Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Mkandara ,unakosea ukisema ACT imetokana na kufukuzwa kwa watu Chadema.

Kwa taarifa yako ACT imekuwepo ni jina tu halikuwa wazi.
Ule waraka wa matusi wa akina Kitila, Zitto na Mwigamba ndiyo ACT yenyewe.

Chama kilikuwa kina operate underground kwa malengo husika, ni kwa sasa tu umeweza kuwaona kwa uwepo wa supreme leader. Jina hilo llilitumika katika waraka wa ACT(ndani ya CDM) kama MM ikimaanisha mhusika mkuu

Pili, hoja hapa si kuvunjika kwa upinzani, ni ile tunayosema kila siku. Haiwezekani turudi miaka 20 nyuma kila siku.

Ndivyo NCCR walivyokuwa, CUF walivyokuwa. Matatizo yote yalitokana na watu kuaminini ni kazi ya 'mungu'
Mchambuzi kaeleza, Mag3 kadadavua. Hii ilikuwa kazi ya watu kwa malengo maalumu(mission)

Jukumu ni kuufahamisha umma yanayozungumzwa ni ulaghai, ipo mission. Ilishtukiwa sasa inafanyika wazi.
Hilo tu, wala si kuiandama ACT au kuilamu ni kuupa umma habari zinazojiri

Tunaeleza kwa kina kile kilichotokea ili kuchuja kati ya pumba na mchele. ACT kuwa chama na kugombea nafasi ni haki yao
Hata hivyo haki hiyo inakuja na maswali na ndiyo tunadadavua.

Mfano, kitendo cha Zitto kusema anachukua mkoa wa Kigoma au majimbo ya upinzani, halina tabu.

Tunajiuliza hivi miaka 50 nani adui wa mtanzania? Na kwamba majimbo ya upinzani yakichukuliwa hilo litaondoa jinamizi la CCM linaloitesa taifa? Zitto lishindwa na sasa anawezaje? Tunahoji tu.

Tatu, katika kuufahamisha umma, hatutakwepa hoja za wahusika. Hatuwezi kukaa kimya utapeli ukitamalaki.

Ni Zitto huyo aliyesema yaliyopita si ndele tugange yajayo. Akasema lengo lao ni kupambana na CCM.

Katibu mkuu ACT anasema lengo ni CUF, Supreme leader anasema ni NCCR, huku kukiwa na tambo za majimbo ya kahama, Kawe na ubungo kuwalenga CDM. Unaweza kuona nguvu za ACT ni dhidi ya nani. Je hilo ndilo unalitaka liwe?Hawa watu wanasimamia wapi?

Unawezaje kuwa UKAWA ukapambana na ukawa ukiacha Ilala, Temeke, na Kindondoni salama salimini? Hivi hili halielezi jambo kweli!! Tunapohoji haya tunaambiwa tunatetea vyama au tuna chuki.

Tunachotakiwa ni kuserebuka kwa hoi hoi nderemo na vifijo tukimpokea supreme leader.
Hatutakiwi kueleza tatizo lililopo. Leo tunaambiwa Zitto kafukuzwa CDM, basi inaishia hapo

Hatuelezwi mazonge zonge yaliyosababisha kuondoka kwake. Huyo mke unayeongelea anapotoka nje na kusema kapewa talaka, ni mwendawazimu tu atakayekubali bila kuhoji, kulikoni? Hatutakiwi kueleza kulikoni, kufanya hivyo ni chuki!.
Tunatakiwa kulia na mama aliyechepuka kama Mwalimu alivyosema.

Leo wanahubiri kufukuza wanachama kwa kushabikia UKAWA.

Ni hao hao walisema suluhu ya matatizo ni vikao na si kufukuzana. Wanatenda walichokikataa.

Wamebadili katiba kwa saa 24 kumpata supreme leader, wanaeneza habari kuna udikteta walikotoka. wanahubiri wasichokitenda.

Ni hao hao walisema demokrasia ya sanduku la kura ni muhimu. Leo wanampata supreme leader kiaina

Wakaaminisha umma chama kinajengwa kwa misingi ya katiba na kuvumiliana.

Ni hao hao wamegeuza katiba 24 hr kwa maoni ya mtu, wakabandika kipengele cha supreme leader.

Wakiwa majukwaani wanasema kipengele cha muda wa uongozi walikotoka kilinyofolewa kinyemela.
Hawawelezi kipengenele cha supreme leader kiliingizwa kinyemela.

Tupo hapa kueleza utapeli wa kisiasa. Tumekaa kimya miaka 50 kwa maumivu, siku hizi CCM wanaiba kisha wanastaafu.

Tusiposimama na kukemea matapeli,tutakluwa tunazalisha matapeli.

Tuanze lini kama si leo na kwa matapeli gani kisiasa waliojidhihiri zaidi ya hawa?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Nguruvi3 na wadau wengioe. Binafsi sioni haja ya kuihusisha ACT juu ya kifo ama uhai wa Upinzani Tanzania.
Mara zote huwa nasema, Wanasiasa wetu hawapaswi kupigania HISIA za watu bali kukubalika ndani ya FIKRA za hao watu. Kwa maana HISIA/MAHABA huanguka wakati wowote, lakini MANTIKI kamwe haitoanguka ila tu kulingana na nyakati na mazingira, hubadilika.

Sasa ipi ni Sura ya Upinzani Tz? Je, Upinzani upo katika mahaba yetu au Fikra zetu? Kama ni vichwani mwetu na si mioyoni mwetu, kufikiria tu kwamba unaweza kuanguka ni USALITI. Utakuwa umeisaliti nafsi yako mwenyewe!

Upinzani uliopo kichwani unapoanguka, basi HAUKUWEPO! Ila tu lilikuwa wimbi la Ushabiki wa watu na Mahaba yao, zao la Hisia zao! Acha upotee!

MANTIKI INAZIDIWA NA MANTIKI SI HULKA.
Nafsi zetu ndio adui yetu wa kwanza katika Unyonge wetu, kwa maana ndaniye imo MANTIKI na HULKA zituongozayo kufanya maamuzi.
Hili ni sawa na Chekecho, tusione tabu kuanza upya tutakapogundua fuko tulilobeba ni pumba tupu. TUANZE UPYA, KWANI MAENDELE NI HESABU NDEFU SANA.
Anaita sasa!
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3,

Sawa tuseme unayoyasema ni kweli.. Je kama Hawa wasingefukuzwa Chadema wangefanya nini kinachofuata maana mwizi mkamate katika wizi wake sio kumuona mtu alokusudia kuiba ukamkamata hata hajafika katika kitendo cha wizi. Na ndivyo wezi hukamatwa na nilidhani Chadema ni kubwa kuliko maamuzi ya mtu mmoja au kundi bali ni chama kinachotaka kuchukua nchi na watatunga policies zenye haki na usawa. Maamuzi yangetafsiri uwezo wao wa ku deal la vitu kama hivi Kitaifa kama watapewa ridhaa hiyo. Kwangu miye nisojua yalokuwepo nyuma ya bpazia imenipa picha mbaya ya uongozi wa Chadema kuwa hawana tofauti na tulokuwa nao leo Kitaifa.

Jambo la Pili, Ingekuwa tamu zaidi kama hila hizi zingepelekwa Baraza kuu zikajadiliwa maana tumeona kumbe hawakuwa wengi hivyo, bali kundi dogo sana la watu. Na pale wajumbe wote wa Baraza kuu wangeambiwa na kupewa ushahidi kisha wakaitwa hawa jamaa kujieleza. Maamuzi yangetokana na Baraza kuu kama kanuni inavyosema na ingewamaliza kabisa Kisiasa na Kitaifa badala yake wamepewa nyenzo mkononi. ndio maana nasema kama ACT ni mpini basi mpini huo umetokana na mti huu wa Chadema yenyewe. K Mkuu sisi wote tunafungwa na sheria na hakuna watu walokuwa juu ya sheria, hivyo nilipingana na maamuzi yale kwa sababu za msingi kabisa...

Listen, mnadhani mnaijua Chadema na watu waliopo sasa madarakani lakini nasema hamuijui kabisa. Wapo watu wameingia kwa maslahi yao ama nje kabisa na kupoteza dira ya Chadema, hivyo ilibidi Chadema kujitazama upya wapi wanaelekea na hawa waloingia chama kutafuta umaarufu tuta deal nao vipi. leo nashangaa mtu kama Mag3 ananiita mimi Mnafiki kwa sababu tu nimeyaona makosa! Unafiki ni nini kama sio Mtu muongo, asoaminika na hata akiaminika hatimizi wajibu, anayetoa ahadi asizitimize.. Huu ndio Unafiki na hapana mahala nimekiuka matarajio ya watu katika mambo hayo.
 
Nguruvi3,

Sawa tuseme unayoyasema ni kweli.. Je kama Hawa wasingefukuzwa Chadema wangefanya nini kinachofuata maana mwizi mkamate katika wizi wake sio kumuona mtu alokusudia kuiba ukamkamata hata hajafika katika kitend cha wizi. Ndivyo wezi hukamatwa na nilidhani Chadema ni kubwa kuliko maamuzi ya mtu mmoja bali chama kinachotaka kuchukua nchi. maamuzi yangetafsiri uwezo wao wa ku deal la vitu kama hivi Kitaifa. Kwangu miye nisojua yalokuwepo imenipa picha mbaya ya uongozi wa Chadema.

Jambo la Pili, Ingekuwa tamu zaidi kama hila hizi zingepelekwa baraza kuu maana tumeona kumbe hawakuwa wengi hivyo bali kundi dogo sana la watu. na pale wajumbe wote wa baraza kuu wangeambiwa na kupewa ushahidi kisha wakaitwa hawa jamaa kujieleza. Maamuzi yangetokana na Baraza kuu kama kanuni inavyosema.. Sisi wote tunafungwa na sheria na hakuna watu walokuwa juu ya sheria, hivyo nilipingana na maamuzi yale kwa sababu za msingi kabisa...

Listen, umnadhani mnaijua Chadema na watu waliopo sasa madarakani lakini nasema hamuijui kabisa. Wapo watu wameingia kwa maslahi yao na kupoteza dira ya Chadema, hivyo ilibidi Chadema kujitazama upya wapi wanaelekea na hawa waloingia chama kutafuta umaarufu tuta deal nao vipi. leo nashangaa mtu kama Mag3 ananiita mimi Mnafiki kwa sabau tu nimeyaona makosa! Unafiki ni nini kama sio Mtu muongo, asominika nahata akiaminika hatimiz wajibu, anayetoa ahadi asizitimize.. Huu ndio Unafiki na hapana mahala nimekiuka matarajio ya watu katika mambo hayo.
Mkuu Mkandara , kwanza nikufahamishe kuwa hoja zetu zinasimama katika umma.

Pili, kama kufukuzwa kwa ACT ni makosa na udhaifu wa CDM hata kukutia mashaka,ungeangalia begani kidogo.

CCM chama kikongwe kimeshindwa kusuluhisha mgogoro wa Mansour Himid hadi kumfukuza

Mansour hakuandika waraka, hakutukana mtu, alitofauatiana na msimamo wa chama, dhambi kubwa! kafukuzwa
Na CCM hiyo unayosema ndiyo imeshika dola, vipi uone kengeza kwa upande wa CDM kwa hatua zile zile

Tatu, hawa akina Zitto na Kitila wamehusika kuleta migogoro wakichochea vijana na makundi mengine.
Kufukuzwa unaona taabu, vipi wao wanapomtishia mtu atakayesema 'UKAWA'' Mbona hilo hulioni kama tatizo

Nne, kufukuzwa kwa wanachama ni hatua nzuri sana ya kujenga kizazi kipya. CDM walifukuza madiwani n.k.

At least unaweza kusema kuliko CCM wanaolea wezi kwa njia za kustaafu, wezi kuandika katiba, na wezi kugombea urais. Hayo ni matokeo ya bureacracy ya kuogopana na kukaa vikao.

CCM wanakaa vikao Lumumba na Dodoma kila mawio na machweo, angalia wimbi la majambazi na wezi linatoka sehemu gani. Ni lazima ifike wakati sisi kama taifa tuangalie njia nyingine na mtazamo mwingine. Hizi fikra za kuamini Zitto ni supreme leader wa nchi na si ACT, hapana! Hizi fikra za kuamini mtu na si taasisi, hapana!

Tano, sheria iliyotumika iliandaliwa na Kitila ikasimamiwa na Zitto katika masuala mengi tu.
Hakuna siku walilolalamikia. Vipi sheria hiyo iwe tamu kwa madiwani na kwao iwe shubiri?

Sita, baada ya kukiukwa kwa taratibu unazosema za baraza kuu, Zitto alikwenda kwa baba hakimu.
Mzee hakimu kasema, hapana, umekosea haki imetendeka.

Sasa wewe ni haki ipi unayozungumzia tena zaidi ya ile ya mahakama?

Mag3 kasema ni mnafiki si kama tusi. Mkandara, huwezi kudai haki ya Zitto kwenda baraza kuu bila kulaani ule waraka wa matusi. Huo ndio unafiki. Huwezi kusema Zitto kafukuzwa, wakati unajua walishajifukuzisha walipoanzisha ACT ndani ya chama.
Huwezi kusimama na kudai CDM wamekosea kuwafukuza, ukaa kimya kwa CCM kumfukuza Mansour kwa sababu laini na si waraka

Mwisho, kwa hakika mimi sielewi CDM, naelewa hoja zinazotokana.

Ni kwa msingi huo, hao CDM wakicheza fyongo tutawaanika tu.

Tutawaanika kama tulivyowahi kuwaeleza mwaka 2011 kuwa Zitto ataporomoka na chama.

Kwamba kama CDM ni Zitto lipo tatizo. Tuliwaonya kuwa Zitto hakuwa asset alikuwa liability leo wanaona ukweli.

Tunataka siasa za kileo, si siasa za kwenda mahakamani kutafuta haki ya demokrasi kumbe ni ya tumbo la mtu

Kama hatutaanza leo, tutarithisha kizazi kijacho matatizo tuliyo nayo miaka 50.
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3,

Mkuu hivi kwa nini mnachukulia CCM kama mfano bora wakati wananchi wamechoka na chama hicho? kwa nini Chadema isiwe tofauti na kuonyesha uwezo mkubwa zaidi wenye kufuata sheria.. Huyu Mnsour Himid alikuwa nani CCM kiasi kwamba awe na impact kwa chama kama ya hawa jamaa?

Na hii habari ya fukuzana ndio sikubaliani nayo hata wao ACT siwaungi mkono katika hilo ikiwa kweli huyo Mwenyekiti kasema kuna fukuza fukuza ya wananchma maana mimi naamini chama ni wanachama wenyewe, Chama pasipo wanachama hukuna chama. Na ndio maana wameweka sheria ya idadi ya wanachama kutoka kila jimbo kuwa kiambatanisho muhimu cha usajili. Pasipo hao huna chama sasa unapokuja andikisha chama kwa sababu yao, kisha ukipata usajili unaanza kufukuza wewe nani kama sio kukifanya chama ni mali yako?..sijui kama nimeeleweka.

Kwa hiyo hoja yangu sio kuwatoa makosa ACT maana hoja nyingi humu nazisoma toka kwa waandishi ambao nashindwa kuthibitisha maneno yao. Kama nakumbuka siku ya uzinduzi wa ACT moja ya kanuni yao inasema hakuna kufukuzana wanachama, sasa hili la kufukuzana limetoka wapi mimi sijui na hapo inanipa shaka aidha na mwandishi JF ama huyo Mwenyekiti juu ya uelewa wao maana ilisomeka kwamba hata Mwenyekiti alitaka kujua yeye na Kiongozi mkuu wa taifa nani mwenye mamlaka zaidi.. sijui kama kuna ukweli au laa..

Mkuu kanuni za Chadema tumezisoma sisi wengine sijui wewe, Diwani sio mjumbe wa kamati kuu, labda awe lakini swala la kuondolewa madarakani viongozi wa kamati kuu limeelezwa vizuri tu hata kama sheria hiyo ilitungwa na Kitila na Zitto maadam ilikubaliwa na baraka kuu hilo tena linabakia hadithi nani kaandika. Ukisha chaguliwa kuwa kiongozi wa kamati kuu huwezi kuondolewa madarakani ktk jambo kama hilo pasipo kupitia Baraza kuu. sababu ya sheria hiyo ni kuepusha viongozi kuumbuana ama kufanya maamuzi kinyume dhidi yao wenyewe - Outside body has to deside (sheria nzuri kabisa)...Maana hawa binadamu na hawawezi kufikiria sawa na misuguano lazima itakuwepo. Kilichofanyika ni tofauti na sheria imewaumbua kiasi kwamba Dr.Slaa alidiriki kusema mjadala huo umefungwa asisikie mwanachama yeyote wa Chadema akijadili tena.. Amri ilitolewa.

Mkuu niliusoma ule waraka na matusi yalokuwemo yaliandikwa na mtu mwingine sio Zitto, disciplinary measure ingechukuliwa na Baraza kuu ndivyo kanuni ilivyotaka na tungeujua ukweli zaidi kuliko hizi hearsay na kufunika kombe kama CCM wanvyofanya katika mambo muhimu kabisa. Hata mitaani leo wewe ukionekana na kosa la kumkashifu rais utakamatwa na ni kazi ya Mahakama kukuweka hatiani, Polisi au TISS watakusomea mashtaka yao na utapekwa mbele ya sheria. Kamati kuu ilichukua mamlaka mikononi mwao na ndio nilichopinga mimi. Polisi wetu na TISS wanakiuka sheria kila siku nna tunalalamika iweje nasi tufanye vivyo hivyo! kosa gani nilolifanya na huo Unafiki uko wapi hapo.

halafu basi, mwisho wa yote mimi nilichokitaka ni AMANI kuondoa chuki na kuwekana sawa juu ya malengo ya chama yawe mbele yasipotoshwe na mambo madogo kama hayo, lakini nyie mmekubaliana na ujenzi wa chuki kama ndio maamuzi ya maana sana. Tumefundishwa Love and Forgiveness na hapana mahala pa kuonyesha unyenyekevu huo kama ndani mwako.

Safi kabisa kuwa neutral katika hoja lakini sidhani kama kweli una nia hiyo hata kidogo. nakusoma vizuri mkuu wangu kama unavyonisoma miye. Tunachotofautiana tu ni Chanzo na Matokeo, wewe umeamua kusema chanzo ni Zitto nami nasema chanzo ni CDM, hivyo pokea sababu zangu kwanza na uamini kuna ukweli ama zikatae kwa kuonyesha ukweli ni upi...
 
Hivi Nccr,Tlp na Cuf zilizoitwa mpini wa CCM dhidi ya upinzani ule mpini ulikatika na kuwa si mpini tena na kwamba mipini ile imegeuka vyama vya upinzani vyenye lengo la kuindoa CCM madarakani?
 
Mkuu Mkandara, nimerudi japo kwa muda mfupi. Naomba nijibu baadhi ya hoza zako kadiri muda utakavyoniruhusu kama ifuatavyo;
Mkandara said:
Unajua mnasiitisha sana nikiwasoma maana kama vile hamjui siasa? sasa ACT imekuja kuvuruga Upinzani kivipi, chama ni wanachama na hunadi itikadi na sera zake ili wapewe nafasi ya kuongoza nchi. Ushindi unatokana na wananchi kuwakubali kwa kile mnachosimamia, iweje ACT ije kuuwa upinzani ikiwa itikadi na sera zao zinatofautiana? Je, Ushindani wa vyama ni kuvunjana au mlitaka mfumo wa chama kimoja maana siwaelewi kabisa.
Granted, yawezekana ni kweli unavyotusoma ni kama vile sisi wengine hatujui siasa ila naomba nikuulize maswali kadhaa, wewe unadhani ACT iliazishwa lini, na watu gani na kwa malengo gani miaka zaidi ya ishirini na miwili baada ya mfumo wa vyama vingi kuanzishwa? Je unadhani katika mtindo huu tutafika? Yaani kila Uchaguzi Mkuu unapokaribia vyama vipya huibuka? Mwaka 2010 kuna chama (CCJ) kilitaka kuanzishwa na waliokuwa viongozi waandamizi ndani ya CCM lakini kama kawaida juhudi zao zilizimwa na hata usajili walinyimwa. Hilo moja lakini la pili ni kwamba Supreme Leader wa ACT alikuwa kiongozi mwandamizi ndani ya chama Kikuu cha upinzani, Chadema, na mwanachama kwa miaka mingi tu lakini ACT iliweza kupata usajili wa haraka bila hata katiba yake wala viongozi wake kujulikana.

Katika kujitangaza, ACT walijipambanua kuwa lengo lao kuu kama alivyotufahamisha Mchambuzi si kuitoa chama tawala madarakani bali kuipiku Chadema na kuwa Chama Kikuu cha Upinzani. Majimbo ambayo waliahidi kuelekeza nguvu zao kuzikomboa ni yale majimbo yaliyokuwa tayari mikononi mwa Wapinzani baadhi yake ikiwa Mwanza, Dar es Salaam, Iringa na Mbeya. Nadhani swali lako la lengo la ushindani wa vyama mpaka hapo limejibiwa na kama bado nikukumbushe tu matamshi ya Mwenyekiti wa ACT, "mwanachama wa ACT atakayeshabikia UKAWA atachukuliwa hatua". Kwa nini asitamke kuwa mwananchama yeyote wa ACT atakayeshabikia chama tawala, CCM, atachukuliwa hatua?
Mkandara said:
Na mnaposema Upinzani mna maana gani maana kuna vyama 22, hiyo UKAWA yenyewe vyama vitatu sijui vinne waloungana, Je wao hawakuvunja Upinzani? Ni kipimo gani mnachotumia kuusema Upinzani ni huu maana vyama vyote 21 kasoro CCM ni Upinzani, iweje mchague vyama vitatu tu na kuuita Upinzani mkaviacha vyama vingine 17 vilivyokuwepo hata kabla ya ACT? vile vyama walivyoviacha nje ya UKAWA havikuwa Upinzani isipokuwa wabunge wa Chadema, CUF na NCCR..Na Mrema kwa nini walimwaga UKAWA? sababu gani na kupitia sheria zipi..Je, Hivi vyama vilivyoachwa nje wakiamua kuungana na kuunda umoja wao watakuwa wamekuja kuvunja Upinzani pia sio? ama wao itakuwa tofauti..nani alowapa ridhaa UKAWA kuwa na mamlaka ya kusema nani awe nao nani asiwe nao ikiwa wote lengo lao ni kuindoa CCM madarakani..
Hapa Mkuu hapa unasema uongo, sijui ni kwa makusudi gani! Je kuna masharti yoyote yaliwekwa kabla ya kujiunga na UKAWA? Nina hakika hakuna chama kilicholazimishwa kujiunga na UKAWA na vilivyofanya hivyo vilifanya kwa hiari yao wenyewe. Unapouliza iweje mchague vyama vitatu tu na kuuita Upinzani mkaviacha vyama vingine 17 vilivyokuwepo hata kabla ya ACT una maana gani Mkandara? Je NLD unaiweka katika kundi gani? This is being more than disingenuous! Hakuna vyama vilivyozuiwa kujiunga na UKAWA ila kuna vyama vya Upinzani vilivyoamua vyenyewe kutounga mkono UKAWA, je kuna ubaya gani hadi hapo? Ni wapi UKAWA ilijipa mamlaka nani asiwe nao? Huu upotoshaji una lengo gani?

Hapana Mkuu, birds of a feather fly together...ndege wafananao huruka pamoja. Wengine labda ni ulafi wao tu wa kula posho uliwafanya wasiunge mkono kususia BMLK ya Sitta/Chenge. Wengine labda ni unafiki wao, wengine kama Mrema labda ni katika kulinda maslahi yao waliyoyaweka mikononi mwa CCM, wengine kama Cheyo labda ni woga wao wa kuandamwa, wengine labda ni ushawishi wa rushwa...nani anajua? Walikuwa na sababu zao za kutojiunga na UKAWA na kwetu wengine tunaelewa vizuri kabisa hofu yao.
Mkandara said:
Nitasema moja tu ya kwamba ACT isingekuwepo kama Chadema wasingewafukuza Kitila, Mwigamba na Zitto. Hivyo maadam Chadema waliona umuhimu wa kuwafukuza wakijua fika kwamba hawa watu ni wanasiasa, kuondoka kwao wataunda chama chao lakini haitakuwa tishio kwao, basi hakuna sababu ya kulalamika leo maana Chadema walijua na walitegemea haya kutokea. Tulionya mkasema Chadema haiwategemei wao waende wanakotaka Chadema Imara, sasa uimara huo unaogopa mpini tu pasipo hata shoka lenyewe....Alaa kumbe Upinzani ni gogo la mti lilosubiri kupasuliwa bahati mbaya tawi lake limejengwa kuwa mpini!..
Kweli ukipenda chongo utaita kengeza.. Mkandara ni hivi, Zitto, Kitila na Mwigamba walipanga kuihujumu Chadema toka mapema kama walivyokiri Kitila na Mwigamba ama kwa kufanya mapinduzi ndani ya Chadema au kwa kuidhoofisha kwa kuwagawa wanachadema. Uzi upo humu ndani unaoelezea mpango mzima ulivyoasisiwa na ulivyopangwa kutekelezwa. Swali ni hili, je walipogundua kwamba Chadema inakoelekea siko kwa nini hawakujiondoa tu na kuanzisha chama kipya, kwa nini waliamua kuihujumu Chadema wakiwa bado wamo humo humo? Kwa hakika lengo lao halikuwa na nia njema kwa Chadema bali kuiacha imevunjika vipande vipande.

Zitto kuing'ang'ania Chadema hadi kuipeleka mahakamani ni mpango ulioandaliwa mapema sana na kwa ustadi mkubwa katika kuhakikisha shughuli za chama zinadumaa. Act ilikuwa ianzishwe come what may ila kwa Chadema kuchukua hatua waliyochukua kulitibua what would habe been a very embarrasing situation kwao. Zitto alikuwa anasubiri tu muda mwafaka kujiondoa Chadema kwa sababu bila yeye ACT was nothing...Kitila na Mwigamba hawana ushawishi wowote wala rasilimali za kuweza kuanzisha chama kipya. Swali linalojitokeza hapa ni nani alikuwa nyuma ya hizo rasilimali, nani angefaidika na kudhoofika kwa chama Kikuu cha Upinzani.
Mkandara said:
Unapomtalakia mkeo, tarajia ya kwamba ipo siku atakuja olewa na mume mwingine. Na haolewi ili akuvunje nguvu wewe bali amefanya maamuzi hayo kwa kutazama maisha yake mwenyewe, yeye kasonga mbele nawe songa mbele usitazame sana maisha ya mtalaka wako. Yote mnayomsema humu Zitto hayana ubaya isipokuwa yeye anaposema ndio mnachukulia -Unaona kasema hivi na vile lakini ya kina Mbowe, Mnyika na Lissu ni maneno matamu sana..
Duh! Hii kali, hiyo ya mke kupewa talaka sidhani kuna haja ya kujibu...Ila nilitaka kukuambia jambo moja Mkandara, kuna mahali umetoa mfano wa Lowassa kwa kumfananisha na Zitto na kudai kuwa CCM, kwa hekima, haitamchukulia hatua ili kulinda umoja ndani ya chama. Naomba nikukumbushe kitu kimoja...pamoja na shutuma zote anazoelekezewa, Lowassa ni moja katika wananchama walio waaminifu kwa CCM. Lowassa hajawahi kutaka kuanzisha chama, hajawahi kufikiria kujiondoa CCM na hajawahi kuusifia Upinzani hata mara moja. Lowassa angetaka angekuwa keshaivuruga CCM na hivi sasa ingekuwa vipande vipande. Lakini pamoja na shutuma na matusi kutoka kwa vijana wasio na adabu kwa wazee wao, bado ni mwana CCM na tofauti na wanafiki kama Sitta/Mwakyembe hajawahi kufikiria kujiondoa CCM. Huo ndio ukweli. Huwezi kumlinganisha Lowassa na wasaliti kama Zitto.
 
Mag3,
Nitakujibu baadaye muda tena maswali ni mengi sana na mengine umeyatolea majibu yako hivyo inakuwa vigumu kuuliza swali wakati tayari wewe unayo majibu yako. Kifupi tu ya swali la kwanza. nikikusoma vizuri umeonyesha vyama huundwa kila Uchaguzi ina maana ACT imeundwa kwa sababu ya Uchaguzi huu, lini kimeundwa sijui isipokuwa nakumbuka Kitila na Mwigamba walitoa taarifa hiyo mwaka jana tu baada ya kufukuzwa. Aidha waliisha jiandaa kabla lakini inanipa shaka na watu waliotoka Chadema. Vyama huzaliwa kimsimu mahala pote duniani nako ni wakati wa Uchaguzi hilo elewa kabisa. na tulizoee kila mwaka kabla ya Uchaguzi lazima kutatokea vitu kama hivi.

Watu wengi walioondoka Chadema wakati ule ni kutokubaliana na kufukuzwa kwa hawa wajumbe kinyume cha Sheria. I myself nilipinga maamuzi hayo bila kujua kama ACT tayari ilikwisha undwa ndani ya chama au laa!. Na hata hivyo hesabu yao pekee inanipa shaka ya mbinu mnayohofia ila pengine utofauti wa mawazo yao inanipa tumaini kwamba walitofautiana sana na viongozi wa Chadema juu ya Itikadi - UJAMAA vs UHAFIDHINA na pengine ndilo tatizo kubwa lilokuwepo.. Just thinking though..
 
Mag3,

kama Upinzani sio UKAWA inakuwaje mnasema ACT ni mpini wa CCM kumaliza Upinzani? - Upinzani upi, ikiwa wao pia ni upinzani..UKAWA iliundwa vipi? hayo kwanza tumalize hapo tuingie mengineyo.
 
Mkandara;12473439]Nguruvi3,

Mkuu hivi kwa nini mnachukulia CCM kama mfano bora wakati wananchi wamechoka na chama hicho?
Huyu Mnsour Himid alikuwa nani CCM kiasi kwamba awe na impact kwa chama kama ya hawa jamaa?
Mkuu nimetoa mfano wa CCM kwasababu ya hoja yako kuwa Chadema wanakutia wasi wasi wa kushika dola kwa fukuzana fukuzana. Tukasema, hapana si kweli, katika fukuzana wanaweza kushika dola mbona CCM walioshika dola wanafukuzana na hujawa na hofu?

Ndipo mfano wa mansour Himid ikaingia

Mansour Himid amekuwa mjumbe wa ngazi ya juu wa CCM visiwani.

Amekuwa waziri aliyetoa maamuzi mazito. Ameshiriki vikao vya BLW na baraza la mawaziri Zanzibar.
Kisiasa ni mtu maarufu sana.

Zitto hajawahi kushika nafasi ya maamuzi ya kiserikali ukiachilia nafasi za chama.

Hivyo Mansour Himid kisiasa na kiserikali bado anamzidi Zitto
Na hii habari ya fukuzana ndio sikubaliani nayo hata wao ACT siwaungi mkono katika hilo ikiwa kweli huyo Mwenyekiti kasema kuna fukuza fukuza ya wananchma maana mimi naamini chama ni wanachama wenyewe, Chama pasipo wanachama hukuna chama. Na ndio maana wameweka sheria ya idadi ya wanachama kutoka kila jimbo kuwa kiambatanisho muhimu cha usajili. Pasipo hao huna chama sasa unapokuja andikisha chama kwa sababu yao, kisha ukipata usajili unaanza kufukuza wewe nani kama sio kukifanya chama ni mali yako?..sijui kama nimeeleweka.
Well said Mkuu, lakini hawa ACT akina Kitila, Zitto na Mwigamba si ndio wamewatimua akina Nyakarungu na Limbu?
Hivi wanawezaje kutuaminisha ni makini! Hujaona kaulaghai hapo!
Mkuu kanuni za Chadema tumezisoma sisi wengine sijui wewe, Diwani sio mjumbe wa kamati kuu, labda awe lakini swala la kuondolewa madarakani viongozi wa kamati kuu limeelezwa vizuri tu hata kama sheria hiyo ilitungwa na Kitila na Zitto maadam ilikubaliwa na baraka kuu hilo tena linabakia hadithi nani kaandika. Ukisha chaguliwa kuwa kiongozi wa kamati kuu huwezi kuondolewa madarakani ktk jambo kama hilo pasipo kupitia Baraza kuu. sababu ya sheria hiyo ni kuepusha viongozi kuumbuana ama kufanya maamuzi kinyume dhidi yao wenyewe - Outside body has to deside (sheria nzuri kabisa)...Maana hawa binadamu na hawawezi kufikiria sawa na misuguano lazima itakuwepo. Kilichofanyika ni tofauti na sheria imewaumbua kiasi kwamba Dr.Slaa alidiriki kusema mjadala huo umefungwa asisikie mwanachama yeyote wa Chadema akijadili tena.. Amri ilitolewa.
Mkuu madiwani walifukuzwa udiwani na uanachama. Hapa tunaongelea uanachama.

Hivyo tuangalie hoja ya jinsi gani mwanachama anafukuzwa.

Ikija upande wa Zitto, kama ulivyosema, wao hawakutumia vikao vile vile unavyosema kufikisha madai yao ya 'Mbowe ana akili ndogo' Unachokiona ni wao kutotendewa haki.

Hata hivyo, bado hujatueleza ni haki gani waliyokosa kama walikwenda mahakamani, sheria na kanuni zikatafsiriwa na wao kuambiwa hakuna kosa? Hebu tufafanulie hapa, mahakama ilikosea wapi?
Mkuu niliusoma ule waraka na matusi yalokuwemo yaliandikwa na mtu mwingine sio Zitto, disciplinary measure ingechukuliwa na Baraza kuu ndivyo kanuni ilivyotaka na tungeujua ukweli zaidi kuliko hizi hearsay na kufunika kombe halafu basi, mwisho wa yote mimi nilichokitaka ni AMANI kuondoa chuki na kuwekana sawa juu ya malengo ya chama yawe mbele yasipotoshwe na mambo madogo kama hayo, lakini nyie mmekubaliana na ujenzi wa chuki kama ndio maamuzi ya maana sana. Tumefundishwa Love and Forgiveness na hapana mahala pa kuonyesha unyenyekevu huo kama ndani mwako.
Zitto, Kitila na Mwigamba walikubali mbele ya kikao wakata yaishe.

Kama haikuwa hivyo Zitto asingefika katika kikao kabisa kuonyesha hakuhusika.

Hata hivyo, Zitto huyu huyu aliyeanzisha ACT akiwa Chadema unawezaje kutafuta ushahidi mwingine kuwa hakuhusika ikiwa mwenyewe anasema alishiriki kuanzisha ACT achilia mbali ile ya ACT ya waraka!
Safi kabisa kuwa neutral katika hoja lakini sidhani kama kweli una nia hiyo hata kidogo. nakusoma vizuri mkuu wangu kama unavyonisoma miye. Tunachotofautiana tu ni Chanzo na Matokeo, wewe umeamua kusema chanzo ni Zitto nami nasema chanzo ni CDM, hivyo pokea sababu zangu kwanza na uamini kuna ukweli ama zikatae kwa kuonyesha ukweli ni upi..
Sijui kama chanzo ni CDM, ninajua kwa ushahidi wa vijana wa Zitto, kwa maandishi ya Kitila magazetini kuwa Zitto alikuwa anachochea migogoro sana ndani ya CDM katika jitihada za kutafuta supremacy. Thank God, sasa ni supreme leader.

Hakuna asiyejua kuwa Zitto amekuwa distraction ya upinzani.

Nadhani umesikia walezi wake wakisema, wanasiasa wakisema. Haiwezekani kila mtu aone kuna tatizo, wewe peke yako umuone lulu

Tunakubaliana kuwa Zitto amejaliwa vitu vingi vinavyoweza kumfanya awe kiongozi bora.

Kwa bahati mbaya ubora wake hautimii kwasababu hana busara.

Na wala haielekei kama atapata maana umri wa kisiasa umeshakwenda.

Miaka 15 na ushee ni umri wa kukua, supreme leader ana via.

Nadhani ni vema kumsaidia abadilike kuliko kumpamba na mashada ya maua yaliyo nyauka.
 
Na hii habari ya fukuzana ndio sikubaliani nayo hata wao ACT siwaungi mkono katika hilo ikiwa kweli huyo Mwenyekiti kasema kuna fukuza fukuza ya wananchma maana mimi naamini chama ni wanachama wenyewe, Chama pasipo wanachama hukuna chama. Na ndio maana wameweka sheria ya idadi ya wanachama kutoka kila jimbo kuwa kiambatanisho muhimu cha usajili. Pasipo hao huna chama sasa unapokuja andikisha chama kwa sababu yao, kisha ukipata usajili unaanza kufukuza wewe nani kama sio kukifanya chama ni mali yako?..sijui kama nimeeleweka.


Mkandara
hii ndo katiba ya ATC wazalendo kuhusu"Haki za wanachama"


Mwanachama atakoma kuwa mwanachama ikiwa:

ii.Atajiuzulu mwenyewe kwa hiari yake kwa kuandika barua kwa Katibu wa ngazi yake au Katibu Mkuu kwa kueleza kusudio la kuacha kuwa mwanachama na kurudisha kadi ya uanachama;

iii.Kujiunga na chama kingine cha siasa;

iv.Kufukuzwa uanachama kwa mujibu wa kanuni zilizowekwa katika Katiba hii; au

v. Atapoteza sifa za uanachama kama zilivyoainishwa katika Katiba hii.

(2)
Mwanachama anaweza kusimamishwa uanachama ili kupisha uchunguzi kuhusu mwenendo wake utakaofanywa na Kamati ya Uadilifu katika nagazi husika.

Mwanachama anaweza kufukuzwa kwenye Chama kwa sababu zinazotokana na mwenendo usiofaa kwa mujibu wa masharti na Kanuni za Katiba hii, na mara baada ya kufukuzwa, uanachama wake utakoma.

(4)
Pamoja na sababu nyingine kama zilivyoelezwa katika katiba hii na kanuni zitakazotungwa na Halmashauri Kuu, mwanachama yeyote ambaye atasaidia, kushawishi, kujiunga, kutoa tamko la kuunga mkono chama kingine au mgombea wakati Chama kimeweka mgombea kwenye uchaguzi wowote kwa mujibu wa Sheria ya Nchi atakuwa amepoteza uanachama wa ACT.

(5)
Hakuna mwanachama atakayesimamoshwa au kufukuzwa uanachama hadi pale ambapo mashart yaliyoainishwa katika Katiba hii na Kanuni za Uendeshaji Chama yatakapokuwa yamefuatwa.


 
Nguruvi3 na Alinda,

Pengine hamnielewi mimi msimamo wangu katika jambo hili la Uanachama. Sikubaliani na fukuza fukuza ya wanachama iwe kwa chama chochote, ni maamuzi ambayo binafsi nayaacha kwa mwanachama mwenyewe. Hivyo vyama vinapoendesha siasa za fukuza fukuza haina maana kwamba wako sawa kwa mtazamo wangu, wako sawa kwa mtazamo wao.

Hivyo inaweza kuwa sawa kwao lakini basi wafuate taratibu na sheria zao zinavyosema. Swala la kina Kitila limeanza katika uongozi kuondolewa kinyume cha taratibu walizoweka Chadema, halafu sababu za kufukuzwa pia hazijitoshelezi kutokana na hizo hizo kanuni zao. Ndio maana napingana nano kwa sheria zao wenyewe na kusherehesha na maoni yangu juu ya kufukuzana.

Halafu kuhusu Masour Himid tunazungumzia wanachama ngazi ya uongozi ndani ya chama. Umuhimu wa Himid katika uongozi wa chama CCM hata iwe Zanzibar ndio nilitaka kujua maana anayefukuzwa ni mwanachama na jinsi gani anahitajika na chama na ndio maana yeye kafukuzwa lakini mtu kama Lowassa ameachwa huru hadi kesho. Na sidhani kama Himid na Lowassa unaweza pima nguvu zao. Hili pia sina maana CCM wamefanya inavyotakiwa ila wajanja ndani ya sheria zao wenyewe. Wametazama maslahi ya chama mbele, kuondolewa kwake kunaweza sababisha mgawanyiko.

Niaminivyo mimi mwanachama yeyote akinyimwa fursa za kushiriki katika mambo yote ya chama basi tayari kisha malizwa kisiasa, maana hata mikutano ya chama hatashirikishwa. Atabakia mwanachama wa kadi tu na kama atapenda kuendelea kushika ganda hilo ni juu yake. Mimi nawaona watu kibao wakijiita Chadema au CCM wakati hawashirikishwi ktk maandalizi ya jambo lolote yaani wana kadi tu. Wakati ninavyoamini mimi kuhusu mfumo wa chama, mtu yeyote anapojiandikisha uanachama ina maana yupo tayari ku volunteer katika jambo lolote atakapo hitajika na chama. Kuchaguliwa kuongoza ama kusaidia chama katika maandalizi ya jambo lolote. sasa huu mpango wa kuwa na wanachama millini 2 ukategemea ati wao ndio watakupigieni kura ni makosa kabisa na nayaona Tanzania tu.

Huku kwenye demokrasia ya ukweli, inapofikia wakati wa kupiga kura kila mwananchi ana ruksa ya kumchagua mtu yeyote na toka chama chochote na asipoteze uanachama wake. Wakati wa kura kila mtu ni free of choice na kama sikosei uchaguzi wa 2008 (awamu ya kwanza ya Obama), Colin Powell a Republican alisema wazi tena mbele ya vyombo vya habari kwamba kura yake atampa Obama (Democratic), na hatukuona akifukuzwa uanachama. Kwa hiyo sina maana ACT ndio wako sawa Kikatiba ila siwezi pindua maamuzi yao na itakuwa vema wafuate masharti waloyaweka. Wakienda nje ya kanuni zao nitawapata vile vile.

Swala la imani kwangu ni la mtu, kuniona Mkandara nimeingia kanisanihaina maana nimepoteza imani bali kuna sababu na sababu hiyo ndiyo pekee haiwezi kuamuliwa kuwa nimebadili imani au laa hasa sisi wengine huenda mazishi ya Kikristu, hushiriki hata katika nyimbo na kuitikia lakini kifuani tumejaa imani nyingine kabisa... Imani sii kujionyesha ama kumfurahisha mtu, imani ni maisha yako sii ya mwingine.
 
Mkandara,

Kuna hoja uliyotoa katika bandiko lako, na hoja hii inastahili kujibiwa inavyostahili. Hii ni kwa sababu, umeanza kuiga tabia ya Zitto ya kulaghai umma kwa nia ya kupotosha mambo for political gain. Ningependa kujadili hoja yako ya kwenye bandiko #217 ambapo umejadili hivi:

Nitasema moja tu ya kwamba ACT isingekuwepo kama Chadema wasingewafukuza Kitila, Mwigamba na Zitto. Hivyo maadam Chadema waliona umuhimu wa kuwafukuza wakijua fika kwamba hawa watu ni wanasiasa, kuondoka kwao wataunda chama chao lakini haitakuwa tishio kwao, basi hakuna sababu ya kulalamika leo maana Chadema walijua na walitegemea haya kutokea. Tulionya mkasema Chadema haiwategemei wao waende wanakotaka Chadema Imara, sasa uimara huo unaogopa mpini tu pasipo hata shoka lenyewe....Alaa kumbe Upinzani ni gogo la mti lilosubiri kupasuliwa bahati mbaya tawi lake limejengwa kuwa mpini!..

Akiwa mkoani Ruvuma mapema wiki hii, Zitto alisema uongo kama wako, tena mbele ya mkutano wa hadhara kwamba – “kufukuzwa kwake ndani ya Chadema kulitokana na msimamo wake wa kutetea maslahi ya wananchi”. Zitto akaendelea kusema kwamba - “baada ya kutambua kwamba chadema wanataka kuwatumia wanyonge kujipatia ruzuku, lakini sio kuwatumikia, yeye na wenzake wameamua kuanzisha chama chao kitakacho watetea wanyonge, ikiwa ni pamoja na wakulima”. Mkandara, kati ya Chadema na CCM, ni nani aliyeangusha wakulima, wanyonge?

Tukirudi kwenye mada, Zitto ni muongo na mpotoshaji mkubwa kwani sio kweli kwamba amefukuzwa chadema kwa sababu ya kufuatilia “mambo ambayo yanakandamiza wanyonge”. Haya ni majigambo ya kitoto. Zitto amefukuzwa Chadema kutokana na usaliti, na kushirikiana na maadui wa Chadema kukichafua chama pamoja na uongozi wake wa juu. Zitto alishakiri kutaka kufanya ‘mapinduzi’ dhidi ya uongozi wa chadema, kinyume na kanuni, taratibu na katiba ya chama hicho. Amekiri kushirikiana na maadui wa Chadema na ushahidi juu ya haya upo wazi.
Katika ziara yake ya Ruvuma, Zitto alienda mbali zaidi na kuwaambia wananchi kwamba ni yeye ndiye aliyeibua hoja za Buzwagi, Richmond, Operesheni Tokomeza, Escrow na Mabilioni ya Uswisi, huku akijigamba kwamba ni juhudi zake katika kutetea wanyonge ndio zimefukuzisha mawaziri kadhaa kazi. Huu ni udanganyifu mkubwa unaolenga kujizolea umaarufu wa kitoto. Tufafanue baadhi ya haya:

· Kashfa ya Buzwagi illibuliwa kwa mara ya kwanza na gazeti la ----------- mwaka 2007, mwezi February, toleo namba 68. Zitto akaidandia hoja hii na kuipeleka bungeni miezi miwili baadae (Mei, 2007). Zitto anadanganya pia anaposema kwamba kazi yake juu ya Buzwagi ndio iliyomtoa Waziri wa Nishati wa wakati ule, Karamagi. Bwana Karamagi aliachishwa kazi February 2008 kutokana na kashfa ya Richmond.

· Hoja ya Richmond iliripotiwa kwa mara ya kwanza na gazeti la daily news baada ya hoja hii kuibuliwa bungeni na Mwenyekiti wa kamati ya nishati na madini, William shelukindo. Gazeti la ----------- likaendelea kulivalia njuga hadi pale Kamati teule ya Bunge chini ya Dr. Mwakyembe ilipohitimisha suala hili.

· Hoja ya mabilioni ya Uswisi, hapa pia Zitto anadanganya. Aliyeibua hoja ya uswisi alikuwa ni mwandishi wa habari za uchunguzi nchini (Investigative reporter) Ndg. Kabendera. Huyu ndiye aliyempa Zitto taarifa zote muhimu, na kuumunganisha Zitto na watu wote muhimu wa ndani nan je ya nchi ili kumwezesha Zitto. Pamoja na majigambo yake (Zitto), umma umekuwa ukisubiri kuona majina hayo ya mabilioni ya uswisi bila mafanikio yoyote,. Katika hili, anachoweza kujivunia Zitto ni kuwa hodari wa kuficha kwapani taarifa zote anazopewa ambazo zina maslahi ya wanyonge.

· Hoja ya Escrow – muasisi wa hoja hii alikuwa ni Mh. Kafulila tarehe 9, Mei, 2014 wakati akichangia bajeti ya ofisi wa waziri mkuu. Kafulila alisema kwamba kiasi cha sh billioni 200 zimechotwa katika akaunti ya escrow, Tegeta kinyume cha utaratibu na akataja wahusika wakuu wa wizi huo huku umma wa watanzania kupitia luninga zao. Ni kafulila ndiye aliyetaka jambo hili lichunguzwe kwa kuwa linaigusa BOT na vigogo serikalini. Zitto alikuwepo bungeni siku hiyo lakini aliyesimama kumuunga mkono Kafulila hakuwa zitto bali Halima Mdee, ambaye Zitto ameshasema kwamba ana nia ya kumwondoa kwenye kiti chake cha ubunge wa kawe kwa gharama zote ili ACT ipate jimbo hilo. Ni juhudi za Kafulila na Mdee ndio zilimsukuma waziri mkuu kuliahidi bunge kwamba uchunguzi utafanyika. Sote tunajua jinsi gani Zitto alikuja kugeuka na kuungana na Andrew Chenge mle mle bungeni kulinda wahusika.

Mkuu Mkandara, jinsi siku zinavyozidi kusonga mbele ndivyo usaliti, uongo na utapeli wa Zitto inavyozidi kung’ara. Wananchi wengi wanazidi kutambua ukweli kwani uongo, usaliti na utapeli wake ndio unasaidia wananchi wazidi kumfahamu vizuri.

Watetezi wengi wa Zitto wanazidi kumkacha kwani wameanza kumshtukia. Mmebakia wachache sana kama mlivyojadiliwa kimakundi na Nguruvi3 awali.
 
Last edited by a moderator:

Mkandara
hii ndo katiba ya ATC wazalendo kuhusu"Haki za wanachama"


Mwanachama atakoma kuwa mwanachama ikiwa:

ii.Atajiuzulu mwenyewe kwa hiari yake kwa kuandika barua kwa Katibu wa ngazi yake au Katibu Mkuu kwa kueleza kusudio la kuacha kuwa mwanachama na kurudisha kadi ya uanachama;

iii.Kujiunga na chama kingine cha siasa;

iv.Kufukuzwa uanachama kwa mujibu wa kanuni zilizowekwa katika Katiba hii; au

v. Atapoteza sifa za uanachama kama zilivyoainishwa katika Katiba hii.

(2)
Mwanachama anaweza kusimamishwa uanachama ili kupisha uchunguzi kuhusu mwenendo wake utakaofanywa na Kamati ya Uadilifu katika nagazi husika.

Mwanachama anaweza kufukuzwa kwenye Chama kwa sababu zinazotokana na mwenendo usiofaa kwa mujibu wa masharti na Kanuni za Katiba hii, na mara baada ya kufukuzwa, uanachama wake utakoma.

(4)
Pamoja na sababu nyingine kama zilivyoelezwa katika katiba hii na kanuni zitakazotungwa na Halmashauri Kuu, mwanachama yeyote ambaye atasaidia, kushawishi, kujiunga, kutoa tamko la kuunga mkono chama kingine au mgombea wakati Chama kimeweka mgombea kwenye uchaguzi wowote kwa mujibu wa Sheria ya Nchi atakuwa amepoteza uanachama wa ACT.

(5)
Hakuna mwanachama atakayesimamoshwa au kufukuzwa uanachama hadi pale ambapo mashart yaliyoainishwa katika Katiba hii na Kanuni za Uendeshaji Chama yatakapokuwa yamefuatwa.
Alinda yaani nashindwa kuelewa hoja ya Mkandara kabisa.
Ukisoma katiba ta ACT, kile walicholalamikia wakiwa CDM ndicho wanakitenda. Mkandara anatetea kitu gani yarabi!

Amemfananisha Zitto na Mansour tukaonyesha tofauti zao.
Sasa anageuka Mansour na Lowassa! Yaani mkuu anahamisha goli kila dakika. Labda nizirejee hoja zake tena

Zutto amekiri kuwa ni mwanzilishi wa ACT. Kama tujuavyo ACT ipo muda sasa, kwahiyo kuanzishwa kwake kulikuwa na input ya Zitto kwa mujibu wake.

Wakati huo huo alikuwa mwanachama wa Chadema. Soma katiba yao 'mwanachama yoyote atakayesaidia, shawishi... atapoteza uanachama'' Zitto na Kitila wanajua hilo, sasa Zitto alikwenda mahakamani kudia nini? Je, tunaposema kuchumia tumbo na utapeli tunakosea wapi?

Soma katiba '' Kuunga mkono mgombea wakati chama kimeweka mgombea wake... atapoteza unachama''

Zitto alishiriki uchaguzi wa Kigoma katika njia mbali mbali!!!

Akatoa tamko la kugombea Urais wakati chama chake kina mgombea.
Kwa tafsiri hakuunga mkono mgombea wa chama chake. Leo amekuwa supreme leader anaanza kuona ubaya wa kile kile alichotekeleza! Jamani hawa walaghai mkiwaacha tutaliumiza taifa

Mkandara kama utakumbuka, CDM Zitto alikuwa kama hayupo. Kwa maana kuwa alikuwa na uanachama wa kadi kama ulivyosema.

Hilo halikuzuia Zitto kuivuruga Chadema. Unafahamu alivyowatumia vijana na mabinti kwa kutumia rasilimali zake ili wavuruge Chadema.

Unakumbuka akina Juliana walivyokuwa wanamtukana katibu mkuu wa CDM, wakitetewa na Kitila magazetini.
Hawa watu walikuwa wanaendesha agenda zao kwa ufundi sana. Huwezi kuwaacha ukabaki salama!

Chadema na Mbowe wamemsitiri sana Zitto kwa maana ile ile unayosema, ni mwanachama abaki na uanachama.

Nadhani umeona miaka 2 alivyovuruga CDM. Hawa ni watu wa kiwango tofauti sana huwezi kuwaacha ukumbini ukaenda kulala chumbani.

Hawa watu ni hatari sana huwezi kuwaamini hata senti moja, ni walaghai wazuri, mafundi wa spinning na matapeli wa kisiasa.
Don't trust them! eti uwaache tu na uanachama! thubutu, muulize Mbowe aliyejaribu!

Chochote kinachotokea au kilichotokea , Mbowe anabeba lawama! amejaribu kufuga nyoka bila kuangalia meno! yeye aliamini nyoka akikaa ndani ya nyumba anabadilika kuwa mjusi.
 
Mchambuzi,

Kwanza nakuomba uniombe samahani kwa sababu hoja ya Zitto na yangu hazifanani kabisa. Kama wewe mkweli nionyeshe kwenye hiyo hoja niloweka wapi nimesema uongo halafu ndio ufananishe na hoja za Zitto ama kuiga tabia yake. Zitto kaongea yake anayoyajua yeye ndani ya Chadema, mimi sikuwepo wala sifahamu na wala hakuna mahala mimi nimekubaliana naye sasa haya yako yametoka wapi? Mbona mimi sizungumzii tabia yako ama kuifananisha na mtu nayemchukia...

Msimamo wangu:- Ushahidi na sababu za kumuondoa Zitto madarakani mimi sikuridhika nazo, na taratibu zilizotumiwa sikubaliani nazo maana ni kinyume cha kanuni, huo ndio msimamo wangu na sii kwa Zitto isipokuwa kwa mwanachama yeyote na ufafanuzi wa mtazamo wangu, pale kuna tofauti na sheria zenu zimeambatanisha na hoja zangu. Sikutunga sheria za Chadema wala sikupendezewa na fukuza fukuza kwa chama chochote, nisome vizuri unielewe.

Hayo unayoyadai juu ya Zitto mimi ningeomba ushahidi tu wa kutosha na siwezi kubeba hearsay za mtu yeyote na wala sii kwake tu tuhuma ngapi ziliwekwa juu ya Mbowe na Slaa na sikuziamini?. Mimi hupenda kushiriki mijadala yenye uhakika wa jambo na tukapewa picha nzima maana ya Mbowe na Zitto nayafahamu mengi pengine kuliko hata Chadema wenyewe na wala hapa sii mahala pake.

Maswala ya Zitto kujitapa ni yake yeye Zitto na siwezi chukua maneno yako wewe ama mtu mwingine asohusika hadi pale mwenye uhakika nalo atajitokeza maana tunajadili nani alopeleka muswada huo bungeni ama kufikia maamuzi ya bunge na sio habari za mjini kwenye matukio.Nilikupeni mfano wa harrison Mwakyembe na Richmond japo umesema Zitto ndiye kadai alilipelekea bungeni.. Iwe isiwe sifa ni za Mwakyembe kwa kazi alokabidhiwa kuifanya kwa ufanisi.

Hata mabunge ya huku nje habari huanzia magazetini ama wananchi kulalamika, sasa inategemea ni mbunge gani atakaye fuatilia na kuyapeleka bungeni. Yapo maswala mengine hufikishwa bungeni yasipate nafasi ya kujadiliwa. Sisi wenyewe tuliomba kupitia mbunge wa Uingereza swala la rada likajadiliwa bunge ktk lao hadi ikabainika BAE walivyohusika katika mikataba mingi ya UFISADI na sio sisi peke yetu. Muswada ule ulimshusha kabisa waziri mkuu wa Uingereza alopita kisiasa nchini humo..

Kwa hiyo sintozungumzia swala ambalo hakuna mbunge alokuja hapa na kupingana na Zitto hata huyo Kafulila mwenyewe hajasema lolote against Zitto maana yawezekana walikuwa pamoja katika hili ila wapambe wa Chadema ndio wamelishikia bango kiasi kwamba wapo wengine wendawazimu wanataka hata kupitia mgongo wa Muhongo ili mradi tu Zitto aonekane msaliti na muongo. Mimi janja hizi hazija nirubuni kitu. Kifupi hakuna habari yoyote ilovumbuliwa na mwanasiasa nchini habari zote zina chanzo chake na hatuzungumzii chanzo ila kazi aliyopewa mbunge huyo kaitimiza au laa!

halafu basi mkuu wangu wewe sio mwanasiasa na wala hutumii akili hapa. Kamati ya PAC ndio watarajiwa kuwa mahakimu wa report ya Escrow leo Mwenyekiti wake ndiye ashiriki kuandaa kesi hiyo kweli inaingia akilini. Sasa ikija kwao tayari yeye kisha onekana kachukua upande sii italeta sura mbaya? Mipango ya wabunge iwe Zitto na Mbowe, Mnyika au Mdee pale bungeni ni mipango yao wao, wewe msikilizaji tu huwezi jua nani kam support nani na wamepanga nani azungumze maana mwenyekiti wa Upinzani ni Mbowe na anayo majukumu yake pale bungeni kama kiongozi wa upinzani.

Aaaah mengine niyaache kama yalivyo, kubishana sana mwisho tunatoka kwenye mada halafu tunaanza dhana zetu wenyewe..
 
Nguruvi3,
Mkuu umeamua kutonisoma ila kubishana tu ili mradi liende. Maelezo yangu yako wazi kabisa na hakuna mahala nimetetea ACT na kanuni zao juu ya fukuza fukuza isipokuwa nakumbuka siku ya ufunguzi kuna mtu hapa JF alisema kwamba amesikia Mwenyekiti akisema ACT haina fukuzana kwa sababu wao wanaamini kumfukuza mtu uanachama ni sawa na kumuondolea Uraia.

Hilo nakubaliana nalo kabisa na ndio msimamo wangu, sasa kama huyu mtu alidanganya au Mwenyekiti hakusema hayo basi, maana mimi sipo TZ hivyo mengi huyasoma tu humu JF. Mengine yana ukweli mengine ni tunzi za watu na JF imeharibika kiasi kwamba hujui lipi la kuamini na lipi ni uongo..
 
Mkandara,

..kwa uelewa wangu Tume ya Warioba imependekeza tuwe na shirikisho.

..UKAWA wanakubaliana na katiba ile iliyopendekezwa na Tume ya Warioba.

..Zitto anapendekeza tusiwe na "maraisi watatu," badala yake tuwe na Raisi mmoja na mawaziri wakuu wawili.

..pamoja na hayo, Zitto hajafafanua tofauti mipaka ya madaraka baina ya hao mawaziri wakuu wa nchi washirika, na maraisi wa nchi washirika ambao wanapendekezwa na tume ya Warioba.

..Sasa kwasababu wewe unamuunga mkono Zitto labda unauelewa zaidi kuhusu tofauti ya mfumo aliopendekeza Zitto na huu uliopendekezwa na Tume ya Warioba na kuungwa mkono na UKAWA. Tunaomba ufafanuzi wako.

cc Nguruvi3, Mag3
 
Last edited by a moderator:
..kwa uelewa wangu Tume ya Warioba imependekeza tuwe na shirikisho.

..UKAWA wanakubaliana na katiba ile iliyopendekezwa na Tume ya Warioba.

..Zitto anapendekeza tusiwe na "maraisi watatu," badala yake tuwe na Raisi mmoja na mawaziri wakuu wawili.

..pamoja na hayo, Zitto hajafafanua tofauti mipaka ya madaraka baina ya hao mawaziri wakuu wa nchi washirika, na maraisi wa nchi washirika ambao wanapendekezwa na tume ya Warioba.

..Sasa kwasababu wewe unamuunga mkono Zitto labda unauelewa zaidi kuhusu tofauti ya mfumo aliopendekeza Zitto na huu uliopendekezwa na Tume ya Warioba na kuungwa mkono na UKAWA. Tunaomba ufafanuzi wako.

cc Nguruvi3, Mag3
Hapana mkuu sidhani kama Warioba anaweza kuwa na mwamko hafifu juu ya miundo ya serikali maana Muungano wa Shrikisho na Jumuiya kuna viashirio vya lazima kuwepo kuziona tofauti zake. Na rasimu imejikita kwenye Jumuiya hata kina Jussa na Sief Hamad husema kila siku wanachokitaka ni kile kilichomo katika rasimu..And we know where they stand..

1. SHIRIKISHO - Serikali kuu ya nchi husika ndiyo yenye mamlaka makubwa zaidi ya Serikali ndogo za kila nchi zenye madaraka ya chini. Hivyo hata bunge lake ni kubwa na hata mahakama yake ni ya juu zaidi kisheria kuliko serikali ndogo. Maamuzi yote makubwa hata ya kibiashara nje na mahusianio hufanywa na serikali kuu, wakati serikali ndogo za nchi zina mamlaka na HUSHUGHULIKA na mambo yake ya ndani ya kiwizara with cordination na serikali kuu kwenye grants na kadhalika. Kodi za serikali kuu ni lazima hazichangiwi kwa pande zote, hutoka asilimia sawa ya mapato yao sio swala la mchango wala kuwa na mfuko maalum. Kuendesha mfumo huu kuna gharama kubwa sana japo unazawadisha nchi au majimbo yenye utajiri zaidi ya nchi maskini. Mifano ni Serikali za USA, CANADA na kadhalika.

2. JUMUIYA ndizo hukuta serikali za nchi kuwa kubwa kuliko ya Muungano na hata bunge lake kubwa ukilingaisha na la serikali kuu. Na kikubwa zaidi hushirikiana tu kwenye MAMBO waloafikiana mengine yote kila nchi ina maamuzi juu yake. Haya tunayaona ktk Europen Union na EAC japo EAC bado haijafikia katika Ulinzi na uhamiaji kama EU.

Hivyo ukiisoma rasimu utaona kuna mengi sana ya KIJUMUIYA kwa maridhiano ya Mambo watakayo shirikiana na sio mamlaka gani ya kushughulikiwa na nani isipokuwa tumegawana kabisa miliki. Huku unakuta Chako chako changu changu, Tulichokubaliana ndio Chetu sote. Rasimu imetaka kila nchi iwe na rais wake na hata makusanyo ya kodi kila nchi ichangie mfuko wa umoja huo. Katika jumuiya mwanachama unaweza kufukuzwa maana sio Muungano. Hivi ndivyo tunavyofanya EAC...
 
Mkandara,

..kwa uelewa wangu Tume ya Warioba imependekeza tuwe na shirikisho.

..UKAWA wanakubaliana na katiba ile iliyopendekezwa na Tume ya Warioba.

..Zitto anapendekeza tusiwe na "maraisi watatu," badala yake tuwe na Raisi mmoja na mawaziri wakuu wawili.

..pamoja na hayo, Zitto hajafafanua tofauti mipaka ya madaraka baina ya hao mawaziri wakuu wa nchi washirika, na maraisi wa nchi washirika ambao wanapendekezwa na tume ya Warioba.

..Sasa kwasababu wewe unamuunga mkono Zitto labda unauelewa zaidi kuhusu tofauti ya mfumo aliopendekeza Zitto na huu uliopendekezwa na Tume ya Warioba na kuungwa mkono na UKAWA. Tunaomba ufafanuzi wako.

cc Nguruvi3, Mag3
JokaKuu, Mkandara kachanganyikiwa. Hii hapa ndio rasimu ya katiba kama ilivyopendekezwa na Tume ya Warioba kuhusu Muundo wa Muungano:

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakuwa na muundo wa shirikisho lenye serikali tatu ambazo ni:

(a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
(b) Serikali yaMapinduzi yaZanzibar; na
(c) Serikali yaTanganyika

Zitto naye kwa kuchanganyikiwa eti alipendekeza mamlaka tatu...Jamhuri, Bara na Visiwani. Alitaka Kiongozi Mkuu wa Jamhuri ndiye aitwe Raisi ila wa Tanganyika na Zanzibar waitwe Viongozi Wakuu wa serikali kama yeye anavyojiita Kiongozi Mkuu wa ACT.


 
Mag3,
Kuandika muungano wa Shrikisho wakati detail zake ndani ni za Jumuiya haina maana yoyote. Soma undani wake ndio unatoa tafsiri ya kitu. Usi judge kitabu kwa gamba lake, tunaishi nchi zenye muungano wa shirikisho na yaliyomo ktk rasimu hayafanani kabisa hata kidogo.
 
Back
Top Bottom