Mwanzo tulihubiriwa kuwa Chadema ni chama cha Wachaga ni chama wa wakristo ni chama cha kibaguzi haya yalisemwa na CCM, watu tulipinga na kuwaionya CCM kuwa huu ubaguzi mnauleta hautaishia kwa Chadema tu utakwenda mbali zaidi..
Kuna kipindi niliwahai kuongea na Mh. Zitto"Zitto alikiri mwenyewe kuwa ni kweli Chadema ni wabaguzi na ni wadini, alienda mbali zaidi na kusema Mbowe na Slaa
Nilimuuliza je kama ni wadini na wanakuonea wifu je ilikuwaje uwe kiongozi mkubwa hali utoki Kaskazini na pia sio mkristo?
Sikupata jibu ila alisema wewe huwafahamu hawa watu...
Kwa hiyo utaona swala la udini na ukabila lilikuzwa na Zitto na yeye ndo alilipeleka CCM..
Hakuna mtu mnafiki kama Zitto nafikiri kama
Mkandara atakuwa mkweli (maana Zitto ni rafiki zako) utakiri hilo..
Sasa rangi za Zitto zinazidi kuonekana wazi, alianza kuhubiri ukabila na udini kwa usiri (hapa kwa wafuasi wake) sasa ameamua kuhubiri ukabila kujenga chuki miongoni mwa watanzani na wachaga akiwa majukwaani..
Leo tunashuhudia wasemaje wa ACT hapa mtandaoni wakijipata kuwa kuna watu hawatompigia kura Slaa (padre) kwa vile ni mkatoliki na hao watawapigia ACT.. Na ukisoma hiki kitu na ukarejea ule waraka wa akina Kitila unaona huyu msemaji wa ACT ambaye ni
Kapwela anawakilisha mawazo ya kwenye waraka.
Hivi kwenye karne hii na chama cha wasomi kama ACT bado wanaendekeza siasa hizi za udini na ukabila?
hivi hatuoni majirani yetu huko Rwanda na Burundi jinsi ukabila unavyowatesa mpaka leo?
tena kwa bahati nzuri
Zitto ana vinasaba vya hizo nchi au na yeye anataka tuanze kupinga kama wenzetu?
Wanasiasa fanyeni siasa zenu lakini tuacheni Tanzania yetu ikiwa na amani