Moja ya hoja za msingi za
Nguruvi3 ni kwamba kwa chama cha ACT, mpinzani wake mkuu ni Chadema kuliko CCM. Wachangiaji kadhaa humu wamepinga hilo wakati huu ni ukweli ambao hata Dr. Kitila Mkumbo ameuthibitisha katika makala yake miezi kadhaa iliyopita titled: "Tunahitaji Chama Mbadala wa CCM na Chadema". Kitila anasema hivi:
"Kuna sababu zingine nyingi kwa nini tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA. Kwanza, kuna uwezekano halisi kabisa ya CCM kushindwa katika Uchaguzi Mkuu ujao kama vyama vya upinzani, na hasa CHADEMA, vitapenda kushinda. Ikitokea CCM ikashindwa mwakani chama hiki kitakufa. CCM itakufa kwa sababu haina wanachama wala washabiki kwa maana halisi ya maneno haya. CCM ni chama dola, na hakuna popote duniani ambapo chama dola kilibaki baada ya kunyanganywa dola. Vyama dola hushikiliwa na dola, na wanachama na washabiki waliopo katika vyama hivi kimsingi hushabikia dola na mara dola inapowatoroka na wanachama nao husepa. Ilikuwa hivyo Zambia kwa UNIP. Ilikuwa hivyo Kenya kwa KANU na ipo hivyo katika nchi nyingi za Afrika pale ambapo vyama vilivyokuwa vinatawala vilipoteza dola. Katika mazingira haya kuna hatari kubwa sana tukazalisha chama kingine dola mara CHADEMA kitakapokuwa madarakani kwa sababu ya upinzani dhaifu."
Kwanza hoja nzima ya Kitila inajengwa katika mazingira ya "uwezekano", sio uhalisia. Hapo juu anasema kwamba
"kuna uwezekano halisi kabisa ya CCM kushindwa katika Uchaguzi Mkuu ujao kama vyama vya upinzani, na hasa CHADEMA, vitapenda kushinda ".
Pili, anathibitisha hoja ya nguruvi3 kwamba mpinzani mkuu wa ACT ni chadema kuliko ccm kwani tayari anakiona chadema kama chama dola kijacho pale anaposema:
Katika mazingira haya kuna hatari kubwa sana tukazalisha chama kingine dola mara CHADEMA kitakapokuwa madarakani kwa sababu ya upinzani dhaifu."
Kitila hazungumzii uhalisia uliopo bali uwezekano, hajadili uhalisia unaotokana na ushahidi kwamba mwenyekiti mtarajiwa wa ACT, Zitto Kabwe, alitumiwa na CCM kuivuruga chadema. Ushahidi mwingi umetolewa ikiwa ni pamoja na mawasiliano yaliyonaswa, bank transfers etc. Sio Zitto Wala Kitila wamekanusha haya.
Katika mazingira haya, Kitila anaacha maswali kuliko majibu pale anaposema kwamba "ushindi wa upinzani 2015 unawezekana hasa iwapo chadema itapenda kushinda". Je alipokuwa chadema hakupenda chadema ishinde? Kilichopunguza uwezekano huo ilikuwa ni nini? Jibu ni waraka na madhara yake. Waraka ulikiuka kanuni, na kama tutakavyo ona, yeye anasema solution ilitakiwa iwe busara na hekima, sio sheria na kanuni.
Kufuatia sakata la waraka, Kitila yupo sahihi kwamba wana chadema wengi wangependa kushinda mwakani. Lakini anasahau kwamba moja ya njia za kufanikisha lengo hilo ni pamoja na kushughulikia tatizo la zitto haraka na kumalizana nalo. Na hivyo ndivyo kamati kuu iliamua kufanya.
Lakini Kitila anashauri jinsi gani sakata lao lingeshughulikiwa, anasema kwamba:
"Sheria na kanuni hazijawahi kuwa nyenzo ya kutatua migogoro katika siasa. Migogoro ya kisiasa hutatuliwa kwa busara, hekima na uvumilivu, mambo ambayo hayapo katika uongozi wa sasa wa CHADEMA na ndio chama kinapoteza mweleko kwa kasi".
Hapa anaacha maswali kuliko majibu kwani yeye akiwa mmoja wa washauri wakuu wa zitto wamemshauri kwenda kuweka pingamizi mahakamani jambo ambalo ni la kisheria na kikanuni zaidi kuliko busara na hekima. Uamuzi wa zitto kwenda mahakamani umembomoa kuliko kumjenga. Busara na hekima ilikuwa ni kukiri kushiriki kwenye waraka, kukiri ilikuwa kinyume cha kanuni na kuomba msamaha. Basi. Chadema ingesonga mbele. Kwa maana nyingine, waraka ule ulikuwa kinyume cha kanuni, na solution yake ingekuwa matumizi ya busara na hekima kwa upande wa zitto, hasa baada ya uongozi wa chadema kumtetea wa muda mrefu. Hapa Kitila anajichanganya.
Nguruvi3 ana hoja nyingine kwamba kitila analaumu chadema kwa kuminya demokrasia halafu anaenda kurudia yale yale ACT. Kitila anathibitisha hoja hii anaposema:
"Ndani ya vyama vyetu hivi kuna wateule na wateuliwa. Kama haupo katika makundi haya huna nafasi na hii sio sifa njema ya chama cha kidemokrasia".
Je haoni kwamba nguruvi3 yupo sahihi kwamba zitto tayari ni mwenyekiti mteule wa ACT? Je wale ambao watapingana na Kitila juu ya uteuzi huu huo ACT watakuwa na nafasi? Je haya ya kitila ACT ni sifa njema ya chama cha kidemokrasia?
Tumalizie kwa kuangalia kwa undani hoja za Kitila juu ya kwanini mbadala wa ccm na chadema unahitajika. Anasema:
"Tunahitaji mbadala wa CCM kwa sababu chama hiki kimelewa madaraka na sasa hakioni wala kusikia, na haielekei kwamba ulevi huu utaisha, zaidi kuwa na dalili zote za usugu.
Tunahitaji sana mbadala wa CHADEMA kwa kuwa chama hiki nacho kimeanza kulewa sifa zinazotokana na umaarufu. Viongozi wa chama hiki wameshaanza kulewa na ndio maana wanaweza wakafanya maamuzi wanayoyaita ni magumu lakini ni ya hovyo bila woga wala hofu. Wanafanya hivi kwa sababu wanajua wanachama na wapenzi wao watawaunga tu mkono kwa sababu hawana namna madamu hawaitaki tena CCM.
Wanasahau kwamba kwa ulevi huu wa umaarufu wanatengeneza mazingira yaleyale ya CCM. Watakapoingia madarakani umaruufu utaisha na wataanza kulewa madaraka, na kwa ubabe wanaounyesha kabla ya dola kuna kila dalili kwamba ulevi wao wa madaraka utakuwa balaa.
Tunahitaji mbadala chama cha siasa cha upinzani kitakachojikita katika kupinga mawazo na falsafa za chama tawala, na sio kupinga sura za watu. Tunahitaji chama kitachokajengwa katika misingi ya demokrasia ya wanachama na sio demokrasia ya viongozi na waasisi wa chama. Tunahitaji chama kitachozingatia misingi ya uadilifu katika maisha binafsi ya viongozi na utumishi wa umma kwa sababu msingi wa uadilifu katika utumishi wa umma unajengwa katika uadilifu binafsi.
Tunahitaji chama ambacho kitalea viongozi ambao watakuwa na ujasiri wa kukiri makosa inapotokea wamekosea na sio kuyahalalisha. Kwa kifupi tunahitaji sana mbadala wa CCM na CHADEMA, na kujenga chama cha namna hii hatuhitaji miongo miwili. "
---------end quote-------------
nguruvi3 ameuliza - upo wapi utaalamu wa kisayansi? Na kwanini utaalamu huo unaungwa sana mkono na chama ambacho sayansi hiyo inalenga kukifanya kuwa mbadala yani chama cha mapinduzi?
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums