Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 51,303
- 40,190
Nguruvi3.
Msome hapa chini kiduchu Dr.Slaa anavyowagawa watanzania.
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbroad Slaa amemtaka Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia kuacha kutisha na kuwakamata wananchi wanaomuuliza maswali katika mikutano ya hadhara akidai amekashifiwa.Akihutubia umati wa wananchi katika Kata ya Mtimbwilimbwi na Nanyamba, Slaa alisema ni uvunjaji wa sheria na ubabe kukamata wananchi waliowapigia kura.Slaa alisema hayo baada ya wananchi kumwelezea kuwa, wamekuwa wakikamatwa na viongozi wa serikali na CCM wanapouliza maswali, ndiyo maana wameingiwa woga.Alisema Ghasia ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), anafanya vitendo hivyo kwa kuwa ana uhakika wa kutogombea tena ubunge katika Jimbo la Mtwara Vijijini baada ya kutambua kuwa hawezi tena kushinda.Slaa alisema maisha ya wakazi wa Mtwara Vijijini na umasikini unaowazunguka, ni aibu kwa uongozi katika miaka 50 ya uhuru, ambapo wajawazito wanalazimika kwenda hospitali wakiwa na vifaa.Enzi za Mwalimu Nyerere hakukuwa na suala hilo, leo hata mtoto mdogo anajua kuwa mama yake anakaribia kujifungua kwa kuwa ni lazima atakuwa anahangaika kutafuta vifaa vya kujifungulia, alisema Dk. Slaa.Alibainisha kuwa, Jimbo la Karatu ambalo wananchi wake hawakuwahi kuwa na waziri kwa miaka 15 sasa, wanafikiria kuingiza maji ndani ya nyumba zao wakati Mtwara Vijijini ambayo mbunge wake ni waziri, wananchi wanatafuta maji umbali wa zaidi ya kilometa 10.Katika hatua iliyoonesha kukithiri kwa umasikini, Dk. Slaa alilishwa supu ya ngozi ya ngombe kama kitoweo, ambapo wananchi walidai wamefanya hivyo kwa kuwa hawana uwezo wa kununua nyama.Walisema hata hizo ngozi ni lazima aende mtu kuzifuata Mtwara mjini na siku inapokosekana wanajihesabia kama wamekosa nyama halisi.Kufuatia hali hiyo, Dk. Slaa aliwataka wananchi wa Mtwara mjini kujiepusha na kuuza uhuru wao kwa gharama ya shilingi elfu tano na badala yake wasimamie ukombozi wa kweli.

Last edited by a moderator: