SAKATA LA ZITTO
YAMETIMIA YALIYOANDIKWA DURU
Kwa wafuatiliaji,sakata la Zitto na washirika wake limeongelewa katika nyuzi hii na nyingine kwa kina na nukta
Yote yaliyozungumzwa yametimia, hatimaye Zitto amejiunga na ACT kama mkakati ulivyokuwa, amefanikiwa kununua muda wa ubunge akijua matokeo yake, na sasa anaendeleza jitihada za kisiasa kwa mitazamo tofauti
Tulisema, mgogoro wa ACT ulitengenezwa na washirika wa Zitto kumuandalia nafasi walioitaka kuanzia walipokuwa CDM
Tulifafanua kuwa, haraka za mkutano wa ACT ziliambatana na muda wa Zitto kujiunga na maandalizi ya uchaguzi mkuu
Hakuna kilichokwenda tofauti na tuliyoongea. Haukuwa utabiri ni jambo lililojulikana ingawa linadhaniwa liliandaliwa kifundi
Katika wiki mbili na ushee, Zitto amekuwa katika mitandao na vyombo vya habari akieleza hatma yake
Kilichoitwa hotuba ya kuaga wabunge ilikuwa ni sehemu ya mbinu za kuendeleza siasa na pengine kuponya majeraha
Kwa uapnde mwingine, ilikuwa maandalizi ya wapenzi wake kumfuata huko aliko(rejea makundi katika bandiko
#154 lililozungumzia kundi la kwanza)
'Hotuba yake bungeni' ilizungumzia kwa ufundi sana namna alivyoishi na wenzake na yale aliyoyafanya. Ikagusia kuhusu kufukuzwa, na wakati huo huo ikimwelezea kama aliyeng'atuka. Hotuba hiyo haikuzungumzia matatizo yake na chama chake, bali kumjenga kama mtu aliyeonewa, na hivyo kutafuta 'sympathy'
Zitto anatambua kuwa kuisema CDM kutaamsha majeraha aliyojisababishia kisiasa kwa majibu asiyopenda yarudiwe midomoni mwa watu. Hata hivyo, wapambe wake wanazidi kumweka katika wakati mgumu pale wanapoituhumu chadema
Ni wakati mgumu kwasababu Zitto asingependa mgogoro uliomfikisha hapo uzungumzwe mara nyingi kwa kutambua unatonesha vidonda vya kisiasa.
Kwa upande mwingine, huo ni mkakati maalum ili asionekane kama mhujumu wa kambi ya upinzani. Iwavyo iwe, Zitto na wapambe wake wanatakiwa wachukue muda kuitathmini kwa kutoa muda wa majeraha kupona
ZITTO ACHUKUA KADI
Zitto amechukua kadi ya ACT katika tawi la Tegeta kama mwanachama mwingine. Huu ni mkakati wa kisiasa uliolenga kupunguza joto la kisiasa na mogoro unaovuma katika chama chake.
Isingekuwa busara kama angechukua kadi hiyo makao makuu, hilo lingewewapa ACT original nafasi ya kuendeleza mgogoro kwa kusema, ACT wahamiaji wamekuja na mtu wao
Na wala isingekuwa busara kuchukua kadi kutoka Kigoma, kwani kufanya hivyo kuendeleza ile hali ya ACT kuwa chama cha Kigoma, jambo ambalo linegkinzana na hoja za Ukanda walizolalamikia miaka mingi.
MKUTANO WA HABARI
Kama ilivyoandikwa na kama haitabadilika, Zitto atakuwa na mkutano na wana habari Serena Hotel
Wengi wanataraji Zitto kuanza kuiandama Chadema.
Wanaofikiri hivyo wamepotoka
Kinachotarajiwa ni Zitto kujitambulisha kama mwanachama,kutimiza ahadi ya kueleza hatma yake kama livyowahisema
Pia atatumia nafasi hiyo kujieleza kama mwanachama anayejiunga kama mwingine ili kuondoa wingu la ujio wake kama linavyojulikana 'uenyekiti''
MKUTANO WA ACT
Mkutano mkuu kama unavyotarajiwa utafanyika siku za karibuni wakati Zitto akiwa mwanachama.
Hizo ndizo hesabu zilizofanyika kuanzia mwanzo na kuleta mtafaruku mkubwa ndani ya ACT.
ACT Wahamiaji walijua ujio wa Zitto, na ACT original walijua ujio wake ni wa uenyekiti
Isitegemewe kuwa Zitto atapewa nafsi yoyote ya uongozi. Pengine hata ujumbe wa kamati muhimu hatapewa
Yote yanafanyika kuondoa hisia,ujio wake ulikusudiwa na kwamba mgogoro ni uenyekiti
Asijedhani awaye kuwa Zitto atachukua uongozi wa chama cha ACT
Pamoja na yote hayo, Zitto atabaki kuwa mtu mwenye nguvu ndani ya ACT bila wadhifa unaojulikana.
Inaeleweka ni muda mfupi kuelekea uchaguzi mkuu na hakuna matumaini ya Zitto kugombe nafasi ya Urasi.
Lengo ni Zitto kuwa mwenyekiti siku za usoni na hesabu hizo zinafanywa kiufundi sana.
Nafasi anayotajiwa kugombea ni ubunge. Haijulikani ni eneo gani, lakini yatosha kusema harakati na haraka zote ni kutengeneza mazingira ya kurejea bungeni na kumuandaa kwa uenyekiti siku za usoni. Kundi la ACT wahamiaji lina mtazamo huo kuanzia CDM
ACT wahamiaji ni sehemu ya kundi la kwanza(rejea bandiko 154) wakiamini kuwa Zitto alizaliwa kuwa mwenyekiti wa vyama vya siasa. Kundi hilo halina sababu za msingi bali mapenzi ya dhati kwa Zitto. Ni kundi lisiloweza kubadilisha msimamo wala kubadilishwa, linaamini katika Zitto na hakuna namna nyingine kwao isipokuwa Zitto
Nini kinafuata miezi miwili ijayo?
Nani ataathirika na hali ya mambo kama ilivyo
Itaendelea...