Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
- Thread starter
- #261
UPOTOSHAJI UNAENDELEA
KILA SIKU KUNA JAMBO JIPYA
Katika dhamira ya kweli ya kuandika katiba ya taifa hakuna sababu za kupotosha.
Katiba ni nyaraka kila mwananchi, kwanini kundi CCM linaelekeza nguvu za upotoshaji na si ujenzi wa hoja?
Hoja ya serikali 3 na gharama imekosa mashiko. Imekosa kwasababu hakuna mtu au watu kutoka S2 wanaoweza kuweka hesabu mezani na kusema zina nafuu kuliko 3.
Hoja imekosa mashiko kwa ukweli, kila siku tunaongeza mikoa na wilaya ikiwa ni sehemu ya ongezeko la gharama.Kuna hoja ya jinsi gani mapesa yanapotea serikalini na mashirika ya umma kwa taarifa za CAG bila wahusika kujulikana.
Mathalan, hadi sasa hakuna anayejua bilioni 27 za rada zilitokaje hazina na nani walihusika.
Mfano wa pili, tunawezaje kulipa milioni 150 kwa siku kwa kampuni moja izalishe au isizalishe umeme halafu tukadai serikali 3 zenye shirikisho ni gharama.
Upotoshaji unaofanyika ni kuzifanya serikali 3 kwa ujumla.
Ukweli ni kuwa ndani ya muundo wa S3 serikali tunaongelea serikali ya Shirikisho tu yenye mambo 7.
Hapa napo wahuni wanakwepa ukweli kuwa ni shirikisho ili kujenga hoja ya S3 ni mzigo.
Hivi mambo 7 yanawezaje kuwa ghali kuliko mambo 22 ya sasa?
Katika mazingaombwe, watu wanasema S3 ni mzigo, si kweli ni upotoshaji.
Tuongelee Serikali ya shirikisho, hizo mbili kila mmoja atajua utaratibu wa kudhibiti gharama zake.
Upotoshaji huo unaonekana kuchuja, wakaja na hoja nyingine za jeshi kutwaa madaraka.
Katika miaka 50 ya uhuru ni Rais Kikwete pekee aliyefikia hatua hiyo.
Viongozi waliomtangulia waliliacha jeshi kama taasisi nyeti isiyohitaji kuingiliwa.
Lakini pia kuna maswali, kama S3 zitalifanya jeshi lisiwe na pesa, mbona kuna mabilioni yameliwa chini ya uongozi wa JK ndani ya jeshi. Kuingiza hoja ya jeshi ni upotoshaji ambao nao umegonga mwamba.
Sasa kuna hoja nyingine imepikwa. Siku za karibuni kuna kijana kada wa CCM ameingia jamvini na hoja kuwa UKAWA wanafadhiliwa na mataifa ya nje ili kuvuruga amani.
Kwamba kuna mataifa ya magharibi ynayowatumia ili kuleta uvunjifu wa amani. Soma... https://www.jamiiforums.com/great-thinkers/647862-nje-ya-bunge-hakuna-katiba-ya-wananchi.html
Jana gazeti la habri leo http://www.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/24753-ukawa-waanza-mivutano limeandika habari kuhusu UKAWA.
Habari hiyo ililenga kuonyesha yapo mataifa yaliyotoa pesa ili kuvuruga amani.
Hii ndiyo hoja inayopelekwa kwa wananchi kwa sasa.
Hizi ni hoja na mbinu za hovyo sana. Wanafunzi wakigoma, wanatumiwa na mataifa ya magharibi. Wafanyakazi wakigoma wanatumiwa na mataifa ya magharibi.
Wakulima wakidai ruzuku wanatumiwa na mataifa ya magharibi.
Hii hoja haina maana ni ya kipuuzi na haina mashiko kwa dunia ya sasa.
Aliyeanzisha mchakato ni JK, aliyeunda tume ni JK.
Miswada yote imepitishwa na bunge la CCM.
Aliyeitisha BMLK ni JK. Waliogomea rasimu aliyosaini Kikwete ni CCM.
Aliyetukana na kudhalilisha tume iliyoandika rasimu na kusainiwa na JK ni JK
Waliogomea kanuni za kupiga kura ni CCM hadi tukapata chotara wazi /siri.
Aliyeleta hoja ya jeshi ni JK
Hivi hapa kuna taifa gani la magharibi limeingilia mchakato?
Kwamba panaotokea kutokuwa na maelewano ya hoja, upande CCM wanafadhiliwa.
Huu ni ukosefu wa fikra, ni unafiki na uzandiki wa hali ya juu.
Hayo yanatokea kwasababu CCM hawana hoja, wameishiwa utetezi na wana hofu.
Hofu kubwa ni baada ya kukosa 2/3 licha ya mbinu zilizopangwa na hujuma chini ya Samwel Sitta.
Hofu inayokuja ni CCM kushindwa kuwasilisha rasimu yao ya porini.
Kubabaika kwa CCM kuna tueleza jambo moja, hawana hoja ya kusimamia S2.
Hawana hoja kilichobaki ni uzushi na upotoshaji.
Kama kuna dhamira ya kweli haya ya upotoshaji yanatoka wapi na yamekusudia nini?
Ndivyo tunataka kujenga taifa. Ni taifa gani la waongo na wazushi tunalotaka kuwaachi watoto na wajukuu
Tusemezane