Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,434
Barubaru,
Nashangaa sana kwanini umekuwa ni shabiki wa historia iliyopotoshwa na inayozidi kupotoshwa.
Nikulize, kwako wewe, nini ni legal foundation ya muungano? Jibuu dhahiri kwa waelewa wa historia ya kweli ni mkataba wa muungano (1964) ambao tume ya katiba imegundua kwamba historia ni kitu ambacho hakiwezi kwepeka; kumbuka mkataba huu ulikuwa na hadhi na pia uhalali wote wa kisheria za kimataifa.
Nikuulize swali lingine: Je articles of the union zinataja Tanganyika na Zanzibar kama nini kati ya haya - nchi shiriki (jamhuri mbili huru ) au serikali mbili shiriki? Jibu kwa swali hili pia kwa waelewa wa historia ni kwamba mkataba (1964) unataja Tanganyika na zanzibar kama jamhuri mbili huru, na katika ibara ndani ya hizi articles, unatambua kwamba jamhuri huru ya Tangayika ina serikali yake na watendaji wake wa kuendesha Taifa la Tanganyika as of April 1964, ndio maana mkataba ule ukasema pawe na kipindi cha mwaka mmoja kama kipindi cha mpito ambapo katiba ya jamhuri ya Tanganyika yenye serikali yake full functional ifanyiwe marekebisho ili iwe ni katiba ya muda ya JMT (kwa mwaka mmoja) na sheria kadhaa zifanyiwe marekebisho ili zitumike zanzibar kwa masuala yasiyokuwa ya muungano wakati zanzibar nayo ikijipanga kikatiba kusimamia masuala hayo kwani bado haikuwa na katiba yake kama jamhuri as of april 1964. Pia ikaelezwa kwamba rais wa muungano katika kipindi cha mpito asimamie masuala ya Tanganyika (kwa muda wa mwaka mmoja tu ambapo ndani ya hicho kipindi cha mpito, jamhuri ya muunngao ilitakiwa ianze mchakato wa katiba mpya. Lakini kilichotokea ni kwamba kile kipindi cha mpito ambapo rais wa jmt alitakuwa asaidiane na makamu wake (kutoka zanzibar) kuteua tume ya katiba na baraza la kutunga katiba, haya hayakufanyika a badala yake zikaja sheria za muungano kwa nia ya kuufunika mkataba, huku pia suala la tume ya katiba na baraza la kutunga katiba vikiachwa bila utekelezaji. Hizi ndio zikawa ni hatua za mwanzo za kukiuka mkataba wa muungano. Kilichofuatia ni katiba ya muda kutangazwa siku chache kabla ya kipindi cha mpito to expire.
Swali langu kwako barubaru: Je unajua asili ya jina na Tanzania Bara ni nini? Jibu ni kwamba miaka miwili baada ya katiba ya muda kupitishwa (yani 1967), uchakachuaji wa mkataba ukazidi kushika kasi ambapo sheria namba 22 ya mwaka 1967 ilipitishwa kwa nia ya kuifukia Tanganyika na kuweka jina la Tanzania Bara kama mbadala. Sambamba na hili, tukumbuke kwamba TANU ilishajiingiza kwenye suala la muungano kupitia sheria za muungano 1965 (kinyume na mkataba wa muungano ambao hautaji vyama), hivyo TANU ikasubii upenyo kupitia sheria batili, na tangia hapo chama hiki kikachukua majukumu ya kusimamia masuala ya muungano na yasiyo ya muungano huku ikisema Tanzania ni nchi ya chama kimoja wakati znz kulikuwa na ASP. Hapa hoja yako juu ya kutofautisha serikali na chama ndio inakuja - TANU ikawa serikali na serikali ikawa TANU, hivyo kimsingi tofauti unayomuuliza Nguruvi3 haikuwa na maana tena.
Hadi hapa, serikali ya Tanganyika ilikuwepo ila jina Tanganyika (kiserikali) likafutwa na sheria tajwa hapo juu lakini kimsingi majukumu yake yakahamishiwa kwenye chama cha siasa ambapo katiba ya 1965 ilikipa chama hiki madaraka ya juu kabisa ya kuendesha nchi. Kwa maana hii, majukumu ya Tanganyika kiserikali yaliendelea kuwepo kupitia chama - mwanzo wa kiini macho.
Hapo juu unajadili juu ya Tanzania bara na kusema Tanganyika haipo, Je unajua kwamba kuna wakati pia kulikuwa hakuna zanzibar bali Tanzania Visiwani? Ni muhimu ukawa na uelewa kwamba kupitia katiba ya JMT ya 1977, katiba hii ilikuja na sheria za kuua zanzibar (kama sheria namba 22 ilivyoua Tanganyika 1967), hivyo sheria ya 1977 ilifuta zanzibar a na kuzalisha Tanzania visiwani. Miaka miwili baadae, Zanzibar ikaja na Katiba yake ya kwanza kama Taifa huru baada ya mapinduzi, na katika mabadiliko yaliyofuatia baadae kikatiba nadhani 1981, wakarudisha jina zanzibar na kulifuta Tanzania visiwani, hivyo kurudisha heshima ya mkataba. Tanganyika ilitakiwa irudi kwa mtindo kama huu wa zanzibar kwa kuipatia Tanganyika katiba yake separate na ile ya JMT. Kwa bahati mbaya Tanganyika haikuweza fanya hivyo kwani Tanganyika ilifanywa ndio Tanzania na kubeba koti la muungano.
Kwa maana hii basi, lazima uelewe hoja ya nguruvi3 hapo juu kwamba Tanganyika imekuwepo throughout kama serikali na vile vile kama nchi kwani legal foundation ya muungano pamoja na uwepo wa katiba ya 1977 iliendelea na inaendelea kuwa mkataba wa 1964 ambao unatambua Tanganyika na znz kama two sovereign states zilizo surrender baadhi tu ya mambo huku yaliyosalia yakitakiwa kuendelea kuwa chini ya nchi shiriki ambapo Tanganyika ilikuwa pia na serikali yake, na znz iliazima sheria za hapa na pale (modified) huku nao wakijipanga kuwa na serikali yao yenye katiba yao ndani ya mwaka mmoja. Kwahiyo basi the fact kwamba nchi iliendelea kutawaliwa chini ya serikali mbili kupitia katiba ya jmt 1977 haina maana kwamba serikali ya muungano had legitimacy kikatiba. Legitimacy yake ilitokana na other things - azimio la arusha, historia ya tanu na asp kutetea wanyonge ndani na nje ya nchi (hasa tanu) na charismatic and integrity ya nyerere. Umma ulikiamini chama na serikali bila kujali katiba. Those days are long gone, ndio maana bila ya uhalali wa kikatiba, ccm haiwezi kuishi kwa amani, kwani umma unataka kushirikishwa katika kujenga uhalali huu, na uhalali huo unazidi kuonyesha kwamba utategemea sana kuheshimiwa kwa legal foundation of the union (mkataba wa 1964) ambao bado unatambua Tanganyika na zanzibar kama two sovereign states zinazotakiwa kuwa na serikali zake kusimamia masuala yao yaliyo nje ya muungano, hence logic ya serikali tatu kwenye rasimu ya katiba.
Huu ni wakati muafaka wa taifa kuongozwa nna serikali ambazo source zake za legitimacy ni katiba, na sio utashi wa vyama vya siasa na mambo mengine ya ovyo.
Mkuu Nguruvi3, historia imepotoshwa sana na wada kama Mkandara inaonekana sio tu kwamba wameafiki upotoshaji huo bali wameanza kuujengea uhalali. Hili ni tatizo. Tutalijadili zaidi ukija na mjadala wako ulioahidi hapo juu ambapo nitatumia fursa hiyo kujibu baadhi ya hoja za mkandara.
Cc JokaKuu
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Last edited by a moderator: