Barubaru
JF-Expert Member
- Apr 6, 2009
- 7,161
- 2,324
Kwanza kabisa nikwambie siasa za kejeri huwa sipendi... kama kuna kitu ambacho hujaelewa sema nami nitaelezea kadri ya uwezo wangu.Tujenge kuheshimiana katika mijadala ndo tutasonga mbele kwani tuko hapa kuelemishana, kukosoana, kufundisha na nk.
Baada ya kuandika hayo.. naomba urejee katika swali langu nililouliza je kama Zitto ni mchanga wa siasa nimuache ili kusudi aendele kueneza hizi sumu za ulaghai na ukanda?
Na je ni wajibu wa nani kukemea mfumo pale tunapoona kuna kasoro?
(Bila kejeri na vijembe tafadhali kama utaweza)
Alinda.
Awali ya yote napenda kukupongeza kwa angalizo ulilolitoa. Japo mimi sijaona kejeli yoyote wala kijembe kwa nilichoandika.Lakin kama umeona hivyo basi niwie radhwi kwani mara zote napenda kutumia lugha ya kistaharabu katika maandiko yangu
Nakuomba nisome vizuri maandiko yangu KWA NIA YA KUNIELEWA na Insh'Allah utanielewa na kama utanisoma kwa NIA YA KUNIPINGA basi kuna mambo utashindwa kuyaona na hivyo kutaka turejee pale pale tulipotoka.
JIBU la suala lako nilishakujibu hapo juu nilisema hivi." Kwa mtazamo wangu na ndivyo ilivyo, kuwa kama SIASA za Tanzania zingekuwa nyoka anayetembea basi ZITTO angekuwa ni mkia. Huwezi kubadilisha chochote kwa nyoka kwa kumkata mkia. Mtu makini anakata KICHWA ili kuuwa huo mfumo".
Kwa kuongezea Masuala ya UDINI, UKABILA na UKANDA yameanza zamani sana huko Tanzania na utakuwa si msemakweli kama utasema Zitto ndio anaye yaanzisha. Huko itakuwa ni kumzulia jambo ambalo lilipandwa zamani sana na sasa ndio lipo katika hatua za mavuno.
Kwa maoni yangu ili kuepuka haya ni vizuri kuhakikisha kuwa Serikali inasimamia HAKI na USAWA kwa jamii yote bila kujali itikadi, dini, kabila wala umaarufu wa watu. NDIO MAANA KULE MWANZO NILISEMA KULETA USAWA NA HAKI NCHINI MWENU mnatakiwa kuchagua VIONGOZI SAHIHI NA WALA SIO VIONGOZI BORA.Ili waweze kusimamia maamuzi sahihi kwa ajili ya maendeleo ya nchi yenu.
Nafikiri mengi nimeandika huko mwanzo sipendi kuyarudia.
Pole sana.