Nami ''mtoto'' ambaye naweza kuwa stupid nichangie hoja zako muungwana tafadhali.
Kwanza, umemaliza vizuri sana kwa kusema tunarudi nyuma kupambana na CCM kutokana na utitiri wa vyama.
Nimelisema sana hili katika bandiko tulilo nalo, na naomba credit kwa wewe kulitumia leo.
Kama umenisoma nimeeleza mara nyingi, sina tatizo na ujio wa chama chochote au mwanachama kuhama chama kimoja kwenda kingine.Hiyo ni sehemu ya demokrasia na haki za msingi za kila mtanzania.
Nina tatizo na aina ya wanasiasa uchwara wanaotumia uelewa finyu wa jamii kuwapoteza kwasababu tu ya matumbo, na si kile wanachokihubiri.
Ninachokikataa ni wasomi kutumia kalamu na elimu zao kuupotosha umma wakitubabaisha wana mbadala.
Kusuluhisha migogoro ni jambo jema na ni sehemu ya ukomavu wa vyama.
Hata hivyo kuna kiwango ambacho kuvumilika inakuwa ni tatizo kubwa kuliko kuwaondoa.
Migogoro huwa ni sehemu ukomavu, lakini pia kumbuka chama kikongwe kama CCM kimemfukuza Mansour Himid kwasababu zao. Kwenye fizikia wanasema, vitu vina yield point, beyond that kunatokea jambo jingine.
Naelewa wewe ni swahiba wa Zitto, niwie radhi nitakapokugusa.
Zitto na Kitila ni mfano mzuri wa wanasiasa wanaotia shaka na hofu ,kimantiki, weledi na moral authority.
In fact kwangu mimi ni political opportunists tu.
Unafahamu ZZK alikuwa ni tatizo CDM,amevumiliwa sana akikingiwa kifua na Mbowe.
Baraza kuu liliwahi kutoa maazimio kumhusu,akavumiliwa.
Zitto ni chanzo cha migogoro akiongoza vijana wa Bavicha waliomtaja kwa kila aina ya ushiriki na ushahidi.
Alikuwa nyuma ya Juliana akitetewa na Kitila magazetini wakizorotesha CDM ili hali ni viongozi waandamizi.
Ni mshiriki wa Masalia and thanks to
Ben Saanane who came to the rescue at the right time.
Mpango wa Juliana uliposhindikana, ukaundwa mpango wa Waraka.
Ikafika mahali ZZK akiwa katibu mkuu anacheza upande wa pili kutuhuma chama chake yeye akiwa kiongozi.
Mpango wa Waraka ambao ukiusoma ni mpango wa hovyo uliposhindwa ndipo ACT ikaanza kuundwa.
Katika kubabaisha watu ZZK akakimbilia mahakamani. Tunajua alitaka kuwa ndani ya BMLK, wala si kutaka kutetea haki.
Katika kumhamisha, Kitila kaanza kutudanganya anamshwishi ajiunge na ACT.
Tunafahamu hawa ni washirika katika shughuli zao, lengo la Kitila lilikuwa kuwaanda washabiki wasioelewa kumfuata Zitto.
Hilo nalo si tatizo, tatizo ni kutufanya sote ni vilaza kama kundi wanalolenga. Hapo tunasema, ney! stop
Tatizo linalojitokeza ni mkakati wa ACT kupambana na wapinzani badala ya CCM.
Hapa ndipo hoja ilipo, hivi hawa wasomi wanatumia nyenzo gani wakati wa kufikiri?
Tumeona kifo cha NCCR, halafu CUF na jinsi upinzani ulivyozorota na nyangumi CCM akitamba kwa ufisadi.
Hawa wasomi akili zao si kuondoa CCM ni kupambana na upinzani, REAL!
Ikifika hapo swahiba wako Zitto ni tatizo kubwa la siasa za nchi.Mshirika wake Kitila anaamini nchi hii lazima iongozwe na Zitto.
Na yote hayo yalizaa vurugu wakati wa chaguzi huku Zitto akileta sintofahamu, Kitila akiwachochea akina Juliana katika jitihada za kukimaliza chama chao wenyewe, na wao wakiwa viongozi.
Zitto katibu mkuu anatangaza kuwania urais wakati mgombea wa chama chake yupo katika kampeni.
Kwa uvivu na uzembe wa CDM walimvumilia kama unavyomvumilia, kwasababu ni mtu muhimu sana kwenye siasa za nchi hii. Real!
Tunazidi kupata ushahidi wa ushirikiano wa Kigoma, CDM,Ludovic, Mwigamba, Zitto, Kitila, Msaki,Lwakatare, CCM,Polisi kila uchao.Ipo siku tutasikia mengine achilia mbali yale ya masalia, text, waraka n.k.
Katika unafiki wa namna hiyo , ni akina
Waberoya wanaoweza kuamini hawa watu wanastahili kupewa benefit of doubt katika nyanja za siasa.Pitia mabadiko ya ACT , hakuna sera ni mipasho tu halafu tunaaminisha ni mbadala wa CCM.
Narudia tena 'mtoto' sikuwahi kuandika chochote kuhusu ACT hadi ilipopata usajili na zaidi ya hapo.
Nimeanza kuandika baada ya akina Kitila na Zitto kuanza kutufanya umma wa Watanzania ni mazezeta.
Tunachojaribu kuwaambia hapa ni kuachana na siasa za majitaka za kitoto na watangulize usomi katika kufanya mambo.
Haya wanayofanya yanatokea kwa PPPT, jahazi au TLP na wala hayatushughulishi.
Kinachotushughulisha kwa hawa wasomi ni kuwa, wao ndio walioandika sera wanazosema ni mbaya leo hii.
Hawa ndio walipiga vita udikteta, wakitaka demokrasia itamalaki.Leo wanakuja na majitaka yale yale waliyokataa huko walikotoka.
Sisi tunasimama na kusema, umma lazima uwaelewa. Hatuwezi kuishi na wanafiki wa CCM miaka nenda rudi na tukae kimya wengine wakizaliwa na tukiwaona.
Lengo la ACT ni kuja kuua upinzani. Hatujali upinzani ni wa chama gani, tunacholaani ni ACT ya Zitto na Kitila kutaka kuturudisha kwa akina Mabere na Mrema. Ni kulaani kurudi kwa CUF ya Seif na Hamad Rashid. CUF ya Seif na Mapalala.
Tunalaani mbinu za kutibu matumbo kama anavyofanya Mrema.
Kukaa kimya ni kufumbia macho gonjwa baya la udanganyifu na siasa uchwara.Tunataka tutoke tulipo na si kuamini majina au watu.
Sina tatizo na ACT hata kidogo kwasababu hata sera zao sijaziona.
Nina tatizo na wanafiki wa ACT wanaotaka kutumia ignorance ya jamii kufanya political exploitation.
Ney, tutasimama, narudia tutasimama kuueleza umma kuhusu wanafiki, wazandiki na wasaliti wanaotibu njaa zao kwa kuwatumia wasiobahatika kuwa na uelewa kama ngazi za kujenga matumbo yao.
Na hapa simungunyi maneno, Kitila na Zitto ni national disaster in political sphere.
Waberoya, Nguruvi3 haangalii makunyanzi. Nimeshamwambia(Nipo katika rekodi) Mbowe mara nyingi, Dr Slaa tena mara ya mwisho ni mwezi uliopita, Mwigulu, Nape, Seif, Lema, Jusa, JK,Mrema na wengine.
Ninasema ninachotaka kukuambia na si kile unachotaka kusikia.