Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Nadhania tu sina uhakika. Chadema walituhumiwa siku nyingi kumhujumu Zitto kwa ukanda na hata ukabila. Ikaelezwa, na wewe ni mmojawapo kuwa kutangaza nia ya kugombea uenyekiti ndicho chanzo cha mgogoro

Tuhuma hizo ziliaminika kwa wengi, sisi tupo katika rekodi hapa jamii forum tukisema 'kutangaza nia halikuwa tatiao, tatizo ni busara na muda' Tukaongeza kusema haiwezekani CDM wawe na mgombea wa Urais halafu Zitto anatangaza nia wakati huo huo. Hii ilikuwa kumfanya mgombea wao 'useless''

Madai hayo ya uenyekiti na Urais ndiyo yaliovuma na kutumia kama hoja
Chadema wakaona hakukuwepo njia nyingine isipokuwa kuelewesha umma yaliyotokea

Mwigamba(Mkulima masikini) akiwa ndani ya kikao alikuwa anaandika na tunasoma hapa JF live.
Mwigamba hakutumia kikao kueleza hisia au asichoridhishwa nacho. Wala waandika waraka hawakutumia vikao kumaliza matatizo yao. Hakukuwepo njia nyingine ya kuaminisha umma kuwa zipo hujuma dhidi ya CDM ispokuwa kuweka waraka hadharani.

Leo tunajua kumbe ACT si chama kichanga, ni chama kilichoanza ndani ya Chama. Waraka unatuleza bila kificho
Nadhani ilikuwa ni muhimu kufanya hivyo, vinginevyo CDM ingeshaporomoka siku nyingi kwa mbinu za ACT-WARAKA

Unakumbuka mambo ya vikao waliyafanya sana. Tuliwatahadharisha kuwa Zitto ataleta tatizo. Hiyo ilikuwa 2011, leo yanatokea. Kuna wakati radical intevention inahitajika. Si katika siasa tu hata maisha ya mwanadamu
Daktari anapotumia dawa bila matokeo mazuri, kuna nykati hutumia kisu kufanya operation. Hiyo ndiyo inaotwa radical intervention.
Ebu rudi nyuma kidogo ujikosoe, Zitto alitangaza lini nia ya kugombea Uenyekiti, na mgombea Urais wa Chadema alitangazwa lini?..
 
Ebu rudi nyuma kidogo ujikosoe, Zitto alitangaza lini nia ya kugombea Uenyekiti, na mgombea Urais wa Chadema alitangazwa lini?..
Nadhani hujaelew maana nzima.

Tunachosema ni kuwa yamekuwepo madai kama ya uenyekiti na Urais yakimhusisha Zitto na kuhujumiwa.
Iwe kwa muda gani hiyo si hoja, hoja ni kuwa mambo hayo yalitumika kuonyesha kahujumiwa vipi. Umeelewa!
 
DAHANA POTOFU INAYOENEZWA NA ACT

NI KUHUSU MGAWANYO WA RASILIMALI NA MAENDELEO

MBEGU INAYOPANDWA NA ACT NI CHAFU NA HATARISHI


Sehemu ya I

Ilipojadiliwa kama Rwanda na Burundi zijiunge EAC, iliundwa tume kukusanya maoni.

Mjadala huo uliingia bungeni . Zitto alinukuliwa akisema Tanzania haipaswi kuhofua kujiunga EAC kwasababu tofauti za kiuchumi hazipo EAC tu, zipo nchini.

Akasema mbona Tanzania ni nchi moja lakini kuna tofauti ya maendeleo kati ya Kigoma na Kilimanjaro!

Zitto na ACT wamenukuliwa akiongelea mgawanyo wa rasilimali, kwamba mikoa inayochangia zaidi pato ipo nyuma kimaendeleo.

Ametolea mfano wa Arusha na Kilimanjaro ikiwa na mchango michache , kimaendeleo ikiwa mbele

Kauli ya supreme leader haina ukweli kuhusu maendeleo bali kutafuta siasa rahisi na umaarufu butu

Supreme ameficha ukweli akijua, kutumbukiza mbegu ya ukabila na ukanda, itasaidia ima kumnyanyua kisiasa, au chama chake .
Ni mbegu ile aliyoikataa alikotoka japo alikuwa ni sehemu ya uongozi

Kauli imelenga kuwagawa wananchi kwa hoja dhaifu bila ukweli ina matatizo si kwa taifa tu bali kwa ACT ya ‘kizalendo ‘inayogawa wazalendo kwa misingi ya kikandaKauli hiyo imekuja kwa shinikizo la kisiasa linaloikabili ACT.

Matarajio ya haraka yanonekana kuwa na ugumu , kila mbinu safi na chafu zitatumika. Wazungu wanasema ‘shoot any moving object''

Tuangalie dhana ya kwanini kuna tofauti za maendeleo kutoka sehemu moja hadi nyingine

Inatosha kusema tatizo la uwiano wa maendeleo si la Tanzania tu. Nchi zilizoendelea zina matatizo hayo kutokana na sababu tofauti

MAENDELEO

Ni hatua ya mabadiliko chanya kwa mtu, watu, jamii na taifa na ni zao la jitihada .
Maendeleo yana vichocheo vingi, vikiwemo elimu, mwamko, mazingira, maeneo na rasilimali kwa uchache wa kutaja

Katika nchi yetu, maendeleo yanaelezwa kwa vigezo kama Historia, jamii, na jiografia.

Hivyo kuangalia maendeleo bila kuangalia chanzo na vichocheo ni kupotosha umma.

Haiwezekani kuongelea Tanzania bila kuzungumzia ukoloni na athari zake, elimu, mwamko wa jamii, matumizi ya rasilimali na eneo husika kwa kuitazama jiografia ya nchi yetu.

Kauli za rahisi za eneo fulani ni tofauti na jingine bila kufafanua, ni za kichochezi, kufilisika kisiasa na dalili mbaya kwa jamii yetu.

Inaendelea…
 
Sehemu ya II

MAREJEO YA NYUMA

Nchi yetu kama koloni imepita vipindi tofauti. Kila mkoloni au mtawala kwa njia yoyote alikuwa na vipaumbele.
Kwa mfano, wajerumani walijenga reli kwasababu za kiichumi.

Walitamani Lushoto kuwa makao makuu, kama ilivyokuw wengine kuifikiria Bagamoyo. Ndivyo ilivyokuwa kwa Kila enzi hizo n.k.

Katika kufanikisha malengo, wakoloni walitaka nguvu kazi, hivyo kuanzisha shule ili kupata wafanyakazi wa shughuli ndogo ndogo 'clerical work' Ikumbukwe ukoloni hauwezi kutengwa na dini .

Mathalani, elimu ya dini ya kiislama ilipatikana mikoa ya pwani, wamishenari wakielekea zaidi ndani

Itategemea mtu ataangalia elimu kwa jicho lipi, ukweli ni kuwa elimu zilipatikana kutokana na interest za watawala na nyakati tofauti.

ELIMU

Mgawanyo wa elimu ulitegemea masilahi ya wakoloni. Shule zilijengwa maeneo tofauti kwasababu tulizoeleza
Elimu ni kichochoe cha mwamko wa jamii . Y
apo maeneo yaliyopata kichochoe kwasababu za rasilimali,uchumi n.k.

RASILIMALI
Uwepo wa migodi kama mwadui, uliwezesha baadhi ya maeneo kunufaika.
Kwa mfano, mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Tabora ilinufaika kwa namna moja au nyingine na kupiga hatua kubwa enzi hizo

Lakini pia mazao kama Pamba, Kahawa, katani na Korosho yalichangia sana katika maendeleo ya maeneo mengine
Uwepo wa rasilimali na mazao ulichangia kuinua hali za maisha ya watu wa eneo fulani ukilinganisha na maeneo mengine.

Vyama vya ushirika kama Nyanza cop, Kilimanjaro native corp Union. Kagera corp n.k vilikuwa na nguvu za kisiasa zilizotokana na nguvu za kiuchumi. Baada ya uhuru hali iliendelea kuwa hivyo.

Mwaka 1966 Tanga ilipewa hadhi ya manispaa kutokana na shughuli za bandari, mkonge n.k.

Mikoa ya Kilimanjaro na Kagera kwa kutumia vyama vya ushirika iliweza kufikia hatua ya juu katika mambo ya elimu hata kufikiria kuwa na vyuo vya elimu ya juu

Ipo mifano mingi, katika miaka ya 1970 mitihani ya shule ilikuwa ya kitaifa.
2/3 ya wafaulu walitoka mikoa miwili au mitatu. Serikali ikaamua kutoa nafasi kwa uwiano wa mikoa.

Hapa maana yake mikoa iliyokuwa imepiga hatua ilinyimwa fursa ya kuendelea, Kilimanjaro na Kagera zikiwa zimeathirika sana

Hata hivyom, kutokana na mwamko wa elimu uliokuwepo toka enzi, na nguvu za kiuchumi wananchi wa mikoa hiyo walianzisha shule binafsi na hata kuwaondoa vijana wao kutoka maeno yenye ushindani kwenda maeneo mengine ili kupata fursa za kusonga mbele

Katika miaka ya 1980+ mkoa wa Kilimanjaro ulikuwa na idadi inayokaribia shule zote za sekondari nchini

Kwa mfano, wilaya moja ya mkoa wa Kilimanjaro ilikuwa na shule nyingi kuliko mkoa wa Kigoma,Tabora na Singida kwa pamoja.

Hadi leo hii Wilaya Changa kama ya Mwanga bado inatoa idadi kubwa ya wanafunzi kutoka shule zao za binafasi na serikali kuliko mkoa wa Lindi. Huu ni ukweli tusiotaka kuusikia

Inaendelea..


 
Inaendelea III

JAMII

Kutokana na elimu na mwamko, jamii za meaneo hayo zimeamaka na kutafuta maendeleo yao kwa njia zao.
Ukienda Kilimanjaro, Barbara nyingi zimejengwa kwa nguvu za wananchi.

Barabara hizo zinapita katika milima na majabali. Majuzi tumesoma katika gazeti la Nipashe, wananchi wa kijiji ‘Nronga?'' wamejenga barabara kwa nguvu zao na wameomba halmashauri ya mji wao kuwasiaidia madaraja.

Wananchi hao( habari ipo ikitakiwa kuwekwa hapa) wameamua kuchangishana kuanzia waliopo kijijini , nje ya kijiji, wilaya au mkoa. Wamechanga milioni zaidi ya 100 kwa mradi usiotegemea serikali. Walisema, barabara itawasaidia kupeleka mazao yao sokoni.

Utaratibu wa wananchi wa eneo fulani kuchangia maendeleo ya kwao umeanza na watu wa Kilimanjaro.

Mheshimiwa waziri mkuu Msuya amelipa gharama kubwa ya kisiasa kwasababu tu alishiriki kuhamasisha watu wake

Kijamii, tunaona wananchi wa maeneo hayo wakirejea makwao, wakijenga kwao na wakienda likizo zinazotaniwa kama kwenda kuhiji, kuhesabiwa ''December''.

Hata kama wanajenga nje ya mikoa yao, wananchi wa Kilimanjaro hawasahau kurudi kwao. Huu ni ukweli usiosemwa.

Kwa wanaoujua mkoa wa Kilimanjaro, hakika ni masikini. Ardhi ni shida na imechoka
Hali za watu wake zinategemea mapato ya vijana wao walioondoka kwenda kutafuta nje ‘remittance''
Ni utaratibu huo huo unaotumika kwa mikoa kama Kagera.

Leo wastaafu wote wa mkoa wa Kagera wapo mwakao au wamefia huko. Wanajenga nje lakini hawasahau makwao

Hii ni tofuati na wananchi wa mikoa mingine. Wakati Tanga imekuwa manispaa mwaka 1966 wananchi waliamua kuhama na kujenga Dar kwa hofu za kuogana.

Ndivyo ilivyo kwa wananchi wa maeneo kama Kigoma, Lindi na Mtwara.
Kila mmoja ana kibanda Dar na huo ndio mwisho wa safari yake. Ni ukweli mchungu tusiotaka kuusema

K'njaro ina wakazi takribani milioni 2, ukilinganisha na eneo lao, population density ni kubwa mno.

Sasa hivi wanahamia mikoa ya Tanga na Morogoro. Huko wanastawi kama walivyostawi nyumbani.
Utashangaa eneo la Mkuranga na Kimbiji, biashara za mihogo na machungwa wanafanya wahamiaji

Je, maeneo hayo yanahitaji rasilimali za taifa au yanahitaji mwamko wa taifa?
Kimazichana Mkamba na Nyamato, mananasi yanaota porini.

Hivi mwananchi wa Kilimanjaro au Arusha anapofanya shughuli ya kuongezea kipato maeneo hayo, anatumia rasilimali gani ya taifa? Na si ukweli kuwa remittance za manansi, mihogo ndizo zinarudi kujenga na kuendeleza makwao?

Kwanini wananchi wa Tanga waone wamenyimwa rasilimali ikiwa shughuli za kiuchumi wanafanya wageni katika ardhi yao?

K'njaro ni eneo lenye vivutio vya utalii. Ni njia ya uchumi kama alivyosema Rais Kikwete daraja lilipovunjika na jeshi kuingiilia kati katika ujenzi. Rais alisema mikoa ya kaskazini ni life line of economy.
Je hatukubali ukweli huo kwa kuangalia jiografia, rasilimali na yale yatokanayo?

Mgao wa pato la taifa unaonekana wazi( Mchambuzi) kaleta takwimu mara nyingi sana.

Zitto anatakiwa aeleze, zile barabara anazosema zimejengwa wakati akiwa mbunge, je, zimejengwa kwa pesa za wana Kigoma peke yao au ni sehemu ya pato la taifa?

Zitto aeleze, daraja la Malagarasi linalojengwa, ni matokeo ya jitihada za wana Kigoma au taifa kwa ujumla?

Je, deni la daraja hilo wanalipa wana Kigoma na Tabora au ni mzigo wa kila mmoja!

Inaendelea...

 
Sehemu ya IV


JIOGRAFIA

Mkoa wa Arusha una utajiri wa utalii. Upo kati ya mikoa ya Kimanjaro na Mara. Umepakana na Kenya na ni sehemu muhimu ya maingiliano ya nchi hzi mbili.Kiuchumi mkoa huu ni mzalishaji na biashara

Arusha inaeleza Mwanza ilivyo kwasasa. Mikoa mingine imepakana na maeneo ya nchi jirani historia ya vita haitoi nafasi kwa mikoa hiyo kusonga mbele.

Kigoma imekuwa na tatizo la wakimbizi na vita ya nchi jirani. Wananchi wameshindwa kufanya shughuli zao kwasababu ya ukosefu wa amani nchi jirani

Pamoja na hayo, panapokuwepo na utulivu tunaona Kigoma inavyosonga mbele japo si kwa kasi inayodhaniwa

MGAWANYO WA RASILIMALI
Sisi ni taifa moja, wananchi wanaruhusiwa kwenda kuishi mahali popote. Nyerere aliondoa uchifu ili kutoa nafasi kwa raia wa kuwa wan chi nzima na si eneo.

Akafanya ardhi mali ya serikali kuondoa ukiritimba unaoweza kuwakazwa wananchi katika kuhama au shughuli zao
Mwananchi wa Singida yupo Lindi, wa Lindi yupo Mwanza, Kigoma yupo Tanga n.k.

Hivyo inapojengwa miundo mbinu si kwa kabila, kanda au mkoa bali kwa taifa zima kwa ujumla

Hakuna mwananchi wa Singida au Kigoma aliyezuiliwa kuishi kule Zitto na ACT wanakosema kuna mchango kidogo na maendeleo zaidi. Nani kutoka Kigoma kazuiliwa kuishi Kilimanjaro

Daraja la Rufiji halikujengwa kwa watu wa Mtwara na Lindi, limejengwa kwa wananchi wan chi nzima. Daraja la malagarasi nalo linajengwa kwa nchi nzima na si kIgoma au Bukoba.

Vipaumbele ni kuhakikisha pale panapoweza kutukomboa, patiliwe mkazo kama taifa na si eneo.

Zitto aeleze, ni eneo gani aliloona bungeni linawanyima mgao wananchi wa Shinyanga. Atueleze yeye alifanya nini kuzuia hali hiyo. Lina alizungumzia suala hilo kwa uwazi

Huo ndio uzalendo na utaifa na wala si kudanganya umma.

NINI LENGO LA ACT
Kwa kauli za supreme, ACT inawaadhibu wananchi wanaojiletea maendeleo yao kwa jitihada zao.

ACT wanaamini ujenzi wa shule za ‘kata' kule Kilimanjaro kabla ya hizi za JK ilikuwa jambo baya.
Kwanini Kilimanjaro walifanya hivyo kwa jitihada zao!

Ujenzi wa barabara kwa njia ya ‘msaragambp' ni makosa, kwanini Kilimanjaro wasisubirii serikali

Kujenga shule ilikuwa makosa kwasnini wasisubiri wenzao wajengewe na serikali kama hizi za kata.

Kwamba, jitihada za wananchi zinaonekana kama uhalifu na supreme anahubiri chuki hiyo hadharani

ACT wanaamini kugawa fungu kubwa sehemu fulani kutaleta maendeleo.

Hawaoni matatizo yanayotokana na kukosekana kwa vitu kama elimu

ACT wakienda Lindi lazima kwanza wawaulize wananchi kwanini shule imefungwa kwa kukosa wanafunzi.
Baada ya hapo ndipo waongelee rasilimali

Na kwamba shule iliyofungwa ilijengwa kwa rasilimali za taifa,kukosa wanafunzi ni tatizo la mgawanyo wa rasilimali!!!!!

Hasira za supreme zimelekezwa kwa mikoa na si watu wawili watu anaotofautiana nao.

Aidha haieleweki kama kauli za supreme ni kauli za ACT au ni zake ambazo kutokana na supremacy zinakuwa za chama

Supreme anachofanya ni kugawa wananchi akIchochea mikoa ya kanda ya Ziwa wamuunge mkono.

Anafahamu wazi katika mikoa inayojielewa ACT itakuwa na wakati mgumu

Hivyo, kauli zake si za kuwatetea bali kuwavuta. Hata kama ni hatari kwa taifa, mradi ukikamilika hilo halina shida.
Ndivyo wenzetu wanavyotanguliza matumbo na taifa kufuata wakijinasibu ni wazalendo

Ni udanganyifu ule ule wa supreme anaelekea mahakamani, nyuma ya pazia alikuwa anapalilia tumbo.

Mwisho wa siku yeye ni mwanzilishi wa ACT. Kumbe kulikuwa na sababu gani za kwenda mahakamani?

Karata hiyo ya Ulaghai inatumbukia nyongo sasa

Inaendelea….,


Inaendelea...
 
Sehemu ya V

KAULI ZA KULIGAWA TAIFA
Kutokana na mwamko na maingiliano ya Watu, kauli za kuligawa taifa zitapokelewa kwa namna tatu.

Kwanza, wapo watakaodharau wakisema ni siasa za ushindani na wengine wakisema ni siasa majitaka
Pili. Wapo watakaokereka na kuona ni hatua mbaya kitaifa

Tatu, ni tangazo la ‘vita' kati ya ACT na mikoa husika

Kundi la kwanza halina tatizo, la pili ni lile lenye wakaazi wanaoishi Tanzania bila kujali maeneo yao.
Mwenyeji wa Kigoma anayeishi Kilimanjaro atakereka na kauli za Kibaguzi.

Kauli za supreme zinalenga kuwatenga Raia kwa misingi ya makabilla na maeneo.

Kundi la Pili litahusisha wananchi wa mikoa mingine wanaoamini katika kuishi kama taifa na si kanda.

Wananchi wanaochukizwa na udini au ukabila na wale wanaoamini maendeleo ni zao la jitihada za mtu, watu au jamii husika, serikali ni msaidizi tu

Kundi la tatu, ni la mikoa inayosemwa imepiga hatua. Kauli za supreme zimeelekea ‘kupiga' marufuku ACT katika mikoa kama Arusha na Kilimanjaro.

Haiwezekani wananchi wa maeneo hayo wakakubali chama kinachowaadhibu kwa jitihada zao na makosa yasiyotokana na wao

Tatizo la maendeleo ni la nchi nzima, CCM walipaswa wa jibu na wala si mikoa. Zitto anafahamu hilI

Kwa sababu zisizoeleweka ameamua kushambulia mikoa michache akidhani ni mkakati wa kisiasa.

Hatuelewi kama Zitto ataungwa mkono na wananchi wa Kagera au Mbeya, Ruvuma au Sumbawanga. Kila mmoja atahoji kama maendeleo yake hayataadhibiwa na ACT siku za mbeleni

Kwa kauli za supreme, ACT imetangaza vita na mikoa na si mahasimu wa kisiasa.

Alichokisema supreme ni upotoshaji, hakuwa na takwimu wala ujenzi wa hoja.

Gharama za kauli zake zitajibiwa na wahusika mbele ya safari.Ni ukosefu wa hekma na busara tunaoueleza hapa kila mara.

Kinachosikitisha, hiki ni chama cha vijana wasomi. Mawazo ya kuligawa taifa ni mabaya kuliko sumu ya mamba.
Hivi ACT hawana la kunadi sasa wanarudia ukanda walioulaani huko walikotoka?

Hii vita ya ACT na Kilimanjaro, Arusha, Mbeya na Kagera ni mbaya na itawagharimu
 
SUPREME LEADER ANAHITAJI LIKIZO

Kwa mwendo na kauli zake zenye utata kila uchao, supreme leader anapaswa kujitathmini.

Pengine shinikizo la kisiasa linapelekea kutoa kauli za kichochezi, dhaifu na zisizo na mashiko

Si kwamba analiweka taifa rehani, bali kauli ya uzalendo inazidi kupoteza maana

Kuhubiri chuki na kutangaza vita na baadhi ya mikoa si siasa zitakazo mnyanyua katika nchi hii

Leo wananchi wa mikoa inayojitafutia maendeleo wanamuona kama ‘adui yao'

Hilo litaathiri sana ACT kwa kutambua kuwa wananchi wa Tanzania hawahitaji tofauti za makabila, kanda au imani zao

Kwa maiaka 50 wameteseka kwa pamoja bila kujali maeneo wanayotoka

Mwalimu msukuma hana kipato tofauti na Mwalimu Mpare

Daktari Mnyamwezi hana tofauti na Daktari Mchaga au Mbondei

Tofauti ya wote hao ni dudu linaloumiza taifa kwa miaka 50.

Hilo ndilo la kuhoji na wala si wananchi wanaojenga barabara zao kwa kujitolea

Tunamshauri supreme leader aiache Tanzania kama ilivyo.

Kwamba anahubiri ukanda ni sera zilizoshindwa jirani na kwao.

Lau kana ana vinasaba basi aelewe Tanzania ni ya Watanzania.

Itakuwepo hata Nyerere alipoiacha, seuse supreme leader

Siasa walizokataa sasa wanazihubiri. Siasa majitaka sasa basi.

Tukawakemee, tukawakaripie wasomi hawa wanaotaka kutumia elimu yao kuvuruga taifa.

Tuwaambie mchana, fanyeni siasa, kama mumeshindwa tuachieni Tanzania yetu salama

Tusemezane
 
SUPREME LEADER ANAHITAJI LIKIZO

Kwa mwendo na kauli zake zenye utata kila uchao, supreme leader anapaswa kujitathmini.

Pengine shinikizo la kisiasa linapelekea kutoa kauli za kichochezi, dhaifu na zisizo na mashiko

Si kwamba analiweka taifa rehani, bali kauli ya uzalendo inazidi kupoteza maana

Kuhubiri chuki na kutangaza vita na baadhi ya mikoa si siasa zitakazo mnyanyua katika nchi hii

Leo wananchi wa mikoa inayojitafutia maendeleo wanamuona kama ‘adui yao'

Hilo litaathiri sana ACT kwa kutambua kuwa wananchi wa Tanzania hawahitaji tofauti za makabila, kanda au imani zao

Kwa maiaka 50 wameteseka kwa pamoja bila kujali maeneo wanayotoka

Mwalimu msukuma hana kipato tofauti na Mwalimu Mpare

Daktari Mnyamwezi hana tofauti na Daktari Mchaga au Mbondei

Tofauti ya wote hao ni dudu linaloumiza taifa kwa miaka 50.

Hilo ndilo la kuhoji na wala si wananchi wanaojenga barabara zao kwa kujitolea

Tunamshauri supreme leader aiache Tanzania kama ilivyo.

Kwamba anahubiri ukanda ni sera zilizoshindwa jirani na kwao.

Lau kana ana vinasaba basi aelewe Tanzania ni ya Watanzania.

Itakuwepo hata Nyerere alipoiacha, seuse supreme leader

Siasa walizokataa sasa wanazihubiri. Siasa majitaka sasa basi.

Tukawakemee, tukawakaripie wasomi hawa wanaotaka kutumia elimu yao kuvuruga taifa.

Tuwaambie mchana, fanyeni siasa, kama mumeshindwa tuachieni Tanzania yetu salama

Tusemezane
Nguruvi3,
Asante sana kunifungua macho. Nitafuatialia kwa ukaribu zaidi kauli za Supreme leader.
 
Jasusi kulikoni? Nani huyo Mbowe?
Yaani mkuu, nimecheka sana! dah
Miaka ya nyuma niliitwa kigagula pale niliposema mtafaruku mkubwa unafukuta CDM( MWAKA 2011), Nikaitwa mnajimu. Mika hiyo hiyo nikaitwa Nyerereist kwasababu nilisimama dhidi ya wale wanaomsingizia(sio wanaomkosoa). Mbowe alipokwenda kwenye togwa la Obama, wafuasi wake wakadai nazorotesha jitihada. Mkandara huzi kasema mimi ni kamati kuu CDM. Leo Zakumi anatoa jina lake, Mbowe ha ha ha!

Nasubiri kesho ni jina lipi nitapewa, silimishwa au batizwa.

Nisichoweza kusubiri ni kueleza ukweli. Na wala sitaomba radhi kwa kusema ukweli. Ukweli ni mtamu, unaniweka huru.
 
Nitapingana na wewe Nguruvi3 Katika hoja anayotoa Zitto kuhusu tofauti ya kiuchumi katika mgawanyo wa mapato,wala ajazungumzia idadi ya shule wala idadi ya barabara,maana kama ni barabara shinyanga IPO..wewe ndio unatengeneza Chuki na katu utofanikiwa bora ungemuomba Zitto afafanue kuliko kujipa tafsiri wewe.kanuni ya uzungumzaji inasema maana ya msingi itakua kwa mzungumzaji,na atawajibika kwa alichokisema,si kwa tafsiri aliotoa hadhira
 
Last edited by a moderator:
Nitapingana na wewe Nguruvi3 Katika hoja anayotoa Zitto kuhusu tofauti ya kiuchumi katika mgawanyo wa mapato,wala ajazungumzia idadi ya shule wala idadi ya barabara,maana kama ni barabara shinyanga IPO..wewe ndio unatengeneza Chuki na katu utofanikiwa bora ungemuomba Zitto afafanue kuliko kujipa tafsiri wewe.kanuni ya uzungumzaji inasema maana ya msingi itakua kwa mzungumzaji,na atawajibika kwa alichokisema,si kwa tafsiri aliotoa hadhira
Adharusi kama utakumbuka, hapo nyuma ukurusa mmoja tu uliopita ulisema Zitto hakusema kuhusu mkabila. Nilikuuliza kasema nini? Hukujibu

Sasa hivi unafanya spinning. Mbona hakuongelea hoja za rasilimali alizosema?
Je hakutakja mikoa na uchangiaji wa pato la taifa?

Ni lazima uelewe, sisi wengine tunatafuna hatusubiri kutafuniwa.

Kauli ya rasilimali ni pana kuliko unavyodhani
Ndio maana mjadala unapanuka na kuziangalia kauli zake kwa jicho mujarabu

Unachoweza kufanya ni kujibu, kukosoa, kukanusha au kutetea.
 
Adharusi njia rahisi ya kumuondoa kwenye tope hili alipozama, ilikuwa ni ya kumuita jukwaani Supreme Leader (SL), aje atoe ufafanuzi wa kile alichokisema juu ya mikoa ya Kilimanjaro na Arusha ama mingine ya namna hiyo kuwa na maendeleo tofauti na mingine. Vinginevyo ufafanuzi wa Nguruvi3 juu ya hatari anayotaka kukusababishia SL sisi watanzania kwa kauli zinazo kosa hekima na weledi unabaki kuwa sahihi.
 
Last edited by a moderator:
Adharusi njia rahisi ya kumuondoa kwenye tope hili alipozama, ilikuwa ni ya kumuita jukwaani Supreme Leader (SL), aje atoe ufafanuzi wa kile alichokisema juu ya mikoa ya Kilimanjaro na Arusha ama mingine ya namna hiyo kuwa na maendeleo tofauti na mingine. Vinginevyo ufafanuzi wa Nguruvi3 juu ya hatari anayotaka kukusababishia SL sisi watanzania kwa kauli zinazo kosa hekima na weledi unabaki kuwa sahihi.

Nina amini anapita humu atajibu tu,iwe JF,Twitter,Fb
 
Last edited by a moderator:
Adharusi njia rahisi ya kumuondoa kwenye tope hili alipozama, ilikuwa ni ya kumuita jukwaani Supreme Leader (SL), aje atoe ufafanuzi wa kile alichokisema juu ya mikoa ya Kilimanjaro na Arusha ama mingine ya namna hiyo kuwa na maendeleo tofauti na mingine. Vinginevyo ufafanuzi wa Nguruvi3 juu ya hatari anayotaka kukusababishia SL sisi watanzania kwa kauli zinazo kosa hekima na weledi unabaki kuwa sahihi.
Ni tope zito na ametitia. Hii si kauli ya SL peke yake, akiwa na hadhi ya supreme ni kauli ya ACT

'Ni tangazo la Vita' dhidi ya wananchi wa maeneo ya mikoa anayoituhumu.
Sijui wananchi wa maeneo hayo wanajisikiaje wiki hii

Huwezi kufanya tathmini ya maendeleo jukwaani bila vigezo tena ukitumia Ukanda na ukabila.
Hilo ni jambo zito linalohitaji umakini sana wakati wa kuliongelea. Kisiasa na kijamii madhara yake ni makubwa

Supreme atakapofanikiwa na hila hizi, ataenda mbali zaidi. Ipo siku atazua jingine katika hii hali ya kusaka umaarufu

Kama yupo, ajitokeze afafanue ana maana gani. Mfano, anaposema mkoa fulani unachangia kidogo ana maana gani.
Huwezi kutegemea Kilimanjaro ilingane kiuchumi na Arusha kwa sababu nyingi sana.

Wala huwezi kufananisha Lindi na Mbeya, kwasababu nyingi sana

Wananchi wa Tanzania ni wa nchi hii bila kujali wanatoka wapi
Mwalimu anayefundisha pale Muheza ni Mnyakyusa na yule wa Iloganzila ni mbondei. Wote wapo Tanzania, ni kwao

Mtu anapoanza kuwagawa kwa hoja za namna ya SL inatia shaka, simanzi, na hata kububujikwa na mchozi!

Kwamba, tumeshindwa kuongelea matatizo ya wazazi kujifungulia juu ya matenga ya baiskeli, walimu kukosa vifaa, madaktari kukosa vifaa, eti tunazama kushambulia mikoa tena iliyojiletea maendeleo

Hizi siasa za kushambulia maeneo zinatoka wapi. Hizi chuki dhidi ya watu wa aina fulani zinatoka wapi.

Wanashambulia mikoa na sio CCM! Nani ametufikisha hapa! Kosa la watu wa Arusha na Kilimanjaro ni lipi

SL alikuwa bungeni, atueleze ni wapi na kwa vipi mikoa hiyo imependelewa au imemegewa zaidi.

Alifanya nini bungeni kuzuia hali hiyo, na kwanini hakuongea bungeni anasubiri kwenda kwenye mikutano.
 
