Duru za siasa: Bunge la Katiba, upotoshaji na kiwewe cha kuzinduka Tanganyika

Duru za siasa: Bunge la Katiba, upotoshaji na kiwewe cha kuzinduka Tanganyika

UPOTOSHAJI UNAENDELEA
KILA SIKU KUNA JAMBO JIPYA

Katika dhamira ya kweli ya kuandika katiba ya taifa hakuna sababu za kupotosha.
Katiba ni nyaraka kila mwananchi, kwanini kundi CCM linaelekeza nguvu za upotoshaji na si ujenzi wa hoja?

Hoja ya serikali 3 na gharama imekosa mashiko. Imekosa kwasababu hakuna mtu au watu kutoka S2 wanaoweza kuweka hesabu mezani na kusema zina nafuu kuliko 3.

Hoja imekosa mashiko kwa ukweli, kila siku tunaongeza mikoa na wilaya ikiwa ni sehemu ya ongezeko la gharama.Kuna hoja ya jinsi gani mapesa yanapotea serikalini na mashirika ya umma kwa taarifa za CAG bila wahusika kujulikana.

Mathalan, hadi sasa hakuna anayejua bilioni 27 za rada zilitokaje hazina na nani walihusika.

Mfano wa pili, tunawezaje kulipa milioni 150 kwa siku kwa kampuni moja izalishe au isizalishe umeme halafu tukadai serikali 3 zenye shirikisho ni gharama.

Upotoshaji unaofanyika ni kuzifanya serikali 3 kwa ujumla.
Ukweli ni kuwa ndani ya muundo wa S3 serikali tunaongelea serikali ya Shirikisho tu yenye mambo 7.

Hapa napo wahuni wanakwepa ukweli kuwa ni shirikisho ili kujenga hoja ya S3 ni mzigo.
Hivi mambo 7 yanawezaje kuwa ghali kuliko mambo 22 ya sasa?

Katika mazingaombwe, watu wanasema S3 ni mzigo, si kweli ni upotoshaji.
Tuongelee Serikali ya shirikisho, hizo mbili kila mmoja atajua utaratibu wa kudhibiti gharama zake.

Upotoshaji huo unaonekana kuchuja, wakaja na hoja nyingine za jeshi kutwaa madaraka.
Katika miaka 50 ya uhuru ni Rais Kikwete pekee aliyefikia hatua hiyo.
Viongozi waliomtangulia waliliacha jeshi kama taasisi nyeti isiyohitaji kuingiliwa.

Lakini pia kuna maswali, kama S3 zitalifanya jeshi lisiwe na pesa, mbona kuna mabilioni yameliwa chini ya uongozi wa JK ndani ya jeshi. Kuingiza hoja ya jeshi ni upotoshaji ambao nao umegonga mwamba.

Sasa kuna hoja nyingine imepikwa. Siku za karibuni kuna kijana kada wa CCM ameingia jamvini na hoja kuwa UKAWA wanafadhiliwa na mataifa ya nje ili kuvuruga amani.
Kwamba kuna mataifa ya magharibi ynayowatumia ili kuleta uvunjifu wa amani. Soma...
https://www.jamiiforums.com/great-thinkers/647862-nje-ya-bunge-hakuna-katiba-ya-wananchi.html

Jana gazeti la habri leo http://www.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/24753-ukawa-waanza-mivutano limeandika habari kuhusu UKAWA.

Habari hiyo ililenga kuonyesha yapo mataifa yaliyotoa pesa ili kuvuruga amani.
Hii ndiyo hoja inayopelekwa kwa wananchi kwa sasa.

Hizi ni hoja na mbinu za hovyo sana. Wanafunzi wakigoma, wanatumiwa na mataifa ya magharibi. Wafanyakazi wakigoma wanatumiwa na mataifa ya magharibi.
Wakulima wakidai ruzuku wanatumiwa na mataifa ya magharibi.

Hii hoja haina maana ni ya kipuuzi na haina mashiko kwa dunia ya sasa.
Aliyeanzisha mchakato ni JK, aliyeunda tume ni JK.

Miswada yote imepitishwa na bunge la CCM.

Aliyeitisha BMLK ni JK. Waliogomea rasimu aliyosaini Kikwete ni CCM.

Aliyetukana na kudhalilisha tume iliyoandika rasimu na kusainiwa na JK ni JK

Waliogomea kanuni za kupiga kura ni CCM hadi tukapata chotara wazi /siri.
Aliyeleta hoja ya jeshi ni JK

Hivi hapa kuna taifa gani la magharibi limeingilia mchakato?
Kwamba panaotokea kutokuwa na maelewano ya hoja, upande CCM wanafadhiliwa.
Huu ni ukosefu wa fikra, ni unafiki na uzandiki wa hali ya juu.

Hayo yanatokea kwasababu CCM hawana hoja, wameishiwa utetezi na wana hofu.
Hofu kubwa ni baada ya kukosa 2/3 licha ya mbinu zilizopangwa na hujuma chini ya Samwel Sitta.

Hofu inayokuja ni CCM kushindwa kuwasilisha rasimu yao ya porini.

Kubabaika kwa CCM kuna tueleza jambo moja, hawana hoja ya kusimamia S2.
Hawana hoja kilichobaki ni uzushi na upotoshaji.

Kama kuna dhamira ya kweli haya ya upotoshaji yanatoka wapi na yamekusudia nini?
Ndivyo tunataka kujenga taifa. Ni taifa gani la waongo na wazushi tunalotaka kuwaachi watoto na wajukuu

Tusemezane
 
KIWEWE CHA KUZINDUKA TANGANYIKA

WAZANZIBAR WACHANGANYIKIWA
MAMA ANASEMA HILI, MTOTO ANASEMA LILE

ILE ZNZ MOJA SASA NI ZAIDI YA MBILI

Kiwewe cha kuzinduka kwa Tanganyika kinaendelea. Baada ya mchakato kuanza kwa uchakachuaji hadi bunge kuahirishwa, kiwewe kimezidi hasa upande wa wanaotaka serikali 2.

Wabunge wa BMLK walikaririwa wakisema wapo wengi kwasababu wanaungwa mkono na wananchi wengi.Akina January Makamba wakasema sera ya CCM ni S2 bila kujali wanamtukana aliyeanzisha mchakato ambaye ni mwenyekiti wa CCM Kikwete.

Pamoja na wingi wao bungeni leo wapo mitaani wakiwashawishi wananchi wakubaliane nao. Wingi uliosemwa bungeni ni upi? Na kwanini wana haha huku na huko kutafutwa kuungwa mkono ikiwa ni wengi tayari bungeni?

UKAWA wakajitoa bungeni, hiyo ilikuwa nafasi adhimu kwa CCM kueleza nini S2, nini wamefanya na nini wanatarajia.

Kilichoendelea mnakikumbuka ni mipasho, matusi, ubaguzi, kejeli n.k.
Kwa siku zaidi ya 10 bungeni hakuna mjadala wa katiba bali tabia, wasifu na hulka za watu.

Kiwewe hicho kimehamia katika mitaa. UKAWA wakiwaeleza wananchi kwanini wanasusia kikao na jana CCM wakifanya mkutano Zanzibar kupiga madongo S3 na si kueleza uzuri wa S2. Kuendeleza tambo za kumchafua mzee Warioba na tume yake.

Tume ya Warioba iliundwa na wazanzibar 15 na wengine 15 wa nchi isiyojulikana ingawa inahisiwa ni nchi ya 'Tanzania bara'. Mawazo ya wanatume kutoka znz ni mawazo ya wazanzibar.

Katika baraza la wawakilishi, wazanzibar wamekuwa kitu kimoja katika masuala kama kuondoa mafuta na gesi, kubadilisha katiba yao mwaka 2010,kukiuka katiba ya JMT na kulalamika znz kufanywa koloni.

Hayo yalisemwa pia na mama Fatma Karume ambaye ni mke wa muasisi akilaani dhulma dhidi ya zanzibar.

Mama Karume alikuwepo jana akipigia debe S2 za muungano.
Amesahau kuwa yeye aliwakarabisha wajumbe wa kamati ya maridhiano na kueleza machungu juu ya muungano.

Pengine nishani ya muungano iimebadili mtazamo wake. Hata hivyo ni mama mtu mzima, na kiwango chake cha ufahamu hakitupi wasi wasi wa kumjadili zaidi.

Tunayeweza kumjadili zaidi ni mwanawe Aman Karume ambaye ndiye aliyeongoza taratibu zote za znz kukiuka na kuvunja katiba ya JMT kama si kuvunja muungano kabisa.

Aman Karume ni muumini wa S3 au mkataba. Lakini pia ni mmoja wa watu waliopokea nishani za CCM za miaka 50 ya uhuru licha ya kuongoza jithada za kuvunja katiba ya JMT.
Yeye ndiye kinara wa kuvunja muungano huu ambao kwasasa haupo ila jina tu.

Kuna waziri kiongozi Shamsa Vuai ambaye baada ya kuvuliwa uwaziri wa ulinzi akilikimbilia znz na kusema yeye anataka znz huru. Miongoni mwa walomuunga mkono ni akina Said Nkumba n.k

Yupo Pandu kificho ambaye ni Spika wa BLW.
Huyu naye kama Aman Karume alisimama kuhakikisha BLW linapitisha sheria za znz kama nchi na kuvunja katiba ya JMT kwakuifanya dhalili na chini ya ile ya znz ya mwaka 2010.

Pandu kwa kushirikiana na Karume walivunja muungano uliopo hata kabla hajafika Dodoma.

Kwa upande mwingine wapo kamati ya maridhiano inayowashirikisha wanachama wa CCM kama mzee Moyo, Mansour Himid.

Kwa upande mwingine wapo akina Jussa na wenzake wanaowakilisha upande wa CUF.
Kamati hii inajulikana kama kiungo cha kuwakutanisha wznz wa pande zote kudai znz huru na yenye mamlaka kamili.

Kamati hii ina baraka za Aman Karume na Maalim Seif, na karume aliitumia kuua muungano kwa kuvunja katiba ya JMT. Ieleweke Karume Aman ndiye aliyevunja muungano wa sasa ambao haupo kama muungano ili jina.

Maalim Seif ni CUF inayoamini katika znz huru na mamlaka kamili. CUF haiamini katika muungano wa S2 na kama mkataba ukishindikana basi ni S3. Maalim Seif anaamini katika mkataba.

