Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
- Thread starter
- #181
Mkuu umezungumza mengi yenye mantiki na kina sana. Ni kubaliane na baadhi ya hoja zako kuanzia chiniMkuu Nguruvi3, umeacha Funzo sahihi....si kwa Watanzania tu ,Waafrika kwa ujumla. NI KUDHIHIRIKA KWA 'IRRELEVANCE OF DEMOCRACY' kwa Mtu mweusi.
Nitaendelea kusema, Kidemokrasia si Zitto wala CDM waliokuwa sahihi.
Pande zote zilishakiuka misingi ya Demokrasia, si kwa bahati mbaya bali ni KUTOKUWA KWAKE NA MANTIKI.
Tunapokosea ni kutazama Ukiukaji wa upande fulani ni 'MAKOSA/MAPUNGUFU' yanayotakiwa kurekebishwa, wakati tunatazama ukiukwaji wa ule upande wa pili kama 'UHALIFU/CRIME' na kuushitakia kwa Umma. It is unfair!
Kwangu linapokuja suala la kukiuka kiapo cha Demokrasia, hakuwezi kuwa kosa hadi pale nitakapotambua DHATI yako, na si suala la Uadilifu bali DHATI.
Cha kusikitisha huwa tunapima dhati za watu kwa HISIA zetu, Uadilifu na Imani tu, na kusahau kuwa Dhati hupimwa na Relevance ya mazingira.
Kinachoendelea ni kupotea kwa Watanzania kwa vioja na vituko visivyoisha.... Asubuhi tutasikia, Sisi ACT ni wanademokrasia na wawazi, jioni wanapgana vijembe na kufukuzana.
Asubuhi utasikia Zitto ndio muanzilishi wa ACT, jioni utasikia Zitto kama foreigner kawatimua waanzilishi wa ACT.
Asubuhi utasikia sisi ni misingi, na jioni utasikia misingi ni batili. Ni porojo kwa kwenda mbele. Yote ni KUDHIHIRIKA KUSHINDWA KWA DEMOKRASIA.
Watz hatupaswi kuzungushwa hivi, tulipaswa ku-focus something. Huu ni ULEVI MZITO.
Tusipochukua hatua wajukuu wetu watakuwa wanapiga the same porojo.
Mkuu Nguruvi3, Maisha ni HESABU. Kamwe hakuna muujiza kwa ustawi wa Taifa. Maendeleo ni HESABU, si bahati na sibu.
Ni kweli tusipochukua hatua wajukuu watapiga same porojo. Huo ndio msingi wa wengine kusimama hapa na kujaribu kufwaeleza, wanaoamini, wanaosikia au wanaona. Wasio sikia hawatasikia
Pili, Watanzania hatupaswi kuzungushwa hivi. Ni kweli na ninawajibu wetu tupambane na wazungushaji kwasababu kupitia uzungushaji wao, ndipo wanaweza kututawala.
Tumewapuuza, wamefikia mahali milioni 10 wanaita pesa za chips dume, bilioni wanasema ni vijipesa katika kijaluba.
Wana haki ya kusema hivyo, wametuona wajinga, na tumewapuuza. ''The chicken have come home to roost''
Tatu, vioja ulivyo orodhesha haviishi,kibaya, vinaambatana na udanganyifu. Tunaambiwa fulani ni mzalendo, alikataa posho.
Mzalendo huyo huyo alikwenda mahakamani ili kuzuia ubunge wake kwasababu ile ile ya posho
Hapana! hivi ni zaidi ya vioja, ni utapeli na ndio unatusukuma kuwaambia wananchi, si kweli ukitoa kwa mkono wa kulia akachukua na wa kushoto, uzalendo upo wapi?
Nne,nikubaliane pia, pande zote zilikiuka misingi ya demokrasia. Na hili nimelisema sana.
Chadema walikiuka msingi kwa kuwa na madaraja.
Wapo waliohukumiwa mapema, na wengine wakipewa muda kama Zitto
Katika mazingira ya kawaida Zitto angeshahukumiwa na chama chake tangu alipoanza kutembea na barua ya kujiuzulu
Mbona madiwani walihukumiwa haraka? Mbona Juliana na Mwampamba hawakupewa fursa aliyopewa Zitto?
standard ipo wapi? Mbona vijana wa undergraduate waliotandikwa chale za makalioni waliadhibiwa, na mfadhili wao hakuadhibiwa. Huwezi kuwa na doube standards ukawa na demokrasia
Kwa upande wa Zitto, ni ''mwalimu'' wa demokrasia. Wakiwa nyuma ya pazia na akina Kitila/Mwigamba, demokrasia ya kusema na kutenda haipo. Walichochee maasi na vurugu kwa kofia ya demokrasia. kwamba, walihubiri demokrasia mchana usiku vurugu
Endapo wangejitokeza na kuzungumza wazi sioni tatizo. Tatizo ni pale walipotulisha dhana ya demokrasia huku wakitenda kinyume
Mkuu, tulikaa kimya kwa muda mrefu tukijua kuna somo.
Siku za karibuni, katika njia zile zile za ulaghai tumesoma mengi ya kuchosha. Mengine ya kupotosha na mengine yasiyo na ukweli
Hapana! tkukikaa kimya uhuni ukichukua nafasi ya demokrasia ni kutotenda haki kwa jamii
Nikubaliane nawe katika Tanzania na Afirka demokrasia ni dhana ngumu. Lakini wapo walioweza,kwanini sisi tushindwe?
Waziri mkuu wa kwanza wa Singapore hayati LKY ameibadili nchi masikini kuwa nchi ya dunia ya kwanza kwa miaka 50
Tumeshindwa kuondoka katika kundi la nchi masikini duniani kwa miaka 54
Tatizo si wananchi, ni matapeli wanaotumia ujanja wakivaa ngozi za kondooo kumbe ni mbwa miwtu
Hatujashindwa, tunaweza kuanza sasa. Pa kuanzia si kusota vidole CCM tu, ni kujenga misingi ya kuwajibika, kuwajibishana na kuwajibishwa. Ni kuanza sasa ili kizazi kijacho tupate akina LKY wa Tanzania
Tukiendekeza magenge ya matapeli, kuyatetea magenge kwa ngojera, ngano na mashiri, tunajidhulumu na kudhulumu wajuu zetu
Tusemezane