Alinda
Platinum Member
- Jun 26, 2008
- 1,695
- 2,149
Nguruvi3:
Kwanini unaomba twakimu wakati maswali mengi tu unaogopa kuyajibu? Kwenye zaidi ya posti tatu nimekuuliza kwanini mnaona uzito kukemea ubaguzi wa kidini, kikabila, kikanda unaofanya wa viongozi wa juu wa vyama vya kisiasa, wafanyabiashara au viongozi wa serikali?
NI viongozi gani, na wa dini gani wamebagua/wabegauliwa na ni kivipi wamebaguliwa? Maana ukisema "Viongozi" bila kutaja aina ya ubaguzi waliofanya utakuwa hautendei haki mjadala.
Pia kwa vile wewe ni Tanzania bila shaka unapinga ubaguzi wa kidini, kikabila, kikanda na nk kwa nguvu zako zote. Je ni lini wapi wewe kama @Zakumi ulikemea hilo?
Je nani anapaswa ukukemea ubaguzi wa aina yeyote ile pindi pale mtu unapoona/au unapohisi sehemu fulani kuna ubaguzi?
Je nikienda TRA, BOT, Usalama wa Taifa, nitapata takwimu zinazoonyesha diversity ya nchi au watu walipata ajira kwa juhudi na sio kubebwa?
Unahusisha matamshi ya Zitto na matukio ya Rwanda. Matatizo ya Rwanda hayakutokea kwa sababu ya siasa tu. Yalikuwa mpaka kwenye muundo wa ajira.
Kwa hiyo sentesi unakubali "matamshi ya Zitto" ni sababu mojawapo inayoweza kuleta machafuko kama yaliyotokea Rwanda.. Sasa kama ni hivi kipi bora kuzikemea mapema ili kuhepusha madhara ya hapo baadaye au kuziacha bila kukemewa na baadaye madhara yakishatokea tuje hapa tuseme "ooh mie nilijua tu kuwa hiki na kile kitakotea"
Kwanini watanzania wanachagua rais kutoka makabila madogo na sio makabila makubwa? Kwanini mhaya ana nafasi ndogo sana ya kuwa rais?
Sasa kama Mhaya hakujitokeza kugombea urais unataka watu wamchague tu kwa vile ni kabila kubwa? au kama hana sifa abebwe na sifa ya kabila lake ambalo ni kubwa? Tusianze kuangalia rais anatoke wapi, au ni kabila gani, au ni dini gani? tunachopeswa kuangalia ni je huyu rais ni Mtanzania? na je anaguswa na matatizo ya Mtanzania? je ni mchapakazi? mpiga vita rushwa na nk. Mambo ya dini, au sehemu atokayo hayana nafasi.
Na nilitegemea mtu kama wewe ambaye umepata bahati ya kuishi katika ulimwengu wa kwanza ungekuwa wa kwanza kupiga vita udini, ukabila na nk. lakini kwa bahati mbaya unangalia mtu kwa kabila lake na ukianza kabila kitakachofuata ni dini, na baada ya hapo ni maumbile.
Je nini walichonacho makabila makubwa na makabila madogo hawana? na Je nini tofauti kati ya mhaya na "mkara" au msimbiti? Sasa kama wote ni sawa, na wote ni watanzani kwani tatizo liko wapi?
Tumtazame mtu kama mtanzania, tumuhukumu kwa matendo yake si kwa dini yake au kwa kabila lake au kwa maubile yake.
Ulaya na Amerika wamepiga hatua ya kwenda mbele baada ya kuondoa kichwani mwao huu ukabila husio na kichwa wala miguu.. mfn mzuri ni Amerika leo Obama ni rais wao, mtu ambaye baba yake si Mmarekani maana wao unachoangalia ni utaifa, uchapakazi wa mtu, mapenzi ya mtu kwa nchi yake na watu wao na nk.
Lakini leo hii sisi tunaanza kumuangalia mtu ambaye ni mtanzania tena utanzania husio na shaka eti ni kabila gani, eti ni dini gani? kweli? hakika ni uchungu!!
Mtu mweusi kupiga hatua kwenda mbele itakuwa ni miujiza maana mtu ambaye ameelimika, amabaye tulitegemea ukasaidie watu wa vijijini wenye mauno ya ukabila na udini kuwapa elimu lakini ndo kwanza mtu huyu huyu anakuwa mstari wa mbele kuangalia vitu kwa jicho la udini/ukabila. Hakika waafrika tunajichimbia mashimo katika bara bara tunayotarajia kupita..
Yaani hakuna kitu kinachoniudhunisha tunapobaguana wenyewe kwa wenyewe...
Mimi kama Alinda ni mkristo, sina tatizo kama leo ningeenda TRA au Bank au ofisi yeyote ile nikakuta waislamu watupu au wachaga watupu, kwangu mimi kitu muhimu ni utanzania (ndo thamani yetu, ndo dhahabu yetu) Nitaumia nikiingia ofisi yeyote ile na kukuta wakristo wakenya.. Hiki kitu kitaniumiza.
Tushikamane, sisi sote ni watanzania, sisi sote ni ndugu, Tanzania ndo mama yetu, ndo baba yetu, haya tunayoyaandika kuhusu wanasiasa yasitufarakanishe... Wewe @Zakumi ni mtanzania mwenzangu na ndo kitu muhimu kwangu...
Najua hii posti utaacha kuijibu.
mmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmm