Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Mkuu kwa nini unazunguka mbuyu. Kwetu sisi tulokusoma tunajua fioka unaficha ya kwamba ZZK na Kitila ndio waasisi wa chama ACT, hivyo unachojaribu kusema hapa ni kwamba haiwezekani Kitila amualike ZZK ACT ili aje kuwa mwenyekiti wakati ni yeye alokianzisha. Sema hivyo tutakuelewa kuliko kuzunguka Kuzungumzia historia ambayo sote tunaijua hapa JF.

Hiyo siasa ya Kisayansi ndio ipi ikiwa uongozi wa CDM walishindwa kusimamia demokrasia ndani ya chama nanyi mkawaunga mkono?... Itakuwa nje! Mimi nimewapinga na nitaendelea kuwapinga kwa maamuzi ambayo yamekiathiri chama na kwa sababu za ubinafsi wao. Cheo ni dhamana na hakuna nidhamu ya kumuogopa kiongozi yeyote! sintosimamamia nidhamu ya woga na unafiki.
Mkuu Mkandara nadhani tuwe honest.

Nilishasema kuwa Waraka ulikuwa childish move, hiyo haina maana naunga mkono kinyume chake.
Ninasimama kwenye hoja kwanza, kama ninavyosimama sasa na kusema Kitila kuteua viongozi ni makosa yale yale aliyokataa na haonekani kujifunza . Nasimama kusema, siasa za Kitila hazilingani na nafasi yake kijamii.
Nasimama kusema kama alivyosema Alinda , wajitokeze wafanye mambo bila kutufanya wajinga.

Kitila alipoandika kuhusu ACT tulijua anaandaa nini, sasa anakuja na njama za kumuokoa ZZK ktuoka katika kesi kiana kwa kusema anamshawishi ili hali tunajua lao moja. Kitila aliyekataa ZZK kushiriki waraka sasa anatuambia kuhusu ushiriki wake.

Kibaya ni utezui wa ZZK kuwa mwenyekiti kama CEO, akiamini Mhusika Mkuu (MM) aliyetakiwa kuwa mwenyekiti sasa anateuliwa kuwa mwenyekiti. Phwee . Angalia nafasi ya hawa jamaa katika jamii halafu angalia uzito wa siasa zao.

Msome Alinda 37, Mchambuzi 38
 
Hakuna anayekataa kwamba CCM kimechoka, kama wapo, basi hawaelewi umuhimu & role ya vyama vya siasa katika maendeleo ya nchi. Socially, politically, economically, CCM is sick, weary and irreparably tainted. The party is no longer fit to govern our nation, and without an alternative, its really frightening to think about what the future holds for our nation.

Vinapojitokeza vyama kama chadema, vyama hivi vinatoa matumaini mengi kwa wale watafuta "mbadala". Chadema chini ya watu kama zitto, kitila etc kilikuwa kinazidi kujijenga kama chama mbadala, siku hadi siku, huku input ya watu hawa ikiwa ni kubwa sana bila ya kujalisha ni nani walikuwa pale juu kwenye uongozi. Ni kama vile watu hawa wakaanza kuona kwamba mchango wao hatuuthamini au umma hauoni kwa vile tu hawapo juu kwenye uongozi wa chama. Hii sio kweli, wananchi wengi sana walitambua mchango wao. Hawakufanya utafiti kabla ya kuandaa mapinduzi yao. Laiti wangefanya utafiti, wangeona ukweli upo wapi, wangekuwa na subira, na demokrasia na haki ingefuata mkondo wake siku moja kwani chama ni watu, sio mtu mmoja mmoja.

All that said and done, chadema kimevurugwa, na wengi tumerudi tena kuanza kutafuta chama mbadala. Baadae tukasikia kwamba wavurugaji wa chadema wameanzisha chama chao. Sasa kwanini tusihoji ili tuone kama chama hiki kipya ni mbadala wetu wa kweli?

Zoezi letu halitaishia na kina Kitila tu, na kila tukisikia juhudi za watu wakijaribu kuleta chama mbadala, our scrutiny becomes of essence kwani tuna kiu kubwa sana for an alternative party. Unfortunately, in ACT, so far we see nothing but "the same alternative" in the offering. Ni kwa mantiki hii, hoja zetu zinaonekana kama vile zinalenga kushambulia watu badala ya chama. Lakini Ukweli unabakia kuwa "chama ni watu".

Mwisho, kwa wale wanaodhania tumeanza this scrutiny na ACT peke yake watembelee profile zetu, watakutana na mijadala mizuri sana na mwenyekiti wa CCK ambae ni mdau humu na aliwasilisha katiba yake ili kuomba mawazo ya wadau. Kitila anashindwa nini kufanya hivyo humu or elsewhere na badala yake anaona jambo muhimu kwa sasa ni kumteua zitto uenyekiti na kuwekeza katika kuchukua wanachama wa chama kile kile (chadema)? Hapa ana maanisha kwamba wanachadema hawapo kule kwa misingi ya sera na itikadi bali mvuto wa zitto. Ushahidi wa hili upo pale anapotanguliza jina la zitto badala ya sera na itikadi ya ACT kuvutia wanachama.
Kitila Mkumbo, wewe ni mdau humu na tunajua unatusoma. Kwa vile umekubali kwamba ccm ni chama kinachokufa, na kwa vile ni chama chenye wanachama wengi kuliko vyama vyote combined, mbadala wa kweli (ACT) ulitakiwa ulenge watu hao, sio wanachama wa chadema kwani pamoja na madhaifu yake, chadema bado ni mbadala kwa wananchi wengi. Wewe kuja na mkakati wa kuleta mbadala for both chama tawala na chama kikuu cha upinzani kwa wakati mmoja ni udhaifu mkubwa sana kimtazamo na kimkakati. Njia hii haiwezi fanikisha ujenzi wa upinzani bali itabomoa upinzani. Lakini Iwapo utafanikisha, basi mwisho wake utakuwa Ni ACT kuwa chama dola, kitu ambacho umejadili Kwamba hakifai kwa demokrasia yetu changa.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:

Tukasema kuwa yale ya Mrema hatuhitaji yatokee tena.
Nimeonyesha NCCR na TLP kama mbadala
CUF Maalim na CUF Hamad Rashid
CUF Maalim na CUF chausta
Kitila kutanguliza jina la mtu na siyo sera 'zilizomvutia' ni kurudisha kule kule kwa akina Mrema, Seif,Hamad na Mapalala

Watu hawataki scrutiny wanataka kupokea ujio tu tena ukiambatanishwa na majina makubwa.

Kuhusu mchango wa akina ZZK na Kitila, hakika subira ni jambo muhimu sana katika maisha yetu.
Hawa watu walikubalika katika siasa za chama chao na ilikuwa suala la muda tu wangeongoza. Tatizo ni subira.

Kuhusu suala la kutanguliza jina, hiyo likuwa ni 'psychology' ya kuwaambia watu yule mwenyekiti wenu mnayemtaka sasa anahamia huku, jiandaeni mje. At the same time ilikuwa kumteua katika nafasi ya ueneyekiti wa chama asichojua sera zake bila kufuata kanuni za demokrasia.

Kitila, sera za chama zinatungulia na zinabaki kuwa za chama, wanachama wanafuata na huondoka ikibidi.
Huwezi kujenga chama kwa msingi wa jina, siyo mbadala ni udhaifu.

Kugawana wanachama na CDM hakuondoi tatizo tulilo nalo la papa kuogelea katika bahari kuu kwa raha zake.
Ulipaswa kuwavuta wanachama kutoka pande zote kwa sera, na pengine ungewapata mbadala wengi wa CCM kuliko mbadala wa CDM ambao wapo wapo tu.
 
Katika hili mimi nitapenda niseme machache tu,

Kwanza ni sifu sera ya chadema Juu ya uongozi kwa vijana wake na matarajio yao,

Utaratibu wakuandaa vijana kuja kuwa viongozi ni sera thabiti na tanzu kabisa katika uga wa siasa za leo ambazo zipo kwenye kizio cha siasa za kiuchumi baada ya kutoka kwenye siasa za ukombozi na maendeleo.

Zitto ni miongoni mwa vijana wa mwanzo na angekuwa muhitimu wa mwanzo wa sera ya kuandaliwa kuwa kiongozi,

Na niseme wazi katika siasa za vijana, itachukua miongo kadhaa kuzaliwa mtu wa aina ya Zitto katika ardhi ya Tanzania,

Ujio wa Chama kiitwacho ACT binafsi ninalaaani kwa nguvu zote, sio ninalani kwakuwa chama kipya kimekuja, laa hasha, bali ninalaani kwakuwa kimekuja katika misingi ya kupambana na upinzani na sio kupambana na chama tawala ili kishike dola,

Nilishalieza hapa mazingira ya ujio wake kwa maana ya usajili wake na uongozi wake na namna kilivyo na mafungamano tata.

Chama cha kilaghai kilichopata usajili kwa mara ya pili baada ya kufeli mpango ovu.

Juzi chama kinachojipembua kuwa ni chama cha siasa cha ACT kimepata usajiri wa kudumu,

Mazingira ya upataji usajili wa kudumu yamejaa utata mtupu na ni hatari kwa demokrasia ikiwa mamlaka za nchi zinaruhusi makundi haya ya kihuni kuitwa chama cha siasa na kupewa usajili.

Nitaeleza kwa kifupi ujio wa kinachoitwa chama na kilikotokea na madhumuni yake.

Mwenyekiti wa ACT ni Kadawi Limbu, Na huyu huyu Kadawi Limbu ndiye Mwenyekiti wa ADC (kipindi inaanza na haijulikani ni lini alihama) . Na akiwa ziara sometimes anaenda Kama Mwenyekiti wa ADC na sometimes anaenda Kama Mwenyekiti wa ACT hii wengi hawajaigundua huyu jamaa anavyofanya

Na pia, huyu Kadawi Limbu ni mdogo wake na Festus Limbu Mbunge wa Jimbo la Magu kwa CCM, na kwao na huyu Kadawi Limbu ni Magu na Kwao na Mwigamba ni Magu Pia( do you see this connection).

Sasa angalia matukio ambayo Kadawi ametumika ndani ya ACT na wakati huo huo ametumika ndani ya ADC

http://issamichuzi.blogspot.com/2014/03/katibu-mkuu-wa-adc-katika-ziara-mkoani.html?m=1

Fungua hiyo ni march 04, mwaka huu, akiwa na ADC

Ya ACT angalia Mwenyekiti ni nani utakuta ni huyo huyo, kijana alicheza na nafasi ya Katibu wa ADC, na Mwenyekiti wa ACT kwa wakati mmoja, na Msajili wa vyama yupo kimya tu na hata wananchi wanaojiunga pia wengi hawajui hili, Hii inamaana ni UTAPELI na Ulagjai unaoendelea hapo.

Na kuanzia hapa ni wazi kuwa wale waliofukuzwa Chadema mwaka jana they deserve kuwa nje ya CDM maana Kama ADC ni Ndugu wa ACT na ACT Mwigamba yupo na nafasi kubwa tu (nahisi ni Katibu mkuu ama Katibu Mkoa wa Mwanza), na ADC ilikuwepo hata kabla hawajapigwa chini na CDM hii ni wazi kuwa mission yao ilikuwa ni kuiua CDM.

Na pia kuna uhusiano wa moja kwa moja Kati ya Kadawi Limbu na Hamadi Rashidi maana hawa wote ni waasi wa CUF, Kadawi kipindi flani aligombea ubunge moja ya majimbo Dar kwa CUF na Mara Hamadi alipotoka CuF naye akameguka ili kuwa mlezi wa ADC

Kama mwezi juzi tu alikuwa anapiga ziara kama Katibu wa ADC, at the same time ana serve Kama Mwenyekiti wa ACT, kuna sheria inayoruhusu mtu mmoja kutumikia vyama viwili? ( Msajiri hapa alichemka), na hiyo connection ya Hicho chama strategies zao kubwa ni Lake zone, na wengi wa wafuasi wa Zito Kama Chagulani ( diwani wa Igoma) alikwenda jimbo la Nkenge ( kagera) na kuweka bendera za ADC kila Kona

http://www.mpekuzihuru.com/2014/03/viongozi-wa-chama-cha-act-tanzania.html?m=1

Hii link ya pili ni gazeti la March 17, mwaka 2014, tofauti ya wiki takribani 2 tu, mtu moja, sehemu moja ambayo ni Mwanza mjini, vyama tofauti.

Haya ndugu zangu hizo ndio siasa za malengo ya mtawala

Yaliyotokea kwake ni sehemu ya mapito ya siasa za kiafrika na za kiswahili,

Ninaisifu na kuishukuru kamati kuu ya Chadema kwahatua madhubuti dhidi ya Zitto na wenzake.
 
Si tuu anajichanganya ila nashangaa ya Firaun wa hawa watu kusambaza sumu ktk mto kwa sababu ya mtu mmoja! maana kama hawa kina Kitila na ZZK ndio waanzilishi wa chama hiki ACT (waliofukuzwa Chadema) inakuwaje ZZK kugombea Uenyekiti ama Kitila kumuomba Zitto agombee uenyekiti liwe tatizo, ati kuna wenyewe walokitokea jasho chama? hao wengine ni kina nani ikiwa una hakika waasisi wa chama hiki ni wale waliofukuzwa kutoka Chadema!. Wangapi wale walofukuzwa Chadema!

Waasisi wa TANU walimuomba mwalimu Nyerere agombee uenyekiti na hakika walimpa nafasi hiyo ktk silver plate maana hata mgombea mwenza Marehemu AbdulWahid aliowamba wajumbe wamchague Nyerere kabla ya kura za pili.. Huyo Mbowe naye aliombwa kama hajui historia ya Chama chake, sasa leo imekuaje Kitila awe mtu wa kwanza kufana kosa la kupendekeza mtu kukiongoza chama kama sii kwa kutumia sheria zao. Tunaambiwa ZZK kafukuzwa CDM na hatakiwi mara bado inaonyesha kuwa ni mwanachama, Kitila atamuomba ZZK ajiunge na ACT mara inaonekana tayari ni mwachama maana ndiye mwanzilishi!.

Sisi Watanganyika wajuzi sana wa kujenga Fitna na hii itatumaliza kwa sababu hatutaki kuona mafanikio ya mtu mwingine hata siku moja na akianguka wataweka mabango mitaani kuitangaza. Hata media zetu wanajua hilo hivyo huandika majanga zaidi ukurasa wa kwanza maana yanauzika kuliko mafanikio..
Mkuu, mimi kwenye kauli ya chama kina wenyewe wanaofanya kazi usiku na mchana halafu hao hao anaowasema siyo wenye chama anageuka tena na kuwasema waanzilishi wa ACT ndiyo imenishangaza sana.

Nimemuuliza swali dogo tu kama hawa binadamu wangehamia TLP and CUF angesema wanauwa CHADEMA?.

Kama aliweza kumtuhumu kuwa Mh. Zitto alikuwa anafahamu waraka ulioandikwa na Dr. Kitila, kwa nini kwa sasa asijenge tena mazingira hayo hayo na kusema Mh. Zitto anafahamu kila jambo linaloendelea ndani ya ACT, hii ni pamoja na kuzielewa katiba na taratibu na sera za ACT.

Yaani CHADEMA inawambia haiwataki na haitaki huduma zao katika jamii halafu tena inaanza kuhofia uwepo wao katika siasa?. Mbona hii ni kali katika siasa!.

Huku ndiyo kunakosemwa, kuogopa vivuli vyao!.
 
Ningeomba kupata ufafanuzi zaidi juu ya chama hiki..

Tumeambiwa kuwa chama hiki ni chama cha uwazi (Allince for change and Transparency.. lakini cha ajabu kuanzia kuanzishwa kwake, waasisi wake, jinsi kilivyopata usajili ni usiri usiri tu hakuna uwazi.. Mfanoi Kitila anasema atamshawishi Zitto awe Mwenyekiti lakini hapo hapo Zitto anasema yeye ni Chadema (mpaka kesi iliyoko mahakani iamuliwe) sasa hapo mie ndio sielewi unawezaje kumpa unyekiti mwanachama tena kiongozi wa chama kingine?? ingekuwa jambo bora kama angesema kutoka na sera zetu tutajaribu kuwashawishi watanzania na watu mbali mbali kama Zitto wajiunge na ACT walau hapo ningemuelewa...

Pia tunasikia kuwa Zitto na Kitila ni Waasisi chama hiki, kwangu mimi ni jambo jema na la kujivunia kwani sio kila mtu anaweza kuanzisha chama maana kuanzisha chama kunahitaji muda, pesa, wataalamu nk. lakini cha ajabu wao wanajificha ficha, hivi kuna ugumu gani wa kusema ndio mimi ni muwasisi wa chama hiki? sasa kwa hili ambalo ni jambo dogo tu watu wanaficha ficha je uwazi tunaoubiriwa huko wapi?

Mwanzoni waliposema uwazi nilitegemea haya mambo ya siri siri sasa mwisho, tutarajie kujua wanzilishi wa chama hiki ni akina nani, sera zao ni zipi, wafadhali wao, na nk.. lakini cha kusikitisha zaidi hawa watu wanaotuhubiria uwazi walishindwa hata kutuonesha mikutano ya kutafuata wadhamini katika mikoa mbali mbali, walicho fanya ni kuleta picha ya mkoa wa Mwanza na yenyewe kuna walio sema huo ulikuwa ni mkutano wa mikopo na nk. ok inawezekani kuwa labda haikuwa ni muhimu kwao lakini unapohubiri uwazi ni lazima huwe muwazi kweli kama utashidwa kuwa muwazi kwa vitu vidogo vidogo je yakapokuwa mambo makubwa itakuwaje?

Wakati ufikie wanasiasa waache uongo, watekeleze wanachohubiri tumechoka kuwa wafuasi wa watu wanatumia umasiki wetu kujitajirisha.. kila mara ulaghai laghai tu ......
Alinda , hapa ndipo kwenye hoja zinazozungumziwa.

Mwanzo tulisikia kunahitajika mbadala wa CCM na CDM, tulifahamu jitihada zilikuwa mbioni. Hakukuwa na tatizo.Shughuli zikaendeshwa kuanzisha chama, hilo halina tatizo. Inafahamika !

Tatizo likajitokeza pale Kitila alipokwenda katika vyombo vya habari.
Niweke sawa, hakuna tatizo la Kitila kutangaza kujiunga na chama cha ACT.

Lakini basi yeye akiwa amejificha na tukijua anafanya hivyo, hakupaswa kwenda mbali zaidi na kutufanya mazuzu.

Kumshawishi Zitto hakuhitaji tangazo kwasababu ''wanashea maono sawa'

Tangazo limewekwa makusudi kabisa ili
1. Kumwezesha Zitto kutoka mahakamani kwa kisingizio cha kushawishiwa tukijua wazi alikwenda ili aende kwenye BMLK (Hapa wawili wanaficha 'uwazi' na wanacheza na karata dah! siitaji.

2. Kuwatangazia wafuasi wa Zitto mwito wa kujiunga na ACT bila kuwa muwazi kama ulivyosema. Hakuna tatizo pia kama Zitto ana watu wake, lakini hilo halikufanywa kwa njia za uwazi na ukweli.

Tukizangatia andiko lake la kifo cha CCM na CDM kuwa mbadala hivyo kunahitajika mbadala zaidi hakuna shaka lengo lake si kupambana na CCM.

3. Kitila hakutangaza sera za chama hicho anachomshauri mwenzake ahamie.
ZZK hajui hata sera au katiba lakini anashawishiwa ajiunge na chama.
Lakini basi, Kitila japo angeanza na kusema anamshauri zzk aondoe kesi ili kujiunga na ACT japo watu wangeelewa elewa hivyo hivyo! la hasha

4. Kubwa lao ni kumtangaza ZZK katika nafasi ya uenyekiti hata kabla ya chama hakijapata katiba. Hii ndio lowest point ya Kitila na inaondoa doubt yoyote iliyokuwepo.

Alinda, hakuna uwazi walioulilia siku nyingi kupitia waraka, kinachofanyika ni kutaka kugeuza wananchi kama mazuzu.

Tunasema , hapana, Kitila tanganza sera, vuta watu kwa hoja, maono na mipango.
Cheap politics kwa dunia ya sasa na nafasi yako katika jamii hazifai.

Huu si mwanzo mzuri na kitendo cha kufakamia matapishi si dalili njema kwa ustawi wa demokrasia na maendeleo ya nchi hii.

Kitila na ZZK ni raia wema wa nchi hii na wana haki zote, lakini wasitumie elimu au siasa za kizamani kutaka kupotosha umma kana kwamba hatujui, ni mazuzu.

Tangazeni sera, omyesheni uwazi, kila la heri. Wakivuka mstari tutawaambia bila haya.
Siasa za unafiki kwa nusu karne zimetufikisha hapa, bado tu tuendelee kumeza!

