Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Mkuu Nguruvi3, umeacha Funzo sahihi....si kwa Watanzania tu ,Waafrika kwa ujumla. NI KUDHIHIRIKA KWA 'IRRELEVANCE OF DEMOCRACY' kwa Mtu mweusi.

Nitaendelea kusema, Kidemokrasia si Zitto wala CDM waliokuwa sahihi.

Pande zote zilishakiuka misingi ya Demokrasia, si kwa bahati mbaya bali ni KUTOKUWA KWAKE NA MANTIKI.

Tunapokosea ni kutazama Ukiukaji wa upande fulani ni 'MAKOSA/MAPUNGUFU' yanayotakiwa kurekebishwa, wakati tunatazama ukiukwaji wa ule upande wa pili kama 'UHALIFU/CRIME' na kuushitakia kwa Umma. It is unfair!

Kwangu linapokuja suala la kukiuka kiapo cha Demokrasia, hakuwezi kuwa kosa hadi pale nitakapotambua DHATI yako, na si suala la Uadilifu bali DHATI.

Cha kusikitisha huwa tunapima dhati za watu kwa HISIA zetu, Uadilifu na Imani tu, na kusahau kuwa Dhati hupimwa na Relevance ya mazingira.

Kinachoendelea ni kupotea kwa Watanzania kwa vioja na vituko visivyoisha.... Asubuhi tutasikia, Sisi ACT ni wanademokrasia na wawazi, jioni wanapgana vijembe na kufukuzana.

Asubuhi utasikia Zitto ndio muanzilishi wa ACT, jioni utasikia Zitto kama foreigner kawatimua waanzilishi wa ACT.

Asubuhi utasikia sisi ni misingi, na jioni utasikia misingi ni batili. Ni porojo kwa kwenda mbele. Yote ni KUDHIHIRIKA KUSHINDWA KWA DEMOKRASIA.

Watz hatupaswi kuzungushwa hivi, tulipaswa ku-focus something. Huu ni ULEVI MZITO.

Tusipochukua hatua wajukuu wetu watakuwa wanapiga the same porojo.

Mkuu Nguruvi3, Maisha ni HESABU. Kamwe hakuna muujiza kwa ustawi wa Taifa. Maendeleo ni HESABU, si bahati na sibu.
Mkuu umezungumza mengi yenye mantiki na kina sana. Ni kubaliane na baadhi ya hoja zako kuanzia chini

Ni kweli tusipochukua hatua wajukuu watapiga same porojo. Huo ndio msingi wa wengine kusimama hapa na kujaribu kufwaeleza, wanaoamini, wanaosikia au wanaona. Wasio sikia hawatasikia

Pili, Watanzania hatupaswi kuzungushwa hivi. Ni kweli na ninawajibu wetu tupambane na wazungushaji kwasababu kupitia uzungushaji wao, ndipo wanaweza kututawala.

Tumewapuuza, wamefikia mahali milioni 10 wanaita pesa za chips dume, bilioni wanasema ni vijipesa katika kijaluba.
Wana haki ya kusema hivyo, wametuona wajinga, na tumewapuuza. ''The chicken have come home to roost''

Tatu, vioja ulivyo orodhesha haviishi,kibaya, vinaambatana na udanganyifu. Tunaambiwa fulani ni mzalendo, alikataa posho.

Mzalendo huyo huyo alikwenda mahakamani ili kuzuia ubunge wake kwasababu ile ile ya posho

Hapana! hivi ni zaidi ya vioja, ni utapeli na ndio unatusukuma kuwaambia wananchi, si kweli ukitoa kwa mkono wa kulia akachukua na wa kushoto, uzalendo upo wapi?

Nne,nikubaliane pia, pande zote zilikiuka misingi ya demokrasia. Na hili nimelisema sana.
Chadema walikiuka msingi kwa kuwa na madaraja.

Wapo waliohukumiwa mapema, na wengine wakipewa muda kama Zitto
Katika mazingira ya kawaida Zitto angeshahukumiwa na chama chake tangu alipoanza kutembea na barua ya kujiuzulu

Mbona madiwani walihukumiwa haraka? Mbona Juliana na Mwampamba hawakupewa fursa aliyopewa Zitto?

standard ipo wapi? Mbona vijana wa undergraduate waliotandikwa chale za makalioni waliadhibiwa, na mfadhili wao hakuadhibiwa. Huwezi kuwa na doube standards ukawa na demokrasia

Kwa upande wa Zitto, ni ''mwalimu'' wa demokrasia. Wakiwa nyuma ya pazia na akina Kitila/Mwigamba, demokrasia ya kusema na kutenda haipo. Walichochee maasi na vurugu kwa kofia ya demokrasia. kwamba, walihubiri demokrasia mchana usiku vurugu

Endapo wangejitokeza na kuzungumza wazi sioni tatizo. Tatizo ni pale walipotulisha dhana ya demokrasia huku wakitenda kinyume

Mkuu, tulikaa kimya kwa muda mrefu tukijua kuna somo.

Siku za karibuni, katika njia zile zile za ulaghai tumesoma mengi ya kuchosha. Mengine ya kupotosha na mengine yasiyo na ukweli

Hapana! tkukikaa kimya uhuni ukichukua nafasi ya demokrasia ni kutotenda haki kwa jamii

Nikubaliane nawe katika Tanzania na Afirka demokrasia ni dhana ngumu. Lakini wapo walioweza,kwanini sisi tushindwe?

Waziri mkuu wa kwanza wa Singapore hayati LKY ameibadili nchi masikini kuwa nchi ya dunia ya kwanza kwa miaka 50

Tumeshindwa kuondoka katika kundi la nchi masikini duniani kwa miaka 54

Tatizo si wananchi, ni matapeli wanaotumia ujanja wakivaa ngozi za kondooo kumbe ni mbwa miwtu

Hatujashindwa, tunaweza kuanza sasa. Pa kuanzia si kusota vidole CCM tu, ni kujenga misingi ya kuwajibika, kuwajibishana na kuwajibishwa. Ni kuanza sasa ili kizazi kijacho tupate akina LKY wa Tanzania

Tukiendekeza magenge ya matapeli, kuyatetea magenge kwa ngojera, ngano na mashiri, tunajidhulumu na kudhulumu wajuu zetu

Tusemezane
 
Nguruvi3 na wengine,nilikua naomba mfanye kitu au tafanye kitu,jee Zitto alijiandaa au aliandaliwa,maana kelele nyingi kwa Zitto naona kuwa taifa lilimtegemea,na inavyoenekana kwa sasa hakuna mbadala wa Zitto,kama Zitto aliandaliwa na akaja kuwasaliti,basi muandae mwingine,ila kama alijiandaa mwenyewe kwa malengo, tuachane nae,kwani mpaka sasa hakuna kijana kariba Zitto kama yupo mpeni mbinu basi ili mbadala,maana mda wa lawama umeisha,siku zinaenda
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3 na wengine,nilikua naomba mfanye kitu au tafanye kitu,jee Zitto alijiandaa au aliandaliwa,maana kelele nyingi kwa Zitto naona kuwa taifa lilimtegemea,na inavyoenekana kwa sasa hakuna mbadala wa Zitto,kama Zitto aliandaliwa na akaja kuwasaliti,basi muandae mwingine,ila kama alijiandaa mwenyewe kwa malengo, tuachane nae,kwani mpaka sasa hakuna kijana kariba Zitto kama yupo mpeni mbinu basi ili mbadala,maana mda wa lawama umeisha,siku zinaenda
Tunaheshimu mawazo yako, na tunaheshimu haki yako ya kutoa mawazo

Tunaheshimu haki ya Zitto na wenzake kujieleza na kuendeleza siasa.
Tuna haki kama hiyo katika kujadili yale wanayozungumza

Hatumlaumu mtu, tunajadili maudhui wanayotupa kupitia habari wanazotoa

Tunataka tubadili mwelekeo wa siasa za kizamani, siasa za ulaghai na utapeli

Tuna dhima ya kueleza wananchi kuhusu ukweli, haki na upotoshaji.

Katika kufanya hivyo hatutegemei kumpendeza kila mmoja. Wapo watakaochukia, nao wana haki kama wale wanaopendezwa
 
Mkuu Mu-sir naomba ulete kile kipande cha gazeti kilichokuwa na maelezo ya Mwigamba. M

Mwigamba katika gazeti aliandika kuwa Zitto ni rafiki yake na walikuwa na mawasiliano ya karibu.

Mwigamba alisema haya '' ...Katibu mkuu ana haki ya kuchukua hatua alizochukua, nasikitika ulimpinga hadharani. Nakusikitikia''

Maneno hayo kayasema Mwigamba, mwenyekiti wa CDM wakati huo, na mshirika wa Zitto katika Waraka na sasa ni katibu mkuu wa ACT ambako Zitto ni mwanachama Ukisoma hoja zangu katika bandiko hili, hakuna mahali nimeeleza sababu za mitafaruku kuwa sahihi au la. Kama

Nimekuwa naeleza mitafaruku kwa ujumla wake. Ukisoma bandiko 172 nimorodhesha matukio yaliyotokea zitto akishiriki au akitajwa.
Ndio maana nilikuuliza swali moja, ni mtafaruku gani wa CDM ambao Zitto hana mkono?

Napenda uelewe, sijachukua upande na wala sijasema Kafulila alikosea.

Nilichosema ni kuwa katika matukio ya CDM Zitto ni ima mhusika au ametajwa. Hapo ndipo ilipo main point.

Sitaingia katika kujadili mambo ya ndani, ninajadili hoja moja tu tena nikiuliza, ni mgogoro gani wa Chadema ambao Zitto hajatajwa

Nitakupa mfano, katika sakata la masalia, Zitto ametajwa kuwachukua vijana kwenda kutandikwa chale za matakoni( dah ashakum)

Sijasema hatua hiyo ya Zitto ni nzuri au mbaya, ninachosema Zitto alishiriki kuwapelekavijana kutengenezwa ''nyungu'' zao kisiasa

Endapo chale chini ya kiuno kwa nyuma inafanya kazi au la, hilo si jukumu langu.

Ninachosema motiisha iliyotolewa na mheshimiwa ndicho kilikuwa kiwe kichochoe cha mtafaruku

Hivyo naongelea motisha na ushiriki wake, siongelei sababu au matokeo ya kutandikwa chale uti wa mgongo unapoishia.

Narudia, sina haja ya kujua mpango wa chale chini ya uti wa mgongo, ninachosema jina la Zitto lililkuwepo kama mshiriki

Again, sina sababu na wala siingi katika details za nini kimefanyika kwasababu ni nje ya muktadha wa bandiko.

Ninachoweza kusema ni kuwa katika hoja yako hapo juu, bado unazidi kuunga mkono hoja yangu kuwa Zitto ametajwa, the bottom line ameshiriki katika mambo mengi yaliyokuwa na dhamira ovu.

Ushahidi ni wanautoa 'fresh graduate' waliolimwa chale!

Kwa haja ya bandiko lililopo, hakuna mgogoro wa Chadema ambao Zitto hana ushiriki
Mkuu bado unakwepa swali nimekuuliza Kafulila alifanya kosa gani maana haya uliyaandika mwenyewe kuwa katika kila makosa ya watu walofukuzwa Zitto alikuwa na mkono ndani sasa tujulishane makosa yenyewe halafu tuutazame mkono wa Zitto. Unaporudisha swali langu kwa swali ni kukwepa kiujanja maana tunataka kujua wapi haki ilipotoshwa na pengine Zitto alihusika vipi badala ya kuendelea kutumia matamshi wya watu ambao hawakuwepo. According tofulani, sii ushahidi wa kuridhisha.

Leo hii mimi hapa napingana na maamuzi kibao ya Chadema haina maana nina mkono ktk kukisambaratisha chama isipokuwa sikubaliani na maamuzi yanayofanywa na nimeeleza kwa nini sikubalianani. Na nakuomba utambue tu kwamba nachopingana na Chadema katika haya yote ni pale kamati kuu inapochukua hatua kumfukuza mjumbe wa kamati kuu pasipo kupitia baraza kuu. Hii ni kanuni ya chama hivyo sitojali nani kasema nini ikiwa nimeona demokrasia inakiukwa na kanuni waloiweka ikivunjwa kwa tuhuma ulojenga WOGA.

Pili ni imani yangu kwamba kamati kuu haina mamlaka ya kumfukuza mwanachama ikiwa imani ya KIITIKADI ndio msingi wa ujenzi wa chama. Chama cha siasa ni Wanachama, na unapofukuza wanachama uanachama unaua imani ya chama na sio mtu. Kwa hiyo mimi narejesha tu yale nisipokubaliana nayo kwa kuzingatia umuhimu wa chama cha siasa kuwa na wanachama wenye imani na itikadi na sio chama kina wenyewe. leo hii Chadema inapendwa kwa sababu ya Mbowe au Slaa. Watu wanatoka uanachama kwa sababu ya Zitto! Imani ya chama KITIKADI iipo wapi ama haikuwepo toka mwanzo!

Kuhusu tuhuma zooote zilizowahi kutolewa juu ya Zitto kuhusika, mimi nachosema hizi zote ni hearsay, hakuna hata mmoja wao alokuja na ushahidi kuhusika kwake katika scandal zote isipokuwa Zitto alitofautiana nao katika maamuzi na usimamizi wa swala zima. Zitto alikuwa tishio kwa baadhi ya watu ambao kwa mila na desturi zao wamezoea kumuondoa mtu ili wao washike nafasi ilowazi.

Wapo radhi kuua hata ndudu zao au watoto wao ili wapate Umaarufu maana siasa zetu zimejengwa ktk umaarufu. Wapo radhi kuua wenye ulemavu wa ngozi ili wapate Utajiri na vivyo hivyo wapo radhi kuzua fitna ili wao wafaidike kwa sababu tunatzama mafanikio ya mtu na kufikiria tukiiga ama kuwa kama huyo nasi tutafaidika. Hii ni asili ya mwafrika maana mchawi sii lazima atembee uchi usiku laa mchawi anaweza kutumia mdomo wake tu na akaathiri wengi.

Kuhusu Mwigamba alichosema ni kwamba alikuwa anamuunga mkono Zitto katika mambo mengi lakini amekuja tofautiana naye pale Zitto alipotaka kugombea Uenyekiti wa chama. Na ukizisoma kwa makini sababu alizotoa utashindwa kuelewa maana hakuna kanuni inayomzuia Zitto kugombea nafasi ya Uongozi na kwa bahati mbaya zaidi Mwigamba anasema alimuunga mkono Zitto hata pale alipoitaka Tanesco wanunue mitambo ya Dowans. Mimi binafsi nilipingana na Zitto nikasema kama kuitafikisha hewala lakini sio kuhalalisha kilicho haramu mkakinunua. Yalofuata sii ndwele, tunatazama haramu kama haramu hata kama italiwa na CCM bado uharamu wake haupotei.

Na hapo chini umemuomba Invisible, kwa kutumia jina langu kama mfano. Mkuu nukuu niliyoiweka mimi ni maneno ya Katibu mkuu Dr.Slaa, mwenyekiti Mbowe na Zitto mwenyewe kuhusiana na swala la Kafulila sikwenda nje ya mada hii ila uyasome tena maelezo yalotolewa juu ya sakata lile na maamuzi yalitoka wapi. na nisingelitoa maelezo hayo tungeendelea kuyumbishana wakati ukweli wa kilichofuatia tunao..
 
Jamani sisi binadamu ni watu wa ajabu sana, Kila siku tunalalamika kuwa serikali haichukui hatua pindi pale viongozi wanapofanya makosa hali sheria ziko wazi, Leo hii chama kinamchukulia hatua mtu aliyefanya makosa tena sio mara moja, lakini bado watu wanalalamika na kusema kwanini hawakukaa chini wakazungumza yakaisha..

Swali langu ni kuwa kama hivyo sheria na adhabu tunanazozitunga ili zituongoze ni za nini? Je hizi sheria tunawatungia wale wasio na uwezo, wale wasio na wafuasi, au wale wasio na ushawishi wowote katika jamii?..


Tukae tusema ukweli matendo ya Zitto yalijulikana tangu mwaka 2008 enzi za kutembea na barua ya kujiudhuru mfukoni. Zitto alifanya siasa za gizani mchana alikuwa ni naibu katibu mkuu na usiku alikuwa adui no.1 wa chama,

Nani hasiyejua ID ya TUNTEMEKE, nani hasiyejua matusi ya akina Juliana na masalia kwa jumla, nani amesahau uchonganishi kati ya Mbowe na Dr. Slaa, hivi ndugu zangu tumesahau siri za chama zilikuwa zinaletwa humu JF kila kukicha, kama tumesahau hilo tumesahau pia na swala la Lwakatare? haya yote yamefanyika tumeyashuhudia na ushaidi huko humu JF na aliyekuwa nyuma ya hayo yote alikuwa kijana mjenga hoja, mpenda media Zitto..

Nakubalina na wanaosema kuwa Chadema kilizembea sana katika swala zima la nidhamu kwa Zitto labda kama kingemkanya mapema, na kumrudiisha katika mstari basi hayo yanayotokea leo yasingetokea..

Ilifikia kipindi nikasema Chadema wanamuogopa Zitto, kwani alifanya mambo mengi ya wazi ila waliosurubiiwa walikuwa wengine. Je tumesahau adhabu ya akina Juliana, madiwani w a Arusha,Kafulila,madiwani wa Mwanza na nk. aliyekuwa nyuma ya haya yote kuwa ni Zitto? Zitto aliota ndevu akwa mfalme katika chama...

Na mgogoro ulipokuwa umefika kulikuwa hakuna namna ambavyo Zitto angeweza kufanya kazi na viongozi wenzake maana uaminifu ulikuwa haupo tena. (kumbuka sakata la mabomu ya Arusha kuna wanaosema alihusika)
Na kwa namna hiyo huamuzi wa Zitto kwenda kwenye chama chake ulikuwa ni wa lazima kwani kulikuwa hakuna jinsi.

Kuna wanaosema Zitto ni mzalendo alikataa posho.. Jamani hata Zitto mwenyewe alisha wahi sema "Husiwaamini wanasiasa" Zitto alikataa posho ya elf 80 ila akakubali posho ya vikao vya PAC ya shilingi laki 4 kwa siku (ushaidi huko humu humu na hayo ni maneno ya Zitto mwenyewe) Sasa hapa uzalendo huko wapi kama sio changa la macho?

Huyu Zitto aliyesema kuwa ni mzalendo hapokei posho ya ellf 80 aliwahi kukodi ndege kwa Mil 70 kwenda Kilimanjaro - Dar pesa za mlalahoi (ushaidi humu JF) Huyu huyu Nyerere (kama wafuasi wake wanavyopenda kumuita) aliwahi kwenda Uganda(nchi sina uhakika) akalipwa posho ya siku 11 lakini alikaa siku 7 na ile posho ya siku 4 alitia mfukoni (ushaidi huku humo na yalisemwa na mbuge mwenzake) Sasa huu uzalendo wa kukataa elf 80 na kukubali mamilioni ni uzalendo wa aina gani?

Sikatai mtu kufanya siasa lakini hizi siasa za kutudangaya na kutufanya watanzania wote ni wajinga na ni wasahulifu mie zinanichefua. kwamba leo unaweza kusema hiki na keshokutwa useme kitu cha kupingana na ulichosema jana kwa zikome.

Tuache kumjaza ujinga tumwambie ukweli ili ajirekebishe! Hapo ndo tutakuwa tunamjenga...
Kusema kweli mimi siyajui alofanya Zitto ndani ya Chadema kiasi kwamba niseme alitakiwa kufukuzwa hadi uanachama. Naomba sana uniwekee hapa mambo hayo na ushahid wake japo kwa maandishi tu kuwa Zitto alihusika katika hili na lile kama njama zake za kukisambaratisha chama. Kama ni ushirikiano hata katika yale ambayo aliyaona hayana nia njema sidhani kama ni kosa.

Hayo ya viongozi wengine wa serikali yalitajwa na tumeyasoma na tumesoma majibu ya viongozi hao dhidi ya kashfa walizopewa baada ya taarifa za tume kutolewa na ndio maana tukasema serikali yetu dhaifu. Udhaifu ama uimara wa Chadeema kweli ni kumfukuza Zitto kwa kosa ambalo hatulijui. Mimi naomba mtu yeyote anayesema ni haki Zitto afukuzwe uanachama atuambie alikikosea nini chama na kwa ushahidi upi?
 
Kusema kweli mimi siyajui alofanya Zitto ndani ya Chadema kiasi kwamba niseme alitakiwa kufukuzwa hadi uanachama. Naomba sana uniwekee hapa mambo hayo na ushahid wake japo kwa maandishi tu kuwa Zitto alihusika katika hili na lile kama njama zake za kukisambaratisha chama. Kama ni ushirikiano hata katika yale ambayo aliyaona hayana nia njema sidhani kama ni kosa.

Hayo ya viongozi wengine wa serikali yalitajwa na tumeyasoma na tumesoma majibu ya viongozi hao dhidi ya kashfa walizopewa baada ya taarifa za tume kutolewa na ndio maana tukasema serikali yetu dhaifu. Udhaifu ama uimara wa Chadeema kweli ni kumfukuza Zitto kwa kosa ambalo hatulijui. Mimi naomba mtu yeyote anayesema ni haki Zitto afukuzwe uanachama atuambie alikikosea nini chama na kwa ushahidi upi?
Hata mimi siyajui ya undani, ninayoyajua ni yale ya wazi, yenye fikra yanayotokana na kauli zake. Ni yale yasiyohitaji chochote bali weledi na matumizi mazuri ya fuvu la kichwa

Kabla sijajibu mabandiko yako mawili, hebu tumsikilize Samson anasemaje kuhusu Zitto
Pengine tunaweza kuokota moja la maana.

Huyu hapa Swahba Samson

tar 9//12/2009
NAKUHURUMIAZITTO KABWE

MHESHIMIWA Zitto Zuberi

Kwa imani niliyokuwa nayo kwako na nikizingatia elimu kubwa uliyokuwa nayo, nafsi yangu ikanituma kufikiria kwamba labda ‘wamekunukuu vibaya'. Nilihudhuria mkutano wenu na waandishi wa habari uliokusudia kuzika tofauti zenu na Mbowe na kusonga mbele kama chama.

Pale ulipoulizwa swali na mwandishi mmoja kwamba utawezaje kufanya kazi na Mbowe wakati wewe ni mjamaa na yeye ni bepari; ukajibu kwa namna ambayo haikukata kiu yangu ndipo nikaamini kwamba kumbe hukunukuliwa vibaya bali ni kweli ulisema maneno hayo.

Nilipingana na wewe pia pale ulipoamua kupinga uamuzi wa kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA).

Unakumbuka kwamba nilialikwa katika uchaguzi huo miongoni mwa wageni wachache wanafunzi, wanahabari, wanaharakati na watu wa kada mbalimbali walioalikwa kushuhudia uchaguzi ule.
Wakati wa uchaguzi wenyewe utakumbuka mimi na wewe tulikaa meza moja na tulitenganishwa na mtu mmoja tu (Mkurugenzi wa Uenezi Taifa wa CHADEMA, Erasto Tumbo).

Nilitegemea mambo yasiyoendana na sera na kauli mbiu za chama chenu ambazo zinatangazwa hata katika jina la chama (DEMOKRASIA na MAENDELEO) ambayo yalifanyika pale ukumbini uliyaona.

Najua jioni wakati wa kutangaza matokeo hukuwepo lakini nategemea ulipata taarifa za kauli za vijana mbalimbali walizotoa pale wakitaja waziwazi majina ya watu walioharibu uchaguzi ule.

Sikutarajia kama Naibu Katibu Mkuu wa chama upinge hatua ile iliyochukuliwa na msimamizi wa uchaguzi pamoja na kikao kingine chochote cha juu ya msimamizi wa uchaguzi eti kwa sababu tu rafiki yako Kafulila alikuwa anaongoza.

Hilo lilinipa taabu kubwa na naomba uniwie radhi rafiki
yangu lakini nasema ukweli wa nafsi yangu kwamba nilifikia kujiuliza mara mbilimbili kama ungechaguliwa wewe kuwa mwenyekiti wa chama hicho taifa, hali ingekuwaje?

Na mwisho nilipingana na wewe pale ulipopinga kwenye vyombo vya habari kuvuliwa wadhifa kwa David Kafulila. Kwanza ulionekana umeweka ubaguzi kwa sababu katika maneno yote uliyonukuliwa ulisisitiza juu ya Kafulila peke yake na hukumgusia kabisa Danda Juju wakati wote walivuliwa kwa sababu
zinazofanana.

Lakini kwa sababu Kafulila ni rafiki yako sana, umemwandaa kuwa mbunge na unamuunga mkono katika harakati zake, na ni mbunge mtarajiwa kwa kuwa anakubalika sana jimboni basi ukamtetea na kumsahau ‘mhanga' mwenzake.

Hilo tu linafanya tutofautiane na zaidi sana tunatofautiana kwa kupinga maamuzi ya Katibu Mkuu wako nje ya vikao, maamuzi aliyoyachukua kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo.Najua yote haya umeamua kuwa kimya hujayatolea

kauli yako ikiwa ni pamoja na yale ya kumfadhili Kafulila kwenda Kigoma kuichafua vizuri CHADEMA.

Lakini kama ni kweli, napingana na wewe na kama unaendelea kukaa kimya nitaamini kwamba ni kweli.


Sasa limeibuka la kusema kwamba unatembea na barua ya kujiuzulu nyadhifa zako zote ndani ya CHADEMA ikiwa ni pamoja na ubunge. Bado pia sijapata kauli yako, narudia kusema kwa kuendelea kunyamaza unanifanya niamini kuwa ni kweli.

Na kama ni kweli, nakuhurumia sana Zitto Kabwe. Sasa naona kile nilichokuambia wakati nikikushauri ujitoe kugombea uenyekiti kinatimia.

Nilikuambia ujitoe haraka tena kimyakimya kwa kumweleza tu Katibu Mkuu aweke fomu yako pembeni lakini hukutaka kunisikia.

Lakini utakumbuka moja ya sentesi zangu ilikuonya kwamba ukingang'ania kugombea iwe umeshinda
uenyekiti ama umeshindwa utapata shida kubwa.

Nilikueleza kwamba hutaaminika tena na Watanzania na kila kitu utakachofanya utaonekana kama ulikuwa ni mamluki ndani ya chama.

Ni kwa bahati kwamba umetokea kuwa na viongozi wenye busara sana kina Freeman Mbowe na kina Dk. Wilbrod Slaa wakisaidiwa na hekima na kamati ya wazee.

Hawa wakaamua kukurejesha kwenye unaibu katibu mkuu.
Nilishuhudia siku ile wajumbe wa Baraza Kuu la CHADEMA walivyoshangilia uteuzi wako na wa Dk.
Slaa na Hamad Yusuph kama wakuu wa Sekretarieti ya chama.

Nilidhani sasa ungetulia na kufanya kazi ya kujenga chama chenu na kusonga mbele lakini haikuwa hivyo.

Baada ya kushauriana sana wakati ule ulipotaka kugombea uenyekiti niliamua kutafuta habari za kiuchunguzi ndani ya CHADEMA.

Nimeongea na viongozi mbalimbali na maofisa wa CHADEMA makao makuu, nimeongea sana na David Kafulila na hata niliwahi kumsikiliza mama yako mzazi akiongea na watu ambao sikuwafahamu.

Nimegundua kitu kimoja tu: kwamba kama mambo haya huyafanyi kwa makusudi na kwa malengo maalumu, basi watu uliowaamini sana ndani ya CHADEMA hata kama walikuwa na nyadhifa ndogo, walikubali kutumiwa ili wakutumie wewe kuimaliza CHADEMA na wewe ukaingia mkenge.

Ukakubali kugombanishwa na viongozi wenzako wa ngazi za juu hasa Mwenyekiti Freeman Mbowe ili malengo ya watu hao yatimie. Sasa nakuonea huruma.

Nakuonea huruma kwa sababu kama ni malengo ya hao watu kukutumia kukimaliza chama

hawatafanikiwa na badala yake watakumaliza wewe bure na utakuja
kushtuka ukiwa umekwisha kisiasa.

Kama ni malengo yako kwa utashi wako umeamua kutumika kukimaliza chama, nakuhurumia kwa sababu utajimaliza wewe na CHADEMA itaendelea kuimarika bila wewe wala Kafulila.

Ukitaka kujua ninachokisema, tuulize sisi waandishi tunaopata mawazo ya Watanzania moja kwa moja. Kwa

kuanzia muulize tu Edward Kinabo kwamba Jumatano iliyopita alipoandika makala ya "Simwelewi Zitto Kabwe" aliungwa mkono na wasomaji wangapi na walikuwa na mawazo gani juu yako. Hapo ndipo utakapoelewa kile ninachokisema.

Namalizia kwa ujumbe wa msomaji wangu mmoja tu kati ya wengi.

Huyu aliniambia anaitwa Meshack na yuko Korogwe. Aliniambia, "Sisi tulishajua

kwamba Zitto anaondoka CHADEMA na kwamba anachosubiri tu ni pensheni yake ya ubunge ambayo huwa inatolewa baada ya Bunge kuvunjwa.
Naomba Mwigamba kwa sababu unaweza kuongea na viongozi wakuu wa CHADEMA, waambie kwamba
wasije wakafanya kosa la kumvua Zitto uongozi wala kumvua uanachama.

Sisi hatutaki apate kisingizio cha kuondoka CHADEMA. Waambie wamuache tu mpaka atakapoondoka mwenyewe ili Watanzania wazidi kumfahamu," mwisho wa kunukuu.

Tafakari mwenyewe ulikofika, uamue cha kufanya. Kumbuka uamuzi wa mwisho ni wako wengine tunakueleza tu maana tumejiapiza kuzungumza ukweli hata katikati ya ugomvi.
Kama utaamua kuondoka CHADEMA ama kujivua tu nyadhifa zako. katika yote nakutakia kila heri!
 
Mkandara;12264480]Mkuu bado unakwepa swali nimekuuliza Kafulila alifanya kosa gani maana haya uliyaandika mwenyewe kuwa katika kila makosa ya watu walofukuzwa Zitto alikuwa na mkono ndani sasa tujulishane makosa yenyewe halafu tuutazame mkono wa Zitto.
Mkuu kuhusu Kafulila sitazungumzia. Ninachoweza kusema ni kuwa mgogoro uliokuwepo Zitto alishiriki kuupalilia. Mwigamba ameeleza vema kama nilivyomnukuu hapo juu.
Hapa nilitaka uone kuwa Zitto hakusimama kama kiongozi, bali alijificha nyuma akichochea kuni. It is one too many!


Unaporudisha swali langu kwa swali ni kukwepa kiujanja maana tunataka kujua wapi haki ilipotoshwa na pengine Zitto alihusika vipi badala ya kuendelea kutumia matamshi wya watu ambao hawakuwepo. According tofulani, sii ushahidi wa kuridhisha
Well kama ulinukuu maneno ya gazeti ya Mbowe na Zitto, kuna kosa lipi nikinukuu kwingine?


Leo hii mimi hapa napingana na maamuzi kibao ya Chadema haina maana nina mkono ktk kukisambaratisha chama isipokuwa sikubaliani na maamuzi yanayofanywa na nimeeleza kwa nini sikubalianani. Na nakuomba utambue tu kwamba nachopingana na Chadema katika haya yote ni pale kamati kuu inapochukua hatua kumfukuza mjumbe wa kamati kuu pasipo kupitia baraza kuu. Hii ni kanuni ya chama hivyo sitojali nani kasema nini ikiwa nimeona demokrasia inakiukwa na kanuni waloiweka ikivunjwa kwa tuhuma ulojenga WOGA
Tena kupingana na mawazo ni jambo zuri sana. Narudia, nimesimama na Zitto kwa mambo mengi aliyopingana na chama chake, kumbu kumbu zipo. Hata hivyo, tofautii na Zitto sisi wengine husema wazi. Zitto hujificha nyuma ya vijana, waraka n.k. akionekana kondooo mwema, not!

Pili ni imani yangu kwamba kamati kuu haina mamlaka ya kumfukuza mwanachama ikiwa imani ya KIITIKADI ndio msingi wa ujenzi wa chama. Chama cha siasa ni Wanachama, na unapofukuza wanachama uanachama unaua imani ya chama na sio mtu. Kwa hiyo mimi narejesha tu yale nisipokubaliana nayo kwa kuzingatia umuhimu wa chama cha siasa kuwa na wanachama wenye imani na itikadi na sio chama kina wenyewe. leo hii Chadema inapendwa kwa sababu ya Mbowe au Slaa. Watu wanatoka uanachama kwa sababu ya Zitto! Imani ya chama KITIKADI iipo wapi ama haikuwepo toka mwanzo!
Chicken are coming home to roost

Aliyeandika utaratibu ni Kitila. Zitto akawa naibu katibu mkuu na kuusimamia.

Mwigamba alikuwa mwenyekiti wa mkoa hakuwahi kupinga

Wakaitwa kamatai kuu, hawakupinga kwenda kwasababu walijua ni halali. Walichopinga ni baada ya kisu kuwakata

Maamuzi mengi yamefanyika wakiwa ndani ya chama na hawakuwahi kukemea. Mkuu msumemo unakata mbele na nyuma

Ni ujinga huo huo wa viongozi wetu kushabikia katiba ya Chenge.

Siku inapowarudi wanasema katiba mbaya, mbovu n.k.
Ndio maana tunatakiwa tujenge kizazi kinachosimama na kusimamia haki, si haki za matumbo yao, bali wananchi na nchi
Kuhusu tuhuma zooote zilizowahi kutolewa juu ya Zitto kuhusika, mimi nachosema hizi zote ni hearsay, hakuna hata mmoja wao alokuja na ushahidi kuhusika kwake katika scandal zote isipokuwa Zitto alitofautiana nao katika maamuzi na usimamizi wa swala zima. Zitto alikuwa tishio kwa baadhi ya watu ambao kwa mila na desturi zao wamezoea kumuondoa mtu ili wao washike nafasi ilowazi.
Vijana wa chale cha matakoni walimtaja.

Tena walisema kama anabisha watoe ushahidi. Utetezi wa Zitto ni kuwa hakushiriki.

Washiriki kutoka pande zote, ya Zitto na wale waliojitoa mhanga walisema Zitto ni mpango mzima. Unataka ushahidi gani?

Alipokwenda kutangaza kugombea Urais wakati mgombea wa chama chake yupo kampeni, hiyo inahitaji ushahidi gani wakati yeye mwenyewe anakubali?!

Mwigamba kamwambia, kama lile la barua ya kujiuzulu ni uongo basi atoke na kukanusha.
Hadi anaondoka CDM hakuwahi kukanusha. Unataka ushahidi gani?

Timbwili la akina Juliana wanaomlilia wakiwa CCM Zitto ametajwa bila shaka. Unataka ushahidi gani?

