizoundiwa tume, kamati n.k. bila, Je, unadhani nini kinahitajika kufanyika ili mfumo huo uendelee ambacho miaka 50 hakikufanyika?
Mkuu wangu mimi nitakujibu ninavyofikiria mimi na sii lazima iwe hivyo. Chukua muda vizuri unisome japo nimejaribu sana kuchukua tu yale yalokuwa yakijitokeza ktk kero za Muungano na haswa kutoka upande wa pili.

Swala zima la kero zetu zimekuwepo toka tupate Uhuru. Kulikuwa na kero za Mapinduzi tukaunda Muungano, kero za siasa ya Ujamaa na Kujitegemea kuingia Ubepari kero za chama tawala tukaingia domkrasia, kero za maisadi, kero za Udini na kadhalika. Kifupi hizi kero hazitakwisha. Kerp haziwezi kuondoka pasipo kuwa na mfumo bora unaolingana na WATU na MAZINGIRA. Hata hiyo Marekani yenyewe kuna kero hadi kesho lazkini za Kisiasa na sio katiba ya nchi yao wala Muungano wao na ndio maana wanafanya tu amendments ktk sheria za katiba yao kuondoa kero. Kero hazisababishi kutunga katiba bali kero hufanyiwa marekebisho pale asheria inapowakwaza.

Nini kinahitajika Kufanyika!

Swala la Ujamaa na kujitegemea sii kero tena, isipokuwa kero bado ni ktk mfumo mzima wa Serikali ya Muungano ambapo Bara tumeutumia Muungano wetu kwa kujinufaisha bara zaidi. Elewa wizara zote zilizopo ktk serikali ya Muungano Zanzibar wamo pia ila kuna wabara wanafikiria kuwa yale yasokuwa na Muungano kwa zanzibar basi na bara pia sii ya Muungano. hapana hakuna seikali ya bara ila ya Muungano ambayo wizara zote za serikali ya Muungano zinawahusu pia Zanzibar.

Miundombinu mipya na mipango mingi ya maendelo inaelekezwa bara japo hii ni serikali ya Muungano. huu ndio ukweli. Hizi habari za kuwapeleka Umeme Zanzibar kutoka bara ni sawa na kuwagawia samaki badala ya kuwawezesha wenyewe kuzalisha umeme. Na wala huu sio msaada kwa sababu uwekezaji ktk umeme nchini ni swala la Muungano sio la bara wala hakuna serikali ya bara. lakini je hujasikia wabara wakisema tunawapa umeme bure? unawapa vipi ikiwa wao ni sehemu ya Muungano? tusilalamikie serikali kutumia umeme bure kwa mawaziri na maofisi yake lakini wepesi kunyoosha kidoe Zanzibar.

Kuna sehemu nimeeleza vizuri tu kuhusu nini tufanye kuondoa hasa kero za Muungano. Kama ningelikuwa rais wa Jamhuri, ningeifanya Zanzibar kuwa freeport na kujenga bandari kubwa ya mizigo ili kutoa service kwa nchi za Kiafrika kama Dubai au Hongkong. UAE na China bara zimefaidika sana kutokana na kuwepo kwa bandari hizo, na kuwepo kwa banmdari Znz hakutazuia bara kutoza ushuru kwa mizigo yote inayopitia hapo ama kushukia bara. Hivyo, badala ya kutoza ushuru mkubwa tungeweka ushuru mdogo maana mali nyingi ingepatikana Znz na hakuna sababu ya wafanyabiashara wa nchi za kiafrika kusafiri hadi China au Dubai, tena kulenga Mataifa jirani wataokuja kutumia port ya Zanzibar. Dar es salaam ni mji mkuu unahitaji kupumua na kupanuka.

Pili, makao makuu ya Utalii na mikutano ya kimataifa ningeihamishia Zanzibar kutokana nafasi yake ktk Utalii, Mahotel mengi yangejengwa zaidi na beach zake kuboreshwa zaidi. Mipango ya wizara ya AFYA na ELIMU ningeiweka ktk serikali ya Muungano na sii mambo yasokuwa ya Muungano hivyo serikali ya Muungano inachukua jukumu moja kwa moja kuwatihani na kutoa nafasi za masomo ya juu kwa wanafunzi wote wa JMT pia huduma za Afya kwa kujenga Hospital kubwa ya kimataifa Znz.

Swala la OIC ningelipa ruksa, ila ningeliweka la Kitaifa hivyo wawekezaji wangetoa huduma zao kama ilivyokuwa AghaKhan enzi za mwalimu. Viongozi wa bara wameogopa OIC kwa sababu tu ya matumizi ya jina na dini inayohusika wakati Aghakhan alotumia jina lake japo ni shirika la kidini na kwa malengo yale yale hakutiliwa shaka, yapo mashirika mangapi ya kidini ambayo tumeyapa ruksa lakini hili maadam limeombwa a serikali ya Zanzibar na kwa Waislaam imekuwa shida.

Hivyo Tukiweza kuondokana na shuku hizi, tukaaminiana ktk imani zetu na tukashikamana Muungano wetu wa serikali 2 hauna dosari zaidi kama yalivyokuwa mashirika ya Umma. Leo hii Elimu na Afya ipo chini ya muafaka baina ya serikali na dini ya Kikristu (MUO), wakilalamika waislaam mnasema na nyie jengeni zenu lakini sio kupitia OIC.. unafikiri Wazanzibar wanalichukulia vipi swala hili?

Ni mfano tu, Ikiwa shirika la sukari lilikuwa likizalisha asilimia 30 ya uwezo wake, kisha wananchi wakakosa sukari a wakaanza kupanga mstari ilikuwa busara gani kuuza kiwanda kwa mtu ambaye atachukua spareparts za kiwanda hicho na kukihamishia nje? Hivi kweli unauza kiwanda kizima kwa maksa ya watu waloshindwa kuzalisha kulingana na uwezo wa kiwanda? mwenye kosa nani haswa hapa tujiuliza!

Kwa hiyo mkuu wangu serikali 3, ni fikra za kimasikini. yaani sisi wepesi sana kugawana umaskini badala ya kuunganisha nguvu. Ni mila na Utamaduni wa mtu mweusi hataki bughudha, Na ndio maana ktk Urithi mzee akifa tu familia wanakimbilia kugawana mali au nyumba. wakati wenzetu Ulaya na mataifa mengine hujumuisha nguvu zao nyuma ya shirika na kugawana ubia. Mashirika mengi tu utaona yameanzishwa toka miaka 100 hadi 200 iliyopita, sisi hatuna hata miaka 50 watu tayari wanataka kugawana umaskini. Hatuna mfano hata mmoja wa kitu kama Mc Donald, sisi ni kugawana tu umaskini wakati wenzetu mali ya mzazi huendelezwa na familia nzima kila mtu akichukua share yake ya tokana na faida (dividend).

Ni kutokana na umaskini huo na fikra hizo za kimaskini ndio maana tunaona kila sababu ya kuunda serikali 3 ili kila mmoja abebe mzigo wake, tusijuane kama tunavyogawana mali za urithi. Na tisa ktk 10, huanguka wote wakarudi kuishi maisha ya chini kabisa. Urithi umepotea na mali imepotea ndivyo navyotarajia hatma ya Muungano ktk serikali 3.
 
Mkandara;8958464 :Mkuu Mkandara unajaribu kukwepa swali la msingi kwa ku insinuate mambo mengi kutuchanganya. Unatuunga mkono zaidi kwa serikali 3 kuliko unavyodai serikali 2.

Miaka 50 kero hazina jibu, ni jambo la kushangaza kufanya kitu kile kile kila siku bila mtokeo mazuri na ukaendelea tu.Huna justifications za kwanini unataka serikali 2 bali mazoea tu
Swala zima la kero zetu zimekuwepo toka tupate Uhuru.Swala ni mfumo mzima wa Serikali ya Muungano ambapo Bara tumeutumia Muungano wetu kwa kujinufaisha.
Wizara zote zilizopo ktk serikali ya Muungano Zanzibar wamo pia ila kuna wabara wanafikiria kuwa yale yasokuwa na Muungano kwa zanzibar basi na bara pia sii ya Muungano.
hapana hakuna seikali ya bara ila ya Muungano ambayo zinawahusu pia Zanzibar
Mkuu, nimekuuliza hili swali umechenga lakini unalirUdia rudia.

