Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Hivi niulize, Zitto alipofukuzwa Chadema walitegemea atafanya nini? arudi Kigoma kuwa mkulima au akatafuta kazi za maofisini? jamani mwanasiasa yeyote ambaye anataka kufanya mageuzi ya kijamii lazima kwanza ajiunge na chama cha siasa na kikubwa zaidi vision yake iwe ktk mrengo anao uafiki kwa ndio njia pekee ya kuwaletea wananchi mendeleo.

Zitto lazima angejiunga na chama cha siasa sasa chama gani hilo ndio wengi walikuwa wakisubiria japo ilijulikana wazi kwamba baada ya kufukuzwa walianzisha chama chao ili kuendelea Fikra na ndoto zao ktk kumkomboa Mtanzania na sio kuivuruga Chadema. Chadema itajivuruga yenyewe maana kuondoka kwa Zitto sii mwisho wa Chadema na sio tu waliamini hivyo bali walijiandaa kwa hilo.

sasa nashangaa sana kuwasoma watu mkisema ACT na Zitto ni Mpini wa CCM ilihali Mapinduzi waotaka kuyafanya ndani ya Chadema na sio kuiweka Chadema chini ya CCM. Mapinduzi walotaka kuyafanya yalihusu utawala wa chama ambao kulingana na katiba na kanuni za Chadema sii lazima wawe viongozi wa Kitaifa. Mwenyekiti sii lazima awe mgombea Urais. Tumeona ya Dr.Slaa na tulitegemea pia mwaka huu atachaguliwa mgombea na sio lazima atoke kati ya wajumbe wa kamati kuu.

I mean mimi nashindwa kabisa kuwaelewa Watanzania maana mliwafukuza mkijua watajiunga na chama kingine hawatakomea hapo maana hawa ni wanasiasa na maisha yao yamejengeka ktk siasa, halafu leo wameamua kutojiunga na chama kingine chochote, bali waendeleze azma yao wenyewe kwa kuunda chama chao imekuwa shida kwenu, kwani hamkujua kwamba hawa watu wataendelea kuwepo ktk SIASA? Yaani kufukuzwa Chadema ndio mlitaka wafikwe na mabaya na uwe mwisho wao!. Kwa nini sisi watu maskini wa roho na mali siku zote ni kuombeana mabaya tu, hakuna mtu anafikiria kumtakia mema mwenzake!.
\- Hizi ndizo huitwa akili ndogo..
Mkuu Nguruvi3, maelezo yako hapo juu kuhusu Zitto, Kitila na madudu ya ccm na madudu ya chadema kwa mujibu wao hao maswahiba kisha mazuri ya act inaonyesha wazi hawa jamaa wanafagilia hili dude liitwalo "DOUBLE STANDARDS".
mkuu mkandala bila kuwa biased jaribu kucheki kwa jicho la 3 chama cha ACT na viongozi wake na waraka wa akina Mkumbo, si vibaya kama utarudia kusoma kwa makini hoja za Nguruvi3 kuanzia mwanzo wa thread hii.
@Mkandara na Adharusi
Nina uhakika hamuelewi dhana halisi ya mabandiko au madailiyopo.

Nina uhakika hamjapitia mabandiko mkajua ni kwanini imeandikwa ‘mpini' wa kumaliza upinzani.
Pitieni mabandiko kabla ya kuingia kati treni ikiwa katika mwendo

Naomba nifafanue kuwa bandiko namba moja tumeeleza haki ya mtu au watu kujiunga na vyama vya siasa.

Bandiko namba 2 limeeleza kwa kina mgogoro na kile walichokataa na kwenda kukifanya kwingine.

Mabandiko yaliyofuata yalikuwa vivyo hivyo

Hakuna aliyesema ni dhambi kufanya siasa, wala kusema unaweza kufanya siasa nje ya vyama katika muundo wetu.
Tunachokifanya ni kuonyesha mbinu zinazotumiwa ambazo nyingi ni za kilaghai

Tunafanya hivyo ili kujenga kizazi cha wanasiasa wakweli,waadilifu na wanaosimama katika kile wanachokisema
Mfano, Zitto alikataa posho kwasababu ya kuona si haki kwa wananchi.

Zitto huyo huyo Mzalendo akakimbia mahakamani si kutafuta haki bali kulinda ubunge wake kwa njia za mahakama.
Hapa huoni tatizo lauadilifu

Kitila alikataa utaratibu wa kufukuza wanachama. Ameenda ACT tayari kamfukukuza mwanzisilishi.

Hakufanya hivyo kutetea demokrasia bali kutengeneza mazingira ya ujio wa rafiki yake Zitto.
Huoni tatizo la uadilifuhapo?

Kitila na Mwigamba wamekemea ‘ufalme'. Huko walikowanatengeneza mazingira ya ufalme ule ule waliokataa kitapeli.
Huoni tatizo lauadilifu?

Zitto anaeleza kufukuzwa, haelezi kwanini amefukuzwa. Mkuu huoni upungufu wa maadili hapo

Mifano inaweza kujaza kura 100. Kwa ufupi tunachofanya hapani kuonyesha aina ya wanasiasa tulio nao na kujenga mwelekeo mpya kimtazamo

Hatuwezi kuwasota vidole CCM peke yao. Tukiwa watu huru tunaosimama kuhesabiwa katika ukweli tutasema kila kinachotokea.Imekuwa ni hivyo kwa mambo mengi tu yanayojiri

Tunafahamu wapenzi na mashabiki wa baadhi ya wanasiasa hawatafurahi achilia mbali kukubaliana na uchambuzi.
Hiyo ni haki yao na wala si dhambi.

Haki yao isivuke mipakana kuingilia haki zetu za kueleza tunachokiona kwa utaratibu wetu

Mkandara, kwavile umebaini hii ni ‘akili ndogo' ni vema ukaicha ifanye mambo yake, usishawishi umma kwa mtazamo wako kuwa mtazamo wa umma

Tutaendelea na utaratibu wetu bila kumuonea awaye, au kumonea haya

Tunaongozwa na ukweli, na katika hilo wapo wasio tutakiamema, hao ni wachache kuliko wale wanaosema yapo wanayoyaelewa na kujifunza

Tunaendelea hapa chini
 
Hivi niulize, Zitto alipofukuzwa Chadema walitegemea atafanya nini? arudi Kigoma kuwa mkulima au akatafuta kazi za maofisini? jamani mwanasiasa yeyote ambaye anataka kufanya mageuzi ya kijamii lazima kwanza ajiunge na chama cha siasa na kikubwa zaidi vision yake iwe ktk mrengo anao uafiki kwa ndio njia pekee ya kuwaletea wananchi mendeleo.

Zitto lazima angejiunga na chama cha siasa sasa chama gani hilo ndio wengi walikuwa wakisubiria japo ilijulikana wazi kwamba baada ya kufukuzwa walianzisha chama chao ili kuendelea Fikra na ndoto zao ktk kumkomboa Mtanzania na sio kuivuruga Chadema. Chadema itajivuruga yenyewe maana kuondoka kwa Zitto sii mwisho wa Chadema na sio tu waliamini hivyo bali walijiandaa kwa hilo.

sasa nashangaa sana kuwasoma watu mkisema ACT na Zitto ni Mpini wa CCM ilihali Mapinduzi waotaka kuyafanya ndani ya Chadema na sio kuiweka Chadema chini ya CCM. Mapinduzi walotaka kuyafanya yalihusu utawala wa chama ambao kulingana na katiba na kanuni za Chadema sii lazima wawe viongozi wa Kitaifa. Mwenyekiti sii lazima awe mgombea Urais. Tumeona ya Dr.Slaa na tulitegemea pia mwaka huu atachaguliwa mgombea na sio lazima atoke kati ya wajumbe wa kamati kuu.

I mean mimi nashindwa kabisa kuwaelewa Watanzania maana mliwafukuza mkijua watajiunga na chama kingine hawatakomea hapo maana hawa ni wanasiasa na maisha yao yamejengeka ktk siasa, halafu leo wameamua kutojiunga na chama kingine chochote, bali waendeleze azma yao wenyewe kwa kuunda chama chao imekuwa shida kwenu, kwani hamkujua kwamba hawa watu wataendelea kuwepo ktk SIASA? Yaani kufukuzwa Chadema ndio mlitaka wafikwe na mabaya na uwe mwisho wao!. Kwa nini sisi watu maskini wa roho na mali siku zote ni kuombeana mabaya tu, hakuna mtu anafikiria kumtakia mema mwenzake!.
\- Hizi ndizo huitwa akili ndogo..
Mkandara,

Nimejaribu kuelewa bandiko lako lakini Nimeshindwa kuelewa ulilenga kujenga hoja gani. Lakini ni vizuri umekiri kwamba Zitto alilenga kufanya mapinduzi ndani ya Chadema, ila haujadili kwamba kufanya hivyo ni kinyume cha kanuni, taratibu, Sheria na Katiba Ya Chadema. Otherwise Sioni any objective analysis Katika bandiko kako, na badala Yake ni hoja zilizojaa uchungu na jazba.

Zitto amekikosea Chadema, Zitto ameikosea demokrasia, Zitto amewakosea wananchi ambao aliwapa matumaini. Haya yote yamejadiliwa vyema humu.
 