Orodha ni ndefu
Na hapo chini umemuomba Invisible, kwa kutumia jina langu kama mfano. Mkuu nukuu niliyoiweka mimi ni maneno ya Katibu mkuu Dr.Slaa, mwenyekiti Mbowe na Zitto mwenyewe kuhusiana na swala la Kafulila sikwenda nje ya mada hii ila uyasome tena maelezo yalotolewa juu ya sakata lile na maamuzi yalitoka wapi. na nisingelitoa maelezo hayo tungeendelea kuyumbishana wakati ukweli wa kilichofuatia tunao..
Hakuna tatizo kwA kukufanyia reference

Nilichofanya ilikuwa kumuomba idhni bwana Invisible ili niende kufukua makabrasha yangu.

Nimeyatoa, mengine yameliwa na panya lakini yanasomeka.

Tutaweka moja baada ya jingine kila uchao

Umemsoma comrade Samson hapo juu?
 
Nguruvi3,\

Mkuu nadhani tuachane na hoja hii maana muda wote umekwepa maswali kiujanja ujanja kwa nukuu za watu ina maana umeamini ktk hearsay. Na ndivyo ilivyo kwa watu wengi ambao hawajui siasa isipokuwa wana ushabiki wa kisiasa. Scandals zote za Zitto zilikuwa blown out of proportion kwa sababu za mfumo wa chama ulojenga UBINAFSI kana kwamba Chama kina wenyewe,na cheo sio dhamana bali ni wajibu kulingana na kanuni.

Nilisema na nitarudia tena kusema kwamba kiongozi yeyote ambaye atapingana na ITIKADI, Mwongozo (Katiba) ya chama ama kuvunja kanuni za chama huyu ndiye anaweza wekwa kitimoto lakini kutokubaliana na maamuzi ya Uchaguzi ama mwenendo wa baadhi ya viongozi hili sio jambo la kufukuzana. Bali ni swala la kutazamwa litaathiri vipi Chama nje na sio ndani kwa sababu huko nje ndiko kuna wapiga kura. Mgogoro wowote ndani ya chama mara nyingi huwa ni kugombea nafasi ya jukwaa tu na hivyo kudhibiti kwake ni rahisi sana na huishia chumbani.

Kosa kubwa wanalofanya Chadema ni kukimbilia magazetini hata katika maswala ya ndani na wanapojibiwa na mhusika kupitia hayo hayo magazeti wao huanza kureact upon what they started. Hivi kweli ugonvi wako na mkeo, kila siku mmoja akiudhiwa akakimbilia magazetini watafika? Chama ni wanachama sasa mkianza wenyewe kukorofishana na kutangazana ktk magazeti ina maana tayari nyote mmekosa nidhamu. Iwe Dr.Slaa au nani haijalishi maana ya ndani hubakia ndani.

Chama cha siasa ni Wanachama sii viongozi wake wala usemi wa pasipo mimi chama hatakufa na ndio maana utakuta vyama vilivyokuwa kisiasa Sekretariet yake huwa sio viongozi wanaopigania Ubunge, ama uongozi wa Kitaifa kwa sababu kazi kubwa ya viongozi wa chama ni kujenga chama, na viongozi wa kitaifa kama kina Dr.Slaa, Mbowe na kamati kuu hawa walitakiwa kuzungumzia maswala mazito ya Kisera ktk MAJIMBO yao na KITAIFA na sio maswala ya ujenzi wa chama.

Hivyo ndio maana utakuta Chadema hushindwa kujigawa katika maswla yanayoingiliana, viongozi wake wakiitwa kwenye uandishi wa katiba Mpya, huko chamani hakuna viongozi na kibaya zaidi watu wale wale wanagombea nafasi chache zilizopo Bavicha au kamati kuu. Sasa Ebu nambie kama Chadema ingeweka mfumo wa kwamba mtu yeyote anayetaka kugombea Ubunge ama uongozi wa nchi kitaifa hawezi kuwa ktk Sekretariet au Bavicha ungeona jinsi nafasi nyingi zingekuwa wazi na pasingekuwepo na scandal zote hizi.

Niseme vizuri, scandal zote za Chadema ni za kugombea Jukwaa, kila mtu anataka kutoka na hakuna nafasi nyingine isipokuwa kupitia Bavicha au ujumbe wa kamati kuu maana ndio njia pekee ya kujulikana. Na hili ndilo limewaponza Chadema CUF, NCCR na TLP miaka yote kutokana na kwamba viongozi wanahofia kuachia nafasi zao maana ndipo riziki zao hupatikana, wakiachia watakula wapi na pengine ndio mwisho wao kisiasa. Na vijana hugombea nafasi za bavicha maana ndio mwanzo wa kubebwa kwenda kamati kuu na tiketi ya kugombea ubunge bila kupingwa!.

Tazama CCM, viongozi wa chama wengine na viongozi wa majimbo na kitaifa wengine hivyo mtu anakuwa na muda wa kufanya kampeni zake jimboni kwa kushirikiana na chama. Wao CCM ugonvi wao mkubwa ni kwamba usipokuwa mbunge hutakuwa waziri hapo ndipo wanatupiana madongo wabunge kwa wabunge maana kila mmoja anataka kuwa waziri mwenye kofia mbili pasipo kujali conflict of interest. Hivyo, kimfumo haiwezekani Katibu mkuu wa chama agombee Ubunge au Urais wakati huo huo akiendeshe chama makao makuu, kiongozi wa chama popote iwe tumaini la udiwani au ubunge na lazima kutakuwepo na conflicts.

Na kama unakumbuka niliwahi kushutumu humu JF kuhusu Mnyika kushika nafasi kama tatu za uongozi wakati fulani. Nikasema jamani kwani Vijana hawapo? mbona hawa vijana wana muda zaidi, uwezo mkubwa kukitangaza chama na wapo kila siku JF wakikitetea chama, leo iweje wasiweze! inakuwaje mtu mmoja kushika nyadhifa nyingi anaelemewa bado mnamuongezea madaraka! Wakajibu tena kwa jeuri ati sii vijana wote wanaaminika! ati kuna siri za chama ambazo baadhi ya watu fulani tu ndio wanaaminika. Toka pale nikasema basi, hiki chama sasa kinaanza kuchukua mkondo mwingine ambao utakiangusha maana chama ni wanachama na kama hawaaminiki basi hatuna chama.

Kwa hiyo tuachena na hizi hearsay, watu wengi wanasema ili wasikike ktk kugombea nafasi chache zilizopo hakuna zaidi. Kama wewe sii kiongozi wa chama una nafasi ndogo sana ya kugombea Ubunge, hata mikoani, Mwenyekiti au Katibu ndio hugombea Ubunge kwa sababu Ulaji upo katika Ubunge, hivyo kuwa kiongozi wa chama ni hatua ya kwanza kufikia Ubunge kwenye mshahara wa Mil.10 kwa mwezi, gari la mkopo na Posho zaidi ya Mil. 50 kwa mwaka.
\
This is where the problem lies! sio kosa la Zitto kumlinda Kafulila ama Mbowe kumsimamia Zitto miaka ya nyuma ndio maana watu kama Ben Saanane wanahangaika ovyo lknwamezimwa na bado hawakati tamaa pasipo kujua kwamba mfumo uliopo ndio unawajenga makundi ya kupeana na kulindana..
 
Mkuu Mkandara

Hili la nafasi katika chama nakubalina nawe. Nilishawahi kusema kuwa tatizo la vyama vya siasa nchini ni kufuata model ya CCM tunayoelewa imefeli.

Kwa mfano, mbunge wa CCM ni mjumbe wa bodi. Hivi hapo anawezaje kusimamia serikali akiwa ni mshiriki wa pande mbili

Tukaja kwenye suala la katiba, ikasemwa mbunge asiwe waziri.

Ni wewe Mkandara unayepinga uwepo wa watu katika nafasi tofauti unayeshabikia katiba ya Chenge na kumponda Warioba. Warioba slisema waziri asiwe mbunge, katika mfumo ule ule unaowatuhumu Chadema.
Hapa nina maana lazima tuwe wakweli kwa pande zote na tuache doubel standards

Suala la ukuu wa mikoa, haiwezekani mtendaji wa serikali akawa ni sehemu ya chama.

Warioba alipendekeza wakuu wa mikoa wapatikane kwa njia tofauti.

Hilo ukapinga na kusema Warioba jakuwa na maono, leo unawgeukia Chadema

Nakubaliana nawe kabisa kuwa chama kama CDM kilitakiwa kiwe mfano wa utaratibu mpya wa uongozi

Kuhusu hearsay, hapa nashindwa kukuelewa. Kitila na Zitto wamekubali kuwa wapo nyuma ya Waraka

Unaweza kuona maudhui ya Waraka yalivyolenga kuvuruga CDM.

Mizozo yote ya CDM ilikuwa katika model ya waraka wa Kitila na Zitto.

Unawezaje kusema ni hearsay wakati wahusika wanasema ni for real

Kuvumiliana kuna muda na kiwango. Walichokuwa wanafanya si kuvunja katiba bali kuleta matatizo ambayo ni kuvunja katiba.

Mfano, Kitila na Zitto walikuwa wanachochea Juliana amtukane katibu mkuu wa chama.

Kitila kaenda katika vyombo vya habari na kuandika 'vijana waachwe wabalehe' akimtetea Juliana.
Hivi huoni hata kama hakuna kuvunja katiba lipo tatizo kubwa kuliko kuvunja katiba? je hiyo ni hearsay

Katiba unayosema inatoa uhuru wa mawazo, sasa kwanini hawa watu hawakutumia uhuru huo usiovunja katiba kujenga hoja bali kutumia vyombo vya habari na uchochezi?

Mfano, unamjua Tuntemeke? Kazi kubwa ilikuwa kutulisha habari za ndani za chama chao.

Hajavunja katiba kwa kutumia jina bandia la Tuntemeke, je aachwe tu kwasababu anatumia jina lisilo lake hata kama analeta madhara?

Mfano wa pili, Mwigamba alikuwa na laptop akitoa habari za vikao vya ndani.

Leo unamtetea kuwa aachwe tu yeye na washirika kawasababu hawakuvunja katiba.

Hivi kutoa siri za ndani za chama si usaliti huo, na hukumu ya usaliti ni nini?

Mkuu, unakumbuka Mbowe alimkingia kifua Zitto ndani ya baraza kuu.

Unakumbuka katika tuhuma zote zinzomkabli kuhusiana na usaliti Zitto ametajwa wazi na hajaweza kuchukua hatua dhidi ya waliomtaja iwe kwa chama au serikalini, vipi leo useme ni hearsay?

Na mwisho, sijui kama unajua Mansour Himid alifukuzwa CCM kwa kusema anataka S3. Just to speak, hakuwa na waraka wala kikundi.

Hilo tu lilitosha kumuondoa, vipi leo uone mambo yanaweza kumalizwa kimya kimya ikiwa CCM unaowazungumzia hawakuweza kufanya hivyo

The bottom line ni kuwa ni wakati wa kujenga siasa za kileo si za kujificha, kuhujumu au kudanganya umma

Ni wakati wa kutenegeneza viongozi watakaosimama na kutetea kilicho cha kweli 'walk the talk'
 
Last edited by a moderator:
Ni wewe Mkandara unayepinga uwepo wa watu katika nafasi tofauti unayeshabikia katiba ya Chenge na kumponda Warioba. Warioba slisema waziri asiwe mbunge, katika mfumo ule ule unaowatuhumu Chadema.
Hapa nina maana lazima tuwe wakweli kwa pande zote na tuache doubel standards
Mkuu wangu sijashabikia katiba ya Chenge hata siku moja isipokuwa sikubaliani na hatua ya UKAWA kutaka serikali 3. Na nadhani nilikuonyesha gharama na hasara zake wakati ule tukibishana juu ya S3 na haswa hiyo katiba ya pili ilopelekwa bungeni.

Pili nilipingana na muundo ambao serikali kuu ina mamlaka katika mambo 7 ambayo hayahusu ukuzaji wamaendeleo Kitaifa wala ukusanyaji wa pato la Taifa ama uwajibikaji kitaifa isipokuwa ktk mambo ambayo hayaunganishi watu wake bali yanawatenganisha. Na tatu, kulikuwa na marais watatu jambo ambalo pia sikulikubali na nilikuonyesha kifungu chake pale ulipouliza.

Kwa hiyo yapo mambo mengi tu nakubaliana na tume ya Warioba na yapo ambayo kutokana na misingi ya ujenzi wa Taifa letu ingekuwa nakubaliana na Uhaini wa hali ya juu kufanyika dhidi ya waasisi wa Taifa letu. Hivyo nilikubaliana na CCM kwa sababu ambazo sio za kiitikadi wala kisera bali UTAIFA wetu. Na nikasema kama kweli mnataka serikali 3 basi haitawezekana leo wala kesho maana kuna hatua zake na ni lazima kwanza ipitishwe referendum kwa Tanganyika wakubali kujitenga, kisha izaliwe Tanganyika, iandikwe katiba yake ama irudishwe ile ya mwaka 1962. Kisha kutambulika kwa nchi hizi mbili tofauti UN halafu ndio wakae na kufikia muafaka juu ya mahusiano ya nchi hizi kufikia maridhiano mnayoyataka.

Hizi hatua zote za nini ikiwa sisi wananchi tuliitaka tu katiba Mpya kwa JMT na sio kuvunja JMT ili tupate nchi mbili? kama ingekuwa swala la kuvunja Muungano basi lingeenda peke yake wananchi wakapiga kura za NDIO au HAPANA badala ya kuhubiri katiba Mpya kumbe mnataka kuvunja muungano. Ni akili ndogo kutawala akili kubwa na hapo warioba nilimpinga na nitaendelea kupinga maana hatuna muda wa kuanza kugawana mbao.

Na mwisho nikasema sisi TANZANIA hatukuungana kwa ajili ya maghusiano ya Kiuchumi manaa yalikuwepo tayari wakati wa EAC. Waasisi wetu waliona haja ya kwenda hatua moja mbele toka mahusiano ya Kiuchumi hadi Kijamii maana tulikoeana kinasaba, leo mnataka kuvunja turudi kule kule tulikotoka kwa sababu ya watu wachache ambao wana sababu zao za kibaguzi.

Hapo mkuu sikuwa na UKAWA na sintokuwa na UKAWA kutokana na Uhaini huu wa kuvunja UDUGU wetu kwa sababu ya fedha. Ile ile asili ya Mwafrika masikini ukiona ndugu wanavunja udugu basi jua kuna swala la fedha. Ama kweli Nyerere mwaka 1962 alipokuwa waziri mkuu alisema - Adui mkubwa wa maskini ni Umaskini wenyewe. Sasa sisi badala ya kupambana na dhana hiyo ndio kwanza tunaiendekeza!..
 

Mkuu Mkandara
Si maudhui ya bandiko hii kujadili mambo ya muungano.
Hata hivyo, inabidi nizirejee hoja zako si kwasababu ni nzito bali zimejaa upotoshaji.
Ni upotoshaji huo huo ndio unaoendelea kwa kuaminishwa Zitto na wenzake hawana makosa



Wanajamvi tuwieni radhi kidogo, tunatoka nje ya mada natutarejea


1 Gharama za muungano wa S3 vs S2 tumezionyesha kwa kutumia model ya Warioba na Chenge.
Tanganyika itabeba gharama100% , Zanzibar 0%

kama hoja yako ni gharama kupungua znz uposahihi, kinyume chake gharama za katiba ya Chenge(S2) ni mara mbili ya Warioba.Tulikuonyesha


2 Mambo 7 yalilenga kutoa uhuru wa kukusanya na kutumia mapato kila upande kwa maendeleo yake.
S2, mapato ya Mtanganyika yanatumika znz, ya mzanzibar yanabaki huko. Kinachookusanywa cha Tanganyika


3. Znz haina mchango, kusema tunakusanya na kutumia pamoja ni sawa na wewe uchange sh 100 mimi 0 halafu tugawane sawa kwasababu tumechanga

4. CCM wanataka S2 kulinda masilahi yao, si kama usemavyo kuwa ni utaifa.

Huwezi kuua azimio la Arusha, ukageuza serikali danguro larushwa ukajinasibu una muenzi Nyerere.

CCM ya Nyerere si ya Chenge. Katiba Chenge ni ya kueleka pesa Uswiss, kama huo ndio utaifa unaozungumzia, hewala


5. Rasimu ya Warioba ilikuwa na marais 3. Katiba ya Chenge ina Marais 6 wengine wakichaguliwa kwa uzanzibar.

Makamu wote wa znz(4) niviongozi wa JMT, na mzigo huo anaubeba Mtanganyika anayehudumia muungano
Tunapata viongozi kwa uzanzibar
waliochaguliwa na kata moja ya mzimuni.

Katiba ya Chenge imetoa ajira kwa wznz, imewapa Watanganyika mzigo mzito kuliko walioubeba sawa


6. Katiba ya 1977 inatokana na ya mpito ya 1965 ambayo ilikuja kutokana na decree ya rais ya Rais, mambo yote ya Tanganyika ndiyo ya Tanzania.

Hata sasa katiba ya JMT ukiondoa neno znz ni yaWatanganyika.
Hawa wznz hawana sababu ya kuitumia kwasababu haiwahusu, nikiherere cha kutaka ajira.


7. Tanganyika haihitaji kura ya maoni. Wenye kelele ni wznzna wanaweza kuondoka leo bila tatizo.

Tanganyika haihitaji znz na hivyo kura yamaoni ni upuuzi. Uwepo wa znz ni kuwabeba, ni useless kwa Mtanganyika.

I mean znz is useless, ni fact hata wao wanajua ndio maanahawaondoki na kelele zao mwisho CHUMBE


8. Scotland haikuomba kiti umoja wa mataifa kabla ya kura yamaoni. England haikuambiwa ipige kura ya maoni.
wznz wakiona mambo hayaendei waondoke tu.Hakuna anyewashkilia kwasababu katika muungano wao ni mzigo na si asset, I meana useless na walaTanganyika haithiriki na kuondoka kwao


9 Hoja ya muungano kwasababu tumeoleana,sijadili. Ni kiwangocha chini nakuachia

10. Kama unadhani muungano utalindwa na S2, unajidanganya.
Watanganyika wameshaona na wanjua wao ndio muungano, mgongoni wameeba zigo la wazaznzibar


Muungano upo katika hali hii.
Wazanzibar watakisikiliza wanaambiwa nini na si kushiriki. Nadhani unaona walewaioko Dodoma wanavyoonekana vituko


Hivi mzanzibar anajadili gesi inamhusu nini? Hivi mznz anajadili mswada wa habari unamhusu nini?
Hivi mzn anajdili wizara ya ulinziana mchango gani.
Kwasasa wabunge wa znz ni kituko na unaona wanvyodharaulika.

Ni watu wanaojadili mambo kwa posho kwasababu hayawahusu. Hivyo, wana hiari yakuendelea kuwa washirika wa muungano au washirikishwa kama ilivyo na katiba ya Chenge inavyowatambua


Watanganyika hawatakubali tena kubeba mzigo wa wznz
Wameshaamka na sasa ni muda tu. Hapo ndipo S2 zinaweza kuuvunjamuungano kama glass.


Nadhani unaona wznz hata jamvini wamekimbia.
Wengi hawakujua kuwa znz haina lolote katika muungano Zaidi ya ukupe na utegemezi, useless


Waliaminishwa ni nchi ya kwanza kuwa na umeme na TV. Tume sasambuasiku hizi kimya, anayeongea ni Mtanganyika kwasababu yeye ndiye anajua uchungu nagharama za muungano.Siku zote watakapokaa alipokaa Mtanganyika wao ni inferior!

Yes inferior maana hawana kitu wanachoweka mezani Zaidi ya kudai vyeo na pesa.



Turudi kwa ACT
 
ACT WAFANYA UCHAGUZI

BANDIKO LIMEKAMILIKA

‘WARUKA KUNI WAKANYAGA MKAA'

Sehemu ya I


Mabandiko ya nyuma tulisema Zitto alikuwa mwanachama waChadema akilinda ubunge wake, kimatendo na fikra alikuwa mwanachama wa ACT.

Kwenda mahakamani ilikuwa kulinda tu ubunge wake ambao ni haki kusema , kulindamasilahi yake


Tulieleza kuwa Waraka ulimkusudia na kwamba, wenzakewalitangulia kumuandalia makao.
Hakuna tatizo katika hayo uliacha ubabaishajiwa kisiasa, ulaghai kama wa kutumia mahakama n.k
.

Tumeeleza hapo nyuma, Zitto hatakuwa mwenyekiti ili kuondoashuku kuwa alichokuwa anakitaka CDM ndicho anakipata

Tulisema pia, mgogoro wa ACT unatokana na ACT wahamiaji kumtaka ‘mtu wao' katika nafasi ya uenyekiti

Tukabainisha, harakati za kuvuta uchaguzi zilimlenga Zitto na kesi ya geresha mahakamani na kuwa, muda haukutoa nafasi wala matokeo ya zuiohayakuleta tija hasa baada ya kuvunjika kwa BMLK

Kilichotokea na kinachoendelea

Katika wiki moja ya uanchama, ACT wamefanya uchaguzi waviongozi.

Uchaguzi umekuja baada ya kikao cha darura cha kubadili ‘katiba' ilikuweka nafasi ya kiongozi mkuu wachama, nafasi iliyokuwa haipo bali kuundwadakika za mwisho


Hayo yamefanyika katika sababu kuu mbili

1 Ili kuondoa mashaka ya neno ‘mwenyekiti' linalomhusishaZitto na uenyekiti kule alikotoka na huko alipo.
Kumtenga Zitto na mgogoro wauenyekiti uliopo


2. Kutengeneza mfumo unaonekana tofauti kama tulivyoelezamabandiko matatu yaliyopita, tukisema vyama vya siasa vina mfumo wa ki-CCM.

Penginewanaliona hilo na kutaka kujitofautisha. Sija jambo baya kama wanasikilizamaoni ya watu


Hata hivyo, ni ukweli usio na shaka kuwa, katika wiki moja,Zitto amekielewa chama kiasi cha kuwa kiongozi mkuu.

Hili linaeleza hoja ya kuwa, Zitto alikuwa ACT siku nyingi hata pale alipkwenda mahakamani.
Nalotulilieleza na kuonyesha ulaghai wa kisiasa


ACT walamba matapishi

Inaendelea...
 
Sehemu ya II

ACT waruka kuni wakanyaga mkaa

Mgogoro wa ACT wahamiaji ilikuwa kuhusu umangi meza ndani yaChadema, kutofuatwa kwa katiba, kubadilishwa vifungu vya katiba kinyemela, nakukosekana kwa uwazi katika shughuli za kila siku za Chadema

Yaliyotokea

1 Kitendo cha kumuondoa mwanzilishi na wanachama wengine kwakuwafukuza, ndicho kile kile walichokilaani wakiwa wamefukuzwa Chadema

2 Kitendo cha kumpkea mtu na kumpa uongozi wa taifa kamamvua, ni umangi meza ule ule walioukataa wakiwa Chadema. Kwamba, chama kinawenyewe, sijui kwa hili ACT haina wenyewe kweli!

3Wamebadili vifungu vya katiba dakika za mwisho ili kukidh ihaja ya Zitto kuwa kiongozi.
Hatujui kama hilo halifanani na lile la kuongezamuda wa uongozi Chadema kinyemela


4 Kukosekana kwa uwazi katika kubadili mambo, hatujui kama hakufanani na malalamiko yale yale yaliyowaondoa

Ukitazama suala zima kwa ujumla wake, hitimisho linalopatikana ni kuwa akina Zitto na Kitila hawakuwa na madai halisi kama wanavyosema.

Kilichokuwa kinadaiwa ni Zitto kuwa mwenyekiti. Hayo waliyafanya
nyuma ya chadema wakichagiza vurugu

Sasa Zitto kawa mwenyekiti, bandiko letu haikukosea kilahatua ‘word to the letter'

Tutaichambua katiba ya ACT na kuona namna ilibyojengwa nakama udikteta waliosema umefikia kikomo.

BOMOA BOMOA INAANZA
ADUI NAMBA MOJA NI UPINZANI

Kiongozi mkuu ni Zitto na washirika katika uongozi ni Mwigamba.

Kitila anabaki kuwa nyuma ya pazia. Kazi ya Waraka imetimia japo si kama ilivyokuwa imepengwa.

Kutokana na yaliyotokea, ACT-waraka wakiongozwa na kiongozi mkuu wataanza kazi rasmi ya kuobomoa upinzani ili kujenga ACT


Hatua hiyo, ni muhimu kuliko kupambana na CCM. Ni katika kutimiza hasira, na kuhakikisha ‘wabaya' wao wanaanguka kisiasa. Suala la ujenzi wa taifa litafuta

Inaendelea...
 
Sehem ya II

Zitto amechaguliwa kama kiongozi mkuu kwa makusudi kabisa.Ndivyo ilivyokuwa, lakini kuna Zaidi ya hapo.


Ni Zitto atakayekuwa face ya ACT na hivyo kuvuta wanachama wengine, wenye kuelewa dira na sera, wanaochumia tumbo, na wanaoishi kwa mgongowa

Hili litatokea siku si nyingi na duru tunasema ni miezi michache. Ondoka ondoka hasa kutoka Chadema ni jambo linalkuja

Ingawa Zitto anaonekana kutozungumzia Chadema kwa jicho la ubaya, ni makosa kama Chadema hawatajiandaa kisaikolojia kama tulivyosema

Kutakuwa na kuhama kwa watu katika makundi tuliyoyasema nahapa tunayarudia

1 Kundi linaloamini katika Zitto kwasababu zozote zile. Hilihalizuiliki na wala halishawishiki.
Ni kundi litakalomfuata Zitto hasa likiona matarajio yamefikiwa


2. Kundi la wasiomwamini Zitto. Hili halitakuwa na habari naACT kwasababu haliamin na halina Imani na Zitto na washirika

3. Kundi lenye mashaka. Limegawanyika. Kwanza, wapo wanaotoabenefit of doubt.
Hawa wanaweza kuondoka kumfuata. Wapo wanaotoa doubt, haohawataondoka

Ondoka na hama hama itaathiri pia vyama vingine kwa namna fulani.Kutakuwa na mitafaraku, kujipanga kwa namna tofauti
.

Kinachotokea hapa si ukubwa wa Zitto kisiasa. Yatakayotokea ni matokeo ya ACT-waraka ambao ndio chanzo cha mitafaruku, na wanaujua upinzani kwani n sehemu ya walioandaa mbinu nyingi

Haki ya kushiriki siasa ni ya kila mtu. Tatizo ni pal haki hiyo itakaposaidia kuzuia malengo na kuleta sintofaham zisizo za maana na kuiondoa taifa katika agenda

Lile jinamizi lnaloumiza taifa kwa miaka 50 linanufaika likiendelea kusema kidumu chama cha mapinduzi.

Kama kuna wakati CCM wamepeta ahueni na watapata usaidizi, wakati huo ni sasa



Tusemezane
 
KAULI YA ZITTO JF

Kiongozi mkuu wa ACT ametoa kauli ya kutaka suluhu ya kisiasa na watu wawe wamoja kukabiliana na CCM

Ni katika wiki hizi, Zitto ametoa kauli au kunukuliwa katikamambo tofauti

Kwanza, alinukuliwa akisema yeye ni mwanzilishi wa ACT. Zittohajakanusha.


Na pili amenukuliwa akisema ACT imevuna wanachama wa CDM,kauli isiyokanushwa

Katibu mkuu wa ACT naye amenukuliwa akiwaandama CUF kamawapinzani wao

Siku za nyuma tumeeleza azma ya ACT ilikuwa kudumuza upinzani.

Tulisema, haki ya kujiunga au kuanzishachama cha siasa ni ya kila mtu na hakuna tatizo la ACT kuanzishwa


Tulisema, tatizo la nchi hii halijawahi kuwa wapinzani,tatizo ni miaka 50 ya kuvia na kudumaa kwa jamii kinaendeleo iwe kisiasa,kiuchumi au kijamii

Makosa ya nyuma yalikuwa wapinzani kupingana na kutoa mwanya kwa jinamiza CCM kuendelea kupumua

Tumesema, ACT wakianzisha vita na wapinzani, hawatafanikiwabali ni kuendeleza udumavu, uwe wa upinzani au wao wenyewe. Kwa hali ya ACTilivyo, kitendo cha kuwashambulia wapinzani kinawarudi

'Wafuasi waaminifu'wanakwazwa na jitihada za ACT dhidi ya wapinzai.
Hilo Zitto ameliona na ndio moja ya sabab za kutafuta' muafaka'


Kwa upande wa pili, kauli ya Zitto inaashiria kuhama kwa wafuasi wake siku za karibuni.
Hofu inayoikumba ACT ni kuwa, hama hama itahusishwa na hujuma na hilo litawatenga na jamii.


Zitto angeanza kuwakemea wafuasi wake, ingeeleweka.

Kitendocha wafuasi wake hata katibu mkuu kuendeleza vita na CUF na CDM hakionyeshi udhati wa kauli ya Zitto

Mtakumbuka tuliwahi kusema, yapo makundi 3 yenye mtazamo tofauti kuhusu Zitto

1 wanaoamini kwasababu wanaamini tu

2. Wasioamini kwasababu hawamwani tena

3 Wenye mashaka, wasiojua kama ni kweli au si kweli

Makundi hayo yapo wazi kadri tuavyokwenda mbele. Wapo wanaoamini kauli ya Zitto ni ya dhati.

Wapo wasioamini kwasababu hawa mwamini kabisa.

Na lipo kundi lenye mashaka, haijui kama litoe benefit of doubt au lifanye nini

Hili la tatu linamtesa sana Zitto. Ndipo hoja yetu inapokuwa na maana, unapokosa public trust unakuwa umepoteza sehemu kubwa sana ya uaminifu katika jamii

Tusemezane




 
KAULI YA ZITTO JF


Mtakumbuka tuliwahi kusema, yapo makundi 3 yenye mtazamo tofauti kuhusu Zitto

1 wanaoamini kwasababu wanaamini tu

2. Wasioamini kwasababu hawamwani tena

3 Wenye mashaka, wasiojua kama ni kweli au si kweli

Makundi hayo yapo wazi kadri tuavyokwenda mbele. Wapo wanaoamini kauli ya Zitto ni ya dhati.

Wapo wasioamini kwasababu hawa mwamini kabisa.

Na lipo kundi lenye mashaka, haijui kama litoe benefit of doubt au lifanye nini

Hili la tatu linamtesa sana Zitto. Ndipo hoja yetu inapokuwa na maana, unapokosa public trust unakuwa umepoteza sehemu kubwa sana ya uaminifu katika jamii

Tusemezane




[/COLOR][/SIZE][/FONT]

wewe upo kundi gani mkuu Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:
wewe upo kundi gani mkuu Nguruvi3

This has been an objective analysis, not a subjective debate. Wewe kama mshiriki ndio unatakiwa kuchagua upande, vinginevyo uje na hoja to challenge hoja zilizowasilishwa.

ACT (the party) is a vehicle to destroy the opposition in Tanzania. Mtu mwenye nia Ya dhati kuondoa ccm ilitakiwa aungane na wenzake kupambana na CCM, esp kwa kutumia fursa Ya mchakato wa Katiba mpya. Hajafanya hivyo, na Baada Ya Buzwagi, hana nia Ya dhati towards that end.

Hata Kinana is doing a better job to criticize Serikali Ya CCM than our fellow from the new "opposition".
 
Last edited by a moderator:
"Nimekuwa naeleza mitafaruku kwa ujumla wake.
Ukisoma bandiko 172 nimorodhesha matukio
yaliyotokea zitto akishiriki au akitajwa.
Ndio maana nilikuuliza swali moja, ni mtafaruku
gani wa CDM ambao Zitto hana mkono?""-@Nguruvi3
swali langu mkuu,vp mgogoro wa Amani Kaburu,Chacha Wange halishiliki?
Tuambie na Mbowe na Slaa migogoro mingapi wameshiriki maana imekua kama CDM yote ni Zitto
 
"Nimekuwa naeleza mitafaruku kwa ujumla wake.
Ukisoma bandiko 172 nimorodhesha matukio
yaliyotokea zitto akishiriki au akitajwa.
Ndio maana nilikuuliza swali moja, ni mtafaruku
gani wa CDM ambao Zitto hana mkono?""-@Nguruvi3
swali langu mkuu,vp mgogoro wa Amani Kaburu,Chacha Wange halishiliki?
Tuambie na Mbowe na Slaa migogoro mingapi wameshiriki maana imekua kama CDM yote ni Zitto

ha ha ha ....umeuliza maswali mazuri

ugomvi wa kaburu na chacha, Nguruvi hawezi kueleza maana ukimgusa chacha unagusa kila kasoro na baya la chadema ambalo limekuwa likilalamikiwa na kila mpenda mabadiliko

Ni hivi, Nguruvi pamoja na kuandika post ndefu ambazo huwa hakuna akili inayotumika kuandika bali mahaba yake kwa Mbowe, huwezi hata kidogo ukamuweka kwenye kundi la GT
 
Adharusi Mkuu Mchambuzialipokujibu sikuchangia tena, majibu yamstari wa kwanza yalijitosheleza

Pili, hatujadili nani kaleta mzozo gani. Hatujui nani kafanyanini, tuna kumbu kumbu za nani kafanya nini.

Bandiko linahusu
ACT ya Zitto,kiongozi mkuu na mwanzilishi akiwa chanzo cha mgogoro kambi ya upinzani


Hatuna kumbu kumbu kama Kaborou alikuwa na mtafaruku na CDM
.

Tunakumbu kumbu alirudi CCM akiwa katibu mkuu wa CDM bila mawaa, kuzawadia nafasin.k.

Jambo la maana alilofanya Amani ni kukaa kimya akitimiza haja zake

Chacha Wangwe, hakuna ushahidi wa wahusika. Kutaja watu kwatukio zito bila ushahidi ni kutowatendea haki wahusika.

Lakini pia hatujui nani alikuwa nyuma ya pazia.

Hatukujua nani anachochea mitafaruku hadi pale, masalia walipojitokeza, Ben Saanane,Mwigamba,Kitila na waraka.

Kama unakumbu kumbu mgogoro wa Wangwe walitajwa watu nyumaya pazia, Unawakumbuka?

Swali utakalouliza , je hii migogoro iliyomhusisha ZZK inaushahidi gani ?

Jibu ni rahisi, ndiyo zipo kumbu kumbu. Waraka, Bavicha,masalia n.k.

Sijui kama unapenda tueleze ushiriki wake kama ulivyotolewaau tuishie hapa

Mwisho, kama unajua migogoro waliosababisha akina Mbowe naSlaa, weka hapa, fanyaia uchambuzi.

Hilo ndilo lengo la majadiliano.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom