Mkandara,
Siku zote watu wanapokaa kitako kuanza kuujadili MUUNGANO wengi sana kutoka upande wa Tanganyika wanakuwa wa kwanza kabisa kuionea huruma ZNZ ikiwa pamoja na kuipitia historia yake wakti munasahau kuwa ya kwenu ni khatari sana.
Nafikiri suala la kwanza mlitakiwa mjiulize KWANINI NYERERE ALIFUNGA SAFARI KWENDA ZNZ KUMUOMBA KARUME WAUNGANISHA NCHI HIZO?
Hapa pana siri kubwa sana kwa Nyerere kwani aliona nchi yake ina matatizo kiasi kikubwa sana na suluhisho ilikuwa ni kuungana na ZNZ. Na ndio maana alikubali kwa nia moja nchi yake wakti ule ikiwa na watu zaidi ya milioni 18 kuungana PASU KWA PASU na nchi yenye watu chini ya laki tatu.
Lakin kubwa zaidi bila kusema uwongo na kuwa wanafiki LAAZIMA MUKUBALI KUWA MUUNGANO WENU NI WA MATAKWA YA VIONGOZI NA SIO WANANCHI NA UNALINDWA KWA GHARAMA KUBWA SANA KIASI CHA KULETA KHOFU NA KUTO KUAMINIANA MIONGONI MWA WANANCHI WA NCHI HIZO.
Waarabu tuna usemi " IN ORDER TO BUILD SOMETHING STRONG IT HELPS TO START WITH BEST AND POSSIBLE MATERIALS"
Sasa nilibainisha hapo awali kuwa MUUNGANO ULIKUWA WA MAGUMASHI NA HAUKUFUATA SHARIA ZA KIMATAIFA. HIVYO lazima mpate shida kwani NYUMBA NI MSINGI. Ndio maana hata katika bunge lenu la KATIBA unaona wazi limetawaliwa na KHOFU NA UWOGA MKUBWA kuhusu MUUNGANO.
SASA msingi mkubwa hapo NI KUUVUNJA KISHA KUREJESHA KWA WANANCHI WAAMUE KAMA WANAUTAKA AU LAA. NA WA AINA GANI KAMA WATAUTAKA. Hakuna jinsi hapo lazima maamuzi ya wananchi yahishimiwe.
Enzi za kuogopa kuujadili muungano zimepitwa na wakti. NI VIZURI MUBADILIKE. ACHENI UWOGA
[/QUOTE
Barubaru,
maswali yako yote yanaonyesha huna majibu wala hujui ilitokana vipi ila unatafuta kujua. Kwa maana hiyo huna elimu ya historia ya Mapinduzi na kwa nini Mapinduzi yalitakiwa ama yaliandaliwa. Sijui kama unakumbuka kwamba siku ile ya mapinduzi kuna picha zinaonyesha Abrahman Babu akiwasili nchini kutoka Cuba, sasa ilikuwaje akajua ni siku hiyo alitakiwa kuwepo Zanzibar.
Pili, wasikilize Karume na Abdurahman Babu walipokuwa wakimtambulisha John Okello baada ya Mapinduzi, utajua hayaMapinduzi yaliandaliwa mapema kabla, na huko nyuma nimekuonyesha mkutano wa Panafrika ulofanyika Mwanza wakimtaka Shamte aungane na ASP, yeye aliporudi Znz tu akawageuka bila kujua kwamba wenzake walikuwa na plan B.
Harakati za Ukombozi wa Afrika zilikwenda sambamba na UMOJA wa nchi huru za Kiafrika, kilichofuata baadaye ni sura kamili ya viongozi wa Kiafrika ambao UNAFIKI ndio sifa yetu kubwa. Labda nikwambie tu ya kwamba Nyerere alimkuta Karume tayari akishirikiana na TAA ya Tanganyika hivo swala la yeye kushirikiana na Karume ilitokana na utaratibu wa uongozi maana alikuwa mwenyekiti wa TANU na pia rais wa kwanza wa Tanganyika huru.
Kwa nini Nyerere alikwenda Zanzibar, haina maana kwamba swala hili halikuzungumzwa kabla ila kuliweka bayana ndipo lilitokea zanzibar. Ni sawa na wewe kwenda peleka uchumba kwa wazazi wa mtoto wa kike haina maana ndio kwanza wewe na mwanamke huyo ndio mnawasiliana. Huwa tayari mmeshakutana na pengine hata kumaliza ndoa kimjini. Muungano ulisha pangwa mapema, rudia hotuba ya Nyerere alipokuwa Ghana kuunganisha Afrika kwa hatua. Tayari iliisha julikana kinachofuata pengine ingekuwa EAC kama sii Idd Amin kutuvuruga.
Na ndio maana Artical of Union ilionekana kuandikwa ktk muda mfupi sana jambo ambalo linawashangaza wataalam. Ukweli ni kwamba vitu vyote vilikwisha andaliwa na ndio maana Karume na babu walokuwa maadui walisimama kutambulisha Zanzibar mpya mara tukashtukizwa na Muungano.
Muungano wetu ni matakwa ya viongozi ndiyo, kwani kuna muungano gani usokuwa matakwa ya viongozi? wengine wamepigwa vita na kulazimishwa kuungana kama mateka itakuwa sisi, tazama States za Marekani, Hiyo Uingereza, Russia na kadhalika kote huko ni viongozi walounda miungano ya nchi zao hakuna hata mmoja ulopitia maoni ya wananchi isipokuwa labda hizo jumuiya ama shirikisho kama EU.
Mimi sipendi kurudia vitu, Mapinduzi yalikuwa halali na muungano ulikuwa halali kama ulivyo Uhuru wa Kenya. Huwezi kusema Kenya sio Huru kwa sababu walipigana vita na kuua watu pasipo ridhaa ya wananchi. Ujinga huo sina muda wa kuuendekeza. Kama hamuupendi Muungano pigeni kura za refendum. Niliwahi kumwambia Hamad Sharrif alipokuja huku kabla ya uchaguzi wa mwaka 2000 - wapeni wananchi fursa wachague kusuka ama kunyoa, wanautaka muungano waseme NDIO wasioutaka waseme HAPANA. akanyamaza kimyaaa kumbe ni mganga njaa tu akilishwa kidogo hana mdomo.
Acheni hizo mkuu wangu Muungano utalindwa kwa nguvu zote na wala sifanyi hivi kwa kuitetea CCM ila maslahi na ya nchi yetu kinyume kabisa cha matakwa ya chama changu.