Mkuu Nguruvi3,

You made very strong and valid points. Sina haja Ya kurudia Lakini Suala la msingi Ni kwamba harakati Za Zitto kuhadaa wananchi haziwezi kunyamaziwa. Huyu ni mtu hatari sana Kwa Taifa kwani anaanza ujenzi wa Mgao wa wananchi, suala ambalo binafsi sikumbuki kiongozi aliyejaribu kufanya hivyo kwa mafanikio. Kama ulivyo jadili, tofauti Ya maendeleo nchini Tanzania ni matokeo Ya factors mbalimbali. Kwa mfano, factors muhimu ni Historical, physical, social, political and economic.

Tukianza na Physical factors, Hizi ni pamoja Na uwepo wa rasilimi mbalimbali Katika maeneo husika pamoja na and climatic issues; hizi ndio zilipelekea historical issues ulizojadili kwa kina. Zitto anaacha kujadili Adui Namba moja Ambae ni foreign capital ambayo inakuja kiholela. Na bado anathubutu kusema kwamba ACT ni Chama cha kijamaa. Katika physical factors Pia zipo climatic issues lakini hajadili mawazo on how we can overcome them via technology; Aidha hana muda huo au hana uelewa huo; social implies education and literacy and population growth; literacy opens up opportunities for the population;
Zitto anatakiwa kujadili hilo kisera; kwa mfano suala la family planning, hili ni moja Ya matatizo mkoani kwake Kigoma ambapo population growth overtakes government's ability (manispaa yake) to provide education, health, water and jobs; tukija kwenye political factors, these are divided into conflict and stability and leadership; on conflict, example is civil wars na unajadili vyema suala la wakimbizi Kigoma; and on leadership, mfano mzuri ni good governance which leads to stable government, stable policies, and safer investments;

Zitto hana muda au hajui umuhimu wa good governance; suala hilo no muhimu kwani it leads to less corruption which in the end it encourages capital accumulation via citizen's willingness to pay taxes and inflow of FDI; good governance also leads to accountability, results being stronger and supportive civil society;lastly is economic factors. Katika hilo kuna core periphery theory & cumulative causations. The former is more important and it has two fronts namely spread effect and backwash effect. Core regions ni Zile Nguruvi3 addressed ambazo zimeendelea for historical, physical and other reasons. In other words, development of core regions are often associated with physical, historical, social and political advantages that make them develop faster than ones in the periphery(kama Kigoma and others); the core are able to go to periphery and take advantage of abundant resources untapped there.

Lastly nifafanue kidogo juu Ya Backwash effect and spread effect. Backwash effect inajitokeza pale resources & labour zinapo elekea to the core meaning kwamba the core develops at the expense of the pheriphery.

Na Spread effects implies kwamba maendeleo in the core regions ( example Dsm, mwanza, etc) inasambaa over onto peripheries (eg Kigoma), kwa mfano spill over of wealth & knowledge. Kwa maana hii, na kwa hoja Ya Nguruvi3, even regions that are at disadvantage kama Kigoma still have potentials kuendelea iwapo watakuja na mikakati na sera bora that will take advantage of knowledge And resources in core areas.

Lawama za Zitto hazina tija.
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi #298 kaeleza kwa ufasaha dhana ya maendeleo na vigezo au vichocheo(factors) .
Kasema, vichochoe hivyo ni kama physical, political. Social na economic.


Tutapitia hoja zake tukiwa na mifano kamili ya kile alichosema

Hoja moja tunayoweza kuichangia kwa sasa ni ile Mchambuzi aliyosema hakuna mwanasiasa wa zama za karibuni aliyefanikiwa kwa kuwagawa Watanzania

Wengine hatukumbuki kiongozi aliyesimama na kuhubiri namna ya kuwagawa wananchi kama alivyofanya supreme leader.

Hoja aliyotoa ya kushambulia mikoa ya Arusha na Kilimanjaro inatisha.


SL anashambulia Kilimanjaro akiwa amesahau kuwa elimu yake ya O-Level ameipata Kilimanjaro.

Supreme leader alipaswa awe na ufahamu mzuri wa mkoa wa Kilimanjaro kuliko ufahamu butu aliouonyesha.


Alipokuwa Kibohehe Sekondari, supreme leader hakuwahi kutengwa kama Muha.

Leo amepata elimu anaitumia kuwalaghai wana Shinyanga kujenga chuki na watu wa Kilimanjaro Arusha, Mbeya n.k.


Mbinu anayoitumia kufunika uozo wa hoja butu ni kuanzisha twitts ili kuwaondoa watu katika mada halisi aliyoianzisha na inayokera

Tutaendelea na mjadala kwa kina kuchambua kauli za supreme leader hasa 'vita' yake na mikoa asiyoitakia mema kama si kuichukia.

Kiongozi ‘mzalendo' anapohubiri chuki dhidi ya wazalendo,inahitajika fikra

Kiongozi mzalendo anapoligawa taifa katika makundi, inatisha

Itandelea..

 
Back
Top Bottom