Last edited by a moderator:
UOTE=Mkandara;9525787]Sikia dada dhana ilokuwepo kwa wengi wetu ni kwamba Zitto na Kitila baada ya kufutwa uanachama Chadema walikwenda na kuanzisha chama cha ACT. Na ndivyo bado akioli ya wengi inawashauri hivyo lakini ukiwasoma hawa watu kwa makini utagundua kwamba Kitila ana kundi lake ambalo ndio wameanzisha chama hiki kama mwalivyoweza kuandika Waraka ule pasipo kumshirikisha ZZK.

Asante sana mkuu Mkandara kwa majibu yako hapo juu.
Kwa hiyo Kitila na kundi lake wameanzisha chama na wanataka kipate promo kwa kupita mgongo wa ZZK? Sasa kama ni hivyo kwa nini ZZK asijitokeze na kueleza umma juu ya jambo hili? huoni ZZK kukaa kimya kwa sisi ambao hatuna info za ndani tutaamini ZZK ni ndumila kuwili yaani yuko Chadema kimasilahi na yuko ACT kimatendo..

Inavyoonyesha katika mikakati yao, na mahesabu yao Zitto angekwisha fukuzwa Chadema na hivyo wanaiacha nafasi hiyo wazi. Swala la mwenyekiti mara nyingi sana hasa wakati chama kinaanzishwa huteuliwa na waasisi wenyewe kwa muda hadi pale uchaguzi wa kwanza wa chama utakapo fanyika. Binafsi sioni tatizo lolote ikiwa hutaamini kwamba ZZK yupo ktk mpango wa kuanzishwa kwa ACT sawa kabisa na ule mpango wa kufanya mageuzi ya viongozi ndani ya Chadema uloandaliwa na kina Kitila. ZZK alihusishwa na waraka ule na sasa anahusishwa na kuundwa kwa ACT.

Hapa sijakupata vizuri ina maana huu ni mkakati wa akina Kitila ila ZZK hana habari na mkakakti huu?
Kwangu mimi sina tatizo na ZZK kuunda chama au ZZK kuwa Mwenyekiti ila tatizo langu ni kuwa wanatangaza uwazi lakini wanatenda matendo yao kisiri siri.. Kama ZZK anajua huu mkakati na yeye hausiki na ACT kwanini hasisimame hadharani na kusema ukweli? na kama ni mmoja wa waanzilisha wa ACT kwanini hasisimame hadharani ni kusema? hapo ndipo tatizo langu lilipo. Uwazi unaoambiwa mbona kinakuwa kiini macho tena kwa vitu vidogo vidogo?

Hivyo watu hawataki kuamini kwamba ZZK sii mwanzilishi wala hahusiki kwa sababu walikwisha lishwa ujinga huo na kina Yudahadi baadhi ya watu kumchukia ZZK ttoka wakati wa waraka. Na kuna wale walomkana ZZK baada ya jogoo la tatu, hivyo ukichanganya yote haya lazima ZZK asulubiwe!

Nafikiri kama kuna watu wanamchukia ZZK basi hao ni wachache sana ila wanachochukia ni matendo yake ya undumila kuwili.. huu usiri siri husio na kicha wa miguu.. ZZK amesimamia mambo mengi katika taifa ili tena mambo ya hatari lakini hakuficha ficha lisimama akaongea anachofikiri ni sahihi..Sasa kwa sasa anashindwa nini kusimama na kuweka mambo sawa? kama ni ACT aseme na kama ni Chadema aseme.. Zaidi ya hapo mie naona yuko Chadema kimaslahi zaidi kitu ambacho ninaanza kujiuliuza juu ya uzalendo wake.

ZZK ana mapungufu yake na kubwa zaidi ni kwamba sii mwanasiasa aliyekomaa bado, mbinu nyingi za kisiasa zinamshinda badala yake anataka sana kutumia elimu yake ya darasa na Uzalendo wake kwa wananchi walalahoi. Siasa haziendi hivyo, hata kidogo ni lazima usimamie itkkadi kwanza, sera na kwa imani hiyo ndio unaamini kuwa njia pekee ya kuwapatia wananchi wako maendeleo. Waswahili wana sema akili nyingi huondoa maarifa ndio tatizo la vijana wetu!

Hapa tuko pamoja ila kwenye uzalendo ninaanza kuwa na wasiwasi.. Tatizo la ZZK ni pupa, dharau, na kupenda kusifiwa na katika hili la sifa ana marafiki wazuri tu na ana marafiki ambao sio wazuri kwake na wanaomuimbia nyimbo za sifa anazopenda kusikia hali huku wakimchonganisha kwa viongozi wake na jamii kwa ujumla, na hawa marafiki waimba sifa wanapata misaada ya aina mbali mbali kutoka kwake kwani ZZK ana roho ya ubindamu sana tena sana tu.
Kifupi ni hivi, ZZK amepitia majaribio mengi sana na siku zote hakuaminiwa iwe na chama au watu binafsio. Kibaya ni kwamba watu hawataki kusikia Ukweli, hivyo ZZK aseme lolote lile hataaminika. Na kama akifuata hayo uloyasema ndio atachukiwa mara 10 maana hataaminika kwanza na kisha atatungiwa hadith mpya! Usaliti wa ZZK unaoekana tu kwa sababu tunaamini ya mwanzo pasipo ushahidi ila kauli ya watu kama Tundu Lissu anajisikia mno na kuutaka Umaarufu kuliko watu wote Chadema.

Kama nakumbuka vizuri Hata Chadema kuna wakati iliandaa nafasi za uongozi kwa watu fulani kutoka CCM ambao wao wenyewe Chadema waliwafuata japo yawezekana leo viongozi wa Chadema wanaweza kukataa. Ni mikakati ya Chama na siwezi kusema hayo yalitokea kwa sababu ya Ukaribu baina ya Mbowe na watu hao ama Dr.Slaa na watu hao. Wapo walosimama hadharani na kukana na wapo walosimama na kukubali baada ya kujiunga na Chadema lakini bado ukweli utasimama ya kwamba UMAARUFU wa mtu ni silaha ya vyama vingi nchini ktk kukijenga na kila chama kinafanya mchezo huo. Haitakiwi kuwa hivyo, lakini ndivyo Tulivyo!

Swala la ZZK, Kwanza hayo maswali uloyaorodhesha tayari yanaelemea upande wa KUTOAMINI lolote kama ilivyokuwa ktk swala la Waraka. Napiokusoma tayari nakuona unaamini nini na ndio maana unaona Undumia kuwili wa Zitto lakini usiuone wa wabunge wa CCM wanaotetea pia maslahi ya wananchi. Yawezekana ZZK alishafuatwa na kina Kitila lakini kwa nini atangaze? hivi kweli itakuwa akili kwa mwanasiasa ambaye anasubiri hukumu kudai kwamba amefuatwa na waasisi wa ACT ili kujiunga na chama hicho? Ili iweje na atapendwa kweli ndani ya chama chake maana siasa sio Mpira!

Je, unajua ni mara ngapi Mbowe kafuatwa na vyama vingine? unajua ni mara ngapi Dr.Slaa kafuatwa sasa ukishajua kwamba hawa viongozi hawakuwahi kutangaza habari hizo utawahukumu vipi? Ama niseme unajua ni viongozi gani wa nje, Chadema imewahi kuwafuata wajiunge hao nao ni wasaliti wa vyama vyao? Hivi kweli Dr.Slaa aliisaliti CCM alipohamia CDM ama ilikuwa haki yake!

Hata kama ingelikuwa mimi ndiye ZZK na ktk nafasi aliyopo na nikafuatwa na Kitila ama iwe nahusika na mpango wa kuanzishwa kwa ACT sina sababu ya kumuomba mtu yeyote ruksa ikiwa hawa watu wanadai hawanitaki ni swala la muda tu, hawakuniamini pindi niliposema Ukweli wangu na wanahaha sasa kusikia vijimambo! ZZK kaapa kwa miungu wote anaowafahamu kuhusu waraka, kuhusu kuhusika na waraka ama mpango wa kukisaliti chama lakini hakuaminiwa ila wameaminiwa wale walosoma tu waraka japo sii mashahidi, ama watunzi wa waraka huo.

ZZK ni sawa na mfungwa alohukumiwa Kifo kwa kosa la jinai ambalo halina Ushahidi isipokuwa sura na mienendo yake imehukumiwa. Sasa huyu mfungwa akifanya mpango wa kutoroka Jela, kweli yeye atakuwa msaliti wa sheria kandamizi asubiri uamuzi wa viongozi wasiomtaka. Sii hawa hawa walituaminisha kuwa Kiongozi Sitta amefuatwa na viongozi wa Chadema kumtaka ajiunge ili kuongeza nguvu ya chama hasa baada ya kuenguliwa kiti cha U spika na akadai hatafanya hivyo hadi apewe Nafasi ya kugombea Urais!. Kuna habari millioni tulozisikia humu JF kuhusu vioongozi mbali mbali lakini hili la ZZK limewashinda kumeza, kutokana na Umaarufu wake unawasumbua watu. Mimi sielewi kwa nini ZZK akiwa maarufu inawasumba watu na sielewi zaidi kwa nini watu wanachukia ZZK kuwa na marafiki wakati Mbowe pia ana marafiki tena wanafiki ndio wengi zaidi. Sisi wa Mujini tunawajua hawa watu wachumia tumbo dada.

Wapo watu wana akili ya Kitumwa zinazowaweka duniani, kazi yao kila siku ni kujipendekeza kwa mwenye nacho waonekane wao waaminifu na wema sana kumbe wanafiki tu upande wa pili, kazi yao kutwa kumpa sifa kiongozi juu ya umahiri wake, Uzuri wake, umakini wake, busara zake, uongozi wake na wengine hadi kuwa makuhadi wake ili mradi tu hawa watu wapate kula ya siku. Usidanganywe na hizi habari za mtaani dada wenye mitaa hiyo tupo! Leo hii hakuna Uzalendo wa Chama ndani ya Chadema ila kuna Uzalendo wa viongozi na nidhamu ya woga kama ilivyo CCM. Kama wewe sii kambi ya Lowassa utakuwa na wakati mgumu sana kupeta kisiasa. Madongo anayopigwa kina Membe, Makamba, Mwandosya, Salim, Warioba yote yana malengo nje kabisa ya uzalendo!

Zilikuwepo habari za Lowassa, kina Mpendazoe na wengine wengi ambao walikuja kuunda chama cha CCJ. Walimsema hadi Mzee Mwanakijiji kuwa mmoja wa waasisi wa chama hicho lakini hata siku moja hukunisikia mimi nikiwahukumu watu hao kwa habari za mitaani na wala sii hoja maana kila Mtu ana haki yake ya URAIA. Pamoja na Yote hayo uliwasikia CCM wakiyabebea bango? sidhani walifanya subira, wakaheshimu haki za hao watu kujiunga nna chama chochote wakiopendacho na baadaye ukweli ukajitokeza nani mwenzao na nani msaliti.

Jamani tuache habari za mipasho na zile hadith za kwamba Muislaam akiingia kanisani basi kesha fanya shiriki ni lazima asilimu upya na wala ZZK sio mbwa kaingia msikitini bali binadamu anayetakiwa kuheshimiwa kwa haki zake za Kiraia kuchagua chama ama kujiunga na chama chochote aklipendacho na kwa wakati wake. Dini ni swala la Kiimani ya roho na sii jengo, rosali wala joho. Viongozi wetu wengi wanavaa majoho na mikufu mizito kifuani lakin ndani kutupu - wasikudanganye!!

Tazama pia tofauti baina ya wapenzi wa Chadema na CCM, ilipotokea fununu za Mh.Sitta na hata Sumaye hakuna mtu aloibebea mbeleko, kama upepo ilikuja na ikapita, leo Mh.Sitta bado yuko CCM aliaminika na anaaminika wala CCM hawakuibebea njuga kwa sababu wao kama Chama wana sheria, kanuni na utaratibu wao na sii kufuata habari za magazetini ama watunzi wa hekaya wa JF. Kitu gani kimejitokeza ktk dunnia ya leo hii na kimefanya watu tuaminishwa dhambi kuwa sii haramu bali choice ya Mtu. Tazama leo ukiupinga sana utawala dhalimu wa Kibepari utaitwa Terrorist. Ukweli nikwamba UONGO unaaminika zaidi kuliko UKWELI na ukitaka kujua Uongo ni upi na nukweli ni upi fuata manenmo yangu. UONGO hauna mwisho, ila UKWELI huwa na MWISHO. Uongo siku zote lazima uendelee kutungiwa uongo tofauti na Ukweli ambao uksha toka hakuna cha kuongeza!

Ukipingana ana mfumo wao (kiuchukmi) utafungiwa wewe milango yote kama Zimbabwe, Cuba na Korea Kaskazini na hata marafiki wako watapigwa chapa usoni wasionekane karibbu yako ili mradi wewe uonekane umeshindwa kiuchumi na kila siku picha za maisha magumu ya wananchi wako zitawekwa ukurasa wa mbele. Hizo sheria, kanuni na taratibu zao ktk kulinda maslahi ya makampuni makubwa ambayo hayakuipewa nafasi ya kupenyeza ktk nchi hizo.

Kifupi Ukiona rais yeyote anasifiwa sana na nchi za magharibi, basi jua ya kwamba huyo rais ndiye Mbwiga kuliko wote ktk kulinda maslahi tya nchi yake. Na ukisikia hapendwi jua ya kwamba huyu anajjali zaidi maslahi ya nchi yake maana NCJHI ni kwa Mapana ya RASILIMALI zake.i
 
Ni wewe unayehimiza tusijadili Watu lakini hoja zako zote hapo juu zinabebwa na Watu.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mkuu Mkandara:

Nini kilikuvutia na kuwa mfuasi au mfuatiliaji wa karibu wa siasa Za chadema?

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Ni wewe unayehimiza tusijadili Watu lakini hoja zako zote hapo juu zinabebwa na Watu.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Mkuu mimi nawazungumzia watu kwa sababu ndio mada yenyewe mloiweka na kuwataja kwa majina yao na sii kinyuma. Nna hata hao wengine nilowataja nimefanya hivyo ili kutoa Mifano na reaction zenu juu ya swala kama hilo na sii vinginevyo. Unaponiona mimi namzungumzia mtu fulani basi ujumbe wangu unakwenda direct kwake iwe ni swali ama ushauri na sii kuanzisha taarabu!

Swali lako la Pili, nilivutiwa na Chadema kutokana na imani kwamba Chadema imejipanga vema kufanya mageuzi ya Kisiasa na Kiuchumi wakichukua dhamana ya WAKULIMA na WAFANYAKAZI na sii Mabwanyeye. Nilijiunga na Chadema kwa sababu niliamini kuwa UFISADI ndio adui mkubwa wa maendeleo ya Mtanzania na Chadema walichukua fursa hiyo kuupiga vita. Nilikuwa na bahati kuwa karibu na baadhi ya viongozi wake kupitia jukwaa hili la JF, nikawasikia kauli zao, nikasikia malengo yao na kikubwa zaidi walikuwa haribu sana na wananchi wakikubali kuipokea mawazo ya wananchi na hata kukosolewa hapa hapa JF.

Nina mashaka sana kama isingekuwa kijiwe hiki cha JF, mahala nilipoweza kuwasoma hawa viongozi na kuwahoji wakati wanatangaza sera za chama, hakika isingekuwa rahisi mimi kujiunga na chama hiki. Lakini baada tu ya chama kupata Umaarufu, kenge nao wakajiunga ktk kundi la Mamba wakiitwa Wapiganaji.Vingozi wenyewe hawakuwa na shida tena na jukwaa hili kwa sababu maskini akipata makalio hulia bwataaa! ndio kafika. Huu ndio mwanzo wa ukweli kujitokeza kama hivi leo unawaona?. Kupitia haya nikawaasa sana viongozi na hata wanachama wa CDM humu humu JF bila kujua kwamba WATU wengi ktk siasa hutafuta UMAARUFU kama hatua ya kwanza, umaarufu ambao utazijenga CV kisiasa ambayo kwao ni Ajira! Leo hii wako wapi?

Mtu yeyote anayejiunga siasa kwa sababu ya ajira, akaomba saana kura zenu ktk majanvi mbalimbali, akajieleza kwa maneno meengi matamu na kufokea sana mabaya mwogope! maana akisha ingia ndani basi ndiye wa kwanza kulilia posho mishahara, Uheshimiwa na kuwaweka ndugu na wake zao ktk nafasi za uongozi. Ukisha ona vile basi jua chama kimeshaingiliwa na walokuwa na moyo haswa wa kukijenga chama na wazalendo wataonekana wachawi kwani nguvu ya pesa siku zote hu control media! Usikubali kuamini yanayoandikwa ktk magazeti na Blogspot maana hii ni biashara na pesa ndio huzungumza kwanza.

Mkuu miomi bado sijakata tamaa na nina hakika kama ningekuwa Kiogozi basi ningewekwa ktk kundi nla ZZK maana ndivyo Tulivyo lakini ukweli naujua mwenyewe. Sikubali kudanganywa na Ngongoto hawa, kama Mbayuwayu nitachanganya na za kwangu!
 
Swadakta Ndugu Mkandara, maneno yako haya ni Mujarrabu kabisa katika mada hii.

Chadema ya 2008 ni tofauti kabisa na Chadema ya 2014, Chadema ya sasa inaendeshwa kwa hoja nyepesi nyepesi, viongozi wasio na nidhamu ya utendaji, wenye ujuaji mwingi (Lissu et al), wenye kusigina katiba ya chama bila hofu yoyote, majungu na wivu wa kisiasa , imekuwa chadema ya watu wasio na uwezo wa kuibua hoja nzito za Kitaifa, chama kisichojali haki za wanachama wake na hivyo kufanya timuatimua isiyo na kichwa wala miguu!

Kiufupi Chadema must reform, ni lazima kirudishe imani kwa wananchi, la sivyo kitajifia kifo cha mende!
 
Haya mh tumekusikia na tunashukuru kwa maoni yako.

Tunaomab turudi kwenye mada, hapa hatuongelei umaarufu wa CCM au udhaifu wa CDM

Tunaongelea ACT/Kitila na uteuzi wa Mwenyekiti Zitto
 
ACT-Tanzania.
Ni kweli ACT- Tanzania inapambana na vyama vya upinzani.
Habari zenu wanajamii wa Tanzania?

Kuna hisia nyingi na za msingi zinazosambaa zikidhaniwa kuwa ni propaganda za msingi na mbinu za kisiasa au mbinu za kishabiki ingawa hazina viwango halisi.

Kumezoeleka wapinzani Tanzania kuzushiana majina na tuhuma feki na za kubuni ili tu wanaozusha hizo propaganda wapate upenyo wa kupigiwa makofi katika majukwaa ya kisiasa.

Kwa leo ngoja nianze kuwajibu wale wanaogopa na kuanza kujificha nyuma ya vivuli vya kigoda kwa kauli wadhaniazo ni propaganda au ushabiki wenye manufaa kwa vyama vyao kinyume cha ACT-Tanzania.

Hii sentenso ya kuwa ACT-Tanzania inapambana na vyama vya upinzani badala ya kupambana na ccm inatajwa sana japo, hawathibitishi ni wapi na lini mpambano huo umetangazwa, ila wanataja kama hisia zao tu kwa hofu ya kupitwa katika mbio ili kesho waepuke aibu ya kushindwa vibaya.

Ni kweli ACT-Tanzania ikiwa ni chama cha siasa kipya chenye malengo ya kiuchumi, kisiasa, kijamii na mengineyo hakiwezi kuyatimiza bila kutwaa dola, na ACT-Tanzania hakiwezi kutwaa dola toka mikono ya ccm bila kuwapora nguvu wapinzani waliotangulia na kufahamika mbele yake kwanza.

Kwa Tanzania sasa miongoni wa vyama vya siasa takribani 23 ACT-Tanzania ni chama kidogo kuliko vyote kwa maana ya upya wake na kutokuwa na mbunge, diwani wala kiongozi wa serikali za mitaa, hivyo kinashika nafasi ya chini kwa ukongwe wa vyama vilivyopo Tanzania.

Doctrine ya ushindani inakutaka uanze kushindana na mshindani unaelekeana nae au unaelingana nae uwezo, uzito na nguvu, kisha uwaze kushindana na wanaokuzidi uwezo ujaribu bahati yako labda utashinda.

Ni kama mashindano ya mbio mnapoanza mbio za kilomita 5 na mkiwa watu 5, mkiwa ndani ya km ya kwanza wenzio wamekutangulia, ukitaka kuwa mbele ya wenzako ni lazima upambane na mtu wa nne ili uweze kumvuka, kisha upambane na wa 3 kisha wa 2, kisha wa kwanza ushindane nae na hatimaye umshinde uwe mbele yao wote.

Kuwapita wote itategemea mwendo kasi wako, ikiwa wewe ni mvivu usiyeitazama nafasi ya kwanza basi utaishia kupambana na huyo wa size yako mpaka mwisho, na ikiwa unatazama nafasi ya kwanza ni lazima utapiga juhudi na kuifikia kwa malengo uliyojipangia.

Wakati wengine walianza kwamwendokasi kana kwamba wanakimbia mbio za kilomita 100 na sasa wanachoka ndipo unawavuka na kuichekelea nafasi ya kwanza.

ACT -Tanzania iko katika nafasi ya 23 kwa sasa, huku CCM ikiwa nafasi ya 1, CUF na CHADEMA wakifuatia, NCCR, TLP, UDP, ADC na vyama vingine vilivyoshiriki chaguzi mbali mbali viko mbele ya ACT -Tanzania.

Katika malengo ya ACT-Tanzania ya kiuchumi, kisiasa na kijamii tuliyoyanuwia hayawezi kutimia bila kushika dola,na mwenye aloshika dola ni CCM ambaye yuko mbele kilomita kadhaa, kutoka ccm mpaka chama chenye nafasi ya 22 sio mbali kiasi hicho ni kilomita kadhaa tu.

Pamoja na kuwa CCM haiko mbali na tulipo hatuwezi kupambana na asili ya ushindani, ni lazima tuanze kupamabana na aliye mbele yetu yaani chama chenye nafasi ya 22, 21.........3...2....kisha tupambane kuhitimisha kuindoa CCM ili tushike dola kusudi kuu liwe kutimiza lengo la uwepo wetu kama chama, yaani kutimiza malengo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa na mengineyo.

Wala msishangae mkiona tunawapita wote kwa kipindi kifupi na kumfikia CCM kwani nimeeleza kuwa inategemeana na mwendo kasi wa washindani, hivyo tegemeeni kuona tukiwabwaga mapema ili tuweze kumbwaga ccm, hatuwezi kuimwaga ccm kabla ya kuwamwaga wapinzani wenzetu walioshindwa kwa miaka zaidi ya 20 sasa tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi.

Hivyo wanaosambaza sentenso za kiuoga za kuwa ACT-Tanzania inapambana na upinzani wala hawakosei ni lazima tupambane nao ili tuwavuke tuweze kupambana kikamilifu na kumuondoa mtawala mkuu ccm ambaye sababu za kumuondoa zinajulikana ni zile zile zinazohubiriwa na wapinzani wote kila siku, lakini nia za kumuondoa ndizo hutofautiana miongoni mwetu, wapo wapinzani wajuzi sana kubwata na kubwatuka majukwaani kana kwamba wana nia hiyo ili hali ni wawinda upenyo tu wa kutimiza malengo yao binafsi.

Tuko tofauti kiitikadi, kifalsafa za vyama vyetu na hata majina ya vyama ni tofauti, na ndio sababu kila chama kinafanya siasa za kuwataka wananchi wakiunge mkono, wanaCHADEMA wanaoshangaa kuanzishwa kwa chama kipya, kwa nini hawashangai chadema kutoiunga mkono NCCR ambayo ilikuwa na nguvu sana miaka hiyo? (nimewataja chadema kwa sababu hawa wamekuwa mabingwa wa hizi propaganda)ili hali wao wakisahau huwa hawaamini katika upinzani bali wanaamini katika chadema tu kwa maana ya jina la chama, rejea kauli za mwenyekiti wa chadema mbowe 2010 aliposema hawezi shirikiana na tuvyama twa hovyo hovyo, kumbuka alipokataa kuunda kambi ya upinzani ya kushirikisha wapinzani wote, kumbuka juzi alivyowabagua tena TLP,UDP n.k.

TUNAPAMBANA NA KILA CHAMA KILICHOPO ILI WANAVYAMA WAO WATUUNGE MKONO ILI TUIONDOE CCM KIRAHISI MAANA VYAMA VYAO VIMESHINDWA KUIONDOA TANGU MWAKA 1992 MPAKA SASA WANAWAYAWAYA.
Tutapambana sio kwa matusi, bali kwa hoja, tutashindana kuwavuta watu sio kwa kashfa bali sera na falsafa yetu, tutawashughulikia wapinzani wetu sio kwa tindikali bali kwa kuwabomoa kwa hoja, hatimaye tutafika lengo.

Nyakarungu 2014
Mwana ACT-Tanzania, Mwanachama Mwandamizi.
+255 755 023 503
diplomatictable@gmail.com
Dr Kitila Mkumbo , ningeshauri ufuate nyao za Nyakarungu. Yeye kasema wazi kama chama cha 'uwazi' kilivyo. Nyakarungu hakuficha hisia na fikra zake. Kaweka wazi kabisa lazima wapambane na wapinzani wenzao. kumbuka, hayo si maneno ya duru za siasa, ni maneno ya mwanachama mwandamizi.

Nyakarungu kaiba kauli ya sera tofauti na ya Dr aliyeamua kukimbilia uteuzi wa mwenyekiti.
Hakuna shaka Nyakarungu anajibu hoja ingawa amekimbia kujumika nasi.

Dr Kitila, Political science na public relation ni muhimu kwa sasa kuliko uteuzi wa mwenyekiti.
Nyakarungu analeta damage uliyoanzisha akijua anafanya damage control wakati akifanya damage zaidi

cc Ng'wamapalala Mkandara JingalaFalsafa Mchambuzi
 
Mkuu, Nguruvi3

Huyo Nyakarungu ndiyo nani?.

Mwanachama Mwandamizi ndiyo nini?.

ACT ina verified name hapa JF na kupitia Verified name ndiyo tunaweza kujadili content zake kwa sababu haya aliyoleta ni mawazo yake binafsi kama yalivyo mawazo yako.
 
Last edited by a moderator:
Dr Kitila Mkumbo , ningeshauri ufuate nyao za Nyakarungu. Yeye kasema wazi kama chama cha 'uwazi' kilivyo. Nyakarungu hakuficha hisia na fikra zake. Kaweka wazi kabisa lazima wapambane na wapinzani wenzao. kumbuka, hayo si maneno ya duru za siasa, ni maneno ya mwanachama mwandamizi.

Nyakarungu kaiba kauli ya sera tofauti na ya Dr aliyeamua kukimbilia uteuzi wa mwenyekiti.
Hakuna shaka Nyakarungu anajibu hoja ingawa amekimbia kujumika nasi.

Dr Kitila, Political science na public relation ni muhimu kwa sasa kuliko uteuzi wa mwenyekiti.
Nyakarungu analeta damage uliyoanzisha akijua anafanya damage control wakati akifanya damage zaidi

cc Ng'wamapalala Mkandara JingalaFalsafa Mchambuzi

Nyakarungu ni msemaji wa ACT?, ana wadhifa gani ndani ya ACT?. Mleta mada,hata kama ni propaganda "haribifu" dhidi ya hiki chama kipya, mbona zinakosa mashiko?.

Kupambana na ACT kwa hoja hiyo ni O.K, lakini kuichafua ACT ukitegemea kuinusuru CHADEMA au chama chochote wala hakusaidii, infact wala hakuwasaidii Watanzania katika kupanua wigo wa demokrasia!
Waswahili walisema Chema chajiuza, Kibaya chajitembeza!. CHADEMA walitake for granted imani ya wananchi wapenda mabadiriko, matokeo yake wakajiona the "untouchable invinsibles", sasa inaonekana wananchi wamepata mmbadala, tusiwakatishe tamaa kwa technique za "fear mongering"!
 
ACT Tanzania inaongozwa na misingi mikuu mitano ifuatayo:

i ) Uzalendo
ACT-Tanzania inaamini kwamba kila mwananchi ana wajibu wa msingi kabisa wa kutoa mchango wake katika jamii na Taifa kwa ajili ya kuhifadhi ustawi wa nchi kwa ajili ya
kizazi cha leo na cha baadaye.

Ili wananchi waweze kutoa mchango huu kwa dhati na kwa moyo, ni muhimu mazingira yawepo ya kuhakikisha kwamba wananchi wanaipenda nchi yao.

Kwa msingi huu, ACT-Tanzania itajenga mazingira mwafaka ya wananchi kuipenda nchi yao ili wajitoe kikamilifu katika kuijenga na kuilinda. ACT-Tanzania itajenga mazingira yatakayoongeza uzalendo wa wananchi kwa kuhakikisha uwepo wa uwazi, ulinzi na utumiaji bora wa rasilimali za taifa na uadilifu wa viongozi.

ii ) Usawa
ACT-Tanzania inaamini katika usawa katika yyanja zote.

Tunaamini kwamba mafanikio ya mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla yatatokana na bidii katika kazi. Kwahiyo, ACT Tanzania kitapigania kuwepo usawa wa fursa na mazingira mazuri kwa wote katika kuhakikisha kwamba kila mtu na kila kundi katika jamii linakuwa
na fursa sawa ya kufanya kazi za kujiajiri au kuajiriwa, na kwamba kipato kitokanacho na kazi halali ndicho kitakuwa kipimo cha mchango wake katika jamii na taifa .

iii ) Uadilifu
Uadilifu katika maisha binafsi na katika jamii utakuwa ndio msingi na mwongozo mkuu wa viongozi na wanachama wa ACT-Tanzania. ACT- Tanzania inaamini kwamba uadilifu ndio msingi na nguzo kuu ya
mapambano dhidi ya rushwa na maovu mengine katika jamii .

iv ) Uwazi na uwajibikaji
ACT Tanzania inaamini katika uwazi kwenye mambo yote ya kijamii na kitaifa. Hivyo basi viongozi na wanachama wa ACT-Tanzania wana wajibu wa kupigania uwazi katika mambo yote wanayofanya kwa ajili ya umma. Sambamba na uwazi,
ACT - Tanzania inaamini kwamba kila mwananchi na kiongozi mwenye dhamana katika umma ana wajibu katika jamii na Taifa kwa ujumla na ni jukumu lake kutekeleza wajibu huo bila kinyongo. Aidha, mwanachama na kiongozi atokanaye na ACT Tanzania anapaswa kuwajibika kwa maneno na matendo yake katika utumishi au nje ya utumishi wa chama au taasisi
yoyote ya umma. ACT Tanzania inaamini kwamba bidii katika kazi ndiyo njia pekee ya kujipatia maendeleo.. Hivyo basi wajibu mkuu wa mwanachama wa ACT Tanzania
utakuwa ni: BIDII KATIKA KAZI.

v ) Demokrasia ya Kweli
ACT -Tanzania inaamini demokrasia ndiyo msingi wa kujenga fikra pevu na kueneza uhuru wa mtu, jamii na Taifa kwa ujumla. Hivyo basi, viongozi na wanachama wa ACT-Tanzania watapigania uwepo wa demokrasia ya kweli katika kila ngazi, ndani na nje ya chama. Kila jambo lenye maslahi mapana katika chama na katika umma litaamuliwa kwa njia ya kidemokrasia ya moja kwa moja au kupitia kwa wawakilishi waliochaguliwa.

Hapo kwenye nguzo ya TANO, hoja ya Nguruvi3 ipo bayana.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Tukasema kuwa yale ya Mrema hatuhitaji yatokee tena.
Nimeonyesha NCCR na TLP kama mbadala
CUF Maalim na CUF Hamad Rashid
CUF Maalim na CUF chausta
Kitila kutanguliza jina la mtu na siyo sera 'zilizomvutia' ni kurudisha kule kule kwa akina Mrema, Seif,Hamad na Mapalala

Watu hawataki scrutiny wanataka kupokea ujio tu tena ukiambatanishwa na majina makubwa.

Kuhusu mchango wa akina ZZK na Kitila, hakika subira ni jambo muhimu sana katika maisha yetu.
Hawa watu walikubalika katika siasa za chama chao na ilikuwa suala la muda tu wangeongoza. Tatizo ni subira.

Kuhusu suala la kutanguliza jina, hiyo likuwa ni 'psychology' ya kuwaambia watu yule mwenyekiti wenu mnayemtaka sasa anahamia huku, jiandaeni mje. At the same time ilikuwa kumteua katika nafasi ya ueneyekiti wa chama asichojua sera zake bila kufuata kanuni za demokrasia.

Kitila, sera za chama zinatungulia na zinabaki kuwa za chama, wanachama wanafuata na huondoka ikibidi.
Huwezi kujenga chama kwa msingi wa jina, siyo mbadala ni udhaifu.

Kugawana wanachama na CDM hakuondoi tatizo tulilo nalo la papa kuogelea katika bahari kuu kwa raha zake.
Ulipaswa kuwavuta wanachama kutoka pande zote kwa sera, na pengine ungewapata mbadala wengi wa CCM kuliko mbadala wa CDM ambao wapo wapo tu.
Yoote uloandika ni jinsi wewe unavyofikiria ni kutuweka sawa kisaikologia ukitumia dhana, bao au ramli. Ulichoacha hapa kusema ni Mimi Nguruvi3 nadhani huyu Kitila ana nia kadhaa wa kadhaa na unadhani ZZK ni mhusika maana hakuna ushahidi wowote ktk maelezo yako. Na hakuna mtu anayekataa dhana inayoelekea ukweli, lakini kwa vile mnatumia nguvu kubwa sana kuelezea jambo hili inasimama katika uONGO.

Katika elimu ya saikologia hiyo hiyo unayotumia hapa husema kwamba - UONGO SIKU ZOTE HAUNA MWISHO lakini UKWELI UNA MWISHO.
Yaani anayesema uongo ataendelea kuongopa maana hakluna ukweli na ili aonyeshe ni kweli itabidi azidi kuongopa lakini enye ukweli jambo huisha palepale.Hii habari ya Kitila na Zitto imekuwepo kwa muda mrefu sana na kila siku inatungiwa hadith ni ktk kuashiria kuna UONGO zaidi ya Ukweli maanake kama yangekuwa na ukweli basi haya maswala yangekwisha siku nyingi. Na kibaya zaidi hadith hii inafanana sana na sinema ya waraka kaiasi kwamba inaonyesha mtunzi wa tamthiria hii ni yule yule - wetu James Hadley Chase!

Hivyo maadam uongo huu unaendelea kutungiwa UONGO.ili ubakie kuwa kama ukweli inanilazimu kutowaamini kwa lolote m,naloandika. Nisichofahamu ni dhamira yenu maana sii ZZK wala Kitila watakao athirika, hawa wnaa maisha yao na wataendelea kuishi kamawalivyokuwa Chadema lakini mimi mlalahoi hii mistari mnayoendelea kuitunga kama nyimbo za Diamond ndio inanipa wasiwasi kama mnayo nia nzuri na hawa watu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom