Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
- Thread starter
- #141
Mkandara: Nitauliza tena kwa wajumbe wa katiba, ikiwa kweli waasisi wetu wa Muungano waliunganisha NCHI 2 kuwa NCHI 1 (Taifa) yenye serikali 2 (nchi 1 serikali 2)na sio nchi 2 zenye serikali 2. Kwa nini Watanzania bara walikuwa wakienda Znz kwa passport ilihali ni nchi 1?. kama ni nchi 1 kwa nini hadi leo Mtanzania bara haruhusiwi kununua ardhi Znz wakati ni nchi 1
Mkuu Zumbemkuu , hili swali ni rahisi kujibika. Urahisi wake ni pale Mkandara atakapokuwa katika nafasi ya kuelewa tofauti ya country, nation and government.
Kwa kumsaidia kidogo,nchi moja inaweza kuwa na serikali tofauti. Hata sisi tuna serikali nyingi zikiwemo za mikoa, miji na majiji. Nchi ina mipaka inayoitambulisha na vile vinavyoifanya nchi ndiyo hutengeneza utaifa.Ukisoma swali lake, amechanganya mambo ya nchi na taifa kisha akaingiza serikali bila kuviangalia vitu hivyo kwa utofauti. Mchunguzi kaeleza vizuri sana sijui kwanini Mkandara hakubaliani naye au hampingi kama ana mbadala.
Kwenda znz kwa passport i: wznz walisema znz ni nchi kutokana na mkataba wa muungano. Hata hivyo walipoambiwa uwezekano wa kurudisha passport kwao kuja Tanganyika upo waliamua kuondoa kwa kujua ni tatizo kwao zaidi ya faraja.
Kwamba ni nchi moja kwanini mbara haruhusiwi kuwa na ardhi, hili nalo ni sehemu ya makosa ya katiba ya 2010 yaliyoipa znz mamlaka yake nje ya mambo ya muungano. Wala si hiylo tu mbona waliunda taasisi zao bila kushauriana na JMT.
Wameondoa bandari na anga, wakaunda baraza lao la mitihani, wakaunda shirika la viwango, wakaunda ZMO n.k.
Ni sehemu ya ukaidi tu wa kutozingatia sheria.
Ili kuondoa ukaidi huo na kutoa nafasi ya wao kutenda bila kuingiliwa, njia muafaka ni kuwa na serikali ya Tanganyika ambayo haitaingilia mambo yao. Warioba kasema ni mambo 7 tu nje ya hapo kila mtu atajishughulikia. Hilo ni bora zaidi kuliko ilivyo sasa.
Unapokuwa na serikali mbili unakuwa na popo ambaye hujui ni ndege au mnyama. Hili ndilo linatokea kwa sasa.
Mfano, znz wanasema ni Watanzania wakitaka ada za Maritime zilipwe kule IMO. Wanaposajili meli mshiko unakwenda kwao kwasababu wao ni nchi na ina vyombo vyake. Hapa Mtanganyika anabaki kuwa mlipa kodi na mzanzibar kuwa mfaidika wa kodi za Mtanganyika. Ili kuondoa utata mambo ya IMO yashughulikiwe na Znz na Tanganyika itakuwa na mambo yake.
Umuhimu wa Tanganyika anaueleza Mkandara vema sana, ila hisia zinamuondoa katika ukweli.