Last edited by a moderator:

Mchambuzi, mkadara nguruvi3

Tunaweza kukubaliana wote kuwa Zitto alikuwa na nyota inayong'aa, lakini ameiharibu mwenyewe. Sidhani kama mimi naweza kuingia huko kwenye kukikosea chama, kuwakosea wananchi na kuikosea demokrasia. Zitto amekuwa na kiherehere na matokeo yake ni kuwa ametutosa watanzania. Sidhani kama Zitto angepungukiwa na kitu kusubiri miaka 10 kuwa mzito, kiherehere chake kimeharibu kila kitu.

Kutoka Chadema kweney ACT ni kujimaliza kisiasa, he will never recover from the sin he commited.

All in all i can say big up CCM, the planned has worked...for now.
 
Mkuu kinachotakiwa ni kuzungumzia Zitto ametendewa nini.Analysis yoyote haitakiwi kwasababu itagusa maeneo ‘yasiyotakiwa' na mashabikina wapenzi.
Mkuu, katika bandiko 151 tumeeleza kuhusu makundi matatu
1 Kundi linaloamini katika Zitto ambalo haliwezikubadilika wala kubadilishwa. Ni kundi lililojitoa kwa Z katika njia za mapenzi yasiyoelezeka. Zitto akitembea utupu kundi hili linaweza kusema hiyo ni fashion mjini.
Ndilo linalichukia habari zake kuandikwa. Linatuita wengine ‘akili ndogo''

2 Kundi lillopotezaimani kwa Zitto. Hili lilikuwa linamwani, kwa bahati nzuri au mbaya limeonambali.
Halimwamini hata kama ataamua kugawa keki, asali, maziwa na mayai' kilasiku

3. Kundi lisloweza kumweka Zitto popote. Lina mashaka nahofu kuhusu nia njema au mbaya.
Ni kundi lilochanganyikiwa kuhusu huyu bwana.
 
Mchambuzi, mkadara nguruvi3

Tunaweza kukubaliana wote kuwa Zitto alikuwa na nyota inayong'aa, lakini ameiharibu mwenyewe. Sidhani kama mimi naweza kuingia huko kwenye kukikosea chama, kuwakosea wananchi na kuikosea demokrasia. Zitto amekuwa na kiherehere na matokeo yake ni kuwa ametutosa watanzania. Sidhani kama Zitto angepungukiwa na kitu kusubiri miaka 10 kuwa mzito, kiherehere chake kimeharibu kila kitu.

Kutoka Chadema kweney ACT ni kujimaliza kisiasa, he will never recover from the sin he commited.

All in all i can say big up CCM, the planned has worked...for now.
Ahsante

Niliwahi kumwambia Zitto mwaka 2011 kuwa yeye hahitajinyadhifa yoyote katika chama.
Anachotakiwa ni kuwa muungwana tu, mnyenyekevu kwa wanachama wenzake na kuondoa kiburi kidogo .

Akifanikiwa hayo, atashangaa kiti kinaletwa, anabebwa nakukalishwa, kisha watu wanafagia njia bila yeye kusema neno hata moja.

Zitto akaendelea na yake, leo kanuni za asili zinamjibu analalamikia watu.
Kanuni za asili zinasema ‘kila jambo lina wakati wake' hata wahenga walisema subira yavuta heri.

Gharama za kwenda kasi zaidi ya muda ni kubwa. Na kwa mwendo alio nao, bado atasubiri muda ule ule aliotakiwa asubiri.

Tofauti nikuwa ‘take off' ya sasa itahitaji mafuta mengine na umakini.

Yes CCM wamefanikiwa.
Inapotokea CCM wanafadhaika mpinzani kukutwa na maswahibu lipo jambo hapo.

CCM wamefanikiwa kwa njia nyingi

1 Walitaka Zitto aendelee ili kuwe na tension ndani yaCDM itakayoondoa focus dhidi yao

2. Zitto aondoke ili kujenga mtafaruku kati ya wapinzani,jambo linalofanywa kiufundi na ACT kwasasa. Fuatilia kauli zao.

3 Hizi habari za Zitto kila siku zimetoa ahueni watukusahau ujahilia wa CCM

Hatuoni kama CCM wana tatizo katika hili. Huo ndiomkakati wao na unafanikiwa.

Tunachojua ni kuwa hakuna shoka linalokata bila mpini!
 
Hivi niulize, Zitto alipofukuzwa Chadema walitegemea atafanya nini? arudi Kigoma kuwa mkulima au akatafuta kazi za maofisini? jamani mwanasiasa yeyote ambaye anataka kufanya mageuzi ya kijamii lazima kwanza ajiunge na chama cha siasa na kikubwa zaidi vision yake iwe ktk mrengo anao uafiki kwa ndio njia pekee ya kuwaletea wananchi mendeleo.

Zitto lazima angejiunga na chama cha siasa sasa chama gani hilo ndio wengi walikuwa wakisubiria japo ilijulikana wazi kwamba baada ya kufukuzwa walianzisha chama chao ili kuendelea Fikra na ndoto zao ktk kumkomboa Mtanzania na sio kuivuruga Chadema. Chadema itajivuruga yenyewe maana kuondoka kwa Zitto sii mwisho wa Chadema na sio tu waliamini hivyo bali walijiandaa kwa hilo.

sasa nashangaa sana kuwasoma watu mkisema ACT na Zitto ni Mpini wa CCM ilihali Mapinduzi waotaka kuyafanya ndani ya Chadema na sio kuiweka Chadema chini ya CCM. Mapinduzi walotaka kuyafanya yalihusu utawala wa chama ambao kulingana na katiba na kanuni za Chadema sii lazima wawe viongozi wa Kitaifa. Mwenyekiti sii lazima awe mgombea Urais. Tumeona ya Dr.Slaa na tulitegemea pia mwaka huu atachaguliwa mgombea na sio lazima atoke kati ya wajumbe wa kamati kuu.

I mean mimi nashindwa kabisa kuwaelewa Watanzania maana mliwafukuza mkijua watajiunga na chama kingine hawatakomea hapo maana hawa ni wanasiasa na maisha yao yamejengeka ktk siasa, halafu leo wameamua kutojiunga na chama kingine chochote, bali waendeleze azma yao wenyewe kwa kuunda chama chao imekuwa shida kwenu, kwani hamkujua kwamba hawa watu wataendelea kuwepo ktk SIASA? Yaani kufukuzwa Chadema ndio mlitaka wafikwe na mabaya na uwe mwisho wao!. Kwa nini sisi watu maskini wa roho na mali siku zote ni kuombeana mabaya tu, hakuna mtu anafikiria kumtakia mema mwenzake!.
\- Hizi ndizo huitwa akili ndogo..

Mkandara,

Mimi nakubaliana na wewe kwa asilimia zote.

Hakika siku zote adui yako muombee Njaa. sasa hapa Chadema walitaka kumuua kabisa ZZK kisiasa na waliamini kwa walivyofanya basi watakuwa wamemmaliza kabisa ZZK kisiasa na kuonekana ni takataka miongoni mwa jamii.

Mimi naamini wazi kuwa ndani ya Chadema hususam wale wabunge walioingia Bungeni hakuna Kichwa kama Zitto. Na kijana alikuwa na msimamo na mara zote alisimamia kile alichoamini kuwa ni sahihi.

Nitatoa mfano mmoja hapo. Chadema walipoingia Bungeni 2010 walikuja na Sera moja ya kupinga POSHO za wabunge na ilifikia pahala mpaka Mbowe kwa mbwembwe kabisa akaonyesha amelipark gari lile la KUB (kiongozi wa upinzani bungeni). Sasa tujiulize sasa kipo wapi? mbowe kinyemela alirudi na kulichukua hilo gari na nasikia ndilo analozunguka nalo nchini mwenu. Na wabunge wengine kinyemela walianza kuzifakamia hizo posho na hata kufikia kudai kuwa ni kiduchu ziongezwe.

Mbunge pekee aliyesimama na msimamo wake wa kupinga ni Zitto. yeye alikana na alikataa kupokea posho hizo.

Kwa tarbia hizo na misimamo hiyo utaona ilikuwa si rahisi kwa kijana kama huyo ambaye aliwahi kutishia kuitaka kugombea nafasi ya uenyekiti lakin baraza la wazee lilimzuia kwa sababu zisizo na msingi katika kidemokrasia.

Tunaamini NDEGE WENYE MBAWA SAWA HURUKA PAMOJA.

Uamuzi wa Zitto ni muafaka na amechukua kwa wakti muafaka kutekeleza kile anachoamini kuwa kina maslah na manufaa kwake na kwa jamii yake.

Kila lenye kheir Zitto kabwe

@Mkandara na Adharusi
Nina uhakika hamuelewi dhana halisi ya mabandiko au madailiyopo.

Ninauhakika hamjapitia mabandiko mkajua ni kwanini imeandikwa ‘mpini' wa kumaliza upinzani.
Pitieni mabandiko kabla ya kuingia kati treni ikiwa katika mwendo

Naomba nifafanue kuwa bandiko namba moja tumeeleza haki ya mtu au watu kujiunga na vyama vya siasa.

Bandiko namba 2 limeeleza kwa kinamgogoro na kile walichokataa na kwenda kukifanya kwingine.

Mabandiko yaliyofuata yalikuwa vivyo hivyo

Hakuna aliyesema ni dhambi kufanya siasa, wala kusemaunaweza kufanya siasa nje ya vyama katika muundo wetu.
Tunachokifanya ni kuonyesha zinazotumiwa ambazo nyingi ni zakilaghai

Tunafanya hivyo ili kujenga kizazi cha wanasiasa wakweli,waadilifu na wanaosimama katika kile wanachokisema
Mfano, Zitto alikataa posho kwasababu ya kuona si haki kwawananchi.

Zitto huyo huyo Mzakendo akakimbia mahakamani si kutafutahaki bali kulinda ubunge wake kwa njia za mahakama.
Hapa huoni tatizo lauadilifu

Kitila alikataa utaratibu wa kufukuza wanachama. Ameenda ACTtayari kamfukukuza mwanzisilishi.

Hakufanya hivyo kutetea demokrasia balikutengeneza mazingira ya ujio wa rafiki yake Zitto. Huoni tatizo la uadilifuhapo?

Kitila na Mwigamba wamekemea ‘ufalme'. Huko walikowanatengeneza mazingira ya ufalme ule ule waliokataa kitapeli. Huoni tatizo lauadilifu?

Zitto anaeleza kufukuzwa, haelezi kwanini amefukuzwa. Mkuuhuoni upungufu wa maadili hapo

Mifano inaweza kujaza kura 100. Kwa ufupi tunachofanya hapani kuonyesha aina ya wanasiasa tulio nao na kujenga mwelekeo mpya kimtazamo

Hatuwezi kuwasota vidole CCM peke yao. Tukiwa watu hurutunaosimama kuhesabiwa katika ukweli tutasema kila kinachotokea.Imekuwa ni hivyo kwa mambo mengi tu yanayojiri

Tunafahamu wapenzi na mashabiki wa baadhi ya wanasiasahawatafurahi achilia mbali kukubaliana na uchambuzi.
Hiyo ni haki yao na wala si dhambi.

Haki yao isivuke mipakana kuingilia haki zetu za kueleza tunachokiona kwa utaratibu wetu

Mkandara, kwavile umebaini hii ni ‘akili ndogo' ni vemaukaicha ifanye mambo yake, usishawishi umma kwa mtazamo wako kuwa mtazamo waumma

Tutaendelea na utaratibu wetu bila kumuonea awaye, aukumonea haya

Tunaongozwa na ukweli, na katika hilo wapo wasiotutakiamema, hao ni wachache kuliko wale wanaosema yapo wanayoyaelewa na kujifunza

Tunaendelea hapa chini
Mkuu nilikusoma toka mwanzo na tunarudia majibu yale yale tulobishana toka mwanzo. Unachofanya wewe ni kuandika baada ya matokeo. Yaani Mtu kampiga talaka tatu mkewe na unamshabikia mume basi mke hatakuwa na haki wala sheria. Usiandike chanzo cha tukio zima kwa kuitaka haki sawia juu ya wagonvi hawa, ili watu wakusome na wachambue nani mbaya, nani hasidi wa ndoa hii isipokuwa unamtaja mbaya wako kwa mabaya yake kama unavyoelewa wewe ama unavyotaka wewe kutokana na uhusiano wako na mume wa ndoa hiii. Umeshachagua Upande, inakuwa vigumu kuwa msuluhishi maana unayaona ya upande mmoja tu ndilo nalokupingeni muda wote.

Aidha mwanamke huyo kasingiziwa kutembea nje ya ndoa mmeshindwa kutuonyesha ufahamu wenu juu ya kisa kizima isipokuwa kwa kutumia madai ya bwana, usisikie kabisa kilio cha mke japo ana haki hiyo. Na pasipo kutafuta undani kama kweli katembea nje ya ndoa ama kasingiziwa ila unatazama baada ya kufukuzwa na mumewe, huyu mwanamke kafanya nini na tafanya nini.. Hutuelezi mwanamme wake kafanya nini ila hoja bado ipo kwa mwanamke, Oooh unaona sasa kenda kuolewa tena na mume mwingine na kusema - "Mnaona tulijua tu huyu mwanamke Malaya!. Kuachwa tu kesha mpata bwana."

Alaa jamani sasa mlitegemea kwamba huyo mwanamke angekuwa na maisha gani baada ya kutalakiwa? Lakini yalofuatia huko Chadema baada ya kuondoka kwa kina Zitto sii muhimu ama kuna makosa ila ni baraka tupu. Ya Chadema kujiunga na CUF ambayo tuliambiwa ni CCM - B 2010 tena waloingia Muafaka na CCM kwa ushahidi juu ya mustakabali wa nchi hii pasipo kuvihusisha vyama vingine ikiwemo Chadema hakuna kosa kwa sababu mnaitaka serikali ya Tanganyika, hivyo hayana uzito wa kusemwa katika mada hii. Chadema imeenda kuwa na mwanamke alokwisha olewa sii kosa kwa sababu mna lengo moja!

Chadema kuwa karibu na Mbatia ambaye tuliambiwa ni kibaraka wa CCM alopewa hadi Ubunge kwa tiketi ya rais hatuyasemi ila mnatupiga changa la macho tusiyaone yalofuatia baada ya ndoa hii kuvunjika na kusema kweli binafsi yangu naamini kabisa CUF hawawezi kuwaaamini Chadema 100% wala Chadema kuwaamini CUF 100% isipokuwa wanachezeana karata za zungu kalala wapi. Wajinga tu ndio wataamini kuna ushirikiano wa kweli baina ya Chadema na CUF kwa sababu walisha jaribu miaka ya nyuma ikashindikana na mkatoleana matusi mazito mazito ya nguoni leo mje kweli kuwa maraifiki kwa sababu ya Insurance na Mirathi!.

Hayo ya kina Kitila kusema kweli mimi sikuyafuatilia kwa ukaribu isipokuwa nilichosoma ni kwamba Mwenyekiti wa ACT alitumia tena kamati kuu kumfukuza Mwigamba pasipo kikao cha baraza kuu ambalo bado liiikuwa halijapatikana. Ugonvi baina ya Mwenyekiti na Mwigamba kuhusiana na uongozi wa ACT siujui wala haikuwa hoja kwangu kwa sababu sizijui kanuni za ACT na hata Kitila alipoingilia ugonvi huo sikuweza kufuatilia.

Na nasema hivi kwa sababu Hata Kafulila alipofukuzwa Chadema Zitto aliigilia kumtetea Kafulila nami sikufuatilia hoja ile kwa sababu sikuwa nimezisoma Kanuni za Chadema ila nilipinga kufukuzwa kwake Uanachama na kusema Sioni haki yoyote ya chama kufukuza wanachama wake kwa sababu uanachma wa Kisiasa ni IMANI ya kiitikadi ambayo huwezi kumvua mtu. Ila chama kinaweza tu kumwondoa mtu madarakani na wasimpe nafasi ya kujitolea ama kuajiliwa ndani ya chama unless kuna uhakika wa kwamba mwanachama huyo ni mwanachama wa Imani nyingine. Labda niseme Uanachama wa chama cha siasa ni sawa na Uraia wa nchi huwezi mvua mtu Utanzania kwa makosa yoyote isipokuwa tu pale itabainika ana uraia wa nchi nyingine. Mtamfunga jela na hata kumnyonga lakini rais hawezi kumvua mtu uraia kwa sababu tu anakisiwa kuwa mhaini.

Lakini maajabu yetu basi ni kwamba kuna watu wana kadi za CCM, Chadema NCCR na haitazamwi kama ni Uhaini wa chama isipokuwa yule anayepinga mwenendo wa baadhi ya viongozi wa chama ndiye mchawi na hatakiwi maana kwa mila na desturi zetu hakuna mtu mbaya kama mchawi maana ina elimu ya kusadikika, vitu tusivyovijua na ndio maana huzungumzia matukio yaani - The aftermarth!. Tunauogopa UCHAWI kuliko kila kitu na ndio maana wachawi wanapata nguvu ya ajabu katika siasa na maisha yetu. Tunaishi maisha ya KUSADIKIKA...
 
Inaendelea…
Kwanza, niwashukuru wachangiaji hapojuu. King Suleiman ame ‘pre-empty' maudhui ya bandiko hili.

Tutaeleza kidogo kushadidia mchango wake, tunamshukuru

ZITTO NA PUBLICITY
Ilifahamika kesi ni kuvutamuda, na kufanikisha hilo imekwisha kabla ya kesi za wabunge wengine kukidhi haja ya ACT

Baada ya kufanikiwa ghiliba, Zitto akaanza uenezi (publicity) kwa vyombo vya habari rasmi na vya kijamii, lengo ni kuandaa mazingira aliyotaka.

Kwa bahati mbayaChadema wakaingia katika anga alizotaka.

CDM hawakupaswa kuzungumzia kesi, walishatoa maamuzi wanayodha ni nisahihi

Aliyekwenda kutafuta haki ni zitto,jukumu la kueleza matokeo ya kesi ni lake. Hilo nikosa la kisiasa lililompa Zitto publicity
Publicity ni kuwaandaa wafuasi wake (kundi la kwanza, bandiko 151) kumfuata

Mgogoro unamatokeo haya

UPANDE WA ZITO
Atajifunza heshima na ukuu katika taasisi,kwamba umaarufu una mipaka

Itamfunza unyenyekevu na namna ya kuishi katika jamii akiwa na umaarufu

Itamuondolea ulimbukeni na kumfungua katika siasa za weledi.litamsaidia kubadilika kama atataka

Kwa upande hasi, Zitto amepoteza public trust. Tukio limeonyesha upande uisojulikana na sura ya pili .

Miongoni mwa wana siasa, hataaminika,jambo litakalomsumbua miaka mingi ijayo

CHADEMA

Upande chanya: Sakata si la kwanza, yapo yaliyotangulia kama kuwaondoa madiwani n.k.

Kwa maneno mengine, CDM wanaweza kujinasibu ikifika wakati wa maamuzi, wana uwezo wa kuchukua maamuzi magumu

Pili, kwamba ni taasisi inayojijenga kama taasisi na si watu

Tunakumbuka katibu mkuu Amani Kaborou kuelekea CCM, Shimwele Chitambaa kuhujumu uchaguzi Mbeya, Kafululia na wenzake kuondoka n.k.

Kwamba, licha ya umaarufu wa watu bado CDM imebaki kama taasisi

Upande hasi: imeonyesha udhaifu wa kushughulikia matatizo kwa wakati muafaka

Huu ni udhaifu mkubwa na pia wasivyoweza kusoma mazingira mbele ya wakati.

Tumeona kosa la publicity iliyofanywa baada ya kesi kumalizwa

aliyekwenda kutafuta haki ni zitto,jukumu la kueleza matokeo ya kesi ni lake.
Hilo nikosa la kisiasa lililompa Zitto publicity

Publicity ni kuwaandaa wafuasi wake (kundi la kwanza, bandiko 151) kumfuata

Inaendelea…
 
NINI KITATOKEA?

Katika miezi miwili hadi mitatu kutakuwa na hama kwa wanachama

Kundi la wanachama wanaoamini katika Zitto litamfuata. Hakuna namna ya kulizuia kwasababu linaamini mtu na si sera wala itikadi.

Kundi la kwanza, wapo wenye masilahi kwa uwepo wa Zitto,wanaoamini tu kkt Zitto

Kundi la pili lisilo na imani na Zitto litabaki na msimamo huo.

Kundi la tatu lililo njia panda likimuelewa na kutomwelewa litabaki hivyo likiamini katika sera.
Kama kutakuwepo na kuhama, itatokea kwasababu wapo wanaoamini katika sera

Katika hama hama kutakuwa na papa na dagaa. Papa ni pamoja na viongozi waliopo CDM wakiwemo wabunge.

Baadhi wataangalia masilahi zaidi kuliko sera za vyama vya sasa au baadaye

KISAIKOLOJIA
CDM wajiandae kwa hama hama. Kwamba,wanaweza kuhimili mikiki,itategemea vitu viwili, na hapa tuseme ‘yes or no

Yes, Kama watafuata misingi na kusimama katika kuamini wanachokitenda.
Ndivyo walivyovuka wakati wa Aman Kaborou, madiwani n.k.
No, Wakipoteza focus na kuingia katika malumbano.

Ni wazi ACT hawana la kupoteza hivyo mchezo wowote mchafu kwao una manufaa hasa publicity

FAIDA NA HASARA ZA HAMA HAMA YA WANACHAMA
Hasara inayotarajiwa ni misuko suko itakayotokana na hama hama katika baadhi ya maeneo.

Kama CDM hawatajianda kisaikolojia hilo litaawthiri

Watapoteza focus ya mambo ya kitaifa na kujikuta wakilumbana na kusaidia uenezi

Faida watakayoipata ni kubaki na wanachama ‘committed' wa sera na itikadi

CDM watakuwa wamejenga nidhamu ya kudumu. Tunakumbuka nidhamu ilivyoshuka wakati wa ''ACT-CDM''

Hama hama itakuwa chujio la wanaosimama na CDM au waliopo kwa masilahi

Wale wanaosimama na sera au wanaosimama na mtu(personality)

Inaendelea..
 
Inaendelea

KOSA

Itakuwa ni kosa CDM kuzuia wanachama kwa njia zozote zile iwe kuhonga nafasi au kuahidi nafasi na mafao.

Wanachotakiwa ni kuacha wanachama waamue kwenda watakako.

Alipoondoka Aman Kaborou, ‘alizaliwa' Zitto na kuwa mkubwa zaidi ya Aman

TAIFA
Taifa na vyama vya siasa vimepata kinachoitwa ‘benchmarks' kwamba ni standard na kioo.

Kumbe inawezekana, watu wakiamua Tunajua kuwa CUF wanaweza, NCCR wanaweza, TPP wanaweza wakiamua kumaliza migogoro
Kwamba, hatuwezi kuimba kuvua gamba na mafisadi, kuna nyakati hatua zichukuliwe ili kujenga utamaduni wa taifa wa kuwajibika,kuwajibishan na kuwajibishwa

Sakata linaonyesha wananchi picha halisi ya viongozi katika nyakati za misuko suko

Kama CDM itakufa kutokana na kuondoka Zitto, litakuwa jambo jema kwa taifa.

Hatuwezi kuwa na vyama vya siasa kama watu na ni haki vinavyosimama kama watu vifutike.

Tutafarijika vikifutika kwasababu hatuhitaji personality tunahitaji institution

Tuliona NCCR na CUF,tunasubiri kama historia itajirudia tena.

Historia inaweza kujirudia kwa njia mbili

Kwanza, kufutika na kudumaa kwa CDM kama ilivyokuwa NCCR /CUF

Pili, kuhimili misuko suko kama ilivyowahi kutokea kwa CDM huko nyuma

Hili ni kipimo kizuri kama kweli tuna taasisi zinazoweza kuwa mbadala.

Ni kioo cha aina na nguvu ya wapinzani.

Na ni picha nzuri ya kuamsha wananchi dhidi ya matapeli wa kisiasa wanaovaa ngozi za kondoo ndani wakiwa mbwa mwitu!

Tusemezane
 
Nguruvi3,

Unajua tofauti yangu na watu wengi humu JF ni kwamba wao walitazama zaidi upande wa Zitto na ACT wakati mimi nilikuwa naitazama Chadema kwa mapenzi ya dhati maana niliwashauri wao kutokurupuka, niliwashauri yenye kuuma na chachu kumezwa lakini ilikuwa lazima yasemwe na sio kuhofia. Nakumbuka Ushauri wa kwanza ulokuwa ktk swala la Zitto ni kwamba swala hili ni la ndani lilitakiwa kuzungumzwa ndani na sio public, wao wakaona sifa kuliweka nje bayana ili watu wamchukie Zitto, WHY sikuelewa.

Wakayaweka makosa yake mbele ya kadamnasi kwa tuhuma za waraka ambao pia sikuona ubaya wake zaidi ya kwamba Kina Kitila walitaka kubadilisha uongozi toka mikononi mwa Mbowe na Dr.Slaa jambo ambalo lilihitaji kura za wajumbe wa baraza kuu. Sikuona mafanikio yake nikashauri maadam imeshajulikana na wanatafuta wajumbe wa kuwaunga mkono basi wasubiri hadi uchaguzi mkuu maana nina hakika Zitto asingeweza kuchukua uongozi wa Chadema kupitia sanduku la Kura. Mara tuhuma hizo zimegeuzwa na kuwa Uhaini kwa kuwasiliana na TISS ambayo inatumiwa na CCM. Zitto akawa sasa ni kibaraka wa CCM sio tena alotaka kupindua Chama.

Haya tukaambiwa walitaka kukipindua Chama, jamani kweli mtu anaweza kupindua chama? kivipi nikauliza sikuambiwa ila mpango wa waraka uliwatisha viongozi wa kamati kuu ambao sikuona sababu ya wao kuogopa ikiwa wajumbe wa baraza kuu na wanachama ndio waamuzi. Kama hawawataki watawaondoa kweli lakini kinyume cha hapo ni porojo tupu mapinduzi hayawezekani. Kamati kuu ikafanya mikutano ya siri pasipo baraza kuu kujulishwa, kisha wakaamua kutoa hukumu ya kuwatimua kina Kitila sii tu uongozi bali hata Uanachama. Tukasema tena haya ni makosa maana kanuni inasema wazi kiongozi yeyote alochaguliwa kushika madaraka ya juu ya kamati kuu ataondolewa tu katika uongozi wake na baraza kuu na zaidi ya hapo huwezi kumfukuza mtu uanachama maana chama ni wanachama na kwa kosa gani?. Madai yao yakawa hata kama ingeenda bazara kuu wangetimuliwa! Alaa sasa mliopoga nini kupeleka baraza kuu kulingana na kanuni!

