Mkuu
Nguruvi3 Nadhani
Kitila Mkumbo siyo mwanachama wa kwanza wa chama cha siasa kumkaribisha kwenye mwanachama mwingine kama utakumbuka Freeman Mbowe alishawahi kumkaribisha Sumaye kujiunga na CDM. kusema Kitila kamteua ZZK kuwa Mwenyekiti ni kumuonea bure kwani pale alikuwa anatoa tu maoni yake ikizingatiwa kuwa ndo kwanza alikuwa anajitambulisha kama mwanachama mpya.[/QUOTE
Nifikiri kama umemsoma
Nguruvi3 vizuri hana tatizo na Zitto kukaribishwa katika chama, kwani swala la kakaribishiwa katika chama ni jambo la kawaida hata mwananchi wa kawaida anakaribishwa katika chama kwa njia mbali mbali kama ukashawishiwa na sera za chama na nk. Lakini tatizo liko iwapo unamkaribisha mtu katika chama chako na kumpa uongozi kabisaa, Je utakuwa na uhakika gani kama mtu huyu sio cheo kilichomfanya kujiunga na chama chenu?
Pili tatizo ambalo mimi linanipa shida ni hili mambo ya kunyang'anyana wanachama, Kama kuna watanzania zaidi ya million 20 wasikuwa na chama chochote kwanini vyama visibuni mbinu za kuwashawishi hawa watu ambao sio wanachama wa chama chochote kujiunga na vyama vyao kuliko kushinda mnanyang'anyana wanachama.. Maana wanachama aliyekuwa CCM na kuamia Chadema, kuna uwezekano mkubwa kuwa kesho atakwenda kwenda ACT na kesho kutwa kurudi CCM/Chadema. Wanachama hawa wanategemea na upepo unapoelekea. Kwa mtizamo wangu ni bora kuwapa elimu wanachama 10 wakaelewa sera za chama, misingi ya chama katiba ya chana na nk. maana hawa watawapa elimu na kushawishi watu mbali mbali, kuliko kupata wanachama 100 unapokwenda kuhutubia katika mikutano ya chama kwa muda wa dk 5 (maana viongozi wengi katika mikutano mara nyingi uhutubia si zaidi ya dk 20) Wanachama hawa mara nyingi ni wafuata mkumbo, wanahamua jambo hapo hapo bila kufikiria na kuelewa sababu ni kwa nini nimejiunga na chama hiki (ingawaje sio wote) na pia kushawishika na kujiunga na chama kingine kirahisi..
Hivyo basi natarajia kuona hiki chama kipya chenye wasomi (kama wanavyojihita) wabuni mbinu za kisomi kuweza kupata wanachama wao kuliko kutumia njia za vilaza(maana tunaambiwa baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa ni vilaza) kujenga chama chao
Alinda ,nadhani
Mtamile hajapitia mabandiko na kuona kiini cha hoja.
Labda nimkumbushe kuwa mazingira aliyoongelea Mbowe na ya Kitila yana tofauti kubwa.
Kwa Mbowe inaweza kuwa sehemu ya maongezi ya kuchangamsha hadhira.
Hata hivyo Mbowe alisema sera za chama chake zinashabihiana na maono ya Sumaye kuhusu rushwa hivyo ajiunge ili atetee hoja yake ya rushwa.
Mbowe alikuwa na hoja ya sera aliyoitumia kumvutia Sumaye so as to speak, ingawaje hilo lisingetokea.
Mbowe na Sumaye hawajawahi kuwa katika 'treni moja' kiasi cha kuhusisha maneno yao.
Siyo maswahiba.
Kitila alisema wana maono yanayoshabihiana na Zitto.
Tunajua walikuwa watu wa waraka kwa pamoja.
Kitila amejiunga na ACT juzi ambapo alimtaka Zitto (mwanachama wa CDM) awe mwenyekiti.
Kitila hakutanguliza sera za kumshaiwishi Zitto, from no where akamteua mwenyekiti.
Katiba ya ACT haijawa tayari, wapi Kitila anapata nguvu za uteuzi na ni kwa mamlaka yapi.
Tunafahamu wana maono sawa ya kisiasa, Kitila angemshauri kwanza Zitto aondoe kesi, ajiunge na ACT halafu mambo mengine yafuate kwa taratibu.
Alichokifanya ni kutulaghai kana kwamba hamjui Zitto. Ni ushauri wa kilaghai ili kumpa Zitto nafasi ya kukimbia mahakamani kwani bunge la katiba halina mwelekeo.
Kitila aliyepinga udinteta alikotoka, sijui kuteua mtu ambaye si mawnachama inaitwa nini.
Ukichanganya na mambo mengine bandiko I, kuna maswali mengi zaidi ya majibu.
Hivi kweli tukae kimya mtu au watu wakitifanya mazezeta? Wakaifanya siasa za kichovu namna hiyo? Lengo lao ni kutaka ZZK aondoke na wanchama JingalaFasalafa anasema wanapulizwa kama upepo.
Hilo wafanye lakini si kwa kutufanya mabubusa.
Kuhusu suala la kuchukua wanachama, mimi hata sioni mantiki yake. Kwa dunia ya leo tulitegemea sera ndizo ziongoze uungwaji mkono, eti bado tunasiasa za majina.
Kuchukuliana wanachama si kwamba kuna ni njia duni kwasababu tatizo si vyama vya upinzani, tatizo ni papa ambaye badala ya kuunganisha kukabliana naye, wapinzani wanapigana vita.
Hizi ndizo siasa za kileo tunazoambiwa! No, lazima watu wabadilike.
Tunahitaji sera si majina, wenye majina wakae nayo mifukoni waache demokrasia istawi.