Duru za siasa: Bunge la Katiba, upotoshaji na kiwewe cha kuzinduka Tanganyika

Duru za siasa: Bunge la Katiba, upotoshaji na kiwewe cha kuzinduka Tanganyika

Mkandara: Nitauliza tena kwa wajumbe wa katiba, ikiwa kweli waasisi wetu wa Muungano waliunganisha NCHI 2 kuwa NCHI 1 (Taifa) yenye serikali 2 (nchi 1 serikali 2)na sio nchi 2 zenye serikali 2. Kwa nini Watanzania bara walikuwa wakienda Znz kwa passport ilihali ni nchi 1?. kama ni nchi 1 kwa nini hadi leo Mtanzania bara haruhusiwi kununua ardhi Znz wakati ni nchi 1
mkuu Nguruvi3 na Mchambuzi hili swali linawahusu maana ingefaa mtoa hoja warioba alijibu ila sidhani kama yupo humu,
Mkuu Zumbemkuu , hili swali ni rahisi kujibika. Urahisi wake ni pale Mkandara atakapokuwa katika nafasi ya kuelewa tofauti ya country, nation and government.

Kwa kumsaidia kidogo,nchi moja inaweza kuwa na serikali tofauti. Hata sisi tuna serikali nyingi zikiwemo za mikoa, miji na majiji. Nchi ina mipaka inayoitambulisha na vile vinavyoifanya nchi ndiyo hutengeneza utaifa.Ukisoma swali lake, amechanganya mambo ya nchi na taifa kisha akaingiza serikali bila kuviangalia vitu hivyo kwa utofauti. Mchunguzi kaeleza vizuri sana sijui kwanini Mkandara hakubaliani naye au hampingi kama ana mbadala.

Kwenda znz kwa passport i: wznz walisema znz ni nchi kutokana na mkataba wa muungano. Hata hivyo walipoambiwa uwezekano wa kurudisha passport kwao kuja Tanganyika upo waliamua kuondoa kwa kujua ni tatizo kwao zaidi ya faraja.

Kwamba ni nchi moja kwanini mbara haruhusiwi kuwa na ardhi, hili nalo ni sehemu ya makosa ya katiba ya 2010 yaliyoipa znz mamlaka yake nje ya mambo ya muungano. Wala si hiylo tu mbona waliunda taasisi zao bila kushauriana na JMT.
Wameondoa bandari na anga, wakaunda baraza lao la mitihani, wakaunda shirika la viwango, wakaunda ZMO n.k.
Ni sehemu ya ukaidi tu wa kutozingatia sheria.

Ili kuondoa ukaidi huo na kutoa nafasi ya wao kutenda bila kuingiliwa, njia muafaka ni kuwa na serikali ya Tanganyika ambayo haitaingilia mambo yao. Warioba kasema ni mambo 7 tu nje ya hapo kila mtu atajishughulikia. Hilo ni bora zaidi kuliko ilivyo sasa.

Unapokuwa na serikali mbili unakuwa na popo ambaye hujui ni ndege au mnyama. Hili ndilo linatokea kwa sasa.
Mfano, znz wanasema ni Watanzania wakitaka ada za Maritime zilipwe kule IMO. Wanaposajili meli mshiko unakwenda kwao kwasababu wao ni nchi na ina vyombo vyake. Hapa Mtanganyika anabaki kuwa mlipa kodi na mzanzibar kuwa mfaidika wa kodi za Mtanganyika. Ili kuondoa utata mambo ya IMO yashughulikiwe na Znz na Tanganyika itakuwa na mambo yake.

Umuhimu wa Tanganyika anaueleza Mkandara vema sana, ila hisia zinamuondoa katika ukweli.
 
1. Je, chini ya mfumo wa serikali tatu kuna ukweli kiasi gani kwamba znz haitaweza kuchangia katika masuala saba ya muungano kwa mujibu wa rasimu ya katiba? Nguruvi3 aliwahi kujadili hili, tunaomba utusaidie tena.

2. Je, kipi ni ukweli kati ya haya - znz haitakuwa na uwezo wa kifedha kuchangia muungano wa serikali tatu au ni kwamba tu znz hawataki kuchangia kwa sababu za kihistoria? (Rejea madhara ya nyongeza ya mambo ya muungano kwa znz).

Vinginevyo ima iwe znz hawana uwezo kiukweli au uwezo utakuwepo chini ya utaratibu ulioanishwa na rasimu lakini wanakwepa tu ukweli, hali hii ni sababu tosha ya kuvunja muungano kwani hatukuungana ili mshirika mmoja aje kumbeba mshirika mwingine, unless kufanya hivyo ilikuwa ni kwa lengo la kwenda serikali moja.

Lakini hakuna ushahidi katika mkataba wa muungano kwamba kulikuwa na lengo la serikali moja.
All that said and done, iwapo znz hawana uwezo (kiukweli au kwa visingizio), huu ni wakati muafaka kwa Tanganyika kuanza kujiendesha kivyake.
Mkuu Mchambuzi , maswali yako ya nyuma yanazidi kubeba uzito kwa kuzingatia ukweli tulishawahi kuyafafanua lakini muhimu zaidi ni jinsi Warioba alivyoyaona katika mtizamo wetu.

Warioba katika majibu amesema serikali ya shirikisho itakuwa na vyanzo vya mapato kutokana na ushuru pamoja na mchango wa washirika. Akaendelea kusema michango itazingatia eneo na idadi.
Hadi hapo Warioba ameonyesha kuwa Zanzibar inaweza kuchangia muungano bia shaka.

Kwa mtazamo wa duru tunasema wale wanaosema kuna ongezeko la gharama kama Nape na Pinda ni wababaishaji wa kupindukia. Katika mambo yaliyopendekezwa na tume ni kama ifuatavyo

1. Ulinzi na usalama. Bila muungano kila nchi itagharamia ulinzi na usalama hilo halina mjadala. Kwasasa ulinzi a usalama ni gharama za Tanganyika ambayo ni Tanzania. Hata siku moja, narudia tena hata siku moja hutawasikia wazanzibar wakidai ulinzi na usalama uondolewe katika muungano.
Katika serikali 3 kila mshirika atachangia na kwa mujibu wa Warioba ni kulingana na eneo na population. Kwa msingi huo mzigo anaoubeba Mtanganyika kwa sasa utakuwa na unafuu kwa ukweli kuwa muungano ukivunjika bado znz itakuwa na jeshi, hivyo bajeti hiyo ipo na ndio wakati wa kuitumbukiza katika serikali ya muungano.

2.Uraia na Uhamiaji: Nayo hoja ni kama hiyo hapo juu. Bila muungano Tanganyika au Zanzibar zitakuwa na wizara hizo, fungu la kila mmoja litumike siyo mmoja atoe mwingine apumue.

3. Mambo ya nje: Tanganyika na Zanzibar zimepewa uhuru wa kujiunga na mashirika ya kikanda au kimataifa kulingana na rasimu na pendekezo la Zanzibar. Hii ina maana Zanzibar watakuwa na uwezo wa kukopa, kupata misaada n.k.na kujenga uwezo wa kulipia gharama hizo. Wizara hiyo haiepukiki kama zilizotangulia.

4. Sarafu na benki kuu: Zanzibar hadi sasa wanataka kuwa na benki kuu yao. Huu ni ushahidi kuwa wana uwezo wa kuchangia jambo hilo kwasababu uwezo wanao tayari na wameonyesha.

3. Katiba ya Shirikisho: Hapa ni gharama za taasisi zinazohusiana na katiba kama Urais na makamu. Znz ina rais na makamu wawili, ina uwezo wa kuchangia taasisi za shirikisho bila msamaha.
Znz ina makamu wawili itashindaje kuhumia Rais na Makam wa muungano kwa kuchangia?

4. Usajili wa vyama vya siasa. Nayo ni taasisi itakayokuwepo iwe kwa muungano au kipekee.
Hapa kuwe na ofisi moja Dar na ndogo Zanzibar. Ile ya znz ihudumiwe na SMZ. Hiyo tu inatosha kuchangia shirikisho.

Ukiangaia mambo hayo kwa uchache hakuna gharama iliyoongezeka, kuna kupungua kwa gharama kwasababu mzigo anaoubeba mmoja utachangiwa pamoja. Kwasasa mzigo huo anaubeba Tanganyika peke yake.

Gharama zinapungua kwasababu hizi.
Katika mambo 22 yanayolalamikiwa 15 yameondolewa. Hii ina maana kuwa kila mshirika atashughulika na yake kwa namna anavyoweza bila kumkwaza mwingine. Mfano, elimu ya juu, Tanganyika itashughulikia wanafunzi wake. Kwasasa Tanganyika inagharamia pande zote na upande mmoja ukiwa na nafasi zake.

Mwaka 2012 Tanganyika ilitoa msaada (siyo mikopo kwasababu wznz hawatakiwi kurudisha) kwa wanafunzi 1000 wa znz. SMZ ikatoa kwa wanafunzi 800 wa znz. Hii inaonyesha SMZ ina uwezo wa kuchangia wanafunzi wake bila kukwaza upande mwingine. Kwa muundo wa serikali 2, wznz wanakuja kuchukua msaada huo kwa jina la Tanzania. Watanzani wa bara hawana nafasi hiyo kule znz.

Rasimu imetoa nafasi kwa znz kujiunga na mashirika ya kimataifa. Kwa maana kuwa zile meli zinazosajiliwa na Zanzibar Maritime sasa zitakuwa chini ya udhibiti wa SMZ.
Kwa muundo wa serikali 2, gharama kule IMO zinalipwa na Tanganyika, znz inakusanya pesa tu.

Mwaka jana meli 4 tu zililipa SMZ zaidi ya dola laki 4 sawa na milioni 640. Hii ina maana znz ina uwezo wa kulipa ada zake kule IMO bila kuumiza upande mwingine. Hapo gharama kwa Tanganyika zitapungua na wala hazitaongeza kitu kwa znz kwasababu hadi sasa wanasanya pesa.

Nafuu hiyo itaendelea hadi taasisi kama bunge. Kutakuwa na kupungua kwa wabunge wapatao 15 wa kuteuliwa tu. gharama zao zinaingizwa katika taasisi ya kusajili vyama vya siasa kutoka kila upande. Wabunge 87 wa znz ndani ya bunge la JMT wanlipwa na Tanganyika. Katika ushirika hawatakuwepo.

Ukitaka kutambua kuwa gharama zitapungua kwa wabunge, ni ukweli kuwa wabunge wa znz katika bunge la JMT NI 87, wajumbe wa BLW ni 50. Hivi kwanini majimbo yatoe idadi tofauti?
Maana ya hili ni moja, SMZ imegawa majimbo ya wawakilishi kwa ukubwa kulingana na hali ya uchumi. Wabunge wanokuja JMT ni wengi kwasababu gharama zazo hazigusi SMZ, hivyo ni sehemu ya ajira tu kwao bila gharama.

Gharama zitapungua zaidi kwasababu serikali ya shirikisho ni ndogo tofauti na ya sasa Itakuwa inashughulikia mambo 7 tu,kwasasa kuna mambo 22. Kupungua kwa ukubwa wa serikali kutatoa nafasi kwa washirika kuelekeza gharama katika maeneno mengine.

Tumalizie kwa kujibu swali la Mchambuzi kuwa Znz ina uwezo wa kuchangia katika shirikisho. Inagoma kuchangia kwa makusudi tu kwa ule utamaduni wa 'tutavunja muungano'
Hapa tulipo hakuna jinsi lazima watachangia, wakikataa basi jahazi linavunjwa.
 
Mkuu Mkandara anasema hotuba ya Warioba imekuwa kuorodhesha matatizo bila suluhu.
Nina uhakika hajaisoma yote amesoma 'caption' chache.
Nimeisoma yote neno kwa neno, hotuba imejaa hekima na inazidi kutufumbua macho.

Warioba ameeleza legal foundation ya muungano wetu kama yulivyoeleza na Mchambuzi huko nyuma. Akasisitiza legal foundation ipo katika Article of union na suluhu ya matatizo ipo hapo.
Hili ni jambo Mkandara hataki kulijadili kwasababu litaondoa na kubomoa hoja zake.
Mkandara anaamini muungano ulitokea tu hakukuwa na chanzo

Warioba amesema kwa miaka 12 tume ya pamoja ya fedha imeundwa kushughulikia matatizo ya mapato, mgawanyo n.k.Tume hiyo haijafanya kazi yoyote kwa maiaka 12.

Hapa ndipo Nape, Pinda na Mkandara wanapopaswa kutufahamisha, kama miaka 12 imeshindikana kuna kitu gani zaidi walicho nacho cha ku sustain huu muungano wa serikali 2.

Warioba akasema matatizo mengi yanatokana na znz kukiuka katiba ya muungano.
Hilo tumeliongelea kwa undani na Mkandara hakubali kuwa ni chanzo cha matatizo huku akipaka rangi kwa kusema tatizo letu ni umoja na kuelekeza uwekezaji Zanzibar zaidi.

Warioba amesema kuwa hadi sasa katiba ya JMT imevunjwa na Zanzibar kwa maamuzi yake. Kwamba, katiba ya Zanzibar sasa inatumika kuamua mambo ya muungano. Hapa napo Mkandara anakubaliana na hilo akisema Znz ni sehemu ya Tanzania hivyo ikivunja katiba ni Tanzania siyo znz

Ukimsoma kwa undani, Warioba na tume yake wanasema inasisitiza raia wa pande zote wasibaguliwe wakiwa katika upande mwingine wa muungano.

Akatoa mfano mgonjwa akihamishwa upande mmoja apokelewe kama mgonjwa mwingine wa sehemu ile.Hapa kuna changamoto ambayo wengi wanaweza wasione mantiki yake.

Kwa maneno mengine Warioba anatoa suluhu kuwa sheria za pande zote ziwiane tofauti na mfumo wa sasa.Katika mfumo wa serikali 2 huduma kama afya zinategemea mtu mwenye kitambulisho cha ukazi kule znz. Lakini mzanzibar akija bara kwakwe ni bwerere.

Hii maana yake ni kuwa Watanganyika wanabaguliwa kule znz kama tunavyoona katika mambo ya uchaguzi. Kwamba, mznz ana haki ya kugombea nafasi bara, wakati Mtanganyika hawezi kufanya hivyo znz. Haki hiyo Mkandara anasema ni Tanzania, ingawa Mtanzania hana haki hiyo ZNZ

Kwa mfano wa huduma za afya, Mtanganyika akibaguliwa visiwani itabidi aende wizara ya afya Dar es Salaam kulalamika.

Atakapofika huko atakutana na Waziri wa afya mzanzibar, katibu mkuu au mkurugenzi mzanzibar. Hao ndio watatoa hukumu ya Mtanganyika kwasababu wao ni sehemu ya muungano.
MaAna yake ni sawa na kesi ya Nyani kula mAhindi ya binadamu unampelekea hakimu Ngedere.

Uwepo wa serikali ya Tanganyika utamwezesha Mtanganyika kutetewa na serikali yake dhidi ya ubaguzi ambao hadi sasa upo na unaendele kule znz ukiwalenga Watanganyika na si raia wengine wa ukanda wa Afrika mashariki.

Hivyo tume inasema serikali 3 zitakuwa suluhisho kwasababu kila raia atapata utetezi wa serikali yake tofauti na sasa ambapo utetezi upo kwa mznz na si Mtanzania.

Warioba katika hotuba yake ameonyesha tume mbali mbali na maoni yake.
Tume iliyonisisimua ni ile ya Amina ambayo iliondoa mambo mengi ya muungano hata yale ya mwaka 1964.

Tume hiyo ikaamua mapato ya TRA ya Zanzibar yabaki kule.
Hapa tunapata ukweli kuwa hakuna mapato ya znz yanayovuka bahari na hotuba inakubaliana na maoni ya Prof Humphrey kuhusu uchangiaji sifuri wa znz katika muungano.
Udanganyifu uliofanywa na wznz kuwa wananyonywa sasa unazidi kutufumbua macho.

Wakati mapato ya TRA yakibaki huko, mapato ya TRA Tanzania bara ambayo ni Tanganyika yanatumika kuhudumia shughuli za muungano yakiwemo mambo yote 22.
Hapa ni kuwa kodi za Mtanganyika ndizo kodi za muungano na za mzanzibar ni za huko kwao.

Tume ya Amina ndiyo iliyoondoa bandari na Anga katika yale 11 ya mkataba wa mwaka 1964.
Znz ilifanya hivyo kwasababu inataka kupata mapato.

Ni jambo la ajabu mtu kusema nchi yenye vyanzo vya mapato kama znz haiwezi kuchangia muungano. Pengine haiwezi kuchangia sawa lakini lazima ichangie.

Haiwezekani ichote tu bila kuwa na msaada wa aina yoyote kwa gharama za Mtanganyika.
Hilo litamalizwa kwa serikali 3 kwasababu kila mshirika atasimamia mambo ya nchi yake na hakuna kubebana mgongoni bila sababu za maana au msingi bali mazoea tu.

Hotuba ya Warioba kama haitamfumbua macho Mtanganyika basi itakuwa ni halali mznz kuendelea na unyonyaji na ukupe. Rejeeni hotuba yake muone jinsi gani matatizo yaliyopo yaliyoundiwa tume na yalivyoshindikana kupatiwa suluhu.

Sasa akina Mkandara, Nape na Pinda wanaposema ni marekebisho kidogo bila kutueleza ni kutufanya mazezeta. Marekebisho gani yaliyoshindikana miaka 50 yanayoweza kutatuliwa na kikao kimoja cha bunge la katiba?
 
Nguruvi3
Mkuu umeyasema mengi sana pasipo kunisoma vizuri ukanielewa. Kuna mahala niliposema Artical of Union sio Legal foundation? ama nimesema hii sio swala la kujadili maana wanaolidai ni wafuasi wa Hizbu.
Nilichosema ni kwamba Katiba haiwezi kupunguza ama kuongeza gharama za matumizi ya serikali ama nchi. Ila swala la utawala uliopo, nikiwa na maana ya kwamba tukiirudisha Tanganyika, sisi ndio tunaweza panga wizara zetu kama walivyokwisha fanya Nyerere, Mkapa Mwinyi na hata JK. JK kaongoza ama kaunganisha wizara mara ngapi?, Na wizara ngapi mpya zimezaliwa?. JK kaongeza mikoa, wilaya, majimbo, JK kaongeza serikali za mitaa na kadhalika yote hayo ni gharama za serikali, na hayakuwa maswala ya katiba isipokuwa JK hakuivunja katiba ni ktk wigo wa madaraka yake.

Hayo mengine sintarudia tena kukujibu isipokuwa nakuuliza wewe swali moja tu unambie. Je,Zaire ni nchi au sio nchi? Tuanze na hapo ili turudi ktk mjadala tunakoenda kutatupoteza zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Kwa kuongezea tu nakuomba unisome vizuri sana hapa chini. Katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010 ni jeuri ya Wazanzibar ktk maswala yaliyokuwa kero kwao nasi tukashindwa kuyatatua kwa miaka 46. Na pindi mh. Pinda aliposema Zanzibar sio nchi, ndipo wakaunda UMOJA wao, wakaandika katiba mpya kwa kutafuta majibu yao wenyewe (kuhusu zile kero) kinyume cha sharia.

Lakini kwa mwenye kujua ukweli ni kwamba zile kero za muungano wao waliamua kuzimaliza kwa kujitungia mamlaka hivyo walikiuka katiba ya Muungano lakini pia sisi tulishindwa kutoa suluhu tukitishia kutoa taraka kama hawataki mfumo uliopo. Kero chache zikazaa kero nyingine mpya, hivyo leo tuna kero millioni na suluhu yake sio kuunda Tanzanyika ambayo mnadai ipo, maana nayo itaweka masharti yake vile vile kujibu Wazanzibar na kukiuka katiba ya JMT.

Narudia swali langu:- Zaire ni nchi au sio nchi?
 
Naona haupo mtandaoni ila nitasubiri majibu yako.
swali la 2. Ikiwa sheria namba 24 ya mwaka 1967 ndio iliyoiua Tanganyika. Kwa nini wewe, Mchambuzi na Warioba mnadai kuwa nchi ya Tanganyika ipo? wakati huo huo mnasema hakuna nci ya Zanzibar! naomba utueleze kwa hatua usinirushie maswali miye kwanza jibu.
 
Mkuu Barubaru,

Hapo juu ulinihoji kuhusu uhalali wa mkataba wa muungano kisheria ambapo nilijadili kwamba kwa mujibu wa sheria za kimataifa (not necessarily za kitaifa), mkataba huu ni halali na wenye kutambulika. Suala la uhalali kwa mujibu wa sheria za ndani ya taifa au mataifa shiriki ni controversial kama ulivyojadili, na mimi nitalijadili hili kwa kadri ya uelewa wangu.

Mkataba wa muungano ulikuwa ni international treaty signed na marais wawili wa mataifa mawili ya tanganyika na zanzibar. Chini ya mfumo wa "common law", mfumo ambao ulifuatwa na Tanganyika na Zanzibar na unaendelea hadi sasa, international treaties lazima ziwe ratified na mabunge ya mataifa husika ili kuzipatia "force of law". Katika mkataba wa muungano (1964)ibara ya (viii) inasema hivi:

Mkataba huu utahitaji kuthibitishwa kwa kutungiwa sheria na bunge la Tanganyika na Baraza la mapinduzi la jamhuri ya watu wa zanzibar kwa kushirikiana na baraza lake la mawaziri, na mkataba kupitishwa na kuundwa kwa serikali ya jamhuri ya muungano na ya Zanzibar kwa kufuata masharti yaliyotajwa.

Nikirudi kwenye ibara ya nane ya muungano hapo juu, ibara hii ina umuhimu wa aina mbili:

1. Ratification.
2. Lakini pia unaweka condition kwamba mabunge ya nchi shiriki yaje na sheria zake za kutekeleza mkataba husika - chini ya two governments kwa kuanzia. Lakini kumbuka pia kwamba suala la two government, moja ya znz, nyingine ya JMT ilikuwa ni kwa kipindi cha mpito tu cha mwaka mmoja ambapo marais wa pande mbili ilitakiwa wateue tume ya katiba na baraza la kutunga sheria ili kuja na katiba mpya ya JMT. Wakati hayo yakisubiriwa, mkataba ukasema kwamba katiba ya tanganyika ifanyiwe marekebisho kidogo iwe ni ya JMT, na masuala ya Tanganyika yasiyo ya muungano yawe chini ya rais wa JMT kwa muda huku ya znz yakiwa chini ya znz tofauti na yale kumi na moja ya muungano; kilichofuatia ni uchakachuaji ambao tumeshajadili elsewhere;

Tukirudi kwenye ibara ya nane ya mkataba wa muungano niliyoijadili hapo juu, bunge la Tanganyika lilifanya hayo. Kwa taarifa zilizopo, ndani ya bunge hilo kulikuwepo pia wajumbe kadhaa wa baraza la mapinduzi kina Jumbe n.k, huku wabunge wa Tanganyika waki debate to ratify the bill. Inaelezwa kwamba Nyerere alitoa hotuba fupi sana ya kufungua mjadala akisisitiza uhusiano wa kihistoria baina ya pande hizi mbili na kuonyesha jinsi gani ni ulikuwa ni uhusiano wa kiasili. Akajadili pia malengo ya kupanua muungano huo katika muktadha wa shirikisho la afrika mashariki na kwamba muungano wa Tanzania hautaathiri malengo hayo. Kisha akajikita kujadili sababu za muungano wa Tanganyika na Zanzibar (source: a commemorative special issue of Tanganyika and Zanzibar New Review published by Tanganyika information services):

The union between Tanganyika and zanzibar has to be determined by our two governments for the interrest of africa and african unity. There is no other reason. Unity in our country doesn't have to come via Moscow or Washington. It is an insult to africa to read cold war politics into every move towards african unity. Africa has its own maturity and its own will. Our unity is inspired by a very simple ideology - UNITY. We don't propose this union in order to support any of the 'isms of this world.

Nirudi kwenye controversy ya ratification kwani ni sehemu kubwa ya hoja yako kwangu.

Wakati ratification kwa upande wa Tanganyika ilifanyika kwa mujibu kwa maelekezo ya mkataba wa muungano (1964), upande wa zanzibar hatuwezi kusema hivyo moja kwa moja. Kama ulivyojadili, controversy juu ya ratification iliibuliwa na Wolfang Dourado, mwaka 1983, huyu alikuwa ni mwanasheria mkuu wa serikali znz wakati wa muungano; dourado anasema katika paper yake presented kwa Tanganyika Law Society (1983) kwamba hapakuwa na sheria yoyote ratifying the articles kwenye stature books of znz na pia hapakuwa na sheria yoyote iliyochapishwa kwenye gazeti la serikali znz. Anaendelea kusema kwamba ushahidi uliopo ni kwa upande wa Tanganyika tu kupitia notice ya serikali ya Tanganyika, #243 tarehe 1 May 1964 iliyosainiwa na acting solicitor general wa wakati ule - P.R.N. Fifoot ikisema kwamba sheria to ratify articles ilifanywa na baraza la mapinduzi kwa ushirikiano na baraza la mawaziri. Prof issa Shivji kupitia machapisho yake confirms kwamba hakuna sheria iliyochapishwa kwenye gazeti la serikali znz lakini anasema kwamba - hakuna conclusive evidence kwamba there was no ratification or enactment of the rellevant law. Mzee jumbe nae katika mahojiano yake na Shivji alisema kwamba baraza la mapinduzi halikuwai kutana to ratify the articles.
Barubaru, tukiwa bado na huyu bwana Dourado unayemtumia kama shahidi, Prof haroub othman (katika publications zake) analisemea suala hili hivi:

What is important also is that the union agreement was ratified by both the Tanganyika national assembly and the revolutionary council. Contrary to what Dourado (1983) says, supported by shivji (1990), the Nyalali commission, of which Dourado was a member, was satisfied that the revolutionary council met to ratify the articles of the union (tume ya nyalali, 1992). And khamis abdalah ameir (and babu), the two umma party members who were in the revolutionary council at the time have confirmed that the matter was discussed in the council, and that while there were reservations on the part of some members, these were 'quashed' by abdalah kassim hanga who made an emotional intervention I support of the union. Once the union agreement had been ratified by the legislative bodies in Tanganyika and zanzibar, there was no further requirement in law to make them enforceable

kwa hoja hizi basi, suala la msingi hapa ni kwamba mkataba wa muungano remains to be the legal foundation of the union, katiba mpya haiwezi badili hilo a badala yake ni kutekeleza hayo iwapo nia ni kudumisha muungano wa serikali tatu kama ilivyokubaliwa chini ya mkatana kwani mbili imeshindikana na moja haiwezekani. On the same token, suala la uhalali wa mkataba wa muungano becomes secondary, huku uchakachuaji wa mkataba wa muungano likibakia suala la msingi katika kuweka sawa nia na historia ya muungano husika.

Cc JokaKuu, Mkandara, Nguruvi3, Pasco

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Hiki kitu kinachoitwa legal foundation wengi hawataki kukijadili kwasababu kinaondoa dhana ya serikali 2. Lakini basi tukiuliza kama legal foundation ni dhana mbaya, watuambie msingi wa serikali 2 ni upi. Hakuna jibu, wanataka tuamini tu kuwa ilikuwa serendipity hivyo tuendelee tu kibubusa kama ilivyotokea.

Serikali 1 imeshindikana, 2 zina matatizo yasiyo na suluhu. Where do we go from here!
Serikali 3, in worst case scenario vunja jahazi
 
Mkuu Barubaru,

Hapo juu ulinihoji kuhusu uhalali wa mkataba wa muungano kisheria ambapo nilijadili kwamba kwa mujibu wa sheria za kimataifa (not necessarily za kitaifa), mkataba huu ni halali na wenye kutambulika. Suala la uhalali kwa mujibu wa sheria za ndani ya taifa au mataifa shiriki ni controversial kama ulivyojadili, na mimi nitalijadili hili kwa kadri ya uelewa wangu.

Mkataba wa muungano ulikuwa ni international treaty signed na marais wawili wa mataifa mawili ya tanganyika na zanzibar. Chini ya mfumo wa "common law", mfumo ambao ulifuatwa na Tanganyika na Zanzibar na unaendelea hadi sasa, international treaties lazima ziwe ratified na mabunge ya mataifa husika ili kuzipatia "force of law". Katika mkataba wa muungano (1964)ibara ya (viii) inasema hivi:

Nikirudi kwenye ibara ya nane ya muungano hapo juu, ibara hii ina umuhimu wa aina mbili:

1. Ratification.
2. Lakini pia unaweka condition kwamba mabunge ya nchi shiriki yaje na sheria zake za kutekeleza mkataba husika - chini ya two governments kwa kuanzia. Lakini kumbuka pia kwamba suala la two government, moja ya znz, nyingine ya JMT ilikuwa ni kwa kipindi cha mpito tu cha mwaka mmoja ambapo marais wa pande mbili ilitakiwa wateue tume ya katiba na baraza la kutunga sheria ili kuja na katiba mpya ya JMT. Wakati hayo yakisubiriwa, mkataba ukasema kwamba katiba ya tanganyika ifanyiwe marekebisho kidogo iwe ni ya JMT, na masuala ya Tanganyika yasiyo ya muungano yawe chini ya rais wa JMT kwa muda huku ya znz yakiwa chini ya znz tofauti na yale kumi na moja ya muungano; kilichofuatia ni uchakachuaji ambao tumeshajadili elsewhere;

Tukirudi kwenye ibara ya nane ya mkataba wa muungano niliyoijadili hapo juu, bunge la Tanganyika lilifanya hayo. Kwa taarifa zilizopo, ndani ya bunge hilo kulikuwepo pia wajumbe kadhaa wa baraza la mapinduzi kina Jumbe n.k, huku wabunge wa Tanganyika waki debate to ratify the bill. Inaelezwa kwamba Nyerere alitoa hotuba fupi sana ya kufungua mjadala akisisitiza uhusiano wa kihistoria baina ya pande hizi mbili na kuonyesha jinsi gani ni ulikuwa ni uhusiano wa kiasili. Akajadili pia malengo ya kupanua muungano huo katika muktadha wa shirikisho la afrika mashariki na kwamba muungano wa Tanzania hautaathiri malengo hayo. Kisha akajikita kujadili sababu za muungano wa Tanganyika na Zanzibar (source: a commemorative special issue of Tanganyika and Zanzibar New Review published by Tanganyika information services):

Nirudi kwenye controversy ya ratification kwani ni sehemu kubwa ya hoja yako kwangu.

Wakati ratification kwa upande wa Tanganyika ilifanyika kwa mujibu kwa maelekezo ya mkataba wa muungano (1964), upande wa zanzibar hatuwezi kusema hivyo moja kwa moja. Kama ulivyojadili, controversy juu ya ratification iliibuliwa na Wolfang Dourado, mwaka 1983, huyu alikuwa ni mwanasheria mkuu wa serikali znz wakati wa muungano; dourado anasema katika paper yake presented kwa Tanganyika Law Society (1983) kwamba hapakuwa na sheria yoyote ratifying the articles kwenye stature books of znz na pia hapakuwa na sheria yoyote iliyochapishwa kwenye gazeti la serikali znz. Anaendelea kusema kwamba ushahidi uliopo ni kwa upande wa Tanganyika tu kupitia notice ya serikali ya Tanganyika, #243 tarehe 1 May 1964 iliyosainiwa na acting solicitor general wa wakati ule - P.R.N. Fifoot ikisema kwamba sheria to ratify articles ilifanywa na baraza la mapinduzi kwa ushirikiano na baraza la mawaziri. Prof issa Shivji kupitia machapisho yake confirms kwamba hakuna sheria iliyochapishwa kwenye gazeti la serikali znz lakini anasema kwamba - hakuna conclusive evidence kwamba there was no ratification or enactment of the rellevant law. Mzee jumbe nae katika mahojiano yake na Shivji alisema kwamba baraza la mapinduzi halikuwai kutana to ratify the articles.
Barubaru, tukiwa bado na huyu bwana Dourado unayemtumia kama shahidi, Prof haroub othman (katika publications zake) analisemea suala hili hivi:

kwa hoja hizi basi, suala la msingi hapa ni kwamba mkataba wa muungano remains to be the legal foundation of the union, katiba mpya haiwezi badili hilo a badala yake ni kutekeleza hayo iwapo nia ni kudumisha muungano wa serikali tatu kama ilivyokubaliwa chini ya mkatana kwani mbili imeshindikana na moja haiwezekani. On the same token, suala la uhalali wa mkataba wa muungano becomes secondary, huku uchakachuaji wa mkataba wa muungano likibakia suala la msingi katika kuweka sawa nia na historia ya muungano husika.

Cc JokaKuu, Mkandara, Nguruvi3, Pasco

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

MCHAMBUZI,

Naona unaogelea kwenye maneno yangu na kukubali yale niliyobainisha. lakin mimi nimechambua hilo la Muungano kwa kutumia International Law (sharia za kimataifa) ambazo nchi zozote zikitaka kuungana zinafuta.

Lakin kumbuka huyo Dourado ndio aliyekuwa mwanasharia mkuu wa Znz kwa wakti huo. Nikuulize je unaweza fanya jambo kubwa kama hilo la muungano bila kumshirikisha mwanasharia mkuu.
JE UNAJUA KWANINI DOURADO AKUSHIRIKISHWA?

NAONA UMEJICHANGANYA KATIKA NENO Ratification. Hebu nisome tartiibu nilivyobainisha.

hizo articles of union!.

Articles zile japo zilikosa sifa ya kisharia ya kuitwa mkataba "contract" kutokana na tatizo la kisharia liitwalo "privity of contract", articles zile zilikuwa na sifa zote za kuitwa ' international treaty" kuunganisha nchi mbili, na ili any international treaty kupata uhalali na nguvu ya kisharia, ni lazima treaty hiyo iwe ratified na mabunge ya nchi husika!.

Ratification is a process ambayo hufanywa kwa procedures maalum na kufanywa in writing!.

Bunge la Tanzania lilifuata sheria, taratibu na kanuni zote ku ratify zile articles of union kwa maandishi!.
Zanzibar, walikuwa ndio kwanza wametoka kwenye mapinduzi, hivyo hawakuwa na bunge, Baraza la Mapinduzi ndilo lililokuwa kila kitu!. Lilipaswa kuziridhia zile articles of union kwa ratification ambayo hufanywa kwa maandishi!. Vikao vyote vya BLM vina hansard, lakini hilo halikufanyika na hakuna kumbukumbu yoyote ya maandishi kwamba ratification ilifanyika!.

LABDA NIKUULIZE HIVI KWANINI MPAKA LEO BLW HAWAJAPELEKEWA HUO MKATANBA KUURIDHIA ILI MUUNGANO UWE HALALI KWA UPANDE WA ZNZ?.
Je kuna siri gani ndanimwe?
 
Nilibainisha huko nyuma katika moja ya mada zangu kuwa NDOTO YA ABOUD JUMBE ITATIMIA.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...imia-zanzibar-huru-hiyoooo-6.html#post8921116

Kulekea miaka 50 ya Mapinduzi Znz, kuna kila dalili ya kutimia kwa ndoto ya Mzee Aboud Jumbe kuhusu kupatikana na Zanzibar Huru na kuanzishwa kwa Serikali ya Tanganyika.

Pamoja na jitihada kuubwa ya JK Nyerere kupinga kwa nguvu zake zote kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika pamoja na mitikisiko yote lakin leo tunadhibitisha Nia na ndoto ya Mzee Aboud Jumbe na Kikwete na G55 zinakaribia kutimia kwa kuanza kuundwa kwa Serikali ya Tanganyyika na wakati huo huo kuundwa kwa Zanzibar Huru.

Kwa wasiojua ngoja niwape kidogo namna Nyerere alivyoweza kutumia nguvu nyingi sana katika uhai wake hapa Duniyani kupinga kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika .Je alikuwa na agenda gani na Serikali ya Tanganyika?

Mdahalo wa kwanza juu ya mfumo na muundo wa Muungano ulianza kwa njia ya maoni juu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano mwaka 1983/84. Hapo, kwa mara ya kwanza ilibainika kuwa viongozi wa juu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, wakiongozwa na Rais Aboud Jumbe, na wale wa Serikali ya Tanzania, wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mwalimu Julius Nyerere, walikuwa na mitazamo tofauti inayokinzana juu ya Muungano.

Jumbe na timu yake walitaka Muungano uwe na Serikali tatu kwa maana ya Serikali ya Tanganyika, Serikali ya Zanzibar (iliyopo sasa) na Serikali ya Muungano yenye kushughulikia mambo ya Muungano tu, ambayo yameainishwa katika Ibara ya 6(a) ya Katiba ya Muungano (Articles of Union) na kifungu cha 8 cha Sheria ya Muungano (Acts of Union) Namba 22 ya 1964, na hatimaye ibara ya 4 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977.

Jumbe alikwenda mbali zaidi kwa kuandaa Hati ya Maombi ya kuhoji na kutaka ufafanuzi kwenye Mahakama Maalum ya Kikatiba juu ya muundo sahihi wa Muungano kwa kutumia ibara ya 125 ya Katiba.
Tofauti hizi kati yake na Mwalimu hazikwisha salama kwa Jumbe kuthubutu kukanyaga mahali "patakatifu" bila kuvua viatu. Jumbe alilazimishwa kuachia ngazi zote za uongozi wa nchi kuanzia Urais wa Zanzibar, Umakamu wa Rais wa Muungano, na nafasi zote za kichama Januari, 1984.

Naielewa vizuri hali ya mtafaruku iliyofuatia hatua hii na kule kutangazwa "kuchafuka" kwa hali ya kisiasa Visiwani, kwani nilikuwa mmoja wa Watanzania ulioishuhudia hali hiyo iliyokuwa imetengenezwa na JKN. Lakini pamoja na kurejea kwa hali ya kawaida, bado matatizo ya Muungano yaliendelea kutawala agenda za vikao vingi vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.

Utata huu uliibuka tena kwa nguvu mpya zaidi wakati Wabunge 55 (maarufu kama G55) wa Bunge la Muungano, walipowasilisha bungeni mwaka 1993, hoja ya kutaka kuundwa/kurejeshwa kwa Serikali ya Tanganyika kwa kukasirishwa na hatua ya Zanzibar kujiunga na OIC kama nchi huru nje ya Muungano, Desemba 1, 1992.
Ukweli, Bunge lilikuwa limekwisha kupitisha kwa kauli moja, Azimio la kuanzishwa kwa Serikali ya Tanganyika Agosti 24, 1993 kwa maana ya kuwa na Serikali ya Muungano inayoundwa na Serikali hai zenye Mamlaka huru, za Tanganyika na Zanzibar, kama vile tu alivyotaka Rais Jumbe mwaka 1983.
Hata hivyo, Azimio hilo lilipigwa rungu zito na Mwalimu Nyerere na likavunjika.. Na kama ilivyokuwa kwa Jumbe, hapa napo mambo hayakuisha salama; safari hii Waziri Mkuu wa wakati ule, John Malecela na Katibu Mkuu wa CCM, Horace Kolimba, walipoteza nyadhifa zao kwa sababu ya ama kunyamazia au kuunga mkono hoja / Azimio la G 55.

Sasa ni wakti muafaka wananchi wa Tz kuamua kusuka au kunyoa na hapa ndio mtamuona nani mnafiki?

kuelekea miaka 50 ya mapinduzi ya Znz naona Zanzibar huru ileeeeeeeeee. Na Serikali ya Tanganyika hiyoooo.

Mkandara,

Siku zote watu wanapokaa kitako kuanza kuujadili MUUNGANO wengi sana kutoka upande wa Tanganyika wanakuwa wa kwanza kabisa kuionea huruma ZNZ ikiwa pamoja na kuipitia historia yake wakti munasahau kuwa ya kwenu ni khatari sana.

Nafikiri suala la kwanza mlitakiwa mjiulize KWANINI NYERERE ALIFUNGA SAFARI KWENDA ZNZ KUMUOMBA KARUME WAUNGANISHA NCHI HIZO?

Hapa pana siri kubwa sana kwa Nyerere kwani aliona nchi yake ina matatizo kiasi kikubwa sana na suluhisho ilikuwa ni kuungana na ZNZ. Na ndio maana alikubali kwa nia moja nchi yake wakti ule ikiwa na watu zaidi ya milioni 18 kuungana PASU KWA PASU na nchi yenye watu chini ya laki tatu.

Lakin kubwa zaidi bila kusema uwongo na kuwa wanafiki LAAZIMA MUKUBALI KUWA MUUNGANO WENU NI WA MATAKWA YA VIONGOZI NA SIO WANANCHI NA UNALINDWA KWA GHARAMA KUBWA SANA KIASI CHA KULETA KHOFU NA KUTO KUAMINIANA MIONGONI MWA WANANCHI WA NCHI HIZO.

Waarabu tuna usemi " IN ORDER TO BUILD SOMETHING STRONG IT HELPS TO START WITH BEST AND POSSIBLE MATERIALS"

Sasa nilibainisha hapo awali kuwa MUUNGANO ULIKUWA WA MAGUMASHI NA HAUKUFUATA SHARIA ZA KIMATAIFA. HIVYO lazima mpate shida kwani NYUMBA NI MSINGI. Ndio maana hata katika bunge lenu la KATIBA unaona wazi limetawaliwa na KHOFU NA UWOGA MKUBWA kuhusu MUUNGANO.

SASA msingi mkubwa hapo NI KUUVUNJA KISHA KUREJESHA KWA WANANCHI WAAMUE KAMA WANAUTAKA AU LAA. NA WA AINA GANI KAMA WATAUTAKA. Hakuna jinsi hapo lazima maamuzi ya wananchi yahishimiwe.

Enzi za kuogopa kuujadili muungano zimepitwa na wakti. NI VIZURI MUBADILIKE. ACHENI UWOGA

[/QUOTE Barubaru,

maswali yako yote yanaonyesha huna majibu wala hujui ilitokana vipi ila unatafuta kujua. Kwa maana hiyo huna elimu ya historia ya Mapinduzi na kwa nini Mapinduzi yalitakiwa ama yaliandaliwa. Sijui kama unakumbuka kwamba siku ile ya mapinduzi kuna picha zinaonyesha Abrahman Babu akiwasili nchini kutoka Cuba, sasa ilikuwaje akajua ni siku hiyo alitakiwa kuwepo Zanzibar.

Pili, wasikilize Karume na Abdurahman Babu walipokuwa wakimtambulisha John Okello baada ya Mapinduzi, utajua hayaMapinduzi yaliandaliwa mapema kabla, na huko nyuma nimekuonyesha mkutano wa Panafrika ulofanyika Mwanza wakimtaka Shamte aungane na ASP, yeye aliporudi Znz tu akawageuka bila kujua kwamba wenzake walikuwa na plan B.

Harakati za Ukombozi wa Afrika zilikwenda sambamba na UMOJA wa nchi huru za Kiafrika, kilichofuata baadaye ni sura kamili ya viongozi wa Kiafrika ambao UNAFIKI ndio sifa yetu kubwa. Labda nikwambie tu ya kwamba Nyerere alimkuta Karume tayari akishirikiana na TAA ya Tanganyika hivo swala la yeye kushirikiana na Karume ilitokana na utaratibu wa uongozi maana alikuwa mwenyekiti wa TANU na pia rais wa kwanza wa Tanganyika huru.

Kwa nini Nyerere alikwenda Zanzibar, haina maana kwamba swala hili halikuzungumzwa kabla ila kuliweka bayana ndipo lilitokea zanzibar. Ni sawa na wewe kwenda peleka uchumba kwa wazazi wa mtoto wa kike haina maana ndio kwanza wewe na mwanamke huyo ndio mnawasiliana. Huwa tayari mmeshakutana na pengine hata kumaliza ndoa kimjini. Muungano ulisha pangwa mapema, rudia hotuba ya Nyerere alipokuwa Ghana kuunganisha Afrika kwa hatua. Tayari iliisha julikana kinachofuata pengine ingekuwa EAC kama sii Idd Amin kutuvuruga.

Na ndio maana Artical of Union ilionekana kuandikwa ktk muda mfupi sana jambo ambalo linawashangaza wataalam. Ukweli ni kwamba vitu vyote vilikwisha andaliwa na ndio maana Karume na babu walokuwa maadui walisimama kutambulisha Zanzibar mpya mara tukashtukizwa na Muungano.

Muungano wetu ni matakwa ya viongozi ndiyo, kwani kuna muungano gani usokuwa matakwa ya viongozi? wengine wamepigwa vita na kulazimishwa kuungana kama mateka itakuwa sisi, tazama States za Marekani, Hiyo Uingereza, Russia na kadhalika kote huko ni viongozi walounda miungano ya nchi zao hakuna hata mmoja ulopitia maoni ya wananchi isipokuwa labda hizo jumuiya ama shirikisho kama EU.

Mimi sipendi kurudia vitu, Mapinduzi yalikuwa halali na muungano ulikuwa halali kama ulivyo Uhuru wa Kenya. Huwezi kusema Kenya sio Huru kwa sababu walipigana vita na kuua watu pasipo ridhaa ya wananchi. Ujinga huo sina muda wa kuuendekeza. Kama hamuupendi Muungano pigeni kura za refendum. Niliwahi kumwambia Hamad Sharrif alipokuja huku kabla ya uchaguzi wa mwaka 2000 - wapeni wananchi fursa wachague kusuka ama kunyoa, wanautaka muungano waseme NDIO wasioutaka waseme HAPANA. akanyamaza kimyaaa kumbe ni mganga njaa tu akilishwa kidogo hana mdomo.

Acheni hizo mkuu wangu Muungano utalindwa kwa nguvu zote na wala sifanyi hivi kwa kuitetea CCM ila maslahi na ya nchi yetu kinyume kabisa cha matakwa ya chama changu.

MKANDARA,

Naona unajiviringisha na kukatataa kutoa historia ya Tanganyika iliyomfanya Nyerere aende Znz kuomba muungano.

LABDA KWA AKILI YA KAWAIDA KABISA INAWEZEKANA VIPI NCHI YENYE UKUBWA WA 885,800 SQ KM NA WATU ZAIDI YA MILIONI 18 WAKTI HUO KUUNGANA NA NCHI YENYE UKUBWA WA 2,000 SQ KM NA WATU CHINI YA LAKI MBILI. MUUNGANO WA 50/50
?

JE NCHI hiyo kubwa inanufaika nini hapo?

Je unataka tuiweke hadhwarani kilichomsukuma Nyerere kwenda Znz kuomba Muungano?

Pole sana lakin kumbuka historia HAIFICHIKI IPO KAMA PEMBE LA NG'OMBE. ATHARI ZAKE NADHANI SASA ZIMEANZA KUCHOMOZA HUKO TGK.

JE unajuwa kwanini Bunge lenu la Katiba limejaa khofu kubwa sana na kutoaminiana linapojadili MUUNGANO?

ZNZ HURU ILEEEEEEEEEEE NA TGK HURU ILEEEEEEEE. pOLE SANA

Hiki kitu kinachoitwa legal foundation wengi hawataki kukijadili kwasababu kinaondoa dhana ya serikali 2. Lakini basi tukiuliza kama legal foundation ni dhana mbaya, watuambie msingi wa serikali 2 ni upi. Hakuna jibu, wanataka tuamini tu kuwa ilikuwa serendipity hivyo tuendelee tu kibubusa kama ilivyotokea.

Serikali 1 imeshindikana, 2 zina matatizo yasiyo na suluhu. Where do we go from here!
Serikali 3, in worst case scenario vunja jahazi

Nguruvi3,

Naungana na wewe. SULUHU YA MUUNGANO NI KUUVUNJA KWANI UPO KWA MASLAHI YA VIONGOZI WA NCHI HIZO MBILI NA WALA SIO MUUNGANO WA WANANCHI.Na ndio maana unazua kuogopana na kutoaminiana baina ya wananchi wa nchi hizo mbili huru.

Kama inatengenezwa KATIBA ya WANANCHI na Muungano ni lazima uwe wa WANANCHI. hivyo hakuna jinsi hapo kwani kufanya lolote kuhusu hilo ni sawa na KUJENGA GHOLOFA KATIKATI BARAFU.

Nakuunga mkono Nguruvi3.

MCHAMBUZI,

Naona unaogelea kwenye maneno yangu na kukubali yale niliyobainisha. lakin mimi nimechambua hilo la Muungano kwa kutumia International Law (sharia za kimataifa) ambazo nchi zozote zikitaka kuungana zinafuta.

Lakin kumbuka huyo Dourado ndio aliyekuwa mwanasharia mkuu wa Znz kwa wakti huo. Nikuulize je unaweza fanya jambo kubwa kama hilo la muungano bila kumshirikisha mwanasharia mkuu. JE UNAJUA KWANINI DOURADO AKUSHIRIKISHWA?

NAONA UMEJICHANGANYA KATIKA NENO Ratification. Hebu nisome tartiibu nilivyobainisha.

hizo articles of union!.

Articles zile japo zilikosa sifa ya kisharia ya kuitwa mkataba "contract" kutokana na tatizo la kisharia liitwalo "privity of contract", articles zile zilikuwa na sifa zote za kuitwa ' international treaty" kuunganisha nchi mbili, na ili any international treaty kupata uhalali na nguvu ya kisharia, ni lazima treaty hiyo iwe ratified na mabunge ya nchi husika!.

Ratification is a process ambayo hufanywa kwa procedures maalum na kufanywa in writing!.

Bunge la Tanzania lilifuata sheria, taratibu na kanuni zote ku ratify zile articles of union kwa maandishi!.
Zanzibar, walikuwa ndio kwanza wametoka kwenye mapinduzi, hivyo hawakuwa na bunge, Baraza la Mapinduzi ndilo lililokuwa kila kitu!. Lilipaswa kuziridhia zile articles of union kwa ratification ambayo hufanywa kwa maandishi!. Vikao vyote vya BLM vina hansard, lakini hilo halikufanyika na hakuna kumbukumbu yoyote ya maandishi kwamba ratification ilifanyika!.

LABDA NIKUULIZE HIVI KWANINI MPAKA LEO BLW HAWAJAPELEKEWA HUO MKATANBA KUURIDHIA ILI MUUNGANO UWE HALALI KWA UPANDE WA ZNZ.
Je kuna siri gani ndanimwe

Mimi kuogelea katika hoja yako ni sawa kwani najadili hoja yako; suala la sheria za kimataifa kwa uelewa wangu finyu ndio kama nilivyojadili, zaidi ya hapo ni mimi kujifunza zaidi juu ya unayoyasema katika muktadha huo;

Tukirudi kwa Dourado kwanini haujadili hoja ya prof haroub othman kama nilivyoiwasilisha?

Kuhusu mkataba wa muungano, shein alishasema nakala ipo ikulu zanzibar, kwahiyo suala la mkataba kutopelekwa kwa BLW wamhoji rais wao wa moja ya nchi shiriki za muungano kwanini anaubania ikulu.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Nilibainisha huko nyuma katika moja ya mada zangu kuwa NDOTO YA ABOUD JUMBE ITATIMIA.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...imia-zanzibar-huru-hiyoooo-6.html#post8921116

Kulekea miaka 50 ya Mapinduzi Znz, kuna kila dalili ya kutimia kwa ndoto ya Mzee Aboud Jumbe kuhusu kupatikana na Zanzibar Huru na kuanzishwa kwa Serikali ya Tanganyika.

Pamoja na jitihada kuubwa ya JK Nyerere kupinga kwa nguvu zake zote kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika pamoja na mitikisiko yote lakin leo tunadhibitisha Nia na ndoto ya Mzee Aboud Jumbe na Kikwete na G55 zinakaribia kutimia kwa kuanza kuundwa kwa Serikali ya Tanganyyika na wakati huo huo kuundwa kwa Zanzibar Huru.

Kwa wasiojua ngoja niwape kidogo namna Nyerere alivyoweza kutumia nguvu nyingi sana katika uhai wake hapa Duniyani kupinga kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika .Je alikuwa na agenda gani na Serikali ya Tanganyika?

Mdahalo wa kwanza juu ya mfumo na muundo wa Muungano ulianza kwa njia ya maoni juu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano mwaka 1983/84. Hapo, kwa mara ya kwanza ilibainika kuwa viongozi wa juu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, wakiongozwa na Rais Aboud Jumbe, na wale wa Serikali ya Tanzania, wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mwalimu Julius Nyerere, walikuwa na mitazamo tofauti inayokinzana juu ya Muungano.

Jumbe na timu yake walitaka Muungano uwe na Serikali tatu kwa maana ya Serikali ya Tanganyika, Serikali ya Zanzibar (iliyopo sasa) na Serikali ya Muungano yenye kushughulikia mambo ya Muungano tu, ambayo yameainishwa katika Ibara ya 6(a) ya Katiba ya Muungano (Articles of Union) na kifungu cha 8 cha Sheria ya Muungano (Acts of Union) Namba 22 ya 1964, na hatimaye ibara ya 4 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977.

Jumbe alikwenda mbali zaidi kwa kuandaa Hati ya Maombi ya kuhoji na kutaka ufafanuzi kwenye Mahakama Maalum ya Kikatiba juu ya muundo sahihi wa Muungano kwa kutumia ibara ya 125 ya Katiba.
Tofauti hizi kati yake na Mwalimu hazikwisha salama kwa Jumbe kuthubutu kukanyaga mahali “patakatifu” bila kuvua viatu. Jumbe alilazimishwa kuachia ngazi zote za uongozi wa nchi kuanzia Urais wa Zanzibar, Umakamu wa Rais wa Muungano, na nafasi zote za kichama Januari, 1984.

Naielewa vizuri hali ya mtafaruku iliyofuatia hatua hii na kule kutangazwa “kuchafuka” kwa hali ya kisiasa Visiwani, kwani nilikuwa mmoja wa Watanzania ulioishuhudia hali hiyo iliyokuwa imetengenezwa na JKN. Lakini pamoja na kurejea kwa hali ya kawaida, bado matatizo ya Muungano yaliendelea kutawala agenda za vikao vingi vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.

Utata huu uliibuka tena kwa nguvu mpya zaidi wakati Wabunge 55 (maarufu kama G55) wa Bunge la Muungano, walipowasilisha bungeni mwaka 1993, hoja ya kutaka kuundwa/kurejeshwa kwa Serikali ya Tanganyika kwa kukasirishwa na hatua ya Zanzibar kujiunga na OIC kama nchi huru nje ya Muungano, Desemba 1, 1992.
Ukweli, Bunge lilikuwa limekwisha kupitisha kwa kauli moja, Azimio la kuanzishwa kwa Serikali ya Tanganyika Agosti 24, 1993 kwa maana ya kuwa na Serikali ya Muungano inayoundwa na Serikali hai zenye Mamlaka huru, za Tanganyika na Zanzibar, kama vile tu alivyotaka Rais Jumbe mwaka 1983.
Hata hivyo, Azimio hilo lilipigwa rungu zito na Mwalimu Nyerere na likavunjika.. Na kama ilivyokuwa kwa Jumbe, hapa napo mambo hayakuisha salama; safari hii Waziri Mkuu wa wakati ule, John Malecela na Katibu Mkuu wa CCM, Horace Kolimba, walipoteza nyadhifa zao kwa sababu ya ama kunyamazia au kuunga mkono hoja / Azimio la G 55.

Sasa ni wakti muafaka wananchi wa Tz kuamua kusuka au kunyoa na hapa ndio mtamuona nani mnafiki?

kuelekea miaka 50 ya mapinduzi ya Znz naona Zanzibar huru ileeeeeeeeee. Na Serikali ya Tanganyika hiyoooo.

Mkuu Barubaru, nilikusoma katika uzi husika ila sikupata nafasi ya kuchangia. Kwa hoja zako kule na hapa, je hauoni kwamba you are self contradictory ambapo upande mmoja unajadili kwamba mkataba wa muungano hauna halali lakini kwa upande wa pili unamuunga mkono jumbe ambae anauheshimu mkataba lakini tatizo kwake ni uchakachuaji mara baada ya nyerere na karume kurudisha kalamu zao mfukoni?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
MKANDARA,

Naona unajiviringisha na kukatataa kutoa historia ya Tanganyika iliyomfanya Nyerere aende Znz kuomba muungano.

LABDA KWA AKILI YA KAWAIDA KABISA INAWEZEKANA VIPI NCHI YENYE UKUBWA WA 885,800 SQ KM NA WATU ZAIDI YA MILIONI 18 WAKTI HUO KUUNGANA NA NCHI YENYE UKUBWA WA 2,000 SQ KM NA WATU CHINI YA LAKI MBILI. MUUNGANO WA 50/50
?

JE NCHI hiyo kubwa inanufaika nini hapo?

Je unataka tuiweke hadhwarani kilichomsukuma Nyerere kwenda Znz kuomba Muungano?

Pole sana lakin kumbuka historia HAIFICHIKI IPO KAMA PEMBE LA NG'OMBE. ATHARI ZAKE NADHANI SASA ZIMEANZA KUCHOMOZA HUKO TGK.

JE unajuwa kwanini Bunge lenu la Katiba limejaa khofu kubwa sana na kutoaminiana linapojadili MUUNGANO?

ZNZ HURU ILEEEEEEEEEEE NA TGK HURU ILEEEEEEEE. pOLE SANA

Hongkong ni sehemu Ya China au sio,Je New York ina ukubwa sawa na Michigan au sivyo...haya maswala ya ukubwa wa nchi yametoka wapi? kuna nchi gani duniani zilizoungana ambazo zina ukubwa sawa iwe wa watu ama eneo?... Mbona unataka kuleta habari za Kibasha mkuu wangu ya kwamba mwanamme asili yake amuoe mwanamme mwenzake maana ndio wanafanana kwa umbo na kulingana nguvu! ahaha haha! haha! acha hizi habari.
 
Mimi kuogelea katika hoja yako ni sawa kwani najadili hoja yako; suala la sheria za kimataifa kwa uelewa wangu finyu ndio kama nilivyojadili, zaidi ya hapo ni mimi kujifunza zaidi juu ya unayoyasema katika muktadha huo;

Tukirudi kwa Dourado kwanini haujadili hoja ya prof haroub othman kama nilivyoiwasilisha?

Kuhusu mkataba wa muungano, shein alishasema nakala ipo ikulu zanzibar, kwahiyo suala la mkataba kutopelekwa kwa BLW wamhoji rais wao wa moja ya nchi shiriki za muungano kwanini anaubania ikulu.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Mchambuzi,

Kwa kukusaidia tu hapa NAKWAMBIA MUUNGANO UPO KWA AJILI YA TGK TU NA SIO ZNZ.

Kwa mantiki hiyo Znz wana haki kisharia kufanya lolote bila kuvunja KATIBA YA JMTz na ndio maana kwa kutumia udhaifu huo walifanya marekebisho makubwa sana ya KATIBA YA ZNZ mwaka 2010.Na JMTz haikuweza kufanya lolote.

Ahali yangu hiyo ndio SHARIA ukikosea tu inakuadhibu.

Mtalalamika na kunung'unika lakin huo ndio ukweli Poleni sana.

Mkuu Barubaru, nilikusoma katika uzi husika ila sikupata nafasi ya kuchangia. Kwa hoja zako kule na hapa, je hauoni kwamba you are self contradictory ambapo upande mmoja unajadili kwamba mkataba wa muungano hauna halali lakini kwa upande wa pili unamuunga mkono jumbe ambae anauheshimu mkataba lakini tatizo kwake ni uchakachuaji mara baada ya nyerere na karume kurudisha kalamu zao mfukoni?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Mchambuzi,
Je ulimsikia Mh Warioba jana Mjengoni akiunguruma?
Znz huru ileeeeeeeeee na ndoto ya Jumbe insha'Allah itatimia. Tumuomuombee uhai mzee wetu huyu aione Znz huru na TGK huru.

Hongkong ni sehemu Ya China au sio,Je New York ina ukubwa sawa na Michigan au sivyo...haya maswala ya ukubwa wa nchi yametoka wapi? kuna nchi gani duniani zilizoungana ambazo zina ukubwa sawa iwe wa watu ama eneo?... Mbona unataka kuleta habari za Kibasha mkuu wangu ya kwamba mwanamme asili yake amuoe mwanamme mwenzake maana ndio wanafanana kwa umbo na kulingana nguvu! ahaha haha! haha! acha hizi habari.

Mkandara.

Wachumi wanasema hakuna Muungano pasipo manufaa kwa wanao ungana. Hata katika ndoa tunaambiwa tunapata manufaa ya mapenzi na kuhurumiana baina ya wanandoa.

Je katika muungano huo wa 50/50 Tgk inanufaika kwa lipi?

Mimi kuogelea katika hoja yako ni sawa kwani najadili hoja yako; suala la sheria za kimataifa kwa uelewa wangu finyu ndio kama nilivyojadili, zaidi ya hapo ni mimi kujifunza zaidi juu ya unayoyasema katika muktadha huo;

Tukirudi kwa Dourado kwanini haujadili hoja ya prof haroub othman kama nilivyoiwasilisha?

Kuhusu mkataba wa muungano, shein alishasema nakala ipo ikulu zanzibar, kwahiyo suala la mkataba kutopelekwa kwa BLW wamhoji rais wao wa moja ya nchi shiriki za muungano kwanini anaubania ikulu.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

MCHAMBUZI

Kumfananisha Dourado na al marhum Prof Haroub Othman Miraji ni sawa na kufananisha chumvi na sukari.

Dourado alikuwa mwanasharia mkuu wa Znz wakti wa Mvungano ambapo mchakato huo wa muungano ulimruka na kumuweka pembeni japo alikuwa mwanasharia mkuu.

Prof Haroub yeye alikuwa mwanazuoni maarufu lakin hakuwa na a madaraka yoyote ya kiserikali kule Znz.

sasa kila mtu ana uzito wake hapo LAKIN DOURADO ANA UZITO ZAIDI KATIKA KADHIA HII.

JE UNAWEZA KUNIAMBIA KWANINI DOURADO HAKUSHIRIKISHWA KATIKA MCHAKATO WA MUUNGANO?

Back
Top Bottom