Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
- Thread starter
- #161
Hivi niulize, Zitto alipofukuzwa Chadema walitegemea atafanya nini? arudi Kigoma kuwa mkulima au akatafuta kazi za maofisini? jamani mwanasiasa yeyote ambaye anataka kufanya mageuzi ya kijamii lazima kwanza ajiunge na chama cha siasa na kikubwa zaidi vision yake iwe ktk mrengo anao uafiki kwa ndio njia pekee ya kuwaletea wananchi mendeleo.
Zitto lazima angejiunga na chama cha siasa sasa chama gani hilo ndio wengi walikuwa wakisubiria japo ilijulikana wazi kwamba baada ya kufukuzwa walianzisha chama chao ili kuendelea Fikra na ndoto zao ktk kumkomboa Mtanzania na sio kuivuruga Chadema. Chadema itajivuruga yenyewe maana kuondoka kwa Zitto sii mwisho wa Chadema na sio tu waliamini hivyo bali walijiandaa kwa hilo.
sasa nashangaa sana kuwasoma watu mkisema ACT na Zitto ni Mpini wa CCM ilihali Mapinduzi waotaka kuyafanya ndani ya Chadema na sio kuiweka Chadema chini ya CCM. Mapinduzi walotaka kuyafanya yalihusu utawala wa chama ambao kulingana na katiba na kanuni za Chadema sii lazima wawe viongozi wa Kitaifa. Mwenyekiti sii lazima awe mgombea Urais. Tumeona ya Dr.Slaa na tulitegemea pia mwaka huu atachaguliwa mgombea na sio lazima atoke kati ya wajumbe wa kamati kuu.
I mean mimi nashindwa kabisa kuwaelewa Watanzania maana mliwafukuza mkijua watajiunga na chama kingine hawatakomea hapo maana hawa ni wanasiasa na maisha yao yamejengeka ktk siasa, halafu leo wameamua kutojiunga na chama kingine chochote, bali waendeleze azma yao wenyewe kwa kuunda chama chao imekuwa shida kwenu, kwani hamkujua kwamba hawa watu wataendelea kuwepo ktk SIASA? Yaani kufukuzwa Chadema ndio mlitaka wafikwe na mabaya na uwe mwisho wao!. Kwa nini sisi watu maskini wa roho na mali siku zote ni kuombeana mabaya tu, hakuna mtu anafikiria kumtakia mema mwenzake!.
\- Hizi ndizo huitwa akili ndogo..
Mkuu Nguruvi3, maelezo yako hapo juu kuhusu Zitto, Kitila na madudu ya ccm na madudu ya chadema kwa mujibu wao hao maswahiba kisha mazuri ya act inaonyesha wazi hawa jamaa wanafagilia hili dude liitwalo "DOUBLE STANDARDS".
@Mkandara na Adharusi
Nina uhakika hamuelewi dhana halisi ya mabandiko au madailiyopo.
Nina uhakika hamjapitia mabandiko mkajua ni kwanini imeandikwa ‘mpini' wa kumaliza upinzani.
Pitieni mabandiko kabla ya kuingia kati treni ikiwa katika mwendo
Naomba nifafanue kuwa bandiko namba moja tumeeleza haki ya mtu au watu kujiunga na vyama vya siasa.
Bandiko namba 2 limeeleza kwa kina mgogoro na kile walichokataa na kwenda kukifanya kwingine.
Mabandiko yaliyofuata yalikuwa vivyo hivyo
Hakuna aliyesema ni dhambi kufanya siasa, wala kusema unaweza kufanya siasa nje ya vyama katika muundo wetu.
Tunachokifanya ni kuonyesha mbinu zinazotumiwa ambazo nyingi ni za kilaghai
Tunafanya hivyo ili kujenga kizazi cha wanasiasa wakweli,waadilifu na wanaosimama katika kile wanachokisema
Mfano, Zitto alikataa posho kwasababu ya kuona si haki kwa wananchi.
Zitto huyo huyo Mzalendo akakimbia mahakamani si kutafuta haki bali kulinda ubunge wake kwa njia za mahakama.
Hapa huoni tatizo lauadilifu
Kitila alikataa utaratibu wa kufukuza wanachama. Ameenda ACT tayari kamfukukuza mwanzisilishi.
Hakufanya hivyo kutetea demokrasia bali kutengeneza mazingira ya ujio wa rafiki yake Zitto.
Huoni tatizo la uadilifuhapo?
Kitila na Mwigamba wamekemea ‘ufalme'. Huko walikowanatengeneza mazingira ya ufalme ule ule waliokataa kitapeli.
Huoni tatizo lauadilifu?
Zitto anaeleza kufukuzwa, haelezi kwanini amefukuzwa. Mkuu huoni upungufu wa maadili hapo
Mifano inaweza kujaza kura 100. Kwa ufupi tunachofanya hapani kuonyesha aina ya wanasiasa tulio nao na kujenga mwelekeo mpya kimtazamo
Hatuwezi kuwasota vidole CCM peke yao. Tukiwa watu huru tunaosimama kuhesabiwa katika ukweli tutasema kila kinachotokea.Imekuwa ni hivyo kwa mambo mengi tu yanayojiri
Tunafahamu wapenzi na mashabiki wa baadhi ya wanasiasa hawatafurahi achilia mbali kukubaliana na uchambuzi.
Hiyo ni haki yao na wala si dhambi.
Haki yao isivuke mipakana kuingilia haki zetu za kueleza tunachokiona kwa utaratibu wetu
Mkandara, kwavile umebaini hii ni ‘akili ndogo' ni vema ukaicha ifanye mambo yake, usishawishi umma kwa mtazamo wako kuwa mtazamo wa umma
Tutaendelea na utaratibu wetu bila kumuonea awaye, au kumonea haya
Tunaongozwa na ukweli, na katika hilo wapo wasio tutakiamema, hao ni wachache kuliko wale wanaosema yapo wanayoyaelewa na kujifunza
Tunaendelea hapa chini