Mkuu nasubiri majibu yako kwanza maana upotoshaji wako bado kabisa hauwezi kujenga hoja ya msingi.Hiki kitu kinachoitwa legal foundation wengi hawataki kukijadili kwasababu kinaondoa dhana ya serikali 2. Lakini basi tukiuliza kama legal foundation ni dhana mbaya, watuambie msingi wa serikali 2 ni upi. Hakuna jibu, wanataka tuamini tu kuwa ilikuwa serendipity hivyo tuendelee tu kibubusa kama ilivyotokea.
Serikali 1 imeshindikana, 2 zina matatizo yasiyo na suluhu. Where do we go from here!
Serikali 3, in worst case scenario vunja jahazi
Nilisema na nitasema tena Artical of Union ni legal foundation ya kuundwa kwa TAIFA moja na sio NCHI moja. Na Nikaendelea kusema Leo hii Tanganyika sio nchi tena baada ya kuliacha jina hilo kisheria na kutumia neno Tanzania kwa kuongeza mapana ya eneo lake ikijumuishwa na Zanzibar. Na sababu ya pili nikasema Tanganyika sio nchi kwa sababu kila nchi ina mihimili mitatu. 1. Serikali, 2 Mahakama na 3. Bunge lake hivyo Tanganyika haipo na haina vitu hivyo isipokuwa Zanzibar ni nchi kwa sababu ina mihimili hiyo. Tanganyika ilikwisha kufa, leo hii tuna Taifa moja tu lijulikanalo kama Tanzania na ukitaka kuiua Tanzania ni kuirudisha Tanganyika na tutakuwa tumekiuka sheria vie vile za katiba tuloapa kuilinda kama walivyofanya Wazanzibar na katiba yao ya mwaka 2010. Hivyo kosa moja haliwezi kupatiwa ufumbuzi kwa kufanya kosa jingine kinyume cha katiba na makubaliano ya Muungano.
Nirudi ktk KERO ZA MUUNGANO - Hizi kero zilikuwepo toka zamani na kwa hatua tofauti, Nilishakueleza huko nyuma hivyo tuliposhindwa kuzitatua na hasa kasheshe lilianza baada ya kutoka mfumo wa Kijamaa na kuingia Ubepari. Tanzania bila kujiandaa tuliingia mfumo huo pasipo kufanya amendments za kichumi ktk katiba yetu ya JMT na katiba ya Zanzibar, hapo ndipo Tanganyika iliyokufa ikaanza kujitokeza maana tuliyatazama kero zile kwa maslahi ya Bara na sii kwa maslahi ya Zanzibar au Tanzania.
Kwa hiyo Wazanzibar wakajiona wao kama ni koloni la Tanganyika. Na nadhani unajua maana ya koloni au territorial government ambayo haina mamlaka kamili. Hivyo toka tumeunda muungano wetu Zanzibar ilikuwa na mihimili yake mitatu kulingana na katiba ya JMT lakini ktk utendaji na utekelezaji wa vitu hivi kulingana na na madai ya WaZanzibar ni kuwa hawakuwa na mamlaka kamili ktk uendeshaji nchi yao. Nadhani pia unaelewa mamalaka kamili walokuwa nayo states za Marekani au Province za Canada au zile za Uingereza na kadhalika, kwa nini kero zao sisi tumeziingiza ktk mamlaka ya JMT pasipo ridhaa ya Wazanzibar(mambo mengine 11 yaloongoezeka)ama yale ya muungano kuinufaisha bara tu.
Hivyo, ilichotakiwa ni viongozi wetu kukaa na kuyapanga mamlaka hayo wazi ili yawe ya Zanzibar au ya JMT bila kuingiliana. Na kwa hekima yangu nilojaaliwa najua fika kwamba kwa wale wanaoitaka tanganyika mpya hawataishia hapo. Wataanza kuweka masharti kwa Wazanzibar na Wazanzibara, kumbuka kuna walalahoi wanaosubiri tu mchafuko huu na hakika Usalama wa Wazanbara utakuwa matatani.
Hivyo basi kama kweli tunaitafuta suluhu ya Muungano wetu tulitakiwa kuzitazama hizo kero za Muungano kabla ya Zanzibar hawajaandika katiba yao mpya ya mwaka 2010. Kila kilichobadilishwa mle (katiba ya Zanzibar) ni kero zilizokuwepo ambazo tulizipuuza na sasa ndizo sababu ya kuzaliwa kwa katiba hiyo na kumezaa Kero mpya kwa Bara. Kero juu ya kero.
Hivyo kero za muungano zimehamia Bara na sasa, nasi tunatafuta dawa yake, jino kwa jino huku tukifanya makosa yale yale waloyafanya Zanzibar ya kukiuka katiba ya Muungano. Kuirudisha Tanganyika itakuja na katiba yake ili kutoa sare kwa katiba ya Zanzibar na sii Muungano. Did we solve our problems? bila shaka ni hapana, ila tumeongeza matatizo yaani sasa sote tumekiuka Katiba ya JMT, hivyo hakuna hata sababu ya bunge hilo la katiba kuwepo.
Kitakacho fuata sasa hivi ni Zanzibar wabadilishe katiba yao ili tukubaliane nao (mjadala mwingine), Tanganyika nao waandike katiba yao halafu ndio Katiba ya JMT iundwe hii itachukua miaka 5 hadi 10 ijayo. Je tumefanikisha lipi - HAKUNA maana hata tukiwa na serikali 3 bvado swala la OIC litakuwa ktk mambo ya nje na serikali kuu (3) bado italizuia kwa sababu zile zile walizotoa tulipokuwa na serikali 2. Tunashindwa kutazama kero zenyewe badala yake tunajitazama sisi kutokana na hii kitu UBEPARI na hatukuwa tayari kuandaa mwongozo unatuwezesdha sote ktk ushirika wa JMT.