Mkandara,
Nadhani sasa ni wasaa wenu kukubali tu ukweli kwamba kiongozi wetu mkuu
Zitto aliteleza. Ni wajibu wenu kumsaidia, na sio kujitoa muhanga kuteleza nae mpaka maka. Naomba nichangie katika sehemu hiyo yenye nyekundu hapo juu.
Unatumia Human Development Index (HDI) kama indicator ya kubaini wananchi wa mkoa upi wapo mbele, na wa mkoa upi wapo nyuma. Pengine wewe na supreme leader wenu zitto hamuelewi HDI composition yake ni nini, ndio maana mnakuwa walaghai. Twende pole pole na tutabaini:
1. Kati ya Shinyanga na Kilimanjaro, nani yupo nyuma na kwa ninim
2. Nini au Nani alaumiwe juu ya hali ya mkoa mmoja kuwa nyuma namkoa mwingine kuwa mbele na kwa nini.
Hiyo Human Development Index yenu inaangalia vigezo vikuu vinne:
1. Life expectancy.
2. Average years of schooling.
3. Expected years of schooling.
4. GDP Per Capita.
Kwa vigezo hivi, kwa mtazamo wako, ambao inaonekana pia upo shared na supreme leader wenu zitto, Shinyanga ipo nyuma ya Kilimanjaro katika yote haya manne. Na bila haya, unahoji Je:
Aloachwa ataweza vipi kuchangia revenue zaidi?
Tujadili:
1. GDP. Tayari tunajua nini maana ya dhana hii.
· Kwa mujibu wa takwimu za 2010/2011 kama mfano, GDP ya Shinyanga ilikuwa ni shilingi bilioni 1.9. Katika kipindi hicho hicho, GDP ya Kilimanjaro ilikuwa ni shilingi bilioni 1.4. Tukiamua kufuata na kuamini bila kuhoji kauli za kilaghai za
Zitto, basi Shinyanga ilichangia zaidi katika pato la taifa kuliko Kilimanjaro. Je ni kweli? Hapana, ni ulaghai. Tutaona punde.
Kwa upande mwingine:
Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2010,tax revenues za mkoa wa shinyanga zilikuwa ni shillingi bilioni 11.2, na kwa kilimanjaro, shillingi bilioni 72.4.
Tukirudi kwenye hoja yako kwamba Aloachwa ataweza vipi kuchangia revenue. Shinyanga imemwacha Kilimanjaro in terms of GDP Contribution (ingawa wala sio kwa kiasi kikubwa), lakini huyu Kilimanjaro anachangia zaidi in terms of Makusanyo ya Kodi, tena kwa mbali sana.
Kwa maana nyingine, Kilimanjaro inachangia mapato ya kodi karibia mara saba ya mchango wa Shinyanga. Kumbuka, GDP haikusanywi, ni hesabu tu bila ya kujalisha nani anamiliki productive assets, tulishajadili hili kwa kina. Lakini Tax revenues, ni zile wananchi wa kada mbalimbali wanatozwa katika jurisdiction husika. Kumbuka, social contract baina ya serikali yoyote katika nchi ya kidemokrasia ni Tax revenues, sio GDP. Ni Tax revenues na matumizi yake ndio yanaipa serikali husika legitimacy ya kutawala au kuinyima legitimacy hiyo.
Jamani, mnahitaji kuambiwa kwa lugha gani ya kistaarbu ili muelewe kwamba Zitto ni mlaghai na mbaguzi?
Tuendelee kuchambua hoja yako na msaliti zitto ambayo inaipa Human Development Index uzito mkubwa kiasi cha kuanza kubagua watanzania. Tuangalie zaidi GDP Per Capita, ambayo ni moja ya vitu vinavyojenga HDI yenu.
Kwa mujibu wa Takwimu za 2010/2011, GDP Per Capita kwa mikoa hii miwili ni kama ifuatavyo:
· Kilimanjaro = approx 1,000,000/=
· Shinyanga = approx 670,000/=
Inaonekana mchumi wenu uchwara na msaliti
Zitto hajui GDP per capita inapatikana vipi. Ni hivi, GDP Per capita ni takwimu tu, ambayo inapatikana kwa kuchukua jumla ya uzalishaji/output (GDP) - mfano ya shinyanga au Kilimanjaro, na kuigawanya na jumla ya idadi ya watu (population) - kwa mfano ya shinyanga au Kilimanjaro.
Population ya Kilimanjaro ni takribani watu 1.4million, huku population ya Shinyanga ikiwa karibia watu 2.8 million, kama mara mbili ya idadi ya watu wa Kilimanjaro. Usisahau hili.
Ukigawanya hizi population katika GDP za mikoa husika unapata rough figures (GDP Per Capita) kama tulivyo ona hapo juu.
Huko nyuma nilimueleza
Zakumi kwamba GDP Per Capita as an indicator imepitwa na wakati na kwamba wataalamu na watafiti mbalimbali wa masuala ya uchumi na maendeleo kutoka nchi zilizoendelea na zinazoendelea, wapo njiani kuibadilisha. KWa mfano, Joseph Stiglitz, Amartya Sen na wengineo. Zakumi akapinga kwa hoja kwamba GDP Per Capita is supreme and it tells the whole story.
Tumeona GDP ya Shinyanga ni kubwa kidogo kuliko Kilimanjaro, lakini GDP Per Capita ya Kilimanjaro kuwa kubwa zaidi ya Shinyanga. Kwanini supreme Zitto hasemi ukweli? Kwanini na nyinyi badala ya kumsaidia mnazidi kupotosha umma?
Kinachofanya GDP Per Capita ya Shinyanga iwe ndogo zaidi ya ile ya Kilimanjaro ni suala moja tu tofauti kubwa ya idadi ya watu baina ya Kilimanjaro na Shinyanga, basi!. Maswali kwenu:
· Je, wananchi wa Kilimanjaro walaumiwe kwa kuwa na mchango mdogo zaidi ya Shinyanga (GDP wise), lakini pato kubwa zaidi (GDP Per Capita) kwa sababu tu wapo makini zaidi linapokuja suala la controlling population growth/family planning?
Tumeona kwamba Kilimanjaro mchango wao ni mdogo zaidi (GDP) ya Shinyanga (ingawa kwa tofauti ndogo sana) lakini mchango wa Kilimanjaro (in terms of tax revenues) ni karibia mara saba ya ule wa Shinyanga. Swali kwenu:
· Je, ni sahihi kusema kwamba Shinyanga wananyonywa na Kilimanjaro? Kwa hoja zipi?
Ni muhimu
Zitto aje humu kukiri kwamba aliteleza, vinginevyo hatuta acha kutetea taifa letu lisivurugwe na wabaguzi na wa binafsi kama Zitto kabwe. Never.
Tuangalie vigezo vingine vya hiyo Human Development Index ambayo Supreme leader zitto anazunguka nayo kwenye mkoba wake wa usaliti na ubaguzi nyinyi wafuasi wake kudandia upuuzi huo bila kutumia akili zenu kuchambua mambo. Vigezo hivyo ni:
Life Expectancy, Average Years of Schooling and Expected Years of Schooling.
Life Expectancy:
Wastani Kitaifa ni miaka 55. Shinyanga, wastani wake (miaka 55), sawa sawa na wastani wa taifa. Tuendelee. Kilimanjaro, life expectancy yake ni zaidi ya wastani wa taifa na wa Shinyanga, yani miaka 67. Je:
Wa kulaumiwa hapa ni nani? Je, ni mkoa ambao unajali zaidi uzazi wa mpango (Kilimanjaro) au mkoa ambao haupo makini katika hilo (Shinyanga)?
· Je Shinyanga wanahitaji nini ili waweze kuwa maini zaidi na masuala ya afya kama vile family planning programme?
· Je, uzazi wa mpango unahitaji fedha kiasi gani cha fedha za walipa kodi ili kufanya ufanikiwe Shinyanga kama Kilimanjaro?
· Je, Kilimanjaro wamekosa nini kuwa makini zaidi katika hilo na wamefanikiwa kwa kumyonya nani?
· Je, kama ni fedha zimetumika, zimetoka wapi, kwenye GDP au Tax Revenues?
Tukiwa bado kwenye suala la Human Development Index, tuangalie kidogo juu ya janga la Ukimwi. Kwa mujibu wa takwimu za NBS, wastani wa taifa (HIV prevalence) ni 5.8%. Kwa mkoa wa Kilimanjaro, ni 1.9%. Kwa mkoa wa Shinyanga, ni 7.6%, kwa maana kwamba Ukimwi mkoani Shinyanga, prevalence yake ni above National Average. Hili ni suala ambalo linahusika moja kwa moja na life expectancy, hence Human Development Index yenu mnayozunguka nayo kwenye mikoba kuladhai na kubagua watanzania. Je:
· Wa kulaumiwa juu ya janga la ukimwi ambalo linachangia life expectancy ya Shinyanga kuwa ndogo kuliko Kilimanjaro, ni wananchi wa Kilimanjaro? Kwa hoja zipi?
Pia kuna suala la Doctor to Patient Ratio. Mkoa wa Kilimanjaro has a higher ratio than Shinyanga kwa maana ya kwamba Kilimanjaro kama mkoa, idadi ya Madaktari kwa kila wananchi elfu moja ni kubwa zaidi kyuliko idadi hiyo kwa mkoa wa Shinyanga. Mbali ya takwimu hii kuwa bora zaidi Kilimanjaro kutokana na mkoa huu kuwa na more effective family planning system kuliko Shinyanga, lakini pia ni jambo lililo wazi kwamba wananchi wa Kilimanjaro wanajulikana sana kwa pia juhudi zao za kusomea fani ya udaktari. Lakini muhimu zaidi, Kilimanjaro inaongoza kwa ku retain madaktari wao mkoani humo baada ya kumaliza masomo ya udaktari. Retain rate ni kubwa kuliko Shinyanga. Swali kwako, Je:
· Ni haki kweli kulaumu wananchi wa Kilimanjaro kuwa na HDI kubwa (refer to life expectancy argument) kuliko wananchi Shinyanga?
Components za mwisho ambazo zinajenga hiyo HDI yenu ni Average Years of Schooling and Expected Years of Schooling. Katika hili, sina haja ya kujadili kwani
Nguruvi3,
Mag3, na wengine wamelijadili vyema sana.
Cc
Waberoya,
Ritz,
adhurusi