Barubaru
JF-Expert Member
- Apr 6, 2009
- 7,161
- 2,324
Suala la zanzibar nilishalijadili huku nikikupa ushahidi kwamba mkataba ulijadiliwa na baraza la mapinduzi, kilichojaa controversy ni suala la ratification, sio suala la BLM kupata fursa ya kujadili mkataba, kisha nikakuuliza mtazamo wako juu ya hoja ya prof haroub othman kwamba dourado akiwa mjumbe wa tume ya nyalali aliafiki kwamba baraza la mapinduzi kufanya ratification, nikahoji, je, inawezekana kwamba dourado alidanganya kwenye paper presentation yake kwa Tanganyika Legal Society conference 1983 lakini akasema ukweli chini ya tume ya nyalali? Haujajibu na badala yake you have become a spinner;
Kwa upande wa Tanganyika, taratibu zote zilifuatwa kama ilivyoelekezwa na mkataba wa muungano, lakini kujibu swali lako kuhusu legal team ya Tanganyika juu ya hili, walikuwa ni:
*Mark Bomani akisaidiwa na Roland Brown na P. Fifoot;
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Mchambuzi,
Nimeona tunachokosa kuelewana ni kitu kidogo sana na NDIO MAANA UNASHINDWA KUNIELEWA NINAPOSEMA MUUNGANO WA tgk NA zNZ NI BATILI KISHARIA.
Nimebainisha mengi sana lakin ninalotaka kukupa darsa hapa ni kuwa KILA SHARIA INAYOTUNGWA BASI INAKUWA NA KAANUN NA UTARATIBU (PROCEDURE) YAKE.
Kwanza turejee katika The article of the Union between Tanganyika and Zanzibar inasema
(v) The existing laws of Tanganyika and of Zanzibar shall remain in force in their respective territories subject to (a) to any provision made hereafter by a competent legislature;
Na mimi nimebainisha wazi kuwa Articles zile japo zilikosa sifa ya kisheria ya kuutwa mkataba "contract" kutokana na tatizo la kisheria liitwalo "privity of contract", articles zile zilikuwa na sifa zote za kuitwa ' international treaty" kuunganisha nchi mbili, na ili any international treaty kupata uhalali na nguvu ya kisheria, ni lazima treaty hiyo iwe ratified na mabunge ya nchi husika!.
Ratification is a process ambayo hufanywa kwa procedures maalum na kufanywa in writing!.
Bunge la Tanzania lilifuata sheria, taratibu na kanuni zote ku ratify zile articles of union kwa maandishi!.
Zanzibar, walikuwa ndio kwanza wametoka kwenye mapinduzi, hivyo hawakuwa na bunge, Baraza la Mapinduzi ndilo lililokuwa kila kitu!. Lilipaswa kuziridhia zile articles of union kwa ratification ambayo hufanywa kwa maandishi!. Vikao vyote vya BLM vina hansard, lakini hilo halikufanyika na hakuna kumbukumbu yoyote ya maandishi kwamba ratification ilifanyika!.
SASA KISHARIA KWA KUVUNJE HIYO PROCEDURE YA RATIFICATION ndio tunasema wamevunja sharia nzima ya international treaty hivyo KUUFANYA MUUNGANO HUO UWE KINYUME CHA SHARIA HIVYO NI MUUNGANO HARAMU.
Sasa sijui ahali yangu nikueleze kitu gani ili uwelewe maana wewe umeshikiria maneno ya akina Shivji, Marhum Haroub na wengineo hao wote hawana nafasi katika sharia hii. MIMI NINACHOSEMA PROCEDURE HAIKUFATWA na kama unasema imefuatwa tuambie maandishi yapo wapi kama procedure inavyotaka? na ndio maana mpaka BLW wameomba huo mkataba wauridhie mpaka leo wanapigwa chenga achilia mbali kushirikishw kwa mwanasharia mkuu wa Znz katika mchakato mzima wa Muungano.
KIFUPI NASEMA MUUNGANO WENU NI WA MAGUMASHI TU. Waachwe Znz wapumue kwa raha zao kwani wao sio miongoni mwenu.
Nafikiri umenielewa hapo.
cc takashi, Foum Jnr, GHIBUU, nguruvi3, Joka kuu, Mkandara, Bobuk, Gombesugu, Ritz, The Big show,Mohamed said.