Mkuu wangu alhan Wasahlan, Kwanza Eid Mubarak,
Mimi nitakwamba ukweli wangu juu ya Historia yako na ile ya Zanzibar na wapi tunatofautiana. Uzawa wako na asili yako kwangu sii hoja bali fikra zako ndizo nazipinga kwa sababu hu represent Uzanzibar bali Asili na nasaba yako na fikra zako zinalenga kuhalalisha kisichowezekana.
Kwanza, nikwambie tu ya kwamba Zanzibar haikuwa huru ila baada ya Mapinduzi! hii kubali usikubali na ndipo tunaposhindana. Na sababu haswa ni kwamba huu uhuru wa Zanzibar ulitoka kwa mtawala gani? maana alokuwa akitawala miaka yote ni Sultan ambaye aliomba hifadhi ya Muingereza kama kinga kuepuka Uvamizi wa Mreno, hivyo swala la Muingereza kuruhusu uchaguzi na kumpa mwanya Sultan kugombea uongozi ulitokana na kutokuwepo na hofu ama Mreno. hivyo aliwajibika kutrudisha utawala ule kwa wenyewe. Utanisamehe lakini kusema kwamba Uhuru wa mwaka 1963 wa Zanzibar hiyo ni sawa kabisa na Uhuru wa Rhodesia November 11 1963 hivi ndivyo inavyoonekana kwa waafrika wote regardless of their race or colour. Na sidhani kama wewe umesimama hapa kutetea Utawala wa Jamheed toka kwa Muingereza alowapa hifadhi, bali Uhuru wa Wazanizbar toka utawala wa kisultan.
Unaweza kuwa Mwarabu mwenye asili ya Oman lakini hukubaliania na utawala wa Sultan na labda nikukumbushe tu ya kwamba wapo makaburu waliokataa Uhuru wa mwaka 1963 wakashirikiana na wenyeji hadi Uhuru kamili wa Zimbabwe ulipopatikana mwaka 1980. yalofuata Allahu Yaalam na wanapigana kumwondoa Mugabe sio tena kaburu maana limeshapita wala hakuna anayezungumzia Uhuru wa mwaka 1963. Hivyo sitokushauri utumie sana asili yako kuhalalisha Uhuru wa Zanzibar kwani Sultan ndiye alikuwa mtawala kabla ya Uhuru na ndiye alokuja kupata ushindi ktk uchaguzi wa mwaka 1963 kwa mchezo mchafu wa kisiasa kama aloufanya Ian Smith.
Tuyaache hayo, ila nakuomba unapozungumzia Zanzibar izungumzie kama mzawa mwenye haki ya kushiriki sawa na Wazanzibar wengine ktk Zanzibar hii huru ambayo inatakiwa kuheshimu haki ya Uraia wako kama mzawa na mwenye historia kubwa na nchi hiyo. Na sii asili yako maana asili yako iko Oman ambako unapa enzi hadi leo hii kama mimi navyo paenzi Ukerewe hata kama ingekuwa chini ya Utawala wa Uganda ama Kenya bado haitaondoa asili yangu maana hii mipaka imewekwa na binaadam.
Swala la Population,
hapa mimi nakubaliana na wewe sana tu lakini nisichokubalianana wewe ni kipimo mnachotumia kwa sababu Zanzibar yenye watu 1.3 Mil wanaweza kufaidika na soko la Tanganyika na zaidi ya fursa na hapo ajira zinazopatikana Tanganyika kama ulivyosema wewe ulisomea Tanganyika na ukafanya azi miaka 8. Pia kumbuka kuna zaidi ya watu mil 3 wenye asili ya Zanzibar waishio Tanganyika leo hii hivyo hesabu hii sio ndogo kama unavyofikiria acha mbali wale waloenda kuishi nje.