Hivi mambo ya
wizara zote za serikali ya Muungano yasiyo ya muungano ni yapi hayo kwa sasa? Na hayo yasiyo ya muungano yashughulikiwe na serikali gani?
Hayo mambo ya bara ni ya nchi gani? Kuna tatizo gani kwa mtu wa bara kudhani kuwa yasiyo ya muungano ni ya muungano pia? Kumbuka hakuna serikali ya bara wala Tanganyika, hiyo ya muungano itawezaje kufanya mambo kwa kuchambua yasiyo ya bara na muungano?

Halafu unajichanganya unaposema kila wizara znz ina mkono!
Ni Mkandara huyu aliyesema znz inaonewa kwa kuingiza mambo yasiyo ya muungano kinyemela katika serikali ya muungano. Where do you stand my friend Mkandara. Kuingiza mambo kinyemela au kutoa huduma sawa kwa mambo yaliyoingizwa kinyemela.

Na kwa hoja zako unataka kutueleza kitu kimoja, kuwepo na serikali itayaoshughulikia mambo ya muungano, Serikali itakayojihusisha na mambo yasiyo ya muungano kwa Tanganyika na SMZ.
Kwa maana ya serikali 3. Vinginevyo huwezi kutenga mambo ya muungano kwa upande wa bara ukayaacha hewani. Nani atashughulikia?

Kuhusu kujinufaisha, nimekueleza huko nyuma kuwa mambo 22 yote yaliyopo hakuna hata moja, na nikaomba unipe mfano mmoja tu wa jambo linalowanufaisha Watanganyika! Huna jibu.

Tume ya Warioba imepunguza hadi 7. Katika 15 yaliyoondolewa nitajie moja tu lililoathiri Tanganyika. Kama hakuna Tanganyika inanufaika na nini?

Pili, nimekuuliza zile huduma ambazo haziwekwi katika monetary values kama free access ya soko la watu milioni 40, Land, manpower, trade and industries unazi quantify vipi katika kuonyesha znz inaonewa?

Ni hoja laini kusema Tanganyika inafaidika na mikopo wakati Tanganyika inatoa mishahara isiyo mikopo au na riba kwa SMZ.
Dr Salmin, Amani Karume, Basil Mramba, Prof Mbilinyi wana ushahidi usio na shaka.
Miundombinu mipya na mipango mingi ya maendelo inaelekezwa bara japo hii ni serikali ya Muungano. huu ndio ukweli.

Hizi habari za kuwapeleka Umeme Zanzibar kutoka bara ni sawa na kuwagawia samaki badala ya kuwawezesha wenyewe kuzalisha umeme.Wala sio msaada kwa sababu uwekezaji ktk umeme nchini ni swala la Muungano sio la bara wala hakuna serikali ya bara.

lakini je hujasikia wabara wakisema tunawapa umeme bure?
unawapa vipi ikiwa wao ni sehemu ya Muungano?
Hapa unatusaidia kuwa iwepo serikali ya Tanganyika itakayoshughulikia mambo ya Tanganyika tu ili kutoinyonya Zanzibar.

Kama unakubali hakuna serikali ya bara, hii bara inaserikali gani?
Huoni hapa ni changu changu, chako changu. Nani anaumia yule mnayetumia vitu pamoja au yule anayejihudumia na wakati huo anatumia chako.

Suala la umeme historia yake inatokana na vyanzo. Miaka ya nyuma umeme wa mafuta ulikula sana bajeti si znz hata bara.

Ujenzi wa mabwawa ulipunguza gharama. Njia ya kupunguza gharama visiwani ilikuwa kupeleka umeme.Ndivyo Wapemba walivyopelekewa mwaka jana.

Ni ukweli usio na ubishi kuwa umeme wa disel turbine ni ghali kuliko wa maji. SMZ haijafadika?
Uwekezaji unaousema ni kuwatafutia vyanzo vya maporomoko.

Hilo nalo unataka liwe tatizo lililosababishwa na muungano! kwamba Tanganyika imejigawia vyanzo vya umeme na kuipunja znz, same sentiment ya wznz. Kwamba mtoto akifeli shule kaonewa hata kama IQ ni ndogo, eti kisa ni mzanzibar. Samaki hawapatikani kutokana na upepo wa kusi sababu kubwa ni muungano.

Wznz wana mpango wa umeme upepo kwa kusaidiwa na Muungano. Unataka msaada upi tena?

Kuhusu umeme wa bure hilo halina ubishi, wanapewa umeme wa bure.
Hivi unajua wnz hawajui mita za umeme hadi walipoondoa Tanesco na kuanzisha Zesco?

Zesco inakusanya pesa,2012 imekusanya bilioni 20. Badala ya kulipa Tanesco zimeliwa na wazanzibar viongozi. Tanesco inakufa, mtu wa kidatu na Pangani falls analipa zaidi kwasababu tu mzanzibar halipi.

Hivi mkuu hapa unataka kuwaambia nini Watanganyika. Kwamba mtu wa Dar es Salaam alipe umeme wake kisha alipe ziada ya mzanzibar ! please.

Jeuri ya wznz kutotaka muungano, wakakimbilia kuanzisha Zesco unilaterally.
Umeme ulipokufa fumbuni iliwachukua miezi 3 kurudisha kwa kukosa bilioni 5 za kununua kifaa Norway.

Nahodha akaja kuomba serikali ya muungano wakapewa.
Hawa ni wale wale waliokuwa na jeuri ya kusema umeme ni wao.

Ulafi na ubinafsi wao wenyewe kula pesa zao, halafu wanakimbilia hazina kwasababu limekuwa jambo la muungano. Tanesco ina element za muungano, Zesco ina element za kiburi na jeuri ya hovyo! mradi wa wakubwa, madhara anatupiwa Mtanganyika.

Tunaendelea kujibu hoja.......
 
Last edited by a moderator:
Inaendelea kujibu hoja za Mkandara

Mkandara: Kama ningelikuwa rais wa Jamhuri, ningeifanya Zanzibar kuwa freeport na kujenga bandari kubwa ya mizigo ili kutoa service kwa nchi za Kiafrika kama Dubai au Hongkong


UAE na China bara zimefaidika sana kutokana na kuwepo kwa bandari hizo, na kuwepo kwa banmdari Znz hakutazuia bara kutoza ushuru kwa mizigo yote inayopitia hapo ama kushukia bara.

Badala ya kutoza ushuru mkubwa tungeweka ushuru mdogo maana mali nyingi ingepatikana Znz na hakuna sababu ya wafanyabiashara wa nchi za kiafrika kusafiri hadi China au Dubai, tena kulenga Mataifa jirani wataokuja kutumia port ya Zanzibar. Dar es salaam ni mji mkuu unahitaji kupumua na kupanuka
Mkuu Mkandara, dunia ya sasa ni ya soko huria.
Kusafiri ni jambo la lazima na kawaida sana.

Watanganyika wameamka, kitendo cha kuwaambia wasitafute masoko ya dunia wasubiri mali zije Zanzibar ni kuwadhalilisha.

Kwa mentality hiyo tumeshindwa na Wakenya kwasababu tulikuwa hatujafunguka.
Siku hizi watu wanachacharika hakuna cha kusbiri Mpemba alete bidhaa.

Wachaga walitoka makwao siku nyingi ndio maana leo wapo mbele.
Usishauri vijana wacheze bao badala ya kutafuta duniani. Ushauri mbaya sana huu.

Kilichoua bandari ya Tanga ni kifo cha mkonge. Meli zilizokuja kuchukua mkonge zilileta bidhaa nyingine. Treni zilikuwa zinapisha majani mapana, Pongwe, Muheza, Mnyuzi, Korogwe, Dar hadi Arusha kila baada ya nusu saa. Sasa hivi hali ni mbaya.

Bandari ya znz imekufa kwasababu biashara ya karafuu na zile haramu za utumwa zimekufa. Mombasa na Beira zinachanja mbuga. Eti tuache kuendeleza bandari za Tanga na Mtwara kwasababu tunatakiwa tuwaachie nafasi Raia bora sana wa Zanzibar. Ney!

Mwambani kunajengwa bandari ambayo itakuwa huru. Mtwara itaibuka kutokana na gesi na ndivyo ya Bagamoyo itakavyokuwa.
Hilo ni suala la maendeleo na halipaswi kuzuai sisi kutumia fursa kwa kuwaendekeza wzn.

Unasahau bandari ni moja kati ya mambo 11 ya mkataba wa mwaka 1964.
Wznz wakliondoa bila mashauriano kwa kuifanya bandari huru.
Watanganyika hawakulalamika, leo eti tuwe na huruma na viburi vyao. Hilo halipo sasa hivi, kila mtu ale kwa jeuri yake. Tanganyika kwanza!

Mkandara, bandari inaangukia katika suala la usalama wa nchi.
Wenzetu hawalioni hilo kwasababu ya ubinafasi. Kuna haja ya kufanya bandari ya Dar huru ili Mtanganyika afadike kama mznz anavyofaidika na bandari huru sasa.

Hatuwezi kuendekeza upuuzi kwasababu tu kuna watu waliojitoa ufahamu.
Bandari ya mwambani ni lazima, Tanga irudi mahali pake.
Huwaoni huruma ndugu zangu wabondei na wazigua, unafikiria znz, kulikoni?

Kuruhusu wznz wawe na bandari huru eti wakusanye ushuru sisi tuwe wateja ni wazo baya mkuu.
Pili, makao makuu ya Utalii na mikutano ya kimataifa ningeihamishia Zanzibar kutokana nafasi yake ktk Utalii, Mahotel mengi yangejengwa zaidi na beach zake kuboreshwa zaidi.

Mipango ya wizara ya AFYA na ELIMU ningeiweka ktk serikali ya Muungano na sii mambo yasokuwa ya Muungano hivyo serikali ya Muungano inachukua jukumu moja kwa moja kuwatihani na kutoa nafasi za masomo ya juu kwa wanafunzi wote wa JMT pia huduma za Afya kwa kujenga Hospital kubwa ya kimataifa Znz.
Utalii wznz walikimbilia kuondoa katika mambo ya muungano wakisema ndicho chanzo chao kikuu cha mapato na hivyo wanataka wakihudumie bila kuingiliwa.

Leo Mkandara anawalaumu Watanganyika kwa maamuzi ya wazanzibar yaliyoongozwa na chuki na ubinafsi.

Kujenga moheteli huko maana yake ni mtu wa Arusha afe njaa kwasababu kuna RAIA bora sana wa wznz wanaotakiwa kuhudumiwa kila kitu.

Hii ni dunia ya ushindani, hatuwezi kuacha kujenga Tanganyika kwa kuendekeza wznz ambao kwao sisi ni adui namba moja wa ukanda huu.
Hakuna aliyewazuia wasijenge hoteli tena wanauza beach kwa Wataliano nani kalalamika kwa hilo.

Mkuu Elimu ni suala la muungano hadi sasa. Takwimu zipo na zina ushahidi wa upendeleo kwa wznz.Wznz wamekimbilia kuondoa baraza la mithani kwasababu si jambo la muungano.
Mkandara anawalaumu Watanganyika kwa maamuzi ya jazaba, jeuri na kiburi

Afya ni suala la muungano, waziri na maafisa wa wizara hiyo ni wazaznibar. Hilo si jambo la muungano ni moja kati ya yale yaliongezwa kinyemela ambayo Mkandara sasa ameshayasomea dua na ni matakatifu kutumiwa na wznz kwasababu tu yana manufaa kwao.

Mkandara hajasema neno kuhusu mafuta na gesi. Tetesi zilipotokea tu wakakimbia BLW kuondoa mambo si ya muungano. Wakati wanaongozwa na ubinfasi habari za gesi zikaingia Tanganyika, kiburi hakuna tena.

Mkandara angekuwa fair kwa kuwalaani wznz kwanza kwani wao wanataka tugawane umasikini, utajiri wao ni wao si wetu. Hii dhana inafika mwisho, Tanganyika inakuja kwa udi na uvumba

Itaendelea kujibu hoja za mwisho za Mkandara....
 
Mkandara: Swala la OIC ningelipa ruksa, ila ningeliweka la Kitaifa hivyo wawekezaji wangetoa huduma zao kama ilivyokuwa AghaKhan enzi za mwalimu.

Viongozi wa bara wameogopa OIC kwa sababu tu ya matumizi ya jina na dini inayohusika wakati Aghakhan alotumia jina lake japo ni shirika la kidini na kwa malengo yale yale hakutiliwa shaka, yapo mashirika mangapi ya kidini ambayo tumeyapa ruksa lakini hili maadam limeombwa a serikali ya Zanzibar na kwa Waislaam imekuwa shida
Mkuu Mkandara, kuhalalisha uvunjaji wa katiba ndio umetufikisha hapa, na bado huonekani kuliona hilo hata kidogo.

Agakhan, Africa Islamic bank, st benedictine fathers, World vision, Islamic League n.k. ni mashirika ya dini. Usajili wake ni wa mashirika kama ilivyo kwa shirika jingine.

OIC ni zaidi ya hapo, inahusu nchi kwa ujumla. Zanzibar walipotaka kujiunga hoja kubwa ni waislam. Mkataba wa mwaka 1964 unahusu mambo ya nje.Nia inaweza kuwa nzuri approach ni mbaya

Mkandara anaamini ushiriki umeombwa na SMZ kwa ajili ya Waislam. ZNZ ni secular state isipokuwa ina population kubwa ya Waislam. Hapa ndipo nilihisi mkuu wangu alipojikita.

Zanzibar ijenge hoja nyingine si kwasababu ya Waislam.
Msumbiji na Uganda zina Waislam wachache lakini ni wanachama.

Kutanguliza dini suala analolipinga Mkandara kwa baadhi ya nyakati ni jambo la hatari sana.
Hilo ndilo lianelekea kuvunja muungano kwasababu watu hawajengi hoja za kiuchumi.

Kuna kitu Mkandara hakijadili. Mauaji ya watu wa imani nyingine haileti picha nzuri kwa dunia achilia mbali Tanzania. Hofu iliyotanda duniani ni znz kuwa somalia nyingine ya alshabaab.Hili ni kosa wanalofanya wznz wenyewe tena nashangaa kama wanaijua dini yao.

Niwie radhi kwa elimu mbovu ya dini. Mitume wote waliishi na wasioafikiana nao kiimani.
Nabii Issa aliteswa na watu waliompinga. Mtume Mohamad(PBUH) aliishi na wa imani nyingine


Huu Uislam unaotaka watu waishi wenyewe unatoka wapi?
Nisaidie kidogo katika mapungufu yangu, na narudia tena wote waniwie radhi kama nimepotoka mahali.


Leo nchi za magharibi zina travel alert znz, nani ataleta dola?
Mkandara hayaoni mapungufu hayo anachokiona ni mahoteli kujengwa.
Nani atapanga kama wznz wanaua , wanamwagia wageni tindikali na wanaandama viongozi wa dini zingine?

Znz watajenga hoja ya OIC kwa nia nzuri lakini image yao ni mbaya.

Tanzania imejikuta katika matitizo ya kidplomasia kwa udhaifu wa Kikwete kuwaachia wznz watumie jina la nchi kujiunga na taasisi zinazopaswa kusimamiwa vema.

Meli za znz zilizobeba mafuta ya Iran zilisajiliwa Znz na pesa ikachukuliwa na SMZ na Zanzibar Maritime Organisation(ZMO) baada ya kujitoa Tanzania Maritime Org.

Ada za ZMO kule International Maritime zinalipwa na JMT, mapato yanaingia SMZ!!

Matatizo yanawakumba Watanganyika kwasababu vikwazo vitaumiza Watanganyika si wznz.

Mkandara mfano huu unaweza kukupa picha busara zilizotumika katika OIC.
Misuse ya uanachama inaweza kuwa na impact katika nchi.
Kutokana na mwenendo uliojengwa na wznz nani wa kulaumiwa.
Haki ipo lakini haki hiyo iambatane na wajibu
Hivyo Tukiweza kuondokana na shuku hizi, tukaaminiana ktk imani zetu na tukashikamana Muungano wetu wa serikali 2 hauna dosari zaidi kama yalivyokuwa mashirika ya Umma.
Mkuu kuna kuaminiana kupi tena?
Tumekuonyesha uhuni wa znz katika kuvunja makubaliano kwa kiburi na jeuri. Nani wa kulaumiwa!

Sijaona mahali mkuu wangu ameonyesha mapungufu ya znz zaidi ya kuonyesha kuonewa ambako hakupo. Hayo ndiyo yanasababisa watu wajiulize, hivi kwanini tuendelee katika maisha haya ya kulaumiwa?

Mvuvi kalala hakupata samaki, sababu ni muungano.

Mkuu laani kwanza uhuni, ujeuri na kiburi cha wznz bila aiibu halafu tujadili the way forward
Mkuu wangu serikali 3, ni fikra za kimasikini. yaani sisi wepesi sana kugawana umaskini badala ya kuunganisha nguvu.
Wepesi huo wano wznz, sisi tulikubali miaka 50, wao wakaanza 1984,2010 na hadi leo. Wao hawataki muungano. Umesahahu Nyerere laanatullah, leo Mkandara unawashwishi vipi hawa waungane na makafiri? Huoni umasikini wa fikra umeanzia visiwani, kwanini umbebeshe Mtanganyika lawama kutokana na maoungufu ya mtu mwingine
Ni kutokana na umaskini huo na fikra hizo za kimaskini ndio maana tunaona kila sababu ya kuunda serikali 3 ili kila mmoja abebe mzigo wake, tusijuane kama tunavyogawana mali za urithi. Na tisa ktk 10, huanguka wote wakarudi kuishi maisha ya chini kabisa. Urithi umepotea na mali imepotea ndivyo navyotarajia hatma ya Muungano ktk serikali 3.
Zanzibar ndiyo iliyoanzisha serikali 3, labda ungewauliza kwanini.
Lakini kizuri zaidi ni kuwa kama hatuwezi kuishi pamoja, na sasa niseme hatuna tena utanzania ni vema kila mtu akakaa kwake.

Kama tutakubaliana kusihi pamoja, ni lazima tujue yapi ya muungano tutakayoshirikiana ambayo Warioba na tume wamesema ni 7 tena kidogo zaidi ya yale ya mwaka 1964.

Tanganyika ishughulike na mambo yake, failure zake na success zake bila kulaumiwa. Huwezi kuificha Tanganyika ili mznanibar ajibanze kwa jina la muungano. Hicho ndicho Mkanda anachoogopa . Anajua wazi kuwa utegemezi wa znz kwa Tanganyika ni kupitia muungano. Ni kwasababu hizo yupo tayari kusema znz ibaki kama znz, halafu iingie katika muungano na nchi isyokuwepo. Znz inapo feli inasingizia muungano. Hilo sasa hatutaki na kama hawataki njia nyeupe kabisa waende wakajenge Dubai tutaenda kwa passport kununu bidhaa kama kuna ulazima.

Yale 7 tutakayokubaliana lazima znz wachangie. Muda wa kuchota bila kutia kitu katika bakuli umekwisha,.
Muda wa kulilia migao wasiyochangia hatutaki.

Muda wa kulalama kuhusu madaraka ni upuuzi, na muda wa kudai vyeo na nafasi za upendeleo sasa basi. Kama hawana cha kuchangia waende wakajenge nchi yao.

Tumechoka kubeba lawana za failure za watu. tumechoka uhuni na jeuri.

Ni aibu taifa la watu milioni 40 kuendeshwa na watu lakini 5 wengine wakiishi Tanganyika.

Hilo sasa halizuiliki ni suala la muda, hata kama litaahirishwa tutalifanyia kazi wananchi wenyewe. Muungano wa kileo ni uchumi, si muungano wa herufi, bla bla naprojo
.
Siyo muungano wa uzushi, fitna kiburi na jeuri.
 
Back
Top Bottom