Ndani ya bunge la katiba mgawanyiko ulikuwa mkubwa sana.
Kwa upande mmoja wapo waliosema S2 ni nzuri na zina faida kwa znz akiwemo waziri wa zamani Shamhuna, waziri Aboud, Vuai, Seif Idd, Pandu kificho n.k.

Wapo waliosema muungano ni adha kwa znz wakiongozwa na akina Mnyaa na Jussa Ismail.

Ukiangalia hali ya mambo ilivyo, kuzinduka kwa Tanganyika kumepelekea kiwewe kikubwa si ndani ya CCM tu bali kwa znz nzima kwa ujumla wake.

Wazanizbar wamegawanyika na kiwewe cha Tanganyika kinawapeleka puta bila kujua wafanye nini. Znz kwasasa hawajui ni nini wanachotaka.

Watanganyika kwa upande mwingine wanaonekana kujua wanataka nini, isipokuwa viongozi wachache walaghai.

Changamoto kwa znz ni kama hizo za mama na mwana kupingana hadharani tena juu ya jambo aliloacha marehemu mzee Karume. Huku ni kuchanganyikiwa kwa hali ya juu.

Kwa upande mwingine CCM wana wakati mgumu sana.
Kwasasa mikutano yao itafanyika na kwa hila wanaweza kupitisha hiyo S2 kwa ulaghai na mbinu. Hata hivyo huo utakuwa mwanzo wa tatizo jingine kubwa sana mbele ya safari.

ZNZ iliungana kuondoa mambo ya muungano kupitia BLW.
Ikarekebisha katiba yake hadi kuondoa mamlaka ya Rais wa JMT, Mamlaka ya Mahakama ya rufani, kuunda majeshi na kukiuka sehemu kubwa sana ya katiba ya JMT.

Ili Watanganyika waelewe hoja za CCM ni sharti kwanza znz wakae na kukubali kubadilisha katiba iendane na ya JMT.

Katiba ndiyo iliyowaunganisha, kuibadili ni kujaribu kuwatenganisha na hilo halina uhalisia na wala halitatokea. Wznz wote kwa ujumla wao ndani ya BMLK hakuna aliyejaribu kukemea uhuni wa katiba yao ya 2010. Wale wa CCM waliisha kusema S2 na kuwatukana Wapemba
Hawakuthubutu kukemea mabadiliko ya 2010 kama chanzo cha mtatizo ya muda mrefu

Watanganyika na wabunge wao wataungana dhidi ya uhuni wa znz kudai nchi huku ikinufaika na rasilimali za nchi ya Tanganyika.
Hivyo jambo litakalowagawa wznz zaidi litawaunganisha Watanganyika.
Kulaani mabadiliko ya 2010 ni agenda ya Watanganyika, kutetea katiba ya 2010 ni agenda ya wznz

CCM bado itakuwa na mtihani mkubwa.
Huenda watapunguza joto lakini litarudi kwa nguvu kubwa zaidi kama ilivyo sasa.
Litakaporudi muungano utafikia hatima hata bila ya uwepo wa S3.

Jibu la matatizo ni kuwasikiliza wananchi, Wananchi wamesema na wasikilizwe.
Kinachoonekana znz kwa sasa ni kurudi katika uhasama wa zamani miongoni mwao.
Hilo litatokea katika miezi chini ya miwili na CCM itajikuta katika wakati mgumu kuliko huko nyuma.

Hakuna znz imara bila uwepo wa Tanganyika.

Kivuli cha Tanganyika kinachowasumbua hadi mama na mwana wapingane hadharani ni dalili njema kabisa kuwa kuna tatizo kubwa linakuja, CCM hawana sluhu miaka 50 na sasa wanaharakisha kifo cha muungano. Kuna tatizo kubwa sana hasa znz na huo ndio utakuwa mwanzo wa mwisho.

Tusemezane
 
Nguruvi3,
Ukweli ni kuwa ndani ya muundo wa S3 serikali tunaongelea serikali ya Shirikisho tu yenye mambo 7.
Hivi kweli wewe unaamini kuna muungano ikiwa mapendekezo yenu ya serikali 3 yana ushirika wa mambo 7 tu?. Kwa nini msiseme tunavunja muungano wazi wazi badala ya kusema saaana kuudanganya Umma kwamba mnaimarisha muungano.
 
Last edited by a moderator:

Ndiyo naamini tena nikiwa na sababu.
1. Tulianza na mambo 11 na sasa ni 22 ambayo yakinyambuliwa ni zaidi ya 40.

Zanzibar wanalalamika kwa kusema mambo mengine yameongezwa kinymela. Mkandara yupo katika rekodi ya kutetea mambo yaliyoingizwa kinyemela kama kuwanyang'anya wznz madaraka.

Kwa mtazamo wa Mkandara, inabidi turudi katika mambo 11 (rekodi ipo).
Nikisema 7 ninamuunga mkono Mknadara, kinachonishangaza leo amekata kona anasema hayapaswi kuwa 7 tu. ZNZ ni nchi vipi tunaweza kuwa na mambo ya pamoja?

Mambo ya pamoja yatakuwa chini ya waziri mkuu ambaye znz hawamtambui, huoni tatizo hapo.
Hayo 7 yanatosha, kama ni mengi basi tuvuje jahazi kila mtu aende anakojua. Miaka 50 ya kubeba kiroba cha samadi sasa basi. tuacheni tupumue.

2. Zanzibar imeondoa mambo zaidi ya 17 katika muungano.
Hii maana yake ni kuwa hawahitaji mambo hayo kuwa ya muungano.

Kubakiza 7 ni msaada mkubwa si kwao tu bali kwa Tanganyika.
Tumeondoa mambo 22 na sasa ni 7 kwa maana ya kuwa tumepunguza zigo la samadi na kuelekeza pesa zao kwa walipa kodi wenyewe.

3. Znz imeshavunja katika ya JMT. Rais wa JMT amepokwa madaraka ya kikatiba juu ya znz, Mahakama imenyimwa uhuru wa kutenda majukumu znz, na znz kwa kuamua tu imeondoa mambo wasiyoyataka bila majadiliano.

Tuna maamir jeshi wawili, mmoja wa znz na mwingine wa JMT. Hatujui nani mkubwa.
Tuna majeshi 2 moja la JMT na lingine la znz. Hatujui majeshi hayo yanapokea 'daily order' kutoka wapi.

Kwa muktadha huyo muungano unaozungumzia sasa umeshavunjwa na haupo.
Kuweka mambo 7 ni bora kuliko ilivyo sasa

Kuendelea na status quo ni kujidanganya.
Tunajua kuwa hakuna muungano, kilichopo ni jina la Tanzania linalotumika na znz kusetiri dhiki na shida zao. Hivyo mambo 7 yana maana zaidi kuliko muungano huu uliovunjwa na wazanzibar.

Yakishindikana, kila mtu na njia yake
 
WAZANZIBAR WATAIYUMBISHA TANZANIA
LEO WANASEMA HIKI, KESHO WANASEMA KILE
SASA NI 'FULL' KUCHANGANYIKIWA

Mkutano wa CCM umefanyika kibanda maiti Zanzibar. Miongoni mwa wazungumzaji alikuwepo katibu mwenezi wa CCM Nape Nnauye. Kama ilivyotarajiwa Nape ametumia muda wake kuporomosha matusi hadi kufanya umma ushangae kuhusu weledi wa katibu wa chama tawala.

Katika hoja dhaifu, Nape amesema ni maruku kuwatukana waasisi wa muungano.
Akiwa hapo znz, hajui CCM ilianza kuwatukana waasisi kwa kuua Azimio la Arusha hapo.
Kwamba, nchi iliondoka katika Ujamaa wa waasisi na kuingia ubepari hapo hapo alipokuwa amesimama.
Ni Nape hatukutegemea jipya.

Aliyeshtua umma ni Kinana, katibu mkuu aliyetaka Maalim Seif aachie ngazi kwa kutumia rasilimali za muungano. Kinana anasahau kuwa mafisadi waliokubuhu na wanaotumia rasilimali za muungano ndio wanaoandika rasimu ya CCM ya mafichoni. Amesahau serikali ya CCM ndiyo imeshindwa kulinda rasilimali kama tembo wanaopukutika kila uchao.

Kinana amesahau wale walioiba rasilimali za meno ya tembo yaliyokamatwa katika meli yake wameshindwa kujulikana au kuchukuliwa hatua na serikali ya CCM. Leo Kinana anapata wapi nguvu za kukemea matumizi mabaya ya rasilimali za muungano?

Ameongea mwakilishi wa BLW Salimin A Salimin. Huyu alitia ganzi kwa kusema unaandaliwa mswada kupelekwa BLW ili serikali ya umoja wa kitaifa ipigiwe kura.Maana yake ni kufuta serikali ya umoja wa kitaifa iliyopigiwa kura na wazanzibar.

Hapa kuna hoja nzito sana za kujadili.
1. Kinana na Nape hawajatetea kwanini wanataka serikali 2 na si tatu. Matusi hayaelezi kwanini S2.
2. Kwanini CCM inahaha kukimbizana na UKAWA ili hali walibaki salama bungeni wenyewe
3. Kwanini wznz watake kuvunja serikali ya umoja wa kitaifa (GNU,au SUK) sasa hiv?

Hoja ya 3 hapo juu ni muhimu sana kuiangalia.
Wakati ZNZ inapeleka mswada wa marekebisho ya katiba 2010 ni wznz hao hao CCM na CUF waliokubaliana kwa pamoja kuunda SUK kwa kisingizio kuwa, wanaowachonganisha wagombane ni Wabara. Leo iweje hao hao wafarikiane tena wakishirikiana na wale wale waliowatuhumu kuwachonganisha?

Katika mswada wa sheria wa 2010 ZNZ ilinyakua mamlaka ya Rais wa JMT, kutangaza Amir jeshi wake, kupoka madaraka ya mhakama ya rufani, kuitenga nchi na kuwa nchi kamili ikiwa na vyombo vyote.

ZNZ ikaendelea kuondoa mambo ya muungano bila kushauriana na CCM au Watanganyika.
Ikavunja muungano kwa ushirikiano wa CCM na CUF kwa kile kilichosemwa 'znz kwanza'

Leo inakuwaje wale walioshiriki uhuni huo,warudi tena BLW kuharamisha uhuni walioshiriki kuutengeneza kama akina Salimin.

Nini walichokiona cha maana hadi kufikia usaliti wa nchi yao yenye Rais, bendera, wimbo wa taifa, mahakama, BLW n.k.

Katika bunge la katiba, wznz waliosimama na kzungumza, hakuna hata mmoja aliyelaani mabadiliko ya katiba ya znz ya 2010.

Wote kwa pamoja wamekubaliana kuwa ni jambo sahihi kwa masilahi ya nchi yao, tena wakisema wanajiondoa katika makucha ya mkoloni Tanganyika.

Endapo wanafikiria kufikisha mswada wa kuvunja SUK, hilo ni wazo zuri.
Lakini kwanza inabidi wapeleke mswada wa marekebisho ya katiba ya 2010 iliyovunja muungano, wahakikishe kuwa yale yote yaliyovunja muungano yanaondolewa.

Kwanza wakatae kuwa znz siyo nchi ila ni sehemu ya Tanzania.
Pili, wakubali kuwa Rais wa JMT ndiye Amir jeshi na mwenye uwezo wa kugawa nchi.
Tatu, warudishe nguvu za mamlaka ya mahakama ya rufani.
Nne, waombe radhi kwa kuonda mambo ya muungano bila kuwasiliana na Tanganyika.
Tano, waombe radhi kwa kitendo cha kuvunja katiba ya JMT.

Wakishafanya hayo, wapeleke mswada wa sheria wa kura ya maoni ya kuvunja serikali ya umoja wa kitaifa. Ikifika hapo watakuwa na uwezo wa kumnyang'anya Maalim Seif kile wanachodhani hapaswi kuwa nacho.

Halafu warejee Dodoma na kuendelea kudai serikali 2 chini ya nchi ya Tanzania.
Wakubaliane na hoja kuwa Rais wa Tanzania ni mmoja, na kwamba watawajibika katika mambo ya kuendesha muungano, hawatadai kisicho chao n.k.

Wakishindwa kufanya hayo basi tujue tuna tatizo kubwa mbele ya safari.
Tatizo hilo ni znz isiyo na utulivu na gharama za hali hiyo ni Mtanganyika kubeba gharama zaidi za ulinzi na usalama wa raia.

CCM itatumia pesa nyingi kulaghai na kununua watu.
Kitu kimoja duru za siasa ina uhakika nacho, muungano ni ridhaa ya wananchi na kwa ajili ya wananchi. Hakuna muungano uliowahi kulindwa kwa deraya za kijeshi, mabomu ya machozi au risasi za moto.

Walijaribu kwa Jumbe moto umelipuka
Wakazima G55 moto umelipuka
Wameunda tume 10 na kuficha matokeo, moto umelipuka

Sudan walijaribu kwa risasi za moto miaka 20, mwishowe wameshindwa
Ethiopia walijaribu kwa nusu karne, hatimaye wamemeguka
Uingereza wamejaribu miaka 300 hatimaye Ireland wanaamua
Canada bado inahangaika na Quebec
Senegambia ipo maktaba za historia
Egypt na Syria sasa ni mahasimu
Somalia ya Siade Barre sasa ni Somaliland na British Somalia

Ukitazama huko kote risasi za rashasha na za moto zilitumika.
Deraya za kijeshi zilitumika na ndege za kivita zikashambulia kutoka angani.
Kwavile hakukuwa na ridhaa anguko halikukwepeka.

Ndiko CCM inapotuelekeza. Leo wanashangiliwa hawajui kuwa wanaowashangilia ndio watakaowazomea.

CCM inatengeneza bomu huko znz kwa kiwewe cha kuzinduka Tanganyika.
Wnz hawajitabui, wamechanganyikiwa.

Hiyo ni hatari kwa usalama wa taifa. Yaliwahi kutokea, yakirudi yatakuwa na nguvu kubwa.
Kwanini Mtanganyika alipe gharama zisizomhusu?

Hakuna dola iliyowahi kushinda nguvu ya umma.

Vox populli vox dei,

S3 haikwepeki

Tusemezane
 
Ndiyo naamini tena nikiwa na sababu.
1. Tulianza na mambo 11 na sasa ni 22 ambayo yakinyambuliwa ni zaidi ya 40.

Zanzibar wanalalamika kwa kusema mambo mengine yameongezwa kinymela. Mkandara yupo katika rekodi ya kutetea mambo yaliyoingizwa kinyemela kama kuwanyang'anya wznz madaraka.

Kwa mtazamo wa Mkandara, inabidi turudi katika mambo 11 (rekodi ipo).
Nikisema 7 ninamuunga mkono Mknadara, kinachonishangaza leo amekata kona anasema hayapaswi kuwa 7 tu. ZNZ ni nchi vipi tunaweza kuwa na mambo ya pamoja?

Mambo ya pamoja yatakuwa chini ya waziri mkuu ambaye znz hawamtambui, huoni tatizo hapo.
Hayo 7 yanatosha, kama ni mengi basi tuvuje jahazi kila mtu aende anakojua. Miaka 50 ya kubeba kiroba cha samadi sasa basi. tuacheni tupumue.

2. Zanzibar imeondoa mambo zaidi ya 17 katika muungano.
Hii maana yake ni kuwa hawahitaji mambo hayo kuwa ya muungano.

Kubakiza 7 ni msaada mkubwa si kwao tu bali kwa Tanganyika.
Tumeondoa mambo 22 na sasa ni 7 kwa maana ya kuwa tumepunguza zigo la samadi na kuelekeza pesa zao kwa walipa kodi wenyewe.

3. Znz imeshavunja katika ya JMT. Rais wa JMT amepokwa madaraka ya kikatiba juu ya znz, Mahakama imenyimwa uhuru wa kutenda majukumu znz, na znz kwa kuamua tu imeondoa mambo wasiyoyataka bila majadiliano.

Tuna maamir jeshi wawili, mmoja wa znz na mwingine wa JMT. Hatujui nani mkubwa.
Tuna majeshi 2 moja la JMT na lingine la znz. Hatujui majeshi hayo yanapokea 'daily order' kutoka wapi.

Kwa muktadha huyo muungano unaozungumzia sasa umeshavunjwa na haupo.
Kuweka mambo 7 ni bora kuliko ilivyo sasa

Kuendelea na status quo ni kujidanganya.
Tunajua kuwa hakuna muungano, kilichopo ni jina la Tanzania linalotumika na znz kusetiri dhiki na shida zao. Hivyo mambo 7 yana maana zaidi kuliko muungano huu uliovunjwa na wazanzibar.

Yakishindikana, kila mtu na njia yake
Mkuu wangu weee lini utanielewa? nishasema mara 100 kidogo ya kwamba hayo MBAMBO YASOKUWA YA MUUNGANO ndio tatizo lenyewe na sii serikali ngapi. Sasa iwe 11 au 22 au 44 yote haya yatazidi kuongezeka ikiwa tutaendelea na kuwa na haya Mambo yasokuwa ya Muungano kwa sababu wakati wake umekwisha na katiba mpya inatakiwa kuyaondoa kutokana na kwamba mwaka 1984 baada ya kuwa na vyama vingi na pia mwaka 1004 baada ya kuachana na Ujamaa hatukuhitaji tena kuwa na MAMBO YA MUUNGANO na YASIYOKUWA YA MUUNGANO sehemu ya 2 kifungu hiki kiondolewe
(3) Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za umma katika Jamhuri ya Muungano, na kwa ajili ya mgawanyo wa madaraka juu ya shughuli hizo baina ya vyombo vilivyotajwa
katika ibara hii, kutakuwa na Mambo ya Muungano kama yalivyoorodheshwa katika Nyongeza ya Kwanza iliyokomwishoni mwa Katiba hii, na pia kutakuwa na Mambo yasiyo ya Muungano ambayo ni mambo mengine yote yasiyo Mambo ya Muungano.
Haya ndio mapungufu ya Katiba ya mwaka 1977 na mabadiliko yote yalowahi kufanyika pasipo kuhakikisha kwamba mambo yote ni ya Muungano isipokuwa shughuli zake zote ndizo sii za Muungano kila nchi, jimbo na mitaa - serikali zake ndizo zina mamlaka ya kuendesha shughuli hizo iwe hata jeshi la Polisi. Mkuu Ikiwa leo mmeondoa mamlaka ya rais wa Zanzibar ambaye alitakiwa kuwa makamu wa rais (katiba 1977) unaweza vipi kuwalaumu wao ilihali sisi ndio tulowavua nguvu na kuwatenga ktk serikali ya JMT na dhahiri Zanzibar kuwa nchi nje ya Muungano wa nchi moja maana mamlaka ya rais wake hayatambuliwi tena bara wala ktk JMT. Kipi haswa usichoelewa hapa mkuu wangu.

Pili, ebu nenda kaisome katiba iliyopo, kisha ondoa kifungu hicho na kuyaacha mambo yote kuwa ya Muungano na tukagawana mamlaka ya utekelezaji wa shughuli za serikali kisha utaona ni kero ngapi zitaondoka kwa pande zote mbili acha kero zetu sisi wenyewe Watanganyika juu ya CCM. Ukisha wapa madaraka kamili Znz na madaraka Mikoani na Halmashauri zake hatuhitaji tena kuitegemea serikali kuu (CCM) kupeleka maji Dodoma au Maendeleo Lindi. Wazanzibari vwatailalamikia serikali yao kama ambavyo sisi tutakavyo walalamikia wabunge, wakuu wa Mkoa, Mameya kabla ya kuitazama serikali kuu!
 
Nguruvi3,
Sudan walijaribu kwa risasi za moto miaka 20, mwishowe wameshindwa
Ethiopia walijaribu kwa nusu karne, hatimaye wamemeguka
Uingereza wamejaribu miaka 300 hatimaye Ireland wanaamua
Canada bado inahangaika na Quebec
Senegambia ipo maktaba za historia
Egypt na Syria sasa ni mahasimu
Somalia ya Siade Barre sasa ni Somaliland na British Somalia
Hii kweli ni mifano mizuri ya kuitumia au mwenzangu una matatizo mengine maana sitopenda kabisa kuiona Tanzania ktk hali yoyote ilowakuta hao mashujaa wako!
 
Nguruvi3,
Hii kweli ni mifano mizuri ya kuitumia au mwenzangu una matatizo mengine maana sitopenda kabisa kuiona Tanzania ktk hali yoyote ilowakuta hao mashujaa wako!
Ujumbe wangu kwako na CCM ni kuwa maoni ya wananchi yaheshimiwa. Muungano ni makuliano na maridhiano baina ya wananchi. Muungano haulindwi kwa deraya au mabomu ya machozi kama mnavytotaka iwe wewe na CCM.

Wananchi wanataka Tanganyika ili wakae pamoja na nchi ya znz na taifa la znz kujadili kama kuna mahali wanaweza kufanya kazi pamoja. Wameseme kupitia maoni ya tume iliyoundwa na Rais ambaye ni mwenyekiti wa CCM na aliyekuwa na ufahamu wa kile kilichojiri. Mabomu hayatazuia muungano kujadiliwa na kuulinza kwa risasi ni njia hafifu.
Risasi hazaijawahi kuunganisha wanadamu, nguvu ya umma haijawahi kushindwa na dola.

Tanganyika haiepukiki, ni kwa masilahi mapana ya Watanganyika na muungano.
 
Utafiti na nukuu ni vizuri uvitumie ktk ujenzi wa hoja zako. Ni Muungano wa nchi zipi ulowahi kuwepo baada ya maridhiano ya wananchi!.
 
Utafiti na nukuu ni vizuri uvitumie ktk ujenzi wa hoja zako. Ni Muungano wa nchi zipi ulowahi kuwepo baada ya maridhiano ya wananchi!.

Mkuu Mkandara,

Ni dhahiri Kwamba wewe ndiye mvivu wa kutafiti na ni moja ya sababu kwanini sikuhizi, hasa kufuatia mchakato wa katiba mpya, umakini wako wa hoja umeyumba sana.

Australia ni shirikisho la kwanza duniani ambalo matokeo yake yalikuja baada ya kura ya maoni. Hii ilikuwa ni mwaka 1898-1900 ambapo kura ya maoni ilipigwa Katika makoloni yake yote. Leo Australia stands Kama moja ya major success stories za muungano duniani, hususan, muungano wa shirikisho.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mkuu wangu kwanza kama nilivyosema mwanzoni.. naomba unipe namba za maoni ya WANANCHI wa majimbo ya Australia kuhusiana na Muungano huo. Nitajie hizo namba kama alivyowakilisha Warioba na isiwe AUSTRALIA iloungana kwa kupitia maafikiano ya viongozi wao kuunda kitu kinachoitwa Federal council of Australia kupitisha sheria.

Na isiwe pia kama ilivyokuwa Muungano wetu Tanzania maana madai yenu ni kwamba muungano wetu sii halali haukupata ridhaa ya wananchi. Sasa nionyesheni wenye ridhaa ya wananchi na tuhesabu maana mimi ninayo Miungano mia kidogo isokuwa na riodhaa ya wananchi bali makubaliano ya viongozi wa nchi husika. Nambie hizo kura za maoni zilifanyika lini (refendum) na wananchi wa states zote walishirikishwa kuchagua hiyo federation na kwa asilimia ngapi?
 
Nadhani haukutegemea kwamba duniani zipo nchi zenye muungano wa referendum. Sasa unaanza kukimbia kivuli chako mwenyewe. Swali ulilo uliza lilikuwa ni wapi duniani muungano ulitokana na referendum, huku ukihimiza Nguruvi3 afanye utafiti kabla ya kutoa hoja. Kumbe wewe ndio haukufanya utafiti, na sasa nimekujibu kwamba ilitokea kwa mara ya kwanza australia ambapo ilichukua miaka miwili kukamilisha zoezi hilo - 1898-1900. Sasa unaniuliza mimi kuhusu takwimu za hiyo referendum? na muda sio mrefu utakuja na maswali nani alikuwa warioba wao na Kikwete wao and other irrelevant questions. Si ufanye utafiti mwenyewe kupata majibu ya maswali yako ya nyongeza kisha ujenge hoja na findings zako?

Nimekusaidia na majibu kwa swali lako la msingi, the rest remains commentary.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mkuu wangu umefungua mwenyewe mlango nzi lazima waingie.. Na wala usihofie hilo la utafiti kwa sababu najua Muungano wa Australia kama navyoujua wa Canada maana hawana tofauti kubwa na bado ni koloni mamboleo la Malkia. Australia kama nchi ilikuwepo kabla ya mwaka 1898 ndani ya Ukoloni wa Malkia. States zake zilikuwa koloni la Malkia na Uhuru wao hauna tofauti na Canada na hadi leo hawana tofauti na Canada. Wananchi hawakupiga kura bali mabunge yao yalipitisha na kuwa sheria kama ilivyopitishwa Muungano wetu na bunge letu. Nyie mnadai sii halali na ndicho alichosema Nguruvi3 ya kwamba Muungano unatakiwa kuwa na ridhaa ya wananchi. Nachokuomba wewe, ni unipe rasimu na takwimu za MAONI YA WANANCHI kwa kila state kufikia maridhiano ya kuunda Muungano wa Australia - sina zaidi!
 
Mkuu Mkandara, kuna mahali sielewi nisaidie kidogo.
Hivi sheria inatangulia na kisha kuridhiwa na bunge, au inapitishwa na bunge kisha kuridhiwa na serikali(Hapa kwetu Rais)
 
Mkuu Mkandara, kuna mahali sielewi nisaidie kidogo.
Hivi sheria inatangulia na kisha kuridhiwa na bunge, au inapitishwa na bunge kisha kuridhiwa na serikali(Hapa kwetu Rais)
Kazi kubwa ya Bunge ni kutunga sheria!
 
Kazi kubwa ya Bunge ni kutunga sheria!
Bunge linatunga sheria, hiyo sheria haiwi kamili mpaka iridhiwe na mamlaka husika (hapa kwetu ni Rais)

Swali langu ni hili, hivi bunge linapeleka mswada na kuujadili kisha kupeleka kwa Rais kusainiwa, au, Sheria ina sainiwa halafu kupelekewa bungeni kuridhiwa?

Nina upungufu kidogo wa kuelewa nisaidie kunifafanulia hapo.

cc Mkandara
 
Mkandara ukipata nafasi naomba unisaidie hilo swali mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wangu kwanza kama nilivyosema mwanzoni.. naomba unipe namba za maoni ya WANANCHI wa majimbo ya Australia kuhusiana na Muungano huo. Nitajie hizo namba kama alivyowakilisha Warioba na isiwe AUSTRALIA iloungana kwa kupitia maafikiano ya viongozi wao kuunda kitu kinachoitwa Federal council of Australia kupitisha sheria.

Na isiwe pia kama ilivyokuwa Muungano wetu Tanzania maana madai yenu ni kwamba muungano wetu sii halali haukupata ridhaa ya wananchi. Sasa nionyesheni wenye ridhaa ya wananchi na tuhesabu maana mimi ninayo Miungano mia kidogo isokuwa na riodhaa ya wananchi bali makubaliano ya viongozi wa nchi husika. Nambie hizo kura za maoni zilifanyika lini (refendum) na wananchi wa states zote walishirikishwa kuchagua hiyo federation na kwa asilimia ngapi?

Mkuu Mkandara,

Ubishi mwingine huwa hauna maana kabisa. Kwanini hautafiti kabla ya kujenga hoja halafu hapo hapo unasema wenginne (e.g Nguruvi3) hawatafiti?

Nilikuwa nakupa fursa uepuke aibu lakini kwa vile umekataa fursa hiyo, sawa.

Unachojaribu kufanya hapa ni kudanganya, na kama nilivyosema, umekuwa mtu wa "self fulfilling prophecy" katika hoja zako nyingi.

Mwaka 1898, kura za maoni zilipigwa juu ya "Commonwealth Constitution Bill", na zilipigwa makoloni ya:

*New South Wales
*South Australia
*Tasmania, na
*Victoria.

Katika kila koloni, majority walipiga kura ya "NDIO", lakini "new south wales", sheria ilitaka minimum ya kura za NDIO iwe ni kura 80,000. Hizi hazikupatikana new south wales.
Matokeo yalikuwa haya (raundi ya kwanza 1898): N for ndio, H for hapana:

New South Wales

71, 595 [Ndio]

66, 228 [Hapana]

South Australia

35,800 N

17,320 H

Tasmania

11,797 N

2,716 H

Victoria

100,520 N

22,090 H

Kufuatia hali hii (south wales kutofikia quota ya 80,000 za ndio), mabadiliko ya katiba yakapendekezwa na new south wales na sheria mpya ikatengua quota ya 80,000 na badala yake kuweka "simple majority." Then ikasema new south wales, na baadae makoloni yakapiga kura nyingine ya maoni mwaka 1899.

Matokeo ya Kura ya Maoni raundi ya pili mwaka 1899 yakawa kama ifuatavyo:

New South Wales

107,420 N

82,741 H

Queensland

38,488 N

30,996 H

South Australia

65,990 N

17,053 H

Tasmania

13,437 N

791 H

Victoria

152,653 N

9,805 H

Kufikia mwaka 1900, "Western Australia" walikuwa bado hawajapewa fursa ya kupiga kura ya maoni. Wakazi wake wakaana migomo na kutaka kujitenga. Ilipofika July 31, 1900, wakati "Commonwealth Constitution Bill" ilishakuwa imepitishwa na bunge la Uingereza, western australia wakapewa fursa ya kupiga kura ya maoni na majority wakaunga mkono "mfumo wa shirikisho." Matokeo ya kura ya maoni western australia mwaka 1900 yakawa kama ifuatavyo:

44,800 N

19,691 H

Ukitaka kwa asilimia, chukua calculator utapata jibu. Source zipo tovuti ya serikali ya Australia.

Na ukae ukijua kwamba maoni ya rasimu ya tume yetu were only "indicative", lakini mnalazimisha yawe "conclusive". Kwanini msiwe wavumilivu kusubiria kura ya maoni? Na tumeonyesha jinsi gani takwimu za tume zinaendana na zile za taasisi za utafiti kama vile afrobaromete na pia taasisi ya twaweza.

Mwisho - Usiwe unapotosha mambo mkuu for self fulfilling prophecy. Suala la katiba mpya ni nyeti na ni la wananchi. Naelewa kwamba wewe ni "conservative" kwani umekuwa ukijitambulisha wazi hivyo. With all due respect, mambo mengine muwe mnasoma alama za nyakati. Hivyo ndivyo tutaweza okoa muungano na taifa letu.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Navyofahamu mimi muswada hupelekwa bungeni ukajadiliwa na ukipita hupelekwa kwa rais kusainiwa ili kuwa sheria!
Ahaa, kamani hivyo, je ndivyo ilivyofanyika katika muungano wetu?
 
Back
Top Bottom