Tatu,
Udogo wa Zanzibar
Udogo sio sababu kabisa kumezwa na Tanganyika ikiwa hatutakuwa tumeungana na kuunda serikali 1. Sidhani kama New York ama Hawaii hazikufaidika kutokana na udogo wao tena katika nchi 50. Itawezekana tu ikiwa tutaunda serikali moja maana serikali moja naweza kuimeza Znz ikawa kama Mkoa tu kwani Zanzibar haitakuwa na seirkali yake tena bali serikali moja ya Muungano. Hivyo Muungano wa serikali 2 au 3 unaondoa swala la kumezwa na ndio maana Zanzibar ina serikali yake leo hii ambayo kwa madai yenu inapewa asilimia 4.5 tu wakati mnasahau kwamba kwenye serikali ya Jamhuri Zanzibar bado ipo katika mambo ya Muungano ambayo bajeti yake huwashirikisha wabunge wa Zanzibar.
Na matumizi na wizara zote hizi za JMT, toka viongozi wake, watumishi hadi ofisi zake kote bara na Zanzibar hulipwa na serikali ya JMT sio serikali ya Znz. Kwa hiyo tusiwasikilize sana wanasiasa uchwara ambao hupotosha aidha makusudi ama kwa kutofahamu ya kwamba JMT ina mfuko wake tofauti na mfuko wa serikali ya Zanzibar na ndio maana tuna JMT kuhudumia nchi 2 na sii Tanganyika. Kwa maana ya kwamba ktk fungu la 10 ukitoa 2 za Serikali ya Znz, JMT inabakiwabakliwa na 8, hizi 8 sii za bara bali za serikali ya JMT ambayo matumizi yake hujadiliwa ktk bunge la JMT na huduma zake hufanyika pande zote mbili.
Na wala isifahamike kwa watu kwamba hizo 8 zilitakiwa kuwa za Tangayika (bara) kama wanavyofikiria kina
Nguruvi3 kwa sababu tu ya mchango mdogo wa Zanzibar ktk mfuko wa taifa wakati wanashindwa kuelewa kwamba Wazanzibar mil 1.3 waishio zanzibar ni asilimia 2.9 ya watu mil.45 wa bara, hivyo Zanzibar ikichangia asilimia 3 tu ya mfuko wa Taifa wametuzidi bara (mathlan JMT imekusanya bil.10 - bil.9.7 wanatakiwa kutoka bara na Zanzibar .3) hapa huwezi kusema ati Zanzibar wananufaika. Hawa wanaosema haya nao ni wapotoshaji wengine ambao somo la uchumi limewapiga magoli kama Brazil na Ujarumani.
Kuhusu Gharama.
Watu wengi wanachukulia swala hili juu juu tu kwa kwa sababu imependekezwa serikali ya JMT kuwa na mambo ya muungano 7 tu. Hii haiwezekani mkuu wangu wa sababu serikali ya JMT hutegemea fungu kutoka serikali zake kwa ajili ya matumizi ya nchi husika. Sasa ikiwa wizara zote zilizowekwa ktk mambo 7 ya Muungano hazizalishi ila ni matumizi matupu unafikiri hiyo serikali kuu itapata wapi fedha za kujiendesha? Na kama haina mamlaka kabisa ktk mambo mengine hiyo serikali itaweza vipi kuweka dhamana juu ya maswala la maendeleo ya nchi hizo ikiwa nchi hizo hazitambuliwi kimataifa? Nani atakaye ikopesha Tanganyika ama Zanzibar pasipo mhuri wa TAIFA maana msidhani kujiunga na UN ni kutambuliwa Uhuru wa nchi na mtawala bali hupata ridhaa ya mataifa hivyo unaweza kukopeshwa ktk miradi ya maendeleo na ukafuata masharti ya kimataifa. Tangayika na zanzbar ni sawa na mtoto wa chini ya Miaka 18 na mzazi ni JMT nani atakaye kubali kumkoposha mtoto ilihali mzazi hayupo labda awe molester!
Nani atakaye ipeleka Zanzibar au Tanganyika mahakama ya Dunia ikiwa nchi hizo zitagoma kulipa mikopo yake ambayo JMT imewawekea dhamana. Je, rais wa JMT akikataa kudhaminia kitu ambacho anakiona hakina umuhimu kwa taifa itakuwaje? Na hata nchi husika wakiamua kuzitumia vibaya fedha hizo huyo rais atakuwa na mamlaka gani ya kusimamisha matumizi hayo maana hayamhusu!. haya ndio maswali tunayotakiwa kujiuliza kwanza kabla ya kuvamia kupendekeza mambo 7 ya Muungano.
Kwa hiyo haiwezekani wala haitawezekana hadi serikali kuu ihusike kikamilifu na maswala ya maendeleo ya nchi hizi japo mipango ya utekelezaji wa shughuli hizo zitapitishwa na kutekelezwa na nchi husika. Na sheria zitakuwepo za JMT na zile za kila nchi ambazo serikali ya JMT haiwezi kupindua.
Halafu, kumbuka lile swala la 10-2 ikabakia 8 ya JMT hili haitakuwepo tena kwa sababu JMT haitakuwa na 10 tena bali Tanganyika na 7.7 kwa sababu Zanzibar hawatachangiza .3 zao, hivyo wao watasubiri kipenga. Na wizara za visiwani/bara hazitapungua ila kutakuwa na ongezeko la matumizi kwa mambo yote isipokuwa hayo 7 ya muungano ni sawa na kusema kati ya 22 za mambo ya muungano toa 7 kuna mambo 14 yatakuwa mzigo mpya kwa bara na visiwani ambao ni maskini. Ni rahisi sana kusema kwani asilimia .3 kitu gani, ila nakuhakikishia hiyo asilimia inaweza kuvunja muungano kwa sababu haitaonekana faida ya kuwa na mambo 7 yanayo wagharimu pande zote pasipo kuwepo vyanzo vya mapato yake yenyewe. Itakuwa swala la mtu una deep ndani ya mfuko wako kugharamia mambo 7 wakati kuna mambo 14 muhimu kwa wananchi wako ambayo yanahitaji fedha,huu utakuwa wendawazimu!. Ni sawa na Mapenzi ukanyimwa Unyumbashughuli yake kubwa sana, japo wanasayansi wanasema huo unyumba ni asilimia 1 tu mambo muhimu ktk ndoa.... I wonder!.
Kuna usemi huku Canada na Marekani watu husema hivi, inakuwaje Marekani au Canada wana madeni ya Trillioni za dollar wakidaiwa na nchi za nje, hawalipi madeni hayo bali wao ndio hutoa mikopo na misaada kwa nchi maskini kwa mabillioni? kwa nini wasitumie fedha hizo kulipa madeni yao?.. Jibu lake ni kwamba mikopo na misaada hiyo ndiyo biashara yenyewe ya Utandawazi, ni sawa na benki inayokupa mkopo wewe mkopo, wao hawana fedha mkononi bali wewe unayeweka akiba ya fedha zako benki ndizo huzunguka kwa kukopesha wengine na wao huvuta interest na mikataba ambayo huwanufaisha benki sio wewe. Hivyo Marekani wanapotupa sisi mikopo wao hufaidika na masharti yenye interest na mikataba mibovu kama tunayowapa hivyo hutengeneza mara 10 ya msaada walioutoa. Sisi woote ni wateja wa nchi matajiri na hivyo hawataisha kutukopesha ili wao watajirike.
Sasa wewe nambie hizi serikali kugharamia hayo mambo 7 ya Muungano watafaidika vipi kiuchumi wakati wangekuwa na nguvu zaidi kama yangekuwa yao, na kwa nini wasichukue mzigo mzima wenyewe? yaani kuua Muungano kabisa hata kama ni wa Shirikisho. Lini maskini wakashirikiana ktk matatizo ya ikadumu kama sio ndugu?