Duru za siasa: Bunge la Katiba, upotoshaji na kiwewe cha kuzinduka Tanganyika

Duru za siasa: Bunge la Katiba, upotoshaji na kiwewe cha kuzinduka Tanganyika

Mtu asiyejua hata mikopo tunayozungumzia ina malengo gani kwani tungeweza vipi kuchimba mafuta pasipo mikopo, tungeweza vipi kuchimba dhahabu, makaa ya mawe kujenga viwanja vya ndege, reli, bandari na zana zake n.k pasipo mikopo. Ikiwa Marekani wenyewe wanakopeshwa itakuwaje ajabu kwa Tanzania kukopeshwa fedha kwa ajili ya maendeleo yake? Sisi tunatengeneza Matrekta? tunatengeneza Ndege? tunatengeneza vifaa vya jeshi? Swala ni mikopo gani tunayoihitaji na kwa manufaa yapi ya Taifa jambo ambalo CCM wanapwaya kwa ufisadi wao. Huyo baba mwenye kiwanja (kiwanja sii nyumba kabla hujakijenga) sio lazima awe na fedha za kujenga nyumba bali tatizo ni pale anapopoteza hadi kiwanja kwa tamaa ya fedha.
The bottom-line tunakopa na nimesema hilo. Nje ya muungano tutakopa nimesema hilo.

Hatuhitaji Zanzibar ili tukope kwasababu sisi na Zanzibar hatukai mizani moja hata kwa bahati mbaya.

Pili, huwezi kuweka uchumi wa bilioni 400 katika mizani moja na Tanganyika.
Tanganyika haihitaji Zanzibar kwa jambo lolote lile.
Huna jibu na hujaweza kushawishi jamvi kwanini unadhani Tanganyika inaihitaji Zaznibar.

Kama wanaona hawawezi kuwa chini ya kivuli cha Tanganyika, njia nyeupee.
Hatuhitaji kwenda kuiba SMZ ambayo haichangii chochote.
Ni afadhali kzungumzia kiwanda cha sigara kwasababu impact yake kiuchumi ni kubwa kuliko SMZ.

Tunasema hivi Mkandara hawa Wazanzibar ambao hufikiri nafasi za ubalozi, kupokezana madaraka, kudai vyeo na rasilimali zisizowahusu waeleimishwe kuwa muungano ni uchumi na si bla bla

Tanganyika haiwezi kuwa employement centre ya Zanzibar.
Na wala hatuna sababu za kubeba shida za Wazanzibar, tuna zetu nyingi zinatosha.

Tunataka Tanganyika na itaxinduka. Muda wa kuwatua umefika na hakuna namna.

Kutaka JMT na SMZ ni sawa na Wasira, na hata sijui kwanini wewe na wasira hamna tofauti za mitazamo. Ni kwavile ame ku-influence kama Mbunge wako wa Bunda ?

Tanganyika itazinduka tu, hilo halina mjadala. Tunataka Tanganyika yetu, period.

Wznz wakiona wamechoka,njiaa nyeupee hatuwahitaji na wala hatutawatafuta kwa bakora au mabomu.Wakae kwao tu inatosha, kwani wanakuja Dodoma ni lazima?

Wakija safari hii waje na hoja za uchumi.
Kuzungumzia nafasi za balozi ambazo hawajui zinalipiwa na nani ni upuuzi.

Kutaka nafasi za ajira asilimi 21 wakati SMZ inaajiri chini ya asilimia 10 ni wendawazimu.
Kutaka mkuu wa majeshi n.k. wakati hawajui gharama za jeshi ni uhayawani.

Wznz uchumi mbele, nafasi za ubalozi mnaacha kuzungumzia mkifika chumbe.
Kama hamuwezi njia nyeupeee hakuna anayewalazimisha.

Ni Mkandara na Wasira wanaodhani ninyi mna umuhimu kiuchumi kwetu.

Dunia inafahamu ninyi ni kupe mgongoni.

Tumechoa tuacheni tupumue, miaka 50 na mfuko wa samadi mgongoni inatosha.
Tunataka tuoge sasa teremekeni chini mtembe wenyewe.

 
KIWEWE CHA TANGANYIKA

WAZEE WAPOTEZA BUSARA NA HEKIMA

HAKUNA KATIBA ISIYO NA MARIHDIANO.

Harakati za bunge la katiba hapo August 5 zinaendelea. Mwenyekiti Samwel Sitta anasema akidi inatosha na bunge llitaendelea. Anachikiona mzee sitta ni akidi tu ambayo basically ni namba ya makubaliano isiyo na nguvu yoyote katika muafaka wa katiba.

Katiba ni maridhiano baina ya wananchi, kila upande ukikubali kutoa au kupokea katika kutafuta kati na kati.Hakuna katiba inayotimiza matwakwa ya wananchi kwa 100%, lakini lazima iwe na maridhiano.

Kwavile lengo la CCM si kutaka rasimu ya Warioba itumike, jitihada zinafanywa kuvunja vifungu 1 na 6 na kuleta hoja ya S2 nje ya rasimu aliyosaini Rais Kikwete.

Wazee kama Sitta walipaswa kutumia busara na hekima kutafuta suluhu. Ndivyo alivyotumia Rais Mwinyi wakati wa kuanzisha vyama vingi. Leo tupo robo karne hatujapata matatizo licha ya vitisho vya CCM ya vyama vingi vingeleta vurugu na vita nchini.

Mzee Mwinyi na wazee wenzake waliongozwa na hekima kufikia muafaka wa kitaifa.
Sitta anaonekana kupwaya kama mwenyekiti wa CCM na hawaonekani kutumia busara wakati ambapo taifa linahitaji busara.

Sitta baada ya kuwakashifu upinzani kwa kuwaita vichwa ngumu, amejikuta katika mkutano na kamati yake ya CCM ambayo kwa kujidanganya anasema imefikia akidi.

Tunajua aliunda kamati hiyo kwa kuangalia CCM na akidi.
UKAWA wamegoma kuhudhuria na kumwacha na aibu kubwa.

Sitta alidhani ubabe alioutumia kubadilisha kanuni Kikwete aende kumkaanga Warioba ungefanya kazi .Kuanzia wakati ule, Sitta alipoteza hekima, busara, mvuto na thamani katika jamii iliyokuwa inamwamini kwa kiasi.

Tarehe 5 atakapokwenda bungeni ataitisha akidi. Uwezekano akidi hiyo ikatosha na shughuli za kuandika rasimu zikaanza. Ni rasimu ya CCM kwa kujua Sitta/CCM walitaka kubadilisha muundo uwe wa S2 waweze kuingiza rasimu yao kinyemela.

Sitta anaweza kufanikiwa kwa muda, lakini ni lazima ajifunze jambo moja au mawili.

UKAWA waliopotoka bungeni, waliobaki kwa zaidi ya siku 10 walikuwa wanaporomosha matusi bila chembe ya wanachokitetea.

August 5 na kuendelea hali itakuwa hiyo.Muda utakuwa kujadili UKAWA na matusi

Sitta atambue UKAWA ni sehemu ya uongozi wa taifa, inaungwa mkono na makundi yote.Huwezi kuitenga UKAWA ukawa na nchi ikabaki salama.

Nguvu ya UKAWA inatokana na maoni ya wananchi kutosikilizwa na si ya CCM 400 katika BMK

Hata kama Sitta atatumia mabomu, atabadili kila jambo na kila mbiu, hataweza kubadili ukweli huu
Katiba anayotaka kuandika na CCM kwa kutumia akidi tu ni ukosefu wa busara na hekima.
Na wala katiba haiwezi kuwa na heshima, itapingwa, katiba mpya itaandikwa tena.

Vurugu zikitokea Samwel Sitta kama mwenyekiti wake hatakuwa na mikono misafi.

Lakini pia kila jambo lina ubaya na uzuri wake. Uzuri wa hili jambo ni wananchi kupandwa na hasira na huenda likawasukuma kuiweka CCM kando.

Wasichotambua hawa wazee wasio na busara, ndani ya CCM wapo wasioridhika na hali iliyopo.
Hasira zitakapojidhihiri, majaaliwa yaweza kuwa safari ya CCM kuelekea maktaba ilipo KANU na UNIP.

Tusemezane
 
Mkuu wangu alhan Wasahlan, Kwanza Eid Mubarak,

Mimi nitakwamba ukweli wangu juu ya Historia yako na ile ya Zanzibar na wapi tunatofautiana. Uzawa wako na asili yako kwangu sii hoja bali fikra zako ndizo nazipinga kwa sababu hu represent Uzanzibar bali Asili na nasaba yako na fikra zako zinalenga kuhalalisha kisichowezekana.

Kwanza, nikwambie tu ya kwamba Zanzibar haikuwa huru ila baada ya Mapinduzi! hii kubali usikubali na ndipo tunaposhindana. Na sababu haswa ni kwamba huu uhuru wa Zanzibar ulitoka kwa mtawala gani? maana alokuwa akitawala miaka yote ni Sultan ambaye aliomba hifadhi ya Muingereza kama kinga kuepuka Uvamizi wa Mreno, hivyo swala la Muingereza kuruhusu uchaguzi na kumpa mwanya Sultan kugombea uongozi ulitokana na kutokuwepo na hofu ama Mreno. hivyo aliwajibika kutrudisha utawala ule kwa wenyewe. Utanisamehe lakini kusema kwamba Uhuru wa mwaka 1963 wa Zanzibar hiyo ni sawa kabisa na Uhuru wa Rhodesia November 11 1963 hivi ndivyo inavyoonekana kwa waafrika wote regardless of their race or colour. Na sidhani kama wewe umesimama hapa kutetea Utawala wa Jamheed toka kwa Muingereza alowapa hifadhi, bali Uhuru wa Wazanizbar toka utawala wa kisultan.

Unaweza kuwa Mwarabu mwenye asili ya Oman lakini hukubaliania na utawala wa Sultan na labda nikukumbushe tu ya kwamba wapo makaburu waliokataa Uhuru wa mwaka 1963 wakashirikiana na wenyeji hadi Uhuru kamili wa Zimbabwe ulipopatikana mwaka 1980. yalofuata Allahu Yaalam na wanapigana kumwondoa Mugabe sio tena kaburu maana limeshapita wala hakuna anayezungumzia Uhuru wa mwaka 1963. Hivyo sitokushauri utumie sana asili yako kuhalalisha Uhuru wa Zanzibar kwani Sultan ndiye alikuwa mtawala kabla ya Uhuru na ndiye alokuja kupata ushindi ktk uchaguzi wa mwaka 1963 kwa mchezo mchafu wa kisiasa kama aloufanya Ian Smith.

Tuyaache hayo, ila nakuomba unapozungumzia Zanzibar izungumzie kama mzawa mwenye haki ya kushiriki sawa na Wazanzibar wengine ktk Zanzibar hii huru ambayo inatakiwa kuheshimu haki ya Uraia wako kama mzawa na mwenye historia kubwa na nchi hiyo. Na sii asili yako maana asili yako iko Oman ambako unapa enzi hadi leo hii kama mimi navyo paenzi Ukerewe hata kama ingekuwa chini ya Utawala wa Uganda ama Kenya bado haitaondoa asili yangu maana hii mipaka imewekwa na binaadam.

Swala la Population,
hapa mimi nakubaliana na wewe sana tu lakini nisichokubalianana wewe ni kipimo mnachotumia kwa sababu Zanzibar yenye watu 1.3 Mil wanaweza kufaidika na soko la Tanganyika na zaidi ya fursa na hapo ajira zinazopatikana Tanganyika kama ulivyosema wewe ulisomea Tanganyika na ukafanya azi miaka 8. Pia kumbuka kuna zaidi ya watu mil 3 wenye asili ya Zanzibar waishio Tanganyika leo hii hivyo hesabu hii sio ndogo kama unavyofikiria acha mbali wale waloenda kuishi nje.

Tatu, Udogo wa Zanzibar

Udogo sio sababu kabisa kumezwa na Tanganyika ikiwa hatutakuwa tumeungana na kuunda serikali 1. Sidhani kama New York ama Hawaii hazikufaidika kutokana na udogo wao tena katika nchi 50. Itawezekana tu ikiwa tutaunda serikali moja maana serikali moja naweza kuimeza Znz ikawa kama Mkoa tu kwani Zanzibar haitakuwa na seirkali yake tena bali serikali moja ya Muungano. Hivyo Muungano wa serikali 2 au 3 unaondoa swala la kumezwa na ndio maana Zanzibar ina serikali yake leo hii ambayo kwa madai yenu inapewa asilimia 4.5 tu wakati mnasahau kwamba kwenye serikali ya Jamhuri Zanzibar bado ipo katika mambo ya Muungano ambayo bajeti yake huwashirikisha wabunge wa Zanzibar.

Na matumizi na wizara zote hizi za JMT, toka viongozi wake, watumishi hadi ofisi zake kote bara na Zanzibar hulipwa na serikali ya JMT sio serikali ya Znz. Kwa hiyo tusiwasikilize sana wanasiasa uchwara ambao hupotosha aidha makusudi ama kwa kutofahamu ya kwamba JMT ina mfuko wake tofauti na mfuko wa serikali ya Zanzibar na ndio maana tuna JMT kuhudumia nchi 2 na sii Tanganyika. Kwa maana ya kwamba ktk fungu la 10 ukitoa 2 za Serikali ya Znz, JMT inabakiwabakliwa na 8, hizi 8 sii za bara bali za serikali ya JMT ambayo matumizi yake hujadiliwa ktk bunge la JMT na huduma zake hufanyika pande zote mbili.

Na wala isifahamike kwa watu kwamba hizo 8 zilitakiwa kuwa za Tangayika (bara) kama wanavyofikiria kina Nguruvi3 kwa sababu tu ya mchango mdogo wa Zanzibar ktk mfuko wa taifa wakati wanashindwa kuelewa kwamba Wazanzibar mil 1.3 waishio zanzibar ni asilimia 2.9 ya watu mil.45 wa bara, hivyo Zanzibar ikichangia asilimia 3 tu ya mfuko wa Taifa wametuzidi bara (mathlan JMT imekusanya bil.10 - bil.9.7 wanatakiwa kutoka bara na Zanzibar .3) hapa huwezi kusema ati Zanzibar wananufaika. Hawa wanaosema haya nao ni wapotoshaji wengine ambao somo la uchumi limewapiga magoli kama Brazil na Ujarumani.

Kuhusu Gharama.
Watu wengi wanachukulia swala hili juu juu tu kwa kwa sababu imependekezwa serikali ya JMT kuwa na mambo ya muungano 7 tu. Hii haiwezekani mkuu wangu wa sababu serikali ya JMT hutegemea fungu kutoka serikali zake kwa ajili ya matumizi ya nchi husika. Sasa ikiwa wizara zote zilizowekwa ktk mambo 7 ya Muungano hazizalishi ila ni matumizi matupu unafikiri hiyo serikali kuu itapata wapi fedha za kujiendesha? Na kama haina mamlaka kabisa ktk mambo mengine hiyo serikali itaweza vipi kuweka dhamana juu ya maswala la maendeleo ya nchi hizo ikiwa nchi hizo hazitambuliwi kimataifa? Nani atakaye ikopesha Tanganyika ama Zanzibar pasipo mhuri wa TAIFA maana msidhani kujiunga na UN ni kutambuliwa Uhuru wa nchi na mtawala bali hupata ridhaa ya mataifa hivyo unaweza kukopeshwa ktk miradi ya maendeleo na ukafuata masharti ya kimataifa. Tangayika na zanzbar ni sawa na mtoto wa chini ya Miaka 18 na mzazi ni JMT nani atakaye kubali kumkoposha mtoto ilihali mzazi hayupo labda awe molester!

Nani atakaye ipeleka Zanzibar au Tanganyika mahakama ya Dunia ikiwa nchi hizo zitagoma kulipa mikopo yake ambayo JMT imewawekea dhamana. Je, rais wa JMT akikataa kudhaminia kitu ambacho anakiona hakina umuhimu kwa taifa itakuwaje? Na hata nchi husika wakiamua kuzitumia vibaya fedha hizo huyo rais atakuwa na mamlaka gani ya kusimamisha matumizi hayo maana hayamhusu!. haya ndio maswali tunayotakiwa kujiuliza kwanza kabla ya kuvamia kupendekeza mambo 7 ya Muungano.
Kwa hiyo haiwezekani wala haitawezekana hadi serikali kuu ihusike kikamilifu na maswala ya maendeleo ya nchi hizi japo mipango ya utekelezaji wa shughuli hizo zitapitishwa na kutekelezwa na nchi husika. Na sheria zitakuwepo za JMT na zile za kila nchi ambazo serikali ya JMT haiwezi kupindua.

Halafu, kumbuka lile swala la 10-2 ikabakia 8 ya JMT hili haitakuwepo tena kwa sababu JMT haitakuwa na 10 tena bali Tanganyika na 7.7 kwa sababu Zanzibar hawatachangiza .3 zao, hivyo wao watasubiri kipenga. Na wizara za visiwani/bara hazitapungua ila kutakuwa na ongezeko la matumizi kwa mambo yote isipokuwa hayo 7 ya muungano ni sawa na kusema kati ya 22 za mambo ya muungano toa 7 kuna mambo 14 yatakuwa mzigo mpya kwa bara na visiwani ambao ni maskini. Ni rahisi sana kusema kwani asilimia .3 kitu gani, ila nakuhakikishia hiyo asilimia inaweza kuvunja muungano kwa sababu haitaonekana faida ya kuwa na mambo 7 yanayo wagharimu pande zote pasipo kuwepo vyanzo vya mapato yake yenyewe. Itakuwa swala la mtu una deep ndani ya mfuko wako kugharamia mambo 7 wakati kuna mambo 14 muhimu kwa wananchi wako ambayo yanahitaji fedha,huu utakuwa wendawazimu!. Ni sawa na Mapenzi ukanyimwa Unyumbashughuli yake kubwa sana, japo wanasayansi wanasema huo unyumba ni asilimia 1 tu mambo muhimu ktk ndoa.... I wonder!.

Kuna usemi huku Canada na Marekani watu husema hivi, inakuwaje Marekani au Canada wana madeni ya Trillioni za dollar wakidaiwa na nchi za nje, hawalipi madeni hayo bali wao ndio hutoa mikopo na misaada kwa nchi maskini kwa mabillioni? kwa nini wasitumie fedha hizo kulipa madeni yao?.. Jibu lake ni kwamba mikopo na misaada hiyo ndiyo biashara yenyewe ya Utandawazi, ni sawa na benki inayokupa mkopo wewe mkopo, wao hawana fedha mkononi bali wewe unayeweka akiba ya fedha zako benki ndizo huzunguka kwa kukopesha wengine na wao huvuta interest na mikataba ambayo huwanufaisha benki sio wewe. Hivyo Marekani wanapotupa sisi mikopo wao hufaidika na masharti yenye interest na mikataba mibovu kama tunayowapa hivyo hutengeneza mara 10 ya msaada walioutoa. Sisi woote ni wateja wa nchi matajiri na hivyo hawataisha kutukopesha ili wao watajirike.

Sasa wewe nambie hizi serikali kugharamia hayo mambo 7 ya Muungano watafaidika vipi kiuchumi wakati wangekuwa na nguvu zaidi kama yangekuwa yao, na kwa nini wasichukue mzigo mzima wenyewe? yaani kuua Muungano kabisa hata kama ni wa Shirikisho. Lini maskini wakashirikiana ktk matatizo ya ikadumu kama sio ndugu?

Mkandara

Naona tuna mitazamo tofauti kwani wewe umejikita zaidi katika jicho la kisiasa na mimi natazama kwa jicho la kiuchumi.

Nilichokubainishia NA KUKUOMBA UFUNGUE UZI MAALUM WA HIZI HOJA ZAKO ili nikudadavulie kwa kina impact ya kila jambo katika mtazamo wa kiuchumi, kijamii na hata kisiasa.

Kifupi Tanganyika na Znz zina tofauti kubwa sana katika mtazamo wa historia na hata changamoto zake. Kumbuka kuwa Znz kuna uunguja na Upemba wakti Tanganyika kuna Uislam na Ukristo. Na haya yote ni makovu ya utawala wa kikoloni kwa nchi hizo.(NB Wakoloni walitumia divide and Rule ).lakin kubwa lingine mila, desturi na sirka za watu wa nchi hizi mbili ni tofauti sana sana kiasi kwa mtazamo hata wa kijamii ilikuwa si rahisi kuungana kabisa kama si mabavu kutumika.

Lakin lingine kubwa wachumi tunabainisha kuna uchumi mpana na uchumi mdogo.Hili ni jambo lenye athari kubwa sana kwa nchi hizi mbili ambazo zimeungana.

Kumbuka kuwa wachumi tunabainisha maendeleo kwa dhana pana sana ikiwa pamoja na uhuru wa kisiasa, usawa wa kiuchumi, huduma za jamii , uhakika wa uwazi na usalama. Hii ni dhana kubwa sana katika muungano wowote duniani.

Nafikiri ukiweka uzi maalum nitakupa darsa kubwa sana kwa hili na UTAGUNDUA KWANINI WAZNZ HATA SIKU MOJA ASILAN ABADAN HAWAWEZI KUKUBALI KUUNDA SERIKALI MOJATU YA MUUNGANO.

Tusivuruge title ya mada hii kwa kuzungumzia mambo mengine.

Samahani sana mkuu.

nakubuka wakt ule nikiwa mwanza zawadi kuuubwa ya kupelekea watu wa ukerewe ilikuwa mikate. je vipi siku hizi bekary zimeshajengwa?

 
Wanaduru

Kila mara tumekuwa tukitoa maoni kama raia wengine wenye upendo na nchi hii.
Kwa bahati mbaya kuna nyakati maoni hayo yanachukuliwa kama sehemu ya 'umbea, propaganda, uzandiki, uzushi n.k.''

Hatujachoka kuandika kwa kuamini kuwa kila mtu ana uhuruna mipaka yake.
Imefika mahali baadhi yetu wakatubatiza, wakatusilimisha, wakasema tuna chuki n.k. bila kuangalia mantiki ya kile tunachokisema.

Naweka baadhi ya nukuu tulizowahi kuandika katika uzi huu kama ushahidi wa kuwa maoni yetu si chuki dhidi ya mtu, watu imani, kabila au taifa. Maoni yetu ni maonyo.


Nikumbushe kuwa mdahalo wa juzi ambao Profesa Palamagamba Kabudi alishiriki na kutoa shule nzito kwa taifa, haukuisha bila kusikiliza maneno yetu. Wenye chuki na duru za siasa sijui chuki hizo watazielekeza wapi.
Profesa aliyebobea kasema maneno haya

' Watanganyika ni wa kuogopwa sana. Mambo ya Zanzibar yapo mezani. Yale ya Watanganyika yapo vifuani. Siku yakitoka itakuwa ni hatari kubwa. Wataidai Tanganyika yao kwa nguvu mitaani....''

Sisi duru miezi mingi sana huko nyuma tulisema haya kwa uchache tu miongoni mwa mengi
Hizi harakati za kugawa peremende kwa wazanzibar hazitaleta utangamano maana wenye muungano wapo mitaani.Ipo siku wataamua hatima ya muungano mitaani na wala si kwenye semina.
Kuna mambo 7 tunaweza kuwasaidia, kinyume chake watatusaidia kuizundua Tanganyika.Mkandara hapa tulipo hakuna tena Utanzania, wznz wameshaharibu na wala usiwasingizie Watanganyika.

Miaka 50 tumekubali kupoteza ID yetu, kinyume chake wznz wanatufanya shamba la bibi la ID wasolipia au kuchangia isipokuwa wanapotaka, naomba, nipe namimi, ongezeka baba, na vilio vya kitoto.Watatusaidia kwa gharama zao kuirudisha Tanganyika.
Mkandara;9824960]Hata hivyo sitapunzika kuonyesha uhuni wa kundi la watu laki kadhaa dhidi ya milioni 43.
Hatuna tatizo na znz, tunataka Tanganyika tusimamie mambo yetu, tuache kuwanyonya na kuwategemea kwa jina.

Hapa tulipofika, hakuna njia, lazima Tanganyika izinduke. Ikishindikana Dodoma wzanz watatusaidia kwa gharama zao.
Tunaposimama kutetea nchi na watu wetu tunaambiwa wapuuzi.
Hate me, love me, I will stand for what is right.
I will stand for mother Tanganyika and my allegiance is unwavering
Hizi harakati za kugawa peremende kwa wazanzibar hazitaleta utangamano maana wenye muungano wapo mitaani.

Ipo siku wataamua hatima ya muungano mitaani na wala si kwenye semina.
Kuna mambo 7 tunaweza kuwasaidia, kinyume chake watatusaidia kuizundua Tanganyika.Mkandara hapa tulipo hakuna tena Utanzania, wznz wameshaharibu na wala usiwasingizie Watanganyika.

Miaka 50 tumekubali kupoteza ID yetu, kinyume chake wznz wanatufanya shamba la bibi la ID wasolipia au kuchangia isipokuwa wanapotaka, naomba, nipe namimi, ongezeka baba, na vilio vya kitoto.

Watatusaidia kwa gharama zao kuirudisha Tanganyika.
Mkandara;9824960]Hata hivyo sitapunzika kuonyesha uhuni wa kundi la watu laki kadhaa dhidi ya milioni 43.Hatuna tatizo na znz, tunataka Tanganyika tusimamie mambo yetu, tuache kuwanyonya na kuwategemea kwa jina.Hapa tulipofika, hakuna njia, lazima Tanganyika izinduke.

Ikishindikana Dodoma wzanz watatusaidia kwa gharama zao.
Tunaposimama kutetea nchi na watu wetu tunaambiwa wapuuzi.

Hate me, love me, I will stand for what is right.
I will stand for mother Tanganyika and my allegiance is unwavering!
Waliosema tuna chuki, kumbe tupo wengi hata Maprofesa. Je ni chuki au ni maonyo?

Hatuta acha kusema kwasababu kuna wenye inda na maoni yetu.
Hutaacha kusema kwasababu tunitwa wenye chuki, makafir, wambea au wazindiki.

Hizo kwetu sisi ni sifa kwavile tu kuna anayeziona kinyume. Zinachoma na kuunguza.
Hata sindano ni chungu lakini inatibu. Tutatibu hata wapige kelele.

Tutawadunga sindano hata kama ni ndefu na butu. Lengo letu ni kuwatibu.

Kumbe wengine wanaona kama tuonavyo.

''Ni bora sisi wajinga maana tuna unyenyekevu, kuliko wapumbavu wenye kukakamaa-Kabudi''
 
wanaduru natumani siku ya leo mmeamka vichwa vikiwa vimeshehen maswali kadhaa kama nilivyo mimi.
miongoni mwa maswali hayo ni kama haya:-
a) je CCM itafanikiwa kupata katiba mpya?
b) je ukawa huko nje wanafanya nini?
c) wananchi wa tanzania wanataka nini?
d) je nini hatma ya huu mgawanyiko wetu, kwenye hii kaatiba kisiasa, kiuchumi na kijamii.
e) je ni taswira gani tunayoijengea nchi yetu mbele za mataifa mengine?

Binafsi kila nikitafakari juu ya haya maswali na mengine kadhaa nakosa nguvu ya kusimama na kujisifu kwamba mimi ni miongoni mwa raia wanaotoka kwenye nchi yenye amani na utulivu. hivi najiuliza twawezaje kusema tusambaze upendo ikiwa sisi wenyewe hatuwez kukaa na kukubaliana nini tunachokitaaka. twawezaje kusema tanzania yenye neema ilihali ule mshikamano na umoja kati yetu haupo?

mbona kama tunajenga nyumba ambayo tayari msingi umeshaanza kupata ufa lkn tunaziba macho kwa kitambaa yasione mpasuko/ufa huo na kuendelea kumwambia fundi aeke tofali juu bila kujali kwamba muda si mrefu ufa ule utadondosha nyumba?

Hebu wenzangu tusemezane hapa je nini kifanyike ili kunusuru hali tukikumbuka kwamba majadiliano yameshashindikana?
 
gfsonwin

Nianze kwa kupitia maswali yako hapo juu.

a)CCM haiwezi kupata katiba. Jamii imezinduka na ulaghai umefikia mwisho. Kauli ya ''you can fool some people for...' sasa ina maana zaidi. Wanaweza kulazimisha lakini mwisho wa safari ni aibu.
Hadi tunaposemezana hapa, wapo Wabunge wenye akili na busara zao wanaotamani ardhi ipasuke waingie.

b)UKAWA wana matatizo. Tatizo lao kubwa ni kufanya kazi kama zima moto na si kwa mpangilio.
Huu ulikuwa wakati mwafaka wa kupita na kutoa elimu ya umma dhidi ya uhuni na uhalifu unaoendelea Dodoma.
Watasubiri hadi CCM watoke Dodoma, ndipo utawasikia Kibandamaiti, Mivinjeni, Chalinze na Malinyi.

c)Wananchi wa Tanzania wanataka katiba mpya.
Katiba itakayowapa uwezo wa kuamua hatima ya nchi yao.
Katiba itakayowawajibisha wahusika na kuwajibisha wananchi.
Katiba itakayoondoa umangi meza wa kuiba na kuambiwa rudisha.
Katiba itakayotoa viongozi kwa sifa na uwezo na si wajihi na maumbo.
Wanataka katiba inayoendana na dunia wanayoishi, dunia ya ushindani.
Katiba itakayomaliza matatizo yasiyomalizika yanayopakwa rangi, kero, usumbufu, hali ya hewa n.k.

d) Tulianza kupOteza taswira yetu kwa kushindwa kuwa viongozi wa kanda na bara.
Sasa hivi tunaficha nyuma ya AU, SADCC n.k. kutoa misimamo yetu.

Hatusimamia haki na usawa duniani. Tunashindwa kusema hili baya hili zuri.
Tumekuwa wapitisha bakuli, wazuri wa kubwabwaja na mitambo ya kufua uongo na si maarifa.
Tukiwauza majirani katika mikataba tuliyosaini ili kufurahisha wanunua suti na mafungu ya uchaguzi

Sasa tupo next level. Tunaligawa taifa kwa kutosikiliza wananchi.
Hatuna uwezo wa kuja pamoja kama taifa.

Tunaongozwa na genge la wahuni wanaojiita wahafidhina.
Hao ndio wamejigeuza taifa na taifa ndio wao.
Ni genge hilo ndilo linachezea maoni ya wanachi pale Dodoma.

Genge la kihalifu linaloogopa TV eti kutoua uzalendo.
Uzalendo ni wezi waliopewa nafasi waandike katiba mafichoni ili tuseme hewala.
Tumepoteza tunu yetu kama watu wa taifa moja.
Tunaelekea kule tulikotoka kuwasuluhisha wenzetu.

Majirani wanajiuliza kumbe mganga hajigangi. Si kweli, mganga wetu wa sasa anatumia madogori.
Waganga wa Tanzania walikuwa weledi wenye maarifa.

Hakuna sababu ya kuona aibu kuhusu umoja wa taifa hili. Taifa hili ni imara, tunachotakiwa kufanya ni kukataa kuwa watumwa wa kundi dogo ndani ya watu milioni 43. Tunaweza tukisimama pamoja.

Tusemezane
 
Watanzania kupata au kutokupata katiba mpya kutategemea Zaidi kura ya maoni kuliko ni namna gani mchakato wa katiba unavyoendeshwa katika Bunge la Katiba.

Kiufupi Iwapo Kura ya Maoni Itaikubali Katiba itakayoletwa na Bunge la CCM , then tunasema THE END JUSTIFIES THE MEANS!!!!. Na kwa kuwa wananchi wenyewe ndio watakuwa Wameipitisha katiba hiyo, hoja ya kudai kwamba katiba mpya siyo zao la wananchi itakufa kifo cha mende!!!!
 
Watanzania kupata au kutokupata katiba mpya kutategemea Zaidi kura ya maoni kuliko ni namna gani mchakato wa katiba unavyoendeshwa katika Bunge la Katiba.

Kiufupi Iwapo Kura ya Maoni Itaikubali Katiba itakayoletwa na Bunge la CCM , then tunasema THE END JUSTIFIES THE MEANS!!!!. Na kwa kuwa wananchi wenyewe ndio watakuwa Wameipitisha katiba hiyo, hoja ya kudai kwamba katiba mpya siyo zao la wananchi itakufa kifo cha mende!!!!
Na hilo ndilo CCM wanalitaka. Kikwazo kikubwa kwao ni namna ya kuingiza S2 katika maandishi. Wanajua mbele ya safari NEC ipo, Msajili yupo, Polisi wapo hakuna tatizo kwa kushinda kura ya maoni, the end justifies the means.

Unfortunate that will not happen this time, CCM is in a precarious situation. The future is uncertain
 

TANGANYIKA INATIA KIWEWE.

CCM KIWEWE TUPU
WANAKULA, WANATAPIKA HALAFU WANAMEZA

HOFU TU , HAWAJUI WASIMAMIE WAPI. HAWAKUMBUKI WALIKATAA NINI

Baada ya kuona ufafanuzi wa Prof Kabudi na Warioba, hatimaye Wajumbe wa BMK-CCM wameamua kujadili ibara 1-15 kwa pamoja. Kuna hoja zinazojitokeza hapa za kushangaza.

Kwanza, viongozi waandamizi wa CCM wamekaririwa mara nyingi wakimtuhumu Jaji Warioba kwa kuleta 'dude' ambalo hakutumwa kulifanyia kazi.

Mwenyekiti wa CCM ambaye ni Rais si kuwa alikaa kimya wakati Warioba anaanikwa hadharani, bali nae katika hotuba ya ufunguzi alitilia shaka takwimu za Warioba.

Midahalo iliyopita, Waziri Wassira, Waziri Lukuvi nao wamesema bila kificho, takwimu zina matatizo.Hoja yao kubwa ikiwa ni idadi ya watu waliohojiwa.

Wanaposimamia ni kuwa ili takwimu zilete maana lazima idadi ifikiie angalau 30%.
Wasira na Lukuvi wamesema katika midahalo mchana kweupe.

Leo Wajumbe wa BMK-CCM wamegawnyika katika kamati ili kujadili vifungu 1-15 vya rasimu ile ile wanayoisema ni 'utunzi' wa mzee Warioba.

Rasimu ile ile wanayotilia shaka takwimu zake na mwenyekiti wao Rais wa JMT.
Na rasimu ile ile waliyoita 'dude' na mawazo ya Warioba.

Inashangaza sana, wanawezaje kufanyia kazi takwimu wasizokubalina nazo?

Je hiyo rasimu yao itakuwa na uhalali gani, ikiwa rasimu ya Warioba ilikosa uhalali wa hadidu za rejea na takwimu?

Je, idadi ya wajumbe wa BMK-CCM inaweza kutoa takwimu halisi (400) kuliko watu waliohojiwa na Warioba(20,000)?

Hii ina maana moja, CCM hawana hoja ya msingi ya kupinga Rasimu ya Warioba.

Wanachotaka ni kukataa tu ili waandike rasimu yao pembeni.

Wakishamaliza kuandika tutawauliza, takwimu wamepata wapi na analysis ya takwimu hizo imefanyaika vipi, tukizingatia walishasema Warioba kaleta kitu asichotumwa, kisicho katika hadidu za rejea.

Huku kubabaika kunazidi kuwaanika CCM na kuwafanya waonekana kama mazuzu.

Hakuna mtu mwenye akili timamu anayezitumia vema anaweza kukaa chini na kueleza kubabaika huku kunatokana na nini na si kujitia wendawazimu bila sababu.

Hoja ilikuwa wakatae kabisa rasimu ya Warioba waliyoita 'dude' ili watengeneze yao.

Kurudi kuifanyia kazi rasimu ile ile waliyokataa kuwa si halali ni sawa na kula, kutapika na halafu kufakamia matapishi yale yale.

Aibu na dhalili sana

Tusemezane

MJINI CHAI
 
Last edited by a moderator:
KIWEWE CHA KUZINDUKA TANGANYIKA

CCM WATAKA S2 MABORESHO

WAMESUBIRI TUME IMALIZE KAZI ILI WAIBIE 'PLAGIARISM''

CCM wapo Dodoma wakijadili rasimu wasiokubalina na takwimu wala upembuzi wake.
Huko nyuma, walidai wanachokitaka ni maboresho ya S2

Maana ya maboresho ni kukubaliana na hoja kuwa kilichopo kinaboa na hivyo wanataka kiboreshwe.

Hawana proposal ya maboresho, walicho nacho ni hoja ya kuboresha.
Hawana tathmini ya maboresho, walicho nacho ni hoja ya maboresho.

Kumbukeni, wanachojadili ni rasimu ya tume ya Warioba.
Rasimu waliyodai Warioba kaja na mawazo yake, takwimu zake, mambo yasiyokidhi haja ya kuandika katiba mpya.

CCM wapo Dodoma wakijadili kitu kile kile wasichokuwa na imani nacho!!!

Wanachotaka kukifanya ni kuweka madai ya wazanzibar mezani na kuanza kuwafariji.
Wasichokielewa , huwezi kuwafariji Wazanzibar kwa kutumia Tanganyika.

Faraja hiyo itakuwa ya kuchagua bega. Faraja wanaoitafuta itazidisha maumivu kwa Watanganyika.
Hapo kitakachotokea hatujui ni kitu gani.

Prof Palamagamba Kabudi kasema, Watanganyika wana yao moyoni.
Siku yakitoka itakuwa hatari.Wataidai Tanganyika yao kwa nguvu.

Kwa mtazamo wetu, kuidai Tanganyika hakutawahusu Watanganyika peke yao.
Kitakachotokea ni wa Tanganyika kudai haki zao kama Watanganyika.

Hakutakuwa na Utanzania tena, kitakachokuwepo ni Utangayika dhidi ya Utanzania.
Mfano, Wazanzibar walifikia mahali pa kuona kuwa ili S3 walizotaka zipatikane, njia rahisi ilikuwa kuwafukuza Watanganyika.
Ndiyo yale ya kuchoma vibanda na watu moto.

Wakati CCM wanatengeneza rasimu ya maboresho S2, wakumbuke hawatafanikiwa kutenda jambo lolote nje ya maoni ya tume.

Kitakachofanyika ni kuchukua maoni ya tume wanayotaka na kuyaingiza katika rasimu yao.
Hatujawahi kuonyeshwa S2 maboresho, hivyo wazo lolote lile litakalofanana na wazo la tume itakuwa ni kuiba kazi.

Ni wizi wa kazi za kitaalam kwasababu, kwanza, hawaamini tume ya Warioba.

Pili, watatumia kazi hizo bila kukiri(acknowledge) kuwa ni maoni ya tume.

Hawawezi ku-acknowledge kwani kufanya hivyo kutaua nguvu ya hoja kwamba yale yalikuwa maoni ya Warioba na si tume na kwamba takwimu ni feki.

Ni kwa maana hiyo, kinachoendelea Dodoma ni mazingaombwe, mwisho wa siku hakuna kitu cha maana watakachopata.
Umma hautawaelewa hata kidogo.

Ni upotevu wa fedha bila sababu.

Tusemezane
 
Watanzania kupata au kutokupata katiba mpya kutategemea Zaidi kura ya maoni kuliko ni namna gani mchakato wa katiba unavyoendeshwa katika Bunge la Katiba.

Kiufupi Iwapo Kura ya Maoni Itaikubali Katiba itakayoletwa na Bunge la CCM , then tunasema THE END JUSTIFIES THE MEANS!!!!. Na kwa kuwa wananchi wenyewe ndio watakuwa Wameipitisha katiba hiyo, hoja ya kudai kwamba katiba mpya siyo zao la wananchi itakufa kifo cha mende!!!!

Na hilo ndilo CCM wanalitaka. Kikwazo kikubwa kwao ni namna ya kuingiza S2 katika maandishi. Wanajua mbele ya safari NEC ipo, Msajili yupo, Polisi wapo hakuna tatizo kwa kushinda kura ya maoni, the end justifies the means.

Unfortunate that will not happen this time, CCM is in a precarious situation. The future is uncertain

unajua nini?? tayari serikali ya CCM imeshaone kwamba hapa ni pachungu, na kwamba kinachotakiwa sasa ni jinsi gani ama nini kifanyike ili kunusuru hali. Kma ulimsikiliza naibu waziri wa fedha ameshajua kwamba wanajitegea upanga waangukie na hapo wanajua kiama inakuja.

kwakua siye tunayo njia nyingine kwamba kwenye kura ya maoni twaweza kukataa ama kukubali basi UKAWA ungekuwa ni muda mwafaka wa wao kupita na kutoa elimu sahihi ili hadi iyo oct tayari wananchi wawe wameshajaa uelewa mzuri na wasiyumbishwe.

kwanza sidhan hata kama hii katiba itapatikana na hapa Sitta kajishusha heshima sana, sijui woga kaupata wapi na kwann kabadilika namna hii.
 
Watanzania kupata au kutokupata katiba mpya kutategemea Zaidi kura ya maoni kuliko ni namna gani mchakato wa katiba unavyoendeshwa katika Bunge la Katiba.

Kiufupi Iwapo Kura ya Maoni Itaikubali Katiba itakayoletwa na Bunge la CCM , then tunasema THE END JUSTIFIES THE MEANS!!!!. Na kwa kuwa wananchi wenyewe ndio watakuwa Wameipitisha katiba hiyo, hoja ya kudai kwamba katiba mpya siyo zao la wananchi itakufa kifo cha mende!!!!
Sijabahatika kuelewa iwapo unabariki the end and means ulizojadili au unapingana nazo.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
UKAWA KUNA MITEGO MIWILI MBELE YENU

JIPANGENI LA SIVYO, MTAJIKUTA KATIKA MKENGE KAMA KAWAIDA

Gazeti maarufu la Rai Mwema toleo la jana limeandika kuhusu mambo mawili.
1. Ghiliba za kutafuta wajumbe 16
2. Kikao cha usuluhishi Dodoma cha Wazito

1. Ghilba ya kununua wajumbe
Katika uzi huu hilo tumeliongelea kama mkakati wa CCM. Jitihada za kuhonga wajumbe 16 ili CCM ipate 2/3 ya Zanzibar zinaendelea. Jitihada hizo ni nyingi zikihusisha kuundoa umma kutoka kwenye hoja ili CCM iweze kufanya vitu vyao.

Kuna tukio limetokea Zanzibar znz siku za karibuni.Tukio hilo halikuja kama mvua, lilikuwa na makusudio.
kwanza, kupunguza nguvu za ushawishi kwa Wazanzibar
pili, kuwatisha wale wanaosita sita na huko ndiko kwenye wajumbe 16
Tatu kuleta mtafaruku katika jamii kwa kujua wnz ni wepesi wa kuhamaki.

Ilikusudiwa yawepo maandamano ili kupunguza nguvu za mjadala wa kaiba.
Kwa bahati nzuri hilo halikutokea na matokeo yake ni midahalo iliyoendelea kwa nguvu kuuelewesha umma nini kinachoendelea.

Siku mbili hizi vyombo vya habari vimeshadidia kurudi kwa Leticia na Shibuda bungeni kana kwamba hakuna asiyewafahamu.

Habari hizo zimepewa uzito kuliko wajumbe zaidi ya 100 na viongozi wao walioko nje.Hizo ni propaganda ili kugawa UKAWA.

Hili la wajumbe 16 kutafutwa kwa ''usikivu wao'' nalo pia lipo njiani.
UKAWA,wajiandae kisaikolojia maana litatokea.

Askofu Abel Muzorewa wa Zimbwabe alipewa nafasi ya kuwa waziri mkuu, akunda serikali ya kibaraka chini ya Ian Smith.
Leo hata Kaburi lake halijuikani lilipo.

Wapo wafanyakazi wa CIA waliomsaliti Martin Luther King.
Leo Marekani imegeukia dhana ya King na wasaliti hawatajwi hata kwa bahati mbaya.

Endapo wana tume ya Warioba na watu wasiozidi 7 wameweza kutetea masilahi ya nchi tena wakiwa hawajulikani wala kuwa na majina, hakuna sababu za watu 100 kushindwa kusimamia masilahi hayo hayo.

Safari ya kutafuta haki si rahisi, imejaa miba na majabali.
Ni wale tu wanaoamini katika haki ndio watafika mstari wa mwisho.

Kama Masiah alisailitiwa nani miongoni mwetu anayeweza kukana usaliti.

Huo ni mtego wa kwanza.

Tuangalie mtego wa pili hapa chini

KIKAO CHA SULUHU DODOMA

Zipo habari za wazee wakubwa wanaotajwa kuwa viongozi wa nchi wastaafu akiwemo JK watakuwa na kikao cha maridhiano Dodoma. Kikao kinakuja wakati UKAWA wakiwa wamegoma na CCM wakiendelea kuandika katiba yao.

UKAWA wanapaswa kutambua kuwa kikao hicho si cha kawaida, kina zaidi ya hapo.

Tunasema hivyo kwasababu nyingi
1. Hadi hapa tulipofika wazee hao hawakuona tatizo?

2. Wazee hao walifanya nini kukemea njia za kuligawa taifa kwa majina na rangi, dini na maeneno

3. Kwanini wazee hao ambao ni CCM bila shaka, walishindwa kukemea chama chao kuweka msimamo wa pamoja

4. Kwanini wazee hao hawajaweza kumsadia mzee Mwenzao Warioba anapowekwa ubaoni kusimangwa

5. Wazee hao wanaolelewa na chama watakuwa na msimamo gani tofauti na chama chao

6. Miongoni mwa wazee hao, wengine walikataa tume zilizopita, leo wanakipi cha tofauti walichoshindwa huko nyuma

7. Kwanini wazee hao waone UKAWA ni muhimu, wakati huo huo waone ni sawa CCM kuendelea kaundika katiba yao

8. Wazee hao wanachotaka ni kitu gani, UKAWA warudi bungeni au kujadili rasimu ya Warioba.

Kwa UKAWA kama kitakuwepo kikao cha namna hiyo, huo utakuwa mtihani mkubwa sana.

Lipo shinikizo la wazee hao na hoja itakuwa ni wao kurudi Bungeni.

Kinachotakiwa kwa sasa na CCM ni kujenga kauhalali ka kisiasa tu basi, si katiba.

Ndio maana kila siku wanatafuta wajumbe 16 ili wapate 2/3.

CCM hawatafuti watu wenye uwezo, akili na busara.
Wanatafuta 2/3 ili kujaza idadi ya watu na kujenga uhalali wa kisiasa.

Kisheria wana uhalali, kisiasa ndipo walipokwama.

UKAWA watajipima kwa kuangalia umma ulio nyuma yao.

Tusemezane
 
KIWEWE CHA TANGANYIKA CHAMKUMBA NAPE
ASHINDWA KUELEWA SHERIA YA RASIMU ILISEMA NINI

DODOMA: KAMATI YA UMMY YATENGENEZA RASIMU YAO

KAMATI ZINAJADILI RASIMU WALIYOSEMA NI MAONI BINAFSI

Jana katibu mwenezi wa CCM alitoa kauli kali dhidi ya tume ya Warioba.
Katika utetezi , katibu alisema lugha ilikuwa nyepesi na isiyo na uungwana.
Akaendelea kutetea haki ya Rais na CCM kutoa maoni.

Alichoshindwa kufahamu mh katibu ni kuwa, sheria iliyoanzisha mchakato na ambayo imepitishwa kibabe na CCM haitoi nafasi kwa Rais au CCM.

Sheria ilisema tume itakusanya maoni katika awamu mbili, ya kwanza kutoka kwa wananchi na ya pili mabaraza ya kata.

Kilichopaswa kuendelea sasa ambacho hakitokei, ni BMK kujadili maoni ya wananchi na mabaraza ya kata.

Maoni ya wananchi yalishatolewa, CCM wakapewa nafasi kama Chama, na viongozi kupewa fursa za kipekee. Huo ndio ulikuwa muda wa kutoa maoni.

Maoni ya sasa ya Rais na CCM hayana nafasi kisheria kwasababu muda huo umepita. Kilichotarajiwa ni kujadili kwa kina maoni ya wananchi na si maoni ya Rais na CCM peke yao.

Nape atambue, katiba ni mali ya wananchi. Uandikwaji wake unapaswa kuwashirikisha kila hatua na kila siku.

Makongamano yanayoendelea ni elimu kwa umma kuelekea kura ya maoni kama ingekuwa ilivyotarajiwa(haitatokea).
Hivyo lazima atafautishe kati ya maoni na mijadala.

Katibu Nape akumbuke ni mara mbili mwenyekiti wake amewasingizia na kuwatuhumu wajumbe wa tume kwa kutumia nafasi yake ya Urais.

Ingekuwa ni kituko kama spinning zilizofanywa dhidi ya tume zingebaki kama ukweli.Rais alianza, na tume wanajitetea.

Hivyo wa kulaumiwa ni mwenyekiti wake,tulitahadharisha mapema mwenendo wa kuishambulia tume hauna tija. Umma umetambua mbivu na mbichi.

BMK-CCM

Mwenyekiti wa kamati moja Ummy Mwalim alisema. kamati yake yenye wajumbe 53 ni 26 tu waliohudhuria, 10 kutoka znz na 16 bara. Hiki nacho ni kituko kweli kweli, kwamba hata katika CCM wenyewe wapo wanaona 'haya' na wapo wasio na soni kama mwaimu.

Ummy amesema kipengele cha shirikisho kimeondolewa katika kamati na rasimu inajadiliwa kwa mfumo wa S2.

Ni hao hao wanaojadili rasimu waliyosema tume imefikisha maoni binafsi mzeeWarioba.Wanajadili maoni binafasi wakiwa hawana takwimu mwananchi 1 dhidi ya 17,000 za Warioba.

Asichoelewa Ummy ni kuwa wanachokifanya ni utoto wa hali ya juu.
Katiba ni mali ya wananchi, na wana haki ya kuipinga popote na wakati wowote.

CCM wanaweza kuandika katiba yao, hawataweza kuandika katiba ya nchi.
Historia ni shahidi kuwa duniani kote hakuna mahali dola iliwahi kushinda nguvu ya umma.

Huu ni ushahidi mzuri ile rasimu ya Lumumba inaingizwa kiujanja ujanja.
Hakuna sababu za kuficha, CCM walete rasimu yao, waijadili na kuipitisha na kila mbinu.

Tuna uhakika Tanzania itaandika katiba yake siku na muda muafaka.
Hii inayoandikwa itatumika Lumumba ikiwa ni haki yao ya msingi kabisa.

VITUKO NDANI YA KAMATI

Ukisoma maoni ya wajumbe waliobaki BMK, utajiuliza kama nchi hii ina watu wa aina gani endapo hao waliopo BMK-CCM ndio tunaowasoma.

Katiba ni sheria kuu ya nchi itakayozaa sheria nyingine,kanuni na miongozo mbali mbali.

Katiba si kanuni za bunge na wala kuandika katiba si kikao cha harusi kinachojadili mchanganuo wa soda, beer na nyama.

Leo wabunge wa BMK-CCM wanasema iwepo sheria ya umiliakaji ardhi itakayotoa vibali wafugaji kuhama sehemu moja hadi nyingine. Real! katiba ya nchi izungumzie regulations za serikali za mitaa!

Tunasubiri wajumbe wengine waje na hoja za katiba kueleza jinsi Nurse atakavyotoa vidonge, Engineer michoro yao iweje n.k

Katiba iseme mashine gani nzuri kwa wavuvi, Walimu waanze kufundisha somo gani, na madaktari wavae makoti gani wawapo kazini. Ndicho kinaendelea katika mjengoni.

Ukisikiliza maoni ya kamati za Sitta, utapima malaria kwa maumivu makali ya kichwa, tumbo kusokota na safari za mara kwa mara msalani.

Badala ya kuvunjika mbavu kwa maoni ya BMK-CCM, mwana duru una jukumu kubwa la kulia, kulia kwa uchungu sana.

Nchi inaelekea katika pori, nchi inaselelea tusikokujua.
Nchi ipo njia panda.

Tusemezane
 
KINANA ANAPOWASIHI CCM WAONGEE WALICHOZUIWA

WAKATI WA KURUVURUGANA UPO NJIANI

Katibu mkuu wa CCM amewataka wajumbe wa BMK-CCM kuacha kuongelea UKAWA na kujadili katiba yao.
Kinana ameshindwa kutambua mambo mawili mahimu
1. Mkinzano wa mawazo ni muhimu katika kutafuta jawabu la matatizo.UKAWA hawapo na hilo halipo
2. CCM imeshawafunga midomo wabunge wake, Kinana angependa waongee nini?

MKinzano wa Mawazo
Kunapokuwa na mawazo tofauti kuna maana ya uwakilishwaji wa mitazamo tofauti ya jamii.
Mijadala yenye ukinzani, kunapokuwa na maafikiano ni kiashirio sehemu kubwa jamii inaafiki.
UKAWA walikuwa ni sehemu muhimu ya mawazo kinzani,kuondoka ni pengo katika uwakilishwaji wa jamii

CCM kuwafunga wabunge midomo
Tendo la kuwalazimisha wabunge wa CCM kufuata maazimio ya vikao, ililenga kuelekeza wafanye na waseme ABCD.
Ndio msingi wa kura ya wazi

Kutokana na hilo, wabunge wa CCM wanaongozwa na falsafa moja, kuafiki kile kilichokubaliwa na wahafidhina.
Hawapaswi kutumia akili kulikutumikia taifa. Wanatakiwa ni kukukubalina wenyewe, walichoambiwa na kusema walichoambiwa.

Mtazamo unawapelekea wabunge waongelee UKAWA na si katiba.
Hoja zao zimeshafungwa, iliyo wazi ni kuongelea UKAWA, ndio sababu kubwa ya wao kuzungumzia UKAWA.
Laiti wangelikuwa huru, wangekuwa na nafasi ya mawazo mapya. Kwasasa wapo gerezani, wakikubali analosema afande.

Tofauti yao ni kuwa ndani ya bunge tu, kiuhalisia bado ni wafungwa wa kisiasa.

Ni makosa kuwaambia waongelee katiba. Kinana hawezi kuwapiga kufuli halafu awaambie waongee.
Wataongea nini ikiwa baadhi yao wana maono tofauti na msimamo wa chama?

Kinana asiwalaumu wabunge, wajilaumu wao waliogeuza wabunge wao wafungwa wa kisiasa.

WATAVURUGANA
Wiki iliyopita tulisema CCM wakibaki wenyewe watauvurugana. Adui yao UKAWA hayupo.
Tayari kuna kamati zimeanza kukosa 2/3 katika BMK-CCMKama wataendelea na kiburi chao, watajikuta katika matatizo mazito.

Ikifika jambo la muungano ambao miaka 50 umekuwa hauna suluhu patachimbika.
Wengi walikuwa hawana ufahamu kuhusu mfumo wa S2 na madhila yake kwa wahusika.

Leo wabunge wa CCM wanaelewa kero kwa wazanzibar ni masilahi,wanapotaka masilahi wznz hukimbilia neno kero.
Wanafahamu Tanganyika inavyomenyeka katika kuuhifadhi muungano, wakati wakijua hilo halina manufaa kwa Watanganyika.

Ni lazima kutakuwa na kutetea masilahi ya maeneo yao,wakifahamu hasira za umma juu y, na kwamba jambo lolote litaangaliwa kwa jicho la mbunge binafsi na si CCM.

CCM wanafahamu wananchi hawakupendelea wanachokifanya. Miaka 50 haikutoa jibu la matatizo.
Mfano, wabunge wa znz watadai account ya pamoja ili kugawana mapato na matumizi kwa haki.

Wabunge wa bara watauliza account hiyo inachangiwa vipi na kwa utaratibu gani.
Endapo serikali haikuweza kutengua kitendawili hicho, hilo likiingia bungeni ni kumwaga mtama kwenye kuku.

Mfano wa pili, CCM-Znz watabaki na msimamo wa katiba ya 2010 ili kutowaudhi wazanzibar.
CCM bara watataka rekebishwe kukidhi haja ya muungano wa S2 kwa wanayoandika(katiba ya CCM)
Hilo litawavuruga kwa kuzingatia ukweli kuwa CCM wengi wameonyesha kukerwa na uwepo wa katiba ya znz.

CCM bara wanaelewa uwepo wa katiba ya znz ni kuvunja katiba ya JMT.
Hawana jibu wanapoulizwa na wasingependa wakakosa jibu siku za baadaye. Hakutakuwa na muafaka miongoni mwao.

Uwepo wa upinzani uliwasaidia sana CCM kuliona tatizo katika jicho la umoja zaidi kuliko walivyo wenyewe sasa hivi.
Kulisaidia mijadala yenye afya kwa masilahi ya taifa.

Tusemezane.
 
BMK-CCM DODOMA

SAMWEL SITTA AJIUNDIA TUME YA KUKUSANYA MAONI

ANAHANGAIKA KUTAFUTA UHALALI WA RASIMU YAKE NA CCM

TUME YA KUKUSANYA MAONI YA SITTA INA 'KATIBU ' SHIBUDA

Mwenyekiti wa BMK-CCM amejigeuza na kuchukua majukumu ya iliyokuwa tume ya Warioba.

Kinyume na matarajio ya kujadili rasimu yao, Sitta ameamua kuunda tume yake mwenyewe kukusanya maoni

Ili kufanikiwa na kazi ya ukusanyaji maoni, mwenyekiti Sitta amemwalika mbunge Shibuda katika picha ya pamoja na wafugaji.

Picha hiyo ilikuwa makusudi kuonyesha jinsi Sitta anavyokusanya maoni ili atengeneze rasimu yake.

Tangau UKAWA waondoke, Samwel Sitta amesisitiza katiba ina mambo mengi mazuri na wala si muundo wa muungano.

Zipo habari za kuaminika yanayojadiliwa katika kamati yamekuwa na matatizo kutokana na misimamo ya muundo wa muungano.

Nia ya Sitta ni kutaka kuaminisha umma alikuwa anakusanya maoni ya wananchi.

Ukweli, anachokifanya hakina maana, ni upuuzi na uzumbu kuku wa sheria.

Sheria anazotumia Sitta zimesema namna ya kupata maoni na kuyaingiza katika rasimu.

Hakuna mahali sheria imetamka Sitta ana uwezo wa kusikiliza maoni ya kundi fulani na kuyaingiza.

Njama za Sitta ni ili siku zijazo awaite wazanzibar na kuwasikiliza. Hao nao kama wafugaji watakuwa wameandaliwa ili kuleta picha ya Sitta anayokusudia. Wameshaandaliwa wazee kutoka Unguja kwa kazi hiyo.

Haijulikani tume ya Samwel Sitta itakutana na Walimu siku gani, na makundi mengine kwa utaratibu gani.

Na wala hakuna ajuaye zaidi ya Sitta na katibu wake Shibuda, wajumbe wa tume yake wengine ni wapi na kutoka eneo gani.

Hizi zote ni dalili za kutaka kuungwa mkono na makundi ya kununua. Kwa mtu mwenye akili tumamu, ni rahisi sana kubaini kuwa tume ya Sitta inafanya kazi za mahusiano ya kijamii na wala si kusikiliza mtu.

Tume hiyo ya watu Sitta na katibu wake haina nguvu za kisheria au baraka za chombo chochote nchini.

Mwenyekiti Sitta ameshindwa kuelewa kuwa hizo zilikuwa dalili za kutosha kumweleza jinsi gani alivyoshindwa kuliongoza bunge, alivyoshindwa uongozi na asiyejua nini kina manufaa na tija kwa taifa hili.

Sitta anazidi kuwa kichekesho cha umma na katika hali aliyo nayo, ni dhalili na aibu ambayo ataishi nayo hadi siku za maishayake.

Ni moja ya mambo yatakayomuandama baada ya kurudiwa na fahamu na kubaini anachokifanya ni maandalizi ya kuliingiza taifa hili katika mtafaruku mkubwa.
 
BMK-CCM DODOMA

SAMWEL SITTA AJIUNDIA TUME YA KUKUSANYA MAONI

ANAHANGAIKA KUTAFUTA UHALALI WA RASIMU YAKE NA CCM

TUME YA KUKUSANYA MAONI YA SITTA INA 'KATIBU ' SHIBUDA

Mwenyekiti wa BMK-CCM amejigeuza na kuchukua majukumu ya iliyokuwa tume ya Warioba.

Kinyume na matarajio ya kujadili rasimu yao, Sitta ameamua kuunda tume yake mwenyewe kukusanya maoni

Ili kufanikiwa na kazi ya ukusanyaji maoni, mwenyekiti Sitta amemwalika mbunge Shibuda katika picha ya pamoja na wafugaji.

Picha hiyo ilikuwa makusudi kuonyesha jinsi Sitta anavyokusanya maoni ili atengeneze rasimu yake.

Tangau UKAWA waondoke, Samwel Sitta amesisitiza katiba ina mambo mengi mazuri na wala si muundo wa muungano.

Zipo habari za kuaminika yanayojadiliwa katika kamati yamekuwa na matatizo kutokana na misimamo ya muundo wa muungano.

Nia ya Sitta ni kutaka kuaminisha umma alikuwa anakusanya maoni ya wananchi.

Ukweli, anachokifanya hakina maana, ni upuuzi na uzumbu kuku wa sheria.

Sheria anazotumia Sitta zimesema namna ya kupata maoni na kuyaingiza katika rasimu.

Hakuna mahali sheria imetamka Sitta ana uwezo wa kusikiliza maoni ya kundi fulani na kuyaingiza.

Njama za Sitta ni ili siku zijazo awaite wazanzibar na kuwasikiliza. Hao nao kama wafugaji watakuwa wameandaliwa ili kuleta picha ya Sitta anayokusudia. Wameshaandaliwa wazee kutoka Unguja kwa kazi hiyo.

Haijulikani tume ya Samwel Sitta itakutana na Walimu siku gani, na makundi mengine kwa utaratibu gani.

Na wala hakuna ajuaye zaidi ya Sitta na katibu wake Shibuda, wajumbe wa tume yake wengine ni wapi na kutoka eneo gani.

Hizi zote ni dalili za kutaka kuungwa mkono na makundi ya kununua. Kwa mtu mwenye akili tumamu, ni rahisi sana kubaini kuwa tume ya Sitta inafanya kazi za mahusiano ya kijamii na wala si kusikiliza mtu.

Tume hiyo ya watu Sitta na katibu wake haina nguvu za kisheria au baraka za chombo chochote nchini.

Mwenyekiti Sitta ameshindwa kuelewa kuwa hizo zilikuwa dalili za kutosha kumweleza jinsi gani alivyoshindwa kuliongoza bunge, alivyoshindwa uongozi na asiyejua nini kina manufaa na tija kwa taifa hili.

Sitta anazidi kuwa kichekesho cha umma na katika hali aliyo nayo, ni dhalili na aibu ambayo ataishi nayo hadi siku za maishayake.

Ni moja ya mambo yatakayomuandama baada ya kurudiwa na fahamu na kubaini anachokifanya ni maandalizi ya kuliingiza taifa hili katika mtafaruku mkubwa.
Sitta amedhihirisha Kwamba ni Adui namba moja sio tu wa Tanganyika Bali pia wa muungano. Kwa Mujibu wa taarifa kutoka Dodoma, ili kuua Dhana ya serikali tatu, Sitta ameelekeza Kwamba mambo yote ambayo hayapo kwenye rasimu yaingizwe yakiwemo mambo yasiyo ya muungano yani ya Tanzania Bara. Hii ni Kinyume cha Sheria ya mabadiliko ya katiba (2011) kunakofanywa na mwanasheria Samuel Sitta. Miongoni mwa mambo ambayo Sitta inasemekana anaagiza Kamati za BLK yaingizwe ni serikali za Mitaa,ardhi, Kilimo, mifugo, uvuvu n.k. Hatua hii itapasua muungano na nchi. Ni suala la muda tu.



Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Sitta amedhihirisha Kwamba ni Adui namba moja sio tu wa Tanganyika Bali pia wa muungano. Kwa Mujibu wa taarifa kutoka Dodoma, ili kuua Dhana ya serikali tatu, Sitta ameelekeza Kwamba mambo yote ambayo hayapo kwenye rasimu yaingizwe yakiwemo mambo yasiyo ya muungano yani ya Tanzania Bara. Hii ni Kinyume cha Sheria ya mabadiliko ya katiba (2011) kunakofanywa na mwanasheria Samuel Sitta. Miongoni mwa mambo ambayo Sitta inasemekana anaagiza Kamati za BLK yaingizwe ni serikali za Mitaa,ardhi, Kilimo, mifugo, uvuvu n.k. Hatua hii itapasua muungano na nchi. Ni suala la muda tu.



Sent from my iPhone using JamiiForums

Not exactly Mchambuzi. Kama mwelekeo ni serikali moja ya Tanzania, na kuifanya ile ya Zanzibar ife (kwa kuchukua mambo yote yasiyo ya muungano na kuyafanya yawe kwenye serikali moja, hilo ni jambo la maana sana. Lakini kwa ujumla ni kwamba 2 wrongs do not make a right.
 
Not exactly Mchambuzi. Kama mwelekeo ni serikali moja ya Tanzania, na kuifanya ile ya Zanzibar ife (kwa kuchukua mambo yote yasiyo ya muungano na kuyafanya yawe kwenye serikali moja, hilo ni jambo la maana sana. Lakini kwa ujumla ni kwamba 2 wrongs do not make a right.
Mkuu hatuwezi kuwa na S1 kwasababu
1. Hilo znz hawataki kulisikia. Kwao kuitwa mzanzibar ni jambo la maana sana.
2. Hatuwezi kuwa na S1 kukiwa na katiba ya 2010 ambayo ina nguvu kuliko ya JMT
3. Hakuna uwezekano wa kuwa na S1 kwasababu, kila jambo la JMT ni la wote na la znz ni lao.

Kwa mfano, Sitta, ameagiza ardhi irudishwe katika katiba. Znz wanasema yao, sasa yetu pamoja ni ipi.

Huu muungano hawezekani katika S1 AU S2. Ni kwamba option zote zimeangaliwa kwa umakini.
Nyerere hakuweza sidhani kama kuna kiongozi yoyote mwenye heshima(na hakuna) ya kuweza.

Muungano unavunjika haraka kuliko ilivyofikiriwa
 
Back
Top Bottom