Haya, Kitila na Zitto wakataka ku appeal maamuzi hayo kwa kuitaka ofisi ya Chadema asajili madai yao ili yafanyiwe maamuzi na baraza kuu, ofisi ya katibu mkuu wakakataa kuyapokea, tukasema tena ni makosa kufanya hivyo, Dr.Slaa kwa mdomo wake akazuia swala la Zitto kuongelewa na mwanachama yoyote!, tukabakia kushangaa. Tukasema huu ni Udikteta lakini hatukusikilizwa kumbe wakati wote walikuwa wakichonga Mpini wamkabidhi Zitto wakitegemea wanalolijua litokeee utafikiri mwezi mwandamo wa mfungo! haya mfungo umefika mnaanza kutafuta nani asiyefunga.

Zitto alipokwenda mahakamani watu wakasema ni mbunge kwa tiketi ya mahakama sii MwanaChadema maana kisha temwa zamani, lakini tena tunakuja ambiwa Zitto kajifukuzisha alipokwenda mahakamani. Flipflop hizi zikatushinda kuelewa maana tuliambiwa kafukuzwa Uongozi na Uanachama sasa kwenda mahakamani kajifukuzisha. Yaani ni baada ya Zitto kwenda mahakamani ndipo kanuni zikatazamwa. Muda wote huu mambo yote waloyashutumu kina Kitila kuhusu Uongozi wa Chadema yakawa yakionekana wazi zaidi. Operation Sangara na nyinginezo zilikufa zote mwaka 2014 hapakuwepo na jipya lolote, chama kikajihusisha zaidi na uandikaji wa Katiba mpya.

Kitu ambacho Chadema haikuzingatia ni kwamba CCM walifanya makusudi kuwachagua viongozi chama cha Chadema kuwa sehemu ya Katiba Mpya wakati chamani kumebakia kutupu. BAVICHA walishindwa kuendeleza uongozi wa chama kwa sababu hawakusundwa kiitikadi kuendeleza yalopatikana toka 2008 wengi wao walijiunga baada ya umaarufu wa chama. Kisha ni vijana walochaguliwa kuongoza BAVICHA baada ya mafanikio makubwa lakini sii kuongoza CHADEMA ktk nafasi za makao makuu pindi viongozi wake watakapokuwa na maswahiba mengineyo muhimu ya Kitaifa. Chama kikaanza kudorora na kuondolewa katika kazi kubwa waloweza kuifanya kwa kipindi kikubwa kufikia mwaka 2010 na muendelezo wake.

Sasa tuangalie viongozi wa Chadema walifikia kufanya nini..Kwanza kabisa uandishi wa Katiba mpya ulivunja sheria kubwa ya NCHI maana katiba huandikwa baada ya kuwepo NCHI HURU. Viongozi wa Upinzani wakataka Katiba Mpya ivunje NCHI kwanza katika uandishi huo jambo ambalo haliwezekani na ni kosa na Uhaini kuua nchi ndani ya Katiba Mpya. Hivyo majadiliano yote ya Kuunda serikali 3 yalikuwa kinyume cha sio tu madai ya wananchi bali hata Uhalali wa Taifa letu. Pasipo kutumia katiba Mpya CCM na CUF waliweza kuzaa nchi ya Zanzibar na kuipa rais wake nje ya yule wa muungano na asiwajibike na serikali ya muungano, leo Chadema ikashawishika na CUF tena kuendeleza madai ya CUF ambayo hayakukubalika na CCM kutenganisha nchi hizi mbili kwa ujanja ujanja wa kudai Identity ya kila nchi katika nchi zilizoungana na kuunda taifa moja. IDENTITY! yaani kweli nchi zilizoungana zinajali zaidi jina lao kutopotea halafu wanadai wanaupenda Muungano!

Kupitia vikao vya Bunge la Katiba, tuliwasikia wabunge wakihoji hata kuwepo kwa Muungano, kuwepo uhalali wa nchi yetu TANZANIA ati ilitokana na matakwa ya mtu mmoja - Nyerere! wengine wakisema walozoea vya kunyonga vya kuchinja hawaviwezi yaani Nyerere akiwa mmoja wao. Haya ni matusi makubwa mbayo sikutegemea kabisa yanaweza kutoka Chadema chama ambacho kilijijenga kwa kutukuza maamuzi mengi ya Mwalimu Nyerere. Chama ambacho Mbowe mwenyewe aliwahi kutumia mifano mingi ya mwalimu dhidi ya CCM hii hata akapongezwa na wazee na waasisi wa chama kina BUTIKU.

Chadema haikuishia hapo tu, kwa kutumia madai ya Katiba Mpya Chadema ikaungana na chama ambacho wao wenyewe walituambia wananchi kuwa ni CCM B na tukabisha sana hadi pale CUF ilipoweka muafaka na CCM juu nya mustakabali wa nchi yetu. TUKAAMINI na zaidi ya hapo CUF ikanukuliwa wakisema Chadema ilitaka kuipundua CUF kwa kumfuata Lipumba na kumhadaa kinyume cha kanuni za chama chao. Urafiki baina ya Chadema na CUF ukafa kifo cha nyani at crucial period right before Uchaguzi wa mwaka 2010. Leo tunaambiwa Chadema wameunda UKAWA na CUF juu ya mustakabali wa nchi hii kuitaka Tanganyika jambo ambalo CUF kwa miaka mingi wamekuwa wakitaka kujitenga na Tanganyika.

Sasa leo tutazame Chadema imesimama wapi? Msaliti nani haswa baina ya Chadema na Zitto maanake tunatazama mustakabali wa nchi yetu na sio Chadema. Walichosahau viongozi wa Chadema ni kwamba sisi wananchi tunaitazama Tanzania kama ni Taifa moja, na madai ya serikali 3 kwa kushirikiana na wale wanaotaka kuvunja muungano kisha mkasingizia ni utekelezaji mzuri wa mamlaka ya uendeshaji serikali huku kila mmoja akidai Utaifa wake kujulikana ni kuifuta historia ya Tanzania. Kinacho nadiwa hapa ni kutengana na sio kuungana maana tulikwisha ungana na CUF inajulikana kuwa haiutaki Muungano ila Maridhiano (Common in law).

Mnaitaka Tanganyika ambayo haijali kutazama mbele kwamba kuna Wazanzibari 800,000 wanaoishi bara ambao baada ya kuzigawa nchi hizi watapata matatizo ya kuwepo Tanganyika maana mifano inaanza na CUF na WaZanzibar kutaka Watanganyika kuondoka kwao. Kuwepo kwa serikali 3 kutazua mgogoro mkubwa juu ya mipaka na hata kuwepo kwa mafuta ndani ya bahari baina ya nchi hizi mbili maana adui mkubwa wa umaskini ni maskini wenyewe na ardhi au maji ni sababu kubwa ya kuhitilafiana na haina suluhu. Kuwepo kwa serikali 3 kutaondoa Uraia na hata uwajibikaji wa mwananchi wa upande mmoja kulitumikia Taifa upande wa pili na mbegu tosha ya kupandikiza Udini baina yetu. Hii ni asili na mila za mtu mweusi UBAGUZI hutafutiwa sababu ndogo tu ukashamiri na kuwa vita vya wenyewe.

Chadema Imeshapoteza mwelekeo, haishauriki wala haitazami makalio yake! ni Akili ndogo kuongoza akili kubwa.
 
Mkuu Mkandara

Hapo juu umeeleza mambo mengi napengine nimeshindwa kufanya connections

Hata hivyo nimedokoa machache na hapa naomba niyapitie

1. Kuhusu mambo kumalizwa ndani, kuna wakati inafika haiwezekani.

a)Tunakumbuka mgogoro wa Kafulila , Zitto alikuwa the brain behind.
Ilikuwa ni yale yale ya kumwandalia mazingira mema kwa njia za mkato, zisizo na busara na zilizojaa ujana kama si utoto

b)Utakumbuka timbwili la Juliana, the brain hehind ni Zitto.hoja ilikuwa uchaguzi wao wa vijana ambapo Zitto alikuwa anapanga safu

c)Utakumbuka, sakata la masalia na chanjo kwenye makalio ya vijana grafuate ' the brain behind ni Zitto''

d)Utakumbuka baraza kuu lilitoa mazimio pale Diamond, Mbowe akagfinyanga finyanga majadiliano katika kumlinda Zitto

e)Utakumbuka wakati chama kina mnadi mgombea, ZZ anatangaza 'urais' akieleza umma anayenadiwa ni ‘magumashi' kwa lugha yao

f)Unakumbuka mkakati wa Waraka, na maudhui yaliyomo yakiwemo matusi.

Waraka upo tuulete hapa utuonyeshe chembe ya busara, si kwa maudhui bali kulingana na ‘uwezo wa brain behind' waraka

g)Kibaya zaidi, zitto na washirika, vikao vikaendelea vya ndani wao wapo busy kutoa habari JF

h)Waraka uliwekwa hadharani kwasababu ‘mkulima masikini' mwigamba, mshauri wa Zitto alikuwa anaweka vitu hadharani.
Kulikuwa na siri gani ya kikao cha ndani?

Katika mazingira hayo, ulihitaji avumiliwe kwa kiasi gani na kwasababu zipi.

2. Tutoke nje ya mada tuzungumzie machache kulingana na hoja zako

Huko nyuma kulikuwa na ‘UPAKA' Ukafa . Wapinzani walijifunza migogoro haisaidii kukabiliana na janimiza kubwa , the CCM.

Kutofautiana kisiasa ni jambo la kawaida katika wakati ambapo kila njia inatumika kukabiliana na Escrow-CCM au Richmond CCM n.k.

Zitto Kabwe aliandika kuhusu serikali 3 katika gazeti. Chama chake hakikuwa na msimamo wa muundo wa muungano.

Nipo katika rekodi za JF nikimsifia na kumtetea Zutto kuwa alitumia haki yake ya mawazo huru.

Hata aliposumamngwa nilisiama na kusema Zitto hana kosa kueleza msimamo wa maono yake.

Nikasema kuwa hakufanya siri bali hadharani. Nikaendelea, tuelezwe Chadema inasimama wapi kuhusu suala la muungano

Kwa mantiki hiyo, ushawishi wa Chadema kuwa na muundo wa S3 ni zao la ushawishi wa Zitto.

Huwezi kuwaluamu kwa kuchukua mawazo ya aliyekuwa kiongozi wao tena akiwa na maono tofauti.

Huwezi kumtenga Zitto na msimamo wa Chadema kuhusu muundo wa muungano

3. Muungano

Ninashanga unapowalaani Watanganyika. Malamiko ya muungano yanatoka kwa wazanzibar kule kwao na hao 800,000 unaosema

Wanataka mamlaka kamili na hawataki muungano kwasababu unawaonya. Wanataka kuelewa ya muungano yapi si ya muungano.

Huwezi kutenga malalamiko yao na muundo wa muungano.

Wazanzibar wanastahili kupewa wanchotaka si wewe kusimama na kuwatetea ikiwa wao hawautaki Utanzania, ni wazanzbar

Tanganyika wamechoka.Unaelewa 800,00 wanaishi na kutegemea Tanganyika, tunategemea wawe sehemu ya utulivu na amani

Hakika wazanzibar wamekuwa tatizo na hilo limeachoshwa Watannganyika.

Watanganyika wanataka kushughulikia umasikini, si jinsi ya kusihi na Wazanzibar wasio na athari katika maisha yao, I mean, useless

S3 zitawasaidia kuwapa heshima. Kwa mwendo uliopo, mbele ya safari watakuwa wamepoteza heshima yao

Tumeona madai yao hayana ukweli ni upuuzi tu na uelewa finyu

Hivyo wakiwa ndani ya S2 watakuwa Raia wa daraja la pili, kwa maana ni ''kundi la viti maalumu la wznz' kama akina mama

Hivyo wana choice, kuwa washirika wa muungano(S3) au kujibanza mgongoni wakiwa na adabu na heshima
 
Nguruvi3,

Mkuu naomba turudi nyuma taratibu moja baada ya jingine..

1. KAFULILA. Nikuulize alifanya kosa gani?\

na Ramadhan Semtawa na Fidelis Butahe

HATIMAYE yule bundi wa kisiasa ambaye alikuwa akiinyemelea Chadema, sasa ametua rasmi baada ya chama hicho kutangaza kuwatimua maafisa waandamizi wawili ambao ni washirika wakubwa wa naibu katibu mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe, ambaye ameeleza bayana kutofautiana na maamuzi hayo. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa alitangaza jana kuwa kwa kutumia mamlaka yake amewavua nyadhifa zao David Kafulila, ambaye alikuwa ofisa habari wa chama hicho, na Danda Juju, ambaye alikuwa anahusika na mambo ya bunge.

"Tena andika mwandishi wala usiogope ni kwamba, leo (jana) kulikuwa na kikao, nimekiongoza mwenyewe na maamuzi nimeyatoa mwenyewe..., tumetengua uteuzi wao. Sasa ni wanachama wa kawaida," alisema Dk Slaa

.Uamuzi huo ambao unaonekana utagusa majeraha ya uchaguzi mkuu wa viongozi wa chama hicho mwezi Septemba, umekuja siku chache baada ya kuvuja kwa taarifa za mkutano wa siri kati ya Mwenyekiti Freeman Mbowe na baadhi ya viongozi, akiwemo Dk Slaa, ambao wanadaiwa kujadili nidhamu ya wanachama hao wawili pamoja na mama mzazi wa Zitto, Shida Salum.

Mbowe alikanusha kuwepo mkutano wenye ajenda hiyo ya kuwatimua wanachama hao akisema taarifa hizo ni "za kizushi", huku Dk Slaa akisema kuwa hakuna haja ya kuitisha kikao ili kuwashughulikia watendaji hao na kuwafananisha na sisimizi katika chama. Jana Dk Slaa alisema kuwa ametengua ajira za watu hao wawili kwa maslahi ya chama na kuongeza:" Tunataka kusafisha chama..., maana tukiacha hali hii tunaweza kuingia Ikulu na mambo ya ajabu."

Kwa mujibu wa Dk Slaa, chama hicho kinaongozwa kwa taratibu na kwamba hakiongozwi na majungu hivyo anayekiuka lazima ashughulikiwe."Tuliwapa muda wa kutosha wa kujitetea," alisema mbunge huyo wa Karatu ambaye anatajwa kuwa atawania urais kwa tiketi ya Chadema. Vyanzo vya habari vilidokeza kwamba wanachama hao walihojiwa kwa takriban saa tano katika mkutano uliofanyika makao makuu Kinondoni, Dar es Salaam kabla ya uamuzi wa kuwatimua.

Alipoulizwa sababu za kuwatimua, Dk Slaa alijibu: "Nimekwambia nimetumia mamlaka yangu, usiniulize vigezo au sababu."Kwani Rais Kikwete (Jakaya) akitengua ajira za watu mbona hamuulizi katumia vigezo gani... na mimi nina mamlaka ya kufanya hivyo bila kuulizwa."

Dk Slaa alifafanua kwamba, Chadema ni chama ambacho kina malengo hivyo lazima kijisafishe kwa kuweka misingi imara ya uongozi na si watu kufanya mambo bila taratibu. Katibu huyo wa Chadema alisema haoni kama uamuzi huo unaweza kukiathiri chama hadi kikagawanyika, akisisitiza:"Nasema hakuna mpasuko wala kambi ndani ya Chadema mimi sioni mpasuko wowote.
"Lakini, pia ni bora mpasuko kuliko chama kufa, tukiachia mambo haya yakiendelea ya watu kujifanyia mambo bila taratibu, chama kitakufa... ninyi mnataka kife au?"\

Dk Slaa pia alikanusha kuwa uamuzi huo ni kisasi cha mambo yaliyojitokeza katika kipindi cha kuelekea uchaguzi wa viongozi wa Chadema ambao ulitawaliwa na vurugu huku matokeo yakibatilishwa kwa kanuni kutofuatwa au rafu. Lakini Zitto, ambaye kwa sasa yuko nje ya nchi, alionekana kutofurahishwa na maamuzi hayo. Katika ujumbe alioutuma kwa gazeti la Mwananchi jana, mbunge huyo wa Kigoma Mashariki alisema: "Ninasikitika kuwa tunachukua maamuzi kama haya kipindi hiki ambacho nchi inahitaji chama imara cha upinzani.

"Kafulila ni mgombea mtarajiwa wa ubunge katika Jimbo la Kigoma Kusini ambalo CCM wamefanya vibaya katika uchaguzi wa serikali za mitaa kuliko majimbo yote nchini. Uamuzi huu unaweza kuwashtua sana wanachama wetu Kigoma Kusini na mkoa wa Kigoma kwa ujumla."

Zitto alikumbusha kuwa Kafulila aligombea uenyekiti wa jumuiya ya vijana ya Chadema na akashinda, lakini uchaguzi ulivurugwa na kufutwa na hivyo utarudiwa na hivyo uamuzi wa kumfukuza Kafulila ni dalili za wazi za watu waliofuta uchaguzi huo kuleta vurugu kwenye chama kwani wanachama hawatakubali uonevu.

"Kwangu mimi Kafulila ni kijana mahiri mwenye kukipenda chama chetu na ndio maana niliamua kumgroom (kumkuza) ili aje kuwa mgombea ubunge na baadaye mbunge katika Jimbo la Kigoma Kusini.

Na baada ya kufukuzwa Kafulila mwaka 2009 uchaguzi ukaahirishwa hadi Ulofuata ambapo Heche alishinda na nanukuu maelezo ya ya Zitto haya hapa. Watu wakaivamia mada kwa sababu Zitto alikuwa akimpendekeza Kafulila toka 2009 Na hata ukisoma mada hii Zitto hakutaja nani kafanya nini ila uchunguzi ufanyike, huyu ni Naibu katibu wa chama lakini tazama walivyompururula! Isome mada nzima. Historia tunaikumbuka mkuu.

UKisha twende la Pili...
 
Mkuu Mkandara

Kwa bandiko lako 173, umefanikiwa kuweka maelezo ya bandikolangu 172 vema sana

Niliporodhesha matukio nilimaanisha kitu kimoja, hakuna mzozo uliowahi kutokea Chadema ambao Zitto hakushiriki au kutajwa. That's my main point na umeionyesha

Pia umeomyesha kama nilivyosema kuwa migogoro ya vijana the brain behind ni huyu jamaa, ama sivyo?

Pili, Kafulila sina uhakika kama alifukuzwa kama ulivyosema.
Ninachojua alivuliwa nyadhifa zake na kubaki mwanachama kama gazeti lilivyosema
 
Mkuu @Mkandara
Kwa bandiko lako 173, umefanikiwa kuweka maelezo ya bandikolangu 172 vema sana
Niliporodhesha matukio nilimaanisha kitu kimoja, hakuna mzozouliowahi kutokea Chadema ambao Zitto hakushiriki au kutajwa. That's my mainpoint na umeionyesha
Pia umeomyesha kama nilivyosema kuwa migogoro ya vijanakuanzia wa Kafulila hadi wa Juliana Shonzo the brain behind ni huyu jamaa, amasivyo?
Pili, Kafulila sina uhakika kama alifukuzwa kama ulivyosema.
Ninachojua alivuliwa nyadhifa zake na kubaki mwanachama kamagazeti lilivyosema. Alijitoa mwenyewe kama nipo sahihi
Mkuu hujajibu swali langu hata kidogo maana nimekuuliza sababu ya Kafulila kufukuzwa na hata maelezo hayo hapo juu Dr.Slaa kasema kwa jeuri katumia wadhifa wake kuwatimua na kutoa mfano wa Kikwete akitengua ajira za watu mbona haulizwi sababu. Lugha hiyo umeisoma mwenyewe sasa ili tushabikie maamuzi hayo nataka kujua wewe ulielewa Kafulila alifanya nini hadi akatimuliwa nawe ukaunga mkono. Usianzishe vijisababu vya kutafuta makosa ya uandishi wangu bali elewa tunatafuta makosa ya mtu mmoja mmoja na Zitto kahusikaje dhidi ya wengine wenye haki.

Zitto kuwa na pingamizi katika maamuzi ya wengineo ndio demokrasia ya kichama inavyotakiwa na utashindwa kwa kura za wengi wape, je ilifanyika ktk kila hatua ambayo Zitto alipingana nao? maana watu wote hamuwezi kufikiria sawa katika mambo ambayo sio ya Kiitikadi ya Kisera. Je ikitokea kupingana ni mfumo gani utumiwe kuondoa malumbano baina ya viongozi -Kufukuzana?. Heche alikuwa na wapambe wake kina Mnyika toka 2009 lakini hawazungumziwi kuathiri uchaguzi ulofuata. Je, hili halikuwa kundi jingine? Na kwa nini tusiseme migogoro yote Chadema imeanzia BAVICHA na sio kutoka Chadema makao makuu.
 
Mkandara;12241244]Mkuu hujajibu swali langu hata kidogo maana nimekuuliza sababu ya Kafulila kufukuzwa na hata maelezo hayo hapo juu Dr.Slaa kasema kwa jeuri katumia wadhifa wake kuwatimua na kutoa mfano wa Kikwete akitengua ajira za watu mbona haulizwi sababu.
Mkuu Mu-sir naomba ulete kile kipande cha gazeti kilichokuwa na maelezo ya Mwigamba. M

Mwigamba katika gazeti aliandika kuwa Zitto ni rafiki yake na walikuwa na mawasiliano ya karibu.

Mwigamba alisema haya '' ...Katibu mkuu ana haki ya kuchukua hatua alizochukua, nasikitika ulimpinga hadharani. Nakusikitikia''

Maneno hayo kayasema Mwigamba, mwenyekiti wa CDM wakati huo, na mshirika wa Zitto katika Waraka na sasa ni katibu mkuu wa ACT ambako Zitto ni mwanachama
Nataka kujua wewe ulielewa Kafulila alifanya nini hadi akatimuliwa nawe ukaunga mkono. Usianzishe vijisababu vya kutafuta makosa ya uandishi wangu bali elewa tunatafuta makosa ya mtu mmoja mmoja na Zitto kahusikaje dhidi ya wengine wenye haki
Ukisoma hoja zangu katika bandiko hili, hakuna mahali nimeeleza sababu za mitafaruku kuwa sahihi au la. Kama

Nimekuwa naeleza mitafaruku kwa ujumla wake. Ukisoma bandiko 172 nimorodhesha matukio yaliyotokea zitto akishiriki au akitajwa.
Ndio maana nilikuuliza swali moja, ni mtafaruku gani wa CDM ambao Zitto hana mkono?

Napenda uelewe, sijachukua upande na wala sijasema Kafulila alikosea.

Nilichosema ni kuwa katika matukio ya CDM Zitto ni ima mhusika au ametajwa. Hapo ndipo ilipo main point.

Sitaingia katika kujadili mambo ya ndani, ninajadili hoja moja tu tena nikiuliza, ni mgogoro gani wa Chadema ambao Zitto hajatajwa

Nitakupa mfano, katika sakata la masalia, Zitto ametajwa kuwachukua vijana kwenda kutandikwa chale za matakoni( dah ashakum)

Sijasema hatua hiyo ya Zitto ni nzuri au mbaya, ninachosema Zitto alishiriki kuwapelekavijana kutengenezwa ''nyungu'' zao kisiasa

Endapo chale chini ya kiuno kwa nyuma inafanya kazi au la, hilo si jukumu langu.

Ninachosema motiisha iliyotolewa na mheshimiwa ndicho kilikuwa kiwe kichochoe cha mtafaruku

Hivyo naongelea motisha na ushiriki wake, siongelei sababu au matokeo ya kutandikwa chale uti wa mgongo unapoishia.

Narudia, sina haja ya kujua mpango wa chale chini ya uti wa mgongo, ninachosema jina la Zitto lililkuwepo kama mshiriki

Zitto kuwa na pingamizi katika maamuzi ya wengineo ndio demokrasia ya kichama inavyotakiwa na utashindwa kwa kura za wengi wape, je ilifanyika ktk kila hatua ambayo Zitto alipingana nao? maana watu wote hamuwezi kufikiria sawa katika mambo ambayo sio ya Kiitikadi ya Kisera. Je ikitokea kupingana ni mfumo gani utumiwe kuondoa malumbano baina ya viongozi -Kufukuzana?. Heche alikuwa na wapambe wake kina Mnyika toka 2009 lakini hawazungumziwi kuathiri uchaguzi ulofuata. Je, hili halikuwa kundi jingine? Na kwa nini tusiseme migogoro yote Chadema imeanzia BAVICHA na sio kutoka Chadema makao makuu
Again, sina sababu na wala siingi katika details za nini kimefanyika kwasababu ni nje ya muktadha wa bandiko.

Ninachoweza kusema ni kuwa katika hoja yako hapo juu, bado unazidi kuunga mkono hoja yangu kuwa Zitto ametajwa, the bottom line ameshiriki katika mambo mengi yaliyokuwa na dhamira ovu.

Ushahidi ni wanautoa 'fresh graduate' waliolimwa chale!

Kwa haja ya bandiko lililopo, hakuna mgogoro wa Chadema ambao Zitto hana ushiriki
 
Mkuu Invisible

Kwa vile Mkandara ameweka kipande cha taarifa za magazeti akitumia haki yake halali , na kwa kuwa tunahitaji mjadala endelevu, ningekuomba tulitendee haki jamvi kama ilivyo kawaida kwa kupata maneno yaliyoandikwa kwa ushahidi na wahusika bila kuweka hisia au nukuu zetu.

Ni kwa muktadha huo, naomba uturuhusu tuweke nukuu za walioko katika mjadala ili kuwatendea haki na sisi kujitendea haki ikiwa ni pamoja na jamvi kwa ujumla

Nina nukuu za magazeti, na hivyo basi naomba idhini yako niiweke hapa

Ninaomba idhni kwa kutambua kuwa ushauri wako ni muhimu katika mazingira yaliyojitokeza siku za karibuni

Naomba ushauri
 
Mkuu Nguruvi3, umeacha Funzo sahihi ambalo kama wewe ulivyolisahau, si Watanzania tu , bali ni Waafrika kwa ujumla wake. NI KUDHIHIRIKA KWA 'IRRELEVANCE OF DEMOCRACY' kwa Mtu mweusi.

Nitaendelea kusema, Kidemokrasia si Zitto wala CDM waliokuwa sahihi. Pande zote zilishakiuka misingi ya Demokrasia, si kwa bahati mbaya bali ni KUTOKUWA KWAKE NA MANTIKI.
Tunapokosea ni kutazama Ukiukaji wa upande fulani ni 'MAKOSA/MAPUNGUFU' yanayotakiwa kurekebishwa, wakati tunatazama ukiukwaji wa ule upande wa pili kama 'UHALIFU/CRIME' na kuushitakia kwa Umma. It is unfair!

Kwangu linapokuja suala la kukiuka kiapo cha Demokrasia, hakuwezi kuwa kosa hadi pale nitakapotambua DHATI yako, na si suala la Uadilifu bali DHATI.
Cha kusikitisha huwa tunapima dhati za watu kwa HISIA zetu, Uadilifu na Imani tu, na kusahau kuwa Dhati hupimwa na Relevance ya mazingira.
Kinachoendelea ni kupotea kwa Watanzania kwa vioja na vituko visivyoisha.... Asubuhi tutasikia, Sisi ACT ni wanademokrasia na wawazi, jioni wanapgana vijembe na kufukuzana. Asubuhi utasikia Zitto ndio muanzilishi wa ACT, jioni utasikia Zitto kama foreigner kawatimua waanzilishi wa ACT. Asubuhi utasikia sisi ni misingi, na jioni utasikia misingi ni batili. Ni porojo kwa kwenda mbele. Yote ni KUDHIHIRIKA KUSHINDWA KWA DEMOKRASIA. Watz hatupaswi kuzungushwa hivi, tulipaswa ku-focus something. Huu ni ULEVI MZITO.
Tusipochukua hatua wajukuu wetu watakuwa wanapiga the same porojo.
Mkuu Nguruvi3, Maisha ni HESABU. Kamwe hakuna muujiza kwa ustawi wa Taifa. Maendeleo ni HESABU, si bahati na sibu.
Anaita sasa!
Anaita sasa!
 
Last edited by a moderator:
Jamani sisi binadamu ni watu wa ajabu sana, Kila siku tunalalamika kuwa serikali haichukui hatua pindi pale viongozi wanapofanya makosa hali sheria ziko wazi, Leo hii chama kinamchukulia hatua mtu aliyefanya makosa tena sio mara moja, lakini bado watu wanalalamika na kusema kwanini hawakukaa chini wakazungumza yakaisha..

Swali langu ni kuwa kama hivyo sheria na adhabu tunanazozitunga ili zituongoze ni za nini? Je hizi sheria tunawatungia wale wasio na uwezo, wale wasio na wafuasi, au wale wasio na ushawishi wowote katika jamii?..

Tukae tusema ukweli matendo ya Zitto yalijulikana tangu mwaka 2008 enzi za kutembea na barua ya kujiudhuru mfukoni. Zitto alifanya siasa za gizani mchana alikuwa ni naibu katibu mkuu na usiku alikuwa adui no.1 wa chama,

Nani hasiyejua ID ya TUNTEMEKE, nani hasiyejua matusi ya akina Juliana na masalia kwa jumla, nani amesahau uchonganishi kati ya Mbowe na Dr. Slaa, hivi ndugu zangu tumesahau siri za chama zilikuwa zinaletwa humu JF kila kukicha, kama tumesahau hilo tumesahau pia na swala la Lwakatare? haya yote yamefanyika tumeyashuhudia na ushaidi huko humu JF na aliyekuwa nyuma ya hayo yote alikuwa kijana mjenga hoja, mpenda media Zitto..

Nakubalina na wanaosema kuwa Chadema kilizembea sana katika swala zima la nidhamu kwa Zitto labda kama kingemkanya mapema, na kumrudiisha katika mstari basi hayo yanayotokea leo yasingetokea..

Ilifikia kipindi nikasema Chadema wanamuogopa Zitto, kwani alifanya mambo mengi ya wazi ila waliosurubiiwa walikuwa wengine. Je tumesahau adhabu ya akina Juliana, madiwani w a Arusha,Kafulila,madiwani wa Mwanza na nk. aliyekuwa nyuma ya haya yote kuwa ni Zitto? Zitto aliota ndevu akwa mfalme katika chama...

Na mgogoro ulipokuwa umefika kulikuwa hakuna namna ambavyo Zitto angeweza kufanya kazi na viongozi wenzake maana uaminifu ulikuwa haupo tena. (kumbuka sakata la mabomu ya Arusha kuna wanaosema alihusika)
Na kwa namna hiyo huamuzi wa Zitto kwenda kwenye chama chake ulikuwa ni wa lazima kwani kulikuwa hakuna jinsi.

Kuna wanaosema Zitto ni mzalendo alikataa posho.. Jamani hata Zitto mwenyewe alisha wahi sema "Husiwaamini wanasiasa" Zitto alikataa posho ya elf 80 ila akakubali posho ya vikao vya PAC ya shilingi laki 4 kwa siku (ushaidi huko humu humu na hayo ni maneno ya Zitto mwenyewe) Sasa hapa uzalendo huko wapi kama sio changa la macho?

Huyu Zitto aliyesema kuwa ni mzalendo hapokei posho ya ellf 80 aliwahi kukodi ndege kwa Mil 70 kwenda Kilimanjaro - Dar pesa za mlalahoi (ushaidi humu JF) Huyu huyu Nyerere (kama wafuasi wake wanavyopenda kumuita) aliwahi kwenda Uganda(nchi sina uhakika) akalipwa posho ya siku 11 lakini alikaa siku 7 na ile posho ya siku 4 alitia mfukoni (ushaidi huku humo na yalisemwa na mbuge mwenzake) Sasa huu uzalendo wa kukataa elf 80 na kukubali mamilioni ni uzalendo wa aina gani?

Sikatai mtu kufanya siasa lakini hizi siasa za kutudangaya na kutufanya watanzania wote ni wajinga na ni wasahulifu mie zinanichefua. kwamba leo unaweza kusema hiki na keshokutwa useme kitu cha kupingana na ulichosema jana kwa zikome.

Tuache kumjaza ujinga tumwambie ukweli ili ajirekebishe! Hapo ndo tutakuwa tunamjenga...
 
Dah! hata sijui nianzie kuchangia wapi maana umesasambua kila kitu kwa umakini na uyakinifu wake. Ngoja niweke Ice kidogo

Watu wanadhani tunajadili Zitto kama mtu wa kawaida, na wengine wanasema ni wivu.
Kila aina ya sababu zinatolewa kumtetea, hatukuzisikia kabla

Wasichokielewa, hatuwezi kubadilisha taifa kwa 'fire work''.Leo fulani kafanya kosa tunalaani, huo ni ufisadi, huo ni utapeli n.k.

Tunakaa na zigo la nchi isiyo wajibika, isiyo na utamaduni wa kuwajishana au kuwajibishwa. Tunabaki kuwa taifa la watu wasiotafuta suluhu ya muda mrefu bali suluhu za matukio

Tunataka viongozi wazalendo wanaotenda yale wanayosema,kama hawatendi wanawajibika

Tunataka model ya taifa yenye 'viongozi wanasisa' wenye maana, si matapeli wanaotumia wananchi(expolitation) kwa faida zao

Ni lazima tuwe wakweli kwa nafasi zetu. Tunazidhulumu nafsi tukiwalaumu CCM kwa kushindwa kuvua magamba, nyuma ya pazi tunadanganya yazungumzwe ndani ya chama.

Tunakuwa majahilia tunaposema Rais ameacha Jairo akastaafu,ni kosa, huku tunajificha nyuma ya 'yazungumzwe' ndani

Utapeli tunaouonyesha kwa wananchi ni kama huu tunaoujadili.

Nitaweka bandiko mtendaji wa ACT alivyosema kuhusu Zitto na anachosema leo kuhusu Zitto! utacheka ukisikia wanajiita wanademokrasia.

Alinda, niliwambia CDM hapa duru 2011 suala la Madiwani na Zitto litawaumiza mbele ya safari.Wanachokifanya kumuogopa Zitto ni double standards.Leo wanashuhudia wakiambiwa Zitto ameonewa, madiwani halali!

Wanakurupuka ikiwa too late. Nidhamu haijengwi kwa kuangalia sura, inajengwa kwa kukata mbele na nyuma

Kuhusu migogoro, Mwigamba, wa ACT ameandika 'rafiki yangu kuna nini kila mkasa unakuhusu" ?
Hiyo ni mwaka 2009, leo tukisema Zitto ndicho chanzo cha migogoro tunaambiwa tuna chuki

Uzalendo wa Zitto ni kukataa posho! watu hawajui kuwa alikimbilia mahakamani ili kulinda ubunge.
Kwa bahati mbaya muda haumpi nafasi kwasababu anatakiwa ajiandae kurudi bungeni kwa njia nyingine October, amesepa!

Hakuwa anasimamia haki mahakamani, alijua haki imetendeka. Alikubali vikao vilivyomwita ni halali alikubali kuachia nafasi abaki mwanachamaKwenda mahakamani alijua ni kuvuta muda.

Leo tunaambiwa ni mzalendo wakati ametumia mahakama akijua haina matokeo tofauti. Alichosimamia ni uzalendo wa tumbo lake

Katika hali ile ile tunayosema ya utapeli, leo anatudanganya ameng'atuka, na si kufukuzwa. Haelezi kwanini amefukuzwa bali kushawishi watu amefukuzwa tu

Katika hali ile ile ya kutotendea nafasi haki, Mwigamba na Kitila, wamekaa na kumfukuza mwanzilishi katika utaratibu ule ule ule wa Waraka.

Lengo ni mtu wao, halafu wanaambiwa CDM wana watu wao. Wao Wanafukuza, hawataki kufukuzwa!!!
Hawajazungumza na Limbu ndani ya vikao haki wanayosema Zitto hakupewa CDM!

Tunataka tujenge taifa la kuwajibika, kuwajibishwa, kuwajibishana bila haya soni au simanzi

Kuogopana ndiko kunapelekea watu kumshangilia mgombea mtarajiwa mwizi, wengine wakiita mil 10 pesa za migebuka, Bilioni 1 kama vijisenti, tumbili n.k. Hapana lazima tuanze na kizazi hiki, kilichotushinda kinaondoka!

Tusimame katika ukweli, ili ukweli utuweke huru
 
Back
